Je, Dhana ya Utatu Inaweza Kutetewa?

23/04/2023

Tangu Bwana Yesu mwenye mwili alipofanya kazi ya Enzi ya Neema, kwa miaka 2,000, Ukristo wote umemfafanua Mungu mmoja wa kweli kama “Utatu.” Kwa kuwa Biblia inataja Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wamechukulia kwamba bila shaka Mungu ni Utatu. Kuna mjadala fulani, lakini watu wengi wameunga mkono dhana ya Utatu bila mabadiliko yoyote. Watu wengine husema “Utatu,” na wengine husema “Watatu katika Mmoja,” mambo ambayo kimsingi ni sawa, na humaanisha kitu kimoja. Tukisema “Utatu” au “Watatu katika Mmoja,” ni kusema kwamba Mungu ana sehemu tatu ambazo ni Mungu Wanapokuwa pamoja, na bila sehemu moja, Wao si Mungu mmoja wa kweli. Wanaweza tu kuwa Mungu mmoja wa kweli wanapokuwa pamoja. Kusema hivyo ni dhihaka kabisa. Je, unaweza kusema kweli kwamba Yehova Mungu si Mungu mmoja wa kweli? Au kwamba Bwana Yesu si Mungu mmoja wa kweli? Je, Roho Mtakatifu si Mungu mmoja wa kweli? Je, dhana hii ya Utatu si njia tu ya kumkana na kumwaibisha Mungu mmoja wa kweli? Je, huku si kumgawanya katika vipande na kumkufuru Mungu mmoja wa kweli? Tunaweza kuona jinsi dhana hii ya Utatu ilivyo ya kipumbavu kabisa. Kwa namna hiyo tu, ulimwengu wa kidini umemfafanua Mungu mmoja wa kweli kama Utatu, ukimgawanya wakati huu wote. Hili ni jambo la kuumiza sana kwa Mungu. Ulimwengu wa kidini unashikilia hili kwa ukaidi na umekataa kubadilika muda huo wote. Sasa Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho Amekuja kufanya kazi ya hukumu, na kuonyesha ukweli wote unaowaokoa wanadamu. Amefichua kabisa uwongo mkubwa zaidi wa Ukristo—Utatu. Jambo hili limefungua macho yetu na tunamsifu Kristo kwa dhati kama njia, ukweli, na uzima, na kusifu hekima ya Mungu na uweza Wake. Mungu asingefunua uongo huu moja kwa moja, tusingeweza kamwe kugundua upuuzi ulio ndani ya dhana ya Utatu. Hebu tuangalie hili kwa makini kwa kusoma baadhi ya maneno ya Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba ‘Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.’ Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati huo huo awe ndani na juu ya ulimwengu. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. … Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?). Maneno ya Mungu ni dhahiri na yana busara. Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na kuna Roho mmoja tu wa Mungu, nafsi moja katika Mungu huyu. Hakuna kabisa nafsi tatu za Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Kabla ya Mungu kuwa mwili kama Bwana Yesu, Mwana hakutajwa. Kulikuwa tu na Roho wa Mungu, ambaye ni Roho Mtakatifu. Mungu alipoumba mbingu, dunia, na vitu vyote, viliumbwa kupitia maneno ya Roho Wake, kwa hivyo si Roho wa Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli? Mungu alipofanya kazi ya Enzi ya Sheria, Aliwatumia wanadamu moja kwa moja. Anayedaiwa kuwa “Mwana” hakuwa wakati huo, lakini Mungu alikuwa Mungu mmoja tu, Muumba. Hakuna aliyewahi kusema kuwa Mungu alikuwa Utatu, na Roho Mtakatifu hakuwahi kutoa ushuhuda kwa Utatu. Kwa hivyo kwa nini watu walianza kumfafanua Mungu kama Utatu mara alipopata mwili, na kuja kama Bwana Yesu? Bwana Yesu alikuwa Roho wa Mungu aliyevaa mwili, na kazi Yake yote iliongozwa na kuonyeshwa moja kwa moja na Roho wa Mungu. Roho aliyekuwa ndani ya Bwana Yesu ni Roho wa Yehova—yaani Roho Mtakatifu. Hivyo Bwana Yesu ndiye Mungu mmoja wa kweli? Ndiyo. Kwa hivyo, si kwamba Mungu aligawanyika katika sehemu tatu—Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu—kwa sababu Alipata mwili, bali watu walisisitiza kumgawanya Mungu kwa sababu hawaelewi kiini cha kupata mwili. Hili ni kosa la kibinadamu, na ni kwa sababu uwezo wa wanadamu wa kuelewa ni mdogo. Mungu ni Mungu mmoja wa kweli. Kuna Mungu mmoja tu na ana Roho mmoja. Alikuwa Mungu mmoja wa kweli kabla ya kupata mwili, na anasalia kuwa Mungu mmoja wa kweli baada ya kupata mwili. Watu walimgawanya Mungu katika sehemu tatu, nafsi tatu kwa sababu Alifanyika mwili, jambo ambalo kimsingi ni kumgawanya Mungu na kumkana Mungu mmoja wa kweli. Je, huo si upumbavu? Je, inaweza kuwa kwamba Alipoumba ulimwengu, hakuwa Mungu mmoja wa kweli? Au kwamba wakati wa Enzi ya Sheria, hakuwa Mungu mmoja wa kweli? Kwa nini Mungu mmoja wa kweli alikuwa Mungu wa Utatu baada ya Yeye kuonekana na kufanya kazi katika mwili katika Enzi ya Neema? Je, hili si kosa lililoletwa na upumbavu na upuuzi wa binadamu? Kama dhana ya Utatu ingekuwa sahihi, kwa nini Mungu hakutoa ushuhuda kwa nafsi Zake tatu alipoumba ulimwengu? Na kwa nini hakuna mtu yeyote aliyetoa ushuhuda kwa hili wakati wa Enzi ya Sheria? Kwa nini hakuna ushuhuda wowote katika Ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu Utatu? Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na hakika kwamba Roho wa Mungu, Roho Mtakatifu, Baba, na Mwana hawajawahi kutoa ushuhuda kwamba Mungu ni Utatu. Wanadamu wapotovu na ulimwengu wa kidini ulitunga nadharia hii ya kipuuzi ya Utatu karne kadhaa baada ya kazi ya Bwana Yesu katika mwili. Ni wazi kwamba wazo la Utatu halikubaliki kabisa, na ni fikira na dhana za kibinadamu tu. Ni uwongo mkubwa zaidi wa ulimwengu wa kidini katika miaka yote 2,000, ambao umewapotosha na kuwadhuru watu wengi.

Sasa, unaweza kujiuliza ni kwa nini Roho Mtakatifu alitoa ushuhuda kwamba Bwana Yesu alikuwa “Mwana mpendwa” na kwa nini Bwana Yesu alimwita Mungu aliye mbinguni “Baba” katika maombi Yake? Hayo yana maana gani? Hebu tuangalie kile ambacho Mwenyezi Mungu amesema kuhusu swali hili. Mwenyezi Mungu anasema, “Aidha kuna wale wasemao, ‘je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?’ Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, ‘Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani yangu,’ hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?). “Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amevaa mwili wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mtu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa ‘Mwana wa Adamu’ jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. … Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?). Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba Roho Mtakatifu kumwita Bwana Yesu Mwana mpendwa ni Mungu aliyekuwa akitoa ushuhuda wa kupata mwili Kwake kutoka kwa mtazamo wa Roho. Roho Mtakatifu asingefanya hivi, hakuna ambaye angejua utambulisho wa kweli wa Bwana Yesu. Kwa hivyo ushuhuda huu wa wazi uliwaruhusu watu kujua kwamba Bwana Yesu alikuwa kupata mwili kwa Mungu. Na Bwana Yesu alimwita Mungu aliye mbinguni Baba alipoomba kwa sababu katika mwili, Hakuwa wa rohoni, bali aliishi na ubinadamu wa kawaida na Alihisi kama mtu wa kawaida. Ndiyo maana alimwita Roho wa Mungu aliye mbinguni Baba, Akisimama mahali pa kiumbe aliyeumbwa. Kuomba kwa njia hii kulikuwa mfano halisi wa unyenyekevu na utiifu wa Kristo. Lakini kulingana na sala za Bwana Yesu kwa Baba, ulimwengu wa kidini ulimgawanya Mungu katika sehemu mbili, na kusema Yesu na Yehova walikuwa na uhusiano wa baba na mwana. Upuuzi ulioje! Filipo, mwanafunzi wa Bwana Yesu, alimwuliza juu ya hili, akisema, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hiyo itatutosha” (Yohana 14:8). Jibu lake lilikuwa lipi? Bwana alisema, “Nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi?(Yohana 14:9-10). Pia alisema, Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja(Yohana 10:30). Bila shaka, Baba na Mwana ni Mungu mmoja, na hawana uhusiano wa baba na mwana jinsi watu wanavyofikiri. Wazo hili la Baba na Mwana lilitukia tu kwa sababu Mungu alipata mwili, na linatumika tu wakati Wake wa kufanya kazi katika mwili. Punde tu kazi ya Mungu katika mwili ilipofikia tamati, Alipata tena umbo Lake la asili na hapakuwa tena na kitu kama Baba na Mwana.

Hebu tuangalie kifungu kingine cha maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo. Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?). Kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaweza kuona kwamba Mungu ni Roho, ambaye ni Roho Mtakatifu. Yeye ni mwenye enzi; Aliumba mbingu, nchi, na vitu vyote, na Hutawala kila kitu. Anaweza kuwa mwili kwa ajili ya kazi Yake na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa njia ya vitendo. Anaonekana kama mtu wa kawaida kutoka nje, lakini kazi Yake yote huongozwa na Roho wa Mungu. Kazi Yake katika mwili inapokamilika, Mungu hupata tena umbo Lake la asili. Umbo la mwili ni jinsi Mungu anavyoonekana kwa wanadamu wakati wa awamu ya kazi Yake. Na kwa hivyo, Mungu afanye kazi moja kwa moja kwa Roho, au Afanye kazi katika mwili, Aitwe Yehova, Yesu, au Mwenyezi Mungu, Yeye ni Roho yule yule. Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anaishi kwa kujitegemea Mwenyewe na ni wa milele, na Aliumba na hutawala vitu vyote. Sasa katika ushirika wetu, nadhani kila mtu anaelewa vyema kwamba kuna Mungu mmoja tu, Mungu mmoja wa kweli. Hakuna mashaka kabisa. Ukristo unashikilia kwamba Mungu mmoja wa kweli ni Utatu, ukisisitiza kumgawanya Mungu katika sehemu tatu, na kueneza imani kwamba Wakiwa watatu pekee kwa pamoja ndiyo wanafanyika Mungu mmoja wa kweli, na Wakiwa tofauti, Wao si Mungu mmoja wa kweli. Je, huku si kumkana Mungu kwa kweli? Binadamu kutomwelewa Mungu kabisa kunathibitisha kwamba hawaelewi Biblia hata kidogo au kujua kiini cha Mungu, na wana kiburi cha ajabu katika jinsi wanavyoelewa maudhui halisi ya Biblia, na wanamwekea Mungu mipaka na kumgawanya kulingana na dhana na mawazo ya wanadamu. Huku kwa hakika ni kumpinga na kumkufuru Mungu.

Na sasa, Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho amekuja, Ameonyesha ukweli ili kufanya kazi Yake, na Amefichua uongo mkubwa zaidi wa ulimwengu wa kidini—Utatu. Sasa tuna hakika kwamba Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli. Roho Wake ndiye Mungu mmoja wa kweli, Roho Mtakatifu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na kupata mwili Kwake ni Mungu mmoja wa kweli. Akiwa Roho Wake, akiwa Roho Mtakatifu, na katika kupata mwili Kwake, Yeye ndiye Mungu mmoja wa kweli na Yeye ni Mungu mmoja. Hawezi kutenganishwa. Iwapo watu hawawezi kukubali ukweli huu lakini wanashikilia kwa ukaidi dhana na mawazo yao, wakisisitiza kuamini Utatu, kumwona Mungu mmoja wa kweli kuwa ni Miungu watatu, hiyo ni dhambi ya kumlaani na kumkufuru Mungu. Kumkufuru Roho wa Mungu ni kumkufuru Roho Mtakatifu, na hakuna anayeweza kustahimili matokeo ya hilo. Wenye busara wana nafasi ya kuamka bila kuchelewa na kuacha kung'ang'ania mtazamo huu usio sahihi ili kuepuka kufanya makosa ya kwenda kinyume na Mungu. Bwana Yesu alisema, “Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja(Mathayo 12:31-32). Ulimwengu wa dini bado unasisitiza kwa ukaidi uongo huu wa Utatu. Wataendelea kumpinga Mungu hadi lini? Ni wakati wa kuamka. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika miaka hii yote, nyinyi mmegawanya Mungu namna hii, na kuendelea kugawanywa zaidi katika kila kizazi kiasi kwamba Mungu mmoja amegawanywa kuwa Mungu watatu. Na sasa haiwezekani kabisa kwa mwanadamu kumuunganisha Mungu kuwa mmoja kwani mmemgawanya zaidi. Ingekuwa si kazi yangu ya upesiupesi kabla ya muda kuyoyoma, haijulikani mngeishi hivi kwa muda gani! Kuendelea kumgawanya Mungu namna hii, Anawezaje kuendelea kuwa Mungu wenu? Je, bado mngeendelea kumtambua Mungu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?). “Je, mantiki yako yaweza kuichangua kazi ya Mungu? Je, waweza kupata utambuzi wa kazi yote ya Yehova? Je, ni wewe kama mwanadamu uwezaye kubaini yote, au ni Mungu Mwenyewe awezaye kuona kutoka milele hadi milele? Je, ni wewe mwanadamu uwezaye kuona tangu milele ya zamani sana hadi milele ijayo, au Mungu ndiye Ana uwezo wa kufanya hivyo? Unasema nini? Unafaa vipi kumweleza Mungu? Maelezo yako yametegemezwa katika misingi gani? Wewe ni Mungu? Mbingu na dunia, na vyote vilivyomo viliumbwa na Mungu Mwenyewe. Si wewe uliyelifanya hili, basi ni kwa nini unatoa maelezo yasiyo sahihi? Sasa, unaendelea kuamini katika utatu mtakatifu? Hufikirii kuwa huu ni mzigo mkubwa kwa njia hii? Itakuwa bora kwako kuamini katika Mungu mmoja, si watatu. Ni bora zaidi kuwa mwepesi, kwani mzigo wa Bwana ni mwepesi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?).

Iliyotangulia: Kupata Mwili Ni Nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Hamjambo ndugu. Tumebahatika sana kukusanyika pamoja—mshukuruni Bwana! Sisi sote ni watu tunaopenda kusikiliza maneno ya Mungu na...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp