Unashuhudia kuwa katika siku za mwisho Mungu huonyesha ukweli na kufanya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu, hivyo ni kwa jinsi gani hasa Mungu humhukumu, kumtakasa na kumwokoa mwanadamu?

08/06/2019

Jibu:

Kila mtu ambaye sasa anatafuta na kuchunguza njia ya kweli anataka kuelewa jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Mwenyezi Mungu ameonyesha maneno mengi kuhusu suala hili la ukweli. Hebu tusome vifungu vichache vya neno la Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa tabia potovu ya mwanadamu na kiini cha asili ya mwanadamu; na uondoaji wa fikira za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo).

Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua ‘siri’ katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa).

Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu tunaona kwamba wakati wa kuhukumu binadamu waliopotoka katika siku za mwisho, Mungu hutumia vipengele vingi vya ukweli na tabia ya haki ambayo Anaonyesha ili kuhukumu, kufichua, na kushutumu asili ya kishetani ya mwanadamu, kutakasa na kubadilisha tabia ya kishetani ya mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Katika hukumu adhimu na yenye ghadhabu na kuadibu kwa Mungu, tunahisi kama kwamba tuko uso kwa uso na Yeye; tunapata kuona waziwazi asili muhimu na ukweli halisi wa kupotoshwa kwetu na Shetani na tunaelewa kwa kweli asili takatifu ya Mungu na tabia Yake ya haki ambayo haiwezi kukosewa. Moyo wa kumcha Mungu unazaliwa ndani yetu na tunakuza ufahamu halisi wa Mungu huku pia tukielewa ukweli mwingi wakati huo huo. Hili linaruhusu tabia yetu ya maisha ibadilishwe, hivyo hatimaye tunaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano halisi wa binadamu wa yule ambaye ni mwaminifu na anamtii Mungu. Maneno yote yanayoonyeshwa na Mungu yanawafunulia wanadamu vipengele vingi vya ukweli: tabia ya Mungu ya haki, kile Alicho na anacho, siri za mpango Wake wa usimamizi, habari za ndani za hatua tatu za kazi ya Mungu, malengo na mapenzi ya Mungu katika wokovu Wake wa wanadamu, chanzo cha dhambi na ukweli wa upotovu wa binadamu, hatima na matokeo ya watu, na kadhalika. Ukweli huu ni maneno ambayo hutupa uzima na njia ya uzima wa milele. Tunaposoma maneno ya Mwenyezi Mungu, tunayasikia kama upanga ukatao kuwili, huku uadhama na ghadhabu ya Mungu vikitoka katika kila neno na kila mstari. Vinaonyesha mawazo kuhusu Mungu ambayo tunashikilia katika vina vya mioyo yetu, malengo yetu yenye kustahili kudharauliwa na nia mbaya katika imani yetu, na hata sumu za Shetani zilizofichwa katika asili yetu bila ya sisi kujua zinafichuliwa, ili tuweze kuona tumepotoshwa kabisa na Shetani. Tunaishi kwa kutegemea sumu, falsafa, mantiki na sheria za Shetani kwa kila namna. Mioyo yetu imejaa uovu, majivuno, tamaa, udanganyifu, na tabia nyingine za shetani. Tunaishi kwa kudhihirisha ushetani tu; tumekuwa uzao wa Shetani, kizazi cha joka kubwa jekundu, ambao wanaasi na kumpinga Mungu. Baada ya kusoma maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo, tunamheshimu sana Mungu, tukihisi uchunguzi Wake wa mioyo yetu ya ndani zaidi. Maneno ya Mungu yanaipiga asili yetu ya kishetani katika kila kipengele kana kwamba tuko uso kwa uso na Yeye, wakati mwingine akitukumbusha au kutuonya, wakati mwingine akitukaripia, kutushughulikia, na kutufundisha nidhamu. Wakati mwingine maneno makali ya Mungu hujaa hasira, na kwayo tunaona ukweli wa upotovu wetu, yakitufanya tuhisi kwamba hatuna pahali pa kujificha na tunaaibika kabisa. Wakati uo huo, tunahisi kwa kina kwamba maneno ya Mungu hakika ni ukweli, yaliyojaa nguvu na mamlaka, na kwamba ni ufunuo wa tabia ya Mungu na nafsi Yake ya maisha. Kiini kitakatifu cha Mungu hakiwezi kunajisiwa na tabia Yake ya haki haiwezi kukosewa. Hatuwezi kufanya lolote bali kusujudu mbele ya Mungu na kutubu Kwake. Tunachukia asili zetu wenyewe za kishetani, tumejawa na majuto na tuko tayari kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Tunashawishika kabisa na kuamua ndani ya mioyo yetu kuishi maisha mapya ili kumridhisha Mungu. Haya ndiyo matokeo ya hukumu ya neno la Mungu juu ya watu waliochaguliwa na Mungu. Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kama huko, wale ambao kweli wanaamini katika Mungu na kupenda ukweli wanaweza kupata ukweli na kukamilishwa na Mungu. Wale ambao hawaupendi ukweli na kweli hawapitii hukumu na kuadibu kwa Mungu hawana budi kuondolewa na Mungu.

Huku Mungu anapohukumu na kuwafichua watu kupitia kwa maneno Yake, pia Yeye huandaa mazingira na matukio mbalimbali ya kuwashughulikia na kuwapogoa watu, kuwajaribu, na kuwafichua. Baada ya kupitia ukweli wa hukumu, kuadibu, kurudi na nidhamu vinavyotujia, tunatambua kwamba asili yetu ya kishetani na tabia ya kishetani ni isiyobadilika kabisa. Tunapokuwa tukijitumia, kuteseka na kulipa gharama kwa ajili ya Mungu, bado tunaweza kumuasi na kumpinga Yeye bila kujua. Chini ya hukumu Yake ya haki, adhimu na yenye ghadhabu, tunaona wazi sura yetu mbaya ya kishetani inayompinga Mungu. Tunaona kwamba sisi ni watoto wa kuzimu na kwamba hatufai kuishi mbele ya Mungu. Mioyo yetu inauma kwa uchungu. Tunatetemeka kwa hofu na kuonyesha majuto. Tunajitelekeza na kujilaani. Tunapotubu kwa kweli mbele ya Mungu, Yeye hutupa huruma na uvumilivu; Yeye hutuangazia, hutupa nuru, hutufariji, na kutusaidia ili tuweze kuelewa nia njema za wokovu wa Mungu kwa ajili yetu na tupate kujua kupendeza Kwake. Tunakuwa tayari kuishi kulingana na ukweli wa neno la Mungu ili kumfariji na kumridhisha Yeye. Hukumu na kuadibu kwa Mungu hutufanya tuone wazi ni nani Anaowapenda, ni nani Anaowaokoa, ni nani Anaowakamilisha, ni nani Anaowabariki, ni nani Anaowachukia, ni nani Anaowaondosha na ni nani Anaowaadhibu na kuwalaani, na hivyo kuelewa kwa kweli tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, tunaelewa kweli kwamba ukweli ulioonyeshwa na Mungu ni hukumu ya wanadamu waliopotoshwa; ni kuadibu, uchunguzi, na utakaso. Mungu lazima afichue tabia Yake ya haki, adhimu, yenye ghadhabu na tabia isiyoweza kukosolewa kwa asili ya wanadamu ya kishetani inayompinga Mungu. Ni hivi tu ndivyo tunavyoweza kukuza moyo wa kumcha Mungu, kufutilia ukweli, kumpenda Mungu na kumtii na kumwabudu Yeye, tukiishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu halisi ili kumtukuza na kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Haya ndiyo matokeo ya hukumu na kuadibu kwa Mungu. Sasa sote tunapaswa kuelewa kwamba kwa wanadamu waliopotoshwa kabisa, Mungu lazima awe mwili ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ili Awasafishe na kuwaokoa wanadamu. Vinginevyo, wanadamu waliopotoshwa hawataokolewa. Tukiachia tu kwa Enzi ya Neema katika imani yetu na tukatae kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, hatuna budi ila kuondolewa na kuangamizwa. Hili ni bila shaka.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp