Unashuhudia kuwa katika siku za mwisho Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa, lakini baada ya kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ninaona kwamba baadhi yayo humhukumu na kumlaani mwanadamu. Kama Mungu humhukumu na kumlaani mwanadamu, si basi mwanadamu atapatwa na adhabu? Na unawezaje kusema kwamba aina hii ya hukumu huwatakasa na kuwaokoa wanadamu?

08/06/2019

Jibu:

Katika siku za mwisho, Mungu huonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ili kuunda kikundi cha washindi, kundi la wale ambao ni wenye moyo mmoja na akili moja na Mungu. Hii iliamuliwa na Mungu alipoumba ulimwengu. Unaweza kusema kuwa tayari Mungu amelifanya kundi la washindi, kwamba wote wamefanyika kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kwamba wametoka katika taabu za mateso ya kikatili ya Chama Cha Kikomunisti cha China. Ni ukweli kwamba tayari Mungu amefanya jambo hili; hakuna mtu anayeweza kulipinga. Kuna watu wengine ambao wanaona kwamba baadhi ya maneno ya Mungu yana shutuma na laana ya watu na wao hukuza mawazo. Huu ni upumbavu. Hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni kiti cheupe cha enzi cha hukumu kilichotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Mungu hufichua tabia Yake yenye haki, uadhama, na ghadhabu, na kuwafichua wanadamu na kutofautisha kila aina ya mtu. Hata zaidi, ni ili kumaliza enzi ya zamani na kuwaondoa wale ambao ni wa Shetani. Hivyo kwa wale wote wa Shetani wanaompinga Mungu, je, Mungu hangewahukumu na kuwalaani? Ingawa kuna maneno fulani ya hukumu na ya kufunua upotovu uliofichuliwa na wateule wa Mungu na mfano wao wa kweli ulipotoka, na haya yanaonekana kuwa hukumu, hii ni kwa ajili ya kuruhusu wateule wa Mungu waone waziwazi asili ya tabia zao potovu na kubaini kitovu cha suala hilo, na kuzaa matunda ya kuelewa ukweli. Mungu asingekuwa mkali sana, kama maneno Yake hayangegonga ndipo, tusingeweza kutambua mfano wetu mbaya na asili za shetani, na isingewezekana kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kufikia matokeo ya kutakasa na kukamilisha wanadamu. Wote wanaopenda ukweli na kuheshimu ukweli wataweza kuona kwamba maneno ya Mungu ni dhahiri, ikiwa ni maneno ya hukumu na adhabu, au shutuma na laana, yote yanakubaliana kabisa na ukweli halisi. Mungu anaongea kwa njia ambayo ni ya busara sana na halisi, na haijatiwa chumvi kabisa. Kutoka kwa matokeo yaliyotimizwa na maneno haya makali ya Mungu, sote tunaweza kuona kwamba upendo wa kweli wa Mungu kwa wanadamu na nia Zake nzuri za kuwaokoa wanadamu zimefichwa kwayo. Ni wale pekee waliochoshwa na ukweli ndio wanaweza kutunga mawazo, na ni wale pekee ambao huchukia ukweli ndio wanaweza kuhukumu na kushutumu kazi ya Mungu. Mungu amekuwa akifanya kazi nchini China kwa zaidi ya miaka 20 na Yeye tayari ameunda kundi la washindi. Wamepitia ukandamizaji wa kinyama na mateso ya serikali ya CCP, na wote wanaweza kusimama na kushuhudia. Haya yote ni matunda yaliyofanikishwa na maneno ya Mungu. Wote wameona upendo wa Mungu ndani ya maneno Yake, na wameona jinsi ambavyo ameteseka ili kuwaokoa wanadamu. Ingawa baadhi ya maneno Yake ni makali sana wote wanaweza kuyatii, na kutoka kwa hilo wana maarifa ya kweli ya tabia ya Mungu. Wamekuza mioyo ya uchaji na upendo kwa Mungu. Wote wanaweza kutekeleza wajibu wao kwa uaminifu, na kumfuata Mungu tokea mwanzo mpaka mwisho. Hii ndio humwaibisha Shetani zaidi, na hii ni ithibati wa Mungu kumshinda Shetani. Kwa mintarafu ya jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwatakasa watu katika siku za mwisho, hebu tuangalie vifungu vingine katika maneno ya Mwenyezi Mungu, na tutakuwa wazi juu ya hili.

Mwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema, ‘Kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu?’ Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu).

Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu).

Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wapotovu na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kwa kusudi la kumkamilisha mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)).

Baada ya kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kila mtu anapaswa sasa kuwa na hakika kuhusu sababu ya Mungu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, siyo? Je, si sasa sote tunaweza kuona ukweli wa jinsi ambavyo wanadamu ni wapotovu kabisa? Binadamu wanaishi chini ya miliki ya Shetani, wanaishi katika dhambi, na hufurahia dhambi hiyo. Hakuna yeyote katika jumuia ya dini ambaye ameangalia kwa makini kuwasili kwa Mungu na hakuna mtu anayependa ukweli au kuukubali. Bila kujali jinsi ambavyo watu wamemshuhudia Mungu au kueneza neno Lake, kuna wangapi ambao wametafuta kwa dhati au kuchunguza kuonekana na kazi ya Mungu? Na kuna wangapi ambao wanaweza kukubali na kujinyenyekeza kwa hukumu na adhabu ya Mungu? Je, si kila mtu angesema kwamba wanadamu hawa ni upeo kamili wa uovu? Isingekuwa kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho, hawa wanadamu ambao wamepotoshwa sana, waliojawa na tabia ya Shetani, na wanaomkana na kumpinga Mungu, wangeweza kusafishwa na kupokea wokovu wa Mungu? Isingekuwa kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho, ni nani ambaye angeunda kundi la washindi? Unabii wa Bwana Yesu ungetimizwaje? Ufalme wa Kristo ungefanikishwaje? Watu wengi wenye imani katika Bwana wanaamini kwamba Mungu ni Mungu mwenye upendo na mwenye huruma na kwamba bila kujali tunafanya dhambi gani, Mungu atatusamehe. Wao wanaamini kuwa bila kujali jinsi tulivyo wapotovu, hakuna atakayetelekezwa na kwamba Bwana hata hivyo atatunyakua hadi katika ufalme wa mbinguni atakaporudi. Je, huu ni mtazamo wenye mantiki? Je, kuna chochote katika neno la Bwana cha kuunga haya mkono? Mungu ni Mungu mtakatifu na mwenye haki; je, hivyo Angewaruhusu watu ambao wametiwa doa na upotovu, waliojaa tabia ya Shetani, wakataao ukweli, na maadui wa Mungu kuingia katika ufalme Wake? La hasha! Kwa hivyo, Bwana Yesu alitabiri kwamba atarudi, na katika siku za mwisho Ataonyesha ukweli, kufanya kazi Yake ya hukumu na kuwasafisha kabisa na kuwaokoa wananadamu. Bwana Yesu alisema: “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). Kwa mintarafu ya mwanadamu ambaye ametiwa doa kabisa na upotovu, Mwenyezi Mungu hakika atatoa ukweli na kutekeleza hukumu na adhabu Yake kwao. Hii ndiyo njia pekee ya kuamsha mioyo na roho za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kusafisha tabia yake ya shetani. Hata ingawa neno la Mungu la hukumu dhidi ya wanadamu kwa ajili ya uchafu wao, upotovu, uasi, na upinzani dhidi ya Mungu ni mkali, hata hivyo linaonyesha tabia ya Mungu takatifu na ya haki, na pia linaturuhusu tuelewe asili yetu ya shetani na ukweli kwamba sisi ni wapotovu. Kwa njia ya kupitia hukumu ya Mungu na adhabu, sisi sote tumeshindwa na neno la Mungu, tunajinyenyekeza bila kusita kwa hukumu Yake, hatua kwa hatua kuja kuelewa ukweli, na kuona wazi tabia yetu na asili ya shetani, tunaweza kufikia ufahamu wa kweli wa Mungu wa tabia ya Mungu yenye haki, tumekuza moyo wa kumcha Mungu, tumebadili njia yetu ya kuangalia mambo bila kujua, tabia yetu ya maisha imebadilika, na tunaweza kumcha Mungu na kuepuka uovu. Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho hatimaye imefanikisha kuundwa kwa kikundi cha washindi, ambayo ni matokeo ya kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, na ni umuhimu wa kweli wa kazi ya hukumu ya Mungu kuanzia na nyumba Yake. Je, hii inaturuhusu tuone nini? Mungu humhukumu na kumfunua mwanadamu kwa neno Lake sio ili kumwadibu na kumwangamiza mwanadamu, lakini kumsafisha, kumbadilisha, na kumwokoa mwanadamu kabisa. Lakini kwa wale watu ambao hukataa kukubali hukumu na utakaso wa neno la Mwenyezi Mungu, maafa makubwa yatakapotokea, watashuka katika maafa na kuadhibiwa.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: Hukumu ni nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp