Kwa nini Tunaweza Tu Kumkaribisha Bwana kwa Kusikiliza Sauti ya Mungu?

13/04/2023

Hivi sasa, waumini wote wanatamani Bwana Yesu aje juu ya wingu, kwa sababu majanga yanazidi kuwa mabaya na mapigo ya kila aina yanaongezeka, na njaa na vita vinakaribia. Waumini wanahisi kwamba Bwana anaweza kurudi wakati wowote, na kwamba hawajui ni wakati gani Atashuka juu ya wingu kwa ghafla, kwa hiyo wao hukesha na kuomba usiku na mchana, wakingojea kuwasili Kwake. Hata hivyo, majanga tayari yameanza kuanguka, lakini hadi leo hawajamwona Bwana akitokea juu ya wingu. Watu wengi wanahisi kuchanganyikiwa, wakishangaa, “Kwa nini Bwana bado hajakuja? Je, anazungumza bila uadilifu?” Hakika sivyo. Bwana ni mwaminifu, na maneno ya Bwana hayatabatilika. Wakati hakuna mtu aliyekuwa akitarajia, Bwana tayari alipata mwili kama Mwana wa Adamu na alishuka kwa siri, na watu wengi walimkaribisha zamani. Baada ya kutafuta nyayo za kazi ya Roho Mtakatifu miaka mingi iliyopita, waligundua kwamba Mwana wa Adamu alikuwa akizungumza na kuonyesha ukweli mwingi. Kadiri walivyozidi kusoma maneno haya, ndivyo walivyohisi zaidi kwamba ilikuwa ni sauti ya Roho Mtakatifu, sauti ya Mungu, na hatimaye wakagundua kwamba Mwana wa Adamu huyu ambaye alikuwa akionyesha ukweli alikuwa Bwana Yesu aliyerudi, Alikuwa Mwenyezi Mungu mwenye mwili! Wote walishangilia kwa furaha: “Bwana Yesu amerudi, hatimaye tumemkaribisha Bwana!” Watu wateule wa Mungu walikimbia kueneza habari, wakitoa ushuhuda kwa Mwenyezi Mungu akionyesha ukweli, Akionekana na kufanya kazi. Watu wengi kutoka madhehebu yote waliopenda ukweli na kutamani kuonekana kwa Mungu walisoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kutambua kwamba yalikuwa sauti ya Mungu, walikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu mmoja baada ya mwingine, na kujiunga na karamu ya arusi ya Mwanakondoo. Hili linatimiza unabii wa Bwana Yesu: “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). Kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu pia kulitimiza kikamilifu unabii huu wa Bwana Yesu: “nakuja kwa haraka” “ujio wa Mwana wa Adamu” “atakapokuja Mwana wa Adamu” na “Mwana wa Adamu katika siku Yake.” Hii ilithibitisha kwamba Mungu ni mwaminifu, na kwamba maneno na unabii Wake wote ulipaswa kutimia. Kama tu asemavyo Bwana Yesu, “Mbingu na dunia vitapita lakini maneno Yangu hayatapita hata kidogo(Mathayo 24:35). Na kama asemavyo Mwenyezi Mungu, “Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au mstari mmoja wa kile Ninachosema kitawahi kupita(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 53). Mwokozi wetu Yesu tayari amerudi, na Yeye ni Mungu Mwenyezi. Ameonyesha ukweli mwingi na anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, zamani sana akikamilisha kundi la washindi. Mwenyezi Mungu amemshinda Shetani na kupata utukufu wote, na kwa hayo majanga makubwa yameanza. Tunaweza kuona kwamba kazi ya Mungu yote ina uhusiano wa karibu. Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli mwingi sana, Akiutikisa ulimwengu wote wa kidini, na dunia nzima yenyewe. Hata hivyo, watu wengi wa kidini bado wanatazama angani, wakisubiri Mwokozi Yesu aje juu ya mawingu. Wote wameanguka katika maafa na bado hawajui kinachoendelea, na wanaweza tu kuchukuliwa kuwa mabikira wapumbavu. Kuna watu wengi wapumbavu na wajinga ambao hudanganywa na kudhibitiwa na nguvu za wapinga Kristo katika ulimwengu wa kidini, bado wanahukumu na kushutumu kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Wanajua vyema maneno Yake ni ukweli, lakini hawayakubali. Bado wanashikilia maneno ya Biblia ya Bwana kuja juu ya mawingu, bila kuichunguza njia ya kweli hata kidogo, sembuse kutafuta kuisikia sauti ya Mungu. Kwa sababu hiyo, wameanguka katika majanga, wakilalamika, kulia na kusaga meno yao. Hili ni jambo linalohuzunisha sana. Wengine wanaweza kuuliza, “Kwa nini tunapaswa kuisikiliza sauti ya Mungu ili kumkaribisha Bwana?” Leo nitashiriki ufahamu wangu kidogo wa suala hili.

Kwanza, lazima tuelewe, Bwana angerudi kutoka mbinguni juu ya wingu na kila mtu angeweza kuona tukio hilo, basi hatungehitaji kusikiliza sauti Yake, lakini tu kutegemea macho yetu. Lakini kwa sababu Bwana anarudi katika mwili, kama Mwana wa Adamu, kwa juu juu Yeye ni mtu wa kawaida tu asiye na mfano wa Mungu, na si wa kimiujiza kabisa. Wanadamu ni viumbe wa kufa, wasioweza kumwona Roho wa Mungu. Tunaweza tu kuliona umbo la kimwili la Mwana wa Adamu, kwa hivyo hakuna njia ya kumtambua Mwana wa Adamu katika mwili kando na kuisikiliza sauti Yake. Anaweza tu kutambulishwa kwa matamshi Yake. Ndiyo maana Bwana Yesu alisema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Kama tunavyojua, miaka 2,000 iliyopita, Mungu alifanyika mwili kama Bwana Yesu ili kuwakomboa wanadamu. Aliishi ndani ya ubinadamu wa kawaida, na alikula, kuvaa, kulala na kusafiri kama watu wa kawaida tu. Hakuna aliyejua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, hata familia Yake haikujua, na hata Bwana Yesu Mwenyewe hakujua kwamba alikuwa Mungu mwenye mwili. Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni kila mahali na kuonyesha ukweli mwingi. Aliwafundisha watu kuhusu kuungama dhambi zao na kutubu, uvumilivu na subira, kuwasamehe wengine mara 70 mara 7, kubeba msalaba na kumfuata. Aliwaambia watu wampende Mungu kwa moyo wao wote, nafsi yao yote, na akili zao zote, na kuwapenda wengine kama wanavyojipenda wenyewe. Bwana Yesu pia alifunua siri za ufalme wa mbinguni, akiwaambia watu ni nani awezaye kuingia katika ufalme, na kadhalika. Ukweli huu ulikuwa njia ya toba ulioonyeshwa na Mungu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu, na haukuwa umewahi kusikiwa au kuonekana na wanadamu. Watu wengi waliomfuata Bwana Yesu walifanya hivyo kwa sababu walisikia jinsi maneno ya Bwana Yesu yalivyokuwa na mamlaka na nguvu, mambo ambayo hakuna kiumbe aliyeumbwa angeweza kuonyesha. Waliitambua sauti ya Mungu na kumfuata Bwana. Hawa walikuwa kondoo wa Mungu wakisikia sauti Yake na kumkaribisha Bwana. Wakati huo huo, wale makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa Dini ya Kiyahudi, ingawa wao pia walikubali mamlaka na uwezo wa maneno ya Bwana, lakini kwa sababu tu Bwana Yesu alifanana na Mwana wa Adamu wa kawaida, asiye na familia mashuhuri, wala hadhi na mamlaka ya juu, kwa sababu maneno Yake hayakuwa katika Maandiko, na jina Lake halikuwa Masihi, ambalo halikulingana na unabii wa Maandiko, walimkana na kumkataa Bwana Yesu, na hata kumhukumu, wakisema Yeye alikufuru. Hatimaye, walimfanya asulubishwe, na hivyo waliadhibiwa na kulaaniwa na Mungu. Kwa hiyo tunaweza kuona jinsi ilivyo muhimu kuisikiliza sauti ya Mungu ili kumkaribisha Bwana! Ikiwa hatusikilizi sauti ya Mungu, lakini tuangalie tu sura ya nje ya Mwana wa Adamu, hatutawahi kuona kwamba Yeye ni Mungu. Tutamhukumu na kumkataa tu Bwana kulingana na fikira na mawazo yetu. Katika siku za mwisho, Mungu amekuwa mwili tena kama Mwana wa Adamu ili kuonekana na kufanya kazi. Kama tunataka kumkaribisha Bwana, tunapaswa kutegemea kuisikiliza sauti ya Mungu, kusikiliza kama haya ni maneno ya Mungu, ikiwa ni ukweli, ikiwa yanatoka kwa Roho Mtakatifu. Ni lazima tuweke dhamira yetu juu ya hili. Hapo tu ndipo tunapoweza kumtambua Kristo, udhihirisho wa Mungu, na ni kwa kusikia tu sauti ya Mungu ndiyo tunaweza kumkaribisha Bwana.

Kama Mwenyezi Mungu asemavyo, “Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa ‘Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.’ Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya). “Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaonyesha jinsi ya kutafuta kuonekana kwa Mungu na njia ya kutambua kupata mwili kwa Mungu. Ni dhahiri kabisa: Kristo ndiye njia, ukweli, na uzima; Uungu wa Kristo unafichuliwa hasa kwa kuonyesha ukweli na sauti ya Mungu. Kwa hivyo haijalishi jinsi mwonekano wa Kristo ulivyo wa kawaida wa kawaida, mradi Anaweza kuonyesha ukweli, kuonyesha tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho, basi Yeye ni udhihirisho wa Mungu. Haijalishi jinsi ubinadamu wa Kristo unavyoweza kuwa wa kawaida, mradi Anaweza kuonyesha ukweli, na kuonyesha sauti ya Mungu, basi Yeye ni mtu aliye na kiini cha uungu—Yeye ni Mungu mwenye mwili. Hakuna shaka juu ya hili. Tangu Mwenyezi Mungu alipotokea na kuanza kufanya kazi, watu wengi kutoka madhehebu yote wanaopenda ukweli wamesoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na kugundua kwamba maneno Yake ni ukweli wote, yametoka kwa Roho Mtakatifu na ni sauti ya Mungu kabisa. Kwa hivyo wamethibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Mungu, Yeye ni Mungu mwenye mwili, Bwana Yesu aliyerudi. Huu ni ukweli ambao watu wote wateule wa Mungu wanaweza kuuthibitisha. Mwenyezi Mungu mwenye mwili anaishi miongoni mwa wanadamu, Akila, akiishi na kuingiliana na wengine, akionyesha ukweli, akinyunyizia, kukuza, na kuwaongoza watu wateule wa Mungu wakati wowote au mahali popote. Tumeshuhudia sura za maneno ya Mungu zikionyeshwa moja baada ya nyingine, na sasa yamekusanywa katika vitabu vya maneno ya Mungu kama vile Neno Laonekana katika Mwili, vikiwa na mamilioni ya maneno kwa jumla. Mwenyezi Mungu amefichua mafumbo yote ya kazi ya usimamizi ya Mungu ya miaka 6,000, kama vile malengo ya Mungu katika kuwasimamia wanadamu, jinsi Shetani alivyowapotosha wanadamu, jinsi Mungu amefanya kazi hatua kwa hatua kuwaokoa, siri za kupata mwili, hadithi ya ndani ya Biblia, jinsi kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inavyotakasa na kuwaokoa wanadamu, jinsi Mungu anavyowapanga watu kulingana na aina yao, kutuza mema na kuadhibu maovu ili kutamatisha enzi, jinsi ufalme wa Kristo unavyotimizwa duniani, na kadhalika. Mwenyezi Mungu pia anahukumu na kufichua kiini cha wanadamu kumpinga Mungu na ukweli wa upotovu wao. Anawapa watu njia ya kujiondolea tabia yao potovu na kupata wokovu. Pia anawaambia watu jinsi ya kuanzisha uhusiano ufaao na Mungu, jinsi ya kutenda kuwa mtu mwaminifu, jinsi ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi ya kufuata njia ya Mungu ya kumcha Mungu na kuepuka maovu, jinsi ya kufanikisha utiifu na upendo kwa Mungu, na zaidi. Ukweli huu wote ni ukweli unaohitajika kwa watu kupata uhuru kutoka dhambini na wokovu kamili wa Mungu katika imani yao. Ukweli huu wote unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu unatimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12–13). Kadiri tunavyosoma maneno ya Mwenyezi Mungu, ndivyo mioyo yetu inavyokuwa angavu, na yanatushinda kikamilifu. Kuona uadilifu wa Mungu, utakatifu, ukuu na ghadhabu Yake ikifichuliwa kupitia katika maneno Yake ya hukumu, na kupitia katika tabia ya Mungu isiyokosewa, tunathibitisha kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na ni sauti ya Mungu, ni maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa. Hebu tafakari—mbali na Mungu, ni nani angeweza kufichua siri za kazi ya Mungu? Ni nani angeweza kuonyesha tabia ya Mungu na kila Alicho na Anacho? Kando na Mungu, ni nani angeweza kuhukumu na kufichua kiini potovu cha binadamu? Nani angeweza kuwaokoa binadamu kutoka dhambini? Hakuna shaka kwamba ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuonyesha ukweli, ni Mungu pekee anayeweza kuwatakasa wanadamu kutoka kwa upotovu, na kuwaokoa kutoka dhambini na nguvu za Shetani. Mwenyezi Mungu anaweza kuonekana kama Mwana wa Adamu wa kawaida tu, lakini kutoka katika maneno na kazi Yake, tunaweza kuona kwamba kando na kumiliki ubinadamu wa kawaida, pia ana kiini kitakatifu. Ana Roho wa Mungu anayekaa ndani Yake, na maneno Yake ni maonyesho ya moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye njia, ukweli, na uzima, Yeye ni Mungu mwenye mwili, na ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Kama tu asemavyo Mwenyezi Mungu, “Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. … Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake).

Katika hatua hii, unapaswa kuwa na uwazi zaidi kuhusu kwa nini tunahitaji kuisikiliza sauti ya Mungu ili kumkaribisha Bwana. Kwa kweli, kuisikiliza sauti ya Mungu si vigumu. Kondoo wa Mungu wanaweza kuisikia sauti ya Mungu—hili limeamriwa na Mungu. Kiwango cha elimu cha watu hakijalishi, maarifa yao ya Biblia na kina cha uzoefu hakijalishi, pia. Yeyote aliye na moyo na roho ambaye husoma maneno ya Mwenyezi Mungu anaweza kuhisi kwamba maneno yote ya Mungu ni ukweli, yana mamlaka na nguvu, na ni sauti ya Mungu. Wanaweza kuhisi upendo wa Mungu kwa binadamu, na tabia ya Mungu ya uadilifu na kuu ambayo haitavumilia kosa lolote la binadamu. Hii ni kazi ya hisia za kiroho na uelewa. Hii ni hisia sawa na tunaposoma maneno ya Bwana Yesu, kwa sababu maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Bwana Yesu vyote ni maonyesho ya Roho mmoja. Yanatoka katika chanzo kimoja. Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu mmoja. Hebu tusome vifungu vichache zaidi vya maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu, kana kwamba mtoto mchanga amezaliwa hivi karibuni. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye ‘Mlima wa Mizeituni’ wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni ‘mtoto mchanga’ Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni).

Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).

Kila neno kutoka kwa Mwenyezi Mungu lina nguvu na mamlaka, likiitikisa mioyo ya watu. Mwenyezi Mungue huzungumza na wanadamu wote kama Muumba. Mamlaka na utambulisho wa Mungu hudhihirishwa kwa uwazi kupitia maneno Yake, na sauti ya maneno hayo, nafasi Anayoshikilia, tabia na kile Anacho na Alicho ambavyo vinaonyeshwa, ni sifa za kipekee za Mungu. Hakuna malaika, hakuna kiumbe aliyeumbwa, hakuna roho mwovu wa kishetani ambaye angeweza kumiliki au kufikia haya yote. Maneno ya Mwenyezi Mungu yanafichua kikamilifu mamlaka ya kipekee ya Mungu, na yanaonyesha tabia ya Mungu ya haki na isiyokosewa. Sote tumeona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni maonyesho na sauti ya Mungu.

Leo, maneno ya Mwenyezi Mungu katika Neno Laonekana katika Mwili na video nyingi za usomaji wa maneno ya Mungu zote zinaweza kupatikana mtandaoni, na watu wengi zaidi kutoka katika nchi zote na madhehebu yote wanamchunguza na kumkubali Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, bado kuna watu wengi ndani ya dini ambao wanashikilia maneno ya Biblia, ambao wanashikilia wazo lao la Bwana kushuka juu ya wingu. Wanamwona Mwenyezi Mungu akionyesha ukweli mwingi, lakini hawatafuti, hawachunguzi, au kusikiliza sauti ya Mungu. Wao hata wanakubaliana na nguvu za wapinga Kristo wa ulimwengu wa kidini, wakihukumu, kukashifu na kumshutumu Mwenyezi Mungu. Ni kana kwamba mioyo yao imepofushwa—wanasikia lakini hawajui, na wanaona lakini hawaelewi. Watu kama hao hawana uwezo wa kusikia sauti ya Mungu, ambayo inaonyesha kwamba wao si kondoo wa Mungu. Wao ndio magugu yaliyofichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, mabikira wapumbavu, ambao sasa wameachwa na kuondolewa na Mungu, na kuanguka katika majanga. Ni vigumu kujua ikiwa wataishi au watakufa. Ikiwa wanaweza kuishi, wanaweza tu kumsubiri Bwana Yesu aje juu ya wingu na kuonekana wazi kwa wote baada ya majanga. Lakini kufikia wakati huo, watakapoona kwamba Mwenyezi Mungu waliyemhukumu na kumpinga ndiye Bwana Yesu aliyerudi, watapigwa na butwaa, lakini muda wa majuto utakuwa umeisha. Watabaki wakilia na kusaga meno. Hili linatimiza kikamilifu unabii wa Ufunuo: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7).

Hatimaye, hebu tusome kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya ‘haiwezekani’! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. … Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitapatikana na wanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kunyakuliwa ni Nini Hasa?

Miaka 2,000 iliyopita, baada ya Bwana Yesu kusulubishwa na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, Aliahidi kwamba Atarudi. Tangu wakati huo,...

Mungu Mmoja wa Kweli Ni Nani?

Siku hizi, watu wengi wana imani na wanaamini kwamba kuna Mungu. Wanaamini katika Mungu aliye mioyoni mwao. Kwa hivyo baada ya muda, katika...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp