Sura ya 47

Mwenyezi Mungu mwenye haki—mwenye Uweza! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo halijawahi kufumbuliwa na binadamu, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndiye fumbo ambalo limefichuliwa, Wewe ni Mungu wa vitendo Mwenyewe; kwa kuwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na tuionapo nafsi Yako, tunaona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho. Kweli hiki ni kitu ambacho hakuna mtu angeweza kuwaza! Wewe uko miongoni mwetu leo, hata ndani yetu, karibu sana nasi; haliwezi kuelezeka! Fumbo lililo ndani ya hili ni lisilo na kifani!

Mwenyezi Mungu amekamilisha mpango Wake wa usimamizi. Yeye ndiye Mfalme mshindi wa ulimwengu. Vitu vyote na mambo yote yanadhibitiwa mikononi Mwake. Watu wote wanapiga magoti katika ibada, wakiliita jina la Mungu wa kweli—Mwenyezi. Kwa maneno kutoka katika kinywa Chake, mambo yote yanafanyika. Kwa nini ninyi ni wazembe sana, msiweze kujielekeza kwa bidii kufanya kazi pamoja na Yeye, kujiunga kwa karibu na Yeye, na kwenda na Yeye katika utukufu? Inawezekana kuwa mko tayari kuteseka? Mko tayari kutupwa nje? Je, ninyi mnafikiri kwamba Sijui ni nani anayejitolea kwa dhati Kwangu, na ni nani ambaye amejitumia kwa dhati kwa ajili Yangu? Ujinga! Wapumbavu! Hamwezi kufahamu nia Zangu, na sembuse kuweza kuidhukuru mizigo Yangu, daima mkinifanya Niwe na wasiwasi kuwahusu, daima mkinifanya nijitahidi kwa ajili yenu. Je, hili litaisha lini?

Kuishi kwa kunidhihirisha Mimi katika kila kitu, kunishuhudia katika kila kitu—je, kufanya hivyo sit u jambo la kufungua midomo yenu na kutunga maneno machache pamoja? Hamjui tofauti kati ya mema na maovu! Hamko na Mimi katika kile mnachofanya, na sembuse Mimi kuwepo katika maisha yenu ya kila siku. Najua kuwa ninyi hamchulii kumwamini Mungu kuwa jambo la uzito, hivyo haya ndiyo matunda mnayozaa! Bado hamko macho, na mkiendelea hivi, mtaliaibisha jina Langu.

Jiulize, unapozungumza, je, Niko pale na wewe? Unapokula au kuvaa nguo zako, je, kuna ahadi Yangu hapo? Kweli, ninyi ni msiojali! Kila wakati ambapo matatizo yako hayakemewi moja kwa moja, basi unaonyesha jinsi ulivyo kweli, na hakuna yeyote kati yenu aliye msikivu. Isingekuwa hivyo, ninyi mngejiona kuwa wakuu na kufikiri kwamba mnamiliki vitu vingi ndani yenu. Je, hamjui kuwa ndani yenu, kilichowajaza ninyi, ni sura ya uovu ya Shetani? Fanyeni kazi na Mimi ili kumwaga vitu hivi vyote nje. Acha kile Nilicho na kile Nilicho nacho kikae ndani yako kabisa; ni hivyo tu ndivyo unaweza kuishi kwa kunidhihirisha Mimi, unishuhudie kwa uhalisi zaidi, na muwe sababu inayowafanya watu zaidi watii mbele ya kiti Changu cha enzi. Lazima mjue mzigo ulio mabegani mwenu ni mzito kiasi gani: kumtukuza Kristo, kumdhihirisha Kristo, kumshuhudia Kristo, ili watu wengi wapate wokovu kwamba ufalme Wangu uweze kusalia imara na usiotikisika. Ninataja haya yote ili kwamba msiboronge tu, bila ya kuelewa umuhimu wa kazi ya leo.

Kutojiweza mnapokabiliwa na matatizo, kama siafu kwenye kikaango kimoto, wakizunguka huku na kule: hii ndiyo tabia yenu. Kwa nje, mnaonekana kama watu wazima, lakini maisha yenu ni yale ya mtoto; kile mnachojua kufanya ni kusababisha usumbufu tu na kuongezea juu ya mzigo Wangu. Ikiwa kuna kitu kidogo zaidi ambacho Sijishughulishi nacho, ninyi husababisha usumbufu. Je, hilo si kweli? Msiwe wenye kujidai. Ninachosema ni ukweli. Msifikirie daima kwamba daima Ninawakaripia bila kukoma, kana kwamba Nilikuwa natumia maneno ya kifahari tu; hii ndiyo hali yenu halisi.

Iliyotangulia: Sura ya 46

Inayofuata: Sura ya 48

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp