Kwa Nini Mungu Anafanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

13/04/2023

Leo hii, ugonjwa wa mlipuko unaenea duniani kote, na maafa yanazidi kuwa mabaya. Tumeona matetemeko ya ardhi, njaa, na vita, na waumini wote wanatazamia kwa hamu kuja kwa Mwokozi, Bwana Yesu, kuinuliwa juu angani ili kukutana na Bwana, na kuepuka mateso ya majanga haya haraka iwezekanavyo. Lakini baada ya kungoja kwa miaka mingi, bado hawajamwona Mwokozi, Bwana Yesu, akishuka juu ya mawingu, sembuse kumwona mtu yeyote akiinuliwa juu angani ili kumlaki Bwana, jambo ambalo limewaacha wengi wakiwa wamevunjwa matumaini. Watu wengi wanashaanga kabisa kwamba badala ya kukaribisha kuwasili kwa Yesu juu ya mawingu, wanaona Umeme wa Mashariki likiwa na ushuhuda wa kurudia kuhusu kurudi kwa Bwana kama Mwenyezi Mungu, ambaye huonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu. Ushuhuda huu huushika usikivu wa watu, ili wauone dhahiri kabisa. Hata hivyo, kutokana na ukandamizaji na kukamatwa kwa kishindo na CCP na kufuru na kashfa mbaya kutoka kwa majeshi ya wapinga Kristo katika ulimwengu wa kidini, watu walipuuza na kutupilia mbali suala la kuichunguza njia ya kweli. Bila kutarajiwa, katika miaka michache tu, Mwana wa Adamu, ambaye alidharauliwa sana, alionyesha ukweli mwingi, watu zaidi na zaidi wameisikia sauti ya Mungu, wote walisimama kumfuata Mwenyezi Mungu. Hili halijautikisa ulimwengu mzima wa kidini tu, bali pia dunia nzima. Neno Laonekana katika Mwili huangaza kama mwanga wa kweli kutoka mashariki hadi magharibi, ukiuangaza ulimwengu mzima, na wale wanaopenda ukweli na kutamani kuonekana kwa Mungu huja kwenye mwanga, huisikia sauti ya Mungu, na kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Ukweli huu umemwacha kila mtu akiwa na mshangao: Huyu ni mtu wa aina gani? Alitoka wapi? Alifanyaje jambo lenye nguvu kiasi hiki? Watu wengi wameuliza: Je, hakika Umeme wa Mashariki ni udhihirisho na kazi ya Mungu? Je, inawezekana kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni sauti ya Muumba inayozungumza na binadamu? “Haiwezekani,” wanafikiri, “Bwana atakaporudi, jambo la kwanza atakalofanya ni kuwainua waumini wakukutane na Yeye angani. Kamwe hataruhusu waumini Wake waanguke katika maafa na hatazungumza kufanya kazi ya hukumu. Hilo haliwezi kutendeka.” Leo, watu wengi wanatazama sinema, nyimbo, na video za ushuhuda za Kanisa la Mwenyezi Mungu, na muhimu zaidi, usomaji wa neno la Mwenyezi Mungu. Kuna kisima chenye maudhui mengi, na maisha katika Kanaani ni tukio la ajabu sana. Ukweli huu unalazimisha watu kukubali kwamba ni kazi ya Roho Mtakatifu pekee na hakuna mtu angeweza kufanikisha hili. Bila kuonekana na kazi ya Mungu, hakuna mtu angeweza kutimiza mambo makubwa kama haya. Hili huwafanya waumini wengi katika Bwana wajiulize: Kwa nini Mungu anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Tumesamehewa dhambi zetu, na Mungu ametuhesabia haki, hivyo kwa nini tunapaswa kupitia hukumu na kuadibu? Hukumu ya Mungu katika siku za mwisho inapaswa kuwalenga wasioamini, kwa hivyo mbona hukumu inaanza na nyumba ya Mungu? Ni nini hasa kinachoendelea hapa? Mada hii itakuwa lengo la ushirika wetu leo.

Kabla ya kuanza ushirika wetu, kwanza tuwe wazi, ukweli kwamba Mungu anakuja katika mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu ni jambo ambalo lilipangwa na Mungu zamani sana. Haijalishi ni mawazo ya watu ni yapi au vizuizi ni vikubwa vipi, kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho haiwezi kubadilishwa kwa mapenzi ya mwanadamu, na haiwezi kusimamishwa na nchi au nguvu yoyote. Hivyo, watu wengine watauliza, je, kuna msingi wa kibiblia kwa kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho? Bila shaka kuna msingi wa kibiblia, na ni wenye nguvu kabisa. Kuna angalau marejeleo mia mbili ya “hukumu” katika Biblia nzima, na Bwana Yesu pia alitabiri mwenyewe kurudi Kwake katika siku za mwisho kama Mwana wa Adamu mwenye mwili ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu. Sasa, hebu tuorodheshe sehemu chache za unabii wa Bwana Yesu. “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47–48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana. … Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:22, 27). “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12–13). Pia kuna 1 Petro 4:17, “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu.” Maneno haya ni wazi kabisa: “Neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho,” “amekabidhi hukumu yote kwa Mwana” “lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” “Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote.” Tunaweza kuona kwamba Bwana atakuja kama Mwana wa Adamu atakaporudi katika siku za mwisho, kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Hili halina ubishi. Leo, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli mwingi na kutekeleza kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kuhukumu na kuwatakasa wote wanaokuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kuwaongoza watu wateule wa Mungu katika kuingia katika ukweli wote. Na Mungu amefanya kundi la washindi kabla ya maafa. Hili linatufanya tuone kwamba unabii huu unatimizwa kabisa na kukombolewa.

Kwa hivyo, wengine watauliza, dhambi zetu tayari zimesamehewa kwa sababu tunamwamini Bwana, kwa hivyo kwa nini tunahitaji kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho? Maneno ya Mwenyezi Mungu yanafichua fumbo hili la ukweli, kwa hivyo hebu tuangalie kile ambaho Mwenyezi Mungu anasema. Mwenyezi Mungu anasema, “Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. … Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Maneno ya Mwenyezi Mungu ni Dhahiri kabisa. Kile ambacho Bwana Yesu alifanya katika Enzi ya Neema ilikuwa ni kazi ya ukombozi. Tukimwamini Bwana, tuungame dhambi zetu, na kutubu, dhambi zetu zinasamehewa. Hatuhukumiwi tena na kuuawa kwa kuvunja sheria, na tunaweza kufurahia neema nyingi za Bwana. Lakini, je, msamaha wa dhambi unamaanisha kuwa tuko huru kutoka dhambini na tumefanywa watakatifu? Je, msamaha wa dhambi unamaanisha tumefikia utiifu wa kweli kwa Mungu? Sivyo kabisa. Sote tunaona dhahiri kwamba waumini hutenda dhambi mchana na kuungama dhambi zao usiku. Tunaishi katika mtego huu, mara nyingi tunatenda dhambi bila hiari, na sote tunamwomba Bwana kusema, “Kwa kweli ninateseka, kwa nini nisiweze kujinasua kutoka kwa mainyororo ya dhambi?” Sote tunataka kujikomboa kutoka katika mitego ya kidunia na kutumia kwa ajili ya Bwana, tunataka kumpenda Bwana kwa kweli na kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe, lakini tunachofanya ni bila hiari, na hatuwezi hata kutatua tatizo la kusema uwongo mara kwa mara. Kwa nini hivi? Kwa sababu watu wana asili ya dhambi na tabia potovu, na hiki ndicho chanzo cha dhambi. Tusipotatua chanzo cha dhambi, hata tukijaribu kujizuia, bado tunatenda dhambi bila hiari. Ingawa baadhi ya watu wanaweza kujitumia kwa ajili ya Bwana kwa dhati, kuteseka, kulipa gharama, na kuvumilia bila malalamiko, lakini katika vina vya mioyo yao, je, wanaweza kumtii Mungu kwa kweli? Je, wanampenda Mungu kwa kweli? Watu wengi hawaoni jambo hili waziwazi. Ili kupata baraka, kuingia katika ufalme wa mbinguni, na kupata tuzo, watu wanaweza kufanya mambo mengi mazuri, lakini ni uchafu gani unaochanganywa na matendo haya mema? Je, wamechafuliwa na mabadilishano au nia zozote? Maafa yakija, na tusiinuliwe juu, lakini badala yake tutupwe ndani ya maafa, je, tutamlalamikia Mungu? Je, tutamlaumu na kumkana Mungu? Kazi ya Mungu inapolingana na fikira za binadamu, tunamshukuru na kumsifu Mungu, lakini kazi ya Mungu isipolingana na fikira zetu na isiwe kile tunachotaka, je, tutamhukumu na kumshutumu Mungu? Kwa mfano, Bwana Yesu anapowaambia wale wanaohubiri na kutoa pepo katika jina Lake, “Tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:23)”, je, watu hao watakuza fikira na kumpinga na kumhukumu Bwana? Fikiria kwamba ikiwa Bwana Yesu bado angekuja katika sura ya Mwana wa Adamu wa Kiyahudi, ili kuonyesha ukweli katika makanisa, ni watu wangapi katika ulimwengu wa kidini wangemkana na kumwacha Bwana? Ni watu wangapi wangekubali ukweli ulioonyeshwa na Bwana Yesu na kusema kwamba Yeye ndiye Mungu mmoja wa kweli? Ni watu wangapi wangemhukumu Bwana Yesu kama mwanadamu badala ya Mungu? Ni vyema kutafakari juu ya ukweli huu. Mafarisayo wa Dini ya Kiyahudi walikuwa watu waliomwamini Mungu kwa vizazi vingi, na ambao mara nyingi walimtolea Mungu sadaka za dhambi. Yehova Mungu alipopata mwili na kuwa Bwana Yesu, kwa nini Mafarisayo hawakujua kwamba Yeye alikuwa mwonekano wa Yehova Mungu? Kwa nini walimhukumu Bwana Yesu, ambaye alionyesha ukweli? Kwa nini Bwana Yesu alitundikwa msalabani? Kiini cha tatizo ni kipi hapa? Kwa nini Mafarisayo hawakujua kuonekana na kazi ya Mungu, licha ya mababu zao kumwamini Mungu kwa vizazi vingi? Kwa nini bado walimhukumu na kumpinga Mungu? Sote tumeona kwa macho yetu kwamba Mungu ameonekana na kufanya kazi kama Mwana wa Adamu mwenye mwili katika siku za mwisho na kuonyesha ukweli mwingi. Kwa hivyo kwa nini watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanapinga, kushutumu, na hata kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa hasira? Ikiwa Bwana Yesu angerudi, akiwa bado na sura ya Mwana wa Adamu wa Kiyahudi, na kuonyesha ukweli katika ulimwengu wa kidini, je, Angetimuliwa kutoka kanisani, au hata kuhukumiwa na kuuawa? Yote yanawezekana. Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli kwa njia sawa na Bwana Yesu, na wote wawili ni Mwana wa Adamu wa kawaida. Ulimwengu wa kidini unampinga Mwenyezi Mungu kwa hasira sana, kwa hivyo wangeweza kumkaribisha Bwana Yesu katika sura ya Mwana wa Adamu? Kwa nini ulimwengu wa kidini bado unawahukumu watu wanaomfuata Mwenyezi Mungu kama waumini wa mtu badala ya Mungu? Kama wangelizaliwa wakati wa Bwana Yesu, je, si wangewahukumu wale wanaomfuata Bwana Yesu kuwa waumini wa mtu badala ya Mungu? Nini, hasa, ndicho kiini cha tatizo hili? Hili hutokea kwa sababu binadamu wapotovu wote wana asili ya kishetani, na sote huishi kwa kufuata tabia zetu za kishetani. Hii ndiyo sababu si ajabu hata kidogo kwamba tunampinga na kumhukumu Mungu. Watu wengi hawaoni hili wazi wazi. Wanafikiri kwamba mara tu dhambi zetu zinaposamehewa na kwamba Mungu hatuoni kuwa wenye hatia, tunakuwa watakatifu. Wanafikiri kwamba dhambi zetu zikishasamehewa, tunaweza kupata kibali cha Mungu kupitia kwa matendo mema. Maoni haya ni potovu sana. Ukweli kwamba Mafarisayo walimpinga na kumhukumu Bwana Yesu unatosha kuona wazi kwamba watu wana asili ya kishetani na tabia potovu, kwa hiyo haijalishi ni miaka mingapi tunamwamini Mungu, tunaielewa Biblia kwa kiasi gani, au tunazaliwa katika enzi gani, sisi sote bado tunachukia ukweli, tunampinga Mungu, tunamhukumu Mungu, na ni wakatili kwa Mungu. Kwa sababu hii pekee, kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ni muhimu! Kwa sababu ya asili yetu ya kishetani, wanadamu potovu wanapaswa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Bila hukumu hii na kuadibu, kwa jinsi tulivyo wapotovu, tutatenda dhambi na kumpinga Mungu daima, hatutakuwa watiifu wa kweli kwa Mungu au kupatana na Mungu, na hatutawahi kustahili kamwe kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ingawa sote tunajua na kuelewa kwamba tabia ya Mungu ni yenye haki, hakuna anayeweza kuona hali ya kuogofya ya kupotoshwa kwetu kwa kina na Shetani, ni kwa kiwango gani tunaweza kumpinga Mungu, au ni kwa kiasi gani tunaweza kumchukia Mwana wa Adamu ambaye anaweza kuonyesha ukweli, ambayo ni kusema, kiwango ambacho tunaweza kuchukia ukweli. Watu hawawezi kuona lolote kati ya mambo haya kwa uwazi. Kwa hivyo, kila mara tuna shaka na fikira nyingi kuhusu kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kila mtu anafikiri kwamba kusamehewa dhambi zetu kunatufanya tuwe watakatifu. Iwapo Mungu hatuchukulii kuwa wenye dhambi, sisi ni watakatifu, kazi ya Mungu ya wokovu imekamilika, Mungu hahitaji tena kufanya kazi ya hukumu. Bwana Yesu atakaporudi, Atatuleta katika ufalme wa mbinguni, na mara tu tunapofika mbinguni, tunahakikishiwa kumtii Mungu na kumwabudu Mungu milele. Lakini je, huu si upuuzi mtupu tu? Watu wanamwamini Mungu duniani na kufurahia neema ya Mungu, lakini bado wanamhukumu na kumshutumu Mungu, hivyo wanawezaje kumtii na kumwabudu Mungu mbinguni? Hili haliwezekani kabisa. Maneno ya Mungu yanasema, “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana(Waebrania 12:14). Sentensi hii ni ukweli, na ni sharti la mbinguni! Sasa tunapaswa kuelewa ni kwa nini Mungu anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Katika uchanganuzi wa mwisho, Mungu amekuja kuwaokoa watu kabisa, ambayo ina maana ya kutakasa na kubadilisha tabia zetu potovu, na vile vile kutuokoa kabisa kutoka dhambini na nguvu za Shetani. Leo, Mwenyezi Mungu alionyesha ukweli wote unaohitajika kutakasa na kuwaokoa binadamu, na Anafanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Watu wengi wateule wa Mungu wamepitia hukumu ya Mungu, kutakasa tabia zao potovu, na sasa wanasifu haki na utakatifu wa Mungu kwa dhati. Wameona jinsi ambavyo watu wamepotoshwa kwa kina na Shetani, ni dhambi zipi hasa wanazoweza kufanya, na ni kiasi gani ambacho wanaweza kumpinga Mungu. Wamefikia kujielewa halisi, wameona ubaya wa upotovu wao wa kishetani, na wote wanahisi kwamba ikiwa hawatapitia hukumu na utakaso wa Mungu, na badala yake waishi katika tabia zao za kishetani, wao wanampinga Mungu, wanamsaliti Mungu, wakiishi kama mashetani, watapelekwa kuzimuni na kuadhibiwa na Mungu, na hawastahili kuishi mbele ya Mungu, kwa hiyo wanahisi majuto makubwa, wanajichukia wenyewe, na wanafikia toba na mabadiliko ya kweli. Wakati tu tunapopitia hukumu na kuadibu kwa Mungu ndipo tunajua kwamba kazi ya hukumu ya Mungu ni wokovu Wake mkuu na upendo mkuu kwa wanadamu.

Watu wengi hawaelewi umuhimu wa kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho na wanafikiri kwamba baada ya Bwana Yesu kumaliza kazi ya ukombozi, binadamu waliokolewa kabisa na kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikamilika, lakini hili ni kosa kubwa! Maneno ya Mwenyezi Mungu ni Dhahiri kabisa. Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho iliitamatisha Enzi ya Neema. Wakati huo huo, iliianzisha Enzi ya Ufalme. Kipengele kimoja cha hukumu katika siku za mwisho ni kuwatakasa na kuwaokoa watu kabisa, kutuweka huru kutoka dhambini na kutoka kwa nguvu za Shetani, na kuturuhusu kupatwa kabisa na Mungu. Kipengele kingine ni kufichua kila aina ya watu na kuwatenganisha kulingana na aina yao, kuharibu nguvu zote za uovu zinazompinga Mungu, na kuikomesha enzi hii nzee yenye giza na uovu. Huu ndio umuhimu wa kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Hebu tusome kifungu kingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu. “Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. … Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). Katika siku za mwisho, Mungu anaonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu, ambayo inafichua kila aina ya mitazamo ya watu kwa ukweli na kwa Mungu. Wale wanaopenda ukweli na kufuatilia upendo kwa Mungu, ndio walengwa wa wokovu na kukamilishwa na Mungu. Wanaisikia sauti ya Mungu, wanarudi kwenye kiti Chake cha enzi, wanakula na kunywa maneno ya Mungu kila siku, wanapitia hukumu, kuadibu, majaribio, na usafishaji wa Mungu, hatimaye wanawekwa huru kutoka kwa utumwa na udhibiti wa dhambi, wanafikia utakaso na mabadiliko ya tabia zao potovu, na kisha wanakamilishwa na Mungu na wanakuwa washindi, ambayo ni kusema, malimbuko. Hata hivyo, wale wanaochukia ukweli na kumpinga Mungu ndio walengwa wa kuachwa na kuondolewa na Mungu. Wanashikilia kwa ukaidi maandishi ya Biblia, na kungoja tu Bwana aje juu ya mawingu huku wakimpinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu kwa hasira. Kwa kufanya hivyo, wanapoteza nafasi yao ya kuinuliwa juu kabla ya maafa, na wataanguka katika janga, watalia na kusaga meno yao. Kuna wengine ambao hutafuta tu baraka na kumkubali Mwenyezi Mungu bila kupenda ili kuepuka maafa. Wanaamini katika neno tu, na asili zao ni kuchukia ukweli. Wanamwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hawatendi ukweli kamwe, wanakataa kukubali au kutii hukumu, kuadibu, upogoaji, na ushughulikiaji wa Mungu, na tabia zao potovu hazibadiliki hata kidogo. Watu kama hao ni wasioamini na watenda maovu ambao wamechanganyika katika nyumba ya Mungu, na wote watafunuliwa na kuangamizwa. Hii inaonyesha kwamba kazi ya hukumu katika siku za mwisho tayari imefichua kila aina ya mtu. Mabikira wenye busara na mabikira wapumbavu, wale wanaopenda ukweli na wale wanaotafuta tu kujaza matumbo yao kwa mkate, ngano na magugu, na mbuzi na kondoo wote wamegawanywa katika makundi tofauti. Hatimaye Mwenyezi Mungu atatuza mema na kuadhibu maovu, na kumtuza kila mtu kulingana na yale aliyoyatenda. Hii inaonyesha kikamilifu tabia ya Mungu yenye haki, na pia inatimiza unabii huu katika Ufunuo, “Yule aliye dhalimu, basi aendelee kuwa dhalimu; na yeye aliye mtakatifu, na awe mtakatifu bado; na yeye aliye mwenye haki, awe mwenye haki bado: na yeye aliye mtakatifu, awe mtakatifu bado(Ufunuo 22:11). “Tazama, Naja upesi; na Nina thawabu Yangu, kumpa kila mwanadamu kulingana na vile matendo yake yatakuwa(Ufunuo 22:12).

Leo, Mwenyezi Mungu tayari ameunda kundi la washindi kabla ya maafa, na kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu imepata mafanikio makubwa. Maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yameenea kwa mataifa yote duniani na kuutikisa ulimwengu, na kuthibitisha kwamba Mungu amemshinda Shetani na kupata utukufu. Kufuatia haya, Mungu atashusha maafa na kuanza kuyahukumu mataifa na watu wote. Kuja kwa maafa ni hukumu ya Mungu kwa enzi hii yenye uovu na pia ni kuwaokoa binadamu. Mungu hutumia maafa kuwalazimisha watu waitafute na kuichunguza njia ya kweli, wapate kuonekana na kazi ya Mwokozi, waje kwa Mungu, na waukubali wokovu Wake. Wakati huohuo, pia Yeye hutumia maafa kumaliza nguvu zote za uovu na waovu wanaompinga Mungu na kuitamatisha kabisa enzi hii ya uovu ambayo Shetani anashikilia mamlaka. Hatimaye, wale wote ambao wamepitia hukumu ya Mungu na wametakaswa watalindwa na Mungu katikati ya maafa, na kisha Atawaleta kwenye hatima nzuri. Hivi ndivyo kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho itakamilishwa. Baada ya hapo, katika ulimwengu mpya, ufalme wa Kristo utatimizwa kikamilifu duniani.

Hatimaye, hebu tusome vifungu viwili vya maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Sababu ya kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu katika kiini ni ili kuwatakasa binadamu kwa ajili ya pumziko la mwisho; bila utakaso wa aina hii, hakuna binadamu yeyote angeainishwa katika makundi tofauti kulingana na aina yakeama kuingia katika pumziko. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. … Kusudi lote la kazi kuu ya Mungu ya kuadhibu maovu na kuthawabisha mema ni kuwatakasa kabisa wanadamu wote ili Aweze kuleta ubinadamu mtakatifu katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mungu Mmoja wa Kweli Ni Nani?

Siku hizi, watu wengi wana imani na wanaamini kwamba kuna Mungu. Wanaamini katika Mungu aliye mioyoni mwao. Kwa hivyo baada ya muda, katika...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp