Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

23/04/2023

Hamjambo ndugu. Tumebahatika sana kukusanyika pamoja—mshukuruni Bwana! Sisi sote ni watu tunaopenda kusikiliza maneno ya Mungu na tunatamani kumkaribisha Bwana. Leo, tutashiriki kidogo kuhusu unabii wa Bwana Yesu na kujadili welewa mbalimbali kuhusu kurudi kwa Bwana. Watu wengi sana wamefafanua kurudi kwa Bwana kama tu kushuka Kwake juu ya mawingu, lakini kulingana na unabii wa Bwana Yesu mwenyewe katika Biblia, Atarudi na kutamka maneno kama Mwana wa Adamu. Bwana alitabiri mara kadhaa kuja, au kuonekana kwa Mwana wa Adamu, na kuja kwa Mwana wa Adamu kunahusu Mungu kuonekana na kufanya kazi katika mwili. Hii pekee ndiyo tafsiri safi zaidi, na pana uwezekano mdogo sana wa kuisikia katika kanisa la kidini. Kuja au kuonekana kwa Mwana wa Adamu ni fumbo kuu, ambalo hakuna ambaye angeweza kulijua pasipo tayari kukaribisha kuonekana Kwake na kazi Yake.

Kuna unabii mwingi unaohusu kurudi kwa Bwana katika Biblia, lakini kiasi kikubwa cha unabii huu ulitoka kwa wanadamu, kama vile mitume au manabii, au kutoka kwa malaika. Unabii ambao watu hupenda kutaja ni ule uliotokana na wanadamu, na hivyo wanatamani kumuona Bwana akishuka juu ya mawingu hadharani. Lakini kwa kweli, kurudi kwa Bwana ndiyo siri iliyotunzwa vizuri zaidi. Bwana Yesu alisema, “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu(Mathayo 24:36). Kwa kuwa hakuna ajiuaye siku hiyo au saa hiyo, hata malaika wa mbinguni au Mwana, je, unabii wowote wa Biblia wa kurudi kwa Bwana uliotolewa na wanadamu au malaika unaweza kuwa sahihi? Hauwezi hata kidogo. Na kwa hivyo, iwapo tunataka kumkaribisha Bwana, lazima tufuate unabii wa Bwana Yesu mwenyewe. Hilo ndilo tumaini letu la pekee la kumkaribisha Bwana. Hivyo, wale wanaomngoja Bwana ashuke juu ya mawingu waziwazi hawana budi kufa katika maafa, wakilia na kusaga meno. Bwana Yesu alisema, “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:24-25). “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote ... bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo 2:7). “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Tunaweza kuona nini katika unabii huu kutoka kwa Bwana Yesu? Maneno ya Bwana yanatuambia wazi kwamba Anarudi katika siku za mwisho kama Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu kwa kweli ni kupata mwili, na kimsingi Atatamka maneno, Ataonyesha ukweli, na kuwaongoza wateule wa Mungu kuingia katika ukweli wote. Bwana atatimiza kazi gani kwa kuja na kuonyesha ukweli? Bila shaka, ni kufanya kazi ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu, ambayo inathibitisha zaidi kwamba Mungu hufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho kwa kuonyesha ukweli. Basi, tunawezaje kumkaribisha Bwana? Kwa kuwa Anakuja kama Mwana wa Adamu, na Mwana wa Adamu ana sura ya kawaida kabisa bila kitu cha wazi cha kimwujiza, hakuna atakayeweza kuona kwamba huku ni kuonekana kwa Mungu kutokana na sura Yake ya nje tu. Jambo la muhimu ni kusikiliza matamshi ya Mwana wa Adamu na kuona iwapo hii ni sauti ya Mungu. Kumkaribisha Bwana kunafanikishwa na kuitambua sauti ya Mungu na kumfungulia mlango. Akitamka ukweli na watu wasikie lakini wasiitambue sauti Yake, hawatakuwa na njia ya kumkaribisha. Imetabiriwa tena na tena katika Kitabu cha Ufunuo “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Revelation Chapters 2, 3). Hili limetajwa mara saba kwa jumla. Hivyo, ili kumkaribisha Bwana, kuisikia sauti ya Mungu ni muhimu kabisa; hii ndiyo njia pekee ya kumkaribisha. Je, sasa unajua msingi wa kumkaribisha Bwana ni nini? Hiyo ni kweli—ili kumkaribisha Bwana, hatuna budi kabisa kutafuta kusikia sauti ya Mungu, na “sauti” hii inataja ukweli ulioonyeshwa na Bwana aliyerudi, ukweli wote ambao watu hawajawahi kusikia hapo awali na mambo ambayo hayakuwahi kurekodiwa katika Biblia. Wanawali wenye busara wanasikia kwamba maneno yote yaliyoonyeshwa na Mwana wa Adamu ni ukweli, yote ni sauti ya Mungu na, wakiwa na furaha mno, wanamkaribisha Bwana. Ni Bwana pekee ndiye anayeweza kuonyesha ukweli; Bwana pekee ndiye njia, na kweli, na uzima. Yeyote anayesikia maneno yaliyoonyeshwa na Mwana wa Adamu bali asalie mwenye kutojali au kuyapuuza, au kukataa kukubali ukweli, ni mwanamwali mpumbavu ambaye ataachwa na Bwana. Hakika atatambukia katika maafa makubwa, akilia na kusaga meno. Kufikia sasa, ulimwengu wa kidini haujamkaribisha Bwana; badala yake, wameshindwa kwenye maafa, wakimlaumu na kumkana Mungu, daima wakiwa katika hali ya kukata tamaa. Wale ambao ni kondoo wa Mungu hutafuta na kuchunguza njia ya kweli kwa hamu baada ya kusikia sauti ya Mungu, hilo likiwaruhusu kumkaribisha Bwana. Kwa hivyo ni lazima tuelewe: Bwana anaporudi katika siku za mwisho, Anaonekana kama Mwana wa Adamu na kuonyesha ukweli wote, na la muhimu kwetu katika kutafuta kuonekana kwa Bwana ni kutafuta mahali ambapo ukweli huu wote ulioonyeshwa na Bwana upo, kutafuta kanisa ambamo Mungu anazungumza. Mara utakapogundua ukweli ulioonyeshwa na Mwana wa Adamu, utaweza kupata kuonekana kwa Mungu na kazi Yake kwa kufuata sauti hiyo hadi kufikia chanzo chake. Mara utakapogundua kwamba ukweli wote ulioonyeshwa na Bwana ndio utakaowatakasa na kuwaokoa wanadamu, utakubali kurudi kwa Bwana, na kisha utakuwa umemkaribisha. Hii ndiyo njia bora, na njia rahisi ya kumkaribisha Bwana. Hakuna haja ya kusimama ukikodolea macho anga, wala hakuna haja ya kusimama juu ya kilele cha mlima ili kumkaribisha Bwana anaposhuka juu ya mawingu, sembuse kusali kila wakati, au kufunga na kuomba. Unahitaji tu kukesha na kungoja, na kamwe usiache kutafuta kusikia sauti ya Mungu.

Sasa, baadhi yenu mnaweza kuwa mkijiuliza: Basi tunawezaje kutambua kile tunachosikia kama ni sauti ya Mungu? Kwa kweli, kusikia sauti ya Mungu si jambo gumu hata kidogo. Bwana Yesu alisema, “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). Kila unaposikia mtu akitoa ushuhuda wa kuonekana kwa Mungu na kazi Yake, au kwamba Ameonyesha ukweli, lazima uchunguze jambo hili mara moja na uone ikiwa maneno haya yanayodaiwa kusemwa na Mungu ni ukweli au la. Iwapo ni ukweli, unapaswa kuyakubali, kwa sababu kondoo wa Mungu wanaweza kusikia sauti Yake. Hili ni jambo lililoamuliwa awali na Mungu, na halitegemei jinsi mtu alivyoelimika, jinsi anavyoijua Biblia vizuri, au kina cha uzoefu wake. Kama Wakristo, tunahisi vipi tunaposikia maneno mengi yaliyonenwa na Bwana Yesu? Hata bila uzoefu au ufahamu wowote kuhusu maneno ya Bwana, punde tunapoyasikia tunaweza kuhisi kwamba ni ukweli, kwamba yana mamlaka na uwezo; tunaweza kuhisi kwamba ni ya maana sana na ya ajabu, kushinda ufahamu wa binadamu—hili ndilo jukumu la msukumo na welewa. Iwe kwamba tunaweza kuonyesha hili kwa uwazi au la, hisia hii ni sahihi, na inatosha kuonyesha kwamba ikiwa mtu ana moyo na nafsi, anaweza kuhisi nguvu na mamlaka ya maneno kutoka kwa Mungu. Hivyo ndivyo kusikia sauti ya Mungu kulivyo. Ili kuchunguza hili zaidi, maneno ya Mungu yana sifa gani nyingine? Maneno ya Mungu hutupa riziki ya maisha; hufunua mafumbo, yanafungua enzi mpya na kutamatisha enzi ya kale. Kama tu Bwana Yesu alivyoweza kuonyesha ukweli wakati wowote na mahali popote ili kuwachunga, kuwanyunyizia, na kuwaruzuku watu; Bwana pia alifichua mafumbo ya ufalme wa mbinguni, Aliwaleta wanadamu kwenye njia ya toba katika ufalme wa mbinguni, Akafungua Enzi ya Neema, Akaitamatisha Enzi ya Sheria, na kukamilisha kazi ya kuwakomboa wanadamu. Hili lilikuwa jambo ambalo hakuna mwanadamu angeweza kulitimiza. Je, si hivyo? Hivyo basi, siku hizi, kuna Mwana wa Adamu ambaye amekuwa Akitamka maneno kwa miaka mingi na kuonyesha ukweli mwingi. Watu wengi wamehisi baada ya kusoma maneno haya kwamba ni matamshi ya Roho Mtakatifu, sauti ya Mungu, na wamehakikisha kwamba Mwana wa Adamu huyu ambaye Anaonyesha ukweli ndiye Bwana Yesu aliyerudi, kwamba Yeye ni Mwenyezi Mungu katika mwili. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli wote unaohitajika kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, Amefichua mafumbo ya mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu, na kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Ameanzisha Enzi ya Ufalme na kutamatisha Enzi ya Neema. Je, kila mtu anataka kusikia baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu, ili kusikia sauti ya Mungu? Hebu tusome vifungu vichache vya matamshi ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”). “Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu, kana kwamba mtoto mchanga amezaliwa hivi karibuni. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye ‘Mlima wa Mizeituni’ wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni ‘mtoto mchanga’ Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni). “Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Je, kila mtu anahisi vipi sasa, baada ya kusikiliza baadhi ya vifungu vya maneno ya Mwenyezi Mungu? Je, hii ni sauti ya Mungu? Kila sentensi ya maneno ya Mwenyezi Mungu ina nguvu na mamlaka, na huwashtua watu sana. Ni nani kando na Mungu anayeweza kuhutubia wanadamu wote? Ni nani awezaye kuonyesha mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu? Ni nani anayeweza kufichua wazi mpango na mipangilio ya Mungu ya kazi Yake katika siku za mwisho na vilevile matokeo na hatima ya mwanadamu mapema? Ni nani awezaye kufanya amri za usimamizi wa Mungu zijulikane ulimwenguni kote? Kando na Mungu, hakuna mtu anayaweza kufanya mambo haya. Matamshi ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wote yanaturuhusu tuhisi mamlaka na uwezo wa maneno ya Mungu. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni matamshi yatokayo moja kwa moja kwa Mungu, sauti ya Mungu Mwenyewe! Maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ni kama tu Mungu kusimama juu mbinguni Akiutazama ulimwengu wote na kuzungumza. Mwenyezi Mungu anazungumza na wanadamu kutoka katika nafasi Yake kama Bwana wa vyote vilivyoumbwa, Akiwafichulia wanadamu tabia ya Mungu ya haki na adhimu ambayo haitavumilia kosa lolote. Ingawa huenda wasielewe ukweli ulio ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu au hawana na uzoefu au ufahamu wowote halisi wanapoyasikia kwa mara ya kwanza, wote ambao ni kondoo wa Mungu bado watahisi kwamba kila neno kutoka kwa Mwenyezi Mungu limejaa nguvu na mamlaka na kuwa na hakika kwamba hii ni sauti ya Mungu na inatoka moja kwa moja kwa Roho wa Mungu. Hii inatimiza maneno ya Bwana Yesu, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27).

Sasa tumeisikia sauti ya Mungu na kuona ukweli ulioonyeshwa na Mungu, kwa hivyo Mungu amekuja kufanya kazi gani kwa kuonyesha ukweli? Amekuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, jambo ambalo linaweza kuthibitishwa na unabii kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe. “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana(Yohana 5:22). “Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:27). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote … na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Na hatuwezi kusahau Sura ya 4, Mstari wa 17 wa kitabu cha kwanza cha Petro: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu”. Unabii huu wote upo wazi kabisa. Hukumu katika siku za mwisho itaanza na nyumba ya Mungu, na itatekelezwa miongoni mwa wote ambao wamekubali kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Yaani, Mwana wa Adamu mwenye mwili ataonyesha ukweli duniani ili kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu, na kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika ukweli wote. Hii ndiyo kazi ya hukumu inayofanywa na Mwokozi katika siku za mwisho, kazi ambayo ilipangwa na Mungu zamani sana. Sasa Mwenyezi Mungu, Mwana wa Adamu katika mwili, Alikuja kitambo sana, Akaonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu, Akiutikisa ulimwengu mzima, Akitikisa dini na sekta zote. Watu wengi zaidi na zaidi wanatii sauti ya Mungu, wakitafuta na kuchunguza njia ya kweli. Mwenyezi Mungu hajafichua tu mafumbo yote makuu ya mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu na kutuambia mafumbo ya ukweli kama vile malengo ya Mungu katika usimamizi Wake wa wanadamu, jinsi Anavyotekeleza hatua Zake tatu za kazi ya kuwaokoa wanadamu, mafumbo ya kupata mwili, na hadithi ya kweli kuhusu Biblia; zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu pia amefichua ukweli wa jinsi ambayo wanadamu wamepotoshwa na Shetani na asili yetu ya kishetani ya kumpinga Mungu, huku Akituonyesha njia ya vitendo ya kuondokana na tabia zetu potovu na kuokolewa kikamilifu. Mwenyezi Mungu pia amefichua matokeo ya kila aina ya mtu, hatima za mwisho na halisi za watu, jinsi Mungu atakavyotamatisha wa enzi, na jinsi ufalme wa Kristo utakavyoonekana. Mafumbo haya yote ya ukweli yamefunuliwa kwetu. Mwenyezi Mungu Ametamka mamilioni ya maneno, na maneno haya yote ni ukweli unaotumiwa kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu. Hii ndiyo kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho. Ni hatua moja ya kazi kupitia maneno pekee ya kuwatakasa kabisa na kuwaokoa wanadamu.

Hivyo basi, Mwenyezi Mungu hutumia vipi ukweli kukamilisha kazi ya hukumu? Hebu tuangalie maneno Yake yanasema nini. Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). “Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Baada ya kusoma maneno ya Mungu inapaswa kuwa wazi kwamba kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kimsingi kwa kuonyesha ukweli, kutumia ukweli kuwahukumu, kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Yaani, katika siku za mwisho, Mungu huwatakasa upotovu wa binadamu kupitia kazi Yake ya hukumu, Anaokoa na kukamilisha kundi la watu, na kufanyiza kundi la wale walio na moyo mmoja na nia moja na Mungu: matokeo ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka 6,000. Hapa ndipo lengo la kazi ya hukumu ya siku za mwisho lilipo! Hii ndiyo sababu Mwokozi, Mwenyezi Mungu, amekuwa Akionyesha ukweli tangu Alipokuja, Akifichua na kuhukumu tabia potovu ya kila aina ambayo watu wanayo. Pia Amekuwa akitakasa na kubadilisha tabia zetu potovu kwa kutupogoa na kutushughulika, kwa kutujaribu na kutusafisha; hii inasuluhisha chanzo kikuu cha dhambi ya mwanadamu, inaturuhusu kuacha kabisa dhambi, kuondokana na ushawishi wa Shetani, na kuweza kumtii na kumwabudu Mungu. Sasa watu wengine huenda wamechanganyikiwa kidogo, wakifikiri kwamba Bwana Yesu tayari amewakomboa wanadamu, kwa hivyo kwa nini bado Mungu anahitaji kuonyesha ukweli katika siku za mwisho ili kuwahukumu wanadamu? Hii ni kwa sababu Bwana Yesu alifanya tu kazi ya ukombozi, kumaanisha kwamba imani katika Bwana Yesu huleta msamaha wa dhambi, au kuhesabiwa haki kwa imani pekee, jambo ambalo huwawezesha watu kuja mbele za Mungu katika maombi, kuwasiliana kwa karibu na Mungu, na kufurahia neema na baraka Yake. Hata hivyo, jukumu la Bwana Yesu kama sadaka ya dhambi liliruhusu tu msamaha wa dhambi za wanadamu; halikutatua kabisa tatizo la kiini cha utenda dhambi wa mwanadamu. Haya yote ni ukweli. Hii ndiyo sababu wale wote wanaoishi katika Enzi ya Neema walikubali ukweli kwamba hata baada ya dhambi za wanadamu kusamehewa, tuliendelea kufanya dhambi kila wakati. Hatukuweza kujizuia, na ingawa tulitamani kuacha dhambi, hatukuweza kufanya hivyo. Tulikuwa tukipitia maisha tukitenda dhambi mchana, na kukikiri usiku. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu alitabiri: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote … na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Hii inataja kazi ya hukumu ya siku za mwisho ambayo Bwana Yesu atafanya Atakapokuja tena, kumtakasa wanadamu kikamilifu kutokana na tabia zao potovu na kutatua kiini cha dhambi zao. Hivi ndivyo watu wanavyoweza kuokolewa kabisa, kikamilifu. Yaani, wale wanaopitia tu ukombozi kutoka kwa Bwana Yesu bila kupitia kazi ya hukumu ya siku za mwisho wanaweza tu kutambua ni tendo lipi kati ya matendo yao ni la dhambi; hawawezi kuona chanzo kikuu cha utenda dhambi wa mwanadamu. Yaani, hawawezi kuelewa asili ya kishetani ya mwanadamu na tabia za kishetani, sembuse kuzitatua. Njia pekee ya kutatua tatizo la tabia potovu, ambalo ndilo chanzo kikuu cha utenda dhambi wa mwanadamu, ni kupitia kazi ya hukumu ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Mungu Mwenyewe amechukua umbo la mwili ili kuja na kufanya kazi ya hukumu, Akionyesha ukweli mwingi, na Anawafichua na kuwahukumu watu kwa muda mrefu. Hivi pekee ndivyo watu wanavyoweza kuona waziwazi ukweli wa upotovu wao na kutambua hali na asili zao wenyewe. Kupitia hukumu hii, watu pia wataona haki na utakatifu wa Mungu, hivyo kukuza uchaji kwa Mungu. Hivi pekee ndivyo tunavyoweza kuacha tabia zetu potovu polepole na kuishi kwa kudhihirisha mfano halisi wa binadamu. Inaweza kusemwa kwamba njia pekee ya kukamilisha hili ni Mungu mwenye mwili kuonyesha ukweli ili kutekeleza kazi ya hukumu. Hii ndiyo sababu Mwenyezi Mungu kutamka maneno, kutumia ukweli kufanya kazi ya hukumu, ni jambo la muhimu sana, na la maana sana!

Msingi wa iwapo muumini anaweza kuokolewa kikamilifu na kuwa na hatima nzuri unategemea ikiwa wanaweza kukaribisha kuonekana kwa Mungu na kazi Yake. Kwa hivyo, jambo lililo gumu kutatua ni iwapo mtu anaweza kusikia sauti ya Mungu au la. Watu wengi humwamini Bwana katika maisha yao yote, lakini hufikia upeo wa maisha yao bila kuwahi kusikia sauti ya Mungu au kumkaribisha Bwana, kumaanisha kuwa juhudi zao zote ni bure. Hii ndiyo sababu kuweza kusikia sauti ya Mungu ndio msingi wa kuamua ikiwa mtu anaweza kupata wokovu kamili na kupata hatima nzuri. Watu wengi husoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kukiri kwamba hayo ni ukweli, lakini bado hawawezi kukiri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana aliyerudi. Hii kwa kweli ni aibu, na ni matokeo ya upumbavu na upofu wa binadamu. Wale wasiomjua Bwana watatumbukia katika majanga, wakilia na kusaga meno.

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno ‘maneno’ linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kunyakuliwa ni Nini Hasa?

Miaka 2,000 iliyopita, baada ya Bwana Yesu kusulubishwa na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, Aliahidi kwamba Atarudi. Tangu wakati huo,...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp