Sura ya 53

Mimi ndiye mwanzo, na Mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyefufuka na kamili. Nasema maneno Yangu mbele yenu, na lazima muamini Ninachosema kwa thabiti. Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au mstari mmoja wa kile Ninachosema kitawahi kupita. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Punde ambapo Nimesema, hakuna neno hata moja limewahi kurudishwa na kila neno litatimizwa. Sasa wakati umewadia na lazima muingie katika uhalisi kwa haraka. Hakuna muda mwingi. Nitawaongoza wana Wangu hadi katika ufalme mtukufu na kile ambacho mmejitahidia na kutamani sana kitafanikishwa. Wanangu! Inukeni haraka na mnifuate! Tayari hakuna muda wa ninyi kuwa mkilifikiri. Muda uliopotezwa hautarudi kamwe, baada ya giza kuna nuru, na unyakuzi uko mbele ya macho yenu. Je, mnaelewa? Fungueni macho yenu! Amkeni upesi! Hamruhusiwi sasa katika kuwasiliana miongoni mwenu kushiriki katika kupiga domo au kusema chochote kisicho cha maana katika ujenzi wa kanisa, kilicho cha muhimu ni kuwaruzuku ndugu na uzoefu wako wa utendaji au jinsi unavyoangazwa mbele ya Mungu na kujijua; yeyote anayeweza kutoa hili atakuwa na kimo! Sasa watu wengine hawaogopi, na bila kujali kile Ninachosema au kiasi gani Ninachokuwa na wasiwasi, bado hauogopi; nafsi yako nzee haijiruhusu kuguswa, kwa hivyo unaweza kuendelea kwa njia hii! Ona ni nani atakayeangamizwa! Daima unafikiri kuhusu kuishika dunia, ukitamani sana utajiri, na kuhisi uhusiano wa karibu sana na wana wako wa kike, wa kiume na mume wako. Haya, unaweza kuendelea kuhisi uhusiano wa karibu! Sio kwamba maneno Yangu hayajazungumzwa kwenu, na mnaweza kuendelea jinsi mnavyotaka! Katika siku za usoni za karibu mtaelewa kila kitu, lakini mtakuwa mmechelewa sana tayari na yote yanayowangoja ni hukumu.

Iliyotangulia: Sura ya 52

Inayofuata: Sura ya 54

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp