Je, Kuamini katika Mwenyezi Mungu ni Usaliti kwa Bwana Yesu?

23/04/2023

Imekuwa miaka 30 kamili tangu Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, alipotokea na kuanza kufanya kazi na kuonyesha ukweli mwaka wa 1991. Ameonyesha Neno Laonekana katika Mwili, mamilioni ya maneno Yake, ambayo yote yako mtandaoni, yakiangaza kutoka Mashariki hadi Magharibi kama mwanga mkuu, na kutikisa ulimwengu wote. Watu wengi kutoka madhehebu yote wanaopenda ukweli wameona kwamba maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, na ni Roho Mtakatifu akizungumza na makanisa. Baada ya kusikia sauti ya Mungu, wamemkubali Mwenyezi Mungu kwa hamu. Wameinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na wanahudhuria karamu ya arusi ya Mwanakondoo, wakila na kunywa maneno ya sasa ya Mungu kila siku, na kufurahia riziki ya maji yaliyo hai. Mioyo yao imepata nuru zaidi na zaidi na wamejifunza ukweli kiasi kikubwa. Wanongozwa na kuchungwa na Mungu Mwenyewe. Tabia zao potovu zinatakaswa na kubadilishwa kupitia hukumu ya Mungu na wana ushuhuda mzuri. Wamefanywa na Mungu kuwa washindi kabla ya maafa, na wamekuwa malimbuko, na kupata kibali na baraka za Mungu. Leo, Kanisa la Mwenyezi Mungu linachipuka katika nchi zote ulimwenguni kama vile machipuko ya kwanza baada ya mvua ya masika, na wateule wa Mungu wanafanya kila wawezalo kueneza injili ya ufalme wa Mungu, wakitoa ushuhuda kwa jina la Mwenyezi Mungu. Watu wengi zaidi na zaidi kutoka nchi zote, maeneo yote, na madhehebu yote wanakubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Injili hii ya ufalme inaenea na kupanuka kwa nguvu na kasi isiyozuilika, na kutimiza kikamilifu unabii wa Biblia: “Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake(Isaia 2:2). “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). Hata hivyo, ingawa waumini wengi wamesoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kusadikishwa, na kukiri kwamba yote ni ukweli, kwa kuwa Mwenyezi Mungu anaonekana kama mtu wa kawaida na si Bwana Yesu akija juu ya wingu, hawathubutu kumkubali. Wengine hushikilia maneno halisi ya Biblia, wakichukulia kuwa mstari “Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima” (Waebrania 13:8) unamaanisha kwamba jina la Bwana Yesu halitabadilika kamwe. Kwa kuwa wameona kwamba Mwenyezi Mungu haitwi Yesu, na Biblia haitaji kamwe jina “Mwenyezi Mungu,” hawamkubali. Wanasema kwamba wakimkubali Yeye, na kusoma tu maneno ya Mwenyezi Mungu wala si Biblia, na kuacha kuomba katika jina la Yesu, huo utakuwa usaliti wa wazi kwa Bwana Yesu. Baada ya kumwamini Bwana, na kufurahia neema Zake nyingi kwa miaka nyingi sana, hawawezi kabisa kumsaliti. Hiyo ndiyo mantiki yao, na pia wanawashutumu wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu kama wasaliti wa Bwana Yesu, na kama waasi. Hili limewazuia wengi kuchunguza njia ya kweli, na wanaweza kukiri kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na ni sauti ya Mungu, lakini bado hawathubutu kumkubali. Kama matokeo, wanashindwa na maafa katika maisha yao. Hili ni jambo la kusikitisha, la kipumbavu, na kijinga. Hili linatimiza jambo lingine katika Biblia: “Wapumbavu hukufa kwa ajili ya ukosefu wa hekima” (Mithali 10:21). “Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa(Hosea 4:6). Kwa hivyo, je, kumkubali Mwenyezi Mungu ni kumsaliti Bwana Yesu, au la? Hebu tufanye ushirika kidogo juu ya hili.

Watu wengi hufikiri kwamba kumkubali Mwenyezi Mungu ni kumsaliti Bwana. Njia bora ya kushughulikia suala hili ni ipi? Hatuwezi tu kufuata ukweli kwamba majina Yao ni tofauti, bali lazima tuelewe iwapo Wao ni Roho mmoja, iwapo ni Mungu mmoja anayetenda kazi. Katika Enzi ya Sheria, ni Yehova Mungu aliyekuwa akifanya kazi, na ni Bwana Yesu katika Enzi ya Neema. Tunaweza kuona hapa kwamba jina la Mungu lilibadilika, kwamba Yeye hakuitwa tena Yehova, bali Yesu. Lakini je, unaweza kusema kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu tofauti na Yehova? Je, unaweza kusema kwamba kumwamini Bwana Yesu kulikuwa kumsaliti Yehova Mungu? Sivyo kabisa. Lakini watu wengi wa dini ya Kiyahudi walikataa kumkubali Bwana Yesu, wakisema kwamba huko kungekuwa kumsaliti Yehova, na hata walisaidia kumsulubisha. Kwa nini? Ni kwa sababu hawakutambua kwamba Bwana Yesu alikuwa Roho wa Yehova Mungu akionekana na kufanya kazi katika mwili. Jina lake lilikuwa tofauti, lakini Bwana Yesu na Yehova walikuwa Roho mmoja, Mungu mmoja. Kuna hadithi nzuri sana iliyorekodiwa katika Biblia ya Filipo akimwambia Bwana Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hiyo itatutosha” (Yohana 14:8). Yesu akajibu, “Nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo(Yohana 14:9-10). Maneno ya Bwana Yesu yalikuwa dhahiri sana. Yeye na Yehova walikuwa Mungu mmoja, na Roho Wake alikuwa Roho wa Yehova. Bwana Yesu alikuwa kuonekana kwa Yehova Mungu, Mungu mmoja wa kweli. Na kwa hivyo, kumwamini Bwana Yesu hakukuwa kumsaliti Yehova Mungu, bali kulikuwa kumtii Yehova. Kulikubaliana na mapenzi ya Mungu. Ukishikilia jina moja katika imani yako na kushikilia maneno halisi ya Biblia bila kumwelewa Roho na kazi Yake, huenda ukapotoka na kumpinga Mungu. Kisha unaelekea kumsaliti Mungu, na matokeo ya hilo hayawezi kuwazika. Bwana alipoonekana na kufanya kazi, watu wa dini ya Kiyahudi walimkataa. Je, huko hakukuwa kumsaliti Yehova Mungu? Kiini cha kitendo chao ni usaliti, ndiyo maana Waisraeli walilaaniwa na Mungu. Pia, muda mrefu kabla ya kuonekana kwa Bwana Yesu na kazi Yake, kulikuwa na unabii wa kibiblia kumhusu, uliosema, “Bikira atapata mimba, na atazaa mtoto mwanamume, na watamwita Imanueli(Mathayo 1:23). Lakini Alipokuja, hakuitwa Imanueli—Aliitwa Yesu. Mafarisayo wa dini ya Kiyahudi walishikilia kwa uthabiti maana ya wazi ya Maandiko, na kwa sababu jina jipya la Mungu halikulingana, walifanya juu chini kumkana na kumhukumu Bwana. Bila kujali mafundisho ya Bwana Yesu yalikuwa na mamlaka na uwezo kiasi gani, walikataa kuyakubali, na hatimaye wakamsulubisha, wakifanya dhambi mbaya sana, na kulaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Hili ni somo linalohitaji kuwaziwa sana! Kwa hivyo kuhusiana na kumkaribisha Bwana, je, tunapaswa kufuata kwa uthabiti maana ya wazi ya Maandiko, na jina la Yesu pekee? Kufanya hivyo kunarahishisha sana kuishia kumpinga na kumhukumu Mungu. Hili ni jambo ambalo waumini wengi hawalitambui, kwa hivyo wanashikilia sana maneno halisi katika Biblia na jina la Yesu, na wanapokuwa wakichunguza njia ya kweli, wanaendelea kuuliza, “Je, kuna msingi wowote wa kibiblia wa jina la Mwenyezi Mungu? Iwapo jina la Mwenyezi Mungu haliko katika Biblia, siwezi kumkubali.” Ukisema kwamba hutamkubali isipokuwa jina la Mwenyezi Mungu liwe katika Biblia, basi kwa nini unamwamini Bwana Yesu, na jina Lake halimo katika Agano la Kale? Je, huo si ukinzani? Bila shaka, watu wengi hawaelewi Biblia kwa kweli, lakini wao hushikilia maana ya wazi ya Maandiko na kanuni pasipo kufikiria. Hawaombi, hawatafuti ukweli kutoka katika maneno ya Mungu au uthibitisho kutoka kwa Roho Mtakatifu, na hii hatimaye itawaua. Kwa kweli, kuna unabii wa Biblia kuhusu Mungu kuonekana na kufanya kazi katika siku za mwisho, anayeitwa Mwenyezi Mungu. “Na Watu wa Mataifa wataiona haki yako, nao wafalme wote watauona utukufu wako; na wewe utaitwa kwa jina jipya, jina ambalo kinywa cha Yehova kitalitamka(Isaya 62:2). “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu Wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu Wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu Wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya(Ufunuo 3:12). “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi(Ufunuo 1:8). “Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala(Ufunuo 11:17). “Na nikaisikia sauti kana kwamba ilikuwa sauti ya umati mkubwa, na kana kwamba sauti ya maji mengi, na kana kwamba radi kuu, ikisema, Haleluya: kwani Bwana Mungu mwenye uenzi hutawala(Ufunuo 19:6). Unaweza pia kuangalia Ufunuo 4:8, na 16:7, na zaidi. Vifungu hivi vya Maandiko vilitabiri kwamba Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho, “Mwenyezi,” yaani, Mwenyezi Mungu. Tunaweza kuona kwamba Mungu anaonekana na kufanya kazi katika siku za mwisho akitumia jina Mwenyezi Mungu, na Mungu alipanga hili zamani sana. Wale wote wanaomkubali Mwenyezi Mungu wamesikia sauti ya Bwana na kumtambua Mwenyezi Mungu kama Bwana Yesu aliyerudi. Wamemkaribisha Bwana, wameinuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi, na wanahudhuria karamu ya arusi ya Mwanakondoo. Hao ndio waumini wa kweli, wenye imani sahihi. Hatimaye wamemkaribisha na kumpata Bwana. Wale wanaoshindwa kumkaribisha Bwana watapoteza imani yao kabisa. Watampoteza Bwana. Wale wanaoshikilia jina la Yesu hawatambui sauti ya Bwana anapokuja. Hawamtambui Mwenyezi Mungu kama Roho wa Bwana Yesu anayetokea na kufanya kazi. Bila kukubali kurudi kwa Bwana Yesu, wanamwamini Bwana bila kumtambua. Huko ni kumpinga Bwana, na hakika wao ndio wanaomsaliti Bwana Yesu. Kumsaliti Bwana ni nini? Ni kumwamini bila kumtambua! Mambo yote sasa ni dhahiri zaidi, siyo?

Hivyo, kwa nini jina la Mungu huendelea kubadilika? Kwa nini Yeye huchukua jina jipya katika kila enzi? Kuna siri ya ukweli ndani ya hili. Hebu tuangalie maneno ya Mwenyezi Mungu ili kuyafafanua zaidi. Mwenyezi Mungu anasema, “Kila wakati ambao Mungu Atawasili hapa duniani, Yeye Atabadilisha jina lake, jinsia yake, mfano wake, na kazi yake; Yeye harudii kazi yake, na Yeye daima yu mpya na kamwe si wa zamani. Wakati Alikuja hapo awali, Aliitwa Yesu; Je, anaweza bado kuitwa Yesu anapokuja tena wakati huu? Alipokuja hapo awali, Alikuwa wa kiume, Ataweza kuwa wa kiume tena wakati huu? Kazi Yake Alipokuja wakati wa Enzi ya Neema ilikuwa ya kusulubishwa msalabani; Atakapokuja tena, je, bado Atawakomboa wanadamu kutoka kwenye dhambi? Je, bado Atasulubishwa msalabani? Je, huko hakutakuwa kurudia kazi Yake? Je, hukujua kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani? Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? … Na kwa hivyo, maneno haya ‘Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani’ yanarejelea kazi yake, na maneno haya ‘Mungu habadiliki’ kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima husonga kwenda mbele.

Mungu siku zote huwa Mungu, na kamwe Yeye hatakuwa Shetani; Shetani daima ni Shetani, na yeye hawezi kuwa Mungu. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, haki ya Mungu, na adhama ya Mungu kamwe hayatabadilika. Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na katika kila enzi Yeye huwaruhusu viumbe Wake kuona mapenzi Yake mapya na tabia Yake mpya. Ikiwa watu hawaoni dhihirisho la tabia mpya ya Mungu katika enzi mpya, wao si watamsulubisha msalabani milele? Na kwa kufanya hivyo, si watakuwa wamebaini Mungu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

‘Yehova’ ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. ‘Yesu’ ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. … Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. ‘Yehova’ linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. ‘Yesu’ linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaeleza waziwazi majina ambayo Mungu hutumia katika kazi Yake katika kila enzi na mafumbo ya ukweli yanayohusu majina Yake. Jina la Mungu hubadilika kulingana na enzi na kazi Anayofanya. Kila moja ya majina Yake huwakilisha kazi Anayofanya katika enzi hiyo. Lakini bila kujali jinsi jina la Mungu au kazi Yake inavyoweza kubadilika, kiini Chake hakibadiliki—Mungu daima ni Mungu. Mungu alifanya kazi kwa jina la Yehova katika Enzi ya Sheria, Alitoa sheria na kuongoza maisha ya wanadamu duniani, na kuwafundisha watu dhambi ni nini na jinsi ya kumwabudu Yehova Mungu. Katika Enzi ya Neema, Roho wa Mungu alijivika mwili kama Mwana wa Adamu. Alionyesha ukweli na kufanya kazi ya ukombozi akitumia jina Yesu. Hatimaye, Alisulubishwa na akawa sadaka ya dhambi ya wanadamu, na kutukomboa kutokana na dhambi zetu. Sasa katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili tena na anafanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho kwa jina Mwenyezi Mungu, Anaonyesha ukweli ili kuhukumu na kuwatakasa wanadamu, Anatuokoa kikamilifu kutokana na dhambi, Anatuokoa kutokana na nguvu za Shetani na kutamatisha ulimwengu huu wa kale wenye giza na uovu. Atamwongoza mwanadamu kwenye hatima nzuri. Hivi ndivyo mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu utakavyotimizwa kikamilifu. Ukweli wa kazi ya Mungu unatuonyesha kwamba majina matatu ya Yehova, Yesu, na Mwenyezi Mungu kila jina linawakilisha mojawapo ya hatua tatu tofauti za kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Kwa nje, inaonekana kama jina la Mungu na kazi Yake vinabadilika, lakini kiini cha Mungu hakibadiliki. Tabia ya Mungu na kile anacho na alicho havibadiliki kamwe. Anabaki kuwa Mungu mmoja, anayeongoza, kukomboa, na kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Tunapotazama maneno ya Yehova Mungu katika Agano la Kale kutoka katika Enzi ya Sheria, maneno ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, na sasa maneno ya Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme, tunaweza kuona ukweli huu wote unatoka kwa Roho mmoja na ni matamshi ya Roho yule yule, kwa sababu matamshi ya Mungu katika enzi tofauti yote yana upendo Wake na tabia Yake yenye haki. Kile Mungu anacho na alicho vimo ndani ya maneno hayo. Upendo wa Mungu, tabia ya Mungu, na kile anacho na alicho vyote vinaunda kiini cha Mungu mmoja wa kweli, mali na nafsi ya Mungu mmoja wa kweli. Katika Enzi ya Neema, kumsikia Bwana Yesu akizungumza kulikuwa tu kama kusikia sauti ya Yehova Mungu. Tunaposikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu, ni kana kwamba Bwana Yesu anazungumza nasi binafsi, na Yehova Mungu anazungumza nasi. Hii inathibitisha kabisa kwamba hatua tatu za kazi ya Mungu zinatekelezwa na Mungu mmoja. Jina la Mungu hubadilika, lakini kiini Chake, kile Anacho na alicho, na tabia ya haki Anayoonyesha ni sawa, bila mabadiliko hata kidogo. Kazi yote ya Mwenyezi Mungu leo inafuata kazi ya Bwana Yesu. Ni hatua ya kazi iliyo juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ambayo ni ya kina zaidi na iliyoinuliwa zaidi—kazi ya kutakasa na kuokoa binadamu kikamilifu. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli kiasi kikubwa sana, na mabli na kufichua mafumbo ya Biblia, pia Anafichua mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu, kama vile malengo ya Mungu katika kazi Yake ya usimamizi, jinsi Mungu anavyotumia hatua Zake tatu za kazi kumwokoa mwanadamu, mafumbo ya kupata mwili, jinsi Mungu anavyowahukumu, kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, jinsi matokeo na hatima ya kila aina ya mtu inavyoamuliwa, jinsi ufalme wa Kristo unavyotimizwa duniani, na zaidi. Mungu pia anafichua ukweli wa mwanadamu kupotoshwa na Shetani, Anahukumu na kufichua asili ya mwanadamu ya kishetani, inayompinga Mungu. Pia Anafafanua kila kipengele cha ukweli ambao wanadamu wanapaswa kutia katika vitendo, na kutupa njia za utendaji za kuondokana na upotovu wetu na kubadili tabia zetu. Ukweli ambao Mwenyezi Mungu anaonyesha ni ukweli wote ambao mwanadamu anahitaji ili kutakaswa na kupata wokovu kamili, na kutimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). Kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inawatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu na kuwaleta watu wote ambao Mungu aliamua kabla kuwaokoa mbele Yake ili watakaswe kupitia hukumu na kuadibu. Tayari amekamilisha kundi la washindi kabla ya maafa. Sasa maafa makubwa yameanza, na Mungu ameanza kulipa wema na kuadhibu uovu. Wale wote ambao ni wa Shetani, wanaompinga Mungu, wataangamizwa, wakati wale wanaotakaswa kupitia hukumu ya Mungu watalindwa na kutunzwa na Mungu hadi mwisho wa maafa. Baada ya maafa, ufalme wa Kristo utaonekana duniani, na kutimiza unabii huu wote wa Ufunuo: “Falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele(Ufunuo 11:15). “Haleluya: kwani Bwana Mungu mwenye uenzi hutawala(Ufunuo 19:6). “Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita(Ufunuo 21:3-4). Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli, na kufanikisha kazi nzuri sana. Hii inathibitisha kwamba Yeye ni Roho wa Mungu katika mwili, Anayeonekana ili kufanya kazi kama Mwana wa Adamu. Yeye haitwi Yesu, na hana sura ya Bwana Yesu wa Kiyahudi, lakini Roho wa Mwenyezi Mungu ni yule wa Bwana Yesu—Yeye ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Mwenyezi Mungu, Bwana Yesu, na Yehova wote ni Mungu mmoja. Ukishaelewa hili ipasavyo, huwezi kabisa kudai kwamba kumwamini Mwenyezi Mungu ni kumsaliti Bwana Yesu, kwa sababu kumkaribisha Mwenyezi Mungu ni kumkaribisha Bwana, kufuata nyayo za Mwanakondoo, na kuinuliwa mbele za Mungu! Wengi katika ulimwengu wa kidini bado wanashikilia maana ya wazi ya Maandiko, wanashikilia jina la Bwana Yesu, wakimngoja Ashuke juu ya wingu, na wanakataa kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Bila kujali Anaonyesha ukweli kiasi gani, wanakataa kukiri kwamba ukweli huu unatoka kwa Roho wa Mungu, kwamba huyu ni Roho wa Bwana Yesu anayeonekana na kufanya kazi. Hata wanamhukumu na kumkataa Mwenyezi Mungu anayetuletea ukweli. Je, hawafanyi kosa lile lile walilofanya Mafarisayo? Wanafikiri huku ni kujitoa kwa Bwana Yesu, lakini Bwana aliwahukumu kuwa watenda maovu. Bwana Yesu alisema, “Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:22-23). Na hivyo, Bwana atawaondoa.

Hebu tuangalie maneno zaidi ya Mwenyezi Mungu ili kumalizia. “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp