185 Nimemwona Mungu

1 Niliisikia sauti ya Mungu na nikaja mbele Yake. Niliita jina Lake kwa sauti, kama ninayerudi kwa mama yangu. Alijua maumivu ndani ya moyo wangu, Alijua nilichokitamani sana. Maneno ya Mungu yalitosheleza moyo wangu wenye kiu, Nilionja utamu wa maneno Yake na wema wa familia Yake. Hukumu ya maneno ya Mungu yanafichua ukweli wa uovu na upotovu wa mwanadamu.Hatimaye niliona nimejazwa na tabia za kishetani na niliishi tu kwa ajili ya mwili. Imani yangu katika Bwana ilikuwa kwa ajili ya baraka tu, kutafuta umaarufu na utajiri. Nilipoteza dhamiri yangu kama mwanadamu zamani sana. Hukumu ya Mungu iliniokoa, acha niishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu. Kwa kuwa Kristo ni ukweli na uzima, niliacha vyote ili kumfuata Yeye.

2 Nimevuna mengi sana kupitia hukumu ya maneno ya Mungu. Ni ukweli na uzima, najua hii kabisa. Maneno ya Mungu yanatakasa upotovu wangu na kunipa kila kitu. Mungu ni mnyenyekevu na amejificha—nimeona hii ni nzuri sana. Hukumu ya Mungu ni kwa wokovu wa wanadamu kabisa. Moyo wa Mungu ni karimu sana. Tabia ya haki ya Mungu haistahimili kosa lolote, ninamcha Yeye na kumtii moyoni mwangu. Nikipitia hukumu ya Mungu, upotovu wangu unatakaswa, nimekutana uso kwa uso na Mungu. Nafurahia maneno Yake kila siku, naishi mbele Yake, moyo wangu umejaa furaha na amani. Upendo wa Mungu ni wa kweli na halisi sana, Anastahili sifa za wanadamu. Ningependa kumpenda na kumshuhudia Mungu, kuwa ubavuni Mwake milele.

Iliyotangulia: 184 Ufalme

Inayofuata: 186 Nimeona Moyo wa Mungu Ndio Unaopendeza na Karimu Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp