Sura ya 41

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na kuzungumza kwa niaba Yangu. Kuwa na imani kwamba mambo na masuala yote yanaruhusiwa na kiti Changu cha enzi na yote yana nia Zangu ndani yayo. Ukiendelea kushiriki kwa hiari kutakuwa na shida, umefikiri kuhusu matokeo? Hii ni aina ya jambo ambalo Shetani atatumia kwa manufaa yake. Kuja mbele Yangu mara nyingi. Nitazungumza kwa uwazi: Kama utafanya kitu bila kuja mbele Yangu, basi usifikiri unaweza kukikamilisha. Ni ninyi ambao mmeniweka katika nafasi hii.

Usivunjike moyo, usiwe dhaifu, Nitakufichulia. Njia ya kwenda kwa ufalme sio laini hivyo, hakuna kitu kilicho rahisi hivyo! Unataka baraka zije kwa urahisi rahisi, sivyo? Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi na hutakuwa na upendo wa kweli Kwangu. Hata kama majaribu haya yanajumuisha hali ndogo tu, kila mtu lazima ayapitie; ni kwamba tu ugumu wa majaribu utakuwa tofauti kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Majaribu ni Baraka kutoka Kwangu, na ni wangapi kati yenu ambao huja mbele Yangu na kupiga magoti mkiomba baraka Zangu? Watoto wapumbavu! Wewe daima huhisi kwamba maneno machache ya bahati huhesabika kama baraka Yangu, lakini huhisi kuwa uchungu ni moja ya baraka Zangu. Wale wanaoshiriki katika uchungu Wangu bila shaka watashiriki utamu Wangu. Hiyo ni ahadi Yangu na baraka Zangu kwenu. Usisite kula na kunywa na kufurahia. Wakati giza litapotea hapa kutakuwa na nuru. Huwa kuna giza kuu kabla ya alfajiri; baada ya wakati huu kutakuwa na mwangaza zaidi polepole, na baadaye jua litainuka. Usiogope au kuwa mwepesi kutishwa. Leo Ninawaunga mkono wana Wangu na kushika mamlaka Yangu kwa ajili.

Inapofikia shughuli za kanisa, usikwepe jukumu lako. Ukilileta suala hilo mbele Yangu kwa uangalifu sana, utapata njia. Jambo dogo kama hili linapotokea, unakuwa na woga na wasiwasi, hujui la kufanya? Nimesema mara nyingi, “Nikaribie mara kwa mara!” Je, mmeweka vitu Nilivyowaambia mweke katika vitendo kwa uangalifu sana? Mmetafakari neno Langu mara ngapi? Kwa hivyo, hamna utambuzi wowote ulio wazi. Hicho si kitu mlichosababisha? Mnawalaumu wengine, mbona hamjichukii? Mmevuruga vitu na baadaye bado hamko makini sana na bado mko wazembe; mtazingatia neno Langu.

Watiifu na wanyenyekevu watapata baraka nyingi. Kanisani, mtasimama imara katika ushuhuda wenu Kwangu, mshikilie ukweli—haki ni haki na mabaya ni mabaya—wala msichanganye nyeusi na nyeupe. Mtakuwa vitani na Shetani na lazima mumshinde kabisa ili asiinuke kamwe. Lazima mtoe kila kitu kulinda ushuhuda Wangu. Hili litakuwa lengo la matendo yenu, usisahau jambo hili. Lakini sasa, mmepungukiwa katika imani na uwezo wa kutofautisha vitu na ninyi daima hamuwezi kuelewa neno Langu na nia Zangu. Hata hivyo, usiwe na wasiwasi; kila kitu kinaendelea kulingana na hatua Zangu na wasiwasi huzaa shida tu. Shinda kwa muda zaidi mbele Yangu na usitilie maanani chakula na nguo kwa mwili wa asili. Tafuta nia Zangu mara nyingi, na Nitakuonyesha wazi ni nini. Pole pole utapata nia Zangu katika kila kitu, ili kwamba nitakuwa na njia ya kwenda ndani ya kila mtu bila vizuizi. Itauridhisha moyo Wangu na mtapata baraka pamoja na Mimi milele na milele!

Iliyotangulia: Sura ya 40

Inayofuata: Sura ya 42

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp