Je, ni Kweli Kwamba Kazi na Maneno Yote ya Mungu Yamo Katika Biblia?

23/04/2023

Mwokozi Mwenyezi Mungu ameonekana na anafanya kazi katika siku za mwisho, na Ameonyesha mamilioni ya maneno. Anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Neno Laonekana katika Mwili, mkusanyiko wa maneno Yake, unapatikana mtandaoni. Hakijatikisa ulimwengu wa kidini tu, bali ulimwengu mzima wenyewe. Baadhi ya wale wanaopenda ukweli na kutamani kuonekana kwa Mungu, kutoka katika kila nchi na kila dhehebu, wamesoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na kuona kuwa ni ukweli na kuwa ni matamshi ya Roho Mtakatifu. Wameisikia sauti ya Mungu, wamemtambua Mwenyezi Mungu kama Bwana Yesu aliyerudi, na wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kama tu Bwana Yesu alivyosema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Lakini ingawa wengi katika ulimwengu wa kidini wanatambua kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, yana nguvu na mamlaka, kwa kuwa maneno Yake hayajaandikwa katika Biblia, wanakataa kuyakubali. Wanaamini kwamba kazi na maneno ya Mungu yote yamo katika Biblia, na hakuna hata moja linaloweza kupatikana nje yake. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, lakini kwa kuwa hayamo katika Biblia, yanawezaje kuwa kazi na maneno ya Mungu? Na wengine, wakiona kwamba washiriki wa Kanisa la Mwenyezi Mungu husoma Neno Laonekana katika Mwili badala ya Biblia, wanashutumu hili, wakisema kuiacha Biblia ni kumsaliti Bwana, kwamba ni uzushi. Hili linanikumbusha Mafarisayo wa Kiyahudi, ambao walimhukumu, kumshutumu, na kupigana dhidi ya Bwana Yesu kwa sababu tu kazi na maneno Yake yalizidi yale ya Maandiko yao na Yeye hakuitwa Masihi. Hata walifanya Asulubishwe, na wakaishia kuadhibiwa na kulaaniwa na Mungu, na kuliangamiza taifa la Israeli. Hili ni funzo la kuchochea mawazo! Watu wengi wa dini leo wanasisitiza kwamba kazi na maneno ya Mungu yote yamo katika Biblia, na hakuna hata moja linaloweza kupatikana nje yake. Wanakanusha na kushutumu kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu, wakishikilia wazo hili potovu. Wengine hata hukubali moja kwa moja kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, lakini bado hawayachunguzi, na kwa sababu hiyo wanaikosa nafasi yao ya kumkaribisha Bwana kabla ya majanga. Cha kusikitisha ni kwamba wameanguka katika majanga. “Kazi na maneno ya Mungu yote yamo ndani ya Biblia, na hakuna linaloweza kupatikana nje yake.” Wazo hili limesababisha watu wengi sana kukosa nafasi yao ya kumkaribisha Bwana, wakisababisha madhara yasiyoelezeka. Tatizo la wazo hili ni lipi kwa kweli? Nitachukua fursa hii kushiriki kile ninachojua juu yake.

Kabla ya kujitosa katika hilo, hebu tufafanue Biblia ilitoka wapi. Inajumuisha sehemu mbili: Agano la Kale, na Agano Jipya. Wayahudi wana imani katika Yehova, na wao hutumia Maandiko ya Agano la Kale, huku Wakristo wanaomwamini Bwana Yesu hutumia Agano Jipya. Agano la Kale na Jipya yote mawili yalikusanywa na wanadamu karne nyingi baada ya Mungu kumaliza kazi Yake. Biblia haikuanguka kutoka mbinguni, na bila shaka Mungu hakuiandika yeye binafsi na kutukabidhi sisi. Iliundwa kwa ushirikiano kati ya viongozi wa kidini wa wakati huo. Bila shaka walikuwa na nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu—hakuna shaka. Kwa kuwa Biblia ilitungwa na wanadamu, hakuna uwezekano kwamba Agano la Kale lingejumuisha yaliyomo katika Agano Jipya, na hakuna uwezekano kwamba Agano Jipya lingeweza kujumuisha kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Hiyo ni kwa sababu watu hawawezi kujua yatakayotendeka katika siku zijazo. Mistari na vitabu vilivyojumuishwa kuwa Biblia vilichaguliwa, na si maandishi yote ya manabii au mitume yaliyowekwa katika Biblia. Vichache kiasi viliachwa au kuondolewa. Lakini hilo si tatizo. Kwa kuwa iliundwa na wanadamu, ni kawaida kwamba kuna uteuzi, kuondolewa na kuachwa kwa aina fulani. Makosa ya watu katika hili ni kusisitiza kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yamo katika Biblia, kana kwamba hayo tu ndiyo Mungu alisema na kufanya katika enzi hizo. Hili ni tatizo la aina gani? Baadhi ya vitabu vya manabii havikuandikwa katika Agano la Kale, na vitabu kadhaa tunavyovijua, kama vile vya Henoko na Ezra, havimo katika Biblia. Na tunaweza kuwa na uhakika kwamba lazima kuwe na vitabu vingine vya mitume ambavyo havikujumuishwa katika Agano Jipya, bila kutaja kwamba Bwana Yesu alikuwa akihubiri kwa zaidi ya miaka mitatu na lazima alisema mambo mengi sana, lakini ni machache sana kati ya hayo yaliyowekwa katika Biblia. Kama mtume Yohana alivyosema, “Na pia kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya, ambayo, yote yakiandikwa, ninafikiri kwamba hata dunia yenyewe haingetosha vitabu hivyo ambavyo vitaandikwa” (Yohana 21:25). Ni wazi kwamba rekodi ya Biblia ya kazi na maneno ya Mungu ni ndogo sana! Tunajua bila shaka kwamba hakuna Agano la Kale wala Jipya lililo na maudhui kamili ya kazi na maneno ya Mungu katika enzi hiyo. Huu ni ukweli ambao wote wataukubali. Kuna watu wengi katika ulimwengu wa kidini ambao hawaelewi Biblia au jinsi ilivyoundwa. Wanaamini kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yamo katika Biblia, na wao hukana na kushutumu chochote ambacho kiko nje ya Biblia. Je, hilo linalingana na ukweli wa kihistoria? Je, madai hayo si kuihukumu kazi ya Mungu? Je, si kumpinga Mungu? Biblia ilikusanywa baada ya ukweli huo na ilifanywa na wanadamu, kwa hiyo wanadamu wangewezaje kuweka hatua inayofuata ya kazi ya Mungu katika Biblia kabla ya wakati? Hilo lisingewezekana, kwa sababu watu hawana uwezo wa kuona kimbele. Wale waliokusanya Agano la Kale hawakuwa hai katika siku za Bwana Yesu na hawakupitia kazi ya Bwana Yesu. Wangewezaje kuweka kazi na maneno Yake, na vitabu vya mitume katika Agano la Kale kabla ya wakati? Pia haingewezekana kwa wale waliokusanya Agano Jipya kuweka kazi na maneno ya Mungu ya siku za mwisho, miaka 2,000 baadaye, katika Maandiko kabla ya wakati. Ulimwengu wote wa kidini leo umeshuhudia kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu. Wengine wameyachunguza na kutambua kwamba maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na yana mamlaka. Lakini kwa kuwa Biblia haina maneno ya Mwenyezi Mungu na jina Lake, na hayapatikani humo, wanakana kwamba Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Mungu Mwenyewe. Je, kosa lao si sawa na la Mafarisayo walipompinga na kumhukumu Bwana Yesu? Mafarisayo walifikiri kwamba kwa kuwa jina la Bwana Yesu halikuwa Masihi, na kazi na maneno Yake hayakulingana na Maandiko yao, wangeweza kukana kuwa Yeye hakuwa Masihi. Watu wa kidini leo wanaona kwamba jina la Mwenyezi Mungu halikutabiriwa katika Biblia na maneno Yake pia hayawezi kupatikana ndani yake, kwa hivyo wanaikana na kuishutumu kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu. Wao wanatenda ile dhambi ya kumsulubisha Mungu msalabani tena. Kwa kweli, ingawa Biblia haina kazi na maneno ya Mungu ya siku za mwisho, kuna unabii kuhusu jina jipya la Mungu katika siku za mwisho, kama huu katika Isaya: “Na Watu wa Mataifa wataiona haki yako, nao wafalme wote watauona utukufu wako; na wewe utaitwa kwa jina jipya, jina ambalo kinywa cha Yehova kitalitamka(Isaya 62:2). Na pia tunaweza kuona katika Ufunuo: “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu Wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu Wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu Wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya(Ufunuo 3:12). “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho…, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi(Ufunuo 1:8). “Haleluya: kwani Bwana Mungu mwenye uenzi hutawala(Ufunuo 19:6). Biblia pia inatabiri kwamba Mungu atazungumza zaidi na kufanya kazi zaidi katika siku za mwisho, kama alivyosema Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Pia kuna onyo inayoonekana katika Ufunuo mara saba: “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo Mlango wa 2 na 3). Ufunuo pia kinatabiri kwamba Mungu ataifungua hati ya kukunjwa iliyotiwa muhuri katika siku za mwisho. Ni dhahiri kwamba Mungu ametabiriwa kuyazungumzia makanisa katika siku za mwisho na kuwaongoza wanadamu kuingia katika ukweli wote. Je, kazi na maneno haya kutoka kwa Mungu katika siku za mwisho yangewezaje kuonekana katika Biblia kabla? Hilo haliwezekani! Kukiwa na unabii na ukweli huu wote ulio wazi, kwa nini watu wengi ni vipofu, macho yao yakiwa wazi kabisa, wakihukumu na kusisitiza kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yako katika Biblia, na hakuna hata moja linaloweza kupatikana nje yake? Kuwa na ujasiri dhahiri wa kumshutumu na kumpinga Mungu kwa kuwa sasa Ameonekana na anafanya kazi, watu hawa hawaielewi kazi ya Mungu, na hawaelewi ukweli hata kidogo. Wanashutumiwa na kuondolewa na Mungu, na tayari wameanguka katika majanga. Hili linatimiza aya hizi za Biblia: “Wapumbavu hukufa kwa ajili ya ukosefu wa hekima” (Mithali 10:21). “Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa(Hosea 4:6).

Hebu tuangalie baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu. Injili Nne zina chini ya sura mia moja zote pamoja ambamo mliandikwa mambo yale yaliotendeka yanayohesabika, kwa mfano Yesu Akilaani mti wa mkuyu, Petro akimkana Bwana mara tatu, Yesu Akiwaonekania wanafunzi Wake baada ya kusulubiwa na ufufuo Wake, Akifunza kuhusu kufunga, kufunza kuhusu maombi, kufunza kuhusu talaka, kuzaliwa na kizazi cha Yesu, uteuzi wa Yesu wa wanafunzi, na mengine mengi. Hata hivyo, mwanadamu anayathamini kama hazina, hata kuthibitisha kazi ya leo kulingana nayo. Hata wanaamini kuwa Yesu Alitenda kiasi tu katika muda baada ya kuzaliwa Kwake. Ni kana kwamba wanaamini kuwa Mungu anaweza kufanya hayo tu, kwamba hakuna kazi nyingine. Je huu si upumbavu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (1)).

Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Akafunika kichwa, Akavunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)).

Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? Kuleta mambo ya zamani leo kunayafanya yawe historia, haijalishi yana ukweli kiasi gani, bado ni historia—na historia haiwezi kushughulikia masuala ya leo. Maana Mungu haangalii historia! Na hivyo, kama unaelewa tu Biblia, na huelewi chochote kuhusu kazi ambayo Mungu anakusudia kufanya leo, na kama unamwamini Mungu, na hutafuti kazi ya Roho Mtakatifu, basi hujui inamaanisha nini kumtafuta Mungu. Ikiwa unasoma Biblia kwa lengo la kujifunza historia ya Israeli, kutafiti historia ya uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia, basi humwamini Mungu. Lakini leo, kwa kuwa unamwamini Mungu, na kutafuta uzima, kwa kuwa unatafuta maarifa juu ya Mungu, na hutafuti nyaraka na mafundisho mfu, au ufahamu wa historia, unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu ya leo, na unapaswa kutafuta uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama ungekuwa mwanaakiolojia ungeweza kusoma Biblia—lakini wewe sio mwanaakiolojia, wewe ni mmoja wa wale wanaomwamini Mungu, na utakuwa bora zaidi ukitafuta mapenzi ya Mungu ya leo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (4)).

Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. Leo, Mungu amefanyika mwili, na Amewachagua wateule wengine katika nchi ya China. Mungu anafanya kazi ndani ya watu hawa, Anaendelea na kazi Yake duniani, Anaendelea kutoka katika kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. Hivyo, kazi ambayo haijawahi kufanywa kabla sio historia, kwa sababu sasa ni sasa, na bado haijawa muda uliopita. Watu hawajui kwamba Mungu amefanya kazi kubwa, mpya duniani, na nje ya Israeli, yaani imevuka mawanda ya Israeli, na zaidi ya unabii wa manabii, ambayo ni kazi mpya na ya kushangaza nje ya unabii, na kazi mpya kabisa nje ya Israeli, na kazi ambayo watu hawawezi kuielewa au kufikiria. Inawezekanaje Biblia kuwa na rekodi za wazi za kazi kama hiyo? Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya. … Kwa kuwa kuna njia ya juu, kwa nini mjifunze hiyo ya chini, njia ya kale? Kwa kuwa kuna matamshi mapya, na kazi mpya, kwa nini uishi katikati ya rekodi za kale za kihistoria? Matamshi mapya yanaweza kukupa, ambayo yanathibitisha kwamba hii ni kazi mpya; rekodi za kale haziwezi kukushibisha, au kutosheleza mahitaji yako ya sasa, kitu ambacho kinathibitisha kwamba ni historia, na sio kazi ya hapa na sasa. Njia ya juu zaidi ni njia mpya zaidi, na kazi mpya, bila kujali njia ya zamani ni ya juu kiasi gani, bado ni historia ya kumbukumbu ya watu, na haijalishi ina thamani kiasi gani kama rejeleo, bado ni njia ya kale. Ingawa imerekodiwa katika ‘kitabu kitakatifu,’ njia ya kale ni historia; ingawa hakuna rekodi yake katika ‘kitabu kitakatifu,’ njia mpya ni ya hapa na sasa. Kwa njia hii inaweza kukuokoa, na kwa njia hii inaweza kukubadilisha, maana hii ni kazi ya Roho Mtakatifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)).

Ukweli Ninaoufafanua hapa ni huu: Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote. Mungu hawezi kueleweka na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Mwishowe, ni lazima bado Nimkumbushe kila mtu: Msimwekee Mungu mipaka katika vitabu, maneno, au tena katika matamshi Yake yaliyopita. Kuna neno moja tu kwa sifa ya kazi ya Mungu—mpya. Hapendi kuchukua njia za zamani au kurudia kazi Yake, na zaidi ya hayo Hapendi watu kumwabudu kwa kumwekea mipaka katika upeo fulani. Hii ndiyo tabia ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hitimisho).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanafanya kila kitu kiwe dhahiri, sivyo? Biblia ni rekodi tu ya hatua mbili za kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Ni kitabu cha kihistoria, na hakiwezi kabisa kuwakilisha kazi na maneno yote ya Mungu. Mungu ndiye Muumba, ndiye chanzo cha uzima wa mwanadamu. Amekuwa akizungumza na kufanya kazi kwa milenia, na Yeye ni chanzo kisichoisha cha riziki kwa wanadamu, akituongoza kwenda mbele kila mara. Maneno Yake ni chemchemi ya maji ya uzima, yanayotiririka daima. Kazi na maneno ya Mungu hayawezi kuzuiwa na mtu au kitu chochote, sembuse kuwekewa vikwazo na Biblia. Hajawahi kuacha kuzungumza zaidi na kufanya kazi mpya kulingana na mpango Wake wa usimamizi na mahitaji ya binadamu. Yehova Mungu alitoa sheria ili kuyaongoza maisha ya wanadamu duniani katika Enzi ya Sheria, wakati hapakuwa na Biblia hata kidogo. Bwana Yesu alihubiri njia ya toba katika Enzi ya Neema na akafanya kazi ya ukombozi, akienda zaidi ya Agano la Kale. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho na anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Amefungua ile mihuri saba na kile kitabu cha kukunjwa, akionyesha ukweli wote unaowatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Hii ni hatua mpya, ya juu zaidi ya kazi inayofanywa juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Enzi ya Neema. Ni kazi mpya na ya vitendo zaidi, na isingeweza kutokea katika Biblia hapo awali. Tunaweza kuona kutokana na hili kwamba kazi ya Mungu daima ni mpya na kamwe si nzee, daima inasonga mbele, na haijirudii kamwe. Kazi yake mpya ni zaidi ya ile iliyo katika Biblia, ikimpa mwanadamu njia mpya na hata ukweli wa juu zaidi. Kwa hivyo imani yetu haiwezi kutegemezwa katika Biblia pekee, na hakika hatuwezi kusema kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yamo katika Biblia. Tunapaswa kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kwenda sambamba na nyayo za kazi ya Mungu, ili kupokea riziki na uchungaji wa maneno ya sasa ya Mungu. Kama vile Ufunuo kinavyosema: “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo(Ufunuo 14:4). Hawa ndio mabikira wenye busara ambao wanaweza kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo na kupata wokovu wa Mungu katika siku za mwisho.

Mwenyezi Mungu amekuwa akifanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho kwa miaka 30 na Ameonyesha mamilioni ya maneno. Maneno Yake ni yenye wingi na hayapungukiwi chochote. Yanafunua mafumbo ya Biblia pamoja na mafumbo yote ya mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000, kama vile malengo Yake katika kuwasimamia wanadamu, jinsi Shetani anavyowapotosha wanadamu, jinsi Mungu anavyowaokoa wanadamu kutoka kwa nguvu za Shetani hatua kwa hatua, jinsi Mungu anavyowatakasa wanadamu na kumfanya mwanadamu mtakatifu kupitia katika majaribu na usafishaji, umuhimu wa kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, mafumbo ya kupata mwili na majina Yake, hadithi halisi ya Biblia, matokeo ya kila aina ya watu, hatima ya mwisho ya mwanadamu, na jinsi ufalme wa Kristo unavyotimizwa duniani. Mwenyezi Mungu pia anahukumu na kufichua ukweli wa upotovu wa binadamu na asili yao ya kishetani ya kumpinga Mungu. Anatuonyesha njia ya kuepuka dhambi na kuokolewa kikamilifu na Mungu, kama vile jinsi ya kutubu kwa kweli, jinsi ya kuutelekeza mwili na kutenda ukweli, jinsi ya kuwa mtu mwaminifu, jinsi ya kufanya mapenzi ya Mungu, jinsi ya kumcha Mungu na kuepuka maovu, jinsi ya kupata maarifa ya kumtii Mungu na kuwa na upendo kwa Mungu, na zaidi. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni yenye wingi zaidi na ya juu zaidi kuliko maneno ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na yote ni ukweli ambao lazima tuwe nao ili tupate wokovu wa Mungu. Ni yenye kuzindua na kukamilisha sana, na hutupatia njia ya kutenda katika kila kitu. Katika maneno ya Mwenyezi Mungu, tunapata kila jibu na suluhu la mapambano na maswali yetu yote katika imani yetu. Neno Laonekana katika Mwili kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni Biblia ya Enzi ya Ufalme, na ndiyo njia ya uzima wa milele ambayo Mungu amempa mwanadamu katika siku za mwisho. Kwa kula, kunywa, na kutenda maneno ya Mwenyezi Mungu, kuhukumiwa, kuadibibiwa kupitia kwa maneno Yake na kuelewa ukweli fulani, watu wateule wa Mungu wanapata ufahamu wa kweli wa Mungu. Tabia zao potovu zinatakaswa na kubadilishwa kwa viwango tofauti, na hatimaye wanaepuka minyororo ya dhambi na kutoa ushuhuda wa kumshinda Shetani. Hao ndio washindi ambao Mungu amewakamilisha kabla ya majanga. Huenda jina, kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu yasiwe yamerekodiwa katika Biblia, lakini matunda yanayozaa, matokeo halisi yanayopatikana na kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu hutimiza kikamilifu unabii wa Biblia. Kuna video na sinema za ushuhuda wa watu wateule wa Mungu mtandaoni sasa, zinazotoa ushuhuda wa kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu kwa ulimwengu. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni kama nuru kuu, inayoangaza kutoka Mashariki hadi Magharibi, ikiuangaza ulimwengu mzima. Watu zaidi na zaidi kutoka kila pembe ya dunia wanaopenda ukweli wanaichunguza njia ya kweli, na kumgeukia Mwenyezi Mungu. Hili ni wimbi kubwa linalopita katika dunia ambalo haliwezi kuzuiwa na nguvu yoyote. Kama tu anavyosema Mwenyezi Mungu, “Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata matamko ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu ‘mtu’ asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu? … Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, ‘Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.’(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili). Enzi ya Ufalme ni Enzi ya Neno. Mungu anatumia maneno Yake kuwashinda, kuwatakasa, na kuwaokoa wanadamu, na amekamilisha kundi la washindi. Hili linaonyesha kikamilifu mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu. Lakini ulimwengu wa kidini unang’ang’ania Biblia, ukikataa kukubali hukumu na utakaso wa Mwenyezi Mungu. Watu hawa wamekwama katika maisha yao ya zamani ya kutenda dhambi, kuungama, na kutenda dhambi tena, na tayari wameondolewa kupitia kazi ya Mungu, wakianguka katika majanga, wakilia na kusaga meno yao. Bado wanasubiri Bwana aje juu ya wingu awanyakue hadi katika ufalme wa mbinguni kwa wapate uzima wa milele. Je, hizo si ndoto za mchana? Kama tu alivyosema Bwana Yesu, “Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai(Yohana 5:39-40). Wale wanaong’ang’ania Biblia hawatapata ukweli au uzima. Ni wale tu wanaomwamini Kristo, wanaomfuata na kumtii Kristo ndio watakaopata ukweli na uzima. Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, sasa anaonyesha ukweli ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Ikiwa tunataka ukweli na uzima, tunapaswa kuipita Biblia na kwenda sambamba na nyayo za Mungu, tukubali na kutii hukumu na utakaso wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuepuka dhambi na kuokolewa kikamilifu na Mungu, na njia pekee ya kulindwa na Mungu katika majanga, na kuingia katika ufalme Wake. Wale wasioiachilia Biblia, lakini wamekwama katika kazi na maneno ya Mungu ya awali, wanaokataa kukubali njia ya ukweli ambayo Mungu anatupa katika siku za mwisho, wataikosa kabisa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na kuwaokoa wanadamu wote, na wanaweza tu kuanguka katika majanga na kuadhibiwa. Kama tu anavyosema Mwenyezi Mungu, “Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Hebu tutamatishe kwa kifungu kingine cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na skamwe hutapata uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kunyakuliwa ni Nini Hasa?

Miaka 2,000 iliyopita, baada ya Bwana Yesu kusulubishwa na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, Aliahidi kwamba Atarudi. Tangu wakati huo,...

Kupata Mwili Ni Nini?

Sote tunajua kwamba miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alikuja mwilini katika ulimwengu wa mwanadamu kama Bwana Yesu ili kuwakomboa...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp