Je, Wokovu Kupitia Imani Kunaruhusu Kuingia katika Ufalme wa Mungu?

23/04/2023

Ugonjwa wa mlipuko unaenea bila kusita, na matetemeko ya ardhi, mafuriko, wadudu wanaopaa, njaa zimeanza kutokea. Watu wengi wako katika hali ya wasiwasi usioisha, na waumini wanangojea kwa hamu kuja kwa Bwana juu ya wingu ili kuchukuliwa juu angani, ili kuepuka mateso kupitia majanga na kuepuka kifo. Hawajui kwa nini bado hawajachukuliwa kwenda juu kumlaki Bwana, na kutazama angani siku nzima bila kuona chochote. Watu wengi wamehuzunika sana, hasa wanapoona maisha ya makasisi wengi yakichukuliwa na janga. Wanajisikia wenye wasiwasi, kwamba wametupwa kando na Bwana na kuanguka katika majanga, na kunusurika kwao hakuna uhakika. Wanahisi kuchanganyikiwa na kupotea. Ufunuo kilitabiri kwamba Bwana Yesu angekuja kabla ya majanga na kutuchukua hadi angani ili kutuzuia tusikubali kushindwa nayo. Hilo ndilo tumaini letu. Imani yetu ni kuepuka maafa na kupata uzima wa milele. Lakini majanga yameanza kushuka, hivyo kwa nini Bwana hakuja juu ya wingu kupokea waumini? Kupitia imani yetu, dhambi zetu zinasamehewa, tunapewa wokovu, na kupewa haki. Kwa nini hatujachukuliwa juu katika ufalme wa mbinguni? Tumemngoja Bwana kwa uchungu na kuteseka miaka mingi. Kwa nini Hajatukujia, akatuchukua ili tukutane na Yeye na kuepuka taabu ya majanga? Je, kweli ametutupa kando? Haya ni maswali ambayo waumini wengi wanayo. Hivyo, je, wokovu kupitia imani kweli unatuingiza katika ufalme? Nitashiriki kidogo kuhusu ufahamu wangu binafsi wa jambo hili.

Lakini kabla ya kufanya ushirika kuhusu hili, kwanza hebu tufafanue jambo moja. Je, wazo la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani, la kuingia katika ufalme kwa njia hiyo linaungwa mkono hata kidogo na neno la Mungu? Je, Bwana Yesu aliwahi kusema kwamba kuhesabiwa haki kwa njia ya imani na neema ya wokovu ndivyo tu tunavyohitaji ili kuingia katika ufalme Wake? Hakuwahi kufanya hivyo. Je, Roho Mtakatifu aliwahi kushuhudia jambo hili? Hapana. Kwa hivyo tunaweza kuwa na hakika kwamba wazo hili ni wazo la kibinadamu tu, na hatuwezi kutegemea hilo kutuingiza katika ufalme. Kwa hakika, Bwana Yesu alikuwa wazi sana kuhusu ni nani angeweza kuingia katika ufalme. Bwana Yesu alisema, “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni. Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:21-23). “Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8:34-35). “Kkwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). “Fuata amani na watu wote, na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana(Waebrania 12:14). Bwana Yesu alituambia wazi kwamba wale tu wanaofanya mapenzi ya Mungu ndio wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni, kwamba wale tu wanaoepuka dhambi na kutakaswa ndio watakaopata nafasi katika ufalme. Hilo pekee ndilo kiwango cha kuingia. Je, kukombolewa na dhambi na kuhesabiwa haki kupitia imani kunamaanisha mtu anafanya mapenzi ya Mungu? Je, ina maana hawatendi tena dhambi, au kumwasi na kumpinga Mungu? Bila shaka hapana. Waumini wote katika Bwana wanaweza kuona ukweli kwamba ingawa tumekombolewa na kuhesabiwa haki kupitia imani, tunatenda dhambi daima, tunaishi katika mzunguko wa kutenda dhambi mchana na kuungama usiku. Tunaishi na uchungu wa kutoweza kuepuka dhambi—hatuwezi kujizuia. Kuna watu ndani ya madhehebu yote ambao wana wivu, na wagomvi, wanaopigania jina na faida, wakisengenyana wao kwa wao. Hili ni jambo la kawaida sana. Na imani ya watu wengi ni kwa sababu wana tamaa ya kupata neema ya Mungu, lakini hawafanyi kama asemavyo. Wanakimbilia kanisani wanapokabiliwa na matatizo, lakini wakati wa amani wanafuata mienendo ya kilimwengu. Na makanisa yanaandaa sherehe moja baada ya nyingine. Hakuna mtu anayeshiriki kuhusu ukweli au kushiriki ushuhuda wa kibinafsi, lakini kushindana tu kuhusu ni nani anayepokea neema zaidi, baraka kuu zaidi. Majanga makubwa yakiwa yanakuja na kumwona Bwana bado haji juu ya wingu kuwanyakua, imani na upendo wa watu wengi unashuka, na wameanza kumlaumu na kumhukumu Mungu. Wengine hata wamemkana na kumsaliti. Ukweli unatuonyesha kwamba kusamehewa dhambi na neema ya wokovu kunaweza kumaanisha kwamba watu wamekuwa na tabia bora, lakini hakumaanishi kwamba wameepuka dhambi kabisa, kwamba hawamwasi Mungu, na hasa si kwamba wamefikia utakatifu na kustahili kuingia katika ufalme. Hayo ni matamanio tu. Kwa hiyo sasa tunaweza kuona ukweli huu na kuelewa kwa nini Bwana Yesu alisema wale waliohubiri na kutoa pepo kwa jina Lake ni watenda maovu, na Hakuwajua kamwe. Ni kwa sababu watu bado wanatenda dhambi daima, ingawa dhambi zao zimesamehewa, na wanamlaumu na kumhukumu Bwana. Wamejaa malalamiko wanapoona Bwana bado hajaja, na wameanza kumkana na kumsaliti. Wengine hata wanasema watamgombeza Bwana kama hatawanyakua na kuwaingiza katika ufalme. Watu hawa si bora kuliko Mafarisayo waliomdhulumu na kumhukumu Bwana Yesu, au labda hata mbaya zaidi. Watu wengine wanaweza kuona jinsi wanavyotenda kwa uwazi sana, na machoni pa Mungu, bila shaka wao ni watenda maovu. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, kwa hivyo, je, Mungu anaweza kuwaruhusu wale ambao daima wanatenda dhambi, kuhukumu na kumpinga Mungu, waingie mbinguni? La hasha. Na kwa hivyo, imani ya watu kwamba kuhesabiwa haki kwa imani kutawaingiza katika ufalme ni mawazo yanayoenda kinyume na maneno ya Bwana mwenyewe, na kinyume na ukweli. Ni fikira na mawazo ya binadamu tu yanayotokana na matamanio yetu ya kupita kiasi.

Katika hatua hii, wengine wanaweza kutaja kwamba kuokolewa kwa njia ya imani kwa neema kuna msingi wa kibiblia: “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” (Warumi 10:10). “Kwani kwa neema mmeokolewa kupitia kwa imani; sio kwa nguvu zenu wenyewe: ni kipawa kutoka kwa Mungu” (Waefeso 2:8). Kwa hivyo ikiwa hatuwezi kuingia katika ufalme kwa njia hiyo, “kuokolewa” kunamaanisha nini hasa? Mwenyezi Mungu anatuambia kuhusu fumbo hili la ukweli. Hebu tuangalie kile ambacho maneno Yake yanasema. Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)). “Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. … Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Tunaweza kuona kutokana na hili kwamba Bwana Yesu alisulubishwa kama sadaka ya dhambi ya wanadamu, Akitukomboa kutoka dhambini. Tunachotakiwa kufanya ni kuungama na kutubu kwa Bwana ili dhambi zetu zisamehewe. Hatuhukumiwi tena na kuuawa chini ya sheria. Bwana hatuoni tena kuwa wenye dhambi na Shetani hawezi tena kutushtaki. Tumeruhusiwa kuja mbele za Bwana kwa maombi na kufurahia amani na furaha anayotupa, pamoja na neema na baraka zake nyingi. Hii ndiyo maana ya "kuokolewa" hapa. Kuokolewa kwa imani kunamaanisha tu kusamehewa dhambi, na sio kuhukumiwa chini ya sheria. Sio kama watu wanavyofikiria, kwamba mara baada ya kuokolewa, wao huokolewa kila wakati na watastahili kuingia katika ufalme. Kutajwa kwa Biblia kuhusu "kuokolewa" ni jinsi Paulo alivyoeleza, lakini si Bwana Yesu wala Roho Mtakatifu aliyewahi kusema hivyo. Hatuwezi kutumia kauli za wanadamu zilizorekodiwa katika Biblia kama msingi wetu, tu maneno ya Bwana Yesu. Wengine wanaweza kuuliza kwamba kwa kuwa Bwana ametusamehe dhambi zetu, Mungu hatuoni tena kama wa dhambi na ametuita wenye haki, kwa hivyo kwa nini hatuwezi kuchukuliwa juu katika ufalme? Ni kweli kwamba Mungu alituita wenye haki, lakini hakusema kwamba kusamehewa dhambi zetu kulitufanya tustahili ufalme, au kwamba kwa kuwa tumesamehewa, bado tunaweza kutenda dhambi ya aina yoyote na bado kuwa watakatifu. Ni lazima tuelewe kwamba tabia ya Mungu ni takatifu na ya haki, na hatawahi kumwita mtu mtakatifu ambaye anatenda dhambi kila mara, au kumwita mtu asiye na dhambi ambaye bado ni mwenye dhambi. Hata mwamini ambaye dhambi zake zimesamehewa anaweza kulaaniwa ikiwa atampinga na kumkufuru Mungu. Kama vile Biblia inavyosema, “Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi(Waebrania 10:26). Mafarisayo walilaaniwa na Bwana Yesu kwa kuhukumu, kulaani, na kumpinga. Je, huo si ukweli? Waumini wote wanajua kwamba tabia ya Mungu haitavumilia kosa lolote, na Bwana Yesu alisema, “Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja(Mathayo 12:31-32). Msamaha wa dhambi kwa kweli ni neema ya Mungu, lakini ikiwa watu wataendelea kuudhi tabia ya Mungu baada ya kusamehewa, bado wanaweza kulaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Ikiwa tutamsulubisha Mungu tena, matokeo yatakuwa mabaya. Lakini Mungu ni upendo na rehema, kwa hiyo anataka kutuokoa kutoka kwa dhambi na uovu, ili tuwe watakatifu. Ndiyo maana Bwana Yesu aliahidi Atakuja tena baada ya kazi Yake ya ukombozi. Kwa nini angerudi? Ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu kutoka dhambini na kutoka kwa nguvu za Shetani, ili tuweze kumgeukia Mungu na kupatwa na Yeye. Ni mwumini anayekaribisha kurudi kwa Bwana pekee ndiye aliye na tumaini lolote la kuingia katika ufalme wa mbinguni. Katika hatua hii, baadhi ya watu wanaweza kushangaa, kwa kuwa dhambi zetu zimesamehewa, tunawezaje kuepuka dhambi kweli na kuwa watakatifu, na kupata kuingia katika ufalme? Hilo linatuleta kwenye jambo kuu. Kukubali tu msamaha wa Bwana Yesu hakutoshi. Pia tunapaswa kukaribisha ujio wa Bwana na kukubali hatua Yake inayofuata ya kazi ili kuepuka dhambi, kuokolewa kikamilifu na Mungu, na hivyo kustahili ufalme. Kama Bwana Yesu alivyotabiri, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana. … Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:22, 27). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Tukitafakari hili kwa makini, tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu anarudi katika siku za mwisho kama Mwana wa Adamu, akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu, Akituongoza kuingia katika ukweli wote, ili tuweze kuwekwa huru kabisa kutoka dhambini, kuwa huru kutoka katika nguvu za Shetani, na kupata wokovu kamili. Kwa hivyo kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa siku za mwisho, na kutakaswa kwa upotovu wetu ndiyo njia yetu pekee ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hebu tuangalie vifungu kadhaa zaidi vya maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Je, maneno ya Mwenyezi Mungu hayaweki kila kitu kiwe dhahiri zaidi? Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, ambayo ilikuwa ni kusamehe dhambi za mwanadamu na kutukomboa kutoka kwazo—hiyo ni kweli. Lakini asili ya dhambi ya watu haijatatuliwa na tunaendelea kumpinga Mungu, kwa hivyo hiyo haihesabiki kama kuokolewa kikamilifu. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho, Akionyesha ukweli mwingi sana, na kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu juu ya msingi wa ukombozi wa Bwana Yesu. Amekuja kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kabisa, kutupeleka katika ufalme wa Mungu. Kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho ndiyo kazi Yake muhimu zaidi, ya msingi zaidi kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu, na ndiyo njia pekee ya sisi kutakaswa na kuokolewa kikamilifu. Hii ni fursa nzuri na nafasi yetu pekee ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tunaweza kusema kwamba kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu inayoanza na nyumba ya Mungu ni kazi ya kuwanyakua waumini. Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, upotovu wetu unaweza kutakaswa, na kisha tutalindwa katika majanga makubwa na kuingia katika ufalme wa Mungu. Huku hasa ndiko kunyakuliwa. Ikiwa hatutaenda sambamba na kazi hii, haijalishi imani yetu imekuwa ya muda gani, tumeteseka au kulipa gharama kiasi gani, yote yatakuwa bure. Huko ni kukata tamaa, na juhudi zetu zote za hapo awali zitakuwa bure. Tungeishia tu kutumbukia katika maafa, kulia na kusaga meno. Mungu hatawahi kumchukua mtu ambaye bado anaweza kumwasi katika ufalme Wake. Hilo linaamuliwa na tabia Yake ya haki.

Wengine wanaweza kuuliza jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu hufanya kazi hii ya hukumu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Hebu tuone kile Anachosema kuhusu hilo. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno katika siku za mwisho, Akituambia ukweli wote tunaohitaji kwa ajili ya utakaso wa upotovu wetu na wokovu wetu. Anahukumu na kufunua asili yetu ya dhambi, inayompinga Mungu ya kishetani na vipengele vyote vya tabia zetu potovu, na Anafichua nia na mawazo yetu yote ya ndani kabisa yaliyofichika na ya kudharauliwa. Kadiri tunavyosoma maneno ya Mungu, ndivyo tunavyopitia hukumu hiyo, na tunaweza kuona jinsi ambavyo Shetani ametupotosha kwa undani sana, jinsi tulivyo wenye kiburi na upinzani. Sisi ni wajanja, wabinafsi, na wenye pupa sana, na tunaishi kwa kufuata falsafa na sheria za kishetani katika kila kitu, daima tukilinda maslahi yetu wenyewe. Hata imani na kazi yetu kwa kanisa ni kwa ajili ya kutuzwa na kuingia katika ufalme. Hatuna dhamiri wala mantiki, bali tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa Shetani kabisa. Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, hatimaye tunaweza kuona haki Yake ambayo haivumilii kosa. Kwa kweli Mungu huona ndani ya mioyo na akili zetu, na hata tusiposema, Mungu ataweka hadharani kile tunachokiwaza, upotovu ulio ndani kabisa ya mioyo yetu. Bila mahali pa kujificha, tunaona aibu sana, na tunazidi kumcha Mungu. Tunaweza kuomba kuhusu yale yaliyo mioyoni mwetu, na kuzungumza kwa uaminifu kuhusu fikira na mawazo yetu potovu, tukipata dhamiri na mantiki. Tukisema uwongo, tutafichua mara moja, na kurekebisha. Tukipitia maneno ya Mungu kwa njia hii, tabia zetu potovu zinatakaswa na kubadilishwa hatua kwa hatua, na tunaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Kupitia hukumu na utakaso wa Mwenyezi Mungu, tunaweza kuhisi kwa kina jinsi kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu ilivyo ya vitendo! Bila hili, hatungeweza kamwe kuona upotovu wetu halisi, na hatungeweza kamwe kutubu au kubadilika kweli. Tunaweza kuona kwamba kuepuka maovu hakuwezi kufanywa kwa bidii yetu wenyewe na kujidhibiti, lakini ni muhimu kwamba tuhukumiwe, tuadibiwe, na kujaribiwa na Mungu. Tunapaswa pia kupogolewa, kushughulikiwa, na kuadhibiwa. Hiyo ndiyo njia pekee ya tabia zetu za maisha kubadilika kweli na sisi kumtii na kumcha Mungu kwa dhati. Kwa hivyo ikiwa tuna ukombozi wa Bwana Yesu katika imani yetu tu, dhambi zetu zinasamehewa na tunahesabiwa haki kwa imani, lakini hatustahili ufalme. Bado tunapaswa kukaribisha kurudi kwa Bwana na kukubali hukumu ya Mwenyezi Mungu ili tuweze kutupilia mbali upotovu na kutatua kabisa asili yetu ya dhambi. Na kwa hivyo, Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, akifanya kazi ya hukumu. Yeye ndiye Mwokozi aliyeshuka chini kufanya kazi binafsi ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Waumini wengi kutoka madhehebu yote husikia sauti ya Mungu na wanamkubali Mwenyezi Mungu. Wao ni mabikira wenye busara na wanahudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Lakini wale wanaomkataa Mwenyezi Mungu wanakuwa wanawali wapumbavu ambao wataanguka katika majanga, wakilia. Sasa tunapaswa kuona kwa nini ulimwengu wa kidini haujamwona Bwana Yesu akishuka juu ya wingu. Wanashikilia kwa ukaidi Maandiko halisi, wakiwa na hakika kwamba Bwana anakuja juu ya wingu ili kuwanyakua, kulingana na mawazo yao wenyewe. Lakini kwa kweli, Bwana tayari amekuja sirini kufanya kazi. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi sana ambao wanakataa kuutafuta. Wanasikia lakini hawasikilizi, na wanaona lakini hawaelewi. Wanapinga bila kufikiri na kumhukumu Mwenyezi Mungu. Wanaendelea kutazama anga, wakingojea Mwokozi Yesu ashuke juu ya wingu. Hii itawaleta kwenye majanga. Nani wa kulaumiwa?

Leo, Mwenyezi Mungu amekamilisha kundi la washindi kupitia kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Maafa yameanza, na watu wateule wa wa Mungu wanajitosa katika kueneza injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu, wakitoa ushuhuda wa kuonekana na kazi ya Mungu. Watu zaidi na zaidi wanachunguza na kukubali njia ya kweli, na Kanisa la Mwenyezi Mungu linaanzishwa katika nchi nyingi zaidi. Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaenezwa na kushuhudiwa kote ulimwenguni. Wale ambao wana kiu ya ukweli na kutafuta kuonekana kwa Mungu wanakuja mbele ya kiti Chake cha enzi, mmoja baada ya mwingine. Hili haliwezi kusimamishwa! Linatimiza unabii huu wa kibiblia: “Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake(Isaia 2:2). Lakini zile nguvu za wapinga Kristo katika ulimwengu wa kidini wanaompinga Mwenyezi Mungu, na wale wanaojiita waumini ambao wamepotoshwa na kudhibitiwa na wao tayari wameanguka katika majanga, wakipoteza nafasi yao ya kunyakuliwa. Wanalia na kusaga meno. Kweli ni janga. Hebu tutazame video ya usomaji wa maneno ya Mungu katika kutamatisha leo. Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp