A. Maneno Juu ya Kufichua Jinsi Shetani Huwapotosha Wanadamu
65. Adamu na Hawa walioumbwa na Mungu hapo mwanzo walikuwa watu watakatifu, ambayo ni kusema, wakati katika bustani ya Edeni walikuwa watakatifu, wasio na uchafu. Walikuwa watiifu kwa Yehova, na hawakujua chochote kuhusu kuasi Yehova. Hii ni kwa sababu hawakuwa na kusumbuliwa na ushawishi wa Shetani, hawakuwa na sumu ya Shetani, na walikuwa watu wasafi kati ya binadamu wote. Waliishi katika bustani ya Edeni, bila kutiwa najisi na uchafu wowote, bila kuingiliwa na mwili, na heshima kwa Yehova. Baadaye, walipojaribiwa na Shetani, wakawa na sumu ya nyoka, na tamaa ya kuasi Yehova, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hapo mwanzo, walikuwa watakatifu na wenye kuheshimu sana Yehova; hivyo tu ndivyo walikuwa binadamu. Baadaye, baada ya kujaribiwa na Shetani, wakala tunda la maarifa ya kujua mazuri na mabaya, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Waliendelea kupotoshwa na Shetani, na wakapoteza sura asili ya mwanadamu. Hapo mwanzo, mwanadamu alikuwa na pumzi ya Yehova, na hakuwa muasi hata kidogo, na hakuwa na uovu wowote katika moyo wake. Wakati huo, mwanadamu alikuwa binadamu wa kweli. Baada ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu akawa mnyama. Fikra zake zikajawa na uovu na uchafu, bila mazuri ama utakatifu. Je, huyu si Shetani?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu
66. Tangu uvumbuzi wa wanadamu wa sayansi ya kijamii, akili ya mwanadamu imechukuliwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa zikawa zana za kuwatawala wanadamu, na hakuna tena nafasi ya kutosha kwa mwanadamu kumwabudu Mungu, na hakuna hali nzuri zaidi kwa kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka chini kabisa katika moyo wa mwanadamu. Bila Mungu mioyoni mwao, ulimwengu wa ndani wa mwanadamu ni giza, usio na tumaini na ni mtupu. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, ilikujaza mioyo na akili za wanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi na zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Katika mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali adhama na ukuu wa Mungu, wasiojali kwamba Mungu yupo, na kanuni kwamba Mungu ana ukuu juu ya vitu vyote. Kuendelea kuishi kwa wanadamu na hatima ya nchi na mataifa si muhimu tena kwao, na mwanadamu anaishi katika ulimwengu ulio mtupu unaojishughulisha tu na kula, kunywa, na kutafuta raha. … Ni watu wachache wanaojishughulisha kutafuta mahali ambapo Mungu anafanya kazi Yake leo, au kutafuta jinsi Anavyosimamia na kupanga hatima ya mwanadamu. Na kwa njia hii, bila ya mwanadamu kujua, ustaarabu wa mwanadamu unashindwa zaidi na zaidi kuendana na matakwa ya mwanadamu, na hata kuna watu wengi zaidi ambao wanahisi kwamba, kuishi katika ulimwengu kama huu, hawana furaha kuliko wale ambao tayari wamekufa. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa hali ya juu wanatoa malalamiko kama hayo. Kwani bila mwongozo wa Mungu, hata kama watawala na wanasosholojia wataumiza akili zao ili kuhifadhi ustaarabu wa mwanadamu, haitakuwa na mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu katika moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uzima wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, starehe na faraja, haya yote yanamletea mwanadamu faraja ya muda tu. Pamoja na mambo haya, mwanadamu bado haepuki kutenda dhambi na kulalamika kuhusu ukosefu wa haki kwa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kujitoa kwao na uchunguzi usio na maana wa mwanadamu vitamwongoza tu kwenye dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele, hadi kufikia kiwango ambacho mwanadamu hata anaogopa sayansi na maarifa, na hata zaidi anahofia hisia ya utupu iliyo ndani yake. Katika ulimwengu huu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, mafumbo, na hatima ya wanadamu, sembuse kuwa na uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosholojia, lakini hakuna mtu mkuu anayeweza kuja kutatua shida kama hizi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Ana Mamlaka Juu ya Hatima ya Wanadamu Wote
67. Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[1] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[2] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Si ajabu, basi, kwamba Mungu mwenye mwili anabakia kufichwa kabisa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wahenga wa zamani? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliyepo katika utumwa bila heshima amemfanya Mungu mtumwa—hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani. Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini usimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini usababishe hamu hiyo ya kukata tamaa kwa Mungu? Kwa nini umfanye Mungu kuita tena na tena? Kwa nini umlazimishe Mungu kuwa na wasiwasi kwa sababu ya Mwana Wake mpendwa? Katika jamii hii ya giza, kwa nini mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba? Kwa nini mwanadamu haelewi, mwanadamu anayeishi katika maumivu na mateso? Mungu amevumilia mateso makubwa kwa ajili yenu, kwa maumivu makubwa Amemtoa Mwanawe wa pekee, mwili wake na damu, kwa ajili yenu, sasa kwa nini bado mnakuwa vipofu? Katika mtazamo mzima wa kila mtu, mnakataa ujio wa Mungu, na mnakataa urafiki wa Mungu. Kwa nini mnakosa busara kiasi hicho? Mko tayari kuvumilia uonevu katika jamii ya giza kama hii? Kwa nini, badala ya kujaza tumbo lenu kwa milenia ya uadui, mnajidanganya wenyewe kwa “kinyesi” cha mfalme wa pepo?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)
Tanbihi:
1. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.
2. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.
68. Kutoka juu hadi chini na kutoka mwanzo hadi mwisho, Shetani amekuwa akivuruga kazi ya Mungu na kutenda katika upinzani Kwake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[1] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii kuna sanamu zilizotapakaa, zenye rangi zote za upinde wa mvua, ambazo huigeuza nchi kuwa dunia yenye kumeta-meta ya furaha za kimwili, huku mfalme wa mashetani akiendelea kucheka kwa uovu, kana kwamba njama zake mbaya zimefaulu. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani, kwa kishindo, kuangamiza kila kitu kuhusu Mungu, na kwa mara nyingine kuchafua na kumwangamiza; nia yake ni kubomoa na kuvunja kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” na kazi yake miongoni mwa wanadamu ulimwenguni? Anawezaje kumruhusu Mungu kuufichua uso wake wa kutisha? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya mahakama yake ya kifalme duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai![2] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemchezea mwanadamu sana kiasi kwamba mwonekano wake umekuwa ule wa mnyama wa mashambani, mbaya sana, na kutoka athari ya mwisho ya mwanadamu asilia imepotea. Aidha, wanatamani kuwa wa nguvu za ukuu duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu kiasi kwamba isiweze kusonga mbele kiasi hata kidogo na wanamfunga mwanadamu kwa nguvu kama kuta za shaba na chuma. Kwa kuwa wametenda madhambi makubwa sana na kusababisha maafa mengi, je, bado wanatazamia kitu kingine zaidi ya kuadibiwa? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)
Tanbihi:
1. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.
2. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”
69. Maarifa ya utamaduni wa kale na historia ambayo imekuwepo kwa maelfu kadhaa ya miaka imefunga fikra na mawazo na akili yake mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kuzifanya kutowezakana kupenyezwa na kutoweza kuoza.[1] Watu wanaishi katika duara la kumi na nane la kuzimu, kana kwamba wamefukuziwa chini na Mungu, wasiweze kuona mwanga tena. Fikra za kishirikina hivyo zimewakandamiza watu kiasi kwamba hawawezi kupumua na wana shida ya kupumua. Hawana nguvu hata kidogo ya kupinga, kimya kimya wanaendelea kuvumilia na kuvumilia…. Hakuna hata mmoja aliyewahi kujaribu kupigana au kusimama kwa ajili ya uadilifu na haki; watu wanaishi maisha ambayo ni mabaya zaidi ya mnyama, chini ya kugongwa na unyanyasaji wa maadili ya kishirikina, siku baada ya siku na mwaka baada ya mwaka. Wanadamu hajawahi kufikiria kumtafuta huyu Mungu ili kufurahia furaha katika ulimwengu wa mwanadamu. Ni kana kwamba mwanadamu amepigwa, kama majani yaliyoanguka ya majira ya kupukutika, yaliyonyauka na kukauka kabisa. Mwanadamu amepoteza kumbukumbu na anaishi bila matumaini kuzimu kwa jina la ulimwengu wa kibinadamu, akisubiri ujio wa siku ya mwisho ili kwamba waweze kupotea pamoja na kuzimu, kana kwamba siku ya mwisho wanayoitamani sana ni siku watakayofurahia pumziko la amani. Maadili ya kishirikina yamempeleka mwanadamu “Kuzimu,” hivyo kudhoofisha zaidi uwezo wa mwanadamu wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali umemlazimisha mwanadamu taratibu kuzama chini kabisa Kuzimu na kutanga mbali kabisa na Mungu. Sasa, Mungu Amekuwa mgeni kabisa kwa mwanadamu, na mwanadamu bado anafanya haraka kumwepuka wanapokutana. Mwanadamu hamtilii maanani na anamtenga kana kwamba mwanadamu hajawahi kumwona hapo kabla. Bado Mungu amekuwa mwenye subira kwa mwanadamu wakati wote katika safari ndefu ya maisha ya binadamu, kamwe harushi ghadhabu Yake isiyoweza kusitishwa kwake, Amekuwa akingoja tu kwa utulivu, bila neno, ili mwanadamu atubu na kuanza upya. Mungu zamani alikuja kwenye ulimwengu wa binadamu na Huvumilia mateso hayo hayo kama mwanadamu. Ameishi na mwanadamu kwa miaka mingi na hakuna aliyegundua kuwepo Kwake. Mungu huvumilia tu kwa kimya taabu ya uchakavu katika ulimwengu wa binadamu huku Akifanya kazi Aliyoleta yeye mwenyewe. Anaendelea kuvumilia kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na kwa ajili ya mahitaji ya wanadamu, Amevumilia, Akipitia maumivu ambayo kamwe mwanadamu hajawahi kupitia. Mbele ya mwanadamu, Amewahudumia kimya kimya na kujinyenyekeza Mwenyewe, kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na mahitaji ya wanadamu. Maarifa ya utamaduni wa kale yamemwiba mwanadamu kimya kimya kutoka kwa uwepo wa Mungu na kumkabidhi mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wanawe. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Bora[a] vimepeleka fikira za mwanadamu na mawazo yake katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Bila kujua kwa mwanadamu, mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje ya moyo wake na kuumiliki yeye mwenyewe kwa furaha ya ushindi tangu wakati huo, mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na uso wa mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa tena hata na chembe ya uhuru na hakuwa na njia ya kujikwamua kutokana na taabu za mfalme wa mashetani. Hakuwa na budi ila kuchukuliwa mateka papo hapo, kujisalimisha na kuanguka chini kwa kutii mbele yake. Hapo zamani, wakati moyo na nafsi ya mwanadamu vilikuwa vichanga, mfalme wa mashetani alipanda ndani yake mbegu ya saratani ya ukanaji Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuwa na kuhisi aibu yoyote au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa sababu ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Kuna wale hata wanaofoka kauli kama zifuatazo, kauli ambazo hazifai kutamkwa. “Mwanadamu alitoka kwa nyani katika nyakati zilizopita, na dunia leo inatoka kwa mfululizo wa jamii zizizostaarabika kuanzia takribani miaka mingi isiyohesabika. Iwapo nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Kwa nyuma, inamfanya mwanadamu kuning’iniza kwenye ukuta au kuweka kwa meza ili kutoa heshima na kumtolea sadaka. Wakati huo huo anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ujinga ulioje! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[2] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[3] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imechubuliwa na kugongwagongwa,[4] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutaleta kutimia kwa matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyo ovyo? Amemharibu mwanadamu kwa kiwango kama hicho mwanadamu hajui mahali pa raha zote, na amekuja kuwa mfu na asiye na hisia. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusitoe nafsi zetu zote kumwangamiza yeye na kumchoma ili kuondoa kabisa hofu yote ya hatari ya siku zijazo na kuruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa mapema? Genge hili la waovu limekuja katika dunia ya wanadamu na kusababisha hofu na shida kubwa. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kumeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda.[5] Hiyo kwa vyovyote vile si rahisi hata kidogo! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu Aliibuka mshindi muda mrefu uliopita, Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)
Tanbihi:
1. “Kutoweza kuoza” imenuiwa kama tashtiti hapa, kumaanisha kwamba watu ni wagumu katika ufahamu, utamaduni na mitizamo yao ya kiroho.
2. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.
3. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.
4. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.
5. “Pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda” ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.
a. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Boara ni vitabu vyenye mamlaka ya Ukonfushashi nchini China.
70. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo falsafa yake ya kuishi na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kutumia kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, na anapata maarifa zaidi, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini, na anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo. Kwa sababu Shetani ameingiza mawazo, mitazamo na dhana fulani ndani ya mwanadamu, mara tu Shetani anapoingiza sumu hii ndani ya mwanadamu, je, si mwanadamu amehadaiwa na kupotoshwa na Shetani? Kwa hivyo mnaweza kusema watu wa siku hizi wanaishi kwa kufuata nini? Je, hawaishi kwa kufuata maarifa na mawazo yaliyoingizwa na Shetani? Na mambo yaliyofichwa ndani ya maarifa na mawazo haya—je, si hayo falsafa na sumu ya Shetani? Mwanadamu huishi kwa kufuata falsafa na sumu ya Shetani. Na ni nini kilicho katika msingi wa wanadamu kupotoshwa na Shetani? Shetani anataka kumfanya mwanadamu amkane, kumpinga, na kwenda dhidi ya Mungu jinsi anavyofanya yeye; hili ndilo lengo la Shetani kumpotosha mwanadamu, na pia ndiyo njia ambayo kwayo Shetani humpotosha mwanadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
71. Katika mchakato wa mwanadamu kujifunza maarifa, Shetani atatumia mbinu zozote, inaweza iwe ni kufafanua hadithi, akimpa tu kipande kimoja cha maarifa, au kumruhusu aridhishe tamaa zake au aridhishe mawazo. Shetani anataka kukuongoza katika njia gani? Watu wanafikiri kwamba hakuna chochote kibaya na kujifunza maarifa, kwamba ni mkondo wa kiasili. Kuisema bila kutia chumvi, kukuza mawazo ya juu ama kuwa na matarajio ni kuwa na hamu ya kupata, na hii inapaswa kuwa njia sahihi katika maisha. Iwapo watu wanaweza kufanikisha mawazo yao wenyewe, ama kuwa na kazi maishani mwao—je, si ni adhimu zaidi kuishi namna hii? Kwa kufanya mambo haya, mtu anaweza kuheshimu babu zake na pia ana nafasi ya sifa yake katika historia—si hili ni jambo zuri? Hili ni jambo zuri katika macho ya watu wa kidunia na kwao linapaswa kuwa la kufaa na njema. Je, Shetani, hata hivyo, na malengo yake maovu, anawapeleka tu watu kwa njia ya aina hii na kisha kuamua amemaliza? Bila shaka la. Kwa kweli, haijalishi jinsi matamanio ya mwanadamu yalivyo makuu, haijalishi matamanio ya mwanadamu ni ya uhalisi jinsi gani ama jinsi yote yanaweza kuwa ya kufaa, yote ambayo mwanadamu anataka kufikia, yote ambayo mwanadamu anatafuta yameunganishwa bila kuchangulika na maneno mawili. Haya maneno mawili ni muhimu sana kwa kila mtu katika maisha yao yote, na ni mambo ambayo Shetani ananuia kuingiza ndani ya mwanadamu. Maneno haya mawili ni yapi? Ni “umaarufu” na “faida”. Shetani hutumia namna ya upole sana, namna ambayo inalingana kabisa na dhana za watu, na isiyokuwa na fujo sana, kuwafanya watu wakubali njia na sheria zake za kuishi, wakuze malengo ya maisha na mielekeo ya maisha, na kuja kuwa na matamanio makuu ya maisha. Haijalishi maelezo ya watu kuhusu matamanio yao maishani yanaweza kuwa ya mbwembwe kiasi gani, daima matamanio haya huzunguka umaarufu na faida. Kila kitu ambacho mtu yeyote mkuu au maarufu—au, kwa kweli, mtu yeyote—hufuatilia katika maisha yake yote kinahusiana tu na maneno haya mawili: “umaarufu” na “faida.” Watu hufikiri kwamba pindi wanapokuwa na umaarufu na faida, wanakuwa na mtaji wa kufurahia hadhi ya juu na utajiri mwingi, na kufurahia maisha. Wao hufikiri kwamba pindi wanapokuwa na umaarufu na faida, wanakuwa na mtaji wa kutafuta anasa na kujihusisha na starehe za mwili zisizo na kizuizi. Kwa ajili ya huu umaarufu na faida wanaoutamani, watu huikabidhi miili yao, mioyo yao, na hata kila kitu walicho nacho kwa Shetani kwa furaha na bila kujua, ikiwa ni pamoja na mustakabali na hatima zao. Wanafanya hivyo bila kusita, bila hata chembe ya shaka, na kamwe hawajui jinsi ya kuvidai tena vitu vyao vyote walivyokuwa navyo. Je, watu wanaweza kubaki na udhibiti wowote juu yao wenyewe punde wanapojikabidhi kwa Shetani na kuwa waaminifu kwake kwa njia hii? Bila shaka, hawawezi. Wanadhibitiwa na Shetani kikamilifu na kabisa. Wamezama kabisa na kikamilifu katika bwawa hili na hawawezi kujinasua. Baada ya mtu kukwama katika umaarufu na faida, hatafuti tena kile kilichong’aa, kile chenye haki ama yale mambo ambayo ni mazuri na mema. Hii ni kwa sababu nguvu za ushawishi ambazo umaarufu na faida yanayo juu ya watu ni kubwa mno, na vinakuwa vitu vya watu kutafuta katika maisha yao yote na pia milele bila kikomo. Hili si ukweli? Watu wengine watasema kwamba kujifunza maarifa si chochote zaidi ya kusoma vitabu ama kujifunza mambo kadhaa ambayo hawajui tayari, ili wasiwe nyuma ya wakati au wasiachwe nyuma na ulimwengu. Maarifa yanafunzwa tu ili waweze kuweka chakula mezani, kwa sababu ya siku zao za baadaye ama kwa sababu ya mahitaji ya kimsingi. Kuna mtu yeyote ambaye atastahimili mwongo wa kusoma kwa bidii kwa mahitaji ya kimsingi tu, ili kutatua swala la chakula tu? Hakuna watu kama hawa. Kwa hivyo ni nini anachotesekea miaka hii yote? Ni kwa sababu ya umaarufu na faida: Umaarufu na faida yanamngoja mbele, yanamwita, na anaamini tu kwa kupitia bidii yake mwenyewe, matatizo na mapambano ndiyo anaweza kufuata ile njia na hivyo kupata umaarufu na faida. Lazima ateseke matatizo haya kwa sababu ya njia yake ya siku za baadaye, kwa sababu ya raha yake ya siku za baadaye na kwa sababu ya maisha bora. Mnaweza kuniambia—haya maarifa kwa hakika ni nini? Je, si kanuni na falsafa za kuishi ambazo Shetani hutia ndani ya mwanadamu, kama vile “Penda Chama, penda nchi, na penda dini yako” na “Mtu mwenye hekima hutii hali”? Je, haya si “maarifa ya hali ya juu” ya maisha yaliyoingizwa kwa mwanadamu na Shetani? Chukua, kwa mfano, mawazo ya watu wakubwa, uadilifu wa watu maarufu ama roho jasiri za watu mashujaa, ama chukua uungwana na wema wa nguli na wenye upanga katika riwaya za kareti—je, si hizi zote ni njia ambazo Shetani anatia mawazo haya? Mawazo haya hushawishi kizazi kimoja baada ya kingine, na watu wa kila kizazi wanaletwa kuyakubali mawazo haya. Wao huhangaika sikuzote wakifuatilia “maarifa ya hali ya juu” ambayo hata watayatoa maisha yao kafara kwa ajili yake. Hii ndiyo njia na namna ambayo Shetani hutumia maarifa kuwapotosha watu. Hivyo baada ya Shetani kuwaelekeza watu kwenye njia hii, je, wanaweza kumtii na kumwabudu Mungu? Na, je, wanaweza kuyakubali maneno ya Mungu na kufuatilia ukweli? La hasha—kwa sababu wamepotoshwa na Shetani. Hebu tuangalie tena maarifa, mawazo, na maoni yaliyotiwa polepole ndani ya watu na Shetani: Je, mambo haya yana ukweli wa utii kwa Mungu na kumwabudu Mungu? Je, kuna ukweli wa kumcha Mungu na kuepuka maovu? Je, kuna maneno yoyote ya Mungu? Je, kuna chochote ndani yao kinachohusiana na ukweli? Hakuna chochote kabisa—vitu hivi havipo kabisa.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
72. Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti mawazo ya watu, akiwafanya wasifikirie chochote isipokuwa vitu hivi viwili, na kuwafanya wapiganie umaarufu na faida, wateseke kwa ajili ya umaarufu na faida, wavumilie fedheha na wabebe mizigo mizito kwa ajili ya umaarufu na faida, watoe kila kitu walicho nacho kwa ajili ya umaarufu na faida, na wafanye kila uamuzi au maamuzi kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani anawaweka watu pingu zisizoonekana, na, wakiwa na pingu hizi, hawana uwezo wala ujasiri wa kujinasua. Bila kujua, wanabeba pingu hizi wanapojikokota mbele hatua kwa hatua, kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida, wanadamu wanapotea kutoka kwa Mungu na Kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu. Kwa njia hii, kizazi kimoja baada ya kingine kinaangamizwa katikati ya umaarufu na faida ya Shetani. Tukiviangalia sasa vitendo vya Shetani, je, nia zake za kudhuru kwa siri si za kuchukiza sana? Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia mbaya za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zinakuwa zanye giza, zilizofifia na zisizo na matumaini. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
73. Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu ridhaa ya muda mfupi, ridhaa ambayo inawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu yakinifu. Mwanadamu anahisi kwamba amepata majibu kutoka kwenye sayansi, kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, yeye anatumia mitazamo yake ya kisayansi kama msingi wa kuthibitisha na kukubali suala hilo. Moyo wa mwanadamu unashawishiwa na sayansi na unamilikiwa nayo kiasi kwamba mwanadamu hana tena hamu ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la kisayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo. Kuna hata baadhi ya waumini wa muda mrefu wa Mungu ambao punde wanapopatwa na tatizo lolote, watatumia kompyuta kuangalia mambo na kutafuta majibu; wanapekua kila aina ya nyenzo, kwa kutumia mitazamo ya kisayansi kujaribu kutatua tatizo. Hawaamini kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, hawaamini kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutatua matatizo yote ya binadamu, hawaoni matatizo ya binadamu yaliyo mengi kutoka katika mtazamo wa ukweli. Haijalishi ni shida gani wanayokumbana nayo, hawamwombi Mungu kamwe au kutafuta suluhu kwa kutafuta ukweli katika maneno ya Mungu. Katika mambo mengi, wanapendelea kuamini kwamba maarifa yanaweza kutatua tatizo; kwao, sayansi ndiyo jibu kamili. Mungu hayupo kabisa katika mioyo ya watu kama hao. Wao ni wasioamini, na maoni yao kuhusu imani katika Mungu si tofauti na yale ya wasomi na wanasayansi wengi mashuhuri, ambao sikuzote hujaribu kumchunguza Mungu kwa kutumia mbinu za kisayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda kwenye mlima ambako safina ilisimama, na hivyo walithibitisha kuwepo kwa safina. Lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini hadithi na historia tu; haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia yakinifu. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe maikrobaiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayoamua kwamba Mungu yupo ama kwamba Ana mamlaka juu ya vitu vyote, Kwa hivyo sayansi humfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Je, haimweki mwanadamu mbali na Mungu? Je, haiwasababishi watu wamsome Mungu? Je, haiwafanyi watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu na ukuu wake, na hivyo kumkana na kumsaliti Mungu? Haya ndiyo matokeo. Kwa hiyo Shetani anapotumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani anajaribu kufikia lengo gani? Anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwahadaa watu na kuwafanya wakose hisia, na kutumia majibu yenye utata kushikilia mioyo ya watu ili wasimtafute au kuuamini uwepo wa Mungu. Kwa hivyo hii ndiyo maana Ninasema kwamba sayansi ni mojawapo ya njia ambazo kwazo Shetani hupotosha watu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
74. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo baadhi yenu hawajui maelezo yote, bado mnajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Hizi ni dhana au hadithi ambazo Shetani alimwandalia mwanadamu kitambo sana, na ambazo zimesambazwa katika nyakati tofauti. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya uchawi mmoja baada ya mwingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali aina hii ya desturi ya kitamaduni, hadithi ama vitu vya ushirikina, mara tu mambo haya yanawekwa katika akili yako, na mara tu yanakwama katika moyo wako, basi ni kama umeduwazwa—unakamatwa na kushawishika na hii mitego ya kitamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hakika huu ni uchawi. Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakatia chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu kuwekwa chini na aina hii ya uchawi, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali kiasi cha kumchukulia kama Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Aidha, kwanza unachukulia hadithi na hekaya hizi kuwa uongo, na kisha bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi na kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Kwa kutokujua kwako, unapokea mawazo haya bila kufahamu na uwepo wa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—bila shaka huu ni uchawi.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
75. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazichukia sana, lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na hata leo bado hawajaziacha kabisa. Mambo kama mipango ambayo vijana hufanya kwa ajili ya sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa, dhifa, na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe; maneno ya zamani ambayo yamerithishwa; shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi; yote haya yanachukiwa sana na Mungu. Hata siku ya ibada (ikiwemo Sabato, kama inavyoadhimishwa na ulimwengu wa dini) inachukiwa naye; mahusiano ya kijamii na mawasiliano ya kidunia kati ya mwanamme na mwanamme pia yanachukiwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, haziamriwi na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo ya sherehe za siku kuu hizi kama vile mashairi, mafataki, kandili, Komunyo, zawadi za Krismasi na sherehe za Krismasi—je, sio sanamu katika akili za wanadamu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na kitani nyembamba navyo ni sanamu zaidi. Siku zote za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizothibitika katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo. Ni uwezo mkubwa wa fikra za binadamu na dhana bunifu ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani alifanya kwa binadamu. Kadri Mashetani wanavyoishi katika eneo fulani, na kadri eneo hilo lilivyo nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi zake za kikabaila zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha ubunifu mkubwa na zinaonekana kujenga daraja kwa kazi ya Mungu, lakini kweli ni vifungo visivyoshikika ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu ili wasije kumjua Mungu—hizi zote ni hila za ujanja za Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Amekwishaharibu zana na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, “waumini wasalihina” bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati huo huo wanaacha kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana wamejawa na upendo wa Mungu lakini kwa uhalisi walimtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Karamu ya Mwisho—watu wanavichukulia hivi kama Bwana wa Mbinguni, wanaviabudu wakati wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia “Bwana, Baba wa Mbinguni.” Je, huu wote sio utani? Hadi leo, misemo mingi ya kimapokeo kama hiyo iliyorithishwa miongoni mwa wanadamu ni chukizo kwa Mungu; inazuia kabisa njia ya kuendelea mbele kwa Mungu na, zaidi ya hayo, inasababisha vipingamizi vikubwa kwa kuingia kwa mwanadamu. Mbali na kiwango ambacho Shetani amemharibu mwanadamu, sheria ya Witness Lee, uzoefu wa Lawrence, uchunguzi wa Watchman Nee, na kazi ya Paulo, haya yote yameuteka moyo wa mwanadamu. Mungu hana namna ya kufanya kazi kwa wanadamu, kwa sababu ndani yao kuna ubinafsi mwingi, sheria, kanuni, taratibu na mifumo, na vitu kama hivi; vitu hivi, ukiongezea vitendo vya watu vya imani za kishirikina, vimewakamata na kuwaharibu wanadamu. Ni kana kwamba mawazo ya watu ni filamu ya ajabu ya kichimbakazi katika rangi kamili, ikiwa na watu wa ajabu wakiendesha mawingu, ya kubuni sana kiasi cha kuwastaajabisha watu, ikiwaacha watu wametunduwazwa na kupigwa butwaa. Kusema kweli, kazi ambayo Mungu huja kufanya leo ni hasa kushughulikia na kuondoa sifa za ushirikina za binadamu na kugeuza kabisa mtazamo wao wa akili. Kazi ya Mungu haijadumu hadi leo kwa sababu ya urithi ambao umepitishwa kwa vizazi na binadamu; ni kazi kama ilivyoanzishwa na Yeye binafsi na kukamilishwa na Yeye, bila haja yoyote ya kuurithi urithi wa mwanadamu fulani mkuu wa kiroho, au kurithi kazi yoyote ya asili ya uwakilishi iliyofanywa na Mungu katika enzi nyingine fulani. Binadamu hawahitaji kujishughulisha na jambo lolote kati ya haya. Mungu ana mtindo mwingine leo wa kuzungumza na wa kufanya kazi, kwa hiyo mbona binadamu wajisumbue? Kama wanadamu watatembea njia ya leo katika mkondo wa sasa huku wakiendeleza urithi wa “babu” zao, hawatafikia hatima yao. Mungu huhisi kinyaa sana kwa hali hii hasa ya tabia ya mwanadamu, jinsi Anavyoichukia mno miaka, miezi na siku za ulimwengu wa binadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (3)
76. Shetani humpotosha na kumtawala mwanadamu kupitia mitindo ya kijamii. Mitindo ya kijamii inajumuisha vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na maeneo mbalimbali kama vile kuabudu watu mashuhuri na wenye kusifika, na vilevile waigizaji wa filamu na wanamuziki mashuhuri, kuwaabudu watu mashuhuri, michezo ya mtandaoni, n.k.—hizi zote ni sehemu ya mitindo ya kijamii, na hakuna haja ya kuingia katika maelezo mengi hapa. Tutazungumzia tu kuhusu mawazo ambayo mitindo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inavyowafanya watu wajiendeshe duniani, na malengo ya maisha na mitazamo ambayo inaleta kwa watu. Hizi ni muhimu sana; zinaweza kudhibiti na kushawishi mawazo na maoni ya watu. Mitindo hii huibuka moja baada ya nyingine, na yote huwa na ushawishi mbaya unaoendelea kumdhalilisha mwanadamu na kuwafanya watu kupoteza dhamiri, ubinadamu na akili, kudhoofisha zaidi maadili yao na ubora wa tabia zao, kiasi kwamba tunaweza hata kusema kwamba watu wengi sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, na wala hawana dhamiri yoyote, sembuse kuwa na akili yoyote. Kwa hivyo mitindo hii ya kijamii ni ipi? Ni mitindo ambayo huwezi kuiona kwa macho. Wakati mtindo mpya unapoenea duniani kote, pengine ni idadi ndogo tu ya watu ndio walio na ufahamu wa juu, wakitenda kama waanzishaji mitindo. Wao huanza kwa kufanya jambo jipya, kisha kukubali aina fulani ya wazo au aina fulani ya mtazamo. Hata hivyo, watu wengi, wataendelea kuambukizwa, kuvutiwa na kustaarabishwa na mtindo huu katika hali ya kutofahamu, hadi wote bila kujua na bila kupenda wanaikubali na wanazama ndani yake na kudhibitiwa nayo. Moja baada ya nyingine, mitindo ya aina hii inawafanya watu ambao si wa mwili na akili timamu, wasiojua ukweli, na hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi, kuzikubali kwa furaha pamoja na mtazamo wa maisha, na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani kuhusu jinsi ya kuyashughulikia maisha na jinsi ya kuishi ambavyo Shetani “amewapatia.” Na hawana nguvu, wala uwezo, wala ufahamu wa kupinga. …
… Shetani hutumia hii mitindo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mitindo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu, ni nini basi mwanadamu anakuwa? Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Kwa nini? Kwa sababu, ni mwelekeo gani wa kisaikolojia uliopo ndani ya moyo wa mwanadamu? Ni kipi ambacho mwanadamu anatetea? Mwanadamu huanza kupenda uovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka. Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mitindo ya aina hii, maarifa ambayo mmefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Je, desturi ya kitamaduni na ushirikina mnayojua yanaweza kuwasaidia kutupilia mbali hii hatari ya kutisha? Je, maadili ya desturi na sherehe za desturi ambazo mwanadamu huelewa zinaweza kumsaidia kujizuia? Kwa mfano, chukua riwaya ya Analects na Tao Te Ching. Je, vinaweza kuwasaidia watu kujikwamua miguu yao kutoka katika tope la mitindo hii miovu? Bila shaka hapana. Hivyo, mwanadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mwenye kiburi, mwenye kujishusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote miongoni mwa jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanakamata riziki zao kwa kutumia ukatili; wanapata vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha? Unatisha sana: Sio tu kwamba walimsulubisha Mungu, bali pia wangewachinja wote wanaomfuata—kwa sababu mwanadamu ni mwovu sana.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
77. “Pesa inaifanya dunia izunguke” ni falsafa ya Shetani, na inaenea miongoni mwa wanadamu wote, katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umewekwa ndani ya moyo wa kila mtu. Tangu mwanzo kabisa, watu hawakuukubali msemo huu, lakini kisha waliukubali kimyakimyabila kusema walipokutana na maisha halisi, na wakaanza kuhisi kwamba maneno haya kweli yalikuwa ya kweli. Je, huu si mchakato wa Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine watu hawaelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana kiwango tofauti cha tafsiri na utambuzi wa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu alionao katika msemo huu, ni nini athari mbaya ambayo inaweza kuwa nayo katika moyo wa mtu? Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu katika dunia hii, ikiwemo kila mmoja wenu. Kitu hiki ni kipi? Ni kuabudu pesa. Je, ni vigumu kuondoa kitu hiki kutoka kwenye moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotoshaji wa Shetani kwa mwanadamu ni wa kina sana! Shetani hutumia pesa kuwajaribu watu, na kuwapotosha ili waabudu pesa na kuabudu vitu vya kimwili. Na ibada hii ya pesa inadhihirika vipi ndani ya watu? Je, mnahisi kwamba hamwezi kuishi katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja bila pesa haiwezi kuishika kabisa? Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa walizo nazo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hupoteza utu na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Je, kupoteza nafasi ya kupata ukweli na kuokolewa si ndiyo hasara iliyo kubwa zaidi kwa watu? Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kujua. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, na unaweza kuujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, lakini hauko radhi kulipa gharama au kuteseka ili kupata ukweli. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyume na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unachogundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Yaani, msemo huu tayari umeyadanganya na kuyadhibiti mawazo yako, tayari umeitawala tabia yako, na unaona afadhali utawale majaliwa yako kuliko uweke kando ufuatiliaji wako wa mali. Kwamba watu wanaweza kutenda namna hiyo, kwamba wanaweza kudhibitiwa na kuongozwa na maneno ya Shetani—si hili linamaanisha kwamba wamedanganywa na kupotoshwa na Shetani? Je, falsafa na mawazo ya Shetani, na tabia ya Shetani, havijakita mizizi ndani ya moyo wako? Unapofuatilia mali bila kufikiri na kuacha ufuatiliaji wa ukweli, je, Shetani hajafanikiwa katika lengo lake la kukudanganya wewe? Hii ndiyo hali halisi hasa. Kwa hivyo, je, unaweza kuhisi wakati unapodanganywa na kupotoshwa na Shetani? Huwezi. Kama huwezi kumwona Shetani akiwa amesimama mbele yako, au kuhisi kwamba ni Shetani anayetenda kisirisiri, je, utaweza kuuona uovu wa Shetani? Je, utaweza kujua jinsi Shetani huwapotosha binadamu? Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu awe mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambazo hujui na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea; hivi ndivyo wanavyoishi watu chini ya mamlaka ya Shetani, na wanamwabudu Shetani bila kujua, na upotoshaji wa Shetani kwa mwanadamu unazidi kuwa wa kina.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
78. Kuna Njia Sita za Msingi Ambazo Shetani Hutumia Kumpotosha Mwanadamu
Ya kwanza ni kudhibiti na kulazimisha. Yaani, Shetani atafanya vyovyote vile kudhibiti moyo wako. “Kulazimisha” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kutumia mbinu za kutishia na kulazimisha kukufanya umtii, kukufanya ufikirie matokeo usipomtii. Unaogopa na huthubutu kumpinga, kwa hivyo basi unamtii.
Ya pili ni kudanganya na kulaghai. “Kudanganya na kulaghai” yanahusisha nini? Shetani hutunga baadhi ya hadithi na uongo, kukulaghai wewe kuziamini. Hakwambii kamwe kwamba mwanadamu aliumbwa na Mungu, wala hasemi pia moja kwa moja kwamba hukuumbwa na Mungu. Hatumii jina “Mungu” kabisa, lakini badala yake hutumia kitu kingine mbadala, akitumia kitu hiki kukudanganya ili kimsingi usiwe na wazo la kuwepo kwa Mungu. Huu ulaghai bila shaka unahusisha vipengele vingi, sio tu hiki kimoja.
Ya tatu ni kufunza kwa nguvu. Watu wanafunzwa nini kwa nguvu? Je, kufunzwa kwa nguvu kunafanywa kwa hiari ya mwanadamu mwenyewe? Je, kunafanywa na idhini ya mwanadamu? Bila shaka sivyo. Hata usipokubali, hakuna unachoweza kufanya kuhusu hilo. Katika kutokujua kwako, Shetani anakutia mafundisho, akitia fikira zake ndani mwako, kanuni zake za maisha na kiini chake.
Ya nne ni vitisho na vishawishi. Yaani, Shetani hutumia hila mbalimbali kukusababisha umkubali, umfuate na ufanye kazi katika Huduma yake. Atafanya chochote kufikia malengo yake. Wakati mwingine yeye hukupa fadhili kidogo, wakati wote akikushawishi utende dhambi. Usipomfuata, atakufanya uteseke na kukuadhibu, na hutumia njia mbalimbali kukushambulia na kukulia njama.
Ya tano ni uongo na kutia ganzi. “Uongo na kutia ganzi” ni wakati ambapo Shetani hutia ndani ya watu maneno na mawazo yanayolingana na dhana zao na yanayoonekana ya kuaminika, kufanya ionekane kwamba anajali hali za kimwili za watu, kuhusu maisha yao na siku zao za baadaye, wakati kwa kweli lengo lake la kweli ni kukudanganya tu. Kisha anakutia ganzi ili usijue kile kilicho sahihi na kile kilicho makosa, ili udanganywe bila kujua na hivyo kuja chini ya udhibiti wake.
Ya sita ni maangamizi ya mwili na akili. Ni sehemu gani ya mwanadamu ambayo Shetani huharibu? Shetani huharibu akili yako, kukufanya kutokuwa na nguvu za kupinga, kumaanisha kuwa, kidogo kidogo, moyo wako unageuka kwa Shetani licha ya wewe mwenyewe. Huingiza mambo haya ndani yako kila siku, na kutumia mawazo na utamaduni huu kukushawishi na kuwakazia mawazo kila siku, akivunja utashi wako kidogo kidogo, ili kwamba hutamani tena kuwa mtu mwema, ili kwamba hutaki tena kutetea kile unachoita “haki”. Bila kujua, huna tena utashi wa kuogelea kinyume na mkondo wa maji, lakini badala yake kuelea na mkondo. “Maangamizi” yanamaanisha Shetani kuwatesa watu sana hadi wanakuwa vivuli vya wao wenyewe, sio wanadamu tena. Hapa ndipo Shetani huchukua fursa ya kuwameza.
Kila mojawapo ya ujanja hizi ambao Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu humfanya mwanadamu akose nguvu ya kupinga; yoyote kati ya ujanja huu inaweza kuwa ya kuangamiza kwa mwanadamu. Kwa maneno mengine, chochote anachofanya Shetani na kila ujanja wowote anatumia inaweza kukufanya upotoke, inaweza kukuleta chini ya udhibiti wa Shetani na inaweza kukuzamisha katika bwawa la uovu na dhambi. Huu ndio ujanja ambao Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
79. Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika “taasisi za elimu ya juu.” Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope. Hata wanaposikia ukweli, wale wanaoishi gizani hawafikiri kuuweka katika vitendo, na wala kuelekea kumtafuta Mungu hata kama wameuona mwonekano Wake. Jinsi gani wanadamu wapotovu kiasi hiki wawe na nafasi yoyote ya wokovu? Jinsi gani wanadamu waovu kiasi hiki kuishi katika mwanga?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu
80. Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake
Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuwadanganya watu. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anatetea haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kuwapotosha na kuwachochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu aidhinishe na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za kuwa mwema na kuondoa baraka zake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kuwaangamiza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ukatili wake; tamanio lake la kuwadhuru na kuwameza watu ndipo litazidi zaidi. Anakasirika kwasababu ya mwamko wa mwanadamu katika kufuata ukweli; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka katika gereza lake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kikatili.
Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake ya uovu. Kati ya matendo yote maovu ambayo Shetani ameyafanya juu ya mwanadamu—kuanzia kwa jitihada zake za awali za kumdanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, hadi ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kumtambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua kiini kiovu cha Shetani; hakuna hata kimoja kinachoshindwa kuthibitisha ukweli kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata kimoja kinachoshindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inayalinda maovu yake, inadumisha uendelevu wa vitendo vyake viouvu inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Matendo haya ya Shetani ni uadui kwa Mungu, na yataangamizwa na ghadhabu ya Mungu. Ingawa Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake ni njia tu ya kudhihirisha asili yake mbaya. Sababu inayomfanya Shetani akasirike na kuwa mkali ni kwa sababu njama zake zilizofichika zimefichuliwa; mipango yake haiwezi tena kufanikiwa kwa urahisi; malengo yake ya kijinga na tamaa yake mbaya ya kuchukua nafasi ya Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila wakati ambao hasira ya Mungu inaachiliwa huwa haifichui tu sura ya kweli ya Shetani iliyo mbaya; bali pia inafichua na kuweka wazi tamaa mbaya ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Mlipuko wa hasira ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huashiria ulinzi na mwendelezo wa mambo mazuri, na huashiria asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II