Hukumu ni nini?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, tunaweza kuona ukweli kwamba chanzo cha ukweli ni Mungu, na chanzo cha vitu vyote chanya ni Mungu. Palipo na vurugu na upotovu wa Shetani na dhambi ya kumpinga Mungu, hapo hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa hakika hufuata. Popote ambapo hukumu ya Mungu ipo, pana kuonekana kwa ukweli na ufunuo wa tabia ya Mungu. Ukweli na tabia ya Mungu hufichuliwa wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu. Palipo na ukweli pekee ndipo pana hukumu na kuadibu; palipo na hukumu na kuadibu pekee ndipo pana ufunuo wa tabia ya Mungu ya haki. Kwa hivyo, popote ambapo hukumu na kuadibu kwa Mungu kupo hapo tunapata nyayo za kazi ya Mungu, na ndiyo njia ya kweli zaidi ya kutafuta kuonekana kwa Mungu. Mungu pekee ndiye ana mamlaka ya kutoa hukumu, na Kristo pekee ndiye ana uwezo wa kuhukumu wanadamu waliopotoka. Hii inathibitisha na kuonyesha kwamba Mwana wa Adamu—Kristo—ndiye Bwana wa hukumu. Bila ya hukumu na kuadibu kwa Mungu watu hawana njia ya kupata ukweli, na hukumu na kuadibu ni kule kunakoonyesha tabia ya Mungu ya haki, kwa kuwapa wanadamu fursa ya kumjua Mungu. Mchakato ambao kwao wanadamu wanauelewa ukweli ni mchakato ambao kwao wanamjua Mungu. Ukweli kwa wanadamu waliopotoka ni hukumu, uchunguzi, na kuadibu. Kinachofichuliwa na ukweli hasa ni haki ya Mungu, uadhama, na ghadhabu. Watu ambao wanauelewa ukweli wanaweza kujikomboa kutokana na upotovu na kujinasua kutokana na ushawishi wa Shetani. Hii inatokana kabisa na nguvu na uweza wa maneno ya Mungu. Mungu anawaokoa watu na kuwakamilisha watu ili kuwaruhusu watu waelewe ukweli na kupata ukweli. Kadiri watu wanapozidi kuelewa ukweli, ndipo wanapozidi kumjua Mungu. Kwa njia hii, watu wanaweza kuachana na upotovu na kufikia utakaso. Watu wanapoishi kwa kudhihirisha ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli, watakuwa wanaishi katika nuru, wanaishi katika upendo, na wanaishi mbele ya Mungu. Haya ndiyo matokeo ambayo Kristo hutimiza kwa kuwasilisha ukweli na kutoa hukumu. Kwa kweli, maneno yote yanayosemwa na Mungu ni ukweli na ndiyo hukumu kwa jamii ya wanadamu. Haijalishi ni enzi gani, maneno ambayo Mungu ananena yana athari ya hukumu. Katika Enzi ya Sheria, maneno ya Yehova Mungu yalikuwa ndiyo hukumu ya wanadamu waliopotoka. Katika Enzi ya Neema, maneno yaliyonenwa na Bwana Yesu ndiyo yaliyokuwa hukumu ya wanadamu waliopotoka. Sasa katika Enzi ya Ufalme, yote ambayo Mwenyezi Mungu anasema katika kazi Yake ya kuhukumu na kuadibu ni hukumu hata zaidi, ambayo hatimaye yatafanya jamii ya wanadamu iweze kuona kwamba hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu ni upendo mkubwa wa Mungu. Kile ambacho hukumu na kuadibu kwa Mungu hutoa kwa jamii ya wanadamu ni wokovu na ukamilifu. Ni kwa kukubali na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu pekee ndipo mtu hupata upendo wa kweli wa Mungu na wokovu kamili. Wale watu wote ambao wanakataa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu watapata adhabu ya Mungu na watazama katika uharibifu na kuangamia kabisa….

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp