Unashuhudia kwamba Bwana amerudi katika mwili ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu na utakaso wa mwanadamu katika siku za mwisho, lakini wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanaamini kwamba Bwana atarudi na mawingu, na kwamba wale wote wanaoamini katika Bwana watabadilika umbo mara moja na watanyakuliwa katika mawingu kukutana na Bwana, kama tu alivyosema Paulo: “Kwani maongezi yetu yako mbinguni; ambako pia tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo: Atakayeubadilisha mwili wetu wa uovu, ili uweze kuwa kwa kadri ya mwili wake wenye utukufu, kulingana na kufanyika ambapo ataweza kuvitiisha vitu vyote kwake” (Wafilipi 3:20-21). Bwana ni mwenye uweza na hakuna kitu ambacho Hawezi kufanya. Mungu atatubadilisha na kututakasa, akifanikisha hili kwa neno moja tu. Hivyo kwa nini bado Anahitaji kupata mwili ili kuonyesha ukweli na kufanya hatua ya kazi ya hukumu na utakaso wa mwanadamu?

07/06/2019

Jibu:

Kazi ya Mungu kila wakati ni isiyoweza kueleweka. Hakuna yeyote anayeweza kueleza unabii wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kuelewa unabii unapotimizwa. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa hakuna mtu anaweza kuelewa busara na kudura ya Mungu. Wakati Bwana Yesu Alionekana kufanya kazi katika Enzi ya Neema, hakuna mtu angeweza kuielewa. Wakati Mwenyezi Mungu Atafanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho katika Enzi ya Ufalme, hakuna mtu anaweza kuijua mapema pia. Kwa hivyo, binadamu anaiona Mungu kuwa mwili katika siku za mwisho kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu kuwa jambo la kushangaza. Lakini wakati kazi ya Mungu imeisha, msiba kuu utafika. Wakati huo, watu wengi watahisi kuwa neno nzima la Mungu limetimizwa. Lakini muda wa kujuta utakuwa umepita. Wanaweza tu kupiga mayowe na kusaga meno katikati ya msiba kuu. Kuhusu jinsi Mungu Anafanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho kutakasa na kuokoa mwanadamu, Jinsi ya kuunda kikundi cha washindi—matunda ya kwanza, itakuwa hata wazi zaidi baada ya sisi kusoma mafungu machache ya neno la Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Mnapaswa kuona mapenzi ya Mungu na kuona kwamba kazi ya Mungu si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Hiyo ni kwa sababu kazi ya leo ni mabadiliko ya wale waliopotoshwa, wale walio baridi kwa kiasi kikubwa zaidi, ni ili kuwatakasa wale walioumbwa lakini wakashughulikiwa na Shetani. Si uumbaji wa Adamu na Hawa, sembuse kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Wakati wa hatua hii ya kazi Yake, Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu. Baada ya kusoma maandishi haya, je, unaamini kuwa kazi ya Mungu ni rahisi vile?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?).

Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kupambana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu).

Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado inahusu dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo mwanadamu atakapopatwa na Mungu na kutakaswa. … Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

…………

Baada ya kuyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaona kuna ukweli na fumbo kuhusiana na kupata mwili kwa Mungu katika siku za mwisho katika kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ya kutakasa na kumkamilisha mwanadamu badala ya kutubadilisha kwa msemo mmoja. Jinsi Mungu Anatakasa na kufanya mwanadamu kamilifu kwa kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho sio rahisi tunavyofikiria kabisa. Na neno moja, Bwana Yesu Alimfufua Lazaro kutoka kwa kifo. Lakini ili Mungu Atakase na kubadili binadamu ambaye amepotoshwa na shetani kabisa kupinga na kutenda kinyume na Mungu awe binadamu anayeelewa, kumtii na kumwabudu Mungu, kubadili binadamu ambaye amepotoshwa kuwa mashetani wanaoishi kwa milenia kuwa binadamu aliye na ukweli na ubinadamu katika miaka ishirini au thelathini, ni mchakato wa kupambana na Shetani. Je, hili ni suala rahisi? Ikiwa Mungu hufufua wafu na kubadili miili yetu na neno moja, je, hii inaweza kumuaibisha Shetani? Katika siku za mwisho, binadamu amepotoshwa na shetani kwa milenia. Asili na tabia ya Shetani zimetopea kwa mwanadamu. Binadamu ana kiburi, ni mchoyo, muongo, mwovu na mlafi. Kwa ajili ya umaarufu na mali, wanapanga njama dhidi yao wenyewe, wanadanganyana na kuchinjana. Mwanadamu anachukia na kudharau ukweli. Amekuwa adui wa Mungu toka kitambo. Ni aina ya Shetani ambaye anampinga na kumsaliti Mungu. Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu kwa kweli ni pambano na Shetani. Kama tu vile Mwenyezi Mungu anavyosema, “Mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kiasi kikubwa, na umekuwa kitu cha kumpinga Mungu, ambacho kinapinga na kukana waziwazi uwepo wa Mungu. Mwili huu uliopotoka ni vigumu sana kushughulika nao, na hakuna kitu ambacho ni kigumu sana kushughulika nacho au kukibadilisha kuliko tabia potovu ya mwili. Shetani anaingia katika mwili wa mwanadamu ili kuchochea usumbufu, na anatumia mwili wa mwanadamu kuisumbua kazi ya Mungu, na kuharibu mpango wa Mungu, na hivyo mwanadamu amekuwa Shetani, na adui wa Mungu. Ili mwanadamu aweze kuokolewa, kwanza ni lazima achukuliwe mateka. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mungu anainuka na kuingia katika vita na Anaingia katika mwili ili afanye kazi ambayo Amekusudia kufanya, na kupambana na Shetani. Lengo Lake ni wokovu wa mwanadamu, mwanadamu ambaye amepotoshwa, na kushindwa na kuangamizwa kwa Shetani, ambaye ameasi dhidi Yake. Anamshinda Shetani kupitia kazi Yake ya kumshinda mwanadamu, na huku akimwokoa mwanadamu aliyepotoka. Hivyo, ni kazi ambayo inatimiza matatizo mawili kwa wakati mmoja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Mungu anataka kubadili binadamu ambaye amepotoshwa na Shetani kutenda kinyume na Mungu kuwa binadamu anayetii Mungu kwa kweli na anayelingana na Mungu. Ugumu wa kazi hii uko juu kabisa. Ni ngumu zaidi kuliko uumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote na Mungu. Uumbaji wa mbingu na nchi na vitu vyote kutoka utupu ulitimizwa na neno moja la Mungu. Lakini kutakasa na kubadili binadamu aliyepotoka kabisa, Mungu lazima awe mwili na kuonyesha ukweli mingi ili kuhukumu na kutakasa mwanadamu. Ili sisi tupate uzoefu wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, kutupilia mbali upotovu na kupokea utakaso, inahitaji mchakato wa wakati mrefu. Huu pia ni mchakato wa mapambano ya Mungu na Shetani. Kulingana na nia asili ya Shetani, wanadamu wamepotoshwa kuwa mashetani wanaoishi. Ikiwa Mungu anaweza kuwabadilisha mashetani hao wanaoishi kuwa wanadamu, Shetani atashawishika. Kwa hivyo Mungu hufuata mpango Wake wa asili kwa kupata mwili kupambana na aina za Shetani. Kwanza kwa kuonyesha ukweli ili kushinda mwanadamu na kisha kutakasa na kumfanya mwanadamu kamili kwa ukweli. Wakati tunaelewa ukweli na kumjua Mungu, tutaona kwa wazi ukweli wa upotovu wetu na Shetani na kuanza kumchukia Shetani, kumwacha Shetani, na kumlaani Shetani. Hatimaye, tutaasi kikamilifu dhidi ya Shetani na kumgeukia Mungu kabisa. Ili Mungu amnyang’anye Shetani mwanadamu kutoka kwa mikono ya Shetani. Watu hawa ambao wameokolewa ni mateka ya Mungu kutokana na kumshinda Shetani. Kwa kufanya kazi hivi tu ndipo Mungu Anaweza kweli kumshinda na kuaibisha Shetani, ambayo pia ni maelezo ya ndani ya kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Je, tunaelewa uhalisi wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho? Ingawa kazi ya Mungu katika siku za mwisho inakaa miaka ishirini ama thelathini pekee, Alitengeneza kikundi cha washindi, Washindi hawa ni matunda ya kwanza yaliyopatwa na kufurahiwa na Mungu. Ikilinganishwa na historia ya binadamu, je, miaka ishirini au thelathini sio kufumba na kufumbua? Biblia inasema, “siku moja ni kama miaka elfu kwa Bwana, na miaka elfu ni kama siku moja” (2 Petro 3:8). Ikiwa inasema kuwa wakati Bwana Atakaporejea katika siku za mwisho, Atabadilisha miili yetu katika muda mfupi sana, kwa kufumba na kufumbua, pia inafaa kabisa kutumika kwa matokeo yanayopatwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Inaweza pia kupokewa kwa njia hii. Lakini Paulo alisema, “Kwani maongezi yetu yako mbinguni; ambako pia tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo: Atakayeubadilisha mwili wetu wa uovu, ili uweze kuwa kwa kadri ya mwili wake wenye utukufu, kulingana na kufanyika ambapo ataweza kuvitiisha vitu vyote kwake” (Wafilipi 3:20-21), tunaweza kufasiri kwa urahisi maneno ya Paulo kama wale wanaoamini Bwana watabadilishwa mara moja na kubebwa hewani kukutana na Bwana Atakaporejea. Hivyo, tulikaa tu bure tukingoja Bwana ashuke juu ya mawingu kutubadilisha na kutunyakua. Je, neno la Paulo halipotoshi? Hatufai kujazwa na dhana na mawazo kuhusu kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu ni la vitendo, inashikika na inaoneka katika kila hatua. Mwenyezi Mungu mwenye mwili ni Mungu wa Matendo ambaye Anakuja duniani kuokoa mwanadamu kwa kueleza ukweli. Tusipokubali, je, hatuasi dhidi ya Mungu na kumpinga Mungu? Tunaweza kupokea vipi sifa na baraka za Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp