Swali la 25: Unashuhudia kuwa Bwana Yesu amekwisha kurudi kama Mwenyezi Mungu, kwamba Yeye huonyesha ukweli wote ambao utawawezesha watu kupata utakaso na kuokolewa, na kwamba sasa Anafanya kazi ya hukumu kuanzia na nyumba ya Mungu, lakini hatuthubutu kukubali hili. Hii ni kwa sababu wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa mara nyingi hutufundisha kwamba maneno na kazi zote za Mungu zimeandikwa katika Biblia na hakuwezi kuwa na maneno mengine au kazi ya Mungu nje ya Biblia, na kwamba kila kitu kinachoipinga au kwenda zaidi ya Biblia ni uasi. Hatuwezi kulitambua tatizo hili, kwa hivyo tafadhali unaweza kutueleza kulihusu.

Jibu:

Aina hii ya mtazamo kutoka kwa jamii ya dini haitokani na neno la Mungu; ilikuja hasa kama matokeo ya kufasiriwa vibaya kwa Biblia. Biblia inashuhudia hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu; hii ni kweli. Hata hivyo, kiandikwacho katika Biblia kina mipaka, na ndani yake hamna maneno yote aliyoyanena Mungu katika hizo hatua mbili za kazi Yake na ushuhuda wote kuhusu kazi hiyo. Kutokana na kuachwa maneno na migogoro miongoni mwa wakusanyaji wa Biblia, baadhi ya utabiri wa manabii, uzoefu wa mitume na ushuhuda wao uliachwa nje; huu ni ukweli unaotambuliwa. Basi, inawezaje kusemwa kwamba mbali na Biblia, hakuna kumbukumbu au ushuhuda zingine kuhusu kazi ya Mungu? Je, unabii na nyaraka hizo zote ambazo hazipatikani zilichanganywa na mapenzi ya binadamu? Bwana Yesu hakuyasema tu maneno yaandikwayo katika Agano Jipya; baadhi ya matamshi na kazi Yake hayakuandikwa humo. Kwa hiyo, je, hii inamaanisha kwamba hayapaswi kuandikwa katika Biblia? Biblia haikuandikwa chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, bali pamoja na watu wengi katika huduma Yake. Bila shaka, mizozo na makosa yangetokea, au matatizo mengine yangezuka. Aidha, watu wa kisasa wana ufasiri na mitazamo mbalimbali ya Biblia. Watu lazima wauheshimu ukweli, hata hivyo, kwa hiyo haiwezi kusemwa kwamba matamshi na kazi ya Mungu hayapo nje ya Biblia; hii haitapatana na ukweli. Mwanzoni, Biblia ilikuwa tu na Agano la Kale. Hakuna alilolisema Bwana alipokuwa Akitenda kazi Yake ya ukombozi linaloweza kupatikana katika Agano la Kale; hivyo, je, kazi ya Bwana Yesu ya maonyesho na ukombozi vilikuwa ndani au nje ya Biblia ya wakati huo? Watu hawafahamu ukweli halisi, na hawajui kabisa kwamba kila wakati Mungu alipoitimiza hatua ya kazi Yake, ndio wakati tu ule ukweli ungetokea na kuandikwa katika Biblia. Kudai kwamba hakuna kumbukumbu nje ya Biblia kuhusu matamshi na kazi ya Mungu kwa kiasi fulani ni dhahania na upuuzi! Yote mawili, Agano la Kale na Agano Jipya kila moja lilitolewa baada ya Mungu kuimaliza hatua ya kazi Yake, lakini baada ya kutokea kwa Biblia, hakuna ajuaye nini kingine Mungu atakitenda au kukisema; huu ni ukweli. Wanadamu hasa hawastahili kuiwekea Biblia mipaka jinsi hii, au kumwekea Mungu mipaka kwa msingi wa kiandikwacho ndani yake. Kuhusu jambo hili, sote tumeona dhahiri jinsi wanadamu wamekuwa kwa kweli wenye kiburi, na kwa hiyo wapumbavu, na wapotovu; wanapokabiliwa na ukweli, hata wanathubutu kutoa maamuzi bila kujali. Je, huku si kulirudia kosa lililofanywa na makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo walipoitumia Biblia kumpinga Mungu? Hivyo, hatuwezi kumwamini Mungu, kumfuata Yeye, au kushika na kujifunza njia ya kweli kabisa kwa kuitegemea Biblia, kwa kuwa inaweza tu kutumiwa kama rejeo. Muhimu zaidi, lazima azimio letu litegemee kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu na kama kuna ukweli au la; hapo tu ndipo msingi huu utakapokuwa halisi; hapo tu ndipo tunaweza kufanya uteuzi sahihi. Kwa hiyo, madai kama “Chochote kipingacho au kipitacho Biblia ni uzushi na uongo,” hakika hayafai. Katika Enzi ya Neema, makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo walimshutumu Bwana Yesu kwa mujibu wa Biblia na walimsulubisha Yeye–tendo ambalo liliichukiza tabia ya Mungu na liliwafanya waadhibiwe na kulaaniwa. Yote haya yalikuwa matokeo ya kuamini bila kufikiri, kuiabudu Biblia, na kumkataa Kristo. Ninaweza kuuliza, je, kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu ilipatana na Biblia au la? Miaka elfu mbili baada ya Bwana Yesu kumaliza kazi Yake ya ukombozi, Mwenyezi Mungu Amekuja kutenda kazi ya kuhukumu katika siku za mwisho; je, hii inapatana na yaliyomo ya Agano Jipya? Jamii za dini zinaitumia Biblia daima kuiwekea mipaka kazi ya Mungu; huu ni upumbavu na upuuzi sana! Kijuujuu, zinaonekana kuiheshimu Biblia, lakini yote zinazoyatenda kwa kweli ni kujaribu kutetea hadhi na utawala wao. Hazitafuti ukweli kwa dhati; njia zinazofuata hakika ni ile ya mpinga Kristo. Kutokana na hili, ni wazi kwamba kuitumia Biblia kama msingi wa kuihukumu njia ya kweli na kuitafiti kazi ya Mungu ni makosa; njia ya pekee ya kuwa sahihi ni kulifanya azimio letu litegemee kile kilicho njia ya kweli na kile kisicho, au kazi ya Mungu, kuhusu kama kazi ya Roho Mtakatifu na ukweli upo au la. Hivyo, ni makosa kusema kwamba mbali na Biblia hakuna matamshi au kazi nyingine ya Mungu; madai kama hayo kwa kweli ni uongo.

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Katika dini, kwa sababu ya kuhubiri kwa wachungaji na wazee wa kanisa, wale wote wanaoamini katika Bwana wanafikiri kuwa neno nzima na kazi ya Mungu imewekwa katika Biblia. Wokovu wa Mungu katika Biblia umekamilika, na hakuna neno na kazi ya Mungu iliyo nje ya Biblia. Imani katika Bwana inapaswa kuwa na msingi katika Biblia na kushikilia Biblia. Mradi tu tusiache Biblia, wakati Bwana Atakuja tutachukuliwa juu katika ufalme wa mbinguni. Wazo kama hilo linaweza kupatana na dhana na fikira za watu, lakini linalingana na maneno ya Bwana Yesu? Je, mnaweza kuhakiki kuwa linapatana na ukweli? Bwana Yesu hajawahi sema kuwa neno la Mungu na kazi yote imerekodiwa katika Biblia, kuwa hakuna neno na kazi ya Mungu nje ya Biblia. Huu ni ukweli. Watu wanaoelewa Biblia wote wanajua kuwa Biblia iliwekwa pamoja na mwanadamu miaka mingi baada ya kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu ilikuja kwanza, na kisha Biblia. Kwa maneno mengine, kila wakati Mungu alikamilisha hatua ya kazi Yake, wale waliopitia kazi ya Bwana wangerekodi chini neno la Mungu na kazi kutoka wakati huo, na rekodi hizi zilikusanywa na watu kuwa Biblia. Tunapofikiria kuihusu, ni vipi kazi ambayo Mungu hajafanya ingewezaje kukusanywa kuwa Biblia awali? Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, hasa, haiwezekani kuwa imerekodiwa katika Biblia. Agano Jipya na Agano la Kale yamekuwa sehemu ya Biblia kwa miaka inayokaribia 2000. Mwenyezi Mungu Ameanza tu kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Kwa hiyo, neno na kazi ya Mungu katika siku za mwisho haiwezekani kuwa ilirekodiwa katika Biblia maelfu ya miaka iliyopita. Je, si Hiyo ni kweli? Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu Amefanya kazi ya hukumu kuanza na nyumba ya Mungu, Akionyesha mamilioni ya maneno mengi. Maneno haya yote ni ukweli unaotakasa na kuokoa mwanadamu, na ni njia ya uzima wa milele iliyoletwa na Kristo wa siku za mwisho. Tayari yamekusanywa kuwa Biblia ya Enzi ya Ufalme. Hiki ni kitabu, “Neno Laonekana katika Mwili.” Ingawa ukweli unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu haukurekodiwa katika Biblia awali, umetimizwa kikamilifu unabii wa Bwana Yesu, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13). “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7). Ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu umethibitisha kikamilifu kuwa Mwenyezi Mungu ni mfano halisi wa Roho wa kweli. Yeye ni Mungu mwenye mwili. Maneno yote yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, hiyo ni, maonyesho ya Roho wa ukweli katika siku za mwisho, ni maneno kutoka kwa Roho Mtakatifu kwa kanisa. Je, tunathubutu kusema haya sio maneno ya Mungu? Bado tunathubutu kukana haya? Ikiwa tutaona ukweli wa mazungumzo na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, bado tungeweza kusema maneno yote ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia na kuwa hakuna neno na kazi ya Mungu nje ya Biblia? Hatuelewi habari ya ndani ya jinsi Biblia iliundwa. Hatujui ukweli kuwa Biblia iliundwa tu baada ya Mungu kukamilisha kila hatua ya kazi Yake, na bado tunahitimisha kiholela na kuamua kuwa hakuna neno na kazi ya Mungu nje ya Biblia. Je, si sisi ni wadhalimu na wapumbavu?

Ikiwa hatuelewi jinsi Biblia iliundwa na habari yake ya ndani, inaweza kuwa rahisi sana kupotoka kwenye njia kuamini kwa Mungu. Wakati wa hatua mbili za kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, maneno yote yaliyoonyeshwa na Mungu hayakurekodiwa kikamilifu katika Biblia. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, kulikuwa na manabii wachache ambao unabii wao haukurekodiwa katika Biblia. Huu ni ukweli pengine ndugu wachache wanafahamu kuuhusu. Kisha katika Enzi ya Neema, kulikuwa hata na maneno zaidi yaliyozungumzwa na Bwana Yesu. Lakini maneno yaliyorekodiwa katika Biblia ni finyu sana. Hebu fikiria. Bwana Yesu Alihubiri duniani kwa miaka tatu na nusu. Ni maneno mangapi Angezungumza kila siku? Kulikuwa na ibada na maneno mengi sana yaliyozungumzwa na Bwana Yesu kwa hiyo miaka mitatu na nusu. Hakuna namna yoyote mtu yeyote angeweza kuhesabu. Kama vile Mtume Yohana alisema: “Na pia kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya, ambayo, yote yakiandikwa, ninafikiri kwamba hata dunia yenyewe haingetosha vitabu hivyo ambavyo vitaandikwa” (Yohana 21:25). Hebu sasa tuangalie Injili Nne za Agano Jipya. Maneno ya Bwana Yesu yaliorekodiwa kwa hizi ni kidogo sana! Ni sehemu kidogo tu! Ikiwa Bwana Yesu Alisema tu hayo maneno machache katika Injili Nne wakati huo wa miaka tatu na nusu, ni vipi Aliweza kuwashinda watu waliomfuta Yeye wakati huo? Ni vipi kazi ya Bwana Yesu imeweza kutikisa Uyahudi nzima? Kwa hivyo, ni wazi kuwa maneno ya Mungu yaliyorekodiwa katika Biblia yana sehemu kidogo sana, bila shaka sio maneno yote yaliyozungumzwa na Mungu wakati wa kazi Yake. Huu ni ukweli hakuna yeyote anayeweza kukataa! Sote tunajua kuwa Mungu ni Bwana wa uumbaji, chanzo cha maisha ya mwanadamu, kisima cha maji ya uzima ambacho hakitawahi kukauka. Utajiri wa Mungu ni usioisha katika ugavi na daima hupatikana kwa matumizi, ilhali Biblia ni rekodi tu ya hatua mbili za kwanza ya kazi ya Mungu. Kiasi cha neno la Mungu lililorekodiwa ni kidogo sana. Ni kama tone katika bahari ya maisha ya Mungu. Ni vipi tumeliwekea neno na kazi ya Mungu mipaka kuwa tu Biblia? Ni kama Mungu anaweza tu kusema hayo maneno kidogo katika Biblia. Je, si hiyo ni kumwekea mpaka, kumdunisha na kumkufuru Mungu? Kwa hivyo, kuwekea mipaka neno nzima na kazi ya Mungu kwa Biblia na kufikiria kuwa hakuna neno na kazi ya Mungu nje ya Biblia ni kosa kubwa!

Ndugu, hebu tusome vifungu vichache vya maneno ya Mwenyezi Mungu, na tutakuwa wazi hata zaidi kwa kipengele cha ukweli. Mwenyezi Mungu anasema, “Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu. Injili Nne zina chini ya sura mia moja zote pamoja ambamo mliandikwa mambo yale yaliotendeka yanayohesabika, kwa mfano Yesu Akilaani mti wa mkuyu, Petro akimkana Bwana mara tatu, Yesu Akiwaonekania wanafunzi Wake baada ya kusulubiwa na ufufuo Wake, Akifunza kuhusu kufunga, kufunza kuhusu maombi, kufunza kuhusu talaka, kuzaliwa na kizazi cha Yesu, uteuzi wa Yesu wa wanafunzi, na mengine mengi. Hata hivyo, mwanadamu anayathamini kama hazina, hata kuthibitisha kazi ya leo kulingana nayo. Hata wanaamini kuwa Yesu Alitenda kiasi tu katika muda baada ya kuzaliwa Kwake. Ni kana kwamba wanaamini kuwa Mungu anaweza kufanya hayo tu, kwamba hakuna kazi nyingine. Je huu si upumbavu?” (“Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. … Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. … Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya” (“Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Alivunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?” (“Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Ukweli Ninaoufafanua hapa ni huu: Kile Mungu alicho na anacho milele hakiishi wala hakina mipaka. Mungu ni chanzo cha uhai na vitu vyote. Mungu hawezi kueleweka na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Mwishowe, ni lazima bado Nimkumbushe kila mtu: Msimwekee Mungu mipaka katika vitabu, maneno, au tena katika matamshi Yake yaliyopita. Kuna neno moja tu kwa sifa ya kazi ya Mungu—mpya. Hapendi kuchukua njia za zamani au kurudia kazi Yake, na zaidi ya hayo Hapendi watu kumwabudu kwa kumwekea mipaka katika upeo fulani. Hii ndiyo tabia ya Mungu” (Hitimisho la Neno Laonekana katika Mwili).

Umetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana