Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wameacha matarajio na kudura yao ya baadaye kiasi. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi kati wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. Moabu ilifukuzwa hadi nchi hii baada ya kulaaniwa. Ukoo wa wana wa Moabu umerithishwa mpaka leo, na ninyi nyote ni uzao wake. Hakuna kitu ambacho Ninaweza kufanya—nani aliyekusababisha uzaliwe katika nyumba ya Moabu? Ninakuhurumia na Siko radhi uwe hivi, lakini ukweli hauwezi kubadilishwa na watu. Wewe ni uzao wa Moabu, na Siwezi kusema kuwa wewe ni uzao wa Daudi. Haijalishi wewe ni uzao wa nani, bado wewe ni mmoja wa viumbe. Ni kwamba tu wewe ni kiumbe wa cheo cha chini—wewe ni kiumbe wa kuzaliwa katika hali duni. Viumbe vyote lazima vipitie kazi yote ya Mungu, vyote ni vyombo vya kushinda Kwake, na lazima vyote viione tabia Yake yenye haki, na kupitia hekima na kudura Yake. Sasa wewe ni uzao wa Moabu na lazima uikubali hukumu hii na kuadibu, hivyo kama hungekuwa uzao wa Moabu, basi pia hungehitaji kukubali hukumu na kuadibu huku? Unapaswa kutambua hili! Kwa kweli, kufanya kazi kwa uzao wa Moabu kwa sasa ni kwa thamani sana na kwenye umuhimu sana. Maadam kazi imefanywa kwenu, ina umuhimu mkubwa mno. Kama kazi ingefanywa kwa uzao wa Hamu haingeweza kuwa muhimu kwa sababu wao hawajazaliwa katika hali duni kama hiyo na kuzaliwa kwao sio sawa na Moabu. Uzao wa mwana wa pili wa Nuhu Hamu umelaaniwa tu—hawakuja kutokana na uasherati. Ni kwamba tu wao ni wa hali ya chini, kwa sababu Nuhu aliwalaani na wao ni watumishi wa watumishi. Wanayo hali ya chini, lakini thamani yao ya asili haikuwa chini. Tukizungumza kuhusu Moabu, watu wanajua kwamba awali alikuwa na hali ya chini kwa sababu alizaliwa kutokana na uasherati. Ingawa nafasi ya Loti ilikuwa ya juu sana, Moabu alizaliwa na Lutu na binti yake. Lutu aliitwa mtu mwenye haki, lakini Moabu bado alikuwa amelaaniwa. Moabu alikuwa wa thamani ya chini na alikuwa na cheo cha chini, na hata kama hakuwa amelaaniwa alikuwa wa uchafu, hivyo alikuwa tofauti na Hamu. Hakukubali na alipinga, aliasi dhidi ya Yehova, ndiyo sababu alianguka katika maeneo yenye giza zaidi. Kufanya kazi sasa kwa uzao wa Moabu ni kuwaokoa wale ambao wameanguka katika giza zaidi. Ingawa walikuwa wamelaaniwa, Mungu yuko tayari kupata utukufu kutoka kwao. Hii ni kwa sababu hapo awali, wote walikuwa watu waliomkosa Mungu mioyoni mwao—kuwafanya tu kuwa wale wanaomtii na kumpenda Yeye ni ushindi wa kweli, na matunda hayo ya kazi ni ya thamani sana na yenye kuridhisha zaidi. Huku tu ni kupata utukufu—huu ndio utukufu ambao Mungu anataka kuupata katika siku za mwisho. Ingawa watu hawa ni wa nafasi ya chini, sasa wanaweza kupata wokovu mkubwa mno, ambao kwa kweli ni kupandishwa hadhi na Mungu. Kazi hii ni ya maana sana, na ni kwa njia ya hukumu ndipo Anawapata watu hawa. Yeye hawaadhibu kwa makusudi, lakini Amekuja kuwaokoa. Kama angekuwa Anafanya kazi ya kushinda katika Israeli wakati wa siku za mwisho ingekuwa ni bure; hata kama ingezaa matunda, haingekuwa na thamani yoyote au umuhimu wowote mkubwa, na Yeye hangeweza kupata utukufu wote. Anafanya kazi kwenu, yaani, wale ambao wameanguka katika maeneo yenye giza zaidi, wao walio nyuma zaidi kimaendeleo. Watu hawa hawakiri kuwa kuna Mungu na kamwe hawajapata kujua kwamba kuna Mungu. Viumbe hawa wamepotoshwa na Shetani hadi kiwango ambapo wamemsahau Mungu. Wamepofushwa na Shetani na hawajui kabisa kwamba kuna Mungu mbinguni. Katika mioyo yenu nyote mnaabudu sanamu, mnamwabudu Shetani—je, si ninyi ni watu wa hali ya chini zaidi, watu walio nyuma zaidi kimaendeleo? Ninyi ni wa hali ya chini kabisa ya mwili, mnakosa uhuru wowote wa kibinafsi, na mnapitia shida pia. Ninyi pia ni watu mlio katika ngazi ya chini kabisa katika jamii hii, bila hata uhuru wa imani. Huu ni umuhimu wa kufanya kazi kwenu. Kufanya kazi kwenu sasa, uzao wa Moabu, sio kuwafedhehesha kwa makusudi, lakini ni kufichua umuhimu wa kazi. Ni kuwainua sana. Ikiwa mtu ana mantiki na utambuzi, atasema: “Mimi ni uzao wa Moabu. Kweli sistahili kuinuliwa kukuu huku na Mungu ambako nimepokea sasa, au baraka hizi nyingi. Kwa mujibu wa yale ninayofanya na kusema, na kulingana na hali na thamani yangu—sistahili kabisa hizo baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Waisraeli wana upendo mkubwa kwa Mungu, na neema wanayoifurahia imefadhiliwa kwao na Yeye, lakini hali yao ni ya juu zaidi kuliko yetu. Abrahamu alijitolea sana kwa Yehova, na Petro alijitolea sana kwa Yesu—ibada yao ilishinda yetu kwa mara mia, na kwa msingi wa matendo yetu hatufai kabisa kufurahia neema ya Mungu.” Huduma ya watu hawa nchini China haiwezi kuletwa mbele za Mungu hata kidogo. Ni fujo kamili tu, na kwamba sasa mnafurahia neema nyingi za Mungu ni kuinuliwa na Mungu kabisa! Je, ni wakati upi mmeitafuta kazi ya Mungu? Je, mmeyatoa maisha yenu kwa Mungu lini? Ni wakati gani mmeiacha familia yako kwa urahisi, wazazi wenu, na watoto wenu? Hakuna hata mmoja wenu aliyelipa gharama kubwa! Kama haingekuwa kwa Roho Mtakatifu kukufanya uonekane, wangapi wenu wangeweza kutoa dhabihu kila kitu? Ni kwa sababu tu mmelazimishwa na kushurutishwa ndipo mmefuata hadi leo. Ibada yenu iko wapi? Utiifu wenu uko wapi? Kulingana na matendo vyenu, mngepaswa kuangamizwa muda mrefu uliopita—mngeondolewa kabisa. Nini kinawafanya mstahili kufurahia baraka nyingi mno? Hamstahili hata kidogo! Nani kati yenu amebuni njia yake mwenyewe? Ni nani kati yenu ameipata njia ya ukweli mwenyewe? Ninyi nyote ni wavivu na walafi, fidhuli msio na maana ambao mnasherehekea katika faraja kwa tamaa! Mnafikiri ninyi ni wakubwa sana? Je, nini mlicho nacho cha kujivunia? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wa Moabu, je, asili yenu, mahali penu pa kuzaliwa ni ya fahari sana? Hata kama Singesema ninyi ni uzao wake, je, si ninyi nyote ni uzao wa Moabu kwa kweli? Ukweli wa mambo unaweza kubadilishwa? Je, kufichua asili yenu sasa kunaenda dhidi ya ukweli wa mambo? Angalieni jinsi mlivyo wanyonge, maisha yenu, na tabia—je, hamjui kwamba ninyi ni wa chini kabisa kati ya walio chini miongoni mwa wanadamu? Nini mlicho nacho cha kujisifia? Angalia nafasi yenu katika jamii. Je, si mko katika kiwango cha chini kabisa? Je, mnadhani kwamba Nimenena vibaya? Ibrahimu alimtoa Isaka. Nini ambacho mmetoa? Ayubu ilitoa kila kitu. Nini ambacho mmetoa? Watu wengi sana wameyatoa maisha yao, wakafa, wakamwaga damu yao ili kutafuta njia ya kweli. Je, mmelipa gharama hiyo? Kwa kulinganisha, hamna sifa zinazostahili hata kidogo kufurahia neema hiyo kubwa, kwa hivyo ni sawa kusema leo kwamba ninyi ni uzao wa Moabu? Msijione kuwa wakuu sana. Huna chochote cha kujisifia. Wokovu mkubwa kama huo, neema hiyo kubwa imepewa kwenu bure. Hamjatoa chochote, lakini mmeifurahia neema bure. Je, hamuoni haya? Je, njia hii ya ukweli ni jambo ambalo ninyi wenyewe mlipata kupitia kutafuta? Je, si ni Roho Mtakatifu aliyewalazimisha kuikubali? Kamwe hamkuwa na moyo wa kutafuta na hasa hamkuwa na mioyo ya kuutafuta ukweli, ya kuutamani ukweli. Mmekuwa tu mkistarehe na kuufurahia, na mmeupata ukweli huu bila jitihada kwa upande wenu. Mna haki gani ya kulalamika? Je, unadhani kuwa wewe ni wa thamani kubwa zaidi? Ikilinganishwa na wale ambao walitoa dhabihu maisha yao na kumwaga damu yao, nini mnachopaswa kulalamikia? Kuwaangamiza hivi sasa litakuwa ni jambo linalotarajiwa! Kando na kutii na kufuata, hamna chaguzi zingine. Ninyi hamstahili kabisa! Wengi wa wale kati yenu waliitwa, lakini kama mazingira hayangewalazimisha au kama hamngeitwa, hamngekuwa tayari kabisa kutokea wazi. Nani yuko tayari kutelekeza mambo kwa namna hii? Ni nani yuko tayari kuacha anasa za mwili? Ninyi nyote ni watu ambao husherehekea kwa ulafi katika faraja na kutafuta maisha ya anasa! Mmepata baraka nyingi mno—nini kingine mnacho cha kusema? Mna malalamiko yapi? Mmefurahia baraka nyingi mno na neema kuu mno mbinguni, na kazi sasa imefichuliwa kwenu ambayo haikuwahi kufanywa duniani awali. Je, si hii ni baraka? Kwa sababu mmempinga na kuasi dhidi ya Mungu, sasa mmepitia kuadibu kiasi hiki. Kwa sababu ya kuadibu huku mmeziona rehema na upendo wa Mungu, na hata zaidi mmeziona haki na utakatifu Wake. Kwa sababu ya kuadibu huku na kwa sababu ya uchafu wa wanadamu, mmeiona nguvu kuu ya Mungu, na mmeuona utakatifu na ukuu Wake. Je, si huu ni ukweli adimu mno? Je! Si haya ni maisha yenye maana? Kazi ambayo Mungu hufanya ina maana tele! Hivyo nafasi yenu ilivyo chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kuinuliwa na Mungu, na ndivyo inavyothibitisha zaidi jinsi kazi Yake ilivyo na thamani kwenu leo. Ni hazina yenye thamani mno hasa! Haiwezi kupatikana popote pengine! Kwa muda mrefu hakuna mtu aliyefurahia wokovu mkubwa hivi. Ukweli kwamba nafasi yenu ni ya chini inaonyesha jinsi wokovu wa Mungu ulivyo mkuu, na inaonyesha kwamba Mungu ni mwaminifu kwa wanadamu—Yeye huokoa, sio kuangamiza.

Watu wa Uchina hawajawahi kumwamini Mungu na hawajawahi kumhudumia Yehova, hawajawahi kumhudumia Yesu. Yote wanayofanya ni kusujudu, kufukiza uvumba, kuchoma sanamu ya Mungu ya karatasi, na kumwabudu Buddha. Wao wanaabudu sanamu tu—wote ni waasi mno, hivyo jinsi nafasi ya watu ilivyo ya chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba kile Mungu hupata kutoka kwenu ni utukufu hata zaidi. Kutoka kwa mtazamo wa watu fulani, wangesema: “Mungu, ni kazi gani Unayofanya? Wewe, Mungu mwenye fahari sana, Mungu mtakatifu mno, ulikuja katika nchi yenye uchafu? Je, Unajidharau sana hivyo? Sisi ni wachafu sana, lakini Uko radhi kuwa pamoja nasi? Uko tayari kuishi kati yetu? Sisi ni wa cheo cha chini sana, lakini Uko radhi kutufanya kuwa kamili? Na Ungetutumia sisi kama mifano na vielelezo?” Ninasema: Huelewi mapenzi Yangu. Huelewi kazi ambayo Nataka kufanya wala huelewi tabia Yangu. Huwezi kufikia umuhimu wa kazi ambayo Ninaenda kufanya. Je, kazi Yangu ingepatana na mawazo ya kibinadamu? Kulingana na mawazo ya kibinadamu, Ningelazimika kuzaliwa katika nchi nzuri ili kuonyesha kwamba mimi ni wa hali ya juu, kuonyesha kwamba Mimi ni wa thamani kubwa, na kuonyesha kuheshimiwa Kwangu, utakatifu, na ukuu Wangu. Kama Ningezaliwa mahali ambapo pananitambua, katika familia ya ngazi ya juu, na kama Ningekuwa wa cheo na hadhi ya juu, basi Ningetendewa vizuri sana. Hiyo haingekuwa na manufaa kwa kazi Yangu, hivyo je, wokovu mkuu mno bado ungeweza kufichuliwa? Wote wanaoniona Mimi wangenitii, na hawangenajisiwa na uchafu. Nilipaswa kuzaliwa katika mahali pa aina hii. Hivyo ndivyo ninyi mnaamini. Lakini litafakari: Je! Mungu alikuja duniani kwa ajili ya raha, au kwa ajili ya kazi? Kama Ningefanya kazi katika aina ya mahali hapo rahisi, mahali penye starehe, je, Ningepata utukufu Wangu kamili? Je, Ningeweza kuvishinda viumbe Vyangu vyote? Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utuu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Je, si kazi Yake yote ni kwa ajili yenu, wanadamu hawa? Kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeishi na kuteswa pamoja na wenye dhambi kwa miaka mingi sana baada ya kuzaliwa horini? Na kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeurudia mwili kwa mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Je, si Mungu ni mwaminifu? Ni aina gani ya kazi Yake ambayo haijakuwa kwa ajili ya wanadamu? Ni aina gani ambayo haijakuwa kwa ajili ya kudura yako? Mungu ni mtakatifu. Hili haliwezi kubadilika! Yeye hanajisiwi na uchafu, ingawa Amekuja katika nchi yenye uchafu; yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana! Hamjui kwamba Yeye hupitia aibu kubwa sana kwa ajili yenu wote na kwa ajili ya kudura yenu? Je, hamjui hivyo? Yeye hawaokoi watu wakuu au wana wa familia tajiri na zenye uwezo, lakini Yeye huwaokoa hasa wale ambao ni wa hali za chini na wanaodharauliwa na wengine. Je, si haya yote ni utakatifu Wake? Je, si haya yote ni haki Yake? Afadhali Azaliwe katika nchi yenye uchafu na kuteseka aibu yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote. Mungu ni halisi sana—Hafanyi kazi ya uwongo. Je, si kila hatua ya kazi Yake imefanyika kwa utendaji hivi? Ingawa watu wote wanamkashifu na kusema kuwa Anakaa mezani pamoja na wenye dhambi, ingawa watu wote wanamdhihaki na kusema kuwa Anaishi na wana wa uchafu, na watu wa hali ya chini sana, bado Anajitolea bila ubinafsi, na bado Anakataliwa kwa njia hii kati ya wanadamu. Je, si mateso Anayoyahimili ni makubwa zaidi kuliko yenu? Je, si kazi Yake ni zaidi ya gharama ambayo mmelipa? Mlizaliwa katika nchi ya uchafu lakini mmepata utakatifu wa Mungu. Mlizaliwa katika nchi ambako mapepo hukusanyika lakini mmepokea ulinzi mkubwa. Je, mna uchaguzi gani mwingine? Ni malalamiko yapi mliyo nayo? Je, si mateso ambayo Amevumilia ni makubwa zaidi kuliko mateso ambayo mmevumilia? Amekuja duniani na hajawahi kufaidi furaha za ulimwengu wa kibinadamu. Anayachukia mambo hayo. Mungu hakuja duniani kufurahia manufaa ya kibinadamu kutoka kwa mwanadamu, wala haikuwa kufurahia mambo mazuri ya wanadamu kula na kuvalia. Hazingatii mambo haya; Alikuja duniani kuteseka kwa ajili ya mwanadamu, si kufurahia mambo mazuri ya kidunia. Alikuja kuteseka, Alikuja kufanya kazi, na kukamilisha mpango Wake wa usimamizi. Hakuchagua mahali pazuri, kuishi katika ubalozi au hoteli ghali mno, wala Hana watumishi kadhaa kumtumikia. Kutokana na kile mmeona, hamjui kama Alikuja kufanya kazi au kufurahia? Je, macho yenu hayafanyi kazi? Amewapa kiasi gani? Kama Angezaliwa katika mahali pazuri Angeweza kuupata utukufu? Je, Angeweza kufanya kazi? Je! Huko kungekuwa na umuhimu wowote? Angeweza kuwashinda kabisa wanadamu? Angeweza kuwaokoa watu kutoka katika nchi ya uchafu? Kulingana na mawazo ya kibinadamu, “Mungu, kwa kuwa Wewe ni mtakatifu, kwa nini Ulizaliwa katika mahali penye uchafu mno kama hapa? Unatuchukia na kutukirihi sisi wanadamu wachafu; Unachukia upinzani wetu na uasi wetu, hivyo kwa nini Unaishi nasi? Wewe ni Mungu mkuu. Ungeweza kuzaliwa mahali popote, kwa hivyo mbona ilibidi uzaliwe katika nchi hii chafu? Unatuadibu na kutuhukumu kila siku na Unajua wazi kwamba sisi ni uzao wa Moabu, basi kwa nini bado Unaishi kati yetu? Kwa nini Ulizaliwa katika familia ya uzao wa Moabu? Kwa nini Ulifanya hivyo?” Aina hii ya ufahamu wenu inakosa mantiki! Ni aina hii ya kazi tu ambayo inawaruhusu watu kuuona ukuu Wake, unyenyekevu na kujificha Kwake. Yuko tayari kutoa kila kitu kwa ajili ya kazi Yake, na Amevumilia mateso yote kwa ajili ya kazi Yake. Anafanya kwa ajili ya wanadamu, na hata zaidi kumshinda Shetani ili viumbe vyote viweze kutii chini ya utawala Wake. Hii tu ni kazi ya maana, yenye thamani. Kama uzao wa Yakobo ungezaliwa nchini China, katika kipande hiki cha ardhi, na wote walikuwa ninyi nyote, basi umuhimu wa kazi iliyofanyika kwenu ingekuwa nini? Shetani angesema nini? Shetani angesema: “Walikuwa wakikuogopa Wewe, walikutii tangu mwanzo, na hawana historia ya kukusaliti. Wao sio waovu kabisa, wa hali ya chini kabisa, au walio nyuma zaidi kimaendeleo kati ya wanadamu.” Ikiwa inafanyika hivi kwa kweli, nani atakayeridhishwa na kazi hii? Kati ya ulimwengu wote, watu wa Kichina ni watu walio nyuma zaidi kimaendeleo. Wamezaliwa na hali ya chini na uadilifu duni, ni wapumbavu na wenye ganzi, nao ni watovu wa adabu na waliofifia. Wameloweshwa na tabia za kishetani, wachafu na waasherati. Mnayo haya yote. Kwa mintarafu ya tabia hizi potovu, baada ya kazi hii kukamilika watu watazitupilia mbali na wataweza kutii kikamilifu na kufanywa kuwa kamili. Tunda tu kutoka kwa aina hii ya kazi ndilo huitwa ushuhuda kati ya viumbe! Je, unaelewa kile kinachoitwa ushuhuda? Je, ushuhuda unapaswa kutolewaje? Aina hii ya kazi imewafanya kuwa foili pamoja na vyombo vya huduma, na hata zaidi, mmekuwa vyombo vya wokovu. Leo ninyi ni watu wa Mungu na baadaye mtakuwa mifano na vielelezo. Katika kazi hii, mnajitwisha majukumu mbalimbali, na hatimaye mtakuwa vyombo vya wokovu. Watu wengi ni hasi kwa sababu ya hili; Je, si wao ni vipofu kabisa? Huwezi kuona chochote waziwazi! Je, cheo hiki tu kinakuzidi? Je, unaelewa kile kinachotajwa kama tabia ya Mungu yenye haki? Je, unaelewa wokovu wa Mungu ni nini? Je, unaelewa upendo wa Mungu ni nini? Huna uaminifu! Unapotajwa vizuri, unafurahi. Unapotajwa vibaya, hutaki kurudi nyuma. Wewe ni nini? Hufuati njia ya kweli! Afadhali uache kutafuta mara moja. Ni jambo la aibu! Jambo dogo sana linakuzidi. Je, si hii ni ishara ya aibu?

Afadhali uweze kujijua kiasi. Usijione kuwa mkuu sana, wala usiwazie kwenda mbinguni. Tafuta tu kushindwa hapa duniani kwa kufanya wajibu ipasavyo. Usifikiri kuhusu ndoto hizo zisizo halisi ambazo hazipo! Mtu akisema mambo kama yafuatayo, haya ni maneno kutoka kwa mtu mwenye hamu ya kupata kitu, mwenye ujasiri: “Ingawa mimi ni wa uzao wa Moabu, niko tayari kujitahidi kumpata Mungu, na katika siku zijazo nitamkana babu yangu wa zamani! Alinizaa na pia alinikandamiza, na hadi sasa nimekuwa nikiishi tu katika giza. Leo Mungu ameniachilia na hatimaye nimeiona mbingu. Kupitia kwa ufunuo wa Mungu hatimaye nimeona kwamba mimi ni wa uzao wa Moabu. Awali nilikuwa gizani, na sikujua kwamba Mungu amefanya kazi nyingi sana; yote ni kwa sababu nimepofushwa na Shetani huyu wa zamani. Nitamkana na kumuaibisha kabisa!” Kwa hivyo, mna azma kama hiyo? Licha ya ukweli kwamba nyote mna mfano wa mwanadamu, mnashindwa kustahimili kasi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, nanyi ni wepesi zaidi wa kuathirika kuhusiana na suala hili. Mara tu inapotajwa kwamba ninyi ni uzao wa Moabu, midomo yenu inapinda kwa kuibibidua. Je! Si hii ni tabia ya nguruwe? Haina maana. Mko tayari kutoa dhabihu maisha yenu kwa ajili ya umaarufu na bahati yenu! Huko tayari kuwa uzao wa Moabu, lakini sivyo ulivyo? Ninasema leo kwamba wewe uko hivyo, na lazima ukiri jambo hilo. Siendi kinyume na ukweli. Watu wengine ni hasi kwa sababu ya jambo hili, lakini wewe ni hasi kuhusu nini? Je, si wewe pia ndiye mtoto wa joka kubwa jekundu? Je, ni udhalimu kusema kwamba wewe ni uzao wa Moabu? Angalia kile unachoishi kwa kudhihirisha, ndani na nje. Kutoka kichwani hadi mguuni, hakuna kitu cha kujisifia. Uasherati, uchafu, upofu, upinzani, uasi—si haya yote ni sehemu ya tabia yako? Daima wewe huishi ndani ya nchi ya uasherati nawe hufanya uovu wote. Unadhani kuwa wewe ni mtakatifu wa ajabu sana, lakini hebu yalinganishe mambo ambayo umeyafanya. Unafurahishwa sana na matokeo yako—nini ulicho nacho cha kujisifia? Wewe ni kama mnyama. Huna ubinadamu! Mnaafikiana na wanyama, mnaishi ndani ya uovu, dhana za kiasherati. Je! Mnakosa kiasi gani? Mnakubali kwamba ninyi ni watoto wa joka kubwa jekundu, na mko tayari kufanya huduma, lakini baadaye inaposemekana kuwa wewe ni uzao wa Moabu unakuwa hasi. Je! Si huu ni ukweli? Sawasawa na ulivyozaliwa na mama na baba yako, haijalishi jinsi walivyo wabaya, bado ulizaliwa na wao. Hata ukipata mama wa kambo na kuondoka katika nyumba hiyo, je, si wewe bado ni mtoto wa wazazi wako wa mwanzo? Je! Ukweli huo unaweza kubadilishwa? Je, nimekupachika tu jina la uzao wa Moabu kwa kubahatisha? Watu wengine wanasema: “Je! Si ungenipa tu jina lingine?” Ninasema: “Je, unaonaje Nikikupa jina la foili?” Hawataki kuwa foili pia. Basi unataka kuwa nini? Foili, watendaji huduma—si ninyi mko hivi? Ungechagua nini kingine? Je, si wewe ni mtu aliyezaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu? Haijalishi ni kiasi gani unasema kuwa wewe ni mwana wa Daudi, haikubaliani na ukweli. Je, hili ni jambo ambalo unalichagua wewe mwenyewe? Je, unaweza kuchagua jina lolote zuri unalolipenda kwa ajili yako mwenyewe? Je, ni kweli kuwa watoto wa joka kubwa jekundu waliozungumziwa zamani ni nyinyi. Kuhusu watendaji huduma waliotajwa—je, si wao pia ni nyinyi, watu mliowapotoshwa? Vielelezo vilivyoshindwa, mifano iliyotajwa—si hivi pia ni nyinyi, watu hawa? Njia ya kukamilishwa—si hilo linasemwa kwa ajili yenu? Wale ambao wanaadibiwa na kuhukumiwa ni nyinyi, na si wale wanaokamilishwa baadaye watakuwa baadhi ya wale miongoni mwenu? Je, jina hili lina maana? Ninyi ni wapumbavu sana kiasi kwamba hamuwezi hata kuona kitu hicho kidogo kwa dhahiri? Hujui nani ni uzao wa nani, lakini Niko dhahiri kulihusu. Nawaambieni. Ikiwa unaweza kulitambua leo hivyo ni vizuri. Usijidhalilishe kila wakati. Zaidi unavyokuwa hasi na kurudi nyuma, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba wewe ni uzao wa Shetani. Kuna mtu ambaye, unapomtaka asikilize wimbo wa kidini, anasema: “Je, uzao wa Moabu unaweza kusikiza nyimbo za kidini? Sitasikiliza; Mimi sistahili!” Ukimtaka aimbe, anasema: “Ikiwa uzao wa Moabu unaimba, Je, Mungu yuko radhi kusikiliza? Mungu ananichukia. Nina aibu sana kwenda mbele za Mungu na siwezi kushuhudia Kwake. Sitaimba kabisa, Mungu asije akakasirika Anapousikia.” Je! Si hii ni njia hasi ya kulishughulikia? Kama mmoja wa viumbe, ulizaliwa katika nchi ya uasherati na wewe ni mtoto wa joka kubwa jekundu, uzao wa Moabu; unapaswa kumkana babu yako wa zamani na kumkana Shetani wa zamani. Huyu tu ndiye mtu anayemtaka Mungu kwa kweli.

Mwanzoni nilipowapa nafasi ya watu wa Mungu mlikuwa mnaruka juu chini—mliruka kwa furaha zaidi kuliko mtu yeyote. Lakini ilikuwaje mara Niliposema kuwa ninyi ni uzao wa Moabu? Ninyi nyote mlishindwa kustahimili! Ungesema kimo chenu kipo wapi? Dhana yenu ya nafasi ni nzito sana! Wengi hawawezi kujiinua. Wengine huenda kufanya biashara, na wengine huenda kazini. Mara tu Ninaposema kwamba ninyi ni uzao wa Moabu nyote mnataka kukimbia. Je, huku ndiko kushuhudia kwa Mungu ambako huwa mnapigia kelele wakati wote? Je! Shetani ataridhishwa kwa njia hii? Si hii ni alama ya aibu? Ni faida gani kuwa na nyinyi? Ninyi nyote ni taka! Ni mateso ya namna gani ambayo mmestahimili, lakini mnahisi kuwa mmetendewa mabaya sana? Mnafikiri kwamba mara tu Mungu amewatesa hadi kiwango fulani Atafurahi, kana kwamba Mungu alikuja kuwahukumu kimakusudi, na baada ya kuwahukumu na kuwaangamiza, kazi Yake itakuwa imekamilika. Je, ni hivyo ndivyo Nimesema? Je, si hii ni kwa sababu ya upofu wenu? Je! Ni kwamba ninyi wenyewe hamjitahidi kufanya vizuri au kwamba Ninawahukumu kwa makusudi? Sijawahi kufanya hivyo—hilo ni jambo ambalo mlilifikiria wenyewe. Sijafanya kazi kwa njia hiyo kabisa, wala Sina nia hiyo. Kama Ningetaka kuwaangamiza kwa kweli, je, Ningehitaji kuteseka sana hivyo? Ningetaka kuwaangamiza kwa kweli, Ningehitaji kuzungumza nanyi kwa dhati? Mapenzi Yangu ni haya: wakati ambapo Nimewaokoa ndipo Nitakapoweza kupumzika. Zaidi mtu alivyo wa hali ya chini, ndivyo alivyo chombo cha wokovu wangu zaidi. Zaidi mwezavyo kuingia kiutendaji, ndivyo Nitakavyofurahia zaidi. Zaidi mnavyoshindwa kustahimili ndivyo Ninavyofadhaika zaidi. Daima mnataka kuingia kwa mwendo wa furaha kuelekea kiti cha enzi, lakini Nitawaambieni, hiyo sio njia ya kuwaokoa kutokana na uchafu. Njozi ya kukaa kwa kiti cha enzi haiwezi kukufanya kuwa mkamilifu; hiyo si kweli. Nasema kuwa wewe ni uzao wa Moabu, kisha unakuwa na huzuni. Unasema: “Ikiwa utanifanya niende kuzimu, sitakuwa na ushuhuda Kwako au kuteswa kwa ajili Yako.” Je, si kufanya kwako hivi ni kunipinga Mimi? Je, hili ni la manufaa kwako? Nimekupa neema nyingi sana—umesahau? Umeudharau na kuufedhehesha moyo wa Mungu, ambao ni kama tu wa mama mwenye upendo; matokeo yatakuwa yapi kwako? Sitakulazimisha iwapo hunishuhudii—lakini unapaswa kujua kwamba utaangamizwa mwishowe. Ikiwa Siwezi kupata ushuhuda ndani yako, Nitaupata kwa watu wengine. Hilo halina maana Kwangu, lakini mwishowe utalijutia, na wakati huo utakuwa umeanguka gizani muda mrefu uliopita. Basi nani atakayeweza kukuokoa? Usifikiri kwamba kazi haiwezi kufanyika bila wewe. Hakungekuwa na wengi sana pamoja na wewe, na hakungekuwa na wachache sana bila wewe. Usijione kuwa mheshimiwa sana. Ikiwa hutaki kunifuata, hiyo inaonyesha tu kwamba wewe ni muasi, na hakuna kitu cha kutamanisha ndani yako. Ikiwa wewe ni msemaji mzuri, si hivyo ni kwa sababu tu umejiandaa na maneno Niliyoyaleta kupitia kwa kazi Yangu? Nini ulicho nacho cha kujisifia? Usiruhusu mawazo yako yafikie hitimisho lisilo la msingi! Ikiwa Siwezi kupata utukufu kutoka kwenu, uzao huu wa Moabu, Nitachagua kikundi cha pili, na cha tatu cha uzao wa Moabu kufanya kazi mpaka Nipate utukufu. Ikiwa huko radhi kuwa na ushuhuda Wangu, basi toka nje! Sitakulazimisha! Usifikiri kwamba Nitashindwa kusonga hatua bila ninyi. Kupata vyombo vinavyofaa kwa kazi Yangu katika nchi hii ya China hakuhitaji jitihada. Hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kupatikana katika nchi hii—watu wachafu, wapotovu bila shaka wako kila mahali na kazi Yangu inaweza kufanyika popote. Usiwe na kiburi sana! Bila kujali wewe ni mwenye kiburi vipi, je, si bado wewe ni mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi? Angalia thamani yako, na ni chaguo gani lingine ulilo nalo? Kukukubali tu kuishi ni kuinuliwa kukubwa, kwa hivyo ni nini unajivunia? Kama haingekuwa kwa ajili ya kazi Yangu kukomesha enzi, je, si ungekuwa umeanguka katika majanga ya kawaida na maafa ya kibinadamu zamani sana? Je! Unaweza bado kuishi kwa raha sana? Bado daima unabishana kuhusu suala hili. Tangu Niliposema kwamba wewe ni uzao wa Moabu umekuwa ukibibidua midomo wakati wote. Hufanyi uchunguzi, husomi maneno ya Mungu, na kamwe huwezi kustahimili kuona hili au mtu yule. Unapowaona watu wengine wakielimishwa, unawavuruga na kusema mambo ya kuvunja moyo. Una ujasiri! Unasema: “Uzao wa Moabu una elimu gani? Sitajisumbua.” Je, si hili ni jambo ambalo mnyama angesema? Je, hata unafikiriwa kuwa mwanadamu? Nimesema mambo mengi kwako, lakini haijafanikisha chochote. Je, Nimefanya kazi hii yote bure? Je, Nimesema maneno haya yote bure? Hata mbwa anaweza kutikisa mkia wake; mtu kama huyu hata si mzuri kama mbwa! Je, unastahili kuitwa mwanadamu? Ninaponena kuhusu uzao wa Moabu, watu wengine hujishusha hadhi kimakusudi. Wanavaa tofauti kuliko hapo awali nao ni wachafu sana kisai kwamba hawaonekani kama watu, nao hunung’unika: “Mimi ni uzao wa Moabu. Sifai kitu. Ni njozi kufikiria kuhusu kupata baraka zozote. Je, uzao wa Moabu unaweza kufanywa kuwa mkamilifu?” Mara tu Ninaponena kuhusu uzao wa Moabu, watu wengi hawana matumaini tena, na kusema: “Mungu anasema kwamba sisi ni uzao wa Moabu—hii inaonyesha nini? Angalia sauti Anayotumia—haibadiliki! Hakuna upendo katika maneno Yake. Je! Si sisi ni malengo ya maangamizo?” Je! Umesahau kile kilichosemwa hapo awali? Leo neno “uzao wa Moabu” ni jambo pekee ambalo umekumbuka? Kwa kweli, maneno mengi ni kwa ajili ya kufikia kitu, lakini pia yanafichua ukweli wa mambo. Watu wengi hawaliamini. Huko tayari kuteseka kwa njia hiyo kwa ajili Yangu. Unaogopa kifo na daima unataka kutoroka. Ikiwa unataka kwenda Sitakulazimisha kukaa, lakini ni lazima Nikweleze wazi jambo moja: Usiishi maisha yote bure, na usisahau mambo yote Nilivyokwambia zamani. Kama mmoja wa viumbe unapaswa kutekeleza wajibu wa mmoja wa viumbe. Usifanye mambo dhidi ya dhamiri yako; unachopaswa kufanya ni kujitolea kwa Bwana wa uumbaji. Uzao wa Moabu pia ni viumbe walioumbwa, ni jinsi tu wao ni foili[a] na wamelaaniwa. Chochote kitokeacho, bado wewe ni mmoja wa viumbe. Hujakosea sana ukisema hili: “Ingawa mimi ni uzao wa Moabu, nimefurahia neema nyingi ya Mungu mbeleni, hivyo ni lazima niwe na dhamiri. Nitakiri tu lakini sitafikiri sana kulihusu. Hata kama nitateseka ndani ya mkondo huu, nitateseka mpaka mwisho. Kama mimi ni wa uzao wa Moabu basi iwe hivyo. Bado nitafuata hadi mwisho!” Lazima ufuate mpaka mwisho. Ukikimbia kwa kweli huna matumaini ya baadaye—umeingia kwenye barabara ya maangamizo.

Ni vizuri kuwafanya muelewe asili yenu, na kuwafanya muuelewe ukweli wa mambo ni wenye manufaa kwa kazi. Vinginevyo, matokeo ambayo yanapaswa kufanikishwa hayatafanikishwa. Hii ni sehemu ya kazi ya kushinda, na ni hatua muhimu katika kazi. Huo ni ukweli. Kufanya kazi hii ni kuziamsha roho za watu, kuamsha hisia za dhamiri zao na kuwaruhusu watu kupata wokovu huu mkubwa. Ikiwa mtu ana dhamiri, anapaswa kumshukuru Mungu hata zaidi anapoona kwamba yeye ni wa hadhi. Anapaswa kuyashikilia maneno Yake mikononi mwake, ashikilie kwa nguvu neema ambayo Amempa, na hata alie kwa uchungu na kusema: “Nafasi yetu ni ya chini sana na hatujapata chochote duniani. Hakuna mtu kutuheshimu, watu hawa wa hali ya chini. Tunateswa katika mazingira yetu ya nyumbani, waume zetu hutukana, wake zetu hutushutumu, watoto wetu hutudharau, na tunapokuwa wazee, binti zetu wakwe pia hututesa. Hakika hatujateseka kidogo, na kwamba sasa tunafurahia upendo mkuu wa Mungu ni furaha sana! Kama haungekuwa wokovu wa Mungu kwetu, tungewezaje kung’amua mateso ya kibinadamu vizuri? Je, si bado tungekuwa tunapotoka katika dhambi hii? Je, huku si Mungu kutuinua? Mimi ni mmoja wa watu duni kabisa, na Mungu ameniinua juu sana. Hata kama nitaangamia bado lazima niulipize upendo Wake. Mungu anatuheshimu na Anazungumza nasi, sisi watu duni mno, uso kwa uso nasi. Anauchukua mkono wangu kunifunza. Kwa kinywa Chake, Ananilisha. Anaishi nami na kuteseka nami. Hata anaponiadibu—ninaweza kusema nini? Je, si kuadibiwa pia ni kuinuliwa na Mungu? Nimeadibiwa lakini naweza kuona haki Yake. Lazima niulipize upendo wa Mungu. Siwezi kuasi dhidi ya Mungu tena.” Nafasi ya Mungu na hadhi Yake si sawa na ya watu, lakini mateso Yake ni sawa, na kile Anachokula na kuvaa ni sawa, ni watu wote tu humheshimu—hii ndiyo tofauti pekee. Je, si kila kitu kingine ambacho kinafurahiwa ni sawa? Hivyo, nini kinawapa haki ya kumwomba Mungu awatendee kwa namna fulani? Mungu amevumilia mateso makubwa mno na kufanya kazi kubwa sana, na nyinyi—mlio chini kuliko mchwa, kuliko wadudu—mmepata kuinuliwa pakubwa leo. Ikiwa huwezi kuulipiza upendo wa Mungu, dhamiri yako iko wapi? Watu wengine hunena kutoka mioyoni mwao na kusema: “Kila wakati nikifikiri kuondoka kutoka kwa Mungu macho yangu yanajawa na machozi nami nahisi kuhukumiwa na dhamiri yangu. Mimi ni mwenye kuwiwa kwa Mungu. Siwezi kufanya hivi. Siwezi kuwa namna hiyo Kwake. Ningekufa na kufa kwangu kuipe kazi Yake utukufu, nitaridhika kupita kiasi. Vinginevyo, hata nikiishi sitahisi amani.” Sikiliza maneno haya—yanaelezea wajibu ambao kiumbe aliyeumbwa anapaswa kutimiza. Ikiwa mtu anakuwa na maono haya ndani yake kila mara, atahisi kuwa dhahiri na starehe ndani yake; atakuwa na uhakika wa mambo haya. Utasema: “Mungu haniumizi na Hanifedheheshi kimakusudi wala Haniaibishi. Ingawa Ananena kwa ukali kwa kiasi fulani na huuchoma moyo, ni kwa ajili yangu mwenyewe. Ingawa Ananena kwa ukali namna hiyo, bado Ananiokoa, na Yeye bado ni mwenye huruma kwa udhaifu wangu. Hanihukumu na ukweli. Naamini kwamba Mungu ni wokovu.” Ikiwa kweli una maono haya, uwezekano wa wewe kutoroka utakuwa mdogo. Dhamira yako haitakuruhusu uende, na shutuma yake itakuambia kwamba hupaswi kumtendea Mungu kwa namna hiyo. Unafikiri kuhusu neema yote uliyoipata, maneno yote ambayo umeyasikia—je, unaweza kuyasikiliza bure? Haijalishi ni nani anakimbia, wewe huwezi. Watu wengine hawaamini, lakini lazima wewe uamini. Watu wengine wanamtelekeza Mungu, lakini lazima wewe umtetee Mungu na kushuhudia Kwake. Wengine humkashifu Mungu, lakini wewe huwezi. Haijalishi jinsi Mungu asivyo na huruma kwako, bado unapaswa kumtendea vyema. Unapaswa kuulipiza upendo Wake na lazima uwe na dhamiri, kwa sababu Mungu hana hatia. Kuja Kwake duniani kutoka mbinguni kufanya kazi miongoni mwa wanadamu kulikuwa aibu kubwa tayari. Yeye ni mtakatifu bila uchafu hata kidogo. Kuja kwenye nchi ya uchafu—ni fedheha kiasi gani ambayo Amevumilia? Kufanya kazi ndani yenu ni kwa ajili yenu. Ikiwa huna dhamiri katika kumtendea Yeye, ingekuwa bora kufa kifo cha mapema!

Hivi sasa, watu wengi wanakosa kipengele hiki cha maono na hawawezi kabisa kuielewa kazi hii na hawajui nini Mungu anataka hasa kukamilisha kupitia kazi hii. Hasa wale waliokanganyika—ni kama wameingia katika matata mengi na kutunduwazwa baada ya zamu chache. Ukifafanua kikamilifu lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu kwao, hawatakanganyikiwa. Watu wengi hawawezi kulielewa, na wanaamini kwamba kazi ya Mungu ni kuwatesa watu. Hawaelewi hekima na maajabu ya kazi Yake, na hawaelewi kwamba kazi Yake ni kufichua nguvu Yake kuu, na hata zaidi ni kuwaokoa wanadamu. Hawaoni yote hayo, wao huona tu kama wana matumaini yoyote, na kama wataweza kuingia mbinguni. Wanasema: “Kazi ya Mungu daima ni ya mzunguko; kama ungetufanya tu tuione hekima Yako moja kwa moja hiyo ingekuwa vizuri. Hupaswi kututesa kwa njia hii. Tunakosa sana katika ubora wa tabia na hatuyafahamu mapenzi Yako. Ingekuwa vizuri sana kama Ungenena na kutenda tu moja kwa moja. Unatufanya tukisie, lakini hatuwezi. Ingekuwa vizuri kama Ungeharakisha na kuturuhusu tuuone utukufu Wako. Nini haja ya kufanya mambo kwa njia ya mzunguko?” Kile mnachokosa sana sasa ni dhamiri. Zingatieni hili zaidi na fungueni macho yenu wazi kabisa ili muone nani hasa anayefanya hatua kwa hatua kwa kazi. Msifikie uamuzi upesi bila kutafakari. Sasa umeelewa zaidi kwa juujuu njia ya maisha unayopaswa kupitia. Bado kuna kiasi kikubwa cha ukweli ambacho unapaswa kupitia, na siku inapokuja ambapo unaweza kuuelewa kikamilifu, hutasema hivyo tena, wala hutalalamika. Wala hutaufafanua bila uzito. Utasema: “Mungu ni mwenye busara sana, mtakatifu sana. Yeye ni mwenye nguvu sana!”

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Kuboresha Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Inayofuata: Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp