Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 40

Kwa nini ninyi ni wa mwendo wa polepole? Kwa nini hamsikii? Makumbusho kadhaa hayajawazindua; hili linanihuzunisha. Kwa kweli Sipendi kuwaona wanangu namna hii. Moyo Wangu unawezaje kustahimili hili? Ah! Lazima Niwafundishe kwa mkono Wangu mwenyewe. Mwendo Wangu unaendelea kuwa wa kasi. Wanangu! Inukeni haraka na mshirikiane na Mimi. Nani wanajitumia kwa dhati kwa ajili Yangu sasa? Ni nani anayeweza kujitolea kikamilifu bila malalamiko hata kidogo? Daima ninyi ni wenye kutosikia na wapumbavu! Ni wangapi wanaoweza kuwa wenye huruma kwa hisia Zangu, na ni nani anayeweza kuelewa kwa kweli Roho ya maneno Yangu? Ninaweza tu kusubiri kwa hamu na kuwa na matumaini; nikiona kwamba kila moja ya hatua zenu haiwezi kuuridhisha moyo Wangu, Ninaweza kusema nini? Wanangu! Kila kitu ambacho Baba anafanya leo ni kwa ajili ya wana Wangu. Kwa nini wanangu hawawezi kamwe kuuelewa moyo Wangu, na kwa nini wana Wangu daima wanisababisha Mimi, Baba yenu, kuwa na wasiwasi? Wanangu watakua lini, wasinisababishe kuhangaika, na kunikubalia kuwaamini wana Wangu? Wanangu wataweza kuishi kwa kujitegemea lini, kusimama, na kurahisisha mizigo iliyo mabegani mwa Baba? Ninawalilia wanangu kimya kimya tu, nami Ninaeleza kila kitu kwa ajili ya kukamilisha mpango wa usimamizi wa Mungu na kuwaokoa wana Wangu, wapendwa Wangu. Sina chaguo lingine.

Ahadi Zangu zimetimia na zinadhihirika mbele ya macho yenu. Kwa nini usiufikirie moyo Wangu? Kwa nini? Kwa nini? Hadi sasa, umehesabu: Ni mambo mangapi uliyotenda ambayo yameuridhisha moyo Wangu, au mambo yaliyolirutubisha na kulilisha kanisa? Tafakari haya kwa makini na usiwe holela. Usiache hata hali moja yenye ukweli. Huwezi tu kulenga umbo la nje na kupuuza kiini. Nyakati zote lazima uchunguze kama kila neno lako na tendo lako na kila hatua yako imepitia hukumu mbele ya kiti cha Kristo, na kama umebadilika na kuwa na sura ya mtu mpya—si kwa kuiga, lakini badala yake kutoka ndani ya maonyesho ya maisha. Usicheleweshe maisha yako ili kuepuka kupitia mateso. Harakisha na urekebishe hali hii, uridhishe moyo Wangu, na uzingatie kanuni za mwenendo: Fanya mambo kwa haki na maadili na uuridhishe moyo Wangu. Usiwe holela. Je, utakumbuka hilo?

Iliyotangulia:Sura ya 39

Inayofuata:Sura ya 41

Maudhui Yanayohusiana

 • Sura ya 31

  Sijawahi kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya watu. Ninapowatafuta watu kweli, wao hufunga na kubana macho yao na kupuuza matendo Yangu, kana kwamba yote…

 • Hakuna Mtu Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

  Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kupona kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika k…

 • Kwenye Hatua za Kazi ya Mungu

  Kutoka nje, inaonekana kwamba hatua za kazi ya sasa ya Mungu tayari zimekamilika, na mwanadamu tayari amehukumiwa, kuadibiwa, kuangamizwa na kusafish…

 • Sura ya 35

  Siku hizi, binadamu wote, kwa viwango vinavyotofautiana, wameingia katika hali ya kuadibu. Kama tu alivyosema Mungu, “Naenda mbele na binadamu sako kw…