Sura ya 42

Sijui kama watu wameona mabadiliko yoyote katika tamko la leo. Huenda watu wengine wameona kidogo, lakini hawathubutu kusema kwa kweli. Labda wengine hawajatambua chochote. Mbona kuna tofauti kubwa sana hivyo kati ya siku ya kumi na mbili na ya kumi na tano ya mwezi? Umetafakari hili? Maoni yako ni gani? Umeelewa chochote kutokana na matamko yote ya Mungu? Ni kazi gani kuu iliyofanywa kati ya tarehe mbili Aprili na tarehe kumi na tano Mei? Mbona, leo, watu wanaonekana hawana habari, wamekanganywa kama kwamba walikuwa wamegongwa na rungu kichwani? Leo, mbona hakuna safu zinazoitwa “Kashfa za Watu wa Ufalme”? Tarehe mbili na tarehe nne za Aprili, Mungu hakuonyesha hali ya mwanadamu; vilevile, katika siku kadhaa baada ya leo Hakuonyesha hali ya watu—mbona hivyo? Kwa hakika kuna fumbo kuhusu hili—kwa nini kulikuwa na mgeuko kabisa? Hebu kwanza tuzungumze kidogo kuhusu kwa nini Mungu alinena hivyo. Hebu tuyaangalie maneno ya Mungu ya kwanza, ambayo kwayo Hakupoteza wakati kusema “Punde tu kazi mpya inapoanza.” Sentensi hiyo inakupa fununu ya kwanza kwamba kazi ya Mungu imeingia katika mwanzo mpya, kwamba Ameanza kazi mpya kwa mara nyingine. Hili linaonyesha kwamba kuadibu kunakaribia kumalizika; inaweza kusemwa kwamba kilele cha kuadibu tayari kimeingiwa, na kwa hiyo lazima mtumie wakati wenu vyema ili mpitie vizuri kazi ya enzi ya kuadibu, ili msibaki nyuma na msiachwe. Hii yote ni kazi ya mwanadamu, na inahitaji kwamba mwanadamu afanye kila awezalo kushirikiana. Wakati ambapo kuadibu kumeondolewa kabisa, Mungu anaanza kuanzisha sehemu inayofuata ya kazi Yake, kwani Mungu asema, “… Nimeendelea kutekeleza kazi Yangu miongoni mwa wanadamu…. Wakati huu, moyo Wangu umejaa furaha kuu, kwani Nimepata sehemu ya watu, na kwa hiyo ‘biashara’ Yangu haiko tena katika hali ya kuporomoka, si maneno matupu tena.” Katika nyakati zilizopita, watu waliona mapenzi ya Mungu ya dharura katika maneno Yake—hakuna uwongo ndani ya hili—na leo Mungu anafanya kazi Yake kwa kasi kuu zaidi. Kwa mwanadamu, hili halionekani kulingana kabisa na matakwa ya Mungu—lakini kwa Mungu, kazi Yake tayari imemalizika. Kwa kuwa mawazo ya watu ni magumu sana kueleweka, fikira yao kuhusu mambo mara nyingi huwa yenye utata mno. Kwa kuwa watu wanadai mengi kutoka kwa watu, lakini Mungu hamdai mwanadamu mengi sana, inaonyesha jinsi tofauti kati ya Mungu na mwanadamu ilivyo kuu. Dhana za watu huwekwa wazi katika yote ambayo Mungu hufanya. Sio kwamba Mungu huwadai watu makuu na watu hawawezi kuyafikia, lakini kwamba watu humdai Mungu makuu na Mungu hawezi kuyatimiza. Kwa sababu, baada ya matibabu, kuna athari ya ugonjwa wa awali ndani ya mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani kwa miaka elfu kadhaa, watu daima wamemtaka Mungu atende mambo “makuu” kama hayo, na hawana huruma hata kidogo, wakiogopa sana kwamba Mungu hapendezwi. Hivyo, kwamba watu hawawezi kufanya kazi katika mambo mengi ni njia ambayo wanajisababishia adhabu; wanapitia athari za matendo yao wenyewe, na hayo ni mateso matupu. Kuhusu taabu inayovumiliwa na watu, zaidi ya asilimia 99 inadharauliwa na Mungu. Kusema waziwazi, hakuna mtu ambaye ameteseka kweli kwa ajili ya Mungu. Wote huvumilia athari za matendo yao wenyewe—na hii hatua ya kuadibu, bila shaka, si tofauti, ni mwiba wa kujidunga, ambao anachukua na kujidunga. Kwa kuwa Mungu hajafichua kusudi halisi la kuadibu Kwake, ingawa kuna sehemu ya watu ambao wamelaaniwa, hili haliwakilishi kuadibu. Sehemu ya watu wamebarikiwa, lakini hili halina maana kwamba watabarikiwa katika siku za baadaye. Kwa watu, inaonekana kwamba Mungu ni Mungu asiyetimiza neno Lake. Usijali. Huenda haya yakawa yamepita mipaka, lakini usiwe hasi; Ninachozungumzia kina uhusiano fulani na kuteseka kwa mwanadamu, lakini Nafikiri lazima uunde uhusiano mwema na Mungu. Lazima umpe “zawadi” nyingi zaidi, hilo bila shaka litamfurahisha. Naamini kwamba Mungu huwapenda wanaompa “zawadi.” Unasema nini, maneno haya ni sahihi?

Kufikia sasa, mmeacha kiasi gani cha matarajio yenu? Kazi ya Mungu itamalizika hivi punde—kwa hiyo lazima muwe mmeacha takribani matarajio yenu yote, sivyo? Mnaweza hata hivyo kujichunguza: Mnapenda kila mara kujiamini, mkijiinua na kujitangaza—hii ni nini? Leo, bado Sijui matarajio ya watu ni gani? Kama watu kweli wanaishi wakiwa wamezingirwa na bahari ya mateso, wanapoishi katikati ya utakaso wa taabu, au chini ya tishio la vifaa mbalimbali vya mateso, au wanapoishi wakati wa kukataliwa na watu wote na kutazama angani na kutanafusi kwa uzito, katika mawazo yao nyakati kama hizi wanaweza, labda, kuyaacha matarajio yao. Hii ni kwa sababu watu hutafuta paradiso ya kufikirika katikati ya kutokuwa na matumaini, na hakuna mtu ambaye katika hali za starehe amewahi kuacha ufukuziaji wake wa ndoto nzuri. Hii huenda ikawa ndoto, lakini Ningependa kwamba hili silo jambo lililo ndani ya mioyo ya watu. Je, bado mnataka kunyakuliwa mkiwa hai? Je, bado mnataka kubadilisha umbo lenu katika mwili? Sijui kama mna maoni sawa, lakini kila mara Nimehisi kwamba hii ni ndoto—mawazo kama haya huonekana ya kupita kiasi sana. Watu husema mambo kama haya: Acha matarajio yako, kuwa wa kweli. Unataka watu waachane na mawazo ya kubarikiwa—lakini wewe je? Wewe hukanushi mawazo ya watu ya kubarikiwa na wewe mwenyewe unatafuta baraka? Huwaruhusu wengine kupokea baraka lakini wewe unazifikiria kwa siri—hilo linakufanya kuwa nini? Tapeli? Unapofanya hivyo, dhamiri yako haishutumiwi? Ndani ya moyo wako, huhisi kuwa na deni? Je, wewe si mdanganyifu? Unachimbua maneno yaliyo ndani ya mioyo ya wengine, lakini husemi lolote kuhusu yaliyo moyoni mwako—wewe kweli ni kipande cha takataka kisicho na thamani! Nashangaa mnachofikiria ndani ya mioyo yenu mnapozungumza—hamngeweza kushutumiwa na Roho Mtakatifu? Hili halifadhaishi hadhi yenu? Kweli hamjui kinachowafaa! Inadhihirika kwamba nyinyi nyote ni kama Bw. Nanguo—ninyi ni walaghai. Si ajabu Mungu aliweka “kujitolea” ndani ya “wote wako radhi ‘kujitolea’” katika mabano. Mungu anamfahamu sana mwanadamu, na haijalishi jinsi udanganyifu wa mwanadamu ulivyo wa kijanja—hata asipofichua chochote, uso wake haubadiliki rangi kuwa mwekundu, moyo wake hauendi kasi—macho ya Mungu yanang'aa, kwa hiyo mwanadamu kila mara amekuwa na tatizo kuepuka kuangaza macho kwa Mungu. Ni kana kwamba Mungu ana mwanga wa eksirei na anaweza kuziona sehemu zilizo ndani ya mwili wa mwanadamu, kana kwamba Anaweza kufahamu watu wana aina gani ya damu bila upimaji. Hekima ya Mungu ni kama hiyo, na haiwezi kuigwa na mwanadamu. Kama asemavyo Mungu, “Kwa nini Nimefanya kazi nyingi sana, lakini hakuna thibitisho lake ndani ya watu? Je, kwani Sijatia bidii ya kutosha?” Ushirikiano wa mwanadamu na Mungu una upungufu mno, na inaweza kusemwa kwamba kuna mengi sana yaliyo hasi ndani ya mwanadamu, na watu huwa na matumaini yoyote kwa shida sana, wao huwa nayo kiasi kidogo mara chache tu, lakini yametiwa doa sana. Hili linaonyesha tu watu wanampenda Mungu kiasi gani; ni kana kwamba kuna sehemu mia kwa milioni ya kumpenda Mungu ndani ya mioyo yao, kati ya hiyo asilimia 50 bado imetiwa doa, ndiyo maana Mungu anasema hapati thibitisho lolote ndani ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya kutotii kwa mwanadamu hasa ndio sauti ya matamko ya Mungu ni katili sana na isiyo na huruma. Ingawa Mungu haneni na mwanadamu kuhusu nyakati ambazo zimepita, watu kila mara hutaka kukumbuka ya kale, ili kujionyesha mbele ya Mungu, na wao kila mara hutaka kuzungumza juu ya nyakati ambazo zimepita—lakini Mungu hajawahi kuchukulia jana ya mwanadamu kama leo; badala yake, Yeye huwashughulikia watu wa leo kwa kutumia leo. Huu ni mtazamo wa Mungu, na katika hili, Mungu ameyasema maneno haya kwa dhahiri, ili kuwazuia watu kusema katika siku zijazo kwamba Mungu hafikirii mno, kwani Mungu hafanyi mambo ya kupita kiasi, bali huwaambia watu ukweli, watu wasije wakakosa kuweza kusimama imara—kwani mwanadamu, hata hivyo, ni mnyonge. Baada ya kuyasikia maneno haya, unasemaje kuyahusu: Je, uko radhi kusikia na kutii, na kutoyafikiria zaidi?

Yaliyo hapo juu yako nje ya mada, haijalishi kama yanazungumziwa au la. Natumai hamtakuwa tofauti, kwa sababu Mungu anakuja kufanya kazi hii ya maneno, na Hupenda kuzungumza kuhusu kila kitu chini ya jua. Lakini Natumai bado mtayasoma, na hamtapuuza maneno haya, Sawa? Mngefanya hivyo? Ilisemwa tu kwamba katika maneno ya leo Mungu amefichua habari mpya: Mbinu ambayo kwayo Mungu hufanya kazi iko karibu kubadilika. Kwa hivyo, ingekuwa bora kulenga mada hii motomoto. Inaweza kusemwa kwamba matamko yote ya leo yanatabiri masuala ya siku za baadaye, yanahusu Mungu kufanya mpango kwa ajili ya hatua inayofuata ya kazi Yake. Mungu karibu amemaliza kazi Yake ndani ya watu wa kanisa, baadaye Atatumia ghadhabu kuonekana mbele ya watu wote. Kama asemavyo Mungu, “Nitawafanya watu walio duniani wakubali mambo Yangu, na mbele ya ‘kiti cha hukumu,’ matendo Yangu yatathibitishwa, ili yakubalike miongoni mwa watu walio kote duniani, ambao watasalimu amri.” Je, uliona chochote ndani ya maneno haya? Humu mna muhtasari wa sehemu inayofuata ya kazi ya Mungu. Kwanza, Mungu atawafanya walinzi wote wanaotawala kwa nguvu za kisiasa waridhike kabisa na wajiondoe katika jukwaa la historia, kutowahi kupigania hadhi tena au kufanya hila na kula njama. Kazi hii lazima itekelezwe kwa njia ya Mungu kusababisha mabaa mbalimbali duniani. Lakini Mungu hataonekana; kwa sababu, wakati huu, nchi ya joka kubwa jekundu bado itakuwa ni nchi ya uchafu, Mungu hataonekana, lakini ataibuka tu kwa njia ya kuadibu. Hiyo ndiyo tabia ya Mungu yenye haki, na hakuna anayeweza kuiepuka. Katika wakati huu, vyote vinavyoishi katika taifa la joka kubwa jekundu vitapitia maafa, ambavyo kwa kawaida ni pamoja na ufalme ulio duniani (kanisa). Huu ndio hasa wakati ambao ukweli hujitokeza, na kwa hiyo unapitiwa na watu wote, na hakuna anayeweza kuepuka. Hili limejaaliwa na Mungu. Ni kwa sababu ya hatua hii ya kazi hasa ndio Mungu asema, “Huu ndio wakati wa kutekeleza mipango mikuu.” Kwa sababu, katika siku za baadaye, hakutakuwa na kanisa duniani, na kwa ajili ya majilio ya machafuko, watu wataweza tu kufikiria kuhusu kile kilicho mbele yao na watapuuza kila kitu kingine, na ni vigumu kwao kumfurahia Mungu katikati ya machafuko, hivyo, watu wanatakiwa kumpenda Mungu kwa moyo wao wote katika wakati huu wa ajabu, ili wasikose nafasi. Ukweli huu unapopita, Mungu amelishinda kabisa joka kubwa jekundu, na hivyo kazi ya ushuhuda wa watu wa Mungu imefika mwisho; baadaye Mungu ataanza hatua inayofuata ya kazi, Akifanya uharibifu kwa nchi ya joka kubwa jekundu, na hatimaye kuwagongomelea watu juu chini msalabani kotekote katika ulimwengu, baadaye Atawaangamiza wanadamu wote—hizi ni hatua za siku za baadaye za kazi ya Mungu. Hivyo, mnapaswa kutaka kufanya lote muwezalo kumpenda Mungu katika mazingira haya ya amani. Katika siku za baadaye hamtakuwa na nafasi zaidi za kumpenda Mungu, kwani watu huwa tu na nafasi ya kumpenda Mungu katika mwili; wanapoishi katika ulimwengu mwingine, hakuna atakayenena kuhusu kumpenda Mungu. Je, hili si jukumu la kiumbe aliyeumbwa? Kwa hiyo unapaswa kumpenda Mungu vipi katika siku zako za uhai? Umeshawahi kufikiri juu ya hili? Je, unangoja mpaka ufe ili umpende Mungu? Je, haya si maneno matupu? Leo, kwa nini hufuatilii kumpenda Mungu? Je, kumpenda Mungu huku ukiwa na shughuli nyingi kunaweza kuwa upendo halisi wa Mungu? Madhumuni ya kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu itafika mwisho hivi punde ni kwa sababu Mungu tayari ana ushuhuda mbele ya Shetani; hivyo, hakuna haja ya mwanadamu kufanya lolote, mwanadamu anatakiwa tu kufuatilia kumpenda Mungu katika miaka ambayo yuko hai—hili ndilo jambo muhimu. Kwa sababu masharti ya Mungu si mengi, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa kuna hamu kuu ndani ya moyo Wake, Amefichua muhtasari wa hatua inayofuata ya kazi kabla ya hatua hii ya kazi kumalizika, ambalo linaonyesha kwa dhahiri kuna kiasi gani cha muda: kama Mungu hangekuwa na hamu ndani ya moyo Wake, je, Angeyanena maneno haya mapema hivyo? Ni kwa sababu muda ni mfupi ndio maana Mungu anafanya kazi kwa njia hii. Inatarajiwa kwamba mnaweza kumpenda Mungu kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote, na kwa nguvu zenu zote, jinsi tu mnavyotunza maisha yenu wenyewe. Je, haya siyo maisha yenye maana kuu zaidi? Ni wapi pengine ambapo mngeweza kupata maana ya maisha? Je, ninyi si vipofu kabisa? Uko radhi kumpenda Mungu? Je, Mungu anastahili upendo wa mwanadamu? Je, watu wanastahili ibada ya mwanadamu? Kwa hiyo, unapaswa kufanya nini? Mpende Mungu kwa ujasiri, bila kusita, na uone kila ambacho Mungu atakufanya. Uone kama Atakuchinja. Kwa muhtasari, kazi ya kumpenda Mungu ni muhimu zaidi kuliko kunukuu na kuandika mambo kwa ajili ya Mungu. Unapaswa kukipa kipaumbele kilicho muhimu zaidi, ili maisha yako yaweze kuwa ya thamani zaidi na yajae furaha, na kisha unapaswa kusubiri “hukumu” ya Mungu kwako. Nashangaa iwapo mpango wako utahusisha kumpenda—Ningependa kwamba mipango ya watu wote iwe ile inayokamilishwa na Mungu, na iwe ya uhalisi.

Iliyotangulia: Sura ya 41

Inayofuata: Sura ya 44 na 45

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp