Sura ya 46

Yeyote anayejitumia na kujitolea kwa uaminifu kwa ajili Yangu, hakika Nitakukinga mpaka mwisho kabisa; mkono Wangu hakika utakushikilia ili kwamba daima una amani na mwenye furaha daima na kila siku una mwanga Wangu na ufunuo. Hakika Nitakupa baraka Zangu mara dufu, ili uwe na kile Nilicho nacho na umiliki kile Nilicho. Kile unachopewa ndani yako ni maisha yako, na hakuna mtu anayeweza kukichukua kutoka kwako. Usijiletee taabu au kufadhaika; ndani Yangu kuna amani na furaha tu. Ninakupenda kwa dhati, wewe mtoto ambaye hunisikiza kwa dhati na kunitii. Wale ambao Ninawachukia zaidi ni wanafiki na hakika Nitawaangamiza. Nitaondoa dalili yoyote ya ulimwengu kutoka kwa nyumba Yangu, na kuondosha vitu vyote ambavyo Siwezi kuvumilia kuona.

Ndani ya moyo Wangu Najua hasa nani ambaye ananitaka kwa dhati na ni nani ambaye hanitaki. Wanaweza kujificha vizuri na kuweka kisingizio kijanja, na inaweza hata kusemwa kuwa wao ni waigizaji bora zaidi duniani, lakini Naona wazi kila kitu wanachoshikilia ndani ya mioyo yao. Usidhani kuwa Sijui yaliyo ndani ya moyo wako; kwa kweli hakuna mtu anayeelewa wazi zaidi kuliko Mimi. Najua kilicho moyoni mwako; wewe uko tayari kujitoa kwa ajili ya Mungu, kutumia kwa ajili ya Mungu, ni kwamba tu hutaki kutumia mazungumzo mazuri ili kuwafanya wengine wafurahie. Ona wazi! Ufalme wa leo haujengwi kwa nguvu za mwanadamu, lakini utajengwa kwa ufanisi kikamilifu kwa kutumia hekima Yangu nyingi na jitihada ya bidii. Yeyote aliye na hekima na anayemiliki kile Nilicho ndani yake atashiriki katika ujenzi wa ufalme. Usiwe na wasiwasi tena, wewe daima huwa na wasiwasi mwingi sana, bila kujali ufunuo au nuru ya mapenzi Yangu ndani yako. Usifanye hivyo tena. Fanya ushirika zaidi na Mimi kuhusu jambo lolote ili kuepuka mateso kutoka kwa matendo yako mwenyewe.

Labda kwa juu inaonekana kama Mimi ni vuguvugu kwa kila mtu, lakini je, unajua kile Ninachofikiria ndani? Mimi daima Ninawainua wanyenyekevu juu kabisa, na daima Ninawaleta chini wale ambao wanajipenda, wanaojikweza. Wale wasioelewa mapenzi Yangu watapoteza sana. Lazima ujue kwamba hiki ndicho Nilicho, ni tabia Yangu—hakuna anayeweza kukibadilisha, hakuna mtu anayeweza kukielewa vizuri. Ni kwa njia ya ufunuo Wangu tu ndiyo unaweza kuelewa, vinginevyo hutakielewa vizuri kabisa pia; usiwe mwenye kiburi. Ingawa watu wengine wanaweza kuzungumza vizuri, mioyo yao huwa sio ya uaminifu Kwangu kamwe, daima kunipingana kisiri; Nitamhukumu mtu wa aina hii.

Usilenge tu kufuata nyayo za wengine, unapaswa kuzingatia mwelekeo Wangu na tabia Yangu. Ni kwa njia hii tu ndiyo hatua kwa hatua utapata kuelewa mapenzi Yangu; vitendo vyako basi vitapatana na mapenzi Yangu na hutafanya makosa. Usilie wala kuwa na huzuni; Naona wazi kila kitu unachofanya, tabia yako yote na yote unayofikiria, na Ninajua matakwa yako na matamanio yako ya dhati; Nitakutumia wewe. Sasa ni wakati muhimu, wakati wa kukujaribu umefika. Je, bado hujaona? Je, bado hajatambua? Kwa nini Nachukua mtazamo kama huu kwako? Je, unajua? Nimekufichulia mambo haya na wewe una ufahamu mdogo. Lakini usiache—endelea kukazana na kuingia kwako na Nitaendelea kukupa nuru. Je, umegundua kwamba kadiri unavyotii na kunisikiza zaidi, ndivyo unavyong’aa zaidi ndani na ndivyo unavyokuwa na ufunuo zaidi ndani? Na ndivyo unavyokuwa na maarifa zaidi kunihusu na ndivyo unavyopata uzoefu zaidi? Usishikilie kwa uthabiti kila mara dhana zako mwenyewe kwani kufanya hivi kutaziba mtiririko wa maji Yangu ya uhai na kuzuia kutekelezwa kwa mapenzi Yangu. Lazima ujue kwamba kumpata mtu mmoja kikamilifu si jambo rahisi. Usifikiri kwa njia ya utata. Fuata tu, na usifikirie tena!

Iliyotangulia: Sura ya 45

Inayofuata: Sura ya 47

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp