71 Furaha Kubwa Zaidi ni Kumpenda Mungu Kweli

1

Hatimaye tumeisikia sauti ya Mungu

na tumeinuliwa mbele ya kiti Chake.

Tunakula na kunywa na kufurahia maneno ya Mungu,

tunaishi katika mwanga Wake.

Tukishiriki ukweli na kushiriki uzoefu wetu,

mioyo yetu imejawa na furaha.

Tukipitia maneno ya Mungu na kuelewa ukweli,

roho zetu zinakuwa huru na kuhisi kuwa changamfu.

Kwa kupitia hukumu ya maneno ya Mungu,

kutakaswa, tumekuwa wanadamu wapya.

Tunatafuta ukweli ili kupata maisha mapya.

Kumpenda Mungu kweli ni furaha kubwa zaidi.

2

Kwa kupitia hukumu mbele ya kiti cha Kristo,

tumeona ukweli wa upotovu wa mwanadamu.

Maneno ya Mungu ni upanga wenye makali kuwili,

unaochoma roho na mioyo yetu.

Kwa kuelewa ukweli na kujijua,

tunayo njia ya kuingia katika uzima.

Kwa kubaini asili na kiini chetu cha kishetani,

tumeamua kutubu na kuanza upya.

Kwa kupitia hukumu ya maneno ya Mungu,

kutakaswa, tumekuwa wanadamu wapya.

Tunatafuta ukweli ili kupata maisha mapya.

Kumpenda Mungu kweli ni furaha kubwa zaidi.

3

Kwa kumpenda Mungu kweli na kutekeleza wajibu wetu,

kwa hakika tutabarikiwa na Mungu.

Tunaacha kila kitu ili kumfuata Yeye

na kuwa na ushahidi mkubwa.

Tunaweka azimio letu mbele za Mungu,

tunaapa kwa maisha yetu kuwa waaminifu hadi mwisho.

Dhihaka, kashfa, ukandamizaji, ama mashaka

havitaingilia kati maendeleo yetu kamwe.

Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu,

kutakaswa, tumekuwa wanadamu wapya.

Tunatafuta ukweli ili kupata maisha mapya.

Kumpenda Mungu kweli ni furaha kubwa zaidi.

Kumpenda Mungu kweli ni furaha kubwa zaidi.

Kumpenda Mungu kweli ni furaha kubwa zaidi.

Iliyotangulia: 70 Msifu Mungu Kwa Moyo Mmoja

Inayofuata: 72 Hatuwezi Kuacha Kuimba Nyimbo za Upendo kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp