44. Mwishowe, Naona Ukweli Kujihusu

Na Shen Xinwei, Italia

Wajibu wangu kanisani mnamo 2018 ulikuwa kutafsiri hati na kufanya kazi na Dada Zhang na Dada Liu.Tulielewana sana. Wakati wa mkutano mmoja, tulishiriki juu ya jinsi kiongozi wa uwongo alivyotambuliwa. Haya yalikuwa makadirio ya Dada Liu ya kiongozi wa uwongo: “Yeye huwabadilisha watu bila kanuni zozote. Alimhamisha Dada Zhang lakini akamwacha dada mwingine ambaye si msikivu au mwenye bidii katika wajibu wake asalie kwenye timu.” Yule kiongozi mwingine alipowasomea haya kina ndugu uso wangu ulianza kuwa mwekundu mara moja. Nilihisi kwamba maneno ya Dada Liu yalikuwa makali sana. Nilijilazimisha kuwa mtulivu, lakini kulikuwa na msukosuko ndani yangu. Kwa kuwa tulikuwa watatu tu kwenye timu, nilikuwa na hakika kwamba alikuwa amenitaja. Nilihisi kama kila mtu angefikiri kwamba sikuwa msikivu au mwenye bidii katika wajibu wangu. Ningewezaje kujiamini baada ya hapo? Nilikuwa mkali kwa Dada Liu tangu wakati huo kutokana na kuogopa kudhalilishwa na uhusiano wetu ukazidi kutokuwa na ukunjufu.

Alichaguliwa kama kiongozi wa timu muda mfupi baadaye. Alikuwa mwangalifu sana na aliangalia kwa makini yote niliyotafsiri. Nilikuwa na mtazamo mzuri mwanzoni, lakini baada ya muda fulani nilianza kuhisi mweye upinzani kwake. Nilihisi kwamba nilikuwa nimefanya wajibu huo kwa muda mrefu lakini bado hakuniamini, kana kwamba sikuwa stadi. Pia alinipa mapendekezo mara kwa mara, kwa hivyo nilihisi kama kwamba alinidharau na alikuwa akifanya mambo yawe magumu. Kile ambacho sikuweza kuvumilia ni kwamba tulipojadili kazi yetu, alitaja kasoro zangu kila wakati mbele ya mtu aliyesimamia. Niliwaza, “Je, hujaribu tu kunifanya nionekane mbaya mbele yake?” Chuki yangu kwake ilizidi kuongezeka na nikazidi kuwa mkali kwake kutokana na kuogopa kudhalilishwa. Katika kazi yetu pamoja baada ya hapo, nilichukia kabisa kumuona na alinikera. Sikupenda alipofuatilia kazi yangu na nilinuna kila aliponipa viashiria. Wakati mwingine nilifikiria jinsi ambavyo ningemfanya aonekane mbaya na kumdunisha. Sikutaka kumsaidia nilipoona matatizo katika wajibu wake, bali badala yake, nilimdharau na hata nilitarajia ashindwe katika wajibu wake ili kumpa funzo. Wakati mmoja, Dada Liu alifungua moyo wake katika mkutano, akisema kwamba alihisi kwamba alizuiwa nami katika ushirikiano wetu, kwamba nilikuwa mkali sana na hakujua jinsi ya kufanya kazi nami. Nilighadhabika mara tu aliposema hayo. Niliwaza, “Je, si wajaribu tu kunifunua kwa wengine kwa kujifanya kwamba unafungua moyo wako? Sasa kwa kuwa kila mtu anajua hasira yangu hukuzuia, watanionaje?” Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo ndivyo nilivyozidi kukasirika. Nilihisi kama kwamba alikuwa akijaribu kunifanya nionekane mbaya. Nilianza kumchukia na niliketi pale nikibibidua mdomo kwa kimya wakati wote wa mkutano. Baadaye, Dada Liu aligundua kwamba nilionekana mwenye tatizo, kwa hivyo alikuja na kuniambia kwa utulivu, “Unaonekana mwenye fadhaa, na hukusema lolote mkutanoni. Iwapo kuna jambo linalokusumbua, nitafurahia kulizungumzia. Unaweza kunijulisha juu ya kasoro zozote nilizo nazo pia.” Lakini sikuweza kuvumilia kumwona na nilimchukia kabisa. Niliwaza, “Lazima uulize kwa kweli? Ni nani anayeweza kufurahia kusikia ‘ukifungua moyo wako’ kwa njia hii?” Kisha akaketi kando yangu. Nilimrushia jicho, nikiwa nimejawa na dharau na sikuweza kabisa kuzuia hasira yangu nilipokumbuka jinsi alivyonikosoa mbele ya kila mtu. Nilimwonyesha makosa yake na upotovu aliouonyesha, nikisema kwamba hakuwa na hekima, aliwafanya wengine waonekane wabaya kwa makusudi, aliwazuia watu na kwamba alikuwa na kiburi sana. Nilisema kwa kirefu. Nilitulia nilipomwona akionekana mwenye huzuni huku akiinamisha kichwa chake. Nilikuwa nimetoa hasira hiyo yote iliyogandamizwa na ambayo nilikuwa nimeshikilia. Kisha Dada Liu akaniambia, “Sikuwahi kufikiria kwamba nilikuwa nimekudhuru sana. Naomba radhi kabisa.” Nilihisi hatia sana nilipomwona akigeuka na kufuta machozi yake. Je, nilikuwa nimevuka mpaka? Je, jambo hili litamtumbukiza katika hali hasi? Lakini nikawaza baadaye, “Nilikuwa nikizungumza tu ukweli. Nilisema hivi ili ajijue.” Wakati huo, niliacha kuhisi hatia. Dada Liu alizuiwa nami hata zaidi baada ya hapo na hakuthubutu tena kufuatilia kazi yangu, sembuse kunipa mapendekezo.

Siku chache baadaye, kiongozi wa kanisa letu aliamuru kila mtu aandike makadirio ya viongozi wa timu ili aweze kutathmini uwezo wao kulingana na kanuni. Nilifurahi kisirisiri niliposikia hayo. Nilikuwa na hamu ya kufunua upotovu wote ambao Dada Liu alikuwa ameonyesha ili kila mtu aweze kumjua kikamilifu na adhalilishwe. Nilihisi wasiwasi wa muda mfupi na nikagundua kwamba mawazo yangu yalikuwa maovu, kwamba nilipaswa kuwa wa haki bila upendeleo na kukubali uchunguzi makini wa Mungu. Nilikusudia kuwa wa haki bila upendeleo katika tathmini yangu, lakini nilipokumbuka jinsi Dada Liu alivyoniingiza matatizoni, nilijawa na chuki kabisa. Nilimimina chuki yangu yote kwake katika makadirio hayo nikitarajia kwamba kiongozi atamshughulikia vikali au hata kumhamisha. Ningefurahi almradi hakuwa kwenye timu yangu. Dada Liu aliachishwa kazi muda mfupi baadaye. Habari hii iliniacha nikiwa na wasiwasi. Niliwaza, “Je, jambo hilo linahusiana na yale niliyoandika? Niliandika tu juu ya upotovu wake kiasi, lakini hiyo haikupaswa kusababisha aachishwe kazi, siyo?” Niliona kwamba Dada Liu alikuwa katika hali hasi baada ya hapo na nilihisi hatia isiyo ya wazi. Sikuwa na nguvu yoyote ya kufanya wajibu wangu.

Nilizungumza na kiongozi kuhusu hali yangu baada ya siku mbili, na akaniambia kwamba Dada Liu alikuwa ameachishwa kazi hasa kwa sababu ya ubora wake duni wa tabia na hakustahili kuwa kiongozi wa timu. Haikuhusiana na makadirio yangu. Lakini alisema kwamba sikuwa na huruma nilipotaja kasoro zake na sikuweza kuwatendea watu kwa haki, kwamba nilitaka kulipiza kisasi na nilikuwa na tabia ya uovu. Nilishtuka niliposikia hayo. Je, “kutaka kulipiza kisasi” na “tabia ya uovu” si mambo tuyasemayo kuhusu watu waovu? Kwa siku chache, nilikumbwa na mawimbi ya majonzi kila nilipokumbuka yale aliyoyasema. Nilijiuliza iwapo kwa kweli nilikuwa mtu mwovu. Nilikuja mbele za Mungu kuomba katika maumivu yangu: “Ee Mungu, dada huyu alisema kwamba nina tabia mbovu, lakini sielewi. Tafadhali nitie nuru ili niweze kujijua kwa kweli.”

Nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu baada ya kuomba: “Je, mna uwezo wa kufikiria njia mbalimbali za kuwaadhibu watu kwa sababu hawawapendezi au kwa sababu hawapatani na ninyi? Je, mmewahi kufanya kitendo cha aina hiyo hapo mbeleni? Je, mmefanya hivyo kiasi gani? Je, hamkuwadhalilisha watu kwa njia isiyo ya moja kwa moja, mkitoa maneno yanayowaumiza na kuwakejeli kila wakati? (Naam.) Je, mlikuwa katika hali gani mlipokuwa mkifanya vitu kama hivi? Wakati huo, mlikuwa mkitoa mawazo bila woga na mlifurahi; mlikuwa mmeshinda. Hata hivyo, mliwaza baadaye, ‘Nilifanya jambo la kustahili dharau sana. Mimi si mcha Mungu na sijamtendea mtu huyo kwa haki.’ Je, ndani kabisa ya mioyo yenu, mlihisi hatia? (Ndiyo.) Ingawa ninyi si wacha Mungu, angalau mna dhamiri kiasi. Kwa hivyo, je, bado mnaweza kufanya kitu cha aina hii tena katika siku zijazo? Je, unaweza kukusudia kuwashambulia na kujitahidi kulipiza kisasi dhidi ya watu, kuwapa wakati mgumu na kuwaonyesha ni nani ndiye bosi kila unapowadharau na unaposhindwa kupatana nao, au kila wanapokosa kukutii au kukusikiliza? Je, utasema, ‘Usipofanya kile ninachotaka, nitatafuta fursa ya kukuadhibu bila mtu yeyote kujua kuhusu hilo. Hakuna mtu atakayegundua, lakini nitakufanya unyenyekee mbele yangu; nitakuonyesha mamlaka yangu. Baada ya hapo, hakuna mtu atakayethubutu kunichezea!’ Niambieni: Mtu anayefanya kitu kama hicho ana ubinadamu wa aina gani? Kwa mintarafu ya ubinadamu wake, yeye ni mwovu. Akipimwa dhidi ya ukweli, yeye hamchi Mungu(“Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilifadhaika baada ya kusoma maneno ya Mungu ya hukumu. Yalikuwa yamefichua hali yangu waziwazi. Ninapokumbuka hapo awali, mimi na Dada Liu tulikuwa tumefanya kazi vizuri sana mwanzoni. Nilianza kuwa na tatizo naye makadirio yake ya mtu mwingine yaliponiathiri na kunidhalilisha mbele ya watu wengine. Alianza kutaja kasoro zangu baada ya yeye kuwa kiongozi wa timu. Nilihisi kama kwamba nilifedheheka na nilikuwa nikiingizwa matatizoni. Alianza kunikera sana na nilitaka kumfanya aonekane mpumbavu. Alipozungumza juu ya hali yake ili kupata utatuzi, nilidhani kwamba alikuwa akifunua tu kasoro zangu na kuniaibisha, akiathiri jinsi kina ndugu wanavyoniona. Chuki yangu kwake iliongezeka na nilitia chumvi matatizo yake ili kumfichua, nikitenda kutokana na uovu na kumfanya awe hasi. Nilitumia makadirio yangu kwake kama nafasi ya kulipiza kisasi. Niliandika kasoro zake zote na upotovu wake ambao nilikuwa nimeona bila kutaja uwezo wake hata kidogo. Nilitaka tu kiongozi apate kumtambua na nilitarajia amhamishe. Kukumbuka jinsi nilivyotenda kulinitia wasiwasi sana. Nilikuwa nimeweka nung'uniko kwa sababu tu maneno ya Dada Liu yalikuwa yameathiri sifa na hadhi yangu, kwa hivyo nilichukua msimamo wa uhasam kwake. Nilifanya chochote nilichotaka. Niligundua kwamba sikumcha Mungu hata kidogo na kwa kweli nilikuwa na asili mbovu sana! Nilikuwa nikifikiri kwamba nilipatana vyema sana na kina ndugu na kwamba nilikuwa na hamu ya kumsaidia yeyote aliyekabiliwa na matatizo. Nilifikiri kwamba nilikuwa mtu mzuri kwa sababu nilifanya mambo kadhaa mazuri. Sasa niligundua hiyo ni kwa sababu tu hakuna mtu yeyote aliyehatarisha masilahi yangu ya kibinafsi. Tabia yangu ya kishetani ilitokea kwa nguvu zote masilahi yangu yalipohusika. Sikuweza kujizuia kushambulia na kulipiza kisasi. Niligundua kuwa bila kutatua tabia hiyo, ningefanya uovu wakati wowote. Hiyo ilikuwa hatari sana!

Nilitafakari juu yangu mwenyewe baada ya hapo. Iwapo nilikuwa na uwezo wa kufanya uovu wa aina hiyo, ni mawazo gani yalikuwa yakinidhibiti? Nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu). “Watu hufikiria namna hii: ‘Kama hutakuwa mwenye fadhila, basi sitakuwa mwenye haki! Ukiwa mwenye kiburi kwangu, basi nitakuwa mwenye kiburi kwako pia! Usiponitendea kwa heshima, kwa nini nikutendee kwa heshima?’ Hii ni fikira ya aina gani? Je, fikira ya aina hiyo si ya kulipiza kisasi? Katika maoni ya mtu wa kawaida, si mtazamo wa aina hii unawezekana? ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino’; ‘hapa onja dawa yako mwenyewe’—miongoni mwa wasioamini, huu wote ni urazini wenye busara na unakubaliana kabisa na mawazo ya wanadamu. Hata hivyo, kama mtu anayemwamini Mungu—kama mtu anayetafuta kuelewa ukweli na kutafuta mabadiliko katika tabia—je, unaweza kusema kwamba maneno kama hayo ni sahihi au si sahihi? Unapaswa kufanya nini ili kuyatambua? Je, mambo kama hayo hutoka wapi? Yanatoka katika asili ovu ya Shetani; yana sumu, na yana sura ya kweli ya Shetani yenye uovu na ubaya wake wote. Yana kiini halisi cha asili hiyo. Je, hulka ya mitazamo, mawazo, maonyesho, usemi, na hata vitendo ambavyo vina kiini cha asili hiyo ni ipi? Je, si hulka ya Shetani? Je, vipengele hivi vya Shetani vinapatana na ubinadamu? Je, vinapatana na ukweli, au na uhalisi wa ukweli? Je, ni vitendo ambavyo wafuasi wa Mungu wanapaswa kufanya, na mawazo na mitzamo wanayopaswa kuwa nayo? (La.)” (Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niligundua kwamba watu ni wapotovu na waovu sana kwa sababu tu ya upotovu wa Shetani. Kupitia elimu rasmi na ushawishi wa kijamii, ibilisi Shetani, hutujaza sumu zake zote kama vile “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake” “Hatutashambulia isipokuwa tukishambuliwa, tukishambuliwa, bila shaka tutarudisha pigo” “Mtendee mja vile anavyokutendea” “Hakuna kuchelewa mno kwa muungwana kulipiza kisasi” Watu huchukulia sumu hizi kama sheria zao za kuendelea kuishi bila hata kutambua. Wao huzidi kuwa wenye kiburi, wajanja, wenye ubinafsi na waovu kila wakati. Watu hawajali au kusamehe kwa kweli na hakuna upendo halisi. Wao hukasirika tu na kujitenga kitu chochote kinapoathiri masilahi yao ya kibinafsi. Wanaweza hata kufanya uadui au kulipiza kisasi. Watu huanza kuwa baridi zaidi na wasio na ukunjufu na wao hupoteza hisia zote za ubinadamu wa kawaida. Nilikuwa nimejazwa mawazo ya aina hiyo tangu nilipokuwa mdogo. Nilikuwa nimeishi kulingana na vitu hivi. Mtu mwingine alipoathiri masilahi yangu mwenyewe, sikuweza kujizuia kumchukia na kulipiza kisasi. Nilipokuwa pamoja na Dada Liu, alisema na kufanya mambo ambayo yalihatarisha masilahi yangu, kwa hivyo nilianza kuwa mwenye chuki na nilitumia nafasi yangu kumlipiza kisasi. Nilitaka anitambue ili asithubutu kunikosea tena. Nilitaka hata kumfukuza. Je, tabia yangu ilikuwa na tofauti gani na wapinga Kristo na watu waovu ambao kanisa lilikuwa limewafukuza? Watu hao walitaka tu kibali na sifa ya wengine lakini hakuweza kuvumilia maneno yoyote ya ukweli yaliyofichua upotovu wao. Walimshambulia mtu yeyote aliyesema au kufanya chochote kilichowakosea. Kwa sababu ya uovu wao wote, waliishia kuikosea tabia ya Mungu, waliwakasirisha wengine na wakafukuzwa kanisani. Walipoteza kabisa nafasi yao ya kuokolewa. Na nilikuwa nikimshambulia Dada Liu kwa sababu tu maneno yake yalikuwa yamenidhalilisha. Nilikuwa nimemdhuru kabisa. Nilikuwa nikifanya uovu! Niliona kwamba nilikuwa na ubinadamu mbaya sana, kwamba nilikuwa na asili na kiini kiovu kama cha mpinga Kristona mwovu, na jambo hili lilimchukiza Mungu. Nisingekutubu mara moja, ningezama tu kwenye uovu na kuadhibiwa na Mungu kama tu mpinga Kristo na mwovu! Jambo hili liliniogofya zaidi nilipokuwa nikilifikiria. Nilikuja mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mungu, sina ubinadamu kabisa. Nilikuwa nikiishi katika tabia yangu potovu na nilimshambulia dadangu. Sifanani na binadamu hata kidogo. Pasipo Wewe kusababisha hali hii ili kunishughulikia, nisingetafakari juu yangu mwenyewe. Ningeendelea kufanya maovu na kumdhuru. Mungu, ninatamani kutubu. Sitaki kuishi tena kulingana na sumu za Shetani. Tafadhali niongoze niwe mtu mwangalifu sana, mwenye busara na ubinadamu.”

Nilisoma haya katika maneno ya Mungu baada ya hapo: “Upendo na chuki ni vitu ambavyo binadamu wa kawaida wanapaswa kuwa navyo, lakini lazima utofautishe waziwazi kati ya yale unayoyapenda na yale unayoyachukia. Moyoni mwako, unapaswa kumpenda Mungu, kuupenda ukweli, kupenda vitu vya kujenga na kuwapenda ndugu zako, wakati ambapo unapaswa kumchukia ibilisi Shetani, kuchukia vitu hasi, kuwachukia wapinga Kristo na kuwachukia watu waovu. Iwapo unawachukia ndugu zako, basi utakuwa na uelekeo wa kuwakandamiza na kulipiza kisasi; jambo hili litakuwa la kutisha sana. Watu wengine wana fikira za chuki na mawazo maovu pekee. Baada ya muda fulani, watu kama hawa wasipoweza kupatana na mtu wanayemchukia, wataanza kujitenga naye; hata hivyo, hawaruhusu jambo hili liathiri wajibu wao au liathiri uhusiano wao wa kibinafsi wa kawaida kwa sababu wana Mungu mioyoni mwao na wanamcha. Hawataki kumkosea Mungu na wanaogopa kufanya hivyo. Ingawa watu hawa huenda wana maoni fulani juu ya mtu fulani, kamwe hawatii mawazo hayo katika vitendo au hata kutamka neno lisilofaa kwani hawataki kumkosea Mungu. Je, hii ni tabia ya aina gani? Huu ni mfano wa wao kutenda na kushughulikia mambo kwa kanuni na bila upendeleo. Unaweza kuwa usiyepatana na tabia ya mtu, na unaweza kutompenda, lakini unapofanya kazi pamoja naye, unasalia mwadilifu na hutaeleza kufadhaika kwako unapofanya wajibu wako, hutaathiri wajibu wako, au kufanya mifadhaiko yako iathiri masilahi ya familia ya Mungu. Unaweza kufanya vitu kulingana na kanuni; hivyo, unakuwa na uchaji wa kimsingi kwa Mungu. Ukiwa na zaidi kidogo ya hayo, basi unapoona kwamba mtu fulani ana makosa au udhaifu fulani—hata ikiwa amekukosea au kuyadhuru masilahi yako mwenyewe—bado utakuwa na moyo wa kumsaidia. Kufanya hivyo kutakuwa hata bora zaidi; kutamaanisha kwamba wewe ni mtu aliye na ubinadamu, uhalisi wa ukweli, na uchaji kwa Mungu(“Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliona kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba wale wanaomcha Mungu wanaweza kuwatendea wengine kulingana na kanuni za ukweli. Wanaweza kuwapendelea kina ndugu wakati mwingine, lakini wao si wakaidi katika mwingiliano wao na hawafanyi lolote la kumkosea Mungu au kuwadhuru wengine. Watu wasiomcha Mungu hufanya kila ambacho mioyo yao ya uovu hutamani na huko ni kufanya uovu na hulaaniwa na Mungu. Dada Liu alikuwa alisema bila kuficha, lakini yale aliyoyasema juu yangu yalikuwa ukweli. Hakuwa akinilenga. Pia, alichukulia wajibu wake kwa makini na kwa uaminifu na mapendekezo yake mengi yalikuwa ya msaada kwa kazi yetu. Sikupaswa kufanya mambo yawe magumu kwake kwa makusudi. Nilimwambia kuhusu upotovu wangu na nikaomba msamaha. Dada Liu alisema kwamba hakujali na alifanya ushirika juu ya ukweli kiasi ili kunisaidia. Nilihisi aibu na nilijichukia hata zaidi. Sikutaka kuishi tena kulingana na tabia yangu potovu. Baada ya hapo, Dada Liu aliponipa mapendekezo au wakati ambapo jambo alilosema au kutenda lilinidhalilisha, niliweza kulishughulikia vizuri na kuzingatia kutafuta ukweli na kujitafakari. Tuliweza kufanya kazi vizuri pamoja tena. Jambo hili lilinipa faraja kuu. Ninashukuru kwa ajili ya hukumu ya Mungu ambayo ilinibadilisha kwa njia hii ndogo.

Iliyotangulia: 43. Kwa Kuacha Ubinafsi, Nimekombolewa

Inayofuata: 45. Kuishi Mbele za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

3. Jaribu la Foili

Na Xingdao, Korea ya Kusini“Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na...

61. Ukweli Umenionyesha Njia

Na Shizai, JapaniMwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp