Kwa Nini Mungu Anahitaji Hatua Tatu za Kazi Ili Kuwaokoa Wanadamu?

13/04/2023

Sote tunajua kwamba miaka 2,000 iliyopita, Bwana Yesu alionekana na kufanya kazi huko Yudea ili kuwakomboa wanadamu, na akahubiri “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). Alionyesha ukweli mwingi na kufichua ishara na maajabu mengi, akalitikisa taifa la Yudea. Viongozi wakuu wa Dini ya Kiyahudi waliona jinsi kazi na maneno ya Bwana Yesu yalivyokuwa na mamlaka na nguvu, na Alikuwa akipata wafuasi kila mara. Viongozi hawa walihisi kama kwamba kazi ya Yesu ilitishia hadhi yao, kwa hivyo walianza kujaribu kutafuta vitu vya kutumia kumpinga, wakibunui uvumi na uongo, kumshutumu Yesu, na kuwazuia watu wasimfuate. Kwa kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Adamu na hakuwa roho liliwafanya wawe wajinga zaidi na wasiojizuia. Kazi na maneno Yake kuizidi sheria ilikuwa kisingizio chao cha kumshutumu na kumfukuza kwa kishindo, na kumsulubisha msalabani. Hilo lilifanya taifa la Israeli lipate laana na adhabu ya Mungu, na maangamizo kwa miaka 2,000. Sasa Yesu amerejea katika siku za mwisho kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, Akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu ili kuwatakasa na kuwaokoa binadamu kikamilifu. Wale wanaotamani kuonekana kwa Mungu kutoka katika madhehebu yote wamesoma maneno ya Mwenyezi Mungu, wametambua sauti ya Mungu, na kumgeukia Mwenyezi Mungu. Lakini viongozi wengi wa kidini hawawezi kukubali jambo hili. Kondoo wao wazuri wameyaacha makundi na hadhi na riziki yao ipo hatarini, jambo ambalo hawawezi kustahimili. Wanatunga uwongo wa kila aina ili kukana na kushutumu kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, wakifanya kila wawezalo ili kuwapotosha waumini na kuwazuia wasiichunguze njia ya kweli. Wanasema kwamba Bwana Yesu tayari aliwakomboa wanadamu na kazi ya Mungu ya wokovu imekamilika, na Atawanyakua waumini Atakapokuja. Hakuna kazi zaidi ya wokovu. Hata wanapiga kelele: “Bwana akirudi na asituchukue katika ufalme, basi Yeye si Bwana kweli! Bwana aliye katika mwili akifanya kazi ya hukumu hawezi kabisa kuwa Bwana! Ni Bwana tu, Bwana tunayemwamini, ikiwa tutanyakuliwa!” Hasa wanapomwona Mwenyezi Mungu hayuko katika umbo la roho, bali ni Mwana wa Adamu wa kawaida, wanakuwa hata wakaidi zaidi na kumstukumu vikali na kumkufuru Yeye. Wanaungana hata na Chama cha Kikomunisti kuwakamata waumini wanaoshiriki injili. Kwa matendo yao, wamemsulubisha Mungu tena. Hebu fikiri. Kwa nini kila hatua ya kazi ya Mungu inakataliwa, kushutumiwa, na kupingwa na ulimwengu wa kidini? Ni kwa sababu binadamu wamepotoshwa sana na Shetani. Kila mtu ana asili ya kishetani; kila mtu anachukia ukweli na amechoshwa nao. Sababu nyingine ni kwamba watu hawaelewi kazi ya Mungu, hivyo wanaiona kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kuwa rahisi kuliko ilivyo kweli. Tunajua kwamba Waisraeli waliamini kwamba mara tu kazi ya Mungu ya Enzi ya Sheria ilipokamilika, wangeitii sheria tu na wangeokolewa, na kwamba Masihi atakapokuja, wangechukuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme. Na kitu gani kilitokea? Bwana Yesu alikuja na watu wa Kiyahudi wakamsulubisha. Wale kutoka katika Enzi ya Neema walifikiri kwamba kwa ukombozi wa Yesu, dhambi zao zilisamehewa na waliokolewa kabisa, hivyo wanapaswa kuchukuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme Bwana atakaporudi. Na kitu gani kilitokea? Mwenyezi Mungu amekuja na Anasulubishwa tena na ulimwengu wa kidini unaoshirikiana na utawala wa Shetani. Wanafikiri kwamba Bwana Yesu alipomaliza kazi Yake, kazi ya Mungu ya wokovu imekamilika. Lakini, je, hiyo hakika ni kweli?

Kwa kweli, kila hatua mpya ya kazi ambayo Mungu hufanya imetabiriwa muda mrefu kabla. Yesu alipokuja kwa ajili ya kazi ya ukombozi, manabii walikuwa tayari wametabiri kuja Kwake. “Bikira atapata mimba, na kuzaa mwana wa kiume, na atamwita Imanueli(Isaya 7:14). “Kwani mtoto amezaliwa kwa sababu yetu, sisi tumepewa mwana wa kiume: na mamlaka ya serikali yatakuwa juu ya bega lake: na jina lake litakuwa Wa ajabu, Mshauri, Mungu mwenye nguvu, Baba wa daima, Mfalme yule wa Amani(Isaya 9:6). Na kuhusu kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, kuna unabii mwingi sana wa kibiblia, angalau 200. Tazama kile ambacho Bwana Yesu alisema: “Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). Na Kitabu cha Petro: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Yeyote aliye na shauku ya kazi ya Mungu anaweza kupata msingi wake kwa urahisi sana, na hivyo hawatasisitiza kumsulubisha Mungu msalabani kwa ukali sana, bila kuyumbayumba. Hili pekee linaonyesha jinsi mwanadamu alivyopotoshwa sana na Shetani. Wanadamu wote wana asili ya kishetani, na ni sawa kusema kwamba wanadamu ni adui za Mungu. Sote tumeona ukweli huu: Kuanzia katika Enzi ya Sheria hadi ukombozi wa Yesu katika Enzi ya Neema, na sasa katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu akifanya kazi ya hukumu akiwa mwili ili kuhitimisha kazi ya enzi hizi, ni wazi kwamba Kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu inajumuisha hatua tatu hasa. Kwa hivyo kwa nini ni muhimu kwa kazi Yake ya wokovu kutekelezwa katika hatua tatu? Ni jambo ambalo wanadamu hawawezi kufahamu, jambo ambalo limewafanya wengi kuipinga na kuishutumu kazi ya Mungu. Madhara ya jambo hili ni makubwa. Ndiyo maana suala tunalochunguza leo ni sababu ya Mungu kutekeleza hatua tatu za kazi.

Katika siku za mwisho, kazi ya Mwenyezi Mungu imefichua mafumbo yote ya mpango Wake wa usimamizi. Hebu tusome kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu ili tuweze kuelewa jambo hili vyema zaidi. Mwenyezi Mungu anasema, “Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika hatua tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hatua hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, yaani, ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati uo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama kazi ya wokovu ilivyogawanywa katika hatua tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika hatua tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani kwa kweli ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu silo jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika hatua moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika hatua na vipindi, na vita vinapiganwa dhidi ya Shetani kulingana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. … Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, hatua tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika hatua tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizwa kupitia kwa hatua kadhaa za kazi: kumpa mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu akamilishwe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu). Tunaweza kuona kwamba kazi ya Mungu ya wokovu inafanyika katika hatua tatu. Hizo ni kazi ya Yehova Mungu katika Enzi ya Sheria, ukombozi wa Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho katika Enzi ya Ufalme. Hatua hizi tatu za kazi zinajumuisha kazi kamili ya wokovu ya Mungu, na hivi ndivyo Mungu anavyowaokoa wanadamu kutoka kwa nguvu za Shetani, hatua kwa hatua, ili tuweze kupatwa kikamilifu na Mungu. Umuhimu wa kila hatua ni mkubwa. Hii yote ni kazi isiyo na mbadala katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu, na sehemu muhimu za mchakato wa kuwaokoa wanadamu wapotovu kutoka dhambini na kutokana na nguvu za Shetani.

Jambo linalofuata, Ningependa kueleza kwa ufupi hatua tatu za kazi za Mungu kulingana na maneno Yake mwenyewe. Kwanza, hebu tuzungumze kuhusu hatua ya kwanza ya kazi ya Mungu kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu: kazi katika Enzi ya Sheria. Sote tunajua kwamba kabla ya Mungu kutekeleza kazi Yake katika Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wajinga kabisa. Hawakujua jinsi ya kumwabudu Mungu au jinsi ya kuishi maisha yao duniani. Walikuwa wakitenda dhambi kila mara na kumchukiza Mungu, na hata hawakujua dhambi ni nini. Ili kuwasaidia watu wajitenge na dhambi na kuishi ipasavyo, Mungu alianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria. Hebu tusome kifungu cha maneno ya Mungu kuhusu jambo hili. “Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. Amri hizi walipewa Waisraeli na Yehova, na hazikuwa na uhusiano kwa Wamisri: zilinuiwa kuwazuia Waisraeli. Yeye alizitumia amri kuwatolea madai. Iwapo waliishika Sabato, iwapo waliwaheshimu wazazi wao, iwapo waliziabudu sanamu, na kadhalika: hizi zilikuwa kanuni ambazo kwazo walihukumiwa kuwa wenye dhambi au wenye haki. Miongoni mwao, kuna baadhi walioangamizwa kwa moto wa Yehova, baadhi waliopigwa mawe hadi kufa, na baadhi waliopokea baraka za Yehova, na haya yaliamuliwa kulingana na iwapo walizitii amri hizi au la. Wale ambao hawakuishika Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakuishika Sabato wangeangamizwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuwaheshimu wazazi wao pia wangepigwa mawe hadi kufa. Yote haya yalikubaliwa na Yehova. Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria). Katika Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na amri nyingi, akiwafundisha wanadamu jinsi ya kumwabudu Mungu na jinsi ya kuishi maisha yao. Wale waliofuata sheria walipata ulinzi na baraka za Mungu, huku wale waliovunja sheria walipaswa kutoa dhabihu ili wasamehewe dhambi zao. Vinginevyo wangekabiliana na adhabu na laana ya Mungu. Wale wa Enzi ya Sheria waliijua haki na ghadhabu ya Mungu binafsi, waliijua tabia Yake isiyokosewa, na walijua rehema na baraka Zake. Hiyo ndiyo maana kila mtu alimwogopa Yehova Mungu na kutii sheria na amri Zake. Walilindwa na Mungu na waliishi maisha yanayofaa duniani. Sasa hebu tuwaze kuhusu jambo hili: Ikiwa Mungu hangefanya kazi Yake ya Enzi ya Sheria, ni kitu gani kingewatendekea wanadamu? Bila vizuizi vya sheria au mwongozo wa Mungu, wanadamu wote wangeanguka katika machafuko makubwa na kukamatwa na Shetani. Mungu kuwapa wanadamu sheria ilikuwa kazi muhimu sana! Kazi Yake ya Enzi ya Sheria ilimfundisha mwanadamu dhambi ni nini, na haki ni nini, na ilimwonyesha mwanadamu kwamba kutenda dhambi kunahitaji dhabihu kwa ajili ya upatanisho na Mungu. Mbali na kuwaleta wanadamu kwenye njia sahihi katika maisha yao, hatua ya kwanza ya kazi ya Mungu pia iliandaa jukwaa, ilitengeneza barabara kwa ajili ya kazi ya ukombozi ya Enzi ya Neema.

Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, binadamu wote walikuwa wamepotoshwa sana na Shetani hivi kwamba walikuwa wakitenda dhambi zaidi na zaidi, na sheria haingeweza tena kuwadhibiti. Hawakuwa na dhabihu za kutosha kutoa kwa ajili ya dhambi zao, kwa hiyo walikuwa wanakabiliwa na shutuma na kuuawa chini ya sheria, wote wakimlilia Mungu katika maumivu yao. Na hivyo, Mungu alifanyika mwili binafsi kama Bwana Yesu na kufanya kazi ya ukombozi, Akianzisha Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria. Hebu tusome maneno zaidi ya Mwenyezi Mungu. “Kisha, katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo kwa mwanadamu, maana Alikuwa amekuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini. Aliweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo kusulubiwa Kwake kuliwakomboa wanadamu kutoka dhambini kabisa. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu kwa rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba ziweze kusamehewa milele(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili). “Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, dunia yote ingekuwa mahali pa kulala pa Shetani, maskani yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji kuonyesha huruma na wema kwa wanadamu; kupitia kwa njia hiyo tu ndio wanadamu wangeweza kupokea msamaha na mwishowe kupata haki ya kukamilishwa na kumilikiwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Katika miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alitumia kufanya kazi Yake hapa duniani alikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha, kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa yule mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaendesha majaaliwa ya wanadamu. Baada ya Yeye kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo alipowakomboa wanadamu. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Akidhihakiwa, kukashifiwa, na kuachwa, kiasi cha Yeye kukosa mahali pa kulaza kichwa chake, mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, huku nafsi Yake yote—mwili mtakatifu na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani. Alivumilia kila namna ya mateso yaliyoko. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na maaskari hata wakamtemea mate usoni; ilhali Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa wanadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ambayo Yesu alifanya inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria wala si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo wanadamu wamepitia—Enzi ya Ukombozi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi). Yesu alipoishi miongoni mwetu, Alihubiri “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). Alimfundisha mwanadamu kuungama na kutubu, kuwapenda wengine kama tunavyojipenda sisi wenyewe, kuwasamehe wengine mara sabini mara saba, kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote, nafsi na akili zetu zote, kumwabudu Mungu katika roho na kweli, na zaidi. Maneno ya Yesu yaliwaonyesha watu maana ya mapenzi ya Mungu nini na kuwapa lengo na mwelekeo tofauti katika imani yao. Hii ilikuwa hatua zaidi ya vizuizi vya sheria na masharti. Pia Alionyesha ishara na maajabu mengi, kuwaponya wagonjwa, kufukuza pepo, na kusamehe dhambi. Alikuwa mwingi wa uvumilivu na subira. Kila mtu angeweza kuhisi upendo na huruma ya Mungu, kuona uzuri Wake, na kumkaribia Mungu zaidi. Mwishowe, Bwana Yesu alisulubishwa msalabani, Akifanyika sadaka ya dhambi ya milele, Akisamehe dhambi zetu kabisa. Baada ya hapo, watu walihitaji tu kuungama na kutubu kwake Bwana ili dhambi zao zisamehewe na wasingeshutumiwa na kuadhibiwa chini ya sheria. Waliweza kuja mbele za Mungu katika maombi na kufurahia amani, shangwe, na baraka nyingi zilizotolewa na Bwana. Ni wazi kwamba kazi ya Yesu ya ukombozi imekuwa baraka kubwa kwa binadamu, ikituwezesha kuendelea kuwepo na kusitawi mpaka leo.

Kwa hivyo basi, kwa kuwa Bwana Yesu alikamilisha kazi Yake na kutukomboa kutoka katika mshiko wa Shetani, je, hiyo inamaanisha kuwa kazi ya Mungu ya wokovu imekamilika? Je, inamaanisha kwamba hatuhitaji tena kazi ya Mungu ya wokovu? Jibu ni: La. Kazi ya Mungu haijakamilika. Binadamu bado anahitaji hatua nyingine ya kazi ya Mungu ya wokovu. Mwanadamu alikombolewa na Bwana Yesu na dhambi zetu zikasamehewa, lakini asili yetu ya dhambi haijatatuliwa. Tunaongozwa na asili yetu ya dhambi, daima tukiishi katika upotovu. Hatuwezi kujizuia kusema uwongo na kutenda dhambi kila wakati. Tunamwasi na kumpinga Bwana, na hatuwezi kuweka maneno Yake katika vitendo. Sote tunaishi katika mzunguko wa kutenda dhambi, kuungama, na kutenda dhambi tena, ndani ya mapambano ya uchungu dhidi ya dhambi. Hakuna awezaye kuepuka minyororo na vikwazo vya dhambi. Kwa hivyo, je, watu wasioweza kuepuka dhambi wangeweza kweli kunyakuliwa na kuingia katika ufalme bila hukumu na utakaso? Bila shaka hawawezi. Mungu ni Mungu mtakatifu. “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana(Waebrania 12:14). Mungu hawezi kuwaruhusu wale ambao bado wanaweza kutenda dhambi na kumpinga waingie katika ufalme Wake. Hiyo ndiyo maana Bwana alitabiri kwamba Angekuja tena baada ya kumaliza kazi Yake ya ukombozi. Kurudi kwa Bwana Yesu ni ili kutatua kikamilifu asili ya dhambi ya mwanadamu, ili kutuokoa kutoka dhambini ili tuweze kuwa watakatifu na kuingia katika ufalme wa Mungu. Kama Bwana Yesu alivyosema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12–13). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli(Yohana 17:17). Ufunuo pia kilitabiri: “Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja(Ufunuo 14:7). Tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu anaonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu baada ya kurudi Kwake, na kumwongoza mwanadamu kuingia katika ukweli wote. Huko ni kuwaokoa wanadamu kikamilifu kutoka dhambini na kutoka katika nguvu za Shetani, na kutuongoza kuingia katika ufalme wa Mungu. Hii ni hatua ya kazi ambayo Mungu alipanga zamani na ndiyo hatua ya mwisho katika mpango wa usimamizi wa Mungu. Hebu tusome baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu ili tuelewe vyema kipengele hiki cha ukweli.

Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Kusoma hili kunatusaidia kuona kwa nini Mungu anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu ilitusamehe tu dhambi zetu, lakini asili yetu ya dhambi bado imekita mizizi. Tunahitaji Mungu anene ukweli zaidi na kufanya hatua ya kazi ya hukumu ili kuwasafisha kabisa na kuwaokoa binadamu. Yaani, kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu ilitayarisha njia kwa ajili ya kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho, ambayo ndiyo sehemu muhimu, sehemu kuu ya kazi yote ya Mungu ya wokovu. Pia ni njia yetu pekee ya wokovu kamili na kuingia katika ufalme. Hatua hii ya kazi itakapokamilika, tabia potovu za mwanadamu zitatakaswa na tutaacha kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Tutaweza kweli kujinyenyekeza na kumpenda Mungu, na kazi ya Mungu ya kuwaokoa binadamu itakamilika kikamilifu. Huo utakuwa ukamilisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000. Mwenyezi Mungu alionekana na kuanza kufanya kazi katika siku za mwisho, na kutamatisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Ameonyesha ukweli wote unaohitajika ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, kufichua mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa Mungu, mbali na kuhukumu na kufichua asili na tabia zote za kishetani za mwanadamu ambazo zinaenda kinyume na Mungu, na kufichua mawazo yetu yote kuhusu Mungu na mawazo yetu potofu katika imani yetu. Pia Ametupa njia ya kuepuka dhambi na kuokolewa kikamilifu, na zaidi. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni yenye thamani kubwa! Haya yote ni uhalisi wa ukweli ambao watu wanapaswa kuwa nao ili kusafishwa na kuokolewa kikamilifu, na ni maneno ambayo Mungu hakuwahi kuyatamka katika Enzi ya Sheria au Enzi ya Neema. Huyu ni Mungu anayetuletea njia ya uzima wa milele katika siku za mwisho. Watu wengi wateule wa Mungu ambao wamepitia hukumu Yake wameona ukweli wa upotovu wao na asili yao ya kishetani inayompinga Mungu, wamepata ufahamu wa kweli wa tabia ya Mungu yenye haki, isiyokosewa, na kukuza uchaji kwa Mungu. Hatimaye wanawekwa huru kutoka katika minyororo ya dhambi na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu. Wote wana ushuhuda wa ajabu wa kuwekwa huru kutokana na dhambi na kumshinda Shetani. Watu wateule wa Mungu wote wanajua kwamba kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho kwa kweli ni wokovu Wake wa mwisho kwa wanadamu! Bila kazi hii ya hukumu, hatungewahi kuona ukweli wa upotovu wetu wenyewe, hatungewahi kujua kiini cha dhambi zetu wenyewe, na hatungeweza kamwe kutakasa na kubadilisha tabia zetu potovu. Mwenyezi Mungu tayari amekamilisha kundi la washindi kabla ya maafa na injili ya ufalme Wake imeenea duniani kote. Ukweli unaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu amemshinda Shetani kikamilifu na kupata utukufu wote, na mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000 umekamilika. Maafa makubwa yameanza, na watenda maovu wote wanaompinga Mungu wataadhibiwa na kuangamizwa katika maafa, huku wale wanaopitia hukumu na kutakaswa watalindwa na Mungu katika maafa. Kisha kutakuwa na mbingu na dunia mpya—ufalme wa Kristo utadhihirika duniani, na wale watakaosalia watakuwa watu wa Mungu ambao wataishi milele katika ufalme wa Mungu na watafurahia baraka Zake na kile ambacho Ameahidi. Hili linatimiza unabii wa Ufunuo kwa kweli: “Naye malaika wa saba akalipiga baragumu; na kukawa na sauti kubwa mbinguni, zikisema, falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele(Ufunuo 11:15). “Na nikasikia kutoka mbinguni sauti kuu ikisema, Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita(Ufunuo 21:3–4).

Katika hatua hii tunaweza kuona jinsi hatua tatu za kazi za Mungu zilivyo za thamani na za vitendo! Kila moja ya hatua hizi ni ili kutatua tatizo la dhambi ya mwanadamu na kukamilisha lengo moja. Hilo ni kuwaokoa wanadamu kutoka kwa nguvu za Shetani na kutoka dhambini, hatua kwa hatua, ili tuweze kuingia katika ufalme wa Mungu na kupokea ahadi na baraka Zake. Kila hatua ya kazi inaunganishwa na ile inayofuata, na kila hatua imejengwa juu ya msingi wa hatua iliyotangulia, kila moja ikiwa kubwa zaidi na ya juu zaidi kuliko iliyotangulia. Zimeunganishwa kwa karibu, ni zisizotenganishwa, na hakuna inayoweza kufanya kazi bila nyingine. Unaona, bila kazi ya Enzi ya Sheria, hakuna mtu ambaye angejua dhambi ni nini, na sote tungekanyagwa na Shetani, tukiishi katika dhambi. Tungenyakuliwa na Shetani, na kuangamizwa. Bila kazi ya ukombozi ya Enzi ya Neema, mwanadamu angekabiliwa na adhabu kwa kutenda dhambi nyingi sana na hatungeweza kufika leo. Na, je, kama Mungu hangefanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho? Bila kazi hiyo hatungeweza kamwe kuepuka minyororo ya dhambi au kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tungeishia kuangamizwa kwa kuwa wenye dhambi sana. Ni wazi kwamba bila hatua moja tu ya hatua hizi tatu za kazi, wanadamu wangemilikiwa na Shetani na hawangeweza kamwe kuokolewa kikamilifu. Hatua hizi tatu za kazi zinajumuisha mpango kamili wa usimamizi wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa Mungu kwa mwanadamu. Kila hatua ni muhimu zaidi kuliko ile iliyotangulia, na zote ni mipango ya Mungu ya uangalifu ya kuwaokoa wanadamu. Hii inatuonyesha kikamilifu upendo mkuu wa Mungu na wokovu kwa binadamu na inatuonyesha hekima na uweza Wake. Kama vile Mwenyezi Mungu asemavyo, “Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Hamjambo ndugu. Tumebahatika sana kukusanyika pamoja—mshukuruni Bwana! Sisi sote ni watu tunaopenda kusikiliza maneno ya Mungu na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp