Je, Bwana Kweli Anarudi Juu ya Wingu?
Tunaona mfululizo wa maafa, na magonjwa ya kuenea yanaenea duniani. Waumini wamekuwa wakisubiri kwa haraka Bwana arudi juu ya wingu na kuwachukua juu angani, ili kuwaokoa kutokana na ulimwengu huu mwovu na kutokana na maafa, na kuwapeleka katika ufalme wa mbinguni. Wamekuwa wakitazama juu angani na kuomba bila kukoma, wakingoja kumwona Bwana juu ya wingu, bila kuthubutu kutazama kando, wakiogopa kwamba Bwana atakuja na watatupwa katika maafa. Lakini limekuwa jambo la kuumiza kwao kuona kwamba maafa yamekuja, lakini bado hawajamkaribisha Bwana Yesu kutoka mbinguni. Wengi wanajiuliza iwapo kwa kweli Bwana Yesu anakuja. Wengine wanahisi wasiwasi, wakifikiri kwamba labda wametupwa katika maafa na Bwana. Kwa kuwa wachungaji wengi wanahisi kutojiweza, wanabadilisha hadithi zao, wakisema kwamba Bwana atakuja katikati au baada ya maafa. Wengine hata wanathubutu kudai kwamba Bwana atakuja katika mwaka wa 2028 au 2030. Ufafanuzi huu wa Maandiko unaweza kuishia kuwatumbukiza waumini katika maafa, lakini wakiwa na hakikisho kwamba kila kitu kiko sawa. Lakini bila kujali wamekuwa na imani muda gani au wamefanya kazi kwa bidii kiasi gani, hawajamkaribisha Bwana. Tunaweza kufikiri jinsi jambo hili bila shaka ni gumu. Watu wote wenye imani wanajua Biblia inasema nini, na kwamba kuanguka katika maafa ukilia na kusaga meno ni ishara ya aibu, wakati mafanikio au kushindwa katika imani yako kunaamuliwa na kumkaribisha Bwana kabla ya maafa. Basi kwa nini wale walio katika ulimwengu wa dini hawajamkaribisha Bwana, lakini wameanguka katika maafa? Je, inaweza kuwa kwamba Bwana si mwaminifu, ndiyo maana bado hajatokea? Sivyo kabisa. Kushindwa kwa ulimwengu wa dini kumkaribisha Bwana hakumaanishi kuwa hajarudi. Kwa kweli, Alirudi katika mwili muda mrefu uliopita, Akionekana na kufanya kazi kama Mwana wa Adamu. Watu wengi wa madhehebu yote wamesikia sauti ya Mungu na kumkaribisha Bwana. Lakini wale watu katika dini wanaoshikilia wazo la Yeye kuja juu ya wingu bado hawajamkaribisha Bwana. Mnamo mwaka wa 1991, kanisa la Umeme wa Mashariki lilianza kutoa ushuhuda wa kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi Yake. Huo umekuwa ushuhuda wao kwa miongo mitatu mizima. Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno na watu kutoka madhehebu yote wanaopenda ukweli wamesoma maneno Yake, wameyatambua kuwa ukweli mtupu, wamegundua kuwa wanasikia sauti ya Mungu, na wamekuja mbele ya Mwenyezi Mungu, na kumkaribisha Bwana. Ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu umekuwa mtandaoni kwa muda mrefu, uking'aa kutoka Mashariki hadi Magharibi kama nuru kuu, na kuangazia ulimwengu mzima, jambo ambalo linatimiza kikamilifu maneno ya Bwana Yesu: “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” (Mathayo 24:27). Kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi Yake vimetikisa ulimwengu mzima, wakati nguvu za wapinga Kristo wa ulimwengu wa dini zimekuwa zikihukumu, kulaani, na kupinga Umeme wa Mashariki bila hata kuchunguza kuonekana kwa Mungu na kazi Yake. Msingi wao wa pekee ni kwamba Bwana Yesu yeyote ambaye haji juu ya wingu ni wa uwongo, na Bwana kuja kama mwili ni Kristo wa uongo. Sote tunaweza kuona kwamba ulimwengu wa dini haujamkaribisha Bwana, lakini umeanguka katika maafa kabisa kwa sababu haujafuata unabii wa Bwana Yesu ili kumkaribisha, bali wamefuata mawazo yao wenyewe, wakiamua bila misingi maalumu kwamba Bwana lazima arudi juu ya wingu. Wanatamani Bwana aje na kuwachukua moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni bila kutia maneno ya Bwana katika vitendo. Kufanya kosa baya sana katika jambo muhimu kama kumkaribisha Bwana kunamaanisha kupoteza nafasi yao ya kunyakuliwa, na wataishia kuanguka katika maafa, wakilia na kusaga meno yao. Hili linatimiza maneno ya Mungu: “Watu wangu wanaangamizwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa” (Hosea 4:6).
Ili kujua kama Bwana Yesu anakuja juu ya wingu au anaonekana ili kufanya kazi kama Mwana wa Adamu mwenye mwili, lazima kwanza tuvute pumzi na kutafakari kwa kina unabii wa Bwana Yesu kuhusu kuja Kwake mara ya pili, na tunaweza kujikuta tumeelimika sana. Hebu tuangalie baadhi ya mistari. “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” (Mathayo 24:27). “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25). “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu” (Mathayo 24:44). “Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa” (Mathayo 24:37). “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6). “Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi, na hutajua saa ambayo nitakuja kwako” (Ufunuo 3:3). “Tazama, mimi nakuja kama mwizi” (Ufunuo 16:15). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20). Tukifikiria mistari hii kwa makini, ni rahisi kuona kwamba unabii wa Bwana wa kurudi Kwake hutaja kila mara “Mwana wa Adamu,” “kuja kwa Mwana wa Adamu,” “atakapokuja Mwana wa Adamu,” “Mwana wa Adamu katika siku yake,” “Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa.” Bwana Yesu alisema “Kuja kwa Mwana wa Adamu” mara nyingi sana, jambo ambalo ni muhimu sana kwetu kumkaribisha Bwana katika siku za mwisho. Hivyo maneno “Mwana wa Adamu” yanahusu nini? Bila shaka, yanahusu Roho wa Mungu aliyevaa mwili kama Mwana wa Adamu. Hii inaweza tu kuhusu kupata mwili kwa Mungu. Bwana pia alisema mara nyingi atarudi “kama mwizi.” Kwa hivyo “kama mwizi” ina maana gani? Inamaanisha kuwa Bwana anakuja kimya kimya, kwa siri—watu wanapokuwa hawajui, Mungu anakuwa mwili kama Mwana wa Adamu, na kushuka kwa siri ili kuzungumza na kufanya kazi. Tunaweza kuwa na hakika kwamba kurudi kwa Bwana katika siku za mwisho ni kama Mwana wa Adamu, na kunafanyika kabla ya maafa, yaani, wakati ulimwengu upo katika giza kuu zaidi. “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6). Kanisa la Umeme wa Mashariki limekuwa likitoa ushuhuda kwa Mwenyezi Mungu tangu mwaka wa 1991, hadi sasa mwaka wa 2021, na kwa miaka hii 30, wamekandamizwa, kukamatwa, na kuumizwa vikali na CCP. Chama Cka Kikomunisti cha China hata kimetumia mashine zake za propaganda za nchi nzima, kimeeneza jina “Mwenyezi Mungu” ambalo Umeme wa Mashariki hushuhudia ulimwenguni kote, na kulifanya kuwa jina la kawaida ambalo kila mtu anafahamu. Hilo linatimiza unabii huu wa Bwana Yesu: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25). Baada ya Umeme wa Mashariki kutoa ushuhuda kwa Mwenyezi Mungu kwa miaka mingi, watu kutoka madhehebu yote waliopenda ukweli walisoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kuyatambua kuwa ukweli, kama maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa. Walisikia sauti ya Mungu, na kumkubali Mwenyezi Mungu kwa furaha. Wao ni wanawali wenye busara ambao wameinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na wanahudhuria karamu ya Bwana. Kuna hata watu wengi ambao walikuwa wakimhukumu na kumlaani Mwenyezi Mungu, ambao walisoma maneno Yake baadaye na kuishia kusikia sauti ya Mungu na kuja mbele ya Mungu. Kisha wanajawa na majuto kwa ajili ya kumpinga na kumhukumu Mwenyezi Mungu. Wanawali hawa wenye busara wanaohudhuria karamu ya arusi ya Mwanakondoo wanatoa ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kuonekana, na kushuka kwa Mwana wa Adamu katika siku za mwisho. Lakini wale wanaoshikilia maana ya wazi ya Maandiko, wakikataa kumkubali yeyote isipokuwa Bwana akija juu ya wingu ni wanawali wapumbavu wanaoanguka katika maafa. Wanaweza tu kungoja kumwona Bwana Yesu akitoka juu ya wingu baada ya maafa makubwa. Sababu kuu ya watu hawa kutomkaribisha Bwana ni kwamba wanaamini tu unabii wa kibiblia kutoka kwa wanadamu, lakini sio unabii kutoka kwa kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe. Watamkubali tu Bwana akija juu ya wingu, lakini wanakataa ukweli wa Mungu katika mwili kuonekana na kufanya kazi kama Mwana wa Adamu. Ni wajinga na wapumbavu kiasi cha kushangaza! Bwana alitaja “Mwana wa Adamu” mara nyingi alipokuwa akizungumza kuhusu kurudi Kwake, lakini wachungaji wengi “wenye akili” na “wenye hekima” na wasomi wa Biblia wamevuruga wazo la Mwana wa Adamu, na kufanya kosa kubwa sana. Wao ni waathiriwa wa hekima zao wenyewe! Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli kiasi kikubwa sana, lakini bado wanakataa kumwona kama Mwana wa Adamu. Je, huo si upofu tu? Asingekuwa Mungu mwenye mwili, Angewezaje kuonyuesha ukweli kiasi hicho? Bado wanashikilia dhana kwamba wanaweza tu kumkubali Bwana Yesu akishuka juu ya wingu, na ndiyo sababu wanapoteza nafasi yao ya kunyakuliwa, lakini wanaanguka katika maafa. Hayo yatakuwa majuto ya milele.
Sote tunaweza kuona kwamba Bwana amerudi kama Mwana wa Adamu mwenye mwili kufanya kazi. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuukana. Lakini watu wengi huuliza kuhusu “Tazama, anakuja na mawingu” katika Ufunuo 1:7, wakifikiri ina maana kwamba Bwana atashuka juu ya wingu. Na je, kusema Atakuja akiwa juu ya mawingu, na kusema atakuja kama Mwana wa Adamu hakupingani? Kunaweza kuonekana hivyo, lakini kwa kweli hakuna ukinzani hapa. Ni changamoto tu kwa ufahamu wa mwanadamu. Unabii wowote wa kibiblia utatimizwa kabisa, lakini kuna mchakato fulani, na kuna hatua. Pia kuna utaratibu wa kuonekana kwa Mwana wa Adamu na kuja kwa Bwana juu ya wingu. Bwana kwanza anapata mwili na kuja kwa siri kufanya kazi, na kisha kutokea waziwazi juu ya wingu. Kwa nini hilo linafanyika kwa hatua mbili? Nini kinatokea kwa sasa? Kuna siri ndani ya hili. Hebu kwanza tuone Bwana Yesu alitabiri nini. Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12-13). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana. … Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu” (Yohana 5:22, 27). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17). Unabii wa Bwana Yesu umetimizwa wote. Mwana wa Adamu alikuja kwa siri wakati wanadamu hawakutarajia na ameonyesha ukweli, na kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Yeye ndiye Roho wa ukweli ambaye anawaongoza wateule wa Mungu kuingia katika ukweli wote na Amekamilisha kundi la washindi kabla ya maafa. Injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu pia imeenea katika kila nchi ulimwenguni. Hii inaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu amemshinda Shetani na kupata utukufu wote. Sasa kwa kuwa maafa makubwa yameanza, Mungu amekamilisha kundi la washindi na kazi Yake kuu inakamilika. Baada ya maafa, Mungu ataonekana waziwazi juu ya wingu kwa watu wote na mataifa yote. Wakati huo, unabii wa kutokea kwa Mwana wa binadamu na kuja kwa Bwana juu ya wingu utatimizwa kikamilifu. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alionekana na kuanza hukumu Yake akianza na nyumba ya Mungu, wale ambao wamemkubali Mwenyezi Mungu wanakula na kunywa maneno ya Mungu kila siku, na kwa kukubali hukumu na utakaso wa Mungu, wanaondokana na dhambi na nguvu za Shetani polepole. Mungu amewafanya wawe washindi kabla ya maafa, na wao ni malimbuko. Hili linatimiza kikamilifu unabii wa Ufunuo: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20). “Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo” (Ufunuo 14:4). Imekuwa miongo mitatu kamili tangu Mwenyezi Mungu alipokuja kwa siri kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Ameonyesha ukweli, na kufichua mafumbo yote ya Biblia na mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu. Amesema mengi sana ili kuhukumu na kufichua kiini kiovu cha mwanadamu, na maneno haya ndiyo njia ya ukweli inayoturuhusu kuondokana na dhambi na nguvu za Shetani, na kuokolewa kikamilifu. Wateule wa Mungu wanahukumiwa, wanaadibiwa, wanapogolewa, wanashughulikiwa, wanajaribiwa, na kusafishwa na Mwenyezi Mungu, wanaona upotovu wao wenyewe kwa wazi, wanahisi aibu bila mahali pa kujificha, na wanainama mbele za Mungu, wakiwa wamejawa na majuto, wakijichukia na kujidharau. Pia wanaona kwamba tabia ya Mungu yenye haki haitavumilia kosa lolote na wanapata kumcha Mungu, na polepole wanakuja kumwogopa Mungu na kuepuka maovu, na wanatubu na kubadilika kwa kweli. Mwenyezi Mungu amekamilisha kundi la washindi kabla ya maafa, na kupata malimbuko. Ushuhuda huu wa washindi umefanywa kuwa video na sinema zinazopatikana mtandaoni, ambazo ni za kusadikisha kabisa kwa wote wanaoziona. Ni dhahiri kabisa kwamba huku ni kuonekana kwa Mungu na kazi Yake katika siku za mwisho! Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli na kufanya kazi nzuri sana, na mbali na kutikisa ulimwengu mzima, pia ametikisa vitu vyote. Mwenyezi Mungu amebadilisha ulimwengu, na kutamatisha enzi ya zamani na kuanza enzi mpya. Enzi ya Ufalme imeanza. Hii inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kuonekana kwa Mwana wa Adamu, Bwana Yesu aliyerudi. Mwokozi wetu ameonekana na anafanya kazi! Kazi ya hukumu inayoanza na nyumba ya Mungu tayari imefanywa kwa kiasi kikubwa na kwa hivyo maafa makubwa yametokea. Tunaweza kusema kwamba maafa tayari yameanza na yataongezeka tu. Watenda maovu na nguvu zote za uovu zinaompinga Mungu zitaadhibiwa na kuangamizwa katika maafa, huku wale ambao wametakaswa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu wa siku za mwisho watalindwa na kutunzwa na Mungu hadi mwisho wa maafa. Maafa yatakapoisha, ulimwengu huu mwovu wa Shetani utaangamizwa, na kisha Mungu ataonekana kwa watu wote waziwazi juu ya wingu. Huo utakuwa utimizo wa unabii katika Ufunuo 1:7: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye.” Kwa nini makabila yote yatalia kwa huzuni? Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli na kufanya kazi nzuri sana, na mbali na kukataa kuichunguza, pia walimhukumu, walimlaani, na kumkufuru pamoja na nguvu za wapinga Kristo wa ulimwengu wa dini. Wamekosea tabia ya Mungu na wameanguka katika maafa. Wataishia tu kujipiga vifua, wakilia na kusaga meno, jambo ambalo litakuwa utimizo wa unabii wenye kuhuzunisha wa Ufunuo kwamba “makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye.” Wale ambao wametakaswa na kukamilishwa kwa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu watamwona Mungu akionekana wazi na watakuwa wakicheza kwa furaha isiyo na kikomo, wakisifu uweza, hekima na haki ya Mungu. Kama Mwenyezi Mungu anavyosema: “Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha watu ambao wanafikiria kama Mimi. Wale ambao hawana fikira sawa na Zangu, wakati ule ule, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako).
Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Hii ndiyo nafasi moja na ya pekee ya wanadamu kuokolewa na kuingia katika ufalme wa Mungu, na ni fursa ya kipekee. Maafa makubwa yanaanza. Wale wanaoamka na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu bila kukawia watakuwa wamewahi, kwa sababu Mwenyezi Mungu asema, “Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26). Tunaweza kuona kwamba watu wengine wataisikia sauti ya Mungu na kuona matendo Yake, watakuja mbele za Mungu, na kupata wokovu Wake katikati ya maafa. Huku ni kunyakuliwa katika maafa na ni nafasi yao ya mwisho kabisa, na ni huruma kuu ya Mungu kwa wanadamu. Wenye busara watajua watakalochagua. Wale wanaongoja kwa hamu Bwana aje juu ya wingu watakuwa na mwisho ambao ni dhahiri. Hebu tuangalie kifungu kimoja cha mwisho cha maneno ya Mwenyezi Mungu leo. “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba ‘Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo’ watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?