Sura ya 54

Ninalielewa kila kanisa kama kiganja cha mkono Wangu. Usifikiri kwamba Siko wazi au Sielewi. Ninawaelewa na kuwajua watu wote mbalimbali wa kila kanisa hata zaidi. Ninahisi hisia ya umuhimu kwamba ni lazima Nikufundishe. Nataka nikufanye ukue hadi utu uzima haraka zaidi ili siku ambayo utaweza kutumiwa na Mimi itakuja haraka zaidi. Nataka vitendo vyenu viwe vimejaa hekima Yangu ili muweze kumdhihirisha Mungu kila pahali. Kwa njia hii lengo Langu kuu litafanikishwa. Wanangu! Mnapaswa kuwa wenye kufikiria nia Zangu, msifanye Nishikilie mikono yenu Ninapowafundisha. Lazima mjifunze kujua nia Zangu, mjifunze kuona hadi kwenye kina cha mambo, kuwawezesha kushughulikia kila jambo linalowajia kwa urahisi na bila ugumu. Pengine katika mafundisho yenu, mara ya kwanza hamtaelewa, kisha mara ya pili, mara ya tatu.... Hatimaye mtaelewa nia Zangu.

Maneno yenu kila mara huwa na sifa isiyopenyeka, mfikiri wenyewe kuwa hii ni hekima, sivyo? Mara mkiwa wasiotii, na mara nyingine mkiwa wenye utani, wakati mwingine na mawazo au wivu wa mwanadamu.... Kwa jumla, mnazungumza bila uthabiti, msijue jinsi ya kuruzuku maisha kwa wengine au jinsi ya kufahamu hali zao, na kushiriki katika mawasiliano ya kibwege. Fikira zenu haziko wazi, hamjui hekima ni nini, ujanja ni nini, ninyi mmechanganyikiwa sana tu. Mnachukulia ujanja na udanganyifu kama hekima, je, hili haliliaibishi jina Langu? Je, hili halinikufuru? Je, hili halileti mashtaka ya uwongo dhidi Yangu? Hivyo lengo mnalotafuta ni lipi? Je, mmefikiria kuhusu hilo? Je, mmejitahidi kufanya hili? Nakuambia, nia Zangu ni mwelekeo na lengo ambalo mnatafuta, vinginevyo, yote yatakuwa bure. Wale ambao hawajui nia Zangu ni wale wasiojua jinsi ya kutafuta, na wataachwa, wataondolewa! Ni dhahiri kwamba, kugundua nia Zangu ni somo la kwanza ambalo lazima mjifunze. Ni kazi ya dharura zaidi, na hairuhusu kuchelewa! Msisubiri Mimi nimkaripie kila mmoja wenu, mmoja baada ya mwingine! Ninyi daima ni wasiojali na wapumbavu. Ni jambo la mzaha! Siwezi kuamini ninyi ni wapumbavu hivi! Hamjali kuhusu nia Zangu! Jiulizeni, ni mara ngapi ninyi huelewa nia Zangu kabla ya kutenda? Mnapaswa kuwa ndio mnaojifunza wenyewe! Mnataka Niwashughulikie mmoja mmoja, hiyo haiwezekani! Mnapaswa kujifunza kupata uzoefu na kupata utambuzi na hekima mnapotenda. Maneno yanayotoka vinywani mwenu ni mazuri, lakini hali halisi ni ipi? Mnapokumbana na uhalisi hamtaweza kufanya chochote. Mnachosema hakilingani na uhalisi. Kwa kweli Siwezi kuvumilia kile ambacho ninyi mnafanya; Natazama na Siwezi kujizuia kuwa na huzuni. Kumbukeni hili! Katika siku zijazo jifunzeni kutambua nia Zangu!

Iliyotangulia: Sura ya 53

Inayofuata: Sura ya 55

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp