Sura ya 41

Mungu humfinyanga mwanadamu vipi? Je, unalifahamu hili? Linaeleweka? Nalo hufanyika vipi kanisani? Unafikiriaje? Je, umewahi kuyafikiria maswali haya? Ni nini ambalo Anatarajia kufanikisha kupitia kwa kazi Yake kanisani? Je, yote yanaeleweka bado? Kama sivyo, yote ambayo unafanya hayana maana, yamebatilika! Je, maneno haya yanaugusa moyo wako? Je, yote ambayo yanahitajika kutimiza tamanio la Mungu ni maendeleo ya utendaji tu, na sio kuwa hasi na kurudi nyuma? Je, ushirikiano wa kijinga unatosha? Je, unapaswa kufanya nini kama bado kuna wingu la utata kuhusu maono? Je, ni sawa kutotafuta? Mungu asema, “Wakati mmoja Nilianza shughuli kubwa miongoni mwa wanadamu, lakini hawakutambua, kwa hivyo ilibidi Nitumie neno Langu ili kuwafichulia. Na hata hivyo, bado mwanadamu hangeweza kuyaelewa maneno Yangu, na akasalia kutojua malengo ya mpango Wangu.” Hili linamaanisha nini? Je, umewahi kufikiria kusudi lake? Je, Mungu hutenda tu bila sababu na kijinga? Na ikiwa ni hivyo, ya nini? Iwapo kusudi si dhahiri, na iwapo mwanadamu haelewi, basi anawezaje kushirikiana kwa kweli? Mungu asema kwamba ukimbizaji wa watu uko ndani ya bahari zisizo na mipaka, ndani ya maneno matupu na mafundisho ya dini. Ninyi hamwezi hata kusema ukimbizaji wenu upo katika kundi lipi. Ni nini ambacho Mungu anataka kutimiza ndani ya mwanadamu? Unapaswa kuelewa mambo haya yote. Je, ni kwa ajili tu ya kuliaibisha joka kubwa jekundu katika hali hasi? Yawezekana kwamba baada ya kuliaibisha joka kubwa jekundu, Mungu ataishi tu kama mtawa asiye na chochote? Basi ni nini ambacho Mungu anataka? Je, kweli Anaitaka mioyo ya wanadamu? Au maisha yao? Au utajiri na mali yao? Hivi vina maana gani? Havina maana kwa Mungu. Je, Mungu amefanya mengi sana ndani ya mwanadamu ili Aweze tu kuwatumia kama ushahidi wa ushindi Wake juu ya Shetani, na kudhihirisha nguvu Zake? Hili halingemfanya Mungu aonekane mwenye kujishughulisha na mambo finyu? Je, kweli Mungu ni Mungu wa aina hiyo? Kama tu mtoto anayewasababisha watu wazima kugombana? Hili lina umuhimu gani? Mwanadamu daima amemchunguza Mungu kupitia kwa fikira zake mwenyewe. Mungu alisema wakati mmoja, “Mwaka una majira manne, na kwa kila majira kuna miezi mitatu.” Mwanadamu alisikiliza, na akayakumbuka maneno Yake, na akaendelea kusema kwamba kulikuwa na miezi mitatu kwa kila majira na majira manne kwa mwaka. Na kisha, Mungu alipouliza, “Kuna majira mangapi katika mwaka? Na miezi mingapi kwa kila majira?” wanadamu wakajibu kwa maafikiano, “Majira manne, miezi mitatu.” Mwanadamu daima hujaribu kumfafanua Mungu kwa kutegemea sheria fulani. Siku hizi katika enzi ya “majira matatu kwa kila mwaka, miezi minne kwa kila majira,” mwanadamu bado hafahamu, inavyoonekana ni mjinga, inaonekana amekuwa kipofu huku akitafuta sheria katika kila kitu. Na sasa mwanadamu anajaribu kutumia amri zake kwa Mungu! Yeye ni mjinga kweli! Haoni sasa hakuna “majira ya baridi,” bali “majira ya kuchipua, majira ya joto, na majira ya majani kupukutika” pekee? Mwanadamu kweli ni mpumbavu! Katika hali ya sasa, mwanadamu bado hafahamu namna ya kumjua Mungu. Yeye ni kama tu watu wa miaka ya 1920, wanaofikiria kwamba njia za usafirishaji ni sumbufu, kwa hivyo wanatembea, au wanatumia punda, au wanaofikiria wanapaswa kutumia taa za mafuta, au njia zingine za kale za maisha. Je, hizi zote si fikira kutoka kwa akili za wanadamu? Kwa hiyo ya nini hata hivyo kuzungumza juu ya huruma na upendo leo? Hili lina maana gani? Kama bikizee anayeparaganya, akisimulia siku zake zilizopita, haya maneno yana maana gani? Hata hivyo, wakati wa sasa ni wakati wa sasa; je, saa inaweza kurudishwa nyuma kwa miaka 20 au 30? Watu kila mara hufuata mkondo; kwa nini ni vigumu sana wao kulielewa hilo. Katika enzi hii ya sasa ya kuadibu, mazungumzo haya ya huruma na upendo yana maana gani? Kana kwamba yote yanayomhusu Mungu ni huruma na upendo? Ni kwa nini katika enzi hii ya “unga na mchele,” watu wanaendelea kulisha watu makapi ya mtama na mboga za porini?Lile ambalo Mungu hataki kulifanya, kwa lazima, mwanadamu anamkomesha kwa nguvu. Kama Angepinga, Angepachikwa jina la “mpinga mapinduzi,” na ingawa ilisemwa tena na tena kwamba Mungu hakuwa mwenye huruma au mwenye upendo, nani angesikiliza? Mwanadamu ni mpuuzi sana. Inaonekana neno la Mungu halina athari. Kila mara wanadamu huyafikiria maneno Yangu kwa njia tofauti. Kila mara Mungu hudhulumiwa na watu, na inaonekana kwamba watu wasio na hatia wanakabiliwa na shtaka lisilo na msingi; ni nani atatenda kulingana na Mungu? Kila mara ninyi mko tayari kuishi katika huruma na upendo wa Mungu, kwa hiyo ni kipi ambacho Mungu astahili kufanya kando na kustahimili matusi ya mwanadamu? Hata hivyo, Natumai mnaweza kufahamu jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi kabla ya kubishana na Mungu. Hata hivyo, Nawasihi sana mfahamu maana ya asili ya neno la Mungu. Usifikiri kwamba wewe ni mwerevu, na kufikiri kwamba neno la Mungu lina najisi. Hili si lazima! Ni nani anaweza kusema ni kiasi gani cha “najisi” kiko ndani ya neno la Mungu? Isipokuwa Mungu aliseme moja kwa moja, au kulionyesha kwa dhahiri. Usijivune sana. Kama mnaweza kuona njia ya kufanya mazoezi kutokana na maneno Yake, basi ninyi mmetimiza masharti. Mnataka kuona nini kingine? Mungu alisema “Sina huruma yoyote tena kwa udhaifu wa mwanadamu.” Hata maneno haya dhahiri, na rahisi hayawezi kufafanuliwa, kwa hiyo mbona uhangaike bure kufanya utafiti, na kufanya uchunguzi zaidi? Bila hata maarifa ya msingi ya uhandisi, mwanadamu angewezaje kustahili kuunda roketi? Je, huyo si mtu tu anayependa kujisifu? Mwanadamu hastahili kuifanya kazi ya Mungu; ni kwa sababu tu Mungu humkuza. Bila kujua Anachopenda, Anachochukia, na kumhudumia tu. Je, hii si mbinu ya kusababisha msiba? Wanadamu hawajielewi, lakini wanafikiri wao ni wa ajabu. Wanafikiri wao ni nani! Wao ni wajinga kweli kuhusu tofauti kati ya mema na maovu. Kumbuka wakati uliopita, na utazame mbele kwa siku za baadaye. Je, unafikiri nini? Kisha upate kujijua.

Mungu amefichua mengi sana kuhusu nia na kusudi la mwanadamu. Mungu alisema, “Ulikuwa wakati huu ambapo Niliona nia na kusudi la mwanadamu. Nilishusha pumzi kutokana na kushindwa kuelewa: Ni kwa nini siku zote lazima mwanadamu atende kwa ajili ya maslahi yake? Je, kuadibu Kwangu hakukusudii kumkamilisha? Je, Najaribu kumvunja moyo?” Ni nini ambacho unajifunza kujihusu kutokana na maneno haya? Je, nia na kusudi la mwanadamu vimeenda kwa kweli? Umewahi kupeleleza? Ni heri muweze kuja mbele za Mungu ili mjifunze, kazi Yake ya kuadibu hutimiza nini ndani yenu? Je, mmefanya muhtasari wake? Labda kiasi kidogo sana, la sivyo huenda mngejiingiza katika kutia chumvi kitambo. Ni nini ambacho Mungu anawataka mtimize? Kuhusu maneno ambayo mmezungumziwa, ni kiasi gani ambacho mmetia katika vitendo? Ni kiasi gani kilisemwa bure? Machoni pa Mungu, kiasi kidogo cha maneno Yake hutekelezwa kwa kweli; hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kamwe kutambua maana Yake ya asili, naye hukubali tu maneno yoyote yanayorudiwa. Kwa njia hii anaweza kuyajua mawazo ya Mungu? Hivi karibuni, Mungu atakuwa na kazi nyingi kwa ajili ya mwanadamu; je, mwanadamu anaweza kuifanikisha kazi hiyo kwa kimo kidogo alicho nacho mwanadamu sasa? Kama si mwenye kosa, mwanadamu ni mpumbavu, au labda mwenye kiburi, asili za watu ni kama hizi. Halieleweki kwa kweli: Kutokana na yote ambayo Mungu amesema, kwa nini mwanadamu haathiriwi nayo? Yawezekana kwamba neno la Mungu ni mzaha tu, lisilonuiwa kuwa na athari yoyote? Yote kwa ajili ya kumwona mwanadamu akiigiza mchezo wa “Furaha, Hasira, Huzuni, na Shangwe”? Ili kumfanya mwanadamu afurahi kwa wakati mmoja, na alie kwa wakati mwingine, na baadaye akitenda kama aonavyo kuwa bora nje ya jukwaa? Hili lingekuwa na athari gani? “Kwa nini matakwa Yangu kwa mwanadamu kila mara huambulia patupu? Je, ni kana kwamba Nilikuwa Namtaka mbwa apande mti? Je, Najaribu kuleta taabu bila sababu?” Maneno yote ya Mungu hulenga hali halisi ya mwanadamu. Haitakuwa na manufaa yeyote kutazama ndani ya watu wote ili aone ni nani anaishi kulingana na neno la Mungu. “Na bado sasa, sehemu kubwa ya mandhari inaendelea kubadilika. Kama siku moja dunia itabadilika kwa kweli kuwa aina nyingine, Nitaiweka kando bila kusita—je, hiyo si hatua ambayo Niko ndani sasa katika kazi Yangu?” Kwa kweli, Mungu yuko katika mchakato wa kazi hii sasa; hata hivyo, Mungu anapotaja “kuweka kando bila kusita,” hii inahusu siku za baadaye, kwa kuwa kila kitu ni mchakato. Je, unaweza kuona kwamba huu ndio mwelekeo katika kazi ya Mungu ya sasa? Kwa ajili ya dosari ya nia ya mwanadamu, pepo wachafu huchukua nafasi ya kujidhihirisha. Wakati huu, “dunia itabadilika kuwa aina nyingine” na watu wakati huo watabadilika kwa ustahilifu, lakini kiini chao kitabaki vilevile. Hii ni kwa sababu kuna kitu kingine katika dunia ya kuendeleza. Kwa maneno mengine, dunia ya asili ilikuwa duni, na mara tu ikishaendelezwa inaweza kutumika. Hata hivyo, baada ya dunia kutumiwa kwa kipindi fulani, na kisha isitumiwe tena, itarudi polepole kwa umbo lake la asili. Huu ni muhtasari wa hatua inayofuata ya kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu ya siku za baadaye itakuwa ngumu zaidi kufahamika, kwa sababu ni wakati wa kuainisha aina mbalimbali za watu. Katika mahali pa mkutano pa mwisho, patakuwa machafuko ya fujo, na mwanadamu hatakuwa na maoni yenye msimamo. Kama tu alivyosema Mungu: “Wanadamu wote ni wachezaji wanaokubaliana na kundi.” Jinsi wanadamu walivyo na uwezo wa kucheza ili kukubaliana na kundi, Mungu hutumia dosari hii kwa ajili ya hatua inayofuata katika kazi Yake, ili aweze kuwafanya wanadamu wote wageuze kasoro hii. Ni kwa sababu hawana kimo halisi kuwa wanadamu ni kama panzi juu ya ukuta. Wangekuwa nacho, wangekuwa miti yenye uwezo mkuu. Mungu anakusudia kutumia sehemu ya kazi ya pepo wachafu ili kuikamilisha sehemu ya mwanadamu, ili watu hawa waweze kufahamu matendo ya mapepo, na kuwawezesha watu wote wawafahamu kwa kweli mababu zao. Ni kwa njia hii pekee wanadamu wanaweza kujinasua kabisa, sio tu kutoroka kizazi cha mapepo, lakini hata zaidi mababu wao. Hili ndilo kusudi la asili la Mungu kulishinda kabisa joka kubwa jekundu, kufanya hivyo ili wanadamu wote wajue umbo halisi la joka kubwa jekundu, Aambue kinyago chake kabisa, na kuona umbo lake halisi. Hili ndilo Mungu anataka kutimiza, nalo ni lengo Lake la mwisho duniani ambalo Amefanyia kazi nyingi sana; Ananuia kulifanikisha hili ndani ya watu wote. Hili linajulikana kama ushawishi wa vitu vyote kwa ajili ya kusudi la Mungu.

Je, mnaelewa jinsi kazi ya siku za usoni itafanywa? Haya yote lazima yaeleweke. Kwa mfano: Kwa nini Mungu asema kwamba wanadamu kamwe hawashughulikii wajibu wao? Kwa nini Anasema kwamba watu wengi wamekosa kukamilisha zoezi ambalo Amewaachia? Vitu hivi vinaweza kutimizwa vipi? Je, umewahi kuyafikiria maswali haya? Haya yamekuwa mada ya mawasiliano yako? Kwa ajili ya hatua hii ya kazi, mwanadamu lazima aelewe makusudi ya Mungu ya sasa. Mara tu hilo likishatimizwa, mengine yanaweza kujadiliwa, ni sawa? Kile ambacho Mungu anatarajia kutimiza ndani ya mwanadamu kinahitaji kuelezwa kabisa, la sivyo haina faida. Hawataweza kuingia ndani yake, na hata huenda isiwezekane kwa wao kulitimiza; ni ya kinadharia tu. Je, mmepata njia ya kufanya mazoezi ya kile ambacho Mungu amesema hivi sasa? Watu hulizingatia neno la Mungu kwa hisia ya woga. Hawawezi kulifahamu, na wanaogopa kumkosea Mungu. Wamepata njia ngapi za kula na kunywa ambazo zimetajwa sasa? Wengi hawajui namna ya kula na kunywa; hili linaweza kutatuliwa vipi? Je, mlipata njia ya kufanya hivyo katika tamko la leo? Ulijaribu kushirikiana kwa njia gani? Na nyote mkishayasikia maneno, huwa mnajadiliana fikira zenu kwa njia gani? Je, mwanadamu hapaswi kufanya hili? Ni jinsi gani unapaswa kuagiza matumizi ya dawa sahihi? Bado unahitaji sauti ya wazi ya Mungu? Je, hili linahitajika? Matatizo haya yanawezaje kukomeshwa kabisa? Hii inategemea iwapo unaweza kushirikiana na Roho Mtakatifu katika matendo na ushirikiano ufaao. Kama kuna ushirikiano wa kufaa, Roho Mtakatifu atafanya kazi kuu. Ikiwa hakuna ushirikiano wa kufaa bali kwa usahihi zaidi ni rabsha, Roho Mtakatifu hatakuwa na uwezo wa kusaidia. “Kama unamjua adui yako na kujijua, utaibuka mshindi kila mara.” Bila kujali yule aliyanena maneno haya kwanza, ni ya kukufaa wewe zaidi. Kwa ufupi, lazima kwanza mjijue kabla ya kuweza kuwajua maadui zenu, na hatimaye mtaweza kushinda kila vita. Lazima nyote muweze kufanya hili. Haijalishi kile ambacho Mungu anataka kutoka kwako, unahitaji tu kujitolea kikamilifu. Natarajia utaweza kuonyesha uaminifu wako kwa Mungu mbele Yake mwishowe, na maadamu unaweza kuiona tabasamu ya Mungu ya kupendeza Akiwa katika kiti Chake cha enzi, hata kama ni wakati wako kufa, lazima uweze kucheka na kutabasamu macho yako yanapofumba. Lazima umfanyie Mungu wajibu wako wa mwisho wakati wa muda wako hapa duniani. Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu. Kiumbe anaweza kumfanyia Mungu nini? Kwa hiyo unapaswa kujitolea kwa rehema ya Mungu mapema iwezekanavyo. Maadamu Mungu anafurahia na Anapendezwa, basi mwache Afanye chochote Atakacho. Wanadamu wana haki gani ya kulalamika?

Iliyotangulia: Sura ya 40

Inayofuata: Sura ya 42

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp