18. Baada ya Uwongo

Na Chen Shi, Uchina

Mwenyezi Mungu anasema, “Mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu). Bwana Yesu pia alisema, “Kweli nawaambia, Ila msipobadilishwa, na kugeuka kama wana wadogo, hamtaingia ndani ya ufalme wa mbinguni(Mathayo 18:3). Tunaweza kuona kutoka kwa maneno ya Mungu kuwa Yeye ni mwaminifu, kwamba Anawapenda wale waaminifu na kuwadharau wale wadanganyifu. na kwamba ni watu waaminifu pekee ndio wanaoweza kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hiyo ndiyo sababu Mungu anatutaka tena na tena tuwe waaminifu, na kwamba tutatue nia zetu za uwongo na udanganyifu. Lakini katika maisha halisi, wakati wowote kitu kilipoathiri sifa na hadhi yangu, Sikuweza kujizuia kusema uwongo na kudanganya. Bila hukumu na ufunuo wa maneno ya Mungu, bila kurudiwa na kufundishwa nidhamu na Yeye, kamwe nisingetubu kwa kweli, nisingeepuka uwongo, na kutia ukweli kwenye vitendo kama mtu mwaminifu.

Miaka michache iliyopita, nilikuwa nikifanya wajibu wa kiongozi wa kanisa. Siku moja kiongozi wangu aliniomba nihudhurie mkutano wa wafanyakazi. Nilifurahi sana. Nilifikiria jinsi nilivyokuwa nimefanya kazi kwa bidii kanisani hivi karibuni, nikifanya mikutano na ushirika kila siku, na ndugu wengi walikuwa wakifanya wajibu wao kwa bidii. Baadhi ya vikundi vilikuwa vimefanya maendeleo mengi, kwa hivyo nilidhani kwa hakika mkutano huu ungekuwa nafasi yangu ya kuonekana. Ningemuonyesha kiongozi na wafanyakazi wenza jinsi nilivyokuwa hodari, kwamba nilikuwa bora kuliko wengine. Nilipofika, niliona kwamba Dada Liu alikuwa akikunja kipaji chake kwa wasiwasi, na akasema huku akihema, “Je, kazi yako ya kuwanyunyizia na kuwasaidia ndugu inaendeleaje? Tuna wakati mgumu. Hakika sina uhalisi wa ukweli. Kuna maswala mengi ambayo siwezi kuyasuluhisha kabisa.” Nilitabasamu na kusema, “Kazi ya kunyunyizia inaendelea vizuri sana katika kanisa letu, vyema zaidi kuliko hapo awali.” Kiongozi aliingia wakati huo huo na akaanza kuuliza juu ya kazi ya kunyunyizia katika makanisa. Nilidhani kuwa ilikuwa nafasi yangu ya kujitokeza, kwa hivyo ilinibidi nijionyeshe vizuri. Ajabu ni kwamba, hakutuuliza juu ya mafanikio yetu katika kazi ya kunyunyizia, lakini aliuliza ni matatizo gani yalikuwa yametokeza, jinsi yalivyokuwa yametatuliwa kupitia ushirika juu ya ukweli, na ni matatizo gani ambayo hayakuwa yametatuliwa. Nilishikwa na hofu. Kwa jumla, niliratibu tu kazi na sikujua maelezo hata kidogo, kwa hivyo sikuwa nimefanya kazi yoyote halisi ya kunyunyizia. Sikujua la kufanya. Ninapaswa kusema nini kiongozi atakaponiuliza? Nikisema ukweli, je, atafikiria kwamba sikuwa nikifanya kazi ya vitendo? Nilikuwa tu nikijisifu kwa Dada Liu, nikisema kuwa kazi ambayo nilikuwa nikiwajibikia ilikuwa ikiendelea vizuri. Ikiwa singezungumza juu ya maelezo, je, angesema kuwa nilikuwa nikijisifu bure? Je, ningefanya nini? Nilihisi mwenye wasiwasi zaidi na zaidi. Wakati huo huo, Ndugu Zhou alizungumza juu ya maswala kadhaa ambayo walikuwa wamekabiliwa nayo katika kazi ya kunyunyizia katika kanisani lao na upotovu ambao alikuwa amefichua katika kazi yake. Kisha akaeleza jinsi alivyokuwa ametafuta ukweli ili kutatua mambo haya. Alieleza hayo kwa njia ya vitendo sana na ya utondoti, ambayo ilituonyesha njia ya utendaji. Nilihisi aibu sana baada ya kusikia ushirika wake. Kwa kujua kuwa sikuwa nimefanya kazi yoyote ya vitendo, niliinamisha kichwa changu na uso wangu ukawasha. Kisha kiongozi akanitaka niongee. Moyo wangu ulipiga kwa kishindo. Napaswa kusema nini? Sikuwa na maelezo ya kushiriki, na muhtasari pekee ungeonyesha kwamba sikuwa nikifanya kazi ya vitendo. Je, watu wangeniona vipi iwapo ningesema ukweli? Nilihisi kuwa singesema ukweli. Kwa hivyo nilisema tu, “Hali yangu ni sawa kabisa na ya Ndugu Zhou. Hakuna haja ya kuirudia.” Kiongozi alisikiza na hakusema lolote, kisha akaanza mkutano kwa kusoma maneno ya Mungu. Katika mkutano huo, nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeiba kitu kutoka kwa mtu. Nilikuwa na wasiwasi sana, nikiogopa siku ambayo kiongozi wangu angekagua au kusimamia kazi yangu, angendua kuwa utendaji wangu haukuwa kama wa Ndugu Zhou, na kuniondoa katika wajibu wangu kwa kutofanya kazi ya vitendo, kwa kusema uwongo na kudanganya. Wasiwasi wangu ulikua lakini bado sikuwa na ujasiri wa kusema ukweli. Niliamua kimya kimya, “Lazima nifanye kazi kabisa jinsi ambavyo Ndugu Zhou hufanya ili nifidie udanganyifu wangu leo.”

Niliporudi kanisani, nilikutana na mashemasi na viongozi wa makundi papo hapo, nikawapa ushirika wa utondoti na wa ana kwa ana, na kuwafanya waanze mara moja. Kisha nikaendesha baiskeli yangu hadi nyumbani kwa Dada Lyu. Nilimwambia juu ya njia ya Ndugu Zhou kwa utondoti, na nikamwambia ashiriki hilo na ndugu wengine juu ya wajibu wa kunyunyizia. Siku tatu zilipita tu hivyo na nilingojea kwa furaha kuvuna matunda ya kazi yangu. Kwa mshangao wangu, waliniambia kuwa walikuwa wamekabiliwa na matatizo mengi katika kazi yao ya kunyunyizia, ambayo mengine hawakuweza kuyatatua, na kwamba wageni walikuwa wamekubali uwongo wa CCP na wachungaji wa kidini kwa sababu hawakuwa wamenyunyiziwa mapema, na kwa hivyo hawakuthubutu kuja mikutanoni tena. Nilizongwa na mawazo. Hilo liliwezaje kutokea? Nilirudi haraka nyumbani kwa Dada Lyu na mara aliponiona, alisema kwa wasiwasi, “Sasa tunapaswa kufanya nini juu ya matatizo haya ya kazi yetu ya kunyunyizia? Sijui kwa kweli.” Sikujua cha kusema kabisa. Nilikuwa nimemwamuru hususan kupitia ushirika na nilikuwa nimeeleza kwa utondoti katika ushirika wangu, lakini bado hakuelewa. Nilijiuliza tatizo la watu hao lilikuwa gani. Nilikuwa nimefanya ushirika waziwazi sana lakini bado hawakuuelewa. Je, kiongozi ataniona vipi kazi yangu isipofanywa vizuri? Kadiri nilivyozidi kufikiria kuhusu hilo, ndivyo nilivyozidi kuvunjika moyo na kuhuzunika. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku huo, nikishindwa kulala, nikihisi nisiye na nguvu kabisa. Mwishowe nilikuja mbele za Mungu katika sala: “Mungu, nimefanya kazi kwa bidii sana katika wajibu wangu siku chache zilizopita, lakini sijafanikisha chochote. Siwezi kuhisi mwongozo Wako, na ninaishi gizani. Mungu, je, ninafanya kitu kilicho kinyume na mapenzi Yako, nikichochea maudhi na chuki Yako? Tafadhali nipe nuru ili niweze kuelewa hali yangu mwenyewe.”

Kisha nikasoma maneno haya ya kufichua kutoka kwa Mungu: “Je, malengo yako hufanywa Nami katika mawazo? Je, maneno na matendo yako husimama mbele Yangu? Mimi huchunguza fikira na mawazo yako yote. Je, si unajihisi mwenye hatia? Unajitwika sura ya bandia ili wengine waone na wewe kwa upole unajifanya kujidai; hili hufanyika ili ujikinge mwenyewe. Wewe hufanya hili ili kuyaficha maovu yako, na hata kutafuta njia za kuusukuma huo uovu kwa mtu mwingine. Ni hila gani hukaa ndani ya moyo wako!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). “Usitende kwa njia moja mbele ya wengine na utende kwa namna nyingine bila wao kufahamu; Ninaona wazi kila kitu unachofanya na ingawa unaweza kuwadanganya wengine huwezi kunidanganya Mimi. Ninaona yote waziwazi. Haiwezekani kwako kuficha chochote; vyote vimo mikononi Mwangu. Usifikiri kuwa wewe ni mjanja sana, kwa kufanya hesabu zako ndogondogo zikufaidi. Nakwambia: Haijalishi mwanadamu anaweza kubuni mipango kiasi kipi, iwe elfu kadhaa ama elfu nyingi, mwishowe hawezi kuepuka kutoka kwenye kiganja cha mkono Wangu. Vitu na matukio yote huendeshwa katika mikono Yangu, sembuse mtu mmoja! Usijaribu kuepuka au kujificha, usijidanganye au kuficha. Je, huwezi kuona kwamba uso Wangu mtukufu, hasira Yangu na hukumu Yangu imefichuliwa hadharani? Nitahukumu mara moja na bila huruma wale wote ambao hawanitaki Mimi kwa dhati. Huruma Yangu imefika mwisho na hakuna tena iliyobaki. Usiwe mnafiki tena na acha njia zako za kishenzi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 44). Nilitafakari kujihusu baada ya kusoma kifungu hiki. Nilikuwa nimekurupuka huku na kule nikifanya mikutano na ushirika na mashemasi na viongozi wa makundi, lakini nilikuwa nikifanya hayo yote kwa ajili ya nini? Je, nilikuwa nikifanya hayo kwa ajili ya kazi ya kanisa, kwa ajili ya maisha ya ndugu zangu? Je, nilikwa nikifanya hayo ili kutatua matatizo yao ya utendaji? Kisha nikafikiria jinsi nilivyokuwa nimedanganya katika mkutano huo. Kiongozi alipouliza juu ya kazi ya kunyunyizia, nilijua vizuri kuwa sikuwa nimefanya kazi yoyote ya vitendo, lakini nilikuwa mdanganyifu ili nisionekane kama mpumbavu, ili watu wasinibaini au kunidharau. Nilikuwa nimerudi haraka kutatua matatizo yaliyokuwa katika kazi yangu ili tu kiongozi asigundue kuwa nilikuwa nimedanganya. Niligundua wakati huo kwamba nilikuwa nimefanya kazi kwa bidii sana ili kuendeleza uwongo wangu, kuficha ukweli kwamba sikuwa nimefanya kazi ya vitendo, na kwa ajili ya sifa na hadhi yangu. Anilikuwa tu nimetumia njia ambayo Ndugu Zhou alikuwa ameshiriki kuhusu badala ya kuelewa kwa kweli matatizo halisi ya kina ndugu na kutatua matatizo yao kwa kufanya ushirika juu ya ukweli. Nilikuwa mzembe katika wajibu wangu, nikihodhi nia hiyo ya kustahili dharau. Hiyo iliwezaje kupatana na mapenzi ya Mungu? Mungu huona ndani kabisa ya mioyo yetu. kwa hivyo Angewezaje kutochukizwa na mimi kujaribu kumdanganya, kumhadaa, na kumghilibu hivyo? Gizani ambako nilikuwa nimetumbukia kulikuwa Mungu kunirudi na kunifundisha nidhamu. Kugundua hili kuliniacha nikiogopa kidogo na nikafikiria kuhusu kutia ukweli katika vitendo kwa mkutano uliofuata. Lakini nilihisi wasiwasi kidogo, nikifikiria jinsi nilivyokuwa nimesema uwongo mkubwa sana. Je, wengine wangeniona vipi iwapo ningeukiri? Je, wangesema kuwa nilikuwa mjanja?

Kisha nikasoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu. “Unaposema uwongo, hupati aibu papo na hapo, lakini moyoni mwako unahisi kuwa umetahayarishwa kabisa, na dhamiri yako itakushutumu kwa kutokuwa mwaminifu. Ndani yako, utajidharau na kujichukia, na utawaza, ‘Kwa nini naishi kwa njia ya kusikitisha sana? Je, kwa kweli ni vigumu sana kusema ukweli? Je, ni lazima niseme uwongo huu kwa ajili tu ya sifa yangu? Kwa nini maisha yanachosha sana kwangu?’ Si lazima uishi maisha ya kuchosha, lakini hujachagua njia ya amani na uhuru. Umechagua njia ya kudumisha sifa na kiburi chako, kwa hivyo kwako maisha ni ya kuchosha sana. Je, ni sifa gani unayopata kutokana na kusema uongo? Sifa ni kitu tupu, na ni kitu kisichostahili hata kidogo. Kwa kusema uwongo, unauza unasaliti uadilifu wako na heshima yako. Uongo huu hukufanya upoteze hadhi yako na usiwe na uadilifu mbele za Mungu. Mungu hafurahii jambo hili na Analichukia sana. Kwa hivyo, je, ni jambo lenye thamani? Je, njia hii ni sahihi? Hapana, siyo, na kwa kuifuata huishi katika nuru. Wakati huishi katika nuru, unahisi uchovu. Wewe daima husema uongo na kujaribu kuufanya uongo huo uwe wa kusadikika, ukipiga bongo zako kufikiria upuuzi wa kusema, ukijisababishia mateso mengi, hadi mwishowe unafikiri, “Lazima nisiseme uwongo tena. Nitanyamaza kimya na niongee machache.” Lakini huwezi kujizuia kabisa. Kwa nini hivi? Huwezi kuacha vitu kama vile sifa na heshima yako, kwa hivyo unaweza tu kuvidumisha kwa kutumia uongo. Unahisi kuwa unaweza kutumia uwongo kushikilia vitu hivi, lakini kwa kweli, huwezi. Mbali na uwongo wako kutofanikiwa katika kudumisha uaminifu wako na heshima yako, pia, muhimu zaidi, umepoteza nafasi ya kutenda ukweli. Hata kama umedumisha sifa na heshima yako, umepoteza ukweli; umepoteza nafasi ya kuutia katika vitendo, na pia nafasi ya kuwa mtu mwaminifu. Hii ndiyo hasara kubwa zaidi(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kila neno la Mungu lilikwenda moja kwa moja moyoni mwangu. Nilidumisha sifa yangu baada ya kusema uwongo wangu, lakini sikuweza kuhisi furaha hata kidogo. Badala yake, nilikuwa na wasiwasi, nikihisi vibaya kila wakati juu ya kile nilichokuwa nimefanya. Wakati mwingine sikutaka kuwaangalia watu machoni niliponena, nikiogopa kuwa wangeona udanganyifu wangu na wasingeniamini tena. Nilijaribu hata mambo ya kila aina ili kuficha uwongo wangu na ili kuufanya uwe wa kuaminika. Ilikuwa njia ngumu na ya kuchosha ya kuishi, na sikuweza kupata faraja yoyote. Nilikuwa nimesema uwongo na kudanganya, na niliishi kwa namna inayostahili dharau na isiyo ya heshima. Kwa kuwa sikutaka kujificha tena, nilimwomba Mungu ili kukiri na kutubu na nikaamua kuwa nitaukana mwili wangu na kufungua moyo wangu wakati mwingine nitakapowaona ndugu.

Kiongozi alikuja kuhudhuria mkutano nasi siku chache baadaye na nikahisi kuwa Mungu alikuwa akinipa nafasi ya kutia ukweli katika vitendo. Niliomba, “Ee Mungu, niko tayari kufichua uwongo na udanganyifu wangu. Tafadhali nipe azimio la kutia ukweli katika vitendo.” Nilipofika, nilipata habari kuwa alikuwa amekuja kuchagua mwenzi wa kazi kutoka kati yetu viongozi wa kanisa. Mapambano ya ndani yaliibuka ndani yangu. Kati yetu viongozi wa kanisa, ubora wangu wa tabia na mafanikio yangu yalikuwa bora kuliko ya wengine kwa kiasi fulani kwa hivyo labda waliniona tayari kama mgombea anayefaa. Lakini iwapo ningesema ukweli na kufichua uwongo wangu, je, wangenidharau? Je, wangefikiria kuwa nilikuwa mjanja sana, na wasinichague? Nitawezaje kujitokeza tena iwapo mtu mwingine atachaguliwa? Niliona kwamba sikuweza kuongea kuhusu hilo. Nilipokuwa tu nikiinamisha kichwa changu huku nikiwaza sana, kiongozi aliniomba nishiriki jinsi nilivyokuwa hivi karibuni. Huku nikigugumiza maneno yangu, nilificha hali halisi. “Nimekuwa katika hali nzuri. Ninapokabiliwa na matatizo, najua kumwomba Mungu na kutafuta ukweli ili kuyatatua. …” Baada ya kusema haya, nilihisi kuwa nilikuwa nimefanya jambo la aibu na nikajawa na wasiwasi. Nilitokwa na jasho. Kiongozi alipoona kwamba niliendelea kufuta jasho, alinipa kikombe cha maji moto na akaniuliza kwa huruma ikiwa nilikuwa na mafua. Nikasema, “Sijui ni kwa nini, nahisi tu wasiwasi na siwezi kuacha kutokwa na jasho.” Kwa kweli, nilijua vizuri sana kwamba ilikuwa kwa sababu nilikuwa nimesema uwongo tena na sikuwa nimetia ukweli katika vitendo. Nilimwomba Mungu kimya kimya: “Mungu, nimesema uwongo mara nyingi, nikikataa kwa ukaidi kutia ukweli katika vitendo. Mimi ni mkaidi na mwasi sana. Tafadhali niongoze ili niweze kutenda ukweli na kuwa mtu mwaminifu.”

kisha Dada Liu alipendekeza tuuimbe wimbo wa maneno ya Mungu. “Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. … Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza(“Mungu Huwabariki Wale Walio Waaminifu” Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipokuwa nikiimba wimbo huu, nilihisi huzuni na aibu. Nilikuwa nimeomba kabla ya mkutano huo kwa sababu nilitaka kufungua moyo wangu kuhusu jinsi nilivyokuwa nimesema uwongo na kudanganya, lakini nilipogundua kuwa kiongozi alikuwa akichagua mtu wa kufanya naye kazi, sikutaka kufumbua jambo lolote. Niliogopa kiongozi na wafanyakazi wenzangu wajue kwamba sikuwa nimefanya kazi ya vitendo na nilikuwa hata nimesema uwongo, kwamba wangesema kuwa nilikuwa mjanja sana na wasingenichagua kwa nafasi hiyo. Kisha ningepoteza nafasi yangu ya kuwa kiongozi. Nilikuwa mdanganyifu sana! Mungu huona kila kitu. Naweza kuwadanganya wengine, lakini Mungu je? Maneno haya yalionekana waziwazi kabisa: “Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi” kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya Nilihisi wasiwasi hata zaidi. Je, si nilikuwa mtu mwenye siri nyingi ambazo nilisita kuzitoboa, kama tu Mungu alivyosema? Nilikuwa nimejuwa vizuri kabisa kuwa sikujua maelezo ya kazi ya kunyunyizia, lakini kiongozi aliponiuliza kuihusu, nilikuwa nimedanganya, na nilikuwa nimesema uwongo kwa makusudi, na niliporudi kanisani sikuwafungulia wengine moyo wangu ili kufichua upotovu wangu na makosa yaliyokuwa katika kazi yangu. Badala yake nilikuwa nimejaribu kuficha uwongo wangu na kuuendeleza huku nikionekana kufanya wajibu wangu. Huko kulikuwaje kufanya wajibu wangu? Ilikuwa tu kwa ajili ya kulinda heshima na hadhi yangu. Nilikuwa nikijaribu kumdanganya Mungu na kuwapotosha watu. Na kwa mara nyingine tena, ili kupata hiki cheo kipya, nilikana kiapo changu bila haya, nikimdanganya Mungu na mwanadamu. Nilikuwa nikisema uwongo na kudanganya mara nyingi! Kisha maneno haya kutoka kwa Mungu yalinijia akilini: “Lakini acheni maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; La, la: kwa maana chochote kinachozidi haya kimetoka kwa aliye mwovu(Mathayo 5:37). “Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo(Yohana 8:44). Nilijua vizuri sana kuwa Mungu huwapenda watu waaminifu, lakini nilikuwa nimesema uwongo na kuficha uwongo wangu tena na tena, nikijaribu kumdanganya Mungu na ndugu zangu. Je, nilitofautiana vipi na Shetani? Je, nilikuwa na ubinadamu mzuri hata kidogo? Nisingetubu na kubadilika, nilijua kwamba ningeelekea kwenye hatima sawa na Shetani. Wazo hili lilinitisha, kwa hivyo nilimwomba Mungu na nikajitia nguvu ya kuharibia sifa yangu mwenyewe. Nilifichua udanganyifu na mbinu ya kuficha makosa ambayo nilikuwa nikitumia na nia zangu za kustahili dharau na za ujanja kwa utondoti, bila kuacha lolote. Baada ya kusema ukweli kabisa nilihisi kana kwamba tatizo kubwa lilikuwa limeondolewa na nikahisi kutulia zaidi ghafla. Nilihisi uhuru na radhi moyoni mwangu.

Kina ndugu hawakunikaripia na kiongozi hata alinisomea kifungu cha maneno ya Mungu. “Watu wanaposhiriki katika udanganyifu, nia zipi zinatokana na hilo? Je, wanaonyesha tabia ya aina gani? Kwa nini wana uwezo wa kuonyesha tabia ya aina hii? Chanzo chake ni nini? Ni kwamba watu huchukulia masilahi yao ya binafsi kuwa ya maana zaidi kuliko mengine yote. Wao hushiriki katika udanganyifu ili kujinufaisha, na hivyo basi tabia zao danganyifu hufichuliwa. Tatizo hili linapaswa kutatuliwa vipi? Kwanza, lazima uachilie masilahi yako. Kuwashawishi watu waachilie masilahi yao ni jambo gumu zaidi kulifanya. Watu wengi zaidi hutafuta faida pekee; masilahi ya watu ni maisha yao, na kuwafanya waache mambo hayo ni sawa na kuwalazimisha watoe maisha yao. Kwa hivyo, unapaswa kufanya nini? Lazima ujifunze kuachilia, kujinyima, kuteseka, na kuvumilia uchungu wa kuacha masilahi unayopenda. Mara unapovumilia uchungu huu na kuachilia masilahi yako machache, utahisi kutulia na kukombolewa kidogo, na kwa njia hii, utaushinda mwili wako. Hata hivyo, ukishikilia masilahi yako na ushindwe kuyaacha, ukisema, ‘Nimekuwa mdanganyifu, lakini, kwa hivyo? Mungu hajaniadhibu, kwa hivyo watu wanaweza kunifanyia nini? Sitaacha lolote!’ Usipoacha lolote, hakuna mtu mwingine yeyote atakayepata hasara; ni wewe mwenyewe utakayepoteza hatimaye. Unapotambua tabia yako potovu, kwa kweli, hii ni fursa yako ya kuingia, kuendelea, na kubadilika; ni nafasi yako ya kuja mbele za Mungu na kukubali uchunguzi Wake na hukumu na kuadibu Kwake. Aidha, hii ni fursa yako ya kupata wokovu. Ukiacha kutafuta ukweli, basi hiyo ni sawa na kuacha nafasi ya kupata wokovu na kukubali hukumu na kuadibu. … Watu wakichagua kutenda ukweli, basi hata ikiwa wamepoteza masilahi yao ya binafsi, wanapata wokovu na uzima wa milele wa Mungu. Watu hao ndio werevu zaidi. Watu wakifaidika kwa gharama ya ukweli, basi wanayopoteza ni uzima na wokovu wa Mungu; watu hao ndio wajinga zaidi. Kwa mintarafu ya kile ambacho mtu atakichagua hatimaye—masilahi yake ya binafsi au ukweli—hili ni jambo linalomfichua mtu zaidi kuliko mambo mengine. Wale wanaopenda ukweli watachagua ukweli; watachagua kunyenyekea mbele za Mungu, na kumfuata. Wanaona ni afadhali waache masilahi yao. Bila kujali wameteseka kiasi gani, wameazimia kuwa mashahidi ili kumridhisha Mungu. Hii ndiyo njia ya msingi ya kutenda ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli(“Kujua Tabia ni Msingi wa Kubadili Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kusikia maneno haya kulichangamsha moyo wangu. Nilitafakari juu ya jinsi nilivyokuwa nimesema uwongo na kudanganya tena na tena hasa kwa sababu nilijali sana sifa na cheo, na kwa sababu nilikuwa na asili danganyifu. Nilikuwa nimeelimishwa na kutiwa kasumba na Shetani tangu nilipokuwa mdogo na nilikuwa nimetekwa na sumu zake nyingi kama vile “Mbingu huwaangamiza wale ambao hawajiwakilishi” “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” “Uwongo utakuwa ukweli ukirudiwa mara elfu kumi,” “Mwanadamu hawezi kutimiza chochote bila kusema uongo,” “Fikiria kabla ya kunena na kisha zungumza kwa kusita" na kadhalika. Falsafa hizo za kishetani ziligeuka kuwa sheria zangu za kuendelea kuishi. Nilikuwa nimeishi kulingana nazo, nikizidi kuwa mbinafsi, mdanganyifu na bandia. Nilifikiria tu masilahi yangu daima na sikuweza kujizuia kusema uwongo na kudanganya kwa sababu hiyo. Ingawa nilihisi hatia na nikajilaumu baada ya kusema uwongo na nilitaka kutubu kwa Mungu na kuwafungulia wengine moyo, hofu yangu ya kuaibishwa na kuchekwa ilinifanya niendelee kujificha na kujifanya. Sikuwa tayari kufungua moyo wangu na kufichua nia zangu za ujanja na tabia danganyifu. Sikuwa hasa na ujasiri wa kujivunjia heshima na kuwa mkweli, nikifikiri kwamba punde ambapo ningewaambia ukweli, watu wangegundua asili yangu ya kweli, na wasingeniheshimu tena. Nilipendelea kupambana gizani na kwa uchungu kuliko kutenda ukweli na kuwa mwaminifu. Niliona jinsi Shetani alivyonipotosha sana! Bila Mungu kunifichua kwa njia hiyo, bila hukumu na ufunuo wa maneno Yake, singeona kamwe jinsi asili yangu ilivyokuwa ya ujanja, na singekuwa nimetiwa hamasa ya kutia ukweli katika vitendo na kufichua hali yangu halisi. Niligundua wakati huo kuwa hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake vilikuwa Yeye kunilinda na kuniokoa, na nilihisi jinsi kufuatilia ukweli na kujizoeza kuwa mwaminifu kulivyo muhimu kwangu.

Kuanzia wakati huo kuendelea, nilikusudia kujizoeza kusema ukweli na kuwa mtu mwaminifu. Baada ya muda, niligundua kuwa kiongozi ambaye alijiunga nasi katika mikusanyiko wakati mwingine alikuwa mwenye kiburi na mwenye kujidai na hakukubali mapendekezo ya wengine kwa urahisi. Nilitaka kumtajia hilo mara kadhaa, lakini nikawaza, “Ni sawa na vyema akikubali nitakachosema. lakini asipokubali, atanionaje?” Niliamua kusubiri na kuona. Siku moja aliniuliza, “Dada, tumejuana kwa muda mrefu sasa. Ukiona tatizo lolote ndani yangu, tafadhali nijulishe. Hiyo itanisaidia.” Nilimtazama na nilikuwa karibu kusema, “Sijaona lolote. Wewe ni mzuri sana.” Lakini niligundua kuwa huo ungekuwa udanganyifu, kwa hivyo nilimwomba Mungu na nikawa tayari kukubali uchunguzi Wake wa makini. Sikuweza kuendelea kusema uwongo na kudanganya, nikichochea maudhi ya Mungu. Kwa hivyo, nilifungua moyo wangu na nikamwambia kuhusu tatizo lake. Alisikiza, kisha akaashiria kwa kichwa na kusema, “Shukrani kwa Mungu! Usingeniambia nisingegundua hili. Ninahitaji kutafakari sana kujihusu na kuelewa hili.” Nilifurahi sana nilipoona kwamba aliweza kulikubali. Nilihisi amani na kufunguliwa sana na kweli nikapata uzoefu wa jinsi ilivyo vizuri sana kutia ukweli katika vitendo na kuwa mtu mwaminifu!

Iliyotangulia: 13. Ukombozi wa Moyo

Inayofuata: 19. Ubora Duni wa Tabia Sio Kisingizio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

40. Tiba ya Wivu

Na Xunqiu, UchinaMwenyezi Mungu anasema, “Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni...

31. Kushikilia Wajibu Wangu

Na Yangmu, Korea ya KusiniNilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu....

32. Roho Yangu Yakombolewa

Na Mibu, Uhispania“Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp