Kuboresha Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea, Ili muweze kuelewa maneno ya Mungu na kujua jinsi ya kutenda kulingana nayo. Hili ndilo hitaji la msingi kabisa. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Haidhuru ni maneno mangapi Ninayosema, ikiwa hamuwezi kufika hapo, ikiwa hamuwezi kuyaelewa bila kujali Ninachosema, hii inamaanisha mna upungufu wa ubora wa tabia. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile Ninachosema. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu. Ni muhimu kuzindua kazi hii ya “kuinua ubora wa tabia ya watu” miongoni mwenu kwa sababu uwezo wenu wa kupokea, uwezo wa kuona mambo, na viwango ambavyo kwavyo mnaishi vimepungukiwa sana, kazi ya “uinuaji wa ubora wa tabia” sharti ifanywe ndani yenu. Hili ni jambo lisiloepukika, na hakuna mbadala. Ni kwa njia hii tu ndiyo matokeo fulani yanaweza kutimizwa; la sivyo, maneno yote Ninayosema hayatafanikiwa, na hamngekumbukwa kama wenye dhambi? Je! Hamngekuwa wapotovu? Je, hamjui ni kazi gani inayofanywa kwenu na ni nini kinachohitajika kutoka kwenu? Mnapaswa kujua ubora wenu wenyewe wa tabia; hauwezi kufikia kile Ninachohitaji kamwe. Je, hii haicheleweshi kazi? Kwa ubora wa tabia na hulka yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye anafaa kushuhudia kwa ajili Yangu, na hakuna mtu anayewezana na kazi ya kulichukua jukumu kubwa la kazi Yangu ya baadaye. Je, hamhisi aibu sana? Mkiendelea kwa njia hii, mnawezaje kuyaridhisha mapenzi Yangu? Unapaswa kuishi maisha yako kikamilifu. Usiruhusu muda upite bure. Hakuna thamani katika kufanya hivyo. Unapaswa kujua mambo ambayo inabidi kujiandaa nayo. Usijione kuwa mjuaji wa kila kitu. Hukaribii hata kidogo! Je! Kuna nini cha kuzungumzia ikiwa huna hata ufahamu wa kimsingi wa ubinadamu? Je, si vyote havingekuwa na maana? Na kwa hivyo hakuna hata mmoja wenu aliye na ubinadamu na ubora wa tabia ninaohitaji kwa ukamilifu. Ni vigumu kupata mtu ambaye anafaa kutumiwa. Mnaamini ninyi ni watu ambao wanaweza kufanya kazi kubwa zaidi kwa ajili Yangu na kujitwika ukabidhi mkubwa kutoka Kwangu. Kwa kweli, hamjui jinsi hata ya kuingia katika masomo mengi mbele yenu, hivyo ingewezekanaje kuingia katika kweli za kina? Kuingia kwenu kunapaswa kufuata mpangilio na kwa viwango. Hakupaswi kuwa kwa vurugu—hiyo haina manufaa. Anzeni na uingiaji wa juu juu kabisa: Yasome maneno haya mstari kwa mstari hadi mfikie ufahamu na ubayana. Mnaposoma maneno ya Mungu, msiyapitie kwa juu juu tu kana kwamba unapendezwa na maua huku ukienda shoti mgongoni mwa farasi, na usilifanye kwa namna isiyo ya dhati. Unaweza pia kusoma baadhi ya vitabu vya kumbukumbu mara kwa mara (kama vile vitabu juu ya sarufi au vya balagha) ili kukuza maarifa yako. Usisome vitabu kama vile riwaya za mapenzi, wasifu za watu mashuhuri au vile vinavyohusu sayansi ya kijamii; hivi havina manufaa, na vinaweza tu kusababisha. Lazima uwe mweledi wa yote unayopaswa kuingia na unapaswa kufahamu. Madhumuni ya kuendeleza ubora wa tabia sio mengine ila kuwasaidia watu kujua asili yao wenyewe, utambulisho, hadhi na thamani. Unapaswa kuelewa kwa nini lazima watu wafuatilie ukweli katika kumwamini Mungu, na iwapo inakubalika kwa watu kutoinua ubora wao wa tabia. Ni muhimu kwamba ujielimishe kila wakati; ni sharti usitupe hili mbali! Lazima uelewe kwa nini ubora wa tabia wa watu sharti uinuliwe, jinsi unavyopaswa kuinuliwa, na ni vipengele vipi unavyopaswa kuingia katika. Lazima muelewe maana ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, kwa nini kazi hii inapaswa kufanywa, na jinsi watu wanapaswa kuratibu. Katika kuelimika, mnapaswa kuwa dhahiri kuhusu vipengele vipi vinayopaswa kufunzwa, na jinsi gani mtu anapaswa kuingia. Nyote mnapaswa kujua lengo la kuelimika ni nini. Je, sio kuyafahamu maneno ya Mungu na kuingia katika ukweli? Hali inayosambaa makanisani sasa ni ipi? Mkimwomba mtu apate kuelimika, anasahau kuhusu furaha ya maneno ya Mungu. Hafanyi chochote siku nzima kando na kuelimishwa. Mkimhitaji kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, anashughulikia tu kuisafisha nyumba yake, kupika, au kununua vyombo vya kupika. Anajali tu kuhusu mambo haya na hajui jinsi ya kuishi maisha ya kanisa kwa kawaida. Umepotoka katika matendo yako ikiwa unabaki katika hali ya sasa. Basi kwa nini unaombwa kuingia katika maisha ya kiroho? Yote unayojifunza ni mambo haya ambayo hayawezi kukusaidia kufikia kile kinachohitajika kwako. Jambo la muhimu zaidi bado ni kuingia kwa maisha. Sababu ya kufanya kazi hii ni kutatua shida ambazo watu hukumbana nazo katika uzoefu wao. Kuinua ubora wa tabia kunakuruhusu kujua ubinadamu na kiini cha mwanadamu—kusudi kuu la kuyajua mambo haya ni ili maisha ya watu ya kiroho yaweze kukua na tabia yao iweze kubadilika. Unaweza kujua jinsi ya kuvaa na kupendeza; unaweza kuwa na utambuzi na hekima, na hata hivyo hatimaye, siku inapokuja kwako kuenda kazini, unashindwa kufanya hivyo. Unapaswa kujua, kwa hiyo, kile unapaswa kufanya pia wakati unainua ubora wako wa tabia. Kukubadilisha ni lengo. Kuinua ubora wa tabia ni jambo la ziada. Haitakubalika kama ubora wako wa tabia hauendelezwi. Ni vibaya hata zaidi ikiwa tabia yako haiwezi kubadilishwa. Moja bila ya nyingine haitoshi. Kuwa na ubinadamu wa kawaida hakumaanishi kwamba umekuwa na ushuhuda mkubwa sana. Kile kinachohitajika kwako si rahisi sana.

Wakati ambapo ubora wa tabia ya mtu umeendelea kiasi kwamba ana hisia na mtindo wa maisha ya ubinadamu wa kawaida na pia kuwa na kuingia kwa maisha, ni hapo tu ndipo ataweza kubadilika na kushuhudia. Siku ya kutoa ushuhuda inapofika, pia kuna haja ya kuzungumza kuhusu mabadiliko katika maisha ya binadamu na kuhusu ufahamu wa Mungu ndani. Mchanganyiko wa vipengele hivi viwili tu ndio ushahidi wa kweli na faida yako ya kweli. Haitakubalika ikiwa una mabadiliko tu katika ubinadamu kwa nje na huna ufahamu kwa ndani. Haitakubalika pia ikiwa una ufahamu na ukweli kwa ndani lakini hutilii maanani kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida. Kazi inayofanyika kwako leo sio kuwaonyesha wengine bali kukubadilisha. Unahitaji tu kuzingatia kujibadilisha. Unaweza kuandika na kusikiliza kila siku, lakini haitawezekana ikiwa hushiriki katika maeneo mengine ya maisha yako. Unapaswa kuwa na kuingia katika kila kipengele. Unapaswa kuwa na maisha ya kawaida ya mtakatifu. Akina dada wengi huvaa kama wanawake matajiri na kaka wanavaa kama waungwana matajiri au mabwana, wakipoteza kabisa ustahifu wa watakatifu. Kipengele kimoja ni kuinua ubora wa tabia ya mtu, ambacho kinaweza kufanikishwa kwa kawaida. Kipengele kingine cha umuhimu mkubwa ni kula na kunywa maneno ya Mungu. Je, haingekuwa kupoteza elimu ikiwa ubora wako wa tabia umeinuliwa lakini haukukutumiwa kwa sababu hukula na kunywa maneno ya Mungu? Lazima vipengele vyote viwili viunganishwe. Kwa nini maarifa ya Mungu yanatajwa katika majadiliano ya kile kinachohitajika kwako? Je, hii si kwa ajili ya matokeo ya kazi ya baadaye? Baada yako kushindwa, lazima uweze kushuhudia kutokana na uzoefu wako mwenyewe. Haitakubalika kama sura yako ya nje ni moja ya ubinadamu wa kawaida lakini huwezi kuonyesha uzoefu wako kupitia kinywa chako. Unapokuwa na maisha ya kawaida ya kiroho, unapaswa kufikia ubinadamu wa kawaida, na vipengele vingi vya ubinadamu wa kawaida vitaweza kufunzwa kwa dhahiri. Je, ungesema kwamba kufagia sakafu kunahitaji mafunzo maalum? Ikiwa unahitaji kutumia saa moja kufanya mazoezi jinsi ya kushikilia vijiti kwa kula, hiyo haikubaliki hata zaidi! Ni nini kinashirikishwa ndani ya ubinadamu wa kawaida? Utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida. Hiyo itakuwa imetosha. Kila kitu kinachohitajika kwako leo kiko katika uwezo wako, na huku si kukulazimisha ufanye kadri ya uwezo wako hata kidogo. Hakuna maneno yasiyo na maana au kazi isiyofaa yatakayotekelezwa kwako. Uovu wote ulioonyeshwa au kufichuliwa katika maisha yako lazima uondolewe. Ninyi mmepotoshwa na Shetani na mna sumu nyingi sana za Shetani. Yote ambayo yanahitajika kwako ni kuiepuka tabia hii potovu ya kishetani, si wewe kuwa mtu mwenye cheo cha juu, au mtu maarufu au mkuu. Hii haina maana. Kazi ambayo imefanyika kwenu inaafikiana na kile ambacho ni cha asili kwenu. Kuna mipaka ya kile Ninachohitaji kutoka kwa watu. Ikiwa watu wa leo wote wangeombwa kutenda kama maafisa wa serikali, na kujizoeza toni ya sauti ya maafisa wa serikali, kujifunza katika namna ya kuzungumza ya viongozi wa serikali wenye cheo cha juu, au kujifunza kwa namna na sauti ya kuzungumza ya waandishi wa insha na waandishi wa riwaya, basi hili halingekubalika pia. Halingeweza kufikiwa. Kwa mujibu wa ubora wa tabia zenu, mnapaswa angalau kuweza kuzungumza kwa hekima na busara na kuelezea mambo wazi. Ni wakati huo ndipo mtakapoyatosheleza mahitaji. Kwa kiwango kidogo sana, utambuzi na hisia vinapaswa kufikiwa. Kwa sasa jambo kuu ni kuitupilia mbali tabia potovu ya kishetani. Lazima uutupilie mbali uovu unaouonyesha. Ikiwa hujavitupilia mbali hivi, unawezaje kugusia hisia na utambuzi wenye mamlaka mkubwa kabisa? Watu wengi wanaona kwamba enzi imebadilika. Hivyo hawajizoezi unyenyekevu au uvumilivu wowote, na pengine pia hawana upendo wowote au mwenendo mwema wa kitakatifu pia. Watu hawa ni wajinga mno! Je, wana kiwango chochote cha ubinadamu wa kawaida? Je, wanao ushuhuda wowote wa kuzungumziwa? Hawana utambuzi na hisia zozote kamwe. Bila shaka, vipengele fulani vya utendaji wa watu vilivyopotoka na vyenye makosa vinapaswa kurekebishwa. Kama vile maisha ya watu ya kiroho yasiyopindika ya zamani au mwonekano wao wenye ganzi na upumbavu—vitu hivi vyote vinapaswa kubadilika. Mabadiliko hayamaanishi kukuruhusu uwe mpotovu au kujiingiza katika mwili, kusema chochote utakacho. Kuzungumza kiholela hakuwezi kukubalika. Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye. Inapaswa kujulikana ni mipaka gani mtu wa kawaida anaweza kufikia kuhusu mabadiliko ya tabia. Ikiwa hiyo haijulikani, hutaweza kuingia katika uhalisi.

Iliyotangulia: Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu

Inayofuata: Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp