Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maneno Mashuhuri Kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

IX Maneno Bora Zaidi Juu ya Kukifichua Asili ya Shetani ya Wanadamu Wapotovu na Asili Yao

1. Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. Kama hisia ya mwanadamu na utambuzi hauwezi kubadilika, basi mabadiliko katika tabia yake hayawezekani, sawa na kuwa baada ya moyo wa Mungu. Kama hisia ya mwanadamu sio timamu, basi hawezi kumhudumia Mungu na hafai kutumiwa na Mungu. “Hisia za Kawaida” inaashiria kutii na kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuwa dhahiri kwa Mungu, na kwa kuwa na dhamiri kwa Mungu. Inamaanisha kuwa na moyo mmoja na akili kwa Mungu, na si kwa kumpinga Mungu kwa makusudi. Wale ambao ni wa akili potovu hawako hivi. Tangu mwanadamu aharibiwe na Shetani, ametunga dhana kuhusu Mungu, na yeye hajakuwa na uaminifu au kumtamani Mungu, pia hana dhamiri kwa Mungu. Mwanadamu kwa makusudi anapinga na huweka hukumu juu ya Mungu, na, zaidi ya hapo, anatupa shutuma Kwake nyuma Yake. Mwanadamu anajua vizuri kuwa Yeye ni Mungu, lakini bado humhukumu nyuma ya mgongo wake, hana nia ya kumtii, na hufanya madai ya kipofu na maombi kwa Mungu. Watu wa aina hii—watu walio na akili potovu—hawana uwezo wa kujua tabia zao za kudharauliwa au ya kujuta uasi wao. Kama watu wana uwezo wa kujijua wenyewe, basi wao wamerudisha kiasi kidogo cha akili zao; Zaidi ya vile watu wanavyomuasi Mungu lakini hawajui wenyewe, ndivyo walivyo zaidi wenye akili isiyo timamu.

kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele ya Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akampiga Yesu misumari juu ya msalaba na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa ya kuchukiza na wa hali ya chini. Kama mwanadamu angekuwa na ubinadamu kidogo, hangekuwa mkatili kiasi hicho katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa hivyo katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo, hangekuwa mwenye “shukrani” kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa katika mwili, lakini yeye hawezi kumshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi nzuri kiasi hicho, na badala yake analaani kuja kwa Mungu, au kupuuza kabisa ukweli wa Mungu aliyepata mwili, na inaonekana anapinga hali hii na anachoshwa nayo. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukua kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake bila kujali—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu. Mwanadamu hajakosa tu shukrani kwa Mungu mwenye mwili kwa kukabidhi maisha na neema nyingi juu ya wanadamu, bali pia anachukia Mungu kwa kumpatia ukweli; ni kwa sababu mwanadamu hana haja ya kujua ukweli hata kidogo ndio maana anamchukia Mungu. Haitoshi kwamba mwanadamu hawezi kuutoa uhai wake kwa ajili ya Mungu mwenye mwili tu, lakini pia anajaribu kutoa neema kutoka kwa Mungu, na anafanya madai kwa Mungu yaliyo mara kadhaa kubwa kuliko kile mwanadamu ametoa kwa Mungu. Watu wa dhamiri na hisia kama hizo huchukua yote haya kama haki yao, na bado wanaamini kuwa wao wamefanya mengi sana kwa ajili ya Mungu, na kwamba Mungu amewapa kidogo sana. Kuna watu ambao wamenipa bakuli la maji na kisha kunyosha mikono yao na kudai sawia na[a] bakuli mbili za maziwa, au kunipa chumba kwa usiku mmoja lakini walijaribu kunilipisha mara nyingi zaidi katika ada ya makazi. Ukiwa na ubinadamu kama huo, na dhamiri ya aina hii, ni jinsi gani bado mnatarajia kupata uzima? Nyinyi ni fukara wa kudharauliwa mlioje!

kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia ya mwanadamu ni usiohisi chochote, ilhali bado anataka apate baraka; ubinadamu wake si wa kuheshimika lakini bado anataka kumiliki ukuu wa mfalme. Ataweza kuwa mfalme wa nani, na hisia kama hiyo? Jinsi gani yeye na ubinadamu kama huo ataweza kukaa kwenye kiti cha enzi? Mwanadamu kwa kweli hana aibu! Yeye ni mdhalili wa kujivuna tu! Kwa wale kati yenu mnaotaka kupokea baraka, Ninawashauri kwanza mtafute kioo na kuangalia picha zenu mbaya—je, una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mwanadamu ambaye anaweza kupata baraka? Hakujawa mabadiliko hata madogo katika tabia yako na wewe hujaweka ukweli wowote katika vitendo, ilhali bado unatamani kuona siku ifuatayo ikiwa ya ajabu. Unajihadaa mwenyewe!

kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Ushawishi wenye madhara ambao maelfu ya miaka ya “roho wa juu sana wa utaifa” umeacha ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu pamoja na fikira za kikabaila ambazo watu wamefungwa nazo na kutiwa minyororo, bila uhuru wowote, na kusababisha watu kutokuwa na hamasa au ustahimilivu, hawana shauku ya kusonga mbele, lakini badala yake wanakuwa baridi na kurudi nyuma, wakiwa na akili ya utumwa ambayo ina nguvu sana, na kadhalika—sababu hizi zimetengeneza taswira chafu na mbaya kwa mitazamo ya njozi, mawazo, maadili, na tabia ya binadamu. Inaonekana, wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kutisha, na hakuna anayetafuta kusonga mbele miongoni mwao, hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora. badala yake, wanaridhika na waliyo nayo maishani, kutumia siku zao kuzaa na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi zao, wakiwa na njozi ya kuwa na familia ya raha na yenye furaha, ya upendo wa ndoa, ya watoto wenye upendo, ya maisha yenye furaha katika miaka yao ya uzeeni wanapoishi kwa kudhihirisha maisha yao kwa amani. … Kwa makumi, maelfu, makumi ya maelfu ya miaka hadi sasa, watu wamekuwa wakipoteza muda wao kwa njia hii, hakuna anayetengeneza maisha makamilifu, wanapigana tu wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu huu wa giza, wakipambana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani amewahi kutafuta mapenzi ya Mungu? Kuna mtu yeyote aliyewahi kutilia maanani kazi ya Mungu? Sehemu hizi zote za binadamu zinazomilikiwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu tangu zamani, kwa hiyo ni vigumu sana kutekeleza kazi ya Mungu na hata watu hawana moyo wa kuzingatia kile ambacho Mungu amewaaminia leo.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga. Kwa hivyo, haiwezekani ukweli kumilikiwa kiasili katika asili ya kila mtu, na zaidi ya hayo, hawawezi kuzaliwa na kiini cha kumwogopa, kiini cha kumheshimu Mungu. Kinyume na hayo, wana asili inayompinga Mungu, isiyomtii Mungu, na isiyopenda ukweli. Asili hii ndilo tatizo Ninalotaka kuzungumzia—usaliti.

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Kuishi kwa mwanadamu kunategemea kupata mwili kwa roho. Kwa maneno mengine, kila mtu anapata maisha ya kibinadamu ya mwili baada ya roho yake kupata mwili. Baada ya mwili wa mtu kuzaliwa, maisha hayo yanaendelea hadi kufikia mipaka ya juu zaidi ya mwili, yaani, wakati wa mwisho ambapo roho inaliacha umbo lake. Mchakato huu unajirudia tena na tena na roho ya mtu ikija na kwenda, ikija na kwenda, hivyo kudumisha maisha ya wanadamu wote. Uhai wa mwili vilevile ni uhai wa roho ya mwanadamu, na roho ya mwanadamu husaidia maisha ya mwili wa mwanadamu. Hiyo ni kusema, uhai wa kila mtu unatoka kwa roho zao; si miili yao ambayo ilikuwa na uhai kwanza. Kwa hivyo, asili ya wanadamu inatoka kwa roho zao; haitoki kwa miili yao. Roho ya kila mtu ndiyo tu inajua jinsi imepitia majaribu, mateso na uovu wa shetani. Mwili wa mwanadamu hauwezi kulifahamu hili. Vivyo hivyo, pasipo kujua mwanadamu anaendelea kuwa mchafu, mwovu na mbaya zaidi na zaidi, ilhali umbali baina Yangu na mwanadamu unaendelea kuongezeka hata zaidi, na siku za mwanadamu zinaendelea kuwa za giza hata zaidi. Roho za wanadamu zote ziko karibu na mikono ya Shetani. Kwa hivyo, ni dhahiri kuwa mwili wa mwanadamu pia umemilikiwa na Shetani. Ingekuwaje miili kama hii na wanadamu kama hawa wasimuasi Mungu na kupatana naye kiasili? Nilimtupa chini Shetani kwa sababu alinisaliti, basi wanadamu wangejinasua vipi kutoka katika matokeo ya hili? Hii ndiyo sababu asili ya mwanadamu ni usaliti.

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Tabia ambayo haiwezi kunitii kabisa ni usaliti. Mwenendo ambao hauwezi kuwa mwaminifu Kwangu ni usaliti. Kunidanganya na kutumia uongo kunilaghai ni usaliti. Kujawa na dhana na kuzieneza kila mahali ni usaliti. Kutozilinda shuhuda na maslahi Yangu ni usaliti. Kubuni tabasamu wakati mtu ameniacha moyoni mwake ni usaliti. Tabia hizi ni mambo yote ambayo daima mna uwezo wa kuyafanya, na pia ni za kawaida kati yenu. Hakuna mmoja wenu anayeweza kufikiri kwamba hilo ni tatizo, lakini Mimi sifikirii hivyo. Siwezi kuchukulia kunisaliti kama jambo dogo, na zaidi ya hayo siwezi kulipuuza. Nafanya kazi miongoni mwenu sasa lakini bado mko hivi. Kama siku moja hakutakuwa na mtu wa kuwalinda na kuwaangalia, si nyote mtakuwa wafalme wa kilima?[b] Kwa wakati huo, nani atavisafisha vitu tena na kuondoa uchafu mnaposababisha janga kubwa?

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Msiamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwamba hamna asili ya usaliti kwa sababu hamjamkosea mtu yeyote. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi unachukiza sana. Maneno ambayo Nimenena kila wakati yamewalenga watu wote, sio tu mtu mmoja au aina ya mtu. Kwa sababu tu hujanisaliti Mimi kwa jambo moja haithibitishi kwamba huwezi kunisaliti katika jambo lolote jingine. Baadhi ya watu hupoteza imani yao katika kuutafuta ukweli wakati wa kipingamizi katika ndoa zao. Baadhi ya watu huwacha wajibu wao wa kuwa waaminifu Kwangu wakati wa kuvunjika kwa familia. Baadhi ya watu huniacha kwa ajili ya kutafuta wakati wa furaha na msisimko. Baadhi ya watu afadhali waanguke katika korongo lenye giza kuliko kuishi katika mwanga na kupata furaha ya kazi ya Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu hupuuza ushauri wa marafiki kwa ajili ya kuridhisha tamaa zao kwa ajili ya mali, na hata sasa hawawezi kuyakubali makosa yao na kugeuka. Baadhi ya watu huishi tu kwa muda chini ya jina Langu ili wapate ulinzi Wangu, wakati wengine hujitolea tu kidogo kwa sababu wameyashikilia maisha na wanahofu kifo. Si vitendo hivi na vingine viovu na zaidi ya hayo visivyofaa tabia tu ambazo watu wamenisaliti kwa muda mrefu ndani ya mioyo yao? Bila shaka, Najua usaliti wa watu haukuwa umepangwa mapema, lakini ni ufunuo wa kimaumbile wa asili zao. Hakuna mtu anayetaka kunisaliti, na zaidi ya hayo hakuna mtu aliye na furaha kwa sababu amefanya kitu kunisaliti. Kinyume chake, wanatetemeka kwa hofu, sivyo? Hivyo mnafikiri kuhusu jinsi mnavyoweza kuzikomboa saliti hizi, na jinsi mnavyoweza kubadili hali ya sasa?

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa kando, wakiokolewa kutoka katika kambi ya Shetani, na kuletwa katika ufalme wa leo. Watu hawa kamwe hawaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hata hivyo, asili ya mwanadamu bado imekita mizizi katika mwili wa mwanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ijapokuwa roho zenu zimeokolewa, asili yenu bado ni ya mwonekano wake wa zamani na uwezekano kuwa mtanisaliti unabakia asilimia mia moja. Ndiyo maana kazi Yangu ni ya kudumu muda mrefu sana, kwa kuwa asili yenu ni isiyotikiswa kabisa. Sasa hivi nyote mnateseka jinsi mnavyoweza katika kutimiza wajibu wenu, lakini ukweli usiopingika ni huu: Kila mmoja wenu ana uwezo wa kunisaliti Mimi na kuirudia miliki ya Shetani, katika kambi yake, na kuyarudia maisha yenu ya zamani. Wakati huo haitawezekana kwenu kuwa hata na chembe ya utu au mwonekano wa binadamu kama mlionao sasa. Katika hali nzito, mtateketezwa, na zaidi mtalaaniwa milele, msipate mwili tena lakini muadhibiwe vikali. Hili ni tatizo lililowekwa mbele yenu.

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Mlitengwa kutoka kwa matope na kwa vyovyote vile, mlichaguliwa kutoka kwa mashapo, wachafu na mliochukiwa na Mungu. Mlikuwa wa Shetani[c] na wakati mmoja mlikanyagwa na kuchafuliwa na yeye. Hii ndiyo maana inasemwa kuwa mlitengwa kutoka kwa matope, na nyinyi si watakatifu, lakini badala yake nyinyi ni vitu visivyo binadamu ambavyo Shetani kwa muda mrefu alikuwa amevifanya vipumbavu. Haya ndiyo maelezo sahihi zaidi yenu. Lazima mtambue kuwa nyinyi ni uchafu unaopatikana katika maji yaliyotuama na matope, kinyume na ushikaji unaofaa kama samaki na uduvi, kwa maana hakuna starehe inayoweza kupatikana kutoka kwenu. Kuzungumza waziwazi, nyinyi ni wanachama wa kiwango cha chini sana cha kijamii, wanyama wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Kusema kweli, kuwahutubia kwa istilahi kama hizo si chuku au kutia chumvi, lakini ni njia ya kurahisisha suala hilo. Kuwahutubia kwa istilahi kama hizo kwa kweli ni njia ya kuwapa heshima. Utambuzi wenu, hotuba, mwenendo kama watu, na vitu yote katika maisha yenu—ikiwa ni pamoja na hali yenu katika matope—vinatosha kuthibitisha kwamba utambulisho wenu ni “wa kipekee.”

kutoka katika “Utambulisho wa Asili wa Mwanadamu na Thamani Yake: Je, ni Nini?” katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Mwanadamu hana nia ya kumfuata Mungu, hana nia ya kutumia mali yake kwa Mungu, hana nia ya kutoa juhudi za milele kwa Mungu, na badala yake anasema kwamba Mungu amepita kiasi, kwamba mengi kuhusu Mungu yanakinzana na dhana za mwanadamu. Na ubinadamu kama huu, hata kama mngekuwa wakarimu katika juhudi zenu bado hamngeweza kupata kibali cha Mungu, bila kutaja kuwa hamumtafuti Mungu. Je, hamjui kwamba ninyi ni bidhaa mbovu za binadamu? Je, hamjui kwamba hakuna ubinadamu ulio mnyenyekevu zaidi kuliko wenu? Je, hamjui “cheo” chenu ni kipi? Wale ambao kweli wanampenda Mungu wanawaita baba wa mbweha, mama wa mbweha, mwanambweha, na mjukuu wa mbweha; nyinyi ni vizazi vya mbweha, watu wa mbweha, na mnapaswa kujua utambulisho wenu na kamwe msiwahi kuusahau. Msidhani kwamba nyinyi ni kiumbe mkubwa zaidi: Nyinyi ni kundi mojawapo la wasio-wanadamu wabaya zaidi miongoni mwa wanadamu. Je, hamjui lolote kuhusu haya? Je, mnajua ni kiasi gani cha hatari Nimechukua ili Nifanye kazi miongoni mwenu? Kama akili yenu haiwezi kurudi kawaida, na dhamiri yenu haiwezi kufanya kazi kwa kawaida, basi kamwe hamtawahi kuwa huru kutokana na jina “mbwa mwitu”, kamwe hamtaitoroka siku ya laana, kamwe hamtaitoroka siku ya adhabu yenu. Mlizaliwa mkiwa duni, kitu kisicho na thamani yoyote. Kwa hivyo nyinyi ni kundi la mbwa mwitu wenye njaa, rundo la uchafu na takataka, na, tofauti na nyinyi, Mimi Sifanyi kazi kwenu ili nipate chochote, lakini kwa sababu ya haja ya kazi. Mkiendelea kuwa waasi kwa njia hii, basi Nitakomesha kazi Yangu, na kamwe sitafanya kazi kwenu tena; badala yake, Nitahamisha Kazi yangu kwa kundi lingine linalonipendeza, na kwa njia hii kuondoka kwenu milele, kwa sababu Mimi sina nia ya kuwaangalia walio katika uadui na Mimi. Hivyo basi, je, mnataka kulingana na Mimi, au katika uadui dhidi Yangu?

kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni yule mwovu anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake, ni matope na imejaa mashimo makubwa, ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Na katika pembe zenye baridi na giza magenge ya mapepo yameshika makazi. Na kila mahali katika dunia ya binadamu, mapepo yanakuja na kwenda katika magenge. Kizazi cha wanyama wa aina yote, waliojawa na uchafu, wanapigana mkono kwa mkono katika mapambano ya kikatili, sauti ambayo huleta hofu moyoni. Nyakati kama hizo, katika dunia kama hiyo, “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kupata hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa tangu mwazo mwigizaji akitenda kwa mfano wa Shetani—hata zaidi, kuwa na mwili wake, wakitumika kama shahidi wa kushuhudia kwa Shetani, kwa uwazi. Aina hii ya jamii ya binadamu, aina hii ya watu wachafu walioharibika tabia, na watoto wa aina hii wa familia hii ya binadamu potovu, inawezaje kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Mtu anaweza kuanza wapi kuongea juu ya shahidi Wangu? Kwa adui ambaye, baada ya kupotosha mwanadamu, anasimama dhidi Yangu, tayari amemchukua mwanadamu—mwanadamu ambaye niliumba kitambo sana na ambaye alikuwa amejawa na utukufu Wangu kuishi kulingana na Mimi—na kumchafua. Amepokonya utukufu Wangu, na yote ambayo imetia moyoni mwa mwanadamu ni sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

kutoka katika “Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. “Mbinguni, Shetani ni adui Yangu, duniani, mwanadamu ni adui Yangu. Kwa sababu ya muungano kati ya mbingu na dunia, vizazi tisa vyao vinapaswa kuchukuliwa kuwa na hatia kwa ushirikiano.” Shetani ni adui wa Mungu; sababu Ninayosema hiyo ni kwa sababu hamlipi Mungu kwa neema na fadhili Zake, lakini badala yake “hupiga kasia kinyume na mkondo,” na kwa kufanya hivyo hatimizi “utiifu wa kuwapenda wazazi” kwa Mungu. Je, watu hawako hivi pia? Hawaonyeshi heshima ya upendo kwa “wazazi” wao na hawalipi malezi na msaada wa “wazazi” wao. Hili linatosha kuonyesha kwamba watu wa dunia ni jamaa ya Shetani mbinguni. Mwanadamu na Shetani ni wa moyo mmoja na akili moja dhidi ya Mungu, na kwa hiyo si ajabu Mungu anahusisha vizazi tisa kama wenye hatia kwa ushirikiano na hakuna anayeweza kusamehewa.

kutoka katika “Sura ya 38” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Hakuna siku ipitayo bila Mungu kuwaita watu Wake ambao wanasinzia ili awaokoe, lakini wote wako katika hali ya uvivu kana kwamba walikuwa wamemeza dawa ya usingizi. Asipowaamsha hata kwa dakika moja wanarudi kwa hali yao ya usingizi, bila ufahamu. Inaonekana kwamba watu Wake wote wamepooza kwa thuluthi tatu. Hawajui mahitaji yao wenyewe au kasoro zao wenyewe, au hata wanachopaswa kuvaa au wanachopaswa kula. Inaonyesha kwamba joka kubwa jekundu limetumia kiasi kikubwa cha jitihada kuwapotosha watu. Ubaya wake unafikia kotekote katika kila mkoa wa Uchina. Hata limewafanya watu kuchukizwa na kutokuwa radhi kuishi tena katika nchi hii ya kuharibika, isiyo na adabu. Kile ambacho Mungu huchukia zaidi ni kiini cha joka kubwa jekundu, ndiyo maana Huwakumbusha watu katika ghadhabu Yake kila siku, na watu huishi chini ya ulinzi wa ghadhabu Yake kila siku. Hata hivyo, wengi sana wa watu bado hawajui kumtafuta Mungu, lakini wao huketi tu wakitazama na kungoja kulishwa kwa mkono. Hata kama wangekuwa wana njaa kabisa hawangekuwa radhi kwenda kutafuta chakula chao wenyewe. Dhamiri za watu zilipotoshwa na Shetani kitambo sana na zikabadilika kwa hali kuwa zisizo na huruma. Si ajabu Mungu alisema: “Kama Mimi Singewazindua, bado usingeamka, lakini, mngeendelea kuwa kama mlioganda, na tena, katika hali ya kubumbwaa.” Ni kana kwamba watu walikuwa kama wanyama ndani ya bumbwaa waliokuwa wakipitisha majira ya baridi na hawakutaka kula au kunywa; hii hasa ni hali ya sasa ya watu wa Mungu, ndiyo maana Mungu huwataka tu watu wamjue Mungu mwenye mwili Mwenyewe katika nuru. Hawashurutishi watu wabadilike kiasi kikubwa au wao kuwa na ukuaji mkubwa katika maisha yao. Hilo lingetosha kulishinda joka kubwa jekundu chafu, lenye kutia kinyaa, hivyo kudhihirisha vizuri zaidi nguvu kuu za Mungu.

kutoka katika “Sura ya 13” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Kazi Yangu itakapomalizika, Sitatafuta tena “msaada wa kifedha” kutoka kwa mwanadamu; badala yake, Nitatekeleza kazi Yangu ya asili, na Nitashusha “vitu vyote vya nyumba Yangu” kwa watu ili wavifurahie. Leo, kila mtu anajaribiwa katikati ya majaribu Yangu. Mkono wangu unapowasili kirasmi miongoni mwa wanadamu, watu hawatanitazama tena kwa macho ya kuvutiwa, lakini watanitendea na chuki, na wakati huu Nitaitoa mioyo yao mara moja ili wawe kielelezo. Ninauchunguza moyo wa mwanadamu chini ya “hadubini”—hakuna upendo wa kweli Kwangu hapo. Kwa miaka, watu wamekuwa wakinidanganya na kunipumbaza—inaonekana kuwa upande wa kushoto wa juu wa moyo na upande wa chini wa kushoto wa moyo zote zina sumu ya chuki Kwangu, na haishangazi, basi, kwamba Nina mtazamo kama huo kwao. Na bado wanabaki wasiojua kabisa kuhusu hili, wala hawalikiri. Niwaonyeshapo matokeo ya uchunguzi Wangu, bado hawaamki; ni kana kwamba, katika akili zao, haya yote ni mambo ya kale, na hayapaswi kutajwa tena leo. Hivyo, watu wanatazama tu “matokeo ya maabara” kwa kutojali. Wanarudisha karatasi na kutoweka kwa haraka. Zaidi ya hayo, wanasema mambo kama, “Haya si muhimu, hayana athari yoyote kwa afya yangu.” Wanatoa tabasamu ndogo ya dharau, na kisha kuna mtazamo unaotisha kidogo katika macho yao, kana kwamba wakidokeza kwamba Sipaswi kuwa mwadilifu sana, kwamba lazima Niwe mzembe zaidi. Ni kana kwamba ufunuo Wangu wa siri zao za ndani umevunja “sheria” za mwanadamu, na hivyo wanakuwa na chuki zaidi Kwangu. Hapo tu ndipo Mimi huona chanzo cha chuki ya watu. Hii ni kwa sababu Ninapotazama, damu yao inatiririka, na baada ya kupita kwa ateri katika miili yao inaingia moyoni, na ni wakati huu tu ndipo Mimi huwa na “ugunduzi” mpya. Ilhali watu hawafikiri chochote kuhusu hili. Wao ni wazembe kabisa, hawafikiri kile wanachopata au kupoteza, ambalo linatosha kuonyesha roho yao ya ibada “isiyo na ubinafsi.” Hawafikirii hali ya afya yao wenyewe, na “kurupuka hapa na pale” kwa ajili Yangu. Huu pia ni “uaminifu” wao na kile “kinachostahili kusifiwa” kuwahusu, kwa hivyo kwa mara nyingine Ninatuma barua ya “sifa” kwao, kwamba waweze kufurahishwa na hili. Lakini wanaposoma “barua” hii, mara moja wanahisi kukerwa kidogo, kwa maana yote wanayofanya kimekataliwa na barua Yangu ya kimya. Daima Nimewaelekeza watu watendavyo, ilhali inaonekana wanachukia sana maneno Yangu; hivyo, punde tu Ninapofungua mdomo Wangu, wanafumba na kubana macho yao na kufunika masikio yao kwa mikono yao. Hawanitazami kwa heshima kwa sababu ya upendo Wangu, lakini daima wamenichukia, kwa maana Nilionyesha upungufu wao, Nikifunua bidhaa zote wanazomiliki, na hivyo walipata hasara katika biashara yao,njia yao ya kupata riziki ikiwa imetoweka. Hivyo, chuki yao Kwangu inaongezeka baadaye.

kutoka katika “Sura ya 32” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Asili ya wanadamu ni kwamba hata chembe ya tumaini ikibaki hawatamwendea Mungu kupata msaada, lakini watachukua mbinu za kujitosheleza za kuendelea kudumu kwa kawaida. Hili ni kwa sababu asili ya wanadamu ni ya kujidai, na wao humdharau kila mtu. Kwa hivyo, Mungu alisema: “hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake.” Hili kweli ni la kusikitisha: Mungu aliwaumba wanadamu, lakini Anapokuja kwa ulimwengu wa wanadamu wao hutaka kumpinga, humfukuza kutoka kwa eneo lao, kana kwamba Yeye ni yatima mzururaji, au mtu asiye na uraia ulimwenguni. Hakuna mtu anayehisi kumpenda Mungu sana, hakuna mtu anayempenda kweli, hakuna mtu ambaye amekaribisha kuja kwake. Badala Yake, wanapoona kuja kwa Mungu, kufumba na kufumbua nyuso zao za furaha huwa na huzuni, kana kwamba dhoruba ya ghafula inakaribia, kana kwamba Mungu angeondoa raha ya familia zao, kana kwamba Mungu hakuwahi kamwe kuwabariki wanadamu, lakini badala yake Alikuwa Amewapa wanadamu taabu. Kwa hivyo, katika akili za wanadamu, Mungu si mwandani kwao, lakini Yule ambaye daima huwalaani; kwa hivyo, wanadamu hawamtilii maanani, hawamkaribishi, kila mara wao huwa hasimu Kwake, na hili halijawahi kubadilika kamwe. Kwa sababu wanadamu wana mambo haya katika mioyo yao, Mungu asema wanadamu hawana akili na ni waovu, na kwamba hata hisia ambazo wanadamu kwa kuwazia wamejizatiti nazo haziwezi kuonekana ndani yao. Wanadamu hawadhihirishi fikira yoyote kwa hisia za Mungu, lakini hutumia kinachoitwa “haki” kumshughulikia Mungu. Wanadamu wamekuwa hivi kwa miaka mingi na kwa sababu hii Mungu amesema tabia yao haijabadilika. Hili linaonyesha wazi kwamba hawana dutu linalozidi manyoya machache.

kutoka katika “Sura ya 14” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[1] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haikuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso na minyanyaso ya nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio ya kujirudia na matusi ya mwanadamu, kwa maneno ya mkato na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa, kwa kutokuwa na ufahamu, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo, mashambulizi na ukali. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa vidole elfu moja vinavyotikisika. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa.[2] Ni idadi gani ya miezi na jua, ni mara ngapi Amekabiliana na nyota, ni mara ngapi Ameondoka alfajiri na kurudi jioni, na kurushwarushwa na kugeuzwa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na “kuvunja” kwa mwanadamu, na “kumshughulikia” na “kumpogoa” mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo[3] wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu, mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na anajaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu kwa namna anavyomtendea Mungu ni wa “ujanja adimu,” na Mungu ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa kwa miguu ya makumi elfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama juu kabisa, kana kwamba angeweza kuwa “mfalme wa kasri,” kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili,[4] “kuendesha mahakama akiwa nyuma ya skrini,” kumfanya Mungu kuwa makini na mwenye kanuni “mwongozaji nyuma ya matukio,” ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu achukue nafasi ya “Mtawala wa Mwisho,” ni lazima Awe “kibaraka,”[5] bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayasemeki, sasa ana sifa gani ya kutaka hili au lile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake ipo wapi? Alivunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, ni muda mrefu toka ameuacha moyo wa Mungu katika vipande. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kiasi kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka;[6] moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote ni mwenye fitina na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila budi ila kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala vyovyote apendavyo.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (9)” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu amestahimili maumivu mengi sana, na kupata mashambulizi mengi sana. Ilhali hata leo, bado mwanadamu hayalegezi matakwa yake kwa Mungu kwa urahisi, bado anamchunguza Mungu, bado hana uvumilivu Naye, na anachofanya ni kumpatia “ushauri,” na “kumkosoa,” na “kumfundisha nidhamu” kana kwamba Mungu atapotoka njia, kwamba Mungu duniani ni hayawani na Hana busara, au Atafanya fujo, au kwamba Hatafanya kitu chochote cha maana. Mwanadamu siku zote huwa na mtazamo wa aina hii kwa Mungu. Inawezekanaje isimhuzunishe Mungu? Kwa kuwa mwili, Mungu amevumilia maumivu na mateso mengi; ni vibaya kiasi gani, kumfanya Mungu akubali mafundisho ya mwanadamu? Kuwasili kwake miongoni mwa wanadamu kumemvua uhuru wote, kama vile Amefungwa Kuzimu, na Amekubali “uchunguzi” wa mwanadamu bila upinzani hata kidogo. Hii sio aibu? Katika kuja miongoni mwa familia ya wanadamu wa kawaida, Yesu amepitia uonevu mkubwa. Na kinachoumiza zaidi ni kwamba Amekuja katika ulimwengu huu wa vumbi na kujinyenyekeza Mwenyewe katika hadhi ya chini kabisa, na Amechukua mwili wa kawaida kabisa. Kwa binadamu kuwa mwembamba, je, Mungu Mwenyezi hapati shida? Je, na hii yote si kwa ajili ya binadamu? Kuna wakati wowote ambapo alikuwa Anajifikiria Mwenyewe? Baada ya kukataliwa na kuuawa na Wayahudi, na kukejeliwa na kudhihakiwa na watu, Hajawahi kulalamika mbinguni au kupinga duniani. Leo, janga hili lenye umri wa milenia limetokea tena miongoni mwa watu hawa wanaofanana na Wayahudi. Je, hawafanyi dhambi ile ile? Nini kinamfanya mwanadamu kuwa na sifa ya kupokea ahadi za Mungu? Je, hampingi Mungu na kisha kukubali baraka Zake? Kwa nini haifikii haki, au kutafuta ukweli? Kwa nini havutiwi na kile ambacho Mungu anafanya? Haki yake iko wapi? Usawa wake uko wapi? Je, ana ujasiri wa kumwakilisha Mungu? Ziko wapi fahamu zake za haki? Ni kiasi gani ambacho kile kinachopendwa na mwanadamu ndicho kile kinachopendwa na Mungu? Mwanadamu hawezi kutambua tofauti muhimu,[7] siku zote anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe,[8] anakandamiza haki na ukweli, na anashikilia kutokuwa na haki wala usawa kwa kiwango kikubwa. Anafukuzia mbali mwanga na anarukaruka gizani. Wale wanaotafuta ukweli na haki badala yake wanafukuza mwanga, wale wanaomtafuta Mungu wanamkanyaga kwa miguu yao, na wanajipandisha angani. Mwanadamu hana tofauti na gaidi.[9] Sababu yake iko wapi? Nani anaweza kutofautisha kati ya jema na baya? Nani anaweza kushikilia haki? Nani yuko tayari kuteseka kwa ajili ya ukweli? Watu ni waovu na wana tabia za kishetani kabisa! Baada ya kumwangika Mungu msalabani wanapiga makofi na kufurahi, vilio vyao havikomi. Wako kama kuku na mbwa, wanashirikiana na kula njama, wameanzisha ufalme wao, udukuzi wao haujaachwa bila kusumbuliwa, wanafumba macho yao na kulia kwa maumivu makali zaidi na zaidi, wote wameungana pamoja, na hali ya kuvurugika imeenea kote, ni harakaharaka na hai, na wale ambao wanajishikamanisha kwa wengine kijinga wanazidi kuibuka, wote wakiwa wameshikilia majina “mashuhuri” ya mababu zao. Hawa mbwa na kuku wamemweka Mungu mbali na akili zao, na hawajawahi kuzingatia kabisa hali ya moyo wa Mungu. Si ajabu kwamba Mungu anasema mwanadamu ni kama mbwa au kuku, mbwa anayebweka anayewafanya mia wengine kutoa mlio mkali; kwa nia hii, kwa makelele mengi ameileta kazi ya Mungu katika siku ya leo, bila kujali kazi ya Mungu ni ya namna gani, bila kujali kuna haki, bila kujali Mungu ana nafasi Yake ya kuweka miguu Yake, bila kujali kesho itakuwaje, uduni wake, na hali yake ya kuwa mchafu. Mwanadamu hajawahi kufikiria juu ya mambo kiasi hicho, hajawahi kuhofia kesho, na amekusanya yale yote ambayo ni ya manufaa na ya thamani na kuyakumbatia, na bila kumwachia Mungu chochote isipokuwa mabaki na makombo.[10] Binadamu ni katili kiasi gani! Hana hisia hata kidogo kwa Mungu, na baada ya kuteketeza kila kitu cha Mungu, anamrusha Mungu nyuma yake na kuacha kujali kabisa kuhusu uwepo wake. Anamfurahia Mungu, halafu anampinga Mungu, na anamkanyagia chini ya miguu yake, wakati mdomoni mwake anamshukuru na kumsifu Mungu; anamwomba Mungu, na anamtegemea Mungu, wakati huo pia anamdanganya Mungu; “analiinua” jina la Mungu, na kuutazama uso wa Mungu, halafu pia bila haya na bila kuwa na aibu anakaa katika kiti cha enzi cha Mungu na “kuhukumu” “udhalimu” wa Mungu; kutoka katika kinywa chake yanatoka maneno haya “anapaswa kumshukuru Mungu,” na anatazama katika maneno ya Mungu, halafu katika moyo wake anavurumisha shutuma kwa Mungu; ni “mvumilivu” kwa Mungu halafu anamkandamiza Mungu, na kinywa chake kinasema ni “kwa ajili ya Mungu”; mikononi mwake ameshikilia vitu vya Mungu, na kinywani mwake anatafuna chakula ambacho Mungu amempatia, bado macho yake yanamtazama Mungu yakiwa hayana hisia kabisa, kana kwamba anatamani kummeza; anautazama ukweli lakini anasisitiza kuwa ni hila za Shetani; anatazama haki lakini analazimisha iwe kujikana nafsi; anatazama matendo ya mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni kile Mungu alicho; anatazama karama za asili za mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni ukweli; anatazama matendo ya Mungu lakini anasisitiza kuwa ni kiburi na majivuno, majigambo na haki binafsi; mwanadamu anapomwangalia Mungu anasisitiza kumpachika uanadamu, na anajitahidi sana kumweka katika kiti cha kiumbe aliyeumbwa akishirikiana na Shetani; anajua kweli kabisa ni matamshi ya Mungu, bado atasema si kitu chochote zaidi ya maandiko ya mwanadamu; anajua kabisa kwamba Roho anatambulika katika mwili, Mungu anakuwa mwili, lakini anasema mwili huu ni uzao wa Shetani; anajua kikamilifu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na hajionyeshi, lakini anasema kwamba Shetani ameaibishwa na Mungu ameshinda. Uzuri wa bure ulioje! Mwanadamu hata hafai kuwa mbwa mlinzi! Hawezi kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, na hata anachanganya kwa makusudi nyeusi ndani ya nyeupe. Je, nguvu za mwanadamu na husuru ya mwanadamu vinaweza kustahimili siku ya ukombozi wa Mungu? Baada ya kumpinga Mungu kwa kukusudia, mwanadamu hakuweza kujali sana, au hata kwenda mbali sana na kumuua, asimpatie Mungu nafasi ya kujionyesha Mwenyewe. Haki iko wapi? Upendo uko wapi? Anakaa kando ya Mungu na kumsukuma Mungu apige magoti ili Aombe msamaha, kutii mipango yake yote, kuridhia hila zake zote, na anamfanya Mungu kuchukua ishara Zake zote kutoka Kwake, la sivyo anaghadhibishwa[11] na kupandwa na hasira. Inawezekanaje Mungu asiwe na maumivu katika ushawishi huo wa giza, ambao unachanganya nyeusi kuwa nyeupe? Angewezaje kukosa kuwa na wasiwasi? Kwa nini inasemwa kwamba Mungu alipoanza kazi yake ya hivi karibuni kabisa, ilikuwa kama alfajiri ya mwanzo mpya? Matendo ya mwanadamu “yana utajiri,” ni “chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima” bila kukoma “yanajaza tena” shamba la moyo wa mwanadamu, wakati “chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima” ya mwanadamu “inashindana” na Mungu bila haya;[12] wawili hawa hawapatani, na anawapa watu vitu kwa niaba ya Mungu bila hofu ya kuadhibiwa wala kuumia, wakati mwanadamu anashirikiana naye bila kujali hatari iliyopo. Na kwa athari gani? Anamtupilia mbali Mungu upande mmoja, na kumweka mbali sana, ambapo watu hawatamzingatia, akiogopa sana kwamba Atavuta usikivu wake, na anaogopa sana kwamba chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima ya Mungu itamteka mwanadamu, na kumpata mwanadamu. Hivyo, baada ya kupitia uzoefu wa miaka mingi wa masuala ya kidunia, anakula njama dhidi ya Mungu, na hata anamfanya Mungu kuwa mlengwa wa “adhabu.” Ni kana kwamba Mungu amekuwa gogo machoni mwake, na anatamani kumnyakua Mungu na kumweka motoni ili Atakaswe na kusafishwa. Mwanadamu anapoona mahangaiko ya Mungu, anapiga kifua chake na kucheka, anacheza kwa furaha, na kusema kwamba Mungu pia Amewekwa motoni, na anasema kwamba atausafisha uchafu wa Mungu, kana kwamba hili ni la urazini na lina maana, kana kwamba hizi tu ndizo njia za haki na zenye mantiki za Mbinguni. Tabia hii ya fujo ya mwanadamu inaonekana kuwa ni ya makusudi na ya kutofahamu. Mwanadamu anafichua uso wake mbaya na roho yake mbaya, vilevile sura ya kusikitisha ya ombaomba; baada ya kufanya ghasia sana, anavaa sura ya kuhurumiwa na kuomba msamaha wa Mbingu, akifanana na udongo wa kufinyangwa. Mwanadamu siku zote hutenda kwa namna asiyotarajiwa, siku zote “anamwendesha duma kuwatisha wengine,”[d] siku zote yeye huigiza, hajali hata kidogo moyo wa Mungu, wala halinganishi hadhi yake mwenyewe. Kimyakimya anampinga Mungu, kana kwamba Mungu amemkosea, na Hapaswi kumtendea hivyo, na kana kwamba Mbingu haina macho na inafanya kwa makusudi mambo kuwa magumu kwake. Hivyo mwanadamu anapanga njama za siri, na hajali matakwa ya Mungu hata kidogo, anatazama kwa macho ya mnyama mkali, anatazama kwa hasira kila kitu Anachokifanya Mungu, hafikirii kwamba yeye ni adui ya Mungu, na ana matumaini kwamba siku itakuja ambapo Mungu atautawanya umande na kuviweka vitu wazi, na kumwokoa kutoka katika “kinywa cha duma” na kulipiza kisasa kwa niaba yake. Hata leo, watu bado hawafikiri kwamba wanatekeleza jukumu la kumpinga Mungu, jukumu ambalo limefanywa kwa enzi nyingi sana, wangewezaje kujua kwamba, katika yote wanayofanya, wamepotoka tangu zamani sana, kwamba yote waliyoyaelewa yamemezwa na bahari zamani sana.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (9)” katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, “kuingia” kwa mwanadamu[13] pia kumefikia kilele chake. Mungu amejishusha kwa kadiri Anavyoweza, na kamwe Hajawahi kuwalalamikia wanadamu au vitu vyote katika ulimwengu. Mwanadamu, wakati ule ule, anasimama juu ya kichwa cha Mungu, akimnyanyasa hadi kilele; yote yamefikia kilele chake, ni wakati wa siku ambapo haki inaonekana. Kwa nini uendelee kuacha huzuni iifunike nchi, na giza kuwavaa watu wote? Mungu ameangalia kwa miaka elfu kadhaa—kwa makumi ya maelfu ya miaka, hata—na uvumilivu Wake umekwisha kufikia kikomo chake. Amekuwa akiangalia kila hatua za wanadamu, Amekuwa akiangalia kwa makini jinsi udhalimu wa mwanadamu utafanya fujo, na bado mwanadamu, ambaye amekuwa wa kutojali kwa muda mrefu, hahisi chochote. Na ni nani aliyewahi kuangalia kwa makini matendo ya Mungu? Nani aliyewahi kuinua macho yake na kutazama mbali sana? Nani aliyewahi kusikiliza kwa makini? Nani aliyewahi kuwa mikononi mwa Mwenyezi? Watu wote wanakerwa na hofu za kubuni[14]. Je, kuna faida gani kwa rundo la nyasi kavu na majani makavu? Kitu pekee wanachoweza kufanya ni kumtesa Mungu aliye hai, Aliyepata mwili hadi kifo. Ingawa wao ni mafungu tu ya nyasi kavu na majani makavu, bado kuna kitu kimoja ambacho wao hufanya “bora zaidi”:[15] kumtesa Mungu hadi kifo Akiwa hai na kisha kulia kwamba “hilo hufurahisha mioyo ya watu.” Kikundi cha jeshi lisilofaa kabisa! La ajabu, katikati ya mkondo usiokwisha wa watu, wao hulenga uangalifu wao juu ya Mungu, wakimzunguka Yeye na zingio lisilopenyeka. Hamasa yao daima ikiwaka moto zaidi,[16] wamemzunguka Mungu katika vikundi, ili Asiweze kusonga hata kidogo. Katika mikono yao, wanashikilia kila aina ya silaha, na kumtazama Mungu kana kwamba wanamwangalia adui, macho yao yakiwa yamejaa hasira; wana hamu ya “kumshambulia Mungu kwa nguvu.” Inafaidi kweli: Kwa nini mwanadamu na Mungu wamekuwa maadui wasioweza kupatanishwa? Inawezekana kwamba kuna chuki ya muda mrefu sana kati ya Mungu wa upendo sana na mwanadamu? Inawezekana kwamba matendo ya Mungu hayana faida kwa mwanadamu? Je, hayo humdhuru mwanadamu? Mtu hulenga jicho la hasira lisiloyumba juu ya Mungu, akiogopa sana kwamba Atapasua zingio la mwanadamu, Arudi mpaka mbingu ya tatu, na mara nyingine tena Amtupe mwanadamu ndani ya gereza. Mwanadamu anajihadhari na Mungu, yeye ni mwenye wasiwasi, na hufurukuta toka upande mmoja hadi upande mwingine wa ardhi kwa mbali, akishikilia “bombomu” ambayo inamlenga Mungu kati ya wanadamu. Ni kana kwamba, Mungu akijitikisa kidogo tu, mwanadamu atafuta kila kitu Chake—mwili Wake wote na yote Anayovaa—bila kuacha kitu chochote. Uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu hauwezi kurekebishwa. Mungu haeleweki kwa mwanadamu; mwanadamu, wakati ule ule, huyafunga macho yake kwa makusudi na kuchezacheza, asiyetaka kabisa kuona kuwepo Kwangu, na kutosamehe hukumu Yangu. Hivyo, wakati mtu hatarajii, Mimi huondoka kimya kimya, na Sitaweza tena kulinganisha nani aliye juu na nani aliye chini na mwanadamu. Wanadamu ni “wanyama” wa chini zaidi kuliko wote na Sitamani kumsikiliza tena. Kwa muda mrefu Nimerudisha neema Yangu yote mahali ambapo Mimi hukaa kwa amani; kwa kuwa mwanadamu ni mkaidi sana, ana sababu gani kufurahia zaidi neema Yangu ya thamani mno?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Ingawa kazi ya Mungu ni yenye ukwasi na maridhawa, kuingia kwa mwanadamu kuna upungufu sana. Kwa “shughuli” ya pamoja kati ya mwanadamu na Mungu, karibu yote ni kazi ya Mungu; kuhusu kiasi gani mwanadamu ameingia, hana ushahidi wa chochote alichopata Mwanadamu, ambaye amechakaa sana na ni kipofu, hata hutathmini nguvu zake dhidi ya Mungu wa leo na “silaha za kale” mikononi mwake. Hawa “sokwe wa kale” huweza kutembea wima kwa shida, na hawaoni aibu katika miili yao iliyo “uchi.” Ni nini kinawastahilisha kutathmini kazi ya Mungu? Macho ya wengi wa sokwe hawa wa miguu minne hujaa ghadhabu, nao hujipambanisha na Mungu kwa silaha za kale za mawe mikononi mwao, wakijaribu kuanzisha mashindano ya sokwe watu ambao dunia haijawahi kuwaona kamwe hapo awali, kuwa na mashindano ya siku za mwisho kati ya sokwe watu na Mungu ambayo yatakuwa maarufu duniani kote. Wengi wa sokwe watu hawa walio nusu wima, zaidi ya hayo, hufurikwa na ridhaa. Nywele zikiwa zimefunika nyuso zao zilizofungamana, wamejaa nia ya kuua na huinua miguu yao ya mbele. Bado hawajageuka kwa ukamilifu kuwa mtu wa kisasa, kwa hiyo wakati mwingine wao husimama wima, na wakati mwingine wao hutambaa, shanga za jasho zikifunika paji la nyuso zao kama matone ya umande yaliyo karibu karibu, hamu yao ni dhahiri. Ukimwangalia sokwe mtu, wa asili, rafiki yake, akiwa amesimama kwa miguu yote minne, miguu yake minne ikiwa mikubwa na ya mwendo wa polepole, inayoweza kukwepa mapigo kwa shida na bila nguvu ya kupigana, anajizuia kwa shida. Kufumba na kufumbua—kabla ya kuwa na wakati wa kuona nini kilichotokea—“shujaa” katika ulingo huanguka chini ghafula, miguu ikiwa hewani. Miguu hiyo, iliyopandwa kwa makosa juu ya ardhi kwa miaka yote hiyo, ghafula imegeuzwa juu chini, na sokwe mtu huyo hana tena hamu ya kupinga. Kuanzia wakati huu kuendelea, sokwe mtu kati ya sokwe watu wa kale zaidi anaondolewa kutoka kwenye uso wa dunia—ni la “kuhuzunisha” kweli. Huyu sokwe mtu wa kale alifikia mwisho wa ghafla. Kwa nini alikuwa na haraka kutoka katika ulimwengu wa ajabu wa mwanadamu mapema hivyo? Kwa nini hakuzungumzia hatua inayofuata ya mkakati na wenzake? Inasikitisha kwamba aliuaga ulimwengu bila kuacha siri ya kutathmini nguvu za mtu dhidi ya Mungu! Haikuwa busara kwa sokwe mtu huyo mzee kufa bila kunong’ona, kuondoka bila kupitisha “utamaduni wa kale na sanaa” kwa dhuria zake. Hakukuwa na wakati wa kuwaita wale walio karibu naye ubavuni mwake kuwaambia juu ya upendo wake, hakuacha ujumbe juu ya kibao cha mawe cha kuandikia, hakutambua jua la mbingu, wala hakusema chochote juu ya shida zake zisizoweza kuzungumziwa. Alipokuwa akipumua pumzi yake ya mwisho, hakuwaita wazao wake ubavuni pa mwili wake uliokuwa ukifa kuwaambia “msiingie ndani ya ulingo ili kumpinga Mungu” kabla ya kufumba macho yake, miguu minne migumu ikijitokeza juu daima kama matawi ya mti ikielekeza angani. Ingeonekana alikufa kifo cha uchungu.... Ghafla, kicheko cha kunguruma kinafoka kutoka chini ya ulingo; mmoja wa sokwe watu aliye nusu wima aliyejizuzua; akiwa ameshika “kigongo cha mawe” cha kuwinda paa au wanyama wengine wa mwitu kilichoendelea zaidi kuliko kile cha sokwe mtu wa kale, anaruka ndani ya ulingo, akiwa amejawa na hasira, akiwa na mpango alioufikiria kwa makini katika akili yake.[17] Ni kana kwamba amefanya kitu chenye kustahili. Kwa kutumia “nguvu” ya kigongo chake cha mawe anafanikiwa kusimama wima kwa “dakika tatu.” Ajabu jinsi “nguvu” ya huu “mguu” wa tatu ilivyo kuu! Alimshikilia sokwe mtu mkubwa, goigoi, mpumbavu aliye nusu wima akisimama kwa dakika tatu—si ajabu sokwe mtu huyu mzee wa kuheshimiwa[18] ni jeuri sana. Kwa kweli, kifaa cha jiwe cha kale “kilikuwa kizuri kama sifa zake”: Kuna mpini wa kisu, makali, na ncha, dosari pekee ni ukosefu wa mng’aro kuelekea ukingo—jinsi hilo linavyosikitisha. Tazama tena “shujaa mdogo” wa nyakati za kale, aliyesimama ulingoni akiwaangalia wale walio chini na kuwakazia macho kwa dharau, kana kwamba wao ni wadhaifu walio duni, na yeye ni shujaa hodari. Katika moyo wake, anawachukia kwa siri wale walio mbele ya jukwaa. “Nchi iko taabani na kila mmoja wetu anawajibika, kwa nini mnaepa? Inawezekana kuwa ninyi mnaona nchi inakabiliwa na maangamizi, lakini hamshiriki katika vita vikali? Nchi inakaribia kuangamizwa—kwa nini ninyi sio wa kwanza kushughulika, na wa mwisho kujifurahisha? Mnawezaje kusimama na kuiangalia nchi ikianguka na watu wake wakianguka katika uozo? Je, mko tayari kubeba aibu ya kutiishwa kwa taifa? Kikundi cha vinyangarika kweli!” Anapofikiria hili, ghasia zinatokea mbele ya jukwaa na macho yake yanakasirishwa hata zaidi, kana kwamba karibu kutupa[19] miale. Ana hamu ya Mungu kushindwa kabla ya vita, akiwa tayari kufanya lolote kumuua Mungu ili awafurahishe watu. Hajui hata kidogo kwamba, ingawa kifaa chake cha jiwe kinaweza kuwa cha sifa inayostahili, hakiwezi kamwe kumchokoza Mungu. Kabla hajapata wakati wa kujikinga, kabla hajapata wakati wa kulala chini na kusimama, anayumba nyuma na mbele, uwezo wa kuona umepotea kutoka kwa macho yote. Anaanguka chini ghafula kwa babu yake wa zamani na hainuki tena; akimshikilia kwa nguvu sokwe mtu wa kale, halii tena, na anakubali udhalili wake, hana tena tamaa yoyote ya kupinga. Sokwe watu hao wawili maskini wanakufa mbele ya ulingo. Ni jambo la kusikitisha kwamba mababu za wanadamu, ambao wamenusurika hadi siku hii, walikufa kijinga katika siku ambayo Jua la haki lilionekana! Ni upumbavu ulioje kuwa wameiacha baraka kubwa sana kama hiyo kuwapita—kwamba, katika siku ya baraka yao, sokwe watu ambao wamengoja kwa maelfu ya miaka wamepeleka baraka Kuzimu ili “kufurahia” na mfalme wa pepo! Kwa nini wasiweke baraka hizi katika ulimwengu wa walio hai ili wafurahie na wana na binti zao? Wanatafuta tu shida! Huku ni kupoteza tu kwamba, kwa ajili ya hadhi ndogo, sifa, na ubatili, wanateseka kwa kuchinjwa, kung’ang’ana kuwa wa kwanza kufungua milango ya jahanamu na kuwa wana wake. Gharama kama hiyo si lazima. Inasikitisha mababu wa zamani kama hao, waliokuwa “wamejawa sana na roho ya kitaifa,” wangekuwa “wakali sana kwao wenyewe lakini wenye kuwavumilia wengine sana,” wakijifungia jahanamu, na kuwafungia wale dhaifu walio duni nje. Ni wapi ambako “wawakilishi wa watu” kama hawa wanaweza kupatikana? Kwa ajili ya “ustawi wa uzao wao” na “maisha ya amani ya vizazi vijavyo,” hawamruhusu Mungu kuingilia kati, na hivyo hawatilii maanani maisha yao wenyewe. Bila kujizuia, wanajitolea kwa “kusudi la kitaifa,” kuingia Kuzimu bila kusema lolote. Utaifa kama huo unaweza kupatikana wapi? Wakipigana na Mungu, hawaogopi kifo, wala kumwaga damu, seuze kuwa na wasiwasi kuhusu kesho. Wanakwenda tu kwenye uwanja wa vita. Inasikitisha kwamba kitu pekee wanachopata kwa “roho yao ya kujitolea” ni majuto ya milele, na kuteketezwa na moto wa kuzimu uwakao milele!

kutoka katika “Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Nimetumia siku nyingi kuwa na mwanadamu, Nimeishi duniani pamoja na mwanadamu, na Sijawahi kutaka vitu zaidi kutoka kwa mwanadamu, Ninamwongoza tu mwanadamu kusonga mbele, Sifanyi chochote bali kumwongoza mwanadamu, na kwa ajili ya hatima ya binadamu, bila kuchoka Nafanya kazi ya kupangilia. Nani ambaye amewahi kuelewa mapenzi ya Baba wa mbinguni? Nani amewahi kusafiri kati ya mbingu na dunia? Sitamani kuishi tena na mwanadamu katika “uzee” wake, kwani mwanadamu ni “wa mtindo wa zamani sana,” hajui chochote, kitu pekee anachojua ni kula na kuvimbiwa kwenye sherehe Niliyoandaa, amejitenga na yote—hafikirii suala jingine lolote lile. Binadamu anateseka sana, makelele, huzuni, na hatari miongoni mwa wanadamu ni kubwa sana, na hivyo Natamani nisiwashirikishe matunda ya thamani ya kupata ushindi wakati wa siku za mwisho. Acha mwanadamu afurahie baraka tele ambazo ametengeneza mwenyewe, maana mwanadamu hanikaribishi—kwa nini Nimshurutishe binadamu kulazimisha tabasamu? Kila pembe ya dunia haina joto, hakuna hata chembe ya chemchemi katika ardhi yote ya nchi, maana, hana joto hata kidogo kama mnyama aishiye majini, ni kama maiti, na hata damu inayopita katika mishipa yake ni kama barafu iliyoganda inayofanya moyo kuwa baridi. Wema upo wapi? Mwanadamu alimsulubisha Mungu msalabani bila sababu yoyote, na baadaye hakuhisi wasiwasi wowote. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na majuto, na madikteta hawa makatili bado wanapanga “kumkamata Akiwa hai”[20] Mwana wa Adamu kwa mara nyingine na kumleta mbele ya kikosi cha kufyatua risasi, kukomesha chuki ndani ya mioyo yao. Kuna faida gani Kwangu, kubaki katika nchi hii ya hatari? Ikiwa Nitabaki, kitu pekee Nitakachomletea mwanadamu ni mgogoro na fujo, na hakutakuwa na mwisho wa shida, maana Sijawahi kumpatia mwanadamu amani, ni vita tu. Siku za mwisho za binadamu lazima zijae vita, na hatima ya mwanadamu lazima ipinduliwe katikati ya vurugu na migogoro. Na Sipo tayari kushiriki katika “furaha” ya vita, Sitaunga mkono umwagaji wa damu na mwanadamu kujitoa mhanga, maana kukataliwa na mwanadamu kumenipeleka katika hali ya kukata tamaa, na Sina moyo wa kuangalia vita vya mwanadamu—hebu mwanadamu apigane kuuridhisha moyo wake, Natamani kupumzika, Nataka kulala, acha mapepo wawe washirika wa binadamu wakati wa siku zao za mwisho!

kutoka katika “Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, tamaa ya[e] hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na watu daima hawawezi kuondoa majaribu haya kutoka kwa Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wanaamini: “Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.” Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu, mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni mibaya kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu vilevile. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza. Je, si fikira na mitazamo yenu ya sasa iko hivi tu? “Kwa kuwa ninaamini katika Mungu ninapaswa tu kumiminiwa baraka na inapaswa kuhakikishwa kwamba hadhi yangu kamwe haitelezi na kwamba iko juu kuliko ile ya wasioamini.” Hamjakuwa mkihodhi mtazamo wa aina hiyo ndani yenu kwa mwaka moja au miaka miwili tu; umekuwa hapo kwa miaka mingi. Mtazamo wenu wa shughuli umekua sana. Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. Watu hawajawahi kuweka kando tamaa yao ya starehe.

kutoka katika “Mbona Huko Tayari Kuwa Foili?” katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Imani ya watu katika Mungu hutafuta kumfanya Mungu kuwapa hatima inayofaa, kuwapa neema yote chini ya jua, kumfanya Mungu mtumishi wao, kumfanya Mungu adumishe uhusiano wa amani, wa kirafiki pamoja nao, na ili kusiwe na mgogoro wowote kati yao. Yaani, imani yao kwa Mungu inahitaji Mungu kutoa ahadi ya kutimiza mahitaji yao yote, kuwapa chochote wanachoomba, kama ambavyo inasema katika Biblia “Nitazisikiliza sala zenu zote.” Wanahitaji Mungu kutomhukumu mtu yeyote au kushughulika na mtu yeyote, kwa kuwa Mungu daima ni Mwokozi Yesu mkarimu, ambaye huwa na uhusiano mzuri na watu wakati wote na mahali pote. Wanavyoamini ni hivi: Watu daima humwomba Mungu vitu bila haya, na Mungu huwapa kila kitu kwa upofu, kama wao ni waasi au watiifu. Wao daima wanataka “malipo ya deni” kutoka kwa Mungu, na Mungu, lazima Alipe “deni Lake” bila upinzani wowote, na “kulipa” mara dufu, kama Mungu amepata chochote kutoka kwao au la. Anaweza tu kuwa chini yao; Hawezi kuwapanga watu kiholela, sembuse Hawezi kuwafunulia watu hekima Yake ya kale ya siri na tabia ya haki kama Anavyotaka, bila ruhusa yao. Wao huungama tu dhambi zao kwa Mungu na Mungu huwasamehe tu, na Hawezi kuchoshwa na hilo, na hii inaendelea milele. Wanamwamuru Mungu tu na Yeye anatii tu, kama ilivyonakiliwa katika Biblia kwamba Mungu hakuja kutumikiwa na mwanadamu, ila kutumikia, na kwamba Alikuja kuwa mtumishi wa mwanadamu. Je, si siku zote mmeamini kwa njia hii? Wakati ambapo hamuwezi kupata chochote kutoka kwa Mungu basi mnataka kukimbia. Na wakati ambapo hamuelewi kitu mnapata hasira, na hata kwenda mbali ili kutoa aina zote za matusi. Hamuwezi tu kumruhusu Mungu Mwenyewe kuonyesha kikamilifu hekima na shani Yake, lakini badala yake unataka tu kufurahia urahisi wa muda na faraja. Hadi sasa, mtazamo wenu katika imani yenu kwa Mungu umekuwa sawa na maoni ya zamani. Mungu akiwaonyesha utukufu mdogo tu mnakosa furaha; je, mnaona sasa jinsi kimo chenu kilivyo? Msifikiri kuwa ninyi nyote ni waaminifu kwa Mungu wakati kwa kweli maoni yenu ya zamani hayajabadilika. Wakati ambapo hakuna chochote kibaya kinachokuangukia, unafikiri kwamba kila kitu kinaelekea kwa urahisi na unampenda Mungu kwa vilele vya juu zaidi. Lakini kitu kidogo kinapokukumba, unakushuka kuzimuni. Je, hii ni wewe kuwa mwaminifu kwa Mungu?

kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumsikiza na aidha nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za dawa ovu na uchawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu alitaka kutoka Kwangu, kisha binadamu alitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata.

kutoka katika “Unajua Nini Kuhusu Imani?” katika Neno Laonekana katika Mwili

25. Leo, kile ambacho mmepata kuelewa ni cha juu zaidi kuliko mtu yeyote kote katika historia ambaye hakufanywa mkamilifu. Iwe ni ufahamu wenu wa majaribio au imani katika Mungu, yote ni ya juu zaidi kuliko ya muumini yeyote katika Mungu. Mambo mnayoyafahamu ni yale mnayokuja kujua kabla ya ninyi kupitia majaribio ya mazingira, lakini kimo chenu halisi hakipatani nayo. Kile mnachojua ni cha juu zaidi kuliko kile mnachotia katika vitendo. Ingawa mnasema kwamba watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumpenda Mungu, na hawapaswi kupania baraka bali kuyaridhisha tu mapenzi ya Mungu, kinachoonekana katika maisha yenu ni tofauti kabisa na hili, na kimewekwa mawaa kabisa. Watu wengi huamini katika Mungu kwa ajili ya amani na manufaa mengine. Isipokuwa kwa manufaa yako, wewe huamini katika Mungu, na ikiwa huwezi kupokea neema za Mungu, wewe huanza kununa. Hiki kingekuwaje kimo chako halisi? Inapofikia matukio ya familia yasiyoepukika (watoto kuwa wagonjwa, mume kwenda hospitalini, mazao mabaya ya mimea, kuteswa kwa watu wa familia, na kadhalika), huwezi hata kufaulu katika mambo haya ambayo hufanyika mara kwa mara katika maisha ya kila siku. Wakati ambapo mambo hayo hufanyika, wewe huingia katika hofu kubwa, hujui la kufanya—na wakati mwingi, wewe hulalamika kuhusu Mungu. Wewe hulalamika kwamba maneno ya Mungu yalikudanganya, kwamba kazi ya Mungu imekuvuruga wewe. Je, hamna mawazo kama haya? Unadhani mambo kama haya hufanyika miongoni mwenu mara chache tu? Mnatumia kila siku kuishi katikati ya matukio kama haya. Hamfikirii hata kidogo sana kuhusu mafanikio ya imani yenu katika Mungu, na namna ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Kimo chenu halisi ni kidogo sana, hata kidogo zaidi kuliko cha kifaranga mdogo. Wakati ambapo biashara ya waume zenu hupoteza pesa ninyi hulalamika kuhusu Mungu, wakati ambapo ninyi hujikuta katika mazingira yasiyo na ulinzi wa Mungu ninyi bado hulalamika kuhusu Mungu, ninyi hulalamika hata wakati ambapo mmoja wa vifaranga wenu hufa au ng’ombe mzee ndani ya zizi anapougua, ninyi hulalamika kama ni wakati wa wana wenu kuanzisha familia lakini familia yenu haina pesa za kutosha, na wakati ambapo wafanyakazi wa kanisa hula milo kadhaa nyumbani kwako lakini kanisa halikulipi au hakuna anayekutumia mboga zozote, wewe hulalamika pia. Tumbo lako limeshindiliwa pomoni na malalamiko, na wakati mwingine wewe huendi katika mikutano au kula na kunywa maneno ya Mungu kwa sababu ya hili, wewe huelekea kuwa mbaya kwa muda mrefu sana. Hakuna chochote kinachokufanyikia leo hii kilicho na uhusiano wowote na matazamio au majaliwa yako; mambo haya yangefanyika pia ikiwa hungeamini katika Mungu, ilhali leo hii unampitishia Mungu wajibu wa haya mambo, na kusisitiza kusema kwamba Mungu amekuondosha wewe. Na kuhusu imani yako katika Mungu, je, umeyatoa maisha yako kwa kweli? Mngepitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, hakuna hata mmoja miongoni mwenu anayemfuata Mungu leo hii angeweza kusimama imara, nyote mngeanguka chini. Na kunayo, kawaida kabisa, tofauti kubwa kati ya ninyi na Petro. Leo, kama nusu ya mali yenu ingetwaliwa mngethubutu kukana kuwepo kwa Mungu; kama mtoto wenu wa kiume au wa kike angechukuliwa kutoka kwenu, mngekimbia barabarani mkilalamika vikali; kama maisha yako yangegonga mwamba, ungejaribu kuanza kujadiliana mada hiyo na Mungu, ukiuliza kwa nini Nilisema maneno mengi sana hapo mwanzo kukutisha wewe. Hakuna kitu chochote ambacho hamngethubutu kufanya katika nyakati kama hizi. Hili linaonyesha kwamba hamjaona kwa kweli, na hamna kimo cha kweli. Hivyo, majaribio yaliyo ndani yenu ni makubwa mno, kwani ninyi huelewa mengi sana, lakini mnachojua kweli sio hata sehemu moja kwa elfu ya kile mnachofahamu. Msikomee kwa ufahamu na maarifa pekee; mngeona vyema kiasi gani mnachoweza kutia katika vitendo kwa kweli, kiasi gani cha jasho la kazi yenu ngumu imegeuzwa kuwa kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na katika matendo mangapi yenu mmetambua azimio lenu wenyewe. Unapaswa kuchukua kimo chako na kutenda kwa dhati. Katika imani yako kwa Mungu, hupaswi tu kujaribu kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati kwa ajili ya yeyote—kama unaweza kupata au la hutegemea ufuatiliaji wako mwenyewe.

kutoka katika “Utendaji (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

26. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.

kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

27. Wakati wowote hatima inatajwa, muichukulie kwa uzito maalumu; nyinyi nyote ni mahususi hasa kuhusu jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye kuwa na hatima nzuri. Naweza kutambua hamu yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Kabisa hamtaki miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kuishi kwa uhuru zaidi na kwa urahisi. Hivyo mnahisi wasiwasi hasa wakati wowote hatima inatajwa, mkihofia kwa undani kwamba msipokuwa waangalifu vya kutosha, mnaweza kosea Mungu na kuwa chini ya adhabu inayostahili. Hamjasita kufanya maafikiano kwa ajili ya hatima zenu, na wengi wenu ambao wakati mmoja walikuwa wa kuzunguka na wapuuzi hata kwa ghafla wamegeuka hususa wapole na wa dhati; unyofu wenu hata una mzizimo. Pasipo kutilia maanani, nyinyi nyote mna mioyo “minyoofu”, na kutoka mwanzo hadi mwisho mmejifungua wazi Kwangu bila kuficha siri zozote katika mioyo yenu, yawe lawama, udanganyifu, au ibada. Kwa jumla, “mmekiri” kwa uwazi Kwangu yale mambo muhimu katika pahali pa siri yenye kina kwenu. Mambo kama yalivyo, Sijawahi kuepuka mambo kama haya, kwa sababu yamekuwa ya kawaida Kwangu. Afadhali muingie katika bahari la moto kwa hatima yenu ya mwisho kuliko kupoteza mlia mmoja wa nywele ili kupata kibali cha Mungu. Sio kwamba Ninakuwa wa kulazimishia imani kwenu; ni kwamba mioyo yenu ya ibada ni pungufu hasa kwa kukabiliana na kila kitu Ninachofanya. Hamuwezi kuelewa Ninachomaanisha, hivyo basi acheni Niwatolee maelezo rahisi: Mnachohitaji si ukweli na maisha; si kanuni za jinsi ya kutenda, na hasa siyo kazi Yangu yenye kujitahidi. Yote mnayohitaji ni yale ambayo mnamiliki katika mwili—mali, hadhi, familia, ndoa, nk. Ninyi mnatupilia mbali kabisa maneno na kazi Yangu, hivyo Naweza kujumlisha imani yako kwa neno moja: shingo upande. Mtafanya lolote ili kutimiza mambo ambayo bila shaka mmejitolea, lakini Nimegundua kwamba hampuuzi kila kitu kwa ajili ya mambo ya imani yenu katika Mungu. Badala yake, nyinyi ni waaminifu tu kiasi, na kiasi. Hiyo ndiyo sababu Nasema kwamba wale wanaokosa moyo wa usafi mkubwa ni washinde katika imani yao katika Mungu. Fikiria kwa uangalifu—je, kunao wengi washinde miongoni mwenu?

Mnapaswa kujua kwamba mafanikio katika kumwamini Mungu yanatimizwa kwa sababu ya matendo ya watu wenyewe; wakati watu hawafanikiwi lakini badala yake wanashindwa, hiyo pia ni kwa sababu ya matendo yao wenyewe, sio matokeo ya vipengele vingine. Ninaamini kwamba mngefanya kitu chochote kitachukua ili kupata kitu kufanyika ambacho ni kigumu zaidi na kinachohitaji mateso zaidi kuliko kumwamini Mungu, na kwamba mngekichukulia kwa makini sana. Hamngetaka hata kufanya makosa yoyote; hizi ni aina za juhudi zisizolegea ambazo nyote mmeweka katika maisha yenu wenyewe. Nyinyi hata mna uwezo wa kunidanganya Mimi katika mwili chini ya hali ambazo hamuwezi kudanganya yeyote wa familia yenu wenyewe. Hii ni tabia yenu thabiti na kanuni ambayo mnatumia katika maisha yenu. Je, si bado mnaendeleza picha ya uongo ili kunidanganya Mimi, kwa ajili ya hatima yenu, na kuwa na hatima nzuri na ya furaha? Nafahamu kwamba ibada yenu na unyofu wenu ni wa muda tu; je, matamanio yenu na gharama mnayolipa ni ya sasa tu na si ya baadaye? Mnataka tu kutumia nguvu moja ya mwisho ili kupata hatima nzuri. Azma yenu ni kubadilisha tu; siyo ili msiwe wenye deni kwa ukweli, na ni hasa msinilipe kwa ajili ya gharama Niliyolipa. Kwa neno, mko tu tayari kutumia ujanja wenu, lakini hamtaki kuipigania. Je, si haya ni matakwa yenu ya dhati? Sio lazima mjifiche, na hata zaidi, sio lazima mpige mbongo zenu juu ya hatima yenu hadi pale ambapo hamuwezi kula au kulala. Je, si ni kweli kwamba hatima yenu itakuwa imeamuliwa hatimaye?

kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

28. Kila siku, fikira na matendo ya kila mmoja yanachunguzwa na Yeye na, katika wakati uo huo, wamo katika matayarisho ya siku zao zinazofuata. Hii ni njia ambayo lazima kila mtu aliye hai aipitie na ambayo Nimeamulia kabla kila mmoja. Hakuna anayeweza kuepuka hili na hakuna atakayepata upendeleo. Nimezungumza maneno yasiyohesabika na zaidi ya yote Nimefanya kazi kubwa mno. Kila siku, Ninatazama vile kila mwanadamu kiasili anafanya yote ambayo anafaa kufanya kulingana na asili yake na vile inavyoendelea. Bila kujua, wengi tayari wamo katika “njia sahihi”, ambayo Niliiweka kwa ufunuo wa mwanadamu wa kila aina. Tayari Nimemweka kila aina ya mwanadamu katika mazingira tofauti tofauti, na katika sehemu zao, kila mmoja amekuwa akionyesha tabia zake za asili. Hakuna mtu wa kuwafunga, hakuna mtu wa kuwatongoza. Wako huru katika nafsi yao yote na lile wanalolieleza linakuja kwa wepesi. Kuna kitu kimoja tu ambacho huwaweka katika nidhamu, na hayo ni maneno Yangu. Kwa hivyo, kuna idadi ya wanadamu husoma tu maneno Yangu shingo upande ili mwisho wao usiwe ule wa mauti, lakini kamwe hawaweki maneno Yangu katika matendo. Kwa upande mwingine, wanadamu wengine huona ugumu kuvumilia siku bila maneno Yangu kuwaelekeza na kuwapa, kwa hivyo wao hushikilia maneno Yangu kiasili wakati wote. Muda unavyopita, wao basi hugundua siri ya maisha ya mwanadamu, hatima ya mwanadamu na thamani ya kuwa na utu. Mwanadamu si zaidi ya haya katika uwepo wa maneno Yangu, na Mimi huruhusu tu mambo yachukue mkondo wake. Sifanyi chochote kinachomlazimisha mwanadamu kuishi kulingana na maneno Yangu kama msingi wa kuwepo kwake. Na kwa hivyo wale wasiokuwa na dhamiri au thamani katika kuwepo kwao hutazama kwa kimya mambo yanavyoenda kisha wanayatupa maneno Yangu kando kwa ujasiri na kufanya vile wanavyopenda. Wanaanza kuchoshwa na ukweli na mambo yote yatokayo Kwangu. Isitoshe, wao huchoka kukaa katika nyumba Yangu. Wanadamu hawa hukaa katika nyumba Yangu kwa ufupi tu kwa ajili ya hatima zao na kuepuka adhabu, hata kama wanafanya huduma. Lakini nia zao huwa hazibadiliki, wala matendo yao. Hii huendeleza zaidi hamu zao za Baraka, hamu za njia moja kwenda katika ufalme ambako wanaweza kubakia milele, na pia njia ya kuingia mbingu ya milele. Jinsi wanavyotamani zaidi siku Yangu ije hivi karibuni, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ukweli umekuwa kizingiti, kizuizi njiani mwao. Wanangoja kwa hamu kuingia katika ufalme ili wafurahie daima baraka za ufalme wa mbinguni, bila kutaka kuufuata ukweli ama kukubali hukumu na kuadibu, na zaidi ya yote, bila kuhitaji kuishi kwa utumishi katika nyumba Yangu na kufanya vile Ninavyoamuru. Wanadamu hawa hawaingii katika nyumba Yangu kuukamilisha moyo unaotaka kujua ukweli wala kufanya kazi pamoja na uongozi Wangu. Lengo lao tu ni wawe miongoni mwa wale ambao hawataangamizwa katika enzi inayofuata. Kwa hivyo nyoyo zao hazijawahi kuujua ukweli wala kujua jinsi ya kuukubali ukweli. Hii ndiyo sababu wanadamu wa aina hii hawajawahi kutia vitendoni ukweli au kujua undani wa ufisadi wao, ilhali wameishi katika nyumba yangu kama “wajakazi” mpaka mwisho. Wanangoja “kwa uvumilivu” kuja kwa siku Yangu, na hawachoki wanaporushwa huku na kule na hali ya kazi Yangu. Haijalishi bidii zao ni kubwa namna gani au ni gharama gani wamelipa, hakuna atakayeona kuwa wameteseka kwa ajili ya ukweli ama kujitoa kwa ajili Yangu. Katika mioyo yao, wanangoja kwa hamu siku ambayo Nitakomesha enzi nzee, na zaidi ya hayo, wanangoja kwa hamu kujua jinsi nguvu na mamlaka Yangu ni kuu. Kile hawajawahi kimbilia kufanya ni kujibadilisha na kufuata ukweli. Wanapenda kile kinachonichosha na kuchoshwa na kile ninachopenda. Wanangoja kwa hamu kile Ninachokuwa na kinyongo nacho lakini wakati uo huo wanaogopa kupoteza kile Ninachochukia. Wanaishi katika dunia hii yenye maovu ila hawajawahi kuwa na chuki nayo na wana hofu sana kuwa Nitaiangamiza dunia hii. Nia walizo nazo zinakanganya: Wanapendezwa na dunia hii Ninayochukia, na kwa wakati uo huo wanangoja kwa hamu Niiharibu dunia hii hivi karibuni. Kwa njia hii, wataepuka mateso ya uharibifu na wabadilishwe kuwa watawala wa enzi mpya kabla hawajapotoshwa kutoka katika njia ya kweli. Hii ni kwa sababu hawapendi ukweli na wanahofia kila kitu kitokacho Kwangu. Huenda ikawa watakuwa “watu watiifu” kwa muda mfupi kwa minajili ya kutopoteza baraka, lakini fikira zao za kungoja baraka kwa hamu na woga wao wa kuangamia na kuingia katika ziwa la moto haziwezi kukingwa kuonekana. Siku Yangu inapokaribia, hamu zao zinazidi kuimarika. Na vile janga lilivyo kubwa, ndivyo wanavyopoteza tumaini wasijue watakapoanzia ili kunifanya Nifurahi na kuzuia wasipoteze baraka ambazo wamezingoja kwa muda mrefu. Pindi mkono Wangu unapoanza kazi yake, wanadamu hawa wana hamu kuchukua hatua kuhudumu kama watangulizi. Wanafikiri tu kusonga kwa nguvu mpaka mstari wa mbele wa majeshi, wakiwa na woga mwingi kuwa Sitawaona. Wanafanya na kusema kile wanachodhani ni ukweli, bila kujua kuwa vitendo na matendo yao hayajawahi na umuhimu kwa ukweli, na kuwa hutatiza na kuingilia tu mipango Yangu. Hata ingawa wanaweza kuwa wameweka juhudi nyingi na wanaweza kuwa wa kweli katika ridhaa na nia zao kustahimili ugumu, kila wanachokifanya hakihusiani na Mimi, kwa maana Sijaona hata mara moja kwamba matendo yao yametoka kwa nia njema, na zaidi ya hayo, Sijawaona kama wameweka kitu chochote kwenye madhabahu Yangu. Hayo ndiyo matendo yao mbele Yangu kwa miaka hii mingi.

kutoka katika “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu” katika Neno Laonekana katika Mwili

29. Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.

kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili

30. Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu. Kwa njia hii, ingawa watu tofauti kila mmoja hufuatilia malengo yao binafsi, lengo la harakati zao na motisha yao yote ni sawa, na, zaidi ya hayo, kwa wengi wao, malengo yao ya ibada kwa kiasi kikubwa ni sawa. Katika kipindi cha elfu kadhaa za miaka iliyopita, waumini wengi wamekufa, na wengi wamekufa na kuzaliwa tena. Sio mtu mmoja au wawili ambao humtafuta Mungu, wala hata watu elfu moja au mbili, ilhali harakati ya wengi wa watu hawa ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe ama matumaini yao tukufu ya siku zijazo. Wale ambao ni waaminifu kwa Kristo ni wachache na nadra. Waumini wengi wanaomcha Mungu bado wamekufa wakiwa wametegwa na nyavu zao wenyewe, na zaidi ya hayo, idadi ya watu ambao wamekuwa na mafanikio, ni ndogo mno. Hadi siku ya leo, sababu za watu kushindwa, au siri ya mafanikio yao, bado haijulikani kwao. Wale ambao wamejawa na hamu ya kumtafuta Kristo bado hawajapata wakati wao wa ufahamu wa ghafla, hawajafikia kina cha mafumbo haya, kwa sababu hawajui. Ingawa wao wanafanya juhudi za mchwa katika harakati zao, njia ambayo wanatembelea ni njia ya kushindwa ambayo ilitembelewa na watangulizi wao, na si njia ya mafanikio. Kwa njia hii, bila kujali jinsi wanavyotafuta, je, si wao wanatembea katika njia ambayo inaelekea gizani? Je, si wanachopata ni matunda machungu? Ni vigumu vya kutosha kutabiri ikiwa watu ambao huiga wale waliofaulu katika nyakati za zamani hatimaye watapata utajiri au msiba. Uwezekano ni mbaya kiasi gani, basi, kwa watu ambao hutafuta kwa kufuata nyayo za wale ambao hawakufaulu? Je, si wao wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutofaulu? Ni thamani gani iliyoko katika njia wanayoipitia? Je, wao si wanapoteza wakati wao? Bila kujali iwapo mtu hufaulu ama hufeli katika harakati yake, kuna, kwa kifupi, sababu kwa nini wao wanafanya hivyo, na si kweli kuwa kufaulu kwao ama kushindwa kwao kunaamuliwa na kutafuta vyovyote watakavyo.

kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

31. Kiini cha imani ya watu wengi katika Mungu ni imani za kidini: Hawana uwezo wa kumpenda Mungu, na wanaweza kumfuata Mungu tu kama roboti, bila kuweza kumtamani Mungu, ama kumwabudu. Wanamfuata tu kimyakimya. Watu wengi wanamwamini Mungu, lakini wapo wachache sana ambao humpenda Mungu; “wanamheshimu” tu Mungu kwa sababu wanaogopa majanga, au hata “wanamstahi” Mungu kwa sababu ni Mwenye nguvu na aliye juu—lakini katika kumheshimu na kuvutiwa kwao hakuna upendo au kutamani kwa kweli. Katika matukio wanayoyapitia wanataka chembe za ukweli, au hata miujiza fulani isiyokuwa na maana. Watu wengi hufuata tu, wanapitia njia mbaya ili tu kupokea baraka; hawataki ukweli, wala kumtii Mungu kwa kweli ili kupokea baraka za Mungu. Maisha ya imani kwa Mungu ya watu wote hayana maana, hayana thamani, na katika imani yao mna fikira na kazi zao za kibinafsi; hawaamini katika Mungu ili kumpenda Mungu, lakini kwa ajili ya kutaka kubarikiwa. Watu wengi hutenda jinsi wapendavyo, hufanya wanachokitaka, na kutojali anachopenda Mungu, au kama wanachokifanya ni kulingana na mapenzi ya Mungu. Watu kama hao hawawezi kupata imani ya kweli, sembuse upendo wa Mungu.

kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

32. Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haikumbukwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.

kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili

33. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wanafikiria ndani yao, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipatia nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteswa sana—je Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati, na mara nyingi hufanya hesabu kama hizi ndani ya mioyo yao, na wao wanatoa madai yao kwa Mungu yanayoonyesha motisha yao na malengo na mipango. Hivi ni kusema, ndani ya moyo wake binadamu siku zote anamweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, na kila wakati anabishana na Mungu kuhusu kesi yake na kujaribu kumfanya Mungu kutoa kauli, ili aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au hawezi. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii mungu kama Mungu. Siku zote amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye kwa kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kuunda mipango na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribio yanapowapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kuhusu Mungu. Tangu wakati ule alipoanza kusadiki Mungu, binadamu amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki yake ya asili na jukumu, huku jukumu la Mungu likiwa ni kulinda na kutunza binadamu na kumtosheleza. Huu ndio uelewa wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaosadiki Mungu, na uelewa wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka kwenye kiini cha asili ya binadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya binadamu kwa kusadiki Mungu huenda isiwe na uhusiano na kuabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, binadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha binadamu ni wazi. Na kiini hicho ni nini? Ni kwamba moyo wa binadamu una kijicho, unabeba udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki, au kile kilicho kizuri, nao ni wenye kuleta dharau na ulafi. Moyo wa binadamu usingeweza kumzuia Mungu zaidi, hajaupatia Mungu kamwe. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa binadamu, wala hajawahi kuabudiwa na binadamu. Haijalishi ni gharama gani ambayo Mungu amelipia, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa binadamu, binadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali. Binadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kujali moyo wake mwenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—mada madogo ambayo ni kwamba binadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo mwanadamu anavyozungukwa na hali mbalimbali leo.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

34. Watu husema Mungu ni Mungu wa haki, na kwamba mradi tu mwanadamu atamfuata mpaka mwisho, basi Hatakuwa na upendeleo kwa mwanadamu, kwani Yeye ni mwenye haki. Je, mwanadamu akimfuata mpaka mwisho kabisa, Mungu anaweza kumtupa mwanadamu nje? Sina upendeleo kwa mwanadamu yeyote, na Huwahukumu wanadamu wote kwa tabia Yangu ya haki, ilhali kuna mahitaji yanayofaa Ninayohitaji kutoka kwa mwanadamu, na Ninahitaji yakamilishwe na wanadamu wote, bila kujali ni nani. Sijali kiwango cha kufuzu kwako au kuheshimiwa kwako; najali tu kama utatembea kwa njia Yangu, na kama unapenda na una kiu ya ukweli. Kama huna ukweli, na unaleta aibu katika jina Langu, na matendo yako ni kinyume cha njia Yangu, kufuata tu bila kujali, basi wakati huo nitakupiga na kukuadhibu kwa uovu wako, na utakuwa na nini la kusema? Utaweza kusema Mungu si mwenye haki? Leo kama umezingatia maneno ambayo nimenena, basi wewe ni mtu ambaye Namkubali. Unasema umeumia ukifuata Mungu, kwamba umemfuata kwa marefu na mapana, na umeshiriki na yeye katika wakati mzuri na mbaya, lakini hujaishi kulingana na maneno yaliyosemwa na Mungu; unataka tu kukimbia huku na kule kwa ajili ya Mungu na kujitumia kwa ajili ya Mungu kila siku, na hujafikiria kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Unasema pia, “Kwa vyovyote, naamini Mungu ni mwenye haki. Nimeteseka kwa ajili Yake, nikashughulika kwa ajili Yake, kujitoa kikamilifu Kwake, na nimefanya bidii ingawa sijapata kutambuliwa; Yeye hakika atanikumbuka.” Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye haki, na haki hii haijatiwa doa na uchafu wowote: Haina mapenzi ya binadamu, na haijatiwa doa na mwili, ama kitendo chochote cha binadamu. Wale wote ambao ni waasi na wako kwa upinzani, na hawazingatii njia Zake wataadhibiwa; hakuna atakayesamehewa, na hakuna atakayeepuka!

kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

35. Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, hivyo pana kazi mpya, na hivyo basi kuwepo na kazi iliyopitwa na wakati. Hapana ukinzani kati ya kazi mpya na ya zamani, ila zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi. Ni haki kusema kuwa katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa dhana mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu kwa mwanadamu ambapo mwanadamu ana kila aina ya dhana kumhusu Mungu—na matokeo yake ni kuwa wengi wa watu wa kidini wanaomhudumia Mungu wamegeuka kuwa adui Zake. Kwa hivyo, kadiri dhana za watu ya kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda Mungu wa zamani ambaye Amejaa mvi na Asiyepiga hatua. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. Labda ni kwa sababu ya usumbufu wa mwanadamu, au kutokiukwa kwa kazi ya Mungu—ila hawa wahubiri bado wanashikilia vitabu vizee na karatasi ilhali Mungu anaendelea na kazi Yake ambayo haijakamilika ya usimamizi kana kwamba hana msaidizi. Japo huu utata unaleta uadui kati ya mwanadamu na Mungu, kiasi kwamba hawapatanishiki, Mungu haujali ukinzani huu. Hata hivyo mwanadamu bado anashikilia imani na dhana zake, na kamwe haiachilii. Ila kitu kimoja kiko wazi: Japo mwanadamu haachi misimamo yake, Mungu mara zote anapiga hatua na kubadilisha misimamo Yake kulingana na muktadha na hatimaye ni mwanadamu atakayeshindwa bila mapambano. Mungu ndiye adui mkubwa zaidi wa maadui wake walioshindwa na vilevile ni bingwa wa wale miongoni mwa wanadamu ambao wameshindwa na wale ambao bado hawajashindwa. Ni nani anaweza kushindana na Mungu na ashinde? Dhana za mwanadamu zinaonekana kutoka kwa Mungu kwani wengi wao walizaliwa kipindi cha kazi ya Mungu. Na bado Mungu hamsamehei mwanadamu kwa sababu ya hili na hata zaidi Hammiminii sifa mwanadamu kwa “kumzalishia Mungu” mazao baada ya mazao ambayo yamo nje ya kazi ya Mungu. Badala yake Mungu hughadhabishwa sana na dhana, imani za zamani za mwanadamu na hata kuzipuuza tarehe ambayo hizi dhana zilitokea. Hakubali kamwe kwamba hizi dhana zinaletwa na kazi Yake kwani dhana za mwanadamu husambazwa na mwanadamu; chanzo chao ni fikira na akili za mwanadamu, na si Mungu, ila ni Shetani. Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwamba kuna maana kidogo sana katika kazi ya Mungu, au kwa sababu kazi ya Mungu hailingani na matakwa ya binadamu—wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu na kukitumia ili kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa mwanadamu hana sifa kabisa za kutoa maoni yake mbele za Mungu, sembuse kubuni apendavyo kanuni zozote zile zisizo na thamani, za kuchukiza na zilizooza—bila kutaja chochote kuhusu hizo dhana zilizooza. Haina maana?

kutoka katika “Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

36. Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

37. Mkitumia dhana zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkiwekea Mungu mipaka katika vigezo vya Biblia kabisa na kumweka katika wigo wenye mipaka wa kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo usiobadilika waliyoshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yule pekee aliyeitwa Masihi ndiye angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu wanadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—basi Yesu asiye na hatia alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, ilhali mwanadamu alikataa kumsamehe, na alishikilia kumhukumu Yeye kifo na basi Yesu Akasulubishwa. Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu amepenyeza kabisa usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwaadamu amepata kila kitu Atendacho Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea vitu. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu kabisa na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili na Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi sana, na kwa sababu maarifa yake ya Mungu hayaafikiani na uhalisi hata kidogo, lakini badala yake kwa uchovu hurudia tu mada ile ile bila mabadiliko na hutumia mwelekeo ule ule katika kila hali. Na hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Anasulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu.

kutoka katika “Waovu Hakika Wataadhibiwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

38. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa na uhakika juu ya hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu?

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

39. Tatizo kubwa zaidi la mwanadamu ni kwamba anaweza kupenda tu vitu ambavyo hawezi kuviona au kuvigusa, vitu ambavyo ni vya siri kubwa na vya kushangaza, na kwamba haviwezi kufikiriwa na mwanadamu na haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Kadiri vitu hivi vinavyokuwa si halisi, kadiri vinavyochambuliwa na mwanadamu, ambaye anavifuata bila kujali kitu chochote, na hujaribu kuvipata. Kadiri vinavyokuwa si halisi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvichunguza na kuvichambua zaidi, hata kwenda kwa kiwango cha kufanya mawazo yake ya kina kuyahusu. Kinyume chake, jinsi vitu vinavyokuwa halisi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvipuuza; huviangalia kwa dharau, na hata huvitweza. Huu hasa si mtazamo weni juu ya kazi halisi Ninayoifanya leo? Kadiri mambo hayo yanavyokuwa halisi, ndivyo unavyozidi kuyadharau. Wala hutengi muda kwa ajili ya kuyachunguza, bali unayapuuza; unayadharau mambo haya halisi, yenye matakwa ya moja kwa moja, na hata unakuwa na dhana nyingi kuhusu Mungu huyu ambaye ni halisi sana, na huwezi tu kuukubali uhalisi na ukawaida Wake. Kwa njia hii, huamini katika hali isiyo dhahiri? Una imani thabiti katika Mungu asiye dhahiri wa wakati uliopita, na wala hupendi kumjua Mungu wa kweli wa leo. Hii si kwa sababu Mungu wa jana na Mungu wa leo wanatoka katika enzi tofauti? Si pia kwa sababu Mungu wa jana ni Mungu wa mbinguni aliyeinuliwa, wakati Mungu wa leo ni mwanadamu mdogo wa duniani? Aidha, si pia kwa sababu Mungu anayeabudiwa na mwanadamu ni yule aliyetokana na dhana zake, wakati Mungu wa leo ni mwili halisi uliotengenezwa duniani? Hata hivyo, si kwa sababu Mungu wa leo ni halisi sana kiasi kwamba mwanadamu hamfuatilii? Maana kile ambacho Mungu wa leo anamtaka mwanadamu afanye ni kile ambacho mwanadamu hayupo radhi kabisa kukifanya, na ambacho kinamfanya ahisi aibu. Huku sio kufanya mambo yawe magumu kwa mwanadamu? Je, hili halionyeshi makovu yake hapa? Kwa namna hii, wengi wao ambao hawafuati uhalisi wanakuwa maadui wa Mungu mwenye mwili, wanakuwa wapinga Kristo. Huu si ukweli dhahiri?

kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

40. Kwa miaka na mikaka Nimeona watu wanaomsadiki Mungu. Kusadiki huku kunachukua mfumo gani? Baadhi ya watu wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu. Watu hawa hawana majibu ya maswali kuhusu uwepo wa Mungu kwa sababu hawawezi kuhisi au kuwa na ufahamu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu, sikuambii hata kuuona waziwazi au kuuelewa. Kwa nadharia yao, watu hawa wanafikiria kwamba Mungu hayupo. Baadhi wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni binadamu. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hawezi kufanya mambo yale ambayo wao hawawezi kufanya, na kwamba Mungu anafaa kufikiria namna wanavyofikiria. Ufafanuzi wa mtu huyu kuhusu Mungu ni “mtu asiyeonekana na asiyegusika.” Kunalo pia kundi la watu wanaosadiki katika Mungu kana kwamba Yeye ni kikaragosi. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hana hisia, kwamba Mungu ni sanamu. Wakati wanapokabiliwa na suala, Mungu hana mwelekeo, hana mtazamo, hana mawazo; Anatawaliwa na binadamu. Watu wanasadiki tu wanavyotaka kusadiki. Wakimfanya kuwa mkubwa, Yeye ni mkubwa; wakimfanya kuwa mdogo, Yeye ni mdogo. Wakati wanapotenda dhambi na wanahitaji rehema ya Mungu, wanahitaji uvumilivu wa Mungu, wanahitaji upendo wa Mungu, basi Mungu anafaa kutoa rehema Zake. Watu hao wanafikiria kuhusu Mungu kwenye akili zao binafsi na kumfanya Mungu kutimiza mahitaji yao na kutosheleza matamanio yao yote. Haijalishi ni lini na ni wapi, na haijalishi hata mtu huyu anafanya nini, watakubali mvuto huu katika matendo yao kwa Mungu na kusadiki kwao katika Mungu. Kuna hata wale wanaosadiki katika Mungu kuweza kuwaokoa baada kuikera tabia ya Mungu. Hii ni kwa sababu wanasadiki kuwa upendo wa Mungu hauna mipaka, tabia ya Mungu ni haki, na kwamba bila kujali ni vipi ambavyo watu wanakosea Mungu, Hatakumbuka chochote. Kwa sababu makosa ya binadamu, dhambi za binadamu na kutotii kwa binadamu ni maonyesho ya mara moja ya tabia ya mtu huyo, Mungu atawapatia watu fursa, kuvumilia na kuwa na subira nao. Mungu angali atawapenda kama awali. Kwa hivyo tumaini la wokovu wao lingali kubwa. Kwa hakika, haijalishi ni vipi mtu anavyosadiki Mungu, mradi tu hafuatilii ukweli basi Mungu anashikilia mwelekeo mbaya kwake. Hii ni sababu wakati unamsadiki Mungu, labda unakithamini kile kitabu cha neno la Mungu unakichambua kila siku, unakisoma kila siku, lakini unamweka Mungu halisi pembeni, unamchukulia kama hewa tupu, unamchukulia Yeye kama mtu, na baadhi yenu mnamchukulia kuwa kikaragosi. Kwa nini Nasema hivi? Kwa sababu kutokana na vile Ninavyoona, licha ya kama unakabiliwa na suala au kukumbana na hali, yale mambo yanayopatikana katika nadharia yako, yale mambo ambayo yameimarishwa ndani kwa ndani—hakuna kati ya haya ambayo yana uunganisho wa neno la Mungu au yanafuatilia ukweli. Unajua tu kile wewe mwenyewe unatafuta, maoni yako wewe binafsi, na kisha mawazo yako binafsi, mitazamo yako binafsi inalazimishiwa Mungu. Inakuwa mitazamo ya Mungu, ambayo inatumika kama viwango vya kutii bila kusita. Kwa muda, kuendelea namna hii kunakufanya uwe mbali zaidi na Mungu.

kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

41. Watu wanapokusanyika pamoja na Mimi, moyo Wangu unajawa na furaha. Mara moja, Ninatoa baraka zilizo mkononi Mwangu miongoni mwa binadamu, ili watu waweze kukusanyika kwa mkutano na Mimi, na kutokuwa maadui wanaoniasi lakini marafiki wanaotangamana na Mimi. Hivyo, Mimi pia ni wa dhati kwa mwanadamu. Katika kazi Yangu, mwanadamu anaonekana kama mwanachama wa shirika la ngazi ya juu, hivyo Ninamzingatia zaidi, kwa maana daima amekuwa kusudi la kazi Yangu. Nimeweka imara mahali Pangu katika mioyo ya watu, ili mioyo yao iweze kuniheshimu—ilhali wanabaki wasiojua kabisa kwa nini Ninafanya hili, na hawafanyi lolote ila kusubiri. Ingawa kuna mahali ambapo Nimeweka imara katika mioyo ya watu, hawahitaji kwamba Niishi hapo. Badala yake, wanamsubiri “Mtakatifu” katika mioyo yao kuwasili ghafla. Kwa sababu utambulisho Wangu ni duni sana, Sifikii mahitaji ya watu na hivyo Naondolewa na wao. Kwa sababu wanachotaka ni “Mimi” ambaye ni mwenye majivuno sana—ilhali Ninapokuja, Sikuonekana kwa njia hii kwa mwanadamu, kwa hivyo aliendelea kuangalia mbali, akimsubiri aliye moyoni mwake. Ninapokuja mbele ya watu, wananikataa mbele ya umma. Ningeweza tu kusimama upande mmoja, Nikisubiri “uamuzi” wa mwanadamu, Nikitazama kuona kile watu wangeishia kufanya na Mimi, hii “bidhaa” pungufu. Siyaangalii makovu ya watu, lakini katika sehemu yao ambayo haina makovu, na kutoka kwa hili Nafurahishwa. Katika macho ya watu, Mimi ni “nyota ndogo” tu ambayo imeshuka kutoka angani, Mimi ni mdogo zaidi tu mbinguni, na ujaji Wangu duniani leo uliagizwa na Mungu. Kwa hiyo, watu wamebuni fasiri zaidi za maneno “Mimi” na “Mungu,” wakiogopa sana kumuunganisha Mungu na Mimi. Kwa sababu taswira Yangu haina sura ya Mungu hata kidogo, watu wote wanaamini kwamba Mimi ni mtumishi ambaye si wa jamii ya Mungu, na kusema kwamba hii si taswira ya Mungu. Pengine kuna watu ambao wamemwona Mungu—lakini kwa sababu ya ukosefu Wangu wa utambuzi ulimwenguni, Mungu hajawahi “kuonekana” Kwangu. Pengine nina “imani” ndogo sana na hivyo watu wananiona kama aliye duni. Watu wanadhani kwamba iwapo mtu kweli ni Mungu, basi hakika atakuwa stadi katika lugha ya mwanadamu, kwani Mungu ndiye Muumba. Lakini ukweli ni kinyume kabisa: Mimi si bingwa tu katika lugha ya mwanadamu, lakini kuna nyakati ambazo Siwezi hata “kukimu” “upungufu” wake. Kwa hiyo, Nahisi kuwa “mwenye hatia” kidogo, kwani Sitendi jinsi watu “wanataka,” lakini Naandaa tu nyenzo na kufanya kazi kwa mujibu wa kile “wanachokosa.” Siulizi mengi kutoka kwa mwanadamu, lakini watu wanaamini vinginevyo. Hivyo, “unyenyekevu” wao unafichuliwa katika kila tendo lao. Daima wanastahili kutembea mbele Yangu wakiniongoza njia, wakiwa na hofu kubwa kwamba Nitapotea, wakiogopa kwamba Nitazurura katika misitu ya kale ndani ya milima. Kwa hiyo, watu daima wameniongoza mbele, wakiwa na hofu sana kwamba Nitaingia katika gereza la chini ya ardhi. Nina “wazo wa kufaa” kidogo kuhusu imani ya watu, kwa maana wamefanya kazi kwa bidii kwa ajili Yangu bila kufikiria chakula au usingizi, kiasi kwamba juhudi zao kwa ajili Yangu zimewaacha bila usingizi mchana na usiku na hata kuzeeka—ambalo linatosha kuonyesha kwamba imani yao “imevuka mipaka” ya ulimwengu, na “kuwapita” mitume na manabii kotekote katika enzi.

kutoka katika “Sura ya 32” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

42. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili—yaani, yeyote asiyeamini kazi na hotuba ya Mungu anayeonekana na haamini Mungu anayeonekana lakini badala yake anaabudu Mungu asiyeonekana mbinguni—hana Mungu katika moyo wake. Ni watu wasiomtii na wanaompinga Mungu. Watu hawa hawana ubinadamu na fahamu, kusema chochote kuhusu ukweli. Kwa watu hawa Mungu anayeonekana na kushikika hawezi kuaminika zaidi, lakini Mungu asiyeonekana wala kushikika ni Mungu wa kuaminika na pia Anayefurahisha nyoyo zao. Wanachotafuta si ukweli wa uhalisi, wala si kiini cha kweli cha uhai, wala nia za Mungu; badala yake, wanatafuta msisimko. Mambo yoyote yanayoweza kuwaruhusu kufikia tamaa zao ni, bila shaka, imani na shughuli zao. Wamwamini Mungu tu ili kuridhisha tamaa zao, si kutafuta ukweli. Hawa watu si watenda maovu? Wanajiamini sana, na hawaamini kwamba Mungu aliye mbinguni atawaangamiza, hawa “watu wazuri.” Badala yake, wanaamini kwamba Mungu atawaruhusu kubaki na, zaidi ya hayo, Atawatuza vizuri sana, kwani wamemfanyia Mungu mambo mengi na kuonyesha kiwango kikubwa cha “uaminifu” Kwake. Kama wangemtafuta Mungu anayeonekana, wangelipiza kisasi mara moja dhidi ya Mungu na kukasirika wakati hawatapata tamaa zao. Hawa ni watu waovu wanaotaka kuridhisha tamaa zao; si watu wa uadilifu wanaosaka ukweli. Watu kama hao ni wale wanaojulikana kama waovu wanaomfuata Kristo. Wale watu wasioutafuta ukweli hawawezi kuamini ukweli. Hawawezi kabisa kutambua matokeo ya baadaye ya binadamu, kwani hawaamini kazi ama hotuba yoyote ya Mungu anayeonekana, na hawawezi kuamini hitimisho la baadaye la binadamu. Hivyo, hata wakimfuata Mungu anayeonekana, bado wanatenda maovu na hawatafuti ukweli, wala hawatendi ukweli Ninaohitaji. Wale watu wasioamini kwamba wataangamizwa kinyume ni kwamba ni wale watu watakaoangamizwa. Wote wanajiamini kuwa wajanja sana, na wanaamini kwamba wao wenyewe ndio wanaotenda ukweli. Wanafikiria mwenendo wao mbovu kuwa ukweli na hivyo wanauthamini. Hawa watu waovu wanajiamini sana; wanachukua ukweli kuwa mafundisho ya dini, na kuchukua vitendo vyao vibovu kuwa ukweli, na mwishowe watavuna tu walichopanda. Watu wanapojiamini zaidi na wanapokuwa na kiburi zaidi, ndipo hawawezi zaidi kupata ukweli; watu wanapomwamini Mungu wa mbinguni zaidi, ndipo wanampinga Mungu zaidi. Hawa ndio watu watakaoadhibiwa.

kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

43. Machoni pa watu, maneno ya Mungu ni kama chombo cha siku zote, hawayachukulii kuwa muhimu kabisa. Hivyo, watu hawawezi kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo—wamekuwa mafidhuli hafifu wanaofahamu ukweli lakini hawautii katika vitendo. Kosa hili la mwanadamu pekee kwa hivyo linatosha kusababisha chukizo ndani ya Mungu kwa kipindi cha muda, na kwa hiyo Asema mara nyingi kwamba watu hawatilii maanani maneno Yake. Lakini katika dhana zao, watu hufikiria yafuatayo: “Kila siku sisi husoma na kuchambua maneno ya Mungu, ingewezekanaje kusemwa hatuyatilii maanani? Je, huku si kutotutendea kwa haki?” Lakini wacha Niwachambulie kidogo—watu watakuwa na haya. Wanaposoma maneno ya Mungu, wao huitikia kwa vichwa vyao, wao hunyenyekea mno, kama mbwa wa pua na mdomo mfupi wenye kunyanzi anayedorora kwa maneno ya bwana wake. Hivyo, wakati huu, watu huhisi hawafai, machozi hutiririka usoni mwao, ni kana kwamba wangependa kutubu na kuanza upya—lakini mara tu wakati huu umepita, kuona aibu kwao hutoweka mara moja, kubadilishwa na hali ya mbwa mwitu, wao huweka maneno ya Mungu upande mmoja, na daima huamini kwamba shughuli zao wenyewe hupewa umuhimu wa kwanza, kwamba mambo ya Mungu huja mwisho, na kwa sababu ya matendo haya yao, huwa hawawezi kamwe kutia maneno ya Mungu katika vitendo. Wakati ukweli unapowasili, wao hunyosha viwiko vyao nje[f]—huku ni kusaliti watu wao wenyewe—si ajabu Mungu asema, “‘anakimbia kwenda upande mwingine’ ilhali ananitegemea kwa riziki.” Ni kutoka kwa hili pekee ndio inaweza kuonekana kwamba hakuna uwongo hata kidogo katika maneno ya Mungu, yote ni kweli, na hayana chuku hata kidogo, lakini yanaonekana kuwa yameshindwa kuelezwa kikamilifu kwa kiasi fulani, kwani kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hana uwezo wa kukubali.

kutoka katika “Sura ya 36” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

44. Watu wengi huyashika maneno ya Mungu kuyasoma siku baada ya siku, kiasi kwamba wanaviweka akilini vifungu vyote maarufu humo kama vitu vyao vyenye thamani zaidi, na zaidi kuyahubiri maneno ya Mungu kila mahali, wakiwatolea na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno Yake. Wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, kuwa na ushuhuda kwa maneno Yake, kwamba kufanya hivi ni kufuata njia ya Mungu; wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kwamba kufanya hivi ni kuleta maneno Yake katika maisha yao halisi, kuwa kufanya hivi kutawawezesha kupokea pongezi ya Mungu, na kuokolewa na kukamilika. Lakini, hata wanapohubiri maneno ya Mungu, hawazingatii maneno ya Mungu katika matendo, ama kujaribu kujileta sambamba na yale yanayofichuliwa katika maneno ya Mungu. Badala yake, wanayatumia maneno ya Mungu kupata upendo na imani ya wengine kwa hila, kuingia katika usimamizi wao wenyewe, na kubadhiri na kuiba sifa za Mungu. Wanatarajia, kwa ubatili, kutumia nafasi waliyopata kwa kueneza maneno ya Mungu ili kupewa kazi ya Mungu na pongezi Yake. Miaka mingapi imepita, lakini hao watu hawajaweza tu kupata pongezi ya Mungu katika hatua ya kuyahubiri maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kugundua njia ambayo wanafaa kufuata katika hatua ya kushuhudia maneno ya Mungu, na hawajajisaidia tu ama kujipatia wenyewe katika hatua ya kuwapa na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kumjua Mungu, ama kuamsha ndani yao uchaji wa kweli wa Mungu, katika hatua ya kufanya haya yote; kwa upande mwingine, kutoelewa kwao kuhusu Mungu kunakuwa hata wenye kina zaidi, kutokuwa na imani kwao kwa Mungu kunazidi kuwa na mashaka, na mawazo yao kumhusu yanatiwa chumvi zaidi. Wakijazwa na kuongozwa na mawazo yao kuhusu maneno ya Mungu, wanaonekana kuwa katika haki yao kamili, kana kwamba wanapitia ujuzi wao bila juhudi, kana kwamba wamepata kusudi lao katika maisha, wito wao, na kana kwamba wameshinda maisha mapya na kuokolewa, kana kwamba, maneno ya Mungu yakibiringika kutoka kwenye ulimi kwa kukariri, wameupata ukweli, kushika nia za Mungu, na kugundua njia ya kumjua Mungu, kana kwamba, katika wakati wa kuhubiri maneno ya Mungu, wanakuja kila wakati uso kwa uso na Mungu, pia, wana “sukumwa” kila wakati mpaka kiwango cha kilio, na kila wakati kuongozwa na “Mungu” katika maneno ya Mungu, wanaonekana kushika bila kukoma wasiwasi Wake wenye ari na nia njema, na wakati uo huo kushika wokovu wa Mungu kwa mwanadamu na usimamizi Wake, kuja kujua kiini Chake, na kuelewa tabia Yake ya haki. Msingi huu ukizingatiwa, wanaoneka kuamini hata zaidi katika uwepo wa Mungu, kujua zaidi hali ya utukufu Wake, na kuhisi hata kwa kina zaidi ukuu Wake na kuvuka mipaka Kwake. Wakiwa wameinuka katika ufahamu wao wa kijuujuu wa maneno ya Mungu, itaonekana kuwa imani yao imekua, kuamua kwao kupitia mateso kumetiwa nguvu, na maarifa yao kwa Mungu yamekuwa na kina. Ila hawajui kwamba, hadi watakapopitia maneno ya Mungu kwa kweli, maarifa yao yote kuhusu Mungu na mawazo yao kumhusu Yeye yanatoka kwa mawazo yao wenyewe ya kufikiri kwa ubunifu na kukisia. Imani yao haiwezi kusimama jaribio lolote kutoka kwa Mungu, wanachoita kiroho na kimo haviwezi kusimama chini ya majaribu ya Mungu na ukaguzi, uamuzi wao ni ngome tu iliyojengwa juu ya changarawe, na wanachoita maarifa juu ya Mungu pia sio zaidi ya ubunifu wa mawazo yao. Kwa hakika, watu hawa, ambao, ilivyokuwa, wameweka juhudi kubwa katika maneno ya Mungu, hawajawahi kutambua imani ya kweli ni nini, kujiwasilisha kwa kweli ni nini, kujali kwa kweli ni nini, ama maarifa ya kweli ya Mungu ni nini. Wanachukua nadharia, mawazo, maarifa, zawadi, utamaduni, ushirikina na hata tabia nzuri za binadamu, na kuyafanya kuwa “uwekezaji wa msingi” na “zana za kijeshi” za kumwamini Mungu na kumfuata, hata kuyafanya kuwa misingi ya imani yao kwa Mungu na katika kumfuata Yeye. Wakati uo huo, pia wanachukua uwekezaji msingi huu na silaha na kuyafanya kuwa hirizi ya uchawi kwa kumjua Mungu, ya kukutana na kubishana na ukaguzi wa Mungu, majaribu, kuadibu, na hukumu. Mwishowe, wanachopata bado hakijumlishi chochote zaidi ya hitimisho kumhusu Mungu zinazoegemea hisia za kidini, katika kabaila za ushirikina, na kwa yote yaliyo ya kimapenzi, ya kustaajabisha, na yenye ugumu kuelewa, na njia yao ya kujua na kumweleza Mungu imepigwa muhuri katika muundo sawa na wa wale watu wanaoamini katika Mbingu iliyo Juu pekee, ama Mtu Mzee aliye Mawinguni, wakati ukweli wa Mungu, kiini Chake, tabia Zake, miliki Zake na asili, na kadhalika, yote yanayomhusu Mungu wa kweli Mwenyewe, ni vitu ambavyo kuvijua kumekosa mshiko, havina uhusiano kabisa na viko mbali kabisa. Katika njia hii, ingawa wanaishi chini ya upaji na ustawishaji wa maneno ya Mungu, hawawezi hata hivyo kutembea kwa kweli katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Sababu ya hakika ya hii ni kwamba hawajawahi kupata kujuana na Mungu, wala hawajawahi kuwa na mawasiliano ya kweli ama ushirika Naye, kwa hivyo haiwezekani kufikia maelewano ya pamoja na Mungu, ama kuamsha ndani mwao imani halisi katika, kufuata, ama ibada ya Mungu. Kwamba wanafaa kuyahusisha maneno ya Mungu, kwamba wanafaa kumhusisha Mungu—mwelekeo huu na tabia imewahukumu kurudi mkono mtupu kutoka kwa jitihada zao, imewahukumu katika maisha yote wasiweze kutembea katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Lengo wanalolengea, na mwelekeo wanaoelekea, inamaanisha kuwa ni maadui wa Mungu milele, na kwamba hata milele hawatawahi kuweza kupokea wokovu.

kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

45. Ninaonekana kwenu katika maisha yenu lakini daima hamjui, na hamnitambui hata. Takriban nusu ya maneno Ninayoyasema ni hukumu ya nyinyi, na nusu yao ni ya ufanisi ili nyote mnavutwa mawazo. Nusu iliyobaki ni maneno ya kuwafundisha kuhusu maisha na jinsi ya kutenda, lakini ni kana kwamba hayapo kwenu, na kana kwamba nyinyi mnasikiliza maneno ya watoto wanaocheza, ambayo daima nyinyi huyatolea tabasamu iliyofichwa, na kisha hakuna kitu kinachofanywa. Hamjawahi kujishughulisha na mambo haya; daima mmefuata matendo Yangu kutokana na udadisi wenu ili kwamba sasa mmeanguka gizani na hamwezi kuuona mwanga—mnalia kwa huruma gizani. Kile Ninachotaka ni utiifu wenu, utiifu wenu usio na masharti na hata zaidi, Nahitaji kwamba muwe na hakika kabisa juu ya kila kitu Ninachosema. Hampaswi kukubali mtazamo wa kutokujali na hasa hampaswi kuuvumilia kwa kuchagua, ni wazi kwamba nyinyi daima hamjali maneno Yangu na kazi Yangu. Kazi Yangu inafanywa katikati yenu na Nimewapa maneno Yangu mengi, lakini mkinilaghai kwa njia hii, Ninaweza tu kutoa bure kile ambacho hamjapata na hamjatia katika vitendo kwa familia za Mataifa. Ni nini kati ya uumbaji hakipo mikononi Mwangu? Wengi wa wale kati yenu ni wa “wa miaka mingi sana” na hamna nguvu ya kukubali aina hii ya kazi Yangu. Nyinyi ni kama ndege wa Hanhao[g], mnaishi kwa shida, na hamjawahi kuyachukulia maneno Yangu kwa uzito. Vijana ni bure sana na wanajifurahisha sana na hata zaidi wanaipuuza kazi Yangu. Hawahisi kufurahia vyakula vitamu vya karamu Yangu; Wao ni kama ndege mdogo ambaye ameruka nje ya tundu lake kwenda mbali kabisa. Je, wazee na vijana wa aina hii wanawezaje kuwa na manufaa Kwangu?

kutoka katika “Maneno kwa Vijana na Wazee” katika Neno Laonekana katika Mwili

46. Kunao baadhi ya watu ambao imani yao haijawahi kutambuliwa katika moyo wa Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu hatambui kwamba watu hawa ni wafuasi Wake, kwa sababu Mungu haisifu imani yao. Kwa watu hawa, haijalishi wamemfuata Mungu kwa miaka mingapi, mawazo na mitazamo yao haijawahi kubadilika. Wao ni kama wasioamini, wanatii kanuni na njia ambayo wasioamini wanafanya mambo yao, kutii sheria zao za kusalia na imani. Hawakuwahi kukubali neno la Mungu kama maisha yao, hawakuwahi kusadiki kwamba neno la Mungu ni ukweli, hawakuwahi kunuia kukubali wokovu wa Mungu, na hawakuwahi kutambua Mungu kama Mungu wao. Wanachukulia kusadiki Mungu kuwa uraibu fulani wa wanagenzi, wakishughulikia Mungu kama riziki ya kiroho, hivyo basi hawafikirii kwamba ipo thamani ya kujaribu na kuelewa tabia ya Mungu, au kiini halisi cha Mungu. Unaweza kusema kwamba kila kitu kinacholingana na Mungu wa kweli hakihusiani kwa vyovyote vile na watu hawa. Hawana hamu yoyote, na hawawezi kusumbuliwa kutilia maanani. Hii ni kwa sababu ndani kabisa ya mioyo yao kunayo sauti ya nguvu ambayo siku zote inawaambia: Mungu haonekani na hagusiki, na Mungu hayupo. Wanasadiki kwamba kujaribu kumwelewa Mungu wa aina hii hakutastahili jitihada zao; itakuwa sawa na wao kujidanganya. Wanamtambua Mungu kwa maneno tu, na hawachukui msimamo wowote halisi. Pia hawafanyi chochote katika hali ya kimatendo, wakifikiri kwamba wao ni werevu sana.

kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

47. Miaka yenu mingi ya matendo mbele Yangu imenipa jibu ambalo Sijawahi kupata hapo awali. Na swali la jibu hili ni: “Mtazamo wa mwanadamu mbele ya ukweli na Mungu wa ukweli ni upi?” Juhudi ambazo Nimemwagia mwanadamu ni dhihirisho la kiini Changu cha kumpenda mwandamu, na vitendo na matendo ya mwanadamu mbele Yangu pia yamedhihirisha kiini cha mwanadamu cha kuchukia ukweli na kunipinga Mimi. Katika wakati wote Mimi hujali wale wote ambao wamenifuata, lakini hakuna wakati ambao wale wanaonifuata wameweza kupokea neno Langu; hawana uwezo kabisa wa kukubali hata maoni yanayotoka Kwangu. Hili ndilo hunihuzunisha zaidi ya yote. Hakuna anayeweza kunielewa na, zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kunikubali, hata ingawa mtazamo Wangu ni wa kweli na maneno Yangu ni ya upole. Wote wanafanya kazi Niliyowaaminia kuifanya kulingana na nia yao ya asili; hawatafuti nia Zangu, wala kuuliza maombi Yangu. Bado wanadai kuwa Wananihudumia kwa uaminifu, wakati huu wote wakiwa wananiasi. Wengi wanaamini kuwa ukweli usiokubalika nao au ukweli ambao hawawezi kutia vitendoni sio ukweli. Kwa watu kama hawa, ukweli Wangu unakuwa kitu cha kukataliwa na kutupiliwa kando. Kwa wakati uo huo Ninakuwa mmoja anayetambuliwa na mwanadamu kwa neno tu kama Mungu, lakini pia kuchukuliwa kama mtu wa nje ambaye sio ukweli, njia na uhai. Hakuna anyejua ukweli huu: Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.

kutoka katika “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu” katika Neno Laonekana katika Mwili

48. Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. Mnapokuwa na hamu ama shauku na kitu chochote kile Mnachokipenda, siku zote mnakuwa ni wakati ambapo mnanifuata, au hata wakati mnaposikiliza maneno Yangu. Hivyo nasema, mnatumia uaminifu ninaowataka muonyeshe, kuwa badala yake waaminifu na kufurahia “vipenzi” wenu. Ingawa mnaweza kutoa sadaka ya kitu kimoja au vitu viwili kwa ajili Yangu, hakuwakilishi vitu vyenu vyote, na haionyeshi kwamba ni Kwangu ambako uaminifu wako uko kwa kweli. Mnajiweka wenyewe katika shughuli ambazo mnazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake. Kwa maana kile ambacho mnakuwa waaminifu kwacho, hujawahi kuhisi kuchoshwa au kukerwa nacho, badala yake, mnatamani kuwa na kiasi kikubwa zaidi na ubora wa vitu ambavyo ninyi mu waaminifu kwavyo na hamjawahi kukata tamaa. Mimi mwenyewe na maneno Yangu daima hutupwa pembeni katika masuala ya vitu mnavyovipenda. Na hamna namna isipokuwa kuyaweka mwisho; wengi hata wanaondoka sehemu ya mwisho kwa ajili ya kuwa waaminifu kwa kitu ambacho hawajakigundua bado. Hawajawahi kuniweka mioyoni mwao kwa kiwango chochote kile. Pengine mtafikiri kwamba ninahitaji mambo mengi sana kutoka kwenu au Ninawahukumu kimakosa, lakini je, mmeshawahi kufikiri kuhusu ukweli huu kwamba mnapotumia muda kwa furaha pamoja na familia yenu, hujawahi kuwa mwaminifu kwangu hata mara moja? Wakati kama huu, hii haiwaumizi? Mioyo yenu inapojawa na furaha kwa kupokea malipo kwa kazi zenu, haiwavunji moyo kwamba hamjajitweka kwa ukweli wa kutosha? Ni lini mmewahi kulia kwa kukosa idhinisho langu? Mnaitesa akili yenu na kupata maumivu makubwa kwa ajili ya watoto wenu, lakini bado hamjaridhika, bado mnaamini kwamba hamjaweka jitihada za kutosha kwao, kwamba hamjatumia nguvu zenu zote. Lakini Kwangu, mmekuwa ajizi na wa kutojali, mkiniweka tu katika kumbukumbu zenu na wala Sidumu ndani ya mioyo yenu. Kujitolea Kwangu na jitihada zangu daima hupita bila nyinyi kuzihisi, na wala hamjawahi kuweka jitihada ili muweze kuelewa. Nyinyi hutafakari kidogo tu na kuamini kwamba hiyo itatosha. “Uaminifu” wa aina hii sio ule ambao Nimekuwa nikiutazamia, bali ni ule ambao umekuwa machukizo Kwangu kwa muda mrefu.

kutoka katika “Wewe U Mwaminifu kwa Nani?” katika Neno Laonekana katika Mwili

49. Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba[h] sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni[i] kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu?

kutoka katika “Wewe U Mwaminifu kwa Nani?” katika Neno Laonekana katika Mwili

50. Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Binadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati familia yao ndogo ina furaha na iko sawa, wanadamu tayari wananiweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, na hivyo kufurahia furaha heri ya familia. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na mkunjufu kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Nusura hawana ubinadamu hata kidogo.

kutoka katika “Sura ya 14” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

51. Katika ufalme, Mimi ni Mfalme—lakini badala ya kunichukulia kama Mfalme, mwanadamu ananichukulia kama Mwokozi aliyeshuka kutoka mbinguni. Kwa sababu hii, anasubiri kwa hamu Nimpe sadaka, na hafuatilii ufahamu Wangu. Wengi sana wamelia mbele Zangu kama waombaji; wengi pia wamenifungulia “mifuko” yao na kunisihi Niwape chakula ili waendelee kuishi; wengi wao wameniwekea macho yenye tamaa, kama mbwa mwitu wenye njaa, wakitamani wanibugie na kujaza matumbo yao; wengi pia wameinamisha vichwa vyao kwa sababu ya dhambi zao na kuona aibu, wakiomba huruma Yangu, au kukubali adhabu Yangu kwa hiari. Ninapozungumza, makosa kadhaa ya mwanadamu yanaonekana ya upuuzi, na umbo lake la kweli linaonekana katika mwanga, na katika mwangaza unaong’aa, mwanadamu hana uwezo wa kujisamehe mwenyewe. Hivyo, anakimbia na kuinama mbele Zangu na kutubu dhambi zake. Kwa sababu ya “uaminifu” wa mwanadamu, Mimi Namvuta tena kwa mara nyingine kwenye gari la wokovu, na kwa sababu hii mwanadamu ana shukurani Kwangu, na kunitupia jicho la upendo. Ilhali bado hana nia ya kujificha kikamilifu ndani Yangu, na hajautoa moyo wake wote Kwangu. Yeye anajigamba tu kwa ajili Yangu, ilhali hanipendi kwa kweli, kwa maana hajaweka mawazo yake Kwangu; mwili wake uko mbele Yangu, ilhali moyo wake uko nyuma Yangu. Kwa sababu kuelewa kwa mwanadamu kwa sheria ni kwa chini sana na hana haja ya kuja mbele Yangu, Mimi Nampa usaidizi unaofaa, ili aweze kugeuka upande Wangu kutoka kati ya upumbavu wake uliokita mizizi. Hii hasa ndiyo huruma ninayompa mwanadamu, na ndiyo njia ambayo nafanya bidii ili kumwokoa mwanadamu.

kutoka katika “Sura ya 22” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

52. Miongoni mwa watu wa dunia ya sasa—wakiwemo wote walioko katika nyumba Yangu—Ni nani wanaotafuta kwa kweli hifadhi Kwangu? Ni nani wanaotoa mioyo yao kwa ajili ya gharama ambayo Nimelipa? Ni nani amewahi kuishi katika nyumba Yangu? Ni nani amewahi kujitolea kwa kweli mbele Zangu? Ninapotoa mahitaji Yangu kwa mwanadamu, anafunga “kijighala” chake mara moja. Ninapompatia mwanadamu, mara moja yeye hufungua mdomo wake kuchukua mali Yangu kichinichini, na katika moyo wake, mara nyingi hutetemeka, akiwa na uoga mwingi kuwa Nitalipiza kisasi. Kwa hivyo kinywa cha mwanadamu ni nusu wazi na nusu kimefungwa na hana uwezo wa kuufurahia kwa kweli utajiri Niliompa. Huwa Simlaani mwanadamu kwa urahisi, lakini kila mara hunishika mkono na kuniomba Nirudishe huruma juu yake; na ni wakati tu mwanadamu anaponisihi ndipo Ninapotoa “huruma” juu yake, na Ninampa maneno makali ya kinywa Changu, kiasi kwamba anashikwa na aibu mara moja, na kwa kuwa hana uwezo wa kupata “huruma” Yangu moja kwa moja, badala yake anawafanya wengine wampishie huruma hiyo. Wakati ameelewa maneno Yangu yote kwa undani, kimo cha mwanadamu kiko sawa na matakwa Yangu, na maombi yake yanazaa matunda, na sio bure au batili; Ninabariki maombi ya mwanadamu yaliyo ya kweli, na sio kujifanya.

kutoka katika “Sura ya 28” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

53. Kwa sababu watu hawanijui na asili zao zinaniasi, hata wale walio waaminifu Kwangu ni kwa ajili ya raha yao wenyewe. Lakini jambo linalowasababishia huzuni likitokea, mioyo yao inabadilika mara moja na wanataka kukimbia kutoka upande Wangu. Hii ndiyo asili ya Shetani. Hampaswi kuwa wanaoshikilia maoni yenu, mkijiamini kuwa waaminifu! Kama hakuna manufaa kwao, kundi hili la wanyama hawawezi kuwa waaminifu Kwangu kabisa. Nisingetangaza amri Zangu za utawala, mngekuwa mlikimbia zamani. Nyote sasa mko matatani, msitake kunihudumia lakini msitake kuangushwa kwa mkono Wangu. Nisingetangaza kwamba maafa makuu yatawafika wowote wanaoniasi wakati wowote, mngekuwa mlikimbia kitambo. Je, Sijui jinsi watu wanaweza kuwa na mawazo finyu? Watu wengi zaidi sasa wanahodhi matumaini haba, lakini matumaini hayo yanapogeuka na kuwa masikitiko hawataki kuendelea zaidi na wanaomba kurudi. Nimekwisha kusema awali kwamba Simweki yeyote hapa kinyume cha mapenzi yake, lakini tahadhari kufikiria matokeo yatakavyokuwa kwako, ni huu ni ukweli, si Mimi kukutisha wewe. Hakuna awezaye kuielewa asili ya mwanadamu isipokuwa Mimi, na wote wanafikiria kwamba wao ni watiifu Kwangu, pasipo kujua kwamba utiifu wao ni mchafu. Uchafu huu utawaangamiza watu kwa kuwa wao ni njama ya joka kubwa jekundu. Hilo lilidhihirishwa na Mimi zamani sana; Mimi ni mwenyezi Mungu, na je, Mimi singeweza kufahamu jambo rahisi kama hili? Mimi ninaweza kupenyeza damu yako na mwili wako ili kuziona nia zako. Si vigumu Kwangu kuielewa asili ya mwanadamu, lakini watu hujaribu kuwa wajuaji, wakifikiria kwamba hakuna mtu ajuaye nia zao isipokuwa wao wenyewe. Je, hawajui kwamba, mwenyezi Mungu anaishi ndani ya mbingu na dunia na vitu vyote?

kutoka katika “Sura ya 118” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

54. Bila kujali jinsi wanavyojaribiwa, utii wa wale wenye Mungu ndani ya mioyo yao hubaki vile vile; lakini kwa wale wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao, wakati kazi ya Mungu hainufaishi miili yao, wanabadilisha mtazamo wao kwa Mungu, na hata kumkimbia Mungu. Hawa ndio wale hawatasimama imara mwishoni, wanaotafuta baraka za Mungu na hawana tamaa ya kujitolea wenyewe kwa Mungu na kujikabidhi wenyewe Kwake. Aina hii ya watu wa msingi watafukuzwa wakati kazi ya Mungu itakapofikia kikomo, na hawafai kuonewa huruma yoyote. Wale wasiokuwa na ubinadamu, hawawezi kumpenda Mungu kwa kweli. Wakati mazingira ni mema na salama, au kama watapata faida, wao ni watiifu kabisa kwa Mungu, lakini wakati walilokuwa wanataka limepatikana au hatimaye kukataliwa, wanageuka mara moja. Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye “mioyo mikunjufu” hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu. Ikiwa mapepo haya hayatarushwa nje, mapepo ambayo yanaweza kuua kwa kufumba na kufumbua jicho, je, hayatakuwa chanzo cha mateso zaidi?

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

55. Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunihadaa, waniruhusu kurudisha uaminifu wa mwanadamu. Nuru Yangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu huenea kwa watu wote, ilhali hivyo pia ukweli halisi wa kila tendo la mwanadamu huenea kwa watu wote, kama ufanyavyo wao kunidanganya. Ni kama kwamba viungo vya udanganyifu wa mwanadamu vimekuwa naye tangu tumboni mwa mamake, kama kwamba amekuwa na mbinu hizi maalum za kuhadaa tangu kuzaliwa kwake. Kuzidisha, hajawahi kufichua siri yake; hakuna mwanadamu aliyewahi kutambua chanzo cha ujuzi huu wa udanganyifu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu anaishi katika udanganyifu bila kujua, na ni kana kwamba yeye hujisamehe mwenyewe, kana kwamba ni mipango ya Mungu na sio yeye kunidanganya. Je, hiki sicho chanzo halisi cha mwanadamu kunidanganya? Je, huu sio mpango wake wa ujanja? Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anayejua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani kimo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”

kutoka katika “Sura ya 21” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

56. Ni mara nyingi Nimemwita mwanadamu kwa Roho Wangu, lakini matendo yake huwa ni kama amechomwa kisu na Mimi, anahusiana nami kwa umbali, katika hofu kubwa kuwa Nitamwongoza kwenda ulimwengu mwingine. Kwa mara nyingi Nimepeleleza ndani ya moyo wa mwanadamu, lakini anabaki bila ufahamu kabisa, akiwa na hofu kubwa kabisa kuwa Nitaingia nyumbani mwake na kuchukua fursa hiyo kumnyang’anya mali yake yote. Kwa hivyo, ananifungia nje, kuniacha bila chochote ila mlango uliofungwa na kukazwa na kuniacha nje kwenye baridi. Ni mara nyingi mwanadamu ameanguka na Nimemwokoa, lakini baada ya kuamka ananiacha mara moja, bila kuguswa na upendo Wangu, mwanadamu kunipiga macho ya hadhari; Sijawahi pasha joto moyo wa mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe kikatili kisichokuwa na hisia. Hata kama amepashwa joto na kumbatio Langu, kamwe hajawahi guswa na jambo hili. Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani. Hajawahi thamini upendo Wangu wa binadamu. Hana nia ya kunikaribia, akipendelea kukaa katika milima, ambapo anavumilia tishio la wanyama pori—lakini bado hana nia ya kuchukua makao ndani Yangu. Simshawishi mwanadamu yeyote: Ninafanya tu kazi Yangu. Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari.

kutoka katika “Sura ya 20” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

57. Ninaelewa kabisa udanganyifu ulio ndani ya mioyo yenu; wengi wenu hunifuata kutokana na udadisi na mmekuja kunitafuta kutokana na utupu. Wakati matakwa yenu ya tatu yanavunjwavunjwa—kwa ajili ya maisha ya amani na yenye furaha—udadisi wenu pia unatapanywa. Udanganyifu ulio ndani ya mioyo ya kila mmoja wenu wote hufunuliwa kupitia maneno na matendo yenu. Kusema kweli, nyinyi mnataka tu kujua kunihusu, hamwogopi; hamjali matamshi yenu, na mnazuia tabia zenu hata mara chache zaidi. Basi imani yenu iko vipi kwa kweli? Je, ni ya kweli? Mnatumia tu maneno Yangu kuondoa wasiwasi wenu na kupunguza uchoshi wenu, ili kujaza nafasi zilizobaki tupu katika maisha yako. Ni nani miongoni mwenu ambaye ameyatia katika vitendo? Nani ana imani ya kweli? Mnaendelea kupiga kelele kwamba Mungu ni Mungu ambaye huona ndani kabisa ya mioyo ya watu, lakini ni vipi Mungu mnayepiga kelele kuhusu mioyoni mwenu analingana na Mimi? Kwa kuwa mnapiga kelele kwa njia hii, basi kwa nini mnatenda kwa njia ile? Inawezea kuwa kwamba huu ndio upendo mnaotaka kunilipizia nao? Hakuna kiasi kidogo cha upendo kwenye midomo yenu, lakini ziko wapi dhabihu zenu, na matendo yenu mema? Isingalikua maneno yenu kuyafikia masikio Yangu, Ningaliwezaje kuwachukia sana? Ikiwa kweli mliniaminia, mngewezaje kuangukia hali kama hii ya dhiki? Mnazo sura za huzuni kwenye nyuso zenu kana kwamba mko kuzimu mkishtakiwa. Hamna uhai wowote, na mnanena kuhusu sauti yenu ya ndani kwa udhaifu; mmejawa hata na malalamiko na laana Mlipoteza imani katika yale Nifanyayo zamani na hata imani yenu ya asili imepotea, basi mnawezaje kufuata mpaka mwisho? Mnawezaje kuokolewa kwa njia hii?

kutoka katika “Maneno kwa Vijana na Wazee” katika Neno Laonekana katika Mwili

58. Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuupatia moyo huo Mungu, au kuufichua kwa Mungu ili Aweze kuuona, amejiekea yeye mwenyewe. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba baadhi mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu kuwafikiria, kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye. Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Maandishi madogo ya haya ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na maono ambayo amezoeana nayo, na akili zake binafsi ili kuamua na kuchagua njia anayofaa kutembelea na haruhusu uingiliaji kati au udhibiti wa Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

59. Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi kuhusu na wana uoga wa majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ni finyu mno kwa mambo anayoweza kuona. Hana shukrani hata chembe kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au wema Wake na utiliaji maanani kwa binadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu na adhama na hasira Yake, binadamu hana hata chembe cha uelewa wa nia nzuri za Mungu. Kwa kutajwa kwa majaribio, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu anazo nia nyingine zisizo wazi na hata baadhi wanasadiki kwamba Mungu ana mipango ya maovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, wakati huohuo kutaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kama hawatakuwa na mshikilio thabiti wa hatima yao binafsi, basi kila kitu walicho nacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha. Binadamu yumo kwenye kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kutekwa nyara na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kusadiki kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi nzima kwa mikono ya Mungu, basi hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea Sheria ya Mungu, nini kipo cha kupoteza? Na hivyo Napendekeza kwamba muwe makinifu kwa vitendo vyenu, mtahadhari na kila kitu ambacho kiko karibu kuwafanyikia ninyi. Usiwe wa pupa au msukumo na umshughulikie Mungu na watu, masuala, vitu alivyokupangilia kwa namna mshawasha unavyokupeleka, au kulingana na nafsi yako ya kiasili au kufikiria na dhana zako; lazima uwe makini katika vitendo vyako na lazima uombe na utafute zaidi, kuepuka kuchochea hasira ya Mungu.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

60. Imani yenu ni nzuri sana; mnasema kwamba mko radhi kutoa maisha yenu kwa kazi Yangu, kufanya chochote na kila kitu kwa ajili yake, lakini tabia yenu haijabadilika sana. Kumekuwa tu na maneno ya kiburi, na matendo yenu halisi ni duni sana. Inaonekana kwamba ulimi na midomo ya mtu iko mbinguni lakini miguu ya mtu iko mbali sana duniani, hivyo maneno na matendo yake na sifa yake bado yako katika hali mbaya sana. Sifa zenu tayari zimeharibiwa, mwenendo wenu unashuka hadhi, njia yenu ya kuzungumza ni ya chini, maisha yenu ni ya kudharauliwa, na hata ubinadamu wenu wote ni wa chini. Nyinyi ni wa mawazo finyu kwa watu na nyinyi hubishana juu ya kila kitu kidogo. Nyinyi hugombana juu ya sifa zenu na hadhi zenu wenyewe, hata kufikia kiasi kwamba mko radhi kushuka kuzimu, katika ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha kiasi kwamba Ninaweza kuamua kuwa nyinyi ni wenye dhambi. Mtazamo wenu juu ya kazi Yangu unatosha Kwangu kutambua kuwa nyinyi ni wale wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kusema kuwa nyinyi ni roho chafu ambazo zimejaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua ni tosha kusema kuwa nyinyi ni watu ambao mmekunywa damu ya kutosha ya pepo wachafu. Wakati kuingia katika ufalme kunapozungumzwa hamfichui hisia zenu. Mnaamini kuwa jinsi mlivyo sasa kunatosha kwenu kuingia katika lango la ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini kuwa mnaweza kupata kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu bila maneno na vitendo vyenu kupitia majaribio Yangu? Ni nani anayeweza kwa ufanisi kuyadanganya macho Yangu mawili? Je, tabia zenu za mazungumzo ya kudharauliwa na duni, zawezaje kuepuka Mimi kuona? Maisha yenu yameamuliwa na Mimi kama maisha ya kunywa damu ya pepo hizo chafu na kula nyama ya pepo hao wachafu kwa sababu mnachukua sura yao mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu tabia zenu zilikuwa mbaya hasa, hivyo, ni vipi Mimi singeweza kuchukizwa? Katika kile mnachosema kuna najisi ya pepo wachafu: Nyinyi hudanganya, huficha, na kujipendekeza kama wale tu wanaofanya uchawi, kama wale wanaodanganya na kunywa damu ya wasio wa haki. Maonyesho yote ya wanadamu ni madhalimu sana, hiyo watu wote wanawezaje kuwekwa katika nchi takatifu ambako wenye haki wapo? Je, unafikiri kwamba tabia hiyo yako ya kudharauliwa inaweza kukubainisha kama mtakatifu dhidi ya wale wadhalimu? Huo ulimi wako unaofanana na nyoka hatimaye utaangamiza mwili wako ambao huleta maangamizi na hufanya machukizo, na mikono yako hiyo ambayo imefunikwa na damu ya pepo wachafu pia itavuta roho yako kuzimu hatimaye, hiyo kwa nini usichukue fursa hii kuitakasa mikono yako iliyofunikwa na uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kuukata ulimi wako huo ambao husema maneno maovu? Inawezekana kuwa uko radhi kuteseka chini ya moto wa kuzimu kwa sababu ya mikono yako miwili na ulimi wako na midomo? Mimi huilinda mioyo ya watu wote kwa macho Yangu mawili kwa sababu muda mrefu kabla ya kuwaumba wanadamu, Nilikuwa Nimeishika mioyo yao ndani ya mikono Yangu. Zamani Nilibaini moyo wa mwanadamu, kwa hiyo mawazo ya ndani ya moyo wa mwanadamu yanawezaje kuyaepuka macho Yangu? Na wanawezaje kuwepo mapema ili kuepuka kuchomwa kwa Roho Wangu?

kutoka katika “Tabia Yako Ni Duni Sana!” katika Neno Laonekana katika Mwili

61. Midomo yako ni yenye huruma zaidi kuliko njiwa lakini moyo wako ni mbaya zaidi kuliko nyoka ya kale, hata midomo yako ni mizuri kama mwanamke Mlebanoni, lakini moyo wako si mwema kama ule wa wanawake Walebanoni na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu sana! Ninachochukia ni midomo ya wadhalimu na mioyo ya wadhalimu pekee. Mahitaji Yangu kwa watu si ya juu kuliko watakatifu, ni vile tu kwamba Mimi huhisi chukizo kwa matendo maovu ya wadhalimu na Natumaini kwamba wadhalimu huenda waweze kuondoa kuchafuka kwao na kukimbia kutoka kwa mashaka yao ya sasa ili waweze kutofautishwa na wale wadhalimu, na kuishi na kuwa watakatifu pamoja na wale wenye haki. Nyinyi mko katika hali sawa na Mimi, lakini mmefunikwa na uchafu, hakuna hata mfano kidogo wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo ndani yenu, na kwa sababu kila siku mnaiga mfano wa hao pepo wachafu na mnafanya kile wanachokifanya na kusema kile wanachokisema, kila sehemu zenu na hata ndimi zenu na midomo yenu imelowa katika maji yao mabaya. Ni kwa kiwango ambacho mmefunikwa kabisa na hayo mawaa na hakuna sehemu hata moja ambayo inaweza kutumiwa kwa kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika ulimwengu huu wa farasi na ng’ombe lakini bado kwa kweli hamjihisi kuwa na wasiwasi; na mmejaa furaha na nyinyi huishi kwa uhuru na kwa urahisi. Mnaogelea katika maji haya mabaya lakini kwa kweli hamjui kwamba mmeanguka katika mazingira haya. Kila siku unaafikiana na pepo wachafu na una shughuli na “kinyesi.” Uhai wako ni duni sana, lakini hujui kwamba bila shaka huendelei kuishi katika ulimwengu wa kibinadamu na kwamba humo ndani ya ufahamu wako mwenyewe. Je, hujui kwamba maisha yako yalikanyagwa na pepo wachafu zamani, kwamba tabia yako ilivunjiwa hadhi na maji machafu zamani? Je, unadhani kuwa unaishi katika paradiso ya kidunia, kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha na pepo wachafu, na kwamba umeishi maisha na kila kitu ambacho wamekuandalia? Je, kuishi kwako kungewezaje kuwa na maana yoyote? Je, maisha yako yangewezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukienda huku na huko kwa ajili ya wazazi wako pepo wachafu, hadi sasa, lakini hujui kwamba wale ambao wanakunasa mtegoni ni hao pepo wachafu, wazazi wako ambao walikuzaa na kukulea. Aidha, hujui kuwa uchafu wako hakika ulipewa wote na wao; yote unayojua ni kwamba wanaweza kukupa “ridhaa,” hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hasa hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa ghadhabu, lakini hukutendea kwa bashasha na kwa ukarimu. Maneno yao hulisha moyo wako na kukupendeza mno ili ukanganywe na bila kulitambua, unavutwa ndani na uko radhi kuwa wa huduma kwao, uwe mlango wao na kadhalika mtumishi wao. Huna malalamiko kamwe lakini uko radhi kutumiwa nao—unadanganywa nao. Kwa sababu hii, bila shaka huna majibu yoyote kwa kazi ambayo Mimi hufanya—si ajabu kwamba wewe daima hutaka kuponyoka kwa siri kutoka kwa mikono Yangu, na si ajabu kwamba wewe daima hutaka kutumia maneno matamu ili kuidanganya fadhila Yangu. Inadhihirika kwamba tayari ulikuwa na mpango mwingine, mpangilio mwingine. Unaweza kuona sehemu ndogo ya vitendo Yangu, vitendo vya Mwenyezi, lakini hujui chembe ya hukumu na kuadibu kwangu. Hujui wakati kuadibu kwangu kulianza; unajua tu jinsi ya kunidanganya Mimi, lakini hujui kuwa Sivumilii ukiukaji na mwanadamu.

kutoka katika “Tabia Yako Ni Duni Sana!” katika Neno Laonekana katika Mwili

62. Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina?

kutoka katika “Tabia Yako Ni Duni Sana!” katika Neno Laonekana katika Mwili

63. Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogondogo, anayependelea na asiye na mantiki, aliyekosa hisia ya haki, mwenye mbinu ovu, danganyifu na za ujanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya kwamba hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasio na ujuzi huu hawatakaribishwa na watapoteza nafasi yao katika nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu.

kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

64. Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi” Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?

kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili

65. Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi” wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?

kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

66. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.

kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

67. Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayakutoshelezi wewe kuelewa hata sehemu ndogo kabisa ya mpango Wangu wa usimamizi. Hivyo kwa nini basi unakuwa mwenye kiburi sana? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika na Yesu hata katika sekunde moja ya kazi Yake! Je, una uzoefu kiasi gani hasa? Yale uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako yote na yale uliyoyafikiria ni kidogo kuliko kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko mchwa! Vyote vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la mchwa! Usifikiri kwamba kwa kuwa tu umepata uzoefu na ukubwa kiasi, unaweza kuashiria kwa shauku na kuzungumza kwa majivuno. Je, uzoefu wako na ukubwa wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba yalikuwa mbadala wa kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kuwa nimepata mwili, na kwa sababu ya hili pekee unajawa na dhana nyingi hizo, na kutoka kwalo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Isingekuwa kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta ulizo nazo ni za ajabu kiasi gani, usingekuwa na dhana hizi nyingi; na. Si fikira zako zinatoka hapa? Kama si kupata mwili kwa Yesu mara hiyo ya kwanza, je, hata ungejua kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako kutoka kwa kupata mwili mara ya kwanza ndio una ufidhuli kuthubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini ukuchunguze badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Wakati umeingia katika mkondo huu na kuja mbele ya Mungu mwenye mwili, je, Angekuruhusu kuchunguza hili? Ni sawa kwako kuchunguza historia ya familia yako, lakini ukijaribu kuchunguza “historia ya familia” ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya uchunguzi kama huo? Je, wewe si kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?

kutoka katika “Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

68. Ni mbinu gani iliyo ya kufaa zaidi ya ufukuziaji katika njia ya leo? Ni umbo la aina gani unalopaswa kujiona mwenyewe kama katika ufukuziaji wako? Unapaswa kujua namna ya kushughulikia kila kitu kinachokufika wewe sasa, yawe ni majaribio au mateso, kuadibu bila huruma au laana—unapaswa kufikiria kwa makini haya yote. Mbona Nasema hili? Kwa sababu hata hivyo, kinachokufika wewe sasa ni jaribio moja fupi baada ya lingine. Labda sio mfadhaiko mkuu kwako sasa kwa hiyo unaacha mambo yaelekee kwa mwelekeo fulani, sio kuuchukulia kama utajiri wa thamani kwa ufukuziaji wako wa maendeleo. Wewe ni mzembe sana! Wewe kwa kweli huchukulia utajiri huu wa thamani kama mawingu yanayoelea mbele ya macho yako, na huthamini mifano hii mifupi ya mapigo makali, ambayo haionekani kuwa ya shida kwako. Wewe huchunguza tu kwa dharau na huyazingatii moyoni, lakini huyaona tu kama yanayogonga mwamba mara chache. Wewe ni mwenye kiburi sana! Wewe huchukua mtazamo wa dharau kwa shambulio moja kali, la dhoruba baada ya jingine, na wakati mwingine wewe hata hutabasamu kwa dharau, kufichua sura ya kutojali. Hili ni kwa sababu hujawahi kufikiria kuhusu kwa nini wewe hupitia aina hii ya “msiba” tena na tena. Yaweza kuwa kwamba Mimi sina haki kiasi hicho kwa watu? Je, Natafuta makosa madogo madogo tu kwako? Ingawa kufikiria kwenu si kwa maana kama Nilivyoeleza, huo mwenendo mtulivu umeeleza ulimwengu wa ndani wa moyo wako waziwazi sana. Ni wazi kwamba, kilichofichwa ndani sana ya moyo wako ni shutuma zisizojali tu na dalili zisizoisha za huzuni ambazo wengine hawawezi kuziona. Ni kwa sababu umepitia aina hizi za majaribio ndiyo unahisi kwamba si haki kabisa, hivyo unavurumisha shutuma huku. Ni kwa sababu ya majaribio haya ndiyo unahisi ulimwengu unahuzunisha sana, hivyo umejawa ghamu. Wewe huoni pigo baada ya pigo na kufundishwa nidhamu baada ya kufundishwa nidhamu kama ulinzi bora zaidi, bali unayaona kama uchokozi usio na busara kutoka Mbinguni au adhabu ya kufaa kwako. Wewe ni mjinga sana! Wewe umefungia bila huruma nyakati bora zaidi katika giza, na wewe huona mara kwa mara majaribio na kufundisha nidhamu kuzuri kama mashambulio kutoka kwa adui. Wewe huwezi kubadili kwa ajili ya mazingira, na hata zaidi, wewe hutaki kubadili. Hili ni kwa sababu wewe hutaki kupata chochote kutoka kwa kuadibu baada ya kuadibu unakoona kuwa katili. Wewe hutafuti au kuchunguza jambo kwa makini, na umekubali bila kulalamika mapenzi ya Mbinguni—popote unapoishia ndipo ulipo. Kurudi unakoona kama katili hakujaubadilisha moyo wako kabisa, wala hakujaumiliki moyo wako. Badala yake, kumeudhuru tu. Wewe umeona tu “kuadibu huku katili” kama adui yako katika maisha haya lakini hujapata chochote. Wewe ni wa kujidai sana! Wewe huamini mara chache kwamba unapitia aina hizi za majaribio kwa sababu wewe ni mwenye kustahili dharau sana, badala yake, wewe huamini kwamba ni wa bahati mbaya sana na zaidi ya hayo, wewe husema kwamba Mimi kila mara Hutafuta makosa madogo madogo kwako. Hadi sasa, ni ufahamu kiasi gani ulionao wewe kwa kweli wa kile ambacho Mimi husema na kile ambacho Mimi hufanya? Usidhani kwamba wewe ni mtu mwenye kipaji cha kuzaliwa, aliyepungukiwa na mbinguni kwa sehemu ndogo sana na anayeenda juu sana ya dunia. Wewe si stadi zaidi kuliko watu wengine, na inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi vizuri kuliko mtu mwingine yeyote wa busara duniani kwa sababu wewe hujiona mwenyewe kuwa muhimu sana; hujawahi kuwa na hisi ya udhalili. Inaonekana kwamba wewe huona kila kitu Nifanyacho dhahiri kabisa. Ukweli ni kwamba wewe siyo mtu wa busara hata kidogo. Hili ni kwa sababu huna habari ya kile Niendacho kufanya, na hujui hata kidogo kile Nifanyacho sasa. Hiyo ndiyo maana Mimi husema kwamba huwezi tu kulinganisha na mkulima mkongwe ambaye hana utambuzi wa maisha ya binadamu ilhali hutegemea baraka kutoka Mbinguni kwa ajili ya ukulima. Wewe ni wa kupuuza sana kuhusu maisha yako mwenyewe na hata wewe hujui kuhusu sifa, na una hata kujijua kidogo zaidi. Wewe ni “mwenye majivuno” mno! Nasikitishwa kweli kuhusu vile wapenda sana starehe au mabibi wadhaifu kama wewe wataweza kuhimili mashambulio ya, pepo na mawimbi makuu zaidi ya dhoruba? Hao wapenda sana starehe hawajali kabisa kuhusu aina ya mazingira ambayo yamewajia sasa. Linaonekana kuwa jambo hafifu—hawana staha kwa mambo haya. Wao si wabaya na hawajioni wenyewe kuwa duni. Badala yake, wao bado wanatembeatembea na kutembea polepole katika “barabara zenye miti kandokando” wakijipungia hewa wenyewe. “Watu” hawa wasiojifunza na wasiojua chochote hawana habari kwa nini Mimi husema mambo haya kwao. Wao hujijua tu wenyewe kidogo sana na mtazamo wa kutaka ugomvi, na baada ya hilo njia zao za uovu hazibadiliki. Baada ya kuondoka Kwangu wao huendelea kukimbia na kuenea pote katika ulimwengu na hutamba na hulaghai. Sura yako hubadilika haraka mno—wewe bado unanidanganya Mimi kwa njia hii. Una ujasiri mno! Na wale mabibi chipukizi wadhaifu ni wa kuchekesha kwa kweli. Wao huyasikia matamshi Yangu muhimu, wao huona mazingira walio ndani na hawawezi kufanya lolote ila kutoa machozi; wao hunengua mwili wao kila mahali kana kwamba wanajaribu kuduwaza. Linachukiza sana! Yeye huona kimo chake mwenyewe na hulala kitandani na hushinda huko, hulia bila kukoma, ni kana kwamba anakaribia kukosa hewa. Kutokana na maneno haya yeye huuona uchanga na uduni wake mwenyewe, na baada ya hilo yeye hujazwa mno na ukanushaji. Yeye hukodoa kwa kutoonyesha hisia, na hakuna nuru katika macho yake; yeye halalamiki, na hanichukii Mimi—yeye ni wa kukanusha sana mpaka hata hasongi. Yeye pia hajifunzi na hajui chochote. Baada ya kuondoka Kwangu yeye mara tena ni mwenye mzaha na wa kucheza, na hicho “kicheko kama kengele ya fedha” ni kama tu “binti mfalme wa kengele ya fedha.” Wao ni wadhaifu mno na vilevile wanaokosa mno kujihurumia! Ninyi nyote, bidhaa zilizoharibika miongoni mwa wanadamu—ninyi mnakosa sana ubinadamu! Ninyi hamjui kujipenda au kujilinda, hamwelewi maana, ninyi hamtafuti njia ya kweli au kupenda nuru ya kweli, na hasa hamjui jinsi ya kujithamini wenyewe. Mmesukuma maneno ya mafunzo Yangu mara kwa mara nyuma ya akili zenu na hata mmeyatumia kwa ajili ya burudani katika wakati wenu wa mapumziko. Ninyi mmeyatumia kila mara kama hirizi yenu wenyewe. Wakati ambapo Shetani hukushitaki, wewe huomba kidogo tu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, wewe hulala, na wakati ambapo wewe huwa na furaha wewe hukimbia kila mahali kama mwenye wazimu. Wakati ambapo Mimi hukukemea, wewe hukubali kwa kichwa na kuinama, lakini wakati ambapo wewe huniacha wewe hucheka kishenzi. Miongoni mwa watu wewe kila mara ndiwe wa juu zaidi na hujawahi kujifikiri mwenyewe kuwa mwenye kiburi zaidi. Wewe kila mara ni mwenye majivuno mno, wa kujiona mno na mwenye kiburi sana. Ni vipi ambavyo aina hiyo ya “kijana wa kiume,” “kijana wa kike,” “mwanamume,” au “bibi” asiyejifunza na asiyejua chochote anaweza kuyachukulia maneno Yangu kama hazina ya thamani? Nitakuuliza zaidi—ni nini ambacho umejifunza kutoka kwa maneno Yangu na kazi Yangu kwa muda huu wote? Hila zako ni janja zaidi? Mwili wako ni mstaarabu zaidi? Mtazamo wako Kwangu ni wa dharau zaidi? Nitakwambia kwa wazi, hii kazi Yangu nyingi kwa kweli imefanya ujasiri wako, ambao ulikuwa ule wa panya, kuwa mkuu zaidi. Woga wako Kwangu hupungua kila siku kwa sababu Mimi ni mwenye huruma sana. Sijawahi kutumia mbinu kali sana kuadhibu mwili wako. Labda vile unavyoona, Nazungumza tu kwa ukali, lakini wakati mwingi Mimi hukutazama kwa tabasamu na Mimi hukukosoa bayana kwa nadra sana. Na hasa ni kwa sababu Mimi kila mara hujali kuhusu udhaifu wako ndiyo imesababisha wewe kunichukulia Mimi kama vile nyoka humchukulia mkulima mwenye huruma. Mimi hupenda kwa kweli ustadi wa wanadamu katika kutathmini watu wengine kwa uangalifu—ni wa kusifika kwa kweli, mzuri sana! Nitakwambia ukweli. Kama una moyo wa uchaji leo au la ni isiyo na maana. Mimi si mwenye woga au wa wasiwasi, lakini Nitakwambia pia wewe “mtu mwenye kipaji” asiyejifunza na asiyejua chochote utaharibiwa mwishowe na ujanja wa kujiona kwako mwenyewe. Wewe ndiwe utakayeteseka, na wewe ndiwe utakayeadibiwa. Singekuwa mpumbavu hivyo kuendelea kufuatana na wewe mpaka jehanamu na kuendelea kuteseka, kwa sababu wewe na Mimi si wa aina moja. Usisahau kwamba wewe ni kiumbe aliyelaaniwa na Mimi, na ambaye hufunzwa na kuokolewa na Mimi. Hakuna chochote ndani yako Ninachotamani sana. Haijalishi wakati ambapo Mimi hufanya kazi, Mimi sipaswi kutii umiliki wa hila wa watu, matukio, au vitu vyovyote. Inaweza kusemwa kwamba mtazamo Wangu kwa, na maoni kuhusu wanadamu yamebaki vilevile kila mara. Sina upendeleo wowote kwako kwa sababu wewe ni kiungo katika usimamizi Wangu; wewe bila shaka huna nguvu kuu nyingi zaidi kuliko kingine chochote. Nakushauri wewe kukumbuka kila mara kwamba wewe si kitu zaidi ya kiumbe tu! Ingawa wewe huishi na Mimi, unapaswa kuijua hali yako na usijione kuwa wa sifa za juu zaidi. Hata kama Sikukosoi wewe au kukushughulikia, na Nakutazama na tabasamu, hili halithibitishi kwamba wewe na Mimi ni wa aina moja. Unapaswa kujua kwamba unatafuta ukweli, wewe mwenyewe siyo ukweli! Lazima ubadilike kulingana na maneno Yangu wakati wowote—huwezi kuepuka hili. Nakushauri ujifunze kitu wakati upo katikati ya nyakati hizi za ajabu, wakati nafasi hii adimu iko hapa, na usijaribu kunidanganya Mimi. Huhitaji kutumia sifa isiyostahilika kunidanganya Mimi. Ninyi kunitafuta Mimi siyo kwa ajili Yangu mwenyewe tu—ni kwa ajili yenu!

kutoka katika “Wale Wasiojifunza na Wasiojua Chochote: Je, Wao si Wanyama?” katika Neno Laonekana katika Mwili

69. Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa huduma ya mwanadamu hupunguzwa taratibu kupitia kwa uzoefu uongezekao na mchakato wa uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake. Mwanadamu akipoteza kile ambacho chaweza kutimizwa kiasili, hawezi kamwe kuitwa mwanadamu, na hafai kusimama kama kiumbe aliyeumbwa au kuja mbele za Mungu na kumtolea huduma. Aidha, hafai kupokea neema ya Mungu au kutunzwa, kulindwa na kukamilishwa na Mungu. Wengi waliopoteza imani ya Mungu hatimaye hupoteza neema Yake. Si kwamba wanachukia makosa yao tu bali pia hueneza wazo kuwa njia ya Mungu si sahihi. Na wale waasi hupinga hata uwepo wa Mungu; itakuwaje watu wenye uasi kama huo waendelee kupata neema ya Mungu? Wanadamu walioshindwa kutekeleza wajibu wao wameasi sana dhidi ya Mungu na wanawiwa mengi na Yeye, lakini wanageuka na kumkong'ota Mungu kwamba ni mkosaji. Je, mwanadamu kama huyo anastahili vipi kufanywa mkamilifu? Je, si huyu ni mmoja wa wale watakaoondolewa na kuadhibiwa? Mwanadamu asiyefanya wajibu wake mbele za Mungu tayari ana hatia ya makosa mazito sana ambayo hata kifo si adhabu stahili, ila bado mwanadamu ana ufidhuli wa kubishana na Mungu na kujilinganisha na Yeye. Pana faida gani kumkamilisha mwanadamu sampuli hiyo? Kama mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo tu ndipo atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa kweli, na ni mwanadamu kama huyu tu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Na wengi wenu je? Mnamtendeaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje wajibu wenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, hamjapokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyahukumu na kuyalinganisha haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna hisia mbovu kunihusu na mko shingo upande. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa hata kidogo? Mnawezaje kuchukuliwa kama kiumbe aliyeumbwa? Je, hamjui wazi mnachopaswa kuonyesha nakuishi kwa kudhihirisha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno Yangu na kazi Yangu, kundi lenu litakuwa la kuadhibiwa. Kamwe hamtapata neema, na hamtakuwa na baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia!

kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

70. Sasa hebu tuangalie dondoo ifuatayo: “Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya sabato” (Mat 12:6-8). “Hekalu” hapa linamaanisha nini? Kwa ufupi, “hekalu” linaashiria jengo refu la kupendeza, na katika Enzi ya Sheria, hekalu lilikuwa ni pahali pa makuhani kumwabudu Mungu. Bwana Yesu aliposema “mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu,” “mmoja” ilikuwa ikirejelea nani? Ni wazi, “mmoja” ni Bwana Yesu katika mwili kwa sababu Yeye tu ndiye aliyekuwa mkuu kuliko hekalu. Na maneno hayo yaliwaambia watu nini? Yaliwaambia watu watoke hekaluni—Mungu alikuwa tayari ameshatoka nje na hakuwa tena akifanyia kazi ndani yake, hivyo basi watu wanafaa kutafuta nyayo za Mungu nje ya hekalu na kufuata nyayo Zake katika kazi Yake mpya. Usuli wa Bwana Yesu kusema haya ilikuwa kwamba chini ya sheria, watu walikuwa wameiona hekalu kama kitu kilichokuwa kikuu zaidi kuliko Mungu Mwenyewe. Yaani, watu waliliabudu hekalu badala ya kumwabudu Mungu, hivyo basi Bwana Yesu akawaonya kutoabudu sanamu, lakini kumwabudu Mungu kwa sababu Yeye ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi. Hivyo basi, alisema: “Naitaka rehema, na siyo sadaka.” Ni wazi kwamba katika macho ya Bwana Yesu, watu wengi sana katika sheria hawakumwabudu tena Yehova Mungu, lakini walikuwa tu wakipitia mchakato wa kutoa sadaka na Bwana Yesu aliamua kwamba mchakato huu ulikuwa ibada ya sanamu. Waabudu sanamu hawa waliliona hekalu kama kitu kikuu, cha juu zaidi kuliko Mungu. Ndani ya mioyo yao kulikuwa tu na hekalu, wala si Mungu, na kama wangelipoteza hekalu, wangepoteza mahali pao pa kukaa. Bila ya hekalu hawakuwa na mahali popote pa kuabudu na wasingeweza kutoa sadaka zao. Mahali pao pa kukaa kama palivyojulikana ndipo walipofanyia shughuli zao kwa jina la kumwabudu Yehova Mungu, na hivyo basi wakaruhusiwa kuishi katika hekalu na kutekeleza shughuli zao binafsi. Ule utoaji sadaka wao kama ulivyojulikana ulikuwa tu kutekeleza shughuli zao za kibinafsi za aibu wakisingizia kwamba walikuwa wanaendesha ibada yao katika hekalu. Hii ndiyo iliyokuwa sababu iliyowafanya watu wakati huo kuliona hekalu kuwa kuu kuliko Mungu. Kwa sababu walilitumia hekalu kama maficho, na sadaka kama kisingizio cha kuwadanganya watu na kumdanganya Mungu, Bwana Yesu alisema haya ili kuwaonya watu. Mkitumia maneno haya kwa wakati wa sasa, yangali bado halali na yenye umuhimu sawa. Ingawa watu wa leo wameweza kupitia kazi tofauti za Mungu kuliko watu wa Enzi ya Sheria walivyowahi kupitia, kiini cha asili yao ni kile kile. Katika muktadha wa kazi leo, watu bado watafanya aina sawa ya mambo kama yale ya “hekalu kuwa kuu kuliko Mungu”. Kwa mfano, watu huona kutimiza wajibu wao kama kazi yao; wanaona kutoa ushuhuda kwa Mungu na kupigana na joka kubwa jekundu kama harakati ya kisiasa ya kulinda haki za kibinadamu, kwa ajili ya demokrasia na uhuru; wao hugeuza wajibu wao ili kutumia weledi wao kuwa ajira, lakini wanachukulia kumcha Mungu na kujiepusha na maovu tu kama kipande cha kanuni ya kidini ya kufuatwa; na kadhalika. Je, maonyesho haya kwa upande wa binadamu hasa hayako sawa na “hekalu ni kuu kumliko Mungu”? Isipokuwa tu kwamba miaka elfu mbili iliyopita, watu walikuwa wakiendeleza shughuli zao za kibinafsi katika hekalu linaloshikika, lakini leo, watu wanaendeleza shughuli zao za kibinafsi katika mahekalu yasiyogusika. Wale watu wanaothamini masharti huona masharti kuwa kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda hadhi huona hadhi kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda ajira zao huziona ajira hizo kuwa kuu zaidi kuliko Mungu na kadhalika—maonyesho yao yote yananifanya Mimi kusema: “Watu humsifu Mungu kuwa ndiye mkuu zaidi kupitia kwa maneno yao, lakini kwa macho yao kila kitu ni kikuu zaidi kuliko Mungu.” Hii ni kwa sababu punde tu watu wanapopata fursa katika njia yao ya kumfuata Mungu ili kuonyesha vipaji vyao, au kuendelea na shughuli zao binafsi za kibiashara au ajira yao binafsi, wanakuwa mbali na Mungu na kufanya kwa bidii ajira wanayoipenda. Kuhusiana na kile ambacho Mungu amewaaminia, na mapenzi Yake, mambo hayo yote yametupiliwa mbali kitambo. Katika hali hii, ni nini tofauti baina ya watu hawa na wale wanaoendesha biashara zao katika hekalu miaka elfu mbili iliyopita?

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

71. Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, na kula chakula cha bure, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao hula chakula cha bure katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila na njama dhidi ya ndugu zao, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?

kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

72. Wanadamu dhalimu! Kufumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye amejirudi. Watu wanatenda matendo kwa ajili ya familia zao, watoto wao, kazi zao, matarajio yao ya baadaye, cheo, majivuno, na pesa, kwa sababu ya chakula, mavazi, na mwili, lakini kuna yeyote ambaye matendo yake kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao wanatenda kwa ajili ya Mungu, ni wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni watu wangapi hawatendi kutokana na maslahi yao? Ni wangapi wasiokandamiza na kutenganisha wengine ili kulinda cheo chao wenyewe? Na hivyo, Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, na mahakimu wakatili wasiohesabika wamemhukumu Mungu na mara nyingine wakamsulubisha msalabani. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu kwa kweli?

kutoka katika “Waovu Hakika Wataadhibiwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

73. Je, mliwahi kutambua kile mfanyacho leo—yaani, kufanya ghasia ulimwenguni, kupanga njama dhidi ya nyinyi kwa nyinyi, kudanganyana, kutenda kwa uongo, kwa siri na kwa ukavu wa macho, kutojua ukweli, kuwa wasio waaminifu na wadanganyifu, kutenda ubembelezaji, nyinyi kujiona daima kuwa waadilifu na bora zaidi kuliko wengine, kuwa wenye kiburi, na kutenda kikatili kama wanyama wa mwitu milimani na kwa fujo kama mfalme wa wanyama—huu ndio mfano wa mwanadamu? Nyinyi ni fidhuli na wasio na busara. Hamjawahi kuliona neno Langu kuwa hazina, lakini badala yake mmechukua mtazamo wa dharau. Kwa njia hii, mafanikio, maisha ya kweli ya binadamu, na matumaini mazuri yangetoka wapi? Je, wazo lako badhirifu litakuokoa kwa kweli kutoka kwa kinywa cha chui? Kweli litakuokoa kutoka kwa moto unaowaka? Je, ungekuwa umeanguka hadi hapa iwapo kwa kweli ungeiona kazi Yangu kuwa kitu cha thamani kubwa mno? Inaweza kuwa kwamba majaliwa yako kweli hayawezi kubadilishwa? Je, uko tayari kufa na majuto kama haya?

kutoka katika “Asili na Utambulisho wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

74. Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?

kutoka katika “Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili

75. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Kweli mnajua vyema kwamba hamstahili hata kidogo. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?

kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

76. Sasa Naishi duniani na Naishi miongoni mwa wanadamu. Wanadamu wote wanashuhudia kazi Yangu na kutazama matamko Yangu, na pamoja na hili Natoa ukweli kwa kila mfuasi Wangu ili waweze kupokea uzima kutoka Kwangu na hivyo apate njia anayoweza kufuata. Kwa maana Mimi ni Mungu, mpaji wa uhai. Katika miaka mingi ya kazi Yangu, mwanadamu amepokea vitu vingi na kujinyima vitu vingi, lakini bado Nasema kuwa mwanadamu haniamini kikamilifu. Kwa maana mwanadamu anakubali kijuujuu tu kuwa Mimi ni Mungu lakini hakubaliani na ukweli Ninaounena, sembuse kuuweka ukweli katika matendo Ninavyohitaji kwake. Hiyo ni kusema, mwanadamu anakubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio ule wa ukweli; mwanadamu hukubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio wa uzima; mwanadamu anakubali tu jina la Mungu, lakini sio kiini Chake. Kutokana na ari yake, mwanadamu amekuwa chukizo mbele Zangu. Kwa kuwa mwanadamu anatumia tu maneno yanayofurahisha masikio kunihadaa, na hakuna anayeniabudu kwa moyo wa kweli. Maneno yenu yanabeba majaribu ya ibilisi. Na maneno yenu ni yenye kiburi kupindukia, ni vile tu kama yamesemwa na malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yamechakaa; tamaa zenu zisizo na kiasi na nia zenu zenye tamaa ni za kukera zikisikizwa. Nyote mmegeuka nondo katika nyumba Yangu, vyombo vya kukataliwa na chukizo. Kwa maana hapana kati yenu ambao ni wapenda ukweli, bali ni wanadamu wanaopenda baraka tu, walio na matamanio ya kupaa mbinguni, na ya kumwona Kristo anapoonyesha nguvu Zake duniani. Lakini mmewahi kuwaza jinsi mwanadamu kama ninyi, aliyepotoka sana, na asiyejua kabisa Mungu ni nini, angestahili kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kustahili kuuona uzuri wa ukuu usio na kifani? Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjawahi kunena maneno ya ukweli Kwangu, wala maneno matakatifu, wala maneno ya kunitii baada ya kulipitia neno Langu. Hatimaye, hii imani yenu ni ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali, mawazo yenu yamejaa mali ya kilimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na vyema zaidi, vitu zaidi vya raha. Vile vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi, wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), mwanao, bintiyo au mlacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata muvike miili yenu ya nje kwa ufahari, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri kila mara, mnafanya kazi na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna yeyote anayeshughulika wala kufikiria kuhusu mapenzi Yangu. Ni nini ambacho bado mnatarajia kufaidi kutoka Kwangu?

kutoka katika “Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

77. Mioyo yenu imejaa maovu, usaliti na uongo na hivyo kuna kiwango kipi cha uchafu katika upendo wenu? Mnafikiri kuwa mmeacha ya kutosha kwa ajili Yangu; mnafikiri kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha. Ila ni kwa nini basi maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo daima? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kunitupa kando. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanihudumia, na bado hamnichi. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, lakini bado hamjawahi kutenda Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuchukuliwa kama upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka mingi sana ya kazi na maneno yote mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hili halistahili kuangaliwa tena kwa makini?

kutoka katika “Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

78. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya kiini cha maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli una imani ya kutembea njia hii, basi zidi kuifuata. Iwapo huwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kwenda zako kabla hujachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Huna uaminifu ama utii hata kidogo, ama moyo ulio na kiu ya haki na ukweli. Na wala huna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yako mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Huwezi kushika unachopaswa wala kusema unachopaswa. Huwezi kuweka katika vitendo kile ambacho unapaswa, na huwezi kutekeleza kazi unayopaswa. Huna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio unalopasa. Hujavumilia mateso unayopaswa kuwa umevumilia, na huna imani unayopaswa kuwa nayo. Huna sifa yoyote kabisa; una heshima binafsi ya kuendelea kuishi? Nakuhimiza kwamba ni bora kufunga macho kwa mapumziko ya milele, hivyo kumtoa Mungu katika kujishughulisha nawe na kuvumilia mateso kwa ajili yako. Unaamini katika Mungu lakini bado hujui mapenzi Yake; unakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado huwezi kukidhi mahitaji Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado humjui, na kuishi ingawa huna lengo la kujaribu kufikia. Huna maadili na huna madhumuni. Unaishi kama mwanadamu lakini huna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Unafikiriwaje kuwa wanadamu? Unaamini katika Mungu lakini unamdanganya. Zaidi ya hayo, unachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, huonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Huwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu ya chini zaidi. Kwa hivyo unawezaje kufikiriwa kuwa mwanadamu? Chakula unachokula na hewa unayopumua vimetoka kwa Mungu, unafurahia neema Yake, na bado mwishowe, huna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, umekuwa mtu asiye na maana anayempinga Mungu. Si basi wewe ni mnyama asiye bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kukuliko wewe?

kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

79. Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele.

kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

80. Ni nini ambacho kila mmoja kati yenu, awe mwanamme ama mwanamke, hutolea uangalifu wake kila siku? Je mnajua yule mnayemtegemea ili kula? Tazama mavazi yako, tazama kile umevuna mikononi mwako, sugua tumbo lako—ni nini matunda ya gharama ya damu na jasho ambayo umelipa? Wewe bado unafikiri kuenda kutalii sehemu maarufu, wewe bado unafikiri kupamba mwili wako wenye uvundo—ni nini thamani ya haya? Unaulizwa kuwa wa kawaida, lakini leo wewe si tu wa kawaida, uko kinyume. Ni vipi mtu wa namna hii anaweza kuthubutu kuja mbele Yangu? Na ubinadamu kama huu, kujionyesha na kufichua mwili wako, kila mara kuishi kati ya tamaa ya mwili, wewe sio mzawa wa mapepo wachafu na roho wabaya? Sitaruhusu pepo mchafu kama huyo kusalia kwa muda mrefu! Na usifikiri kwamba sijui ni nini unachofikiria moyoni mwako. Unaweza kudhibiti vikali tamaa na mwili wako, lakini Singeweza kujua fikira iliyo ndani ya moyo wako na yote ambayo macho yako yatamani? Je, nyinyi wanawake wadogo hamjitayarishi kupendeza kama maua ili kuonyesha miili yenu? Wanaume ni wa faida gani kwenu? Wanaweza kweli kuwaokoa nyinyi kutoka ziwa la mateso? Na nyinyi wanaume wapenda sana starehe nyote mnavaa kujifanya muonekane waungwana na wenye heshima—sio ili kuonyesha sura zenu? Na ni nani mnayemfanyia haya? Wanawake ni wa manufaa gani kwenu? Wao sio chanzo cha dhambi zenu? Nyinyi wake na waume, Nimenena maneno mengi kwenu, ilihali mmetekeleza machache kwa hayo. Masikio yenu ni mazito, macho yenu yameingia giza, na nyoyo zenu ni ngumu, kiasi kwamba hakuna chochote ila tamaa katika miili yenu; mmetegwa ndani yake, hamuwezi kutoroka. Nani anayetaka kwenda mahali popote karibu na nyinyi mabuu, wanaofurukuta kwa taka na uchafu? Msisahau kwamba nyinyi sio kitu zaidi ya wale ambao Nimewainua kutoka kwenye rundo la samadi, kwamba mwanzoni, hamkuwa na ubinadamu wa kawaida. Ninachoomba kwenu ni ubinadamu wa kawaida ambao hamkuwa nao awali; Siulizi kwamba muonyeshe tamaa yenu, au kwamba muipe uhuru miili yenu iliyooza, ambayo imefundishwa na ibilisi kwa miaka mingi. Mnapojivisha nguo hivi, hamwogopi kuwa mtategwa zaidi milele? Je, hamjui kwamba kiasili mlikuwa wa dhambi? Je, hamjui kwamba miili yenu imejazwa na tamaa? Ni kiasi kwamba tamaa zenu hata zimepenya kutoka kwenye mavazi yenu, zikifichua hali yenu kama pepo mchafu, mbaya asiyevumilika. Je, si hii ndiyo iliyo wazi kabisa kwenu nyote? Mioyo yenu, macho yenu, midomo yenu—je, si yote yamechafuliwa na pepo wachafu? Je, hayo si machafu? Unadhani kwamba mradi tu usipofanya chochote kilicho kiovu,[j] wewe ni mtakatifu zaidi; unadhani kuvaa vizuri kunaweza kufunika nafsi zenu duni—hakuna uwezekano wa hilo! Ninawashauri kuwa wa kweli zaidi: msiwe wadanganyifu na bandia, wala msijitembeze. Mnaringiana tamaa yenu, lakini yote mtakayopata ni mateso ya milele na adabu katili! Je, una haja gani kuonyeshana mapenzi na kuwa katika mapenzi? Je! Huu ni uadilifu wenu? Je, hii inawafanya wenye nguvu? Ninawachukia wale miongoni mwenu wanaotenda tiba ya uchawi na kushiriki katika usihiri, Nawachukia vijana kati yenu wanaopenda miili yao wenyewe. Itakuwa vyema mkijizuia, kwa kuwa leo Ninaomba umiliki ubinadamu wa kawaida, sio kwamba uringe kwa sababu ya tamaa yako. Daima mnachukua fursa yoyote mnayoweza, kwa kuwa miili yenu ni maridhawa sana, na tamaa yenu ni kubwa sana!

kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

81. Wakati wa kazi Yangu, daima nyinyi hutenda dhidi Yangu, hamyatii maneno Yangu kamwe. Ninafanya kazi Yangu, na wewe unafanya kazi yako mwenyewe, unatengeneza ufalme wako mdogo mwenyewe—nyinyi kundi la mbweha na mbwa, kila kitu mnachofanya ni dhidi Yangu! Nyinyi daima mnajaribu kuwaleta wale wanaowapenda tu katika kumbatio lenu—uko wapi uchaji wenu? Kila kitu mnachofanya ni kidanganyifu! Hamna utii au uchaji, kila kitu mnachofanya ni udanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hao wanaweza kuokolewa? Wanaume zinzi, wa kiasherati daima hutaka kuwavuta kwao wale makahaba wabembe kwa ajili ya raha yao wenyewe. Sitawaokoa mapepo wenye uasherati kama hao, Nawachukia ninyi mapepo wachafu, uasherati wenu na kupiga bemba kwenu kumewatumbukiza kuzimu—mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi pepo mchafu na roho wabaya ni waovu sana! Nyinyi ni wa kuchukiza! Takataka kama nyinyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi bado wanaweza kuokolewa? Ukweli huu, njia hii, na maisha haya hayapendezi kwenu; mnavutiwa na dhambi, pesa, hadhi, umaarufu na faida, ridhaa za mwili, maumbile mazuri ya wanaume na ubembe wa wanawake. Ni nini kinachowapa sifa zinazostahili kuingia katika ufalme Wangu? Taswira yenu ni kubwa zaidi kuliko Mungu, hali yenu ni ya juu zaidi kuliko Mungu, kutosema chochote cha sifa yenu kati ya wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hamjabadilika kuwa malaika mkuu? Wakati mwisho wa watu unafichuliwa, ambao pia ni wakati kazi ya wokovu inafikia kikomo, wengi wenu mtakuwa maiti ya maiti ambayo haiwezi kuokolewa na lazima muondolewe.

kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

82. Wanadamu ni wanyonge wasio na thamani kwa sababu hawajithamini. Kama hata hawajipendi, bali hujikandamiza, hili halionyeshi kwamba hawana thamani? Wanadamu ni kama mwanamke mwovu ambaye hujihadaa na ambaye hujitoa kwa wengine kwa hiari kuingiliwa bila heshima. Lakini hata hivyo, bado hawajui vile walivyo duni. Wao hufurahia kuwatumikia wengine, au kuzungumza na wengine, kujiweka chini ya utawala wa wengine; huu kweli si uchafu wa wanadamu? Ingawa Sijapitia maisha miongoni mwa wanadamu, kwa vile Sijapitia kweli maisha ya binadamu, Nina ufahamu kamili wa kila mwendo, kila hatua, kila neno, na kila kitendo cha mwanadamu. Naweza hata kuwaweka wanadamu wazi mpaka waaibike kabisa, kiasi cha kutoweza tena kuthubutu kuonyesha hila zao na kutoweza tena kuthubutu kujiachilia kwa tamaa zao. Kama konokono ambaye hurudi ndani ya kombe lake, hawathubutu tena kuonyesha hali zao mbaya. Kwa sababu wanadamu hawajijui, dosari yao kubwa sana ni kuonyesha kwa hiari haiba yao mbele ya wengine, wakionyesha sura yao mbaya; Hiki ni kitu ambacho Mungu hukichukia zaidi. Kwa sababu mahusiano kati ya watu si ya kawaida, na hakuna mahusiano ya kawaida ya mtu mmoja na mwingine kati ya watu, sembuse kuwa na uhusiano wa kawaida[k] na Mungu. Mungu amesema mengi sana, na kwa kufanya hivyo lengo Lake kuu ni kumiliki nafasi ndani ya mioyo ya wanadamu, kuwafanya watu waondoe sanamu zote ndani ya mioyo yao, ili Mungu aweze kuwatawala wanadamu wote na Atimize lengo Lake la kuwa duniani.

kutoka katika “Sura ya 14” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

83. Nimefanya kazi na kusema kwa njia hii miongoni mwenu, Nimetumia nguvu na juhudi, ila ni wakati upi kamwe mmewahi kusikiliza kile Ninachowaambia wazi wazi? Ni wapi mmeniinamia Mimi, Mwenyezi? Kwa nini mnanitendea namna hii? Kwa nini kila kitu mnachokisema na kufanya huchochea hasira Yangu? Kwa nini, mioyo yenu imeshupaa? Je, Nimewahi kuwapiga kumbo kamwe? Kwa nini hamfanyi kitu chochote kingine ila kunifanya mwenye huzuni na wasiwasi? Mnasubiri siku ya ghadhabu Yangu, Yehova, kuja juu yenu? Je, mnanisubiri Mimi kutuma hasira kwenu iliyochochewa na makosa yenu? Si kila kitu Ninachokifanya ni kwa ajili yenu? Ilhali kila wakati mmenitendea Mimi, Yehova, kwa njia hii: kuiba sadaka Yangu, kuchukua sadaka ya madhabahu Yangu nyumbani kulisha watoto wa mbwa mwitu na vitukuu vyake katika makazi ya mbwa mwitu; watu wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wakikabiliana na mtazamo wa hasira kwa panga na mikuki, kurusha maneno ya Mimi, Mwenyezi, kwenye choo kuwa machafu kama kinyesi. Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu umekuwa unyama! Mioyo yenu kwa muda mrefu imegeuka kuwa jiwe. Je, hamjui kwamba siku Yangu ya ghadhabu itakapofika itakuwa ndio wakati Nitakapokuhukumu mabaya mliyotenda dhidi Yangu leo, Mwenyezi? Je, mnafikiri kwamba kwa kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa kutupa maneno Yangu katika matope na kutoyasikiza—unafikiri kwamba kwa kutenda namna hii nyuma Yangu mnaweza kutoroka macho Yangu ya ghadhabu? Je, hamjui kwamba mlishaonekana na macho Yangu, Mimi Yehova, wakati mliiba sadaka Yangu na kutamani mali Yangu? Je, hamjui kwamba wakati mliiba sadaka Yangu, ilikuwa mbele ya madhabahu ambapo dhabihu hutolewa? Mnawezaje kujiamini wenyewe mlivyo wajanja kutosha kunidanganya Mimi kwa njia hii? Ghadhabu Yangu kali ingewezaje kuondoka kutoka katika dhambi zenu za kuchukiza? Ghadhabu Yangu yenye hasira ingepitaje juu ya matendo yenu maovu? Maovu mnayotenda leo hayawafungulii njia yenu kutokea, bali huhifadhi kuadibu kwa ajili ya kesho yenu; yanachochea kuadibu Kwangu, Mwenyezi, kwenu. Matendo yenu maovu na maneno yenu mabaya yangewezaje kuepuka kuadibu Kwangu? Maombi yenu yangeyafikiaje masikio Yangu? Ningefunguaje njia kwa ajili ya udhalimu wenu? Ningewezaje kuyatupilia mbali matendo yenu maovu ya kunikaidi? Ingewezekanaje Nisizikate ndimi zenu ambazo ni za sumu kama ya nyoka? Hamniombi msaada kwa ajili ya haki yenu, lakini badala yake mnahifadhi ghadhabu Yangu kama matokeo ya udhalimu wenu. Ningewezaje kuwasamehe? Katika macho Yangu, Mwenyezi, maneno na matendo yenu ni machafu. Macho Yangu, Mwenyezi, huona udhalimu wenu kama kuadibu kusikolegea. Kuadibu Kwangu kwa haki na hukumu vingeondokaje kwenu? Kwa sababu mmenitendea hivi, na kunifanya mwenye huzuni na ghadhabu, Ningewaachaje nyinyi muepe kutoka mikono Yangu na muondoke katika siku ambayo Mimi, Yehova, Nawaadibu na kuwalaani wewe? Je, hamjui kwamba maneno yenu yote mabaya na matamko tayari yamefikia masikio Yangu? Je, hamjui kwamba udhalimu wenu tayari umelilaghai vazi Langu takatifu la haki? Je, hamjui kwamba makosa yenu tayari yameichochea hasira Yangu kali? Je, hamjui kwamba kwa muda mrefu mmeniacha Nikitokota, na kwa muda mrefu mmeujaribu uvumilivu Wangu? Je, hamjui kwamba tayari mmeshauharibu mwili Wangu kuwa matambara? Nimevumilia mpaka sasa, kiasi kwamba Natoa hasira Zangu, kutokuwa mvumilivu kwenu tena. Je, hamjui kwamba matendo yenu maovu tayari yamefikia Macho Yangu, na kwamba kilio changu tayari kimefikia masikio ya Baba Yangu? Angewaruhusu vipi mnitendee Mimi jinsi hii? Kuna kazi yoyote Ninayofanya ndani yenu isiyo kwa ajili yenu? Ilhali nani kati yenu amekuwa na upendo zaidi kwa kazi Yangu, Yehova? Ningeweza kutokuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Baba Yangu kwa sababu Mimi ni mnyonge, na kwa sababu ya uchungu Nilioupitia? Je, hamwelewi Moyo Wangu? Nasema na ninyi kama Yehova alivyofanya; je, Sijajinyima mengi kwa ajili yenu? Hata ingawa Niko tayari kuvumilia mateso haya yote kwa ajili ya kazi ya Baba Yangu, ni jinsi gani nyinyi mnaweza kuachwa huru kutokana na kuadibu ambako Nawaleteeni kama matokeo ya mateso Yangu? Je, hamjanifurahia kwa wingi sana? Leo, Nimetolewa kwenu na Baba Yangu; hamfahamu kwamba mnafurahia zaidi ya maneno Yangu mengi? Je, hamjui kwamba maisha Yangu yalibadilishwa na maisha yenu na mambo yote mnayofurahia? Je, hamjui kwamba Baba Yangu alitumia maisha Yangu kupigana na Shetani, na kwamba Yeye pia ametoa maisha Yangu kwenu, na kusababisha nyinyi kupokea mara mia zaidi, na kuwaruhusu kuepuka majaribu mengi? Je, hamjui kwamba ni kwa njia ya Kazi Yangu kwamba mmepewa msamaha kutokana na vishawishi vingi, na kuadibu kwingi kukali? Je, hamjui kwamba ni kwa sababu Yangu tu ndio Baba Yangu anawaruhusu kufurahia mpaka sasa? Jinsi gani nyoyo zenu zimebaki ngumu leo, kama kwamba zimekuwa sugu? Maovu mnayoyatenda leo yangeepukaje siku ya ghadhabu itakayofuata kuondoka Kwangu duniani? Ningewezaje kuwaruhusu wale ambao ni wenye mioyo migumu kuepuka hasira ya Yehova?

kutoka katika “Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

84. Ninyi, minyoo wadogo wenye uvundo mnaiba sadaka kutoka kwa madhabahu ya Mimi, Yehova; kwa kufanya hivyo, mnaweza kuokoa majina yenu yaliyoharibika, yenye kasoro kuwa wateule wa Israeli? Ninyi ni mafukara wasio na haya! Hizo sadaka juu ya madhabahu zilizotolewa Kwangu na watu, kuonyesha hisia karimu kutoka kwa wale ambao hunicha Mimi. Ni za udhibiti Wangu na za matumizi Yangu, kwa hiyo inawezekanaje wewe kuniibia Mimi hua wadogo waliotolewa na watu? Je, huogopi kuwa Yuda? Je, huogopi nchi yako kuwa “konde la damu”? Wewe kitu kisicho na haya! Unadhani kwamba hua waliotolewa na watu wote ni wa kustawisha tumbo la wewe buu? Kile ambacho Nimekupa ni kile ambacho Nimefurahia na kuwa radhi kukupa wewe; kile ambacho Sijakupa kiko chini ya Mamlaka Yangu, na huwezi tu kuiba sadaka Yangu. Yule Anayefanya kazi ni Mimi, Yehova—Bwana wa uumbaji, na sababu ya watu kutoa sadaka ni Mimi. Unadhani kwamba ni fidia ya kukimbia kila mahali ambako wewe hufanya? Wewe kwa kweli ni usiye haya! Ni nani ambaye unamkimbilia kila mahali? Je, si kwa ajili yako mwenyewe? Kwa nini wewe huiba sadaka Zangu? Kwa nini wewe huiba pesa kutoka kwa mfuko Wangu wa pesa? Je, wewe si mwana wa Yuda Iskariote? Sadaka Zangu, za Yehova, ni za kufurahiwa na makuhani. Je, wewe ni kuhani? Wewe huthubutu kula kwa kujisikia sadaka Zangu na hata unazitandaza juu ya meza; huna thamani yoyote! Wewe fukara asiye na thamani! Moto Wangu, wa Yehova, utakuteketeza wewe!

kutoka katika “Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili

85. Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ndiye mtu mwovu zaidi na mwenye nia mbaya zaidi duniani. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa ujanja? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja wenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake; vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati, na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.

kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

86. Nimeeleza maneno mengi sana, na pia nimeeleza mapenzi Yangu na tabia, lakini hata hivyo, bado watu hawana uwezo wa kunijua Mimi na kuniamini. Au, inaweza kusemwa, bado hawana uwezo wa kunitii. Wale wanaoishi katika Biblia, wale wanaoishi katika sheria, wale wanaoishi juu ya msalaba, wale ambao wanaishi kwa mujibu wa mafundisho, wale wanaoishi miongoni mwa kazi Ninayofanya leo—yupi kati yao analingana na Mimi? Ninyi mnafikiria tu kupokea baraka na tuzo, na hamjawahi kamwe kufikiria jinsi ya kulingana na Mimi, au jinsi ya kujizuia wenyewe kutoka katika uadui na Mimi. Nimeaibishwa sana na nyinyi, kwa kuwa Nimewapa mengi sana, ilhali Mimi Nimepokea kidogo sana kutoka kwenu. Udanganyifu wenu, kiburi chenu, tamaa yenu, tamaa yenu yenye fujo, usaliti wenu, kuasi—lipi kati ya haya linaweza kujificha kutoka kwa macho Yangu? Mnafanya mzaha na Mimi, mnanidanganya Mimi, mnanitusi, mnanilaghai, mnanilazimisha, mnapata sadaka kutoka Kwangu kwa nguvu—ni jinsi gani tabia ya kudhuru kama hii itaepuka ghadhabu Yangu? Udhalimu wenu ni thibitisho la uadui wako Kwangu, na ni thibitisho la uwiano wenu na Mimi. Kila mmoja wenu anaamini mwenyewe akilingana na Mimi, lakini ikiwa ni hivyo, basi ni kwa nani ushahidi huu dhahiri unatumika? Mnaamini wenyewe kwamba mnao ukweli wa juu sana na uaminifu Kwangu. Mnafikiri kwamba nyinyi ni wema sana, wenye huruma sana, na mmetoa sana Kwangu. Mnafikiri kwamba mmefanya vya kutosha kwa ajili Yangu. Bado hamjawahi kulinganisha imani hizi dhidi ya tabia zenu wenyewe? Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu atakayesamehewa kutoka kwa hayo, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe. Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu? Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo.

kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

87. Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hujitahidi kupata mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii hasa, wengi kati yenu wanajaribu daima kujipendekeza kwa Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu aliye ndani ya mioyo yenu. Hiyo ni kusema, Mungu mnayemwabudu, Mungu asiye dhahiri mnayempenda, hayupo kabisa. Kinachonifanya niseme haya kwa uhakika ni kwamba mko mbali sana na Mungu wa kweli. Uaminifu mnaomiliki unatokana na kuwepo kwa sanamu mioyoni mwenu, na kunihusu Mimi, Mungu anayeonekana kama asiye mkubwa wala mdogo machoni penu, mnachofanya ni kunikiri kwa maneno tu. Ninaposema juu ya umbali wenu mkubwa kutoka kwa Mungu, Ninamaanisha jinsi mlivyo mbali sana na Mungu wa kweli, ilhali Mungu asiye dhahiri Anaonekana kuwa karibu. Nisemapo “asiye mkubwa,” inamaanisha jinsi Mungu mnayemwamini siku ya leo anaonekana tu kuwa mwanadamu asiye na uwezo mkubwa; mwanadamu asiye wa fahari sana. Na Nisemapo, “asiye mdogo,” inamaanisha kuwa ingawa mwanadamu huyu hawezi kuita upepo na kuamuru mvua, hata hivyo Anaweza kumwita Roho wa Mungu kufanya kazi inayotingisha mbingu na dunia, hivyo kumchanganya mwanadamu kabisa. Kwa nje, nyote mnaonekana kuwa watiifu sana kwa huyu Kristo aliye duniani, lakini kwa kiini hamna imani Kwake wala kumpenda. Ninachomaanisha ni kwamba yule mliye na imani kwake kwa kweli ni yule Mungu asiye dhahiri katika hisia zenu, na yule kweli mnayempenda ni Mungu mnayemtamani usiku na mchana, lakini bado hamjamwona kamwe kibinafsi. Na kuhusu huyu Kristo, imani yenu ni sehemu tu, na upendo wenu Kwake si kitu. Imani inamaanisha imani na kusadiki; upendo unamaanisha kusujudu na kusifu ndani ya mioyo yenu, bila kuondoka. Lakini imani yenu na upendo wenu kwa Kristo wa siku ya leo vimepunguka chini ya hili. Ikujapo kwa imani, mna imani Kwake jinsi gani? Ikujapo kwa upendo, mnampenda jinsi gani? Hamjui kabisa kuhusu tabia Yake, sembuse kiini Chake, hivyo ni jinsi gani kwamba mna imani Kwake? Uko wapi uhalisi wa imani yenu Kwake? Mnampenda jinsi gani? Uko wapi uhalisi wa upendo wenu Kwake?

kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

88. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna anayemchukulia kama mwanadamu wa kawaida mwenye kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao humtendea kikawaida wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa “Kristo wa kweli.” Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.

kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

89. Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao huenda hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa “kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani” na “kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake.” Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu ananiweka katika mazingira mapya, mimi daima hutii na silalamiki na aidha siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zozote nilizopewa na Mungu mimi hufanya kadri ya uwezo wangu na kamwe mimi si mvivu. Kama ndivyo hali, Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na Yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Saa mbili? Imani yenu inaweza kuwa ya kustahili sifa, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia, na akili yako isiyotii na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena, malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako duni utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama Yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi. Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?

kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

90. Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, ila kikundi cha washirika ambao wanaopigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha moyo?

kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

91. Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote, kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa. Mamlaka haya ni uungu Wake, yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe, ambayo huamua utambulisho Wake. Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe; haijalishi upande Anaosimama Akiongea na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu, haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe. Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vile vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu. Kama Kristo hangekuwa mwenye umbo la ubinadamu wala nia ya kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe aliyeumbwa, lakini badala yake kumiliki ubinadamu mkuu, basi kuna uwezekano hakungekuwa na uasi katika mwanadamu yeyote. Sababu ya binadamu kuwa tayari kuamini katika Mungu Asiyeonekana mbinguni ni kwa sababu Mungu mbinguni hana ubinadamu na Yeye hana sifa ya kiumbe hata moja. Hivyo binadamu siku zote humchukua Yeye kwa heshima kubwa, lakini anayo tabia ya dharau kwa Kristo.

kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

92. Inapofika katika swala la imani, watu wengi hufikiri kwamba wanamfuata Mungu kwa sababu wako na imani, la sivyo hawangevumilia mateso hayo. Basi Nakuuliza hivi: Ni kwa nini humheshimu Mungu ilhali unaamini kuwepo Kwake? Ni kwa nini, basi, haumchi Mungu moyoni mwako iwapo unaamini kuwa Mungu Yupo? Unakubali kuwa Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, basi ni kwa nini uwe na dharau Kwake? Kwa nini unatenda bila heshima Kwake? Ni kwa nini unamhukumu wazi wazi? Ni kwa nini siku zote unachunguza Yeye aliko? Mbona usijisalimishe katika mipango Yake? Ni kwa nini hutendi kulingana na neno Lake? Ni kwa nini unamhadaa na kumpokonya matoleo Yake? Ni kwa nini unazungumza katika nafasi ya Kristo? Ni kwa nini unatoa hukumu ya kubaini iwapo kazi Yake na neno Lake ni ya kweli? Mbona unathubutu kumkufuru Yeye kisiri? Ni mambo haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?

Kila sehemu ya usemi na tabia zenu hufichua dalili za kutoamini katika Kristo ulizobeba ndani yako. Nia na malengo yenu kwa yale mnayoyafanya yamejaa kutoamini; hata hiyo hisi itokayo kwa macho yenu imetiwa doa na dalili hizi. Kwa maneno mengine, kila mmoja wenu, katika kila dakika ya kila siku, amebeba vipengele vyenu vya kutoamini. Hii ina maana kuwa kila wakati mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu iliyo ndani ya mishipa yenu imechanganyika na kutomwamini Mungu Aliyepata mwili. Kwa hivyo, Ninasema kwamba nyayo mnazoziwacha katika njia ya imani katika Mungu si nyingi. Safari yenu katika njia ya kumwamini Mungu haina msingi mzuri, na badala yake mnafanya kazi bila ya kujali matokeo yake. Nyinyi huwa na shaka na neno la Kristo na huwezi kulitia katika matendo mara moja. Hii ndio sababu ya nyinyi kutokuwa na imani katika Kristo, na daima kuwa na fikira kumhusu Kristo ndio sababu nyingine ya nyinyi kutoamini Kristo. Kuwa na shaka kila mara kuhusu kazi ya Kristo, kuacha neno Lake kuangukia sikio lisilosikia, kuwa na maoni kwa kila kazi inayofanywa na Kristo na kutoifahamu vizuri kazi hiyo, kuwa na ugumu wa kutupilia mbali fikira zako hata baada ya nyinyi kupewa sababu za kufanya vile, na kadhalika; hizi zote ni dalili za kutoamini zilizochanganyika ndani ya mioyo yenu. Ingawa mnafuata kazi ya Kristo na kamwe hubaki nyuma, kuna uasi mwingi uliochanganyika ndani ya mioyo yenu. Uasi huu ni doa la uchafu katika imani yenu kwa Mungu. Pengine hamkubaliani na haya, lakini iwapo huwezi kutambua nia yako kutoka kwayo, basi wewe ndiwe utakayeangamia. Kwa maana Mungu hustawisha wale wanaomwamini kwa kweli pekee, wala sio wale walio na shaka na hasa wale wanaomfuata shingo upande licha ya kutowahi kuamini kuwa Yeye ni Mungu.

kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

93. Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye dharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

94. Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa ulilazimishwa. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

95. Kwa wakati huu, kuna kutoamini kwingi sana ndani yenu. Jaribu kuangalia kwa makini ndani yako na kwa hakika mtajionea jibu mwenyewe. Unapopata jibu halisi, basi utakubali kuwa wewe kweli si muumini wa Mungu, bali ni mdanganyifu, unayekufuru, unayemsaliti, na usiye mwaminifu kwa Mungu. Kisha utagundua kuwa Kristo si mwanadamu, ila ni Mungu. Siku hiyo itakapowadia, basi utamheshimu, utamcha na utampenda kwa dhati Kristo. Kwa sasa, imani yenu ni asilimia thelathini tu ya moyo wenu, ilhali asilimia sabini zimekumbwa na shaka. Tendo lolote likifanywa na sentensi yoyote ikitamkwa na Kristo vyaweza kusababisha muwe na fikira na maoni kumhusu Yeye. Fikira na maoni haya hutokana na kutokuwa na imani kabisa ndani Yake. Mnamtamani na kumcha tu Mungu msiyemwona aliye mbinguni lakini hauna haja na Kristo Anayeishi duniani. Hii pia si ni ukosefu wa imani? Mnamtamani tu Mungu Aliyefanya kazi kitambo kile lakini hutaki kukumbana na Kristo wa leo. Hizi ndizo huwa “imani” zilizochanganyika katika mioyo yenu isiyomwamini Kristo wa leo. Sikuchukulii kwa hali ya chini kwa maana ndani yako mna kutoamini kwingi, ndani yenu mna uchafu mwingi sana ambao lazima uchunguzwe kwa kina. Madoa na uchafu huu ni ishara kuwa huna imani hata kidogo; ni alama za ninyi kumkana Kristo na huonyesha kuwa nyinyi ni msaliti wa Kristo. Hiyo ni kama kitambaa kinachofunika ufahamu wenu wa Kristo, kizuizi cha nyinyi kupatwa na Kristo, kitu kinachowakinga kulingana na Kristo, na dhihirisho kuwa Kristo Hawatambui.

kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

96. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na asiye mwaminifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa bila moyo wa ukarimu na upendo wema kama tu binadamu wa kawaida. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na asili yenye huruma na ukarimu ziko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu ni kitu ambacho mwanadamu huwekea matumaini yake ya mazuri na mema, na mtu maarufu aliyebuniwa na mwanadamu. Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu huyu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ifikapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ifikapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani. Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni haathiriwi na hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana motisha za kibinafsi tu na Hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande mdanganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni. Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa msimamo wa wadhalimu na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Yaani, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa kiasi cha kutoonekana kwenu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana sura zilizo kuu na kuheshimu wanaojulikana kwa ajili ya umbuji wao. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayejaza mikono yenu na utajiri, na mnatamani sana Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti hata moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, sembuse kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Je, mmefikiria kuhusu maswali kama haya? Kile ufanyacho hakimkosei huyu Kristo tu; cha muhimu hata zaidi, kinakosea Mungu aliye mbinguni. Nadhani kwamba, haya siyo madhumuni ya imani yenu kwa Mungu!

kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

97. Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, lakini sio ushughulikiaji na upogoaji Wake; hata zaidi hamwezi kukubali mpangilio Wake wote, kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni gani hapa? Kimsingi, imani yenu ni kaka tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada. Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mkondo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kujipendekeza kwa Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na hauwezi kuchukuliwa kuwa imani ya kweli hata kidogo. Kifaranga anaweza kujitokezaje kwa imani kama hii? Kwa maneno mengine, ni tunda lipi ambalo imani kama hii inaweza kuzalisha? Azma ya imani yenu kwa Mungu ni kutimiza nia zenu kupitia kumtumia Mungu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo.

kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

98. Kila moja ya kanisa lina watu wanaolivuruga kanisa, watu wanaokatiza kazi ya Mungu. Watu hawa wote ni Shetani wanaojifanya katika familia ya Mungu. Mtu wa aina hii ni mjuzi wa kuiga, akija mbele Yangu kwa heshima, akitikisa vichwa kwa kukubali na kuinama, akitenda kama mbwa wengi walio hafifu, akijitolea “yote” yake ili kufikia malengo yake mwenyewe, lakini akionyesha sura yake mbaya mbele ya ndugu. Anapomwona mtu akiutenda ukweli anamshambulia na kumtenga; anapomwona mtu wa kutisha kumpiku yeye mwenyewe, anamsifu mno na kujipendekeza kwake, wakitenda kama viongozi wa kiimla kanisani. Inaweza kusemwa kuwa mengi ya makanisa yana aina hii ya “nyoka mwovu wa ndani,” aina hii ya “mbwa wa kupakata” kati yao. Wanatembea kwa siri kwa pamoja, wakikonyezana na kuashiriana, na hakuna hata mmoja wao anayetenda ukweli. Yeyote aliye na sumu zaidi ndiye “ibilisi mkuu,” na yeyote aliye na hadhi ya juu zaidi huwaongoza, akipeperusha bendera yao juu zaidi. Watu hawa wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani, wakieneza ubaya wao, wakiachilia kifo, wakifanya watakavyo, wakisema wanachopenda, bila anayethubutu kuwakomesha, wakijawa na tabia za kishetani. Punde tu wanapoanza kusababisha usumbufu, hewa ya kifo inaingia ndani ya kanisa. Wale wanaotenda ukweli katika kanisa wanaachwa na wanashindwa kufikia uwezo wao, ilhali wale wanaovuruga kanisa na kusambaza kifo wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani. Cha ziada ni, watu wengi huwafuata. Aina hii ya kanisa iko chini ya udhibiti wa Shetani na ibilisi ni mfalme wao. Iwapo watu wa kanisa hawataamka na kuwafukuza hao ibilisi wakuu, basi pia watakuja kuangamia siku moja. Kuanzia leo na kuendelea hatua lazima zichukuliwe dhidi ya kanisa la aina hii. Ikiwa wale wanaoweza kuuweka ukweli mdogo katika vitendo hawajihusishi na utafutaji, basi kanisa hilo litapigwa marufuku. Ikiwa hakuna mtu yeyote kanisani aliye radhi kuutenda ukweli, hakuna yeyote anayeweza kuwa shahidi kwa Mungu, basi kanisa hilo linapasa kutengwa kabisa, miunganisho yao na makanisa mengine kukatizwa. Hili linaitwa kuzika kifo; na kumfukuza Shetani. Iwapo kuna waonevu kadhaa waovu ndani ya kanisa, na vilevile “nzi” wadogo wanaowafuata wale wasio na ufahamu kabisa, ikiwa wale wa kanisa bado hawawezi kutoa vifungu na ushawishi wa nyoka hawa baada ya wao kuona ukweli, basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa! Wale walio wa Shetani watarudishwa kwa Shetani, ilhali wale walio wa Mungu hakika watakwenda kutafuta ukweli; hili linaamuliwa na asili zao. Acheni wale wote wanaomfuata Shetani waangamie! Hakuna huruma watakayoonyeshwa watu hawa. Acheni wale wanaofuata ukweli wapate utoaji na muwakubalie kufurahia neno la Mungu hadi mioyo yao itosheke. Mungu ni mwenye haki; Yeye hawatendei watu kwa udhalimu. Ikiwa wewe ni ibilisi basi hutakuwa na uwezo wa kuutenda ukweli. Ikiwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli basi ni wazi kuwa hutatekwa nyara na Shetani—hili halina tashwishi yoyote.

kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

99. Wale wasiotafuta kuendelea daima wanataka wengine wawe wabaya na watepetevu kama wao wenyewe, wale wasiotenda ukweli wanawaonea gere wale wanaotenda ukweli. Wale wasiotenda ukweli daima wanataka kuwadanganya wale wapumbavu na wasio na ufahamu. Mambo ambayo watu hawa wanaeneza yanaweza kukufanya usawijike, kuteleza kwenda chini, kuwa na hali isiyokuwa ya kawaida na kujawa na kiza ndani yako; yanaweza kukufanya usogezwe mbali na Mungu, na yanakufanya uuthamini mwili na kujihusisha na tamaa. Wale ambao hawapendi ukweli, ambao daima humshughulikia Mungu kwa uzembe hawana maarifa ya binafsi, na tabia zao huwashawishi watu kufanya dhambi na kuasi Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo wala kuwaruhusu wengine kutenda ukweli. Wanathamini dhambi na hawana chuki kwao wenyewe. Hawajifahamu wenyewe na huwakomesha wengine kujifahamu wenyewe, na huwakomesha wengine kuwa na matamanio ya kujua ukweli. Wale wanaowadanganya hawawezi kuona mwangaza na huanguka gizani, hawajijui wenyewe, na ukweli kwao si wazi na wanakuwa mbali zaidi na zaidi na Mungu. Hawaweki ukweli katika vitendo na huwakomesha wengine kutenda ukweli, wakiwaleta watu hao wajinga mbele yao. Badala ya kusema kuwa wanamwamini Mungu ingekuwa vyema kusema kuwa wanawaamini mababu zao, kwamba kile wanachoamini ni sanamu zilizo mioyoni mwao. Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa. Kuna watu wengi kanisani ambao hawana ufahamu, na jambo la uongo linapotendeka wanasimama tu upande wa Shetani. Wanapoitwa vibaraka wa Shetani wanahisi kuwa wamekosewa sana. Wanasemekana kuwa hawana ufahamu, lakini daima wanasimama upande usiokuwa na ukweli. Hakujakuwa na wakati muhimu ambapo wamesimama upande wa ukweli, hakuna wakati mmoja ambapo wamesimama na kutetea mjadala juu ya ukweli, kwa hivyo je, hawana ufahamu? Kwa nini daima wanasimama upande wa Shetani? Kwa nini hawasemi neno lolote la haki ama lenye mantiki kwa ukweli? Je, hali hii kweli imetokana na kuchanganyikiwa kwao kwa ghafla? Kadri mtu anapokuwa na ufahamu mdogo, ndivyo anavyozidi kushindwa kusimama upande wa ukweli. Je, hili linaonyesha nini? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu wanapenda uovu? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu ni watoto waaminifu wa Shetani? Je, ni kwa nini daima wanaweza kusimama upande wa Shetani na kuzungumza lugha moja naye? Kila neno na tendo lao, na maonyesho yao yanathibitisha vya kutosha kuwa wao sio wapenzi wa ukweli kwa namna yoyote, lakini badala yake wao ni watu wanaochukia ukweli. Kwamba wanaweza kusimama upande wa Shetani kunadhihirisha kuwa hakika Shetani anawapenda ibilisi hawa wadogo wanaopigana kwa ajili ya Shetani katika maisha yao yote. Je, taarifa hizi za kweli si wazi sana? Ikiwa hakika wewe ni mtu unayependa ukweli, basi kwa nini huwezi kuwaheshimu wale wanaotenda ukweli, na mbona unawafuata mara moja wale wasiotenda ukweli punde tu wanapokuwa na mabadiliko ya sura? Je, hili ni tatizo la aina gani? Sijali iwapo una ufahamu au la, sijali kwamba umelipa gharama kuu kiasi gani, sijali kuwa nguvu zako ni kuu kiasi gani na sijali ikiwa wewe ni nyoka mwovu wa ndani ama kiongozi anayepeperusha bendera. Ikiwa nguvu zako ni kuu basi ni kwa ajili tu ya usaidizi wa nguvu za Shetani; ikiwa hadhi yako iko juu, basi ni kwa sababu kuna wengi waliokuzunguka wasiotenda ukweli; ikiwa hujafukuzwa basi ni kwa kuwa sasa sio wakati wa kazi ya kufukuza, bali ni wakati wa kazi ya kuondoa. Hakuna haraka ya kukufukuza sasa. Ninahitaji tu kusubiri siku ifike ambayo utakuwa umeshaondolewa ili Nikuadhibu. Yeyote asiyetenda ukweli ataondolewa!

kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

100. Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walio tayari kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walio radhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walio radhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni waakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasiotenda ukweli hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa makusudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasiotenda ukweli hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtu kufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasiotenda ukweli lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda.

kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

101. Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu? Hata wale walio tu na moyo nusu wa utii hawawezi kutembea hadi mwisho, sembuse hawa wadhalimu wasio na utii hata kidogo kwa mioyo yao. Kazi ya Mungu haipatwi virahisi na mwanadamu. Hata mwanadamu akitumia nguvu yake yote, ataweza kupata kipande tu na kufikia ukamilifu mwishowe. Na vipi basi kuhusu watoto wa malaika mkuu wanaotaka kuharibu kazi ya Mungu? Je, hawana hata matumaini madogo zaidi ya kupatwa na Mungu?

kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

102. Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo.

kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

103. Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

104. Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[21] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba si chochote zaidi ya nzi katika kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kutegemea nguruwe na mbwa wa wazazi wao. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno.[22] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu anajua kidogo kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujazwa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza kazi yao tena ya utesaji, wakiendeleza kazi yao yenye umri wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

105. Katika Biblia, tathmini ya Mafarisayo kwa Bwana Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “walisema, Yeye si wa akili sawa. … Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Mafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa ikiiga mambo au ikifikiria tu kutoka popote—ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho yao ilitolewa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele ya watu ni kana kwamba ilikuwa imeshughulikiwa vyema, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kuvumilia. Nguvu zao mchafukoge za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua maono yao binafsi yasiyo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na maumbile yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na maono yao yasiyo na misingi, ya wivu, na hali ya ubovu na ubaya na ukatili wao dhidi ya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, walimshambulia bila mpango, bila subira, kwa njia za kishenzi, na kwa makusudi ya kijicho pamoja na kutupilia mbali kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilikuwa hadi kufikia kiwango cha kutupilia mbali Roho Wake bila kubagua, Yaani, Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu. Hivi ndivyo waliyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli,” na “mkuu wa pepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa pepo. Waliweza kupatia sifa ya kazi ambayo Roho wa Mungu mwenye mwili alikuwa amevalia kama kurukwa akili. Hawakukufuru tu Roho wa Mungu kama Beelzebuli na mkuu wa pepo, lakini waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upingaji wao na kukufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kutumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na wajumbe wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na mapambano yao na Mungu yasiyoisha. Kiini cha upingaji wao kwa Mungu na mwelekeo wao wa ukatili kwake Yeye, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa ya na yale waliyoyasema na kufanya, na akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusameheka ulimwenguni humu na hata baadaye, kama vile tu maandiko yafuatayo yanasema: “Wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” na “Yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.”

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

106. Kunayo siri kubwa moyoni mwako, ambayo hujawahi kuifahamu kamwe, kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu bila mwanga. Moyo wako na roho yako vimepokonywa na yule mwovu. Macho yako yamezuiwa kwa giza yasione, na huwezi kuliona jua angani wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu, na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako kwa haki, kila kitu ambacho Mwenye uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya mateso isiyokuwa na mwisho, bila nguvu ya kukuokoa, bila matumaini ya kurudi ukiwa hai, na yote unayofanya ni kupambana na kusonga kila siku.… Tokea wakati huo, hungeweza kuepuka kuteswa na yule mwovu, uliwekwa mbali na baraka za mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa mwenye Uweza, unatembea katika njia ambayo huwezi kurejea nyuma tena. Kuitwa mara milioni hakuwezi kusisimua moyo wako na roho yako. Unalala fofofo mikononi mwa yule mwovu, ambaye amekushawishi katika ulimwengu usio na mipaka, bila mwelekeo na bila alama za barabarani. Tokea hapo, umepoteza hali yako ya asili ya kutokuwa na hatia na utakatifu wako, na kuanza kujificha kutokana na utunzaji wa mwenye Uweza. Ndani ya moyo wako, yule mwovu anakuelekeza katika kila jambo na anakuwa uhai wako. Humwogopi tena, kumwepuka, au kumshuku; badala yake, unamchukulia kama Mungu aliye moyoni mwako. Unaanza kumtukuza na kumwabudu, na nyinyi wawili mnakuwa msiotengana kama mwili na kivuli chake, kila akitoa nafsi yake kwa mwingine katika uzima na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu mahali ulikotoka, kwa nini ulizaliwa, au kwa nini utakufa. Unamtazama Mwenye uweza kama mgeni; hujui mwanzo Wake, sembuse yale yote ambayo Amekutendea. Kila kitu kitokacho Kwake kimekuwa cha kuchukiza kwako. Huvitunzi wala kujua thamani yavyo. Unatembea kando na yule mwovu, kuanzia siku ile ulipoanza Mwenye uweza alianza kukukimu. Wewe na yule mwovu mmepitia maelfu ya miaka ya dhoruba na tufani pamoja, na pamoja naye, mnampinga Mungu ambaye alikuwa chanzo cha uhai wako. Hujui lolote kuhusu kutubu, sembuse kwamba umefikia ukingo wa kuangamia. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu na kukutesa; umesahau asili yako. Kwa njia hii, yule mwovu amekuwa akikuharibu, hatua baada ya hatua, hata mpaka leo. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Umeacha kulalamika juu ya maudhi ya dunia ya wanadamu, na huamini tena kwamba dunia si ya haki. Bado hujali sana kama Mwenye uweza yupo. Hii ni kwa sababu ulimchukulia yule mwovu kuwa baba yako wa kweli kitambo, na huwezi tena kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyo moyoni mwako.

kutoka katika “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili

107. Alfajiri inapofika, nyota ya asubuhi inaanza kuangaza mashariki. Hii ni nyota ambayo haijawahi kuwepo hapo awali. Inaliangaza anga lililo bado na nyota, ikikuwasha nuru iliyozimwa katika mioyo ya wanadamu. Watu si wapweke tena, kwa sababu ya mwanga huu, ambao hukuangazia wewe sawia na wengine. Lakini ni wewe tu unayebaki ukiwa umelala fofofo katika usiku wa giza. Huwezi kuisikia sauti, wala kuiona nuru, hujui kuhusu ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, enzi mpya, kwa sababu baba yako hukwambia, “Mwanangu, usiamke, bado ni mapema. Hali ya anga ni baridi, kwa hivyo usiende nje, usije ukachomwa machoni kwa mkuki na upanga.” Unaamini maonyo ya baba yako pekee, maana unaamini kwamba baba yako tu ndiye yuko sahihi, kwa sababu baba yako ana umri mkubwa kuliko wewe na kwamba baba yako anakupenda sana. Maonyo kama hayo na upendo kama huo unakufanya uwache kuamini hekaya kwamba kuna nuru ulimwenguni, na uwache kujali kama ukweli bado upo ulimwenguni humu. Huthubutu tena kutumainia ukombozi kutoka kwa mwenye Uweza. Umeridhika kuwa katika hali hiyo, hutumainii tena ujio wa nuru, na hutazamii tena kuja kwa Mwenye uweza kama ilivyo katika hekaya. Inavyokuhusu wewe, yote yaliyo mazuri hayawezi kufufuliwa tena, wala hayawezi kuendelea kuwepo. Kesho ya wanadamu, siku za baadaye za wanadamu zinapotea, zinaharibika kabisa machoni pako. Unayashika sana mavazi ya baba yako kwa nguvu zako zote, ukifurahia kushiriki taabu zake, ukiogopa kumpoteza mwenza wako wa kusafiri na “mwelekeo” wa safari yako ya mbali. Ulimwengu huu mkubwa na wenye giza wa binadamu umewaunda wengi wenu, kuwa majasiri na watu wa kujitahidi sana katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ulimwengu huu. Umewaunda “mashujaa” wengi ambao hawaogopi kifo kabisa. Zaidi ya hayo, umetengeneza kundi baada ya kundi la watu waliokufa ganzi na wanadamu waliopooza ambao hawajui makusudi ya kuumbwa kwao. Macho ya Mwenye uweza hukagua kila mmoja wa jamii ya wanadamu walio katika mateso makali. Anachosikia ni vilio vya wale wanaoteseka, Anachoona ni kutokua kwa aibu kwa wale wanaoteseka, na Anachohisi ni kutojiweza na hofu ya jamii ya wanadamu ambayo imepoteza neema ya wokovu. Wanadamu wanakataa utunzaji Wake, wakichagua kutembea katika njia yao wenyewe, na wakijaribu kukwepa macho Yake yanayochunguza kwa karibu, wakiona ni afadhali waonje uchungu wa kilindi cha bahari hadi mwisho, pamoja na adui. Kutanafusi kwa Mwenye uweza hakusikiki tena na binadamu. Mikono ya Mwenye uweza haiko tayari kuwapapasa tena wanadamu hawa wenye huzuni. Anarudia kazi Yake, mara kwa mara akikamata tena, na mara kwa mara akipoteza tena, na kutoka wakati huo, Yeye anaanza kuchoka, kujihisi mchovu, na hivyo Anasitisha kazi inayofanyika, na kuwacha kutembea kati ya wanadamu…. Wanadamu hawana ufahamu kabisa kuhusu mabadiliko haya, hawajui kuhusu kuja na kuondoka, huzuni na ghamu ya Mwenye uweza.

kutoka katika “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili

108. Usiku uingiapo polepole, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au wapi linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu hukaribisha mwanga wa mchana, lakini ikija kwa kulikotoka nuru na jinsi imeliondoa giza la usiku, mwanadamu anajua hata machache na hata ana ufahamu mchache zaidi Mabadiliko haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu kutoka kipindi kimoja hadi kingine, kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine, wakati huu wote yakihakikisha kwamba kazi ya Mungu katika kila kipindi na mpango Wake wa kila enzi unatekelezwa. Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili. Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu.

kutoka katika “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

1. “Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

2. “Anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa” ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.

3. “Upendeleo” unahusu tabia ya watu ya ukaidi.

4. “Kuchukua mamlaka kamili” inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni ya uadui kwa Mungu.

5. “Kibaraka” inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.

6. “Kuongezeka haraka” inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.

7. “Hawezi kutambua tofauti muhimu” inaonyesha wakati ambapo watu wanageuza mapenzi ya Mungu kuwa kitu cha kishetani, ikitaja kwa upana tabia ambayo kwayo watu humkataa Mungu.

8. “Anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe” inahusisha kuchanganya ukweli na njozi, na haki na uovu.

9. “Gaidi” inatumiwa kuonyesha kwamba watu ni wapumbavu na hawana ufahamu.

10. “Mabaki na makombo” inatumiwa kuonyesha tabia ambazo kwazo watu humdhulumu Mungu.

11. “Anaghadhibishwa” inahusu uso mbaya wa mwanadamu aliye na hasira na aliyeudhika.

12. “Bila haya” inahusu wakati ambapo watu hawajali, na hawana uchaji kuhusiana na Mungu hata kidogo.

13. “Kuingia kwa mwanadamu” hapa inaonyesha tabia ya mwanadamu ya uasi. Badala ya kutaja kuingia kwa watu katika maisha—ambako ni kuzuri—kunahusu tabia na matendo yao mabaya. Inahusu kwa upana matendo yote ya mwanadamu yaliyo katika upinzani na Mungu.

14. “Wanakerwa na hofu za kubuni” inatumiwa kudhihaki maisha ya binadamu wa mwanadamu yasiyo na mwelekeo. Inahusu hali mbaya ya maisha ya wanadamu, ambayo watu huishi pamoja na pepo.

15. “Bora zaidi” inasemwa kwa dhihaka.

16. “Hamasa yao daima ikiwaka moto zaidi” inasemwa kwa dhihaka, na inahusu hali mbaya ya mwanadamu.

17. “Mpango alioufikiria kwa makini katika akili yake” inasemwa kwa dhihaka, na hii inahusu jinsi watu hawajijui na hawajui kimo chao halisi. Hii ni kauli ya kimatusi.

18. “Wa kuheshimiwa” inasemwa kwa dhihaka.

19. “Kutupa” inaonyesha hali mbaya ya watu ambao hughadhabika kwa hasira wakati ambapo wanashindwa na Mungu. Inaonyesha kiwango cha upinzani wao kwa Mungu.

20. “Kumkamata akiwa hai” inahusu tabia ya vurugu na yenye kustahili dharau ya mwanadamu. Mwanadamu ni katili na hayuko tayari kumsamehe Mungu hata kidogo, na hufanya madai ya upuuzi Kwake.

21. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

22. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

a. Nakala ya awali inasoma “sarafu za dhahabu kwa.”

b. Msemo wa Kichina, maana halisi ambayo ni “magaidi wanaoimiliki milima na kujitangaza kama wafalme.”

c. Nakala ya awali inasema “yeye.”

d. Huu ni msemo wa Kichina.

e. Nakala ya asili haina maneno “tamaa ya.”

f. “Nyoosha kiwiko cha mtu nje” ni nahau ya Kichina, ambayo inamaanisha mtu anawasaidia wengine kwa gharama ya watu walio karibu na mtu huyo, kwa mfano wazazi, watoto, jamaa au ndugu.

g. Hadithi ya ndege wa Hanhao inafanana sana na hekaya ya Aesop ya mchwa na panzi. Ndege wa Hanhao hupenda zaidi kulala kuliko kujenga kiota wakati hali ya hewa ni ya vuguvugu—licha ya onyo la marudio kutoka kwa jirani wake, ndege wa jamii ya kunguru. Wakati majira ya baridi hufika, ndege huyo huganda hadi kifo.

h. Matini ya asili haina kauli “kuelewa kwamba.”

i. Kurudi ufuoni: nahau ya Kichina, ikiwa na maana kwamba “mtu kuacha njia zake za uovu.”

j. Nakala ya asili inacha “kiovu.”

k. Makala ya asili hayana neno “kawaida.”

Iliyotangulia:Maneno Bora Zaidi Juu ya Kufichua Jinsi Shetani Huwapotosha Wanadamu

Inayofuata:Maneno Bora Zaidi Juu ya Katiba, Agizo za Utawala na Amri za Enzi ya Ufalme

Maudhui Yanayohusiana

 • Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Sehemu ya Mwisho ya Njia

  Ninyi sasa mko katika kipindi cha mwisho cha njia, na ni sehemu muhimu ya njia. Labda umepitia mateso mengi, umefanya kazi nyingi, umesafiri barabara…

 • Dibaji

  Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze …

 • Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!

  Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya k…

 • Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

  Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima.…