Sura ya 39

Hebu twende nje ya maneno ya Mungu na tuzungumze kidogo juu ya masuala yanayohusu maisha yetu, ili maisha yetu yasitawi, na tufikie matumaini ya Mungu kwetu. Hasa, pamoja na ujaji wa leo—wakati wa kila mmoja kuainishwa kulingana na aina, na wa kuadibu—kuna haja kubwa ya kuyalenga mambo muhimu na kumakinikia “maslahi ya pamoja.” Haya ni mapenzi ya Mungu, na kile kinachopaswa kutimizwa na watu wote. Tungewezaje kukosa kujitolea kwa ajili ya mapenzi ya Mungu mbinguni? Mungu “hutoa idadi kwa kila aina ya watu na Huweka alama tofauti kwa kila aina ya mtu, ili babu zao waweze kuwaongoza kurudi kwa jamii zao,” ambalo linaonyesha kuwa watu wameainishwa kulingana na aina, na kutokana na hilo, kila aina za watu wanafichua umbo lao halisi. Kwa hivyo, ni haki kusema kuwa watu ni waaminifu kwa babu zao, sio kwa Mungu. Hata hivyo, watu wote pia wanatoa huduma kwa Mungu kwa uongozi wa babu zao, ambao ni ajabu ya kazi ya Mungu. Vitu vyote vinamhudumia Mungu, na hata kama Shetani anawasumbua watu, Mungu hutumia fursa hii kutumia “rasilimali za mahali hapo” kumhudumia. Watu, hata hivyo, hawawezi kutambua hili. Kama Mungu Anavyosema, “hivyo, Nagawa kazi pia, na kusambaza juhudi. Hii ni sehemu ya mpango Wangu, na hauwezi kuvurugwa na mtu yeyote.” Watu hawawezi kuona yote yanayodhamiriwa na Mungu, na yote ambayo Mungu anataka kufanikisha, kabla ya Yeye kuyafanya. Wanaweza kuyaona tu wakati ambapo kazi ya Mungu imekamilika; kama sivyo, wao ni vipofu, na hawaoni chochote.

Leo, Mungu ana kazi mpya miongoni mwa makanisa. Yeye Hufanya kila kitu kifuate hali ya asili ya maisha, kwa kweli kutumia kazi ya mwanadamu. Kama Mungu anavyosema, “Natawala kila kitu miongoni mwa vitu vyote, Naamuru kila kitu miongoni mwa vitu vyote, Nikisababisha vyote vilivyoko kufuata hali halisi ya maisha na kutii amri ya asili.” Sijui ni utambuzi mahiri gani mlio nao katika “kufuata hali ya asili ya maisha,” basi hebu tuzungumze kuhusu hili. Hivi ndivyo Ninavyoliona: Kwa sababu wanaongozwa kwenda nyumbani na babu zao, watu wa aina zote wanapaswa kutokea na “kutekeleza.” Na kwa sababu wanafuata hali ya asili ya maisha, kile ambacho ni cha asili kwao kinatumika kutumia kazi yao ya asili, kikiwafanya kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu kulingana na mwelekeo huu wa kawaida. Kazi ya Roho Mtakatifu hutekelezwa kulingana na hali iliyo ndani ya kila mtu; kusema kweli, hii inaitwa “Mungu hushawishi vitu vyote ili vimhudumie,” hili basi linahusiana na kufuata hali ya asili ya maisha. Ingawa mtu ana vitu vya asili ya shetani ndani yake, Mungu atavitumia hivi, Akiongeza kazi ya Roho Mtakatifu kwa msingi wa kile kilicho ndani yake kwa asili, Akiwafanya kutosha kutoa huduma kwa Mungu. Haya ndiyo yote Nitakayosema kuhusu “kufuata hali ya asili ya maisha”—labda mna mapendekezo mengine makuu zaidi. Natumaini mnaweza kutoa maelezo fulani ya thamani, au vipi? Je, mko tayari kushirikiana katika kufuata hali ya asili ya maisha? Je, mko tayari kugawanya kazi na Mungu? Mmewahi kufikiria kuhusu jinsi ya kulitimiza hili? Natumaini kwamba watu wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu, kuwa wanaweza kuwa wenye mawazo sawa katika kumridhisha Mungu kwa ajili ya maadili ya pamoja, na wanaweza kuendelea pamoja katika njia ya kuelekea kwa ufalme. Kuna haja gani ya kuja na dhana zisizohitajika? Ni kuweko kwa nani kufikia leo hakujakuwa kwa ajili ya Mungu? Na kwa kuwa ni hivyo, kuna haja gani ya huzuni, ghamu, na tanafusi? Hili halina faida kwa mtu yeyote. Maisha yote ya watu yapo mikononi mwa Mungu, na isingekuwa kwa ajili ya azimio lao mbele ya Mungu, ni nani angekuwa radhi kuishi bure katika dunia hii tupu ya mwanadamu? Kwa nini ujisumbue? Kurupuka ndani na nje ya ulimwengu, wasipomfanyia Mungu chochote, je, maisha yao yote hayatakuwa ya bure? Hata kama Mungu hayaoni kwamba matendo yako yanastahili kutajwa, je, hutatoa tabasamu la kuridhika wakati wa kifo chako? Unapaswa kufuatilia maendeleo ya kujenga, sio kurudi nyuma hasi—je, huu sio utendaji bora? Kama matendo yako ni kwa ajili ya kumridhisha Mungu kabisa, basi hutakuwa hasi au wa kurudi nyuma. Kwa sababu daima huwa kuna mambo ambayo hayaeleweki mioyoni mwa watu, bila wao kutambua nyuso zao zimefunikwa na mawingu ya giza, ambalo husababisha kuonekana kwa “mitaro” kadhaa katika nyuso zao bila wao kujua, ambayo inaonekana ni kwa sababu ardhi inaendelea kupasuka. Ni kama kwamba ardhi inaendelea kusonga, ikisababisha “viduta” au “miteremko” juu ya ardhi kusongeza mahali bila watu kutambua. Katika hili, Siwadhihaki watu, bali Nazungumzia “maarifa ya kijiografia.”

Ingawa Mungu amewaongoza watu wote katika kuadibu, Hasemi chochote juu ya hili. Badala yake, Anaepuka mada hii kwa makusudi na kuanza mpya, ambalo katika suala moja ni kwa sababu ya kazi ya Mungu, na katika lingine, ni ili kukamilisha mara moja hatua hii ya kazi. Kwa sababu malengo ya Mungu katika kutekeleza hatua hii ya kazi yalitimizwa kitambo, hakuna haja ya kusema chochote zaidi. Leo, sijui ni kiasi gani mmeona kuhusu mbinu za kazi ya Mungu; katika ufahamu Wangu, siku zote Mimi Huhisi kuwa kazi ya Mungu haijagawanywa kwa dhahiri katika hatua na vipindi vya muda kama ilivyokuwa awali. Badala yake, kila siku huleta njia zake za kufanya kazi, mabadiliko hutokea karibu kila siku tatu hadi tano, na hata katika siku tano, kunaweza kuwa na aina mbili tofauti za maudhui kwa kazi ya Mungu. Hili linaonyesha kasi ya kazi ya Mungu; kabla ya watu kuwa na muda wa kufurahia na kuangalia kwa makini, Mungu ashaenda asionekane tena. Hivyo, Mungu daima Hashikiki kwa watu, ambalo limesababisha kutotambulika kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa nini Mungu daima Husema maneno kama “na kwa hiyo Nilimwacha mwanadamu”? Watu wanaweza kuzingatia kidogo maneno haya, lakini hawaelewi maana yake. Na je, wakati huu, mnaelewa? Si ajabu watu hawana ufahamu wa kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Kutafuta kwao kwa Mungu daima huwa chini ya mwanga wa mwezi usio dhahiri—hili ni kweli kabisa—na ni kama kwamba Mungu anamtania mwanadamu kwa makusudi, Akifanya mabongo ya watu wote kufura, ili wahisi kizunguzungu na kukanganyika. Wao hujua wanachofanya kwa taabu sana, ni kama kwamba wanaota, na mara wanapoamka, hawajui kilichotokea. Kinachohitajika tu ni maneno machache ya kawaida kutoka kwa Mungu kuwafanya watu wasijue la kufanya. Si ajabu, basi, kwamba Mungu asema, “Leo, Nawatupa watu wote katika ‘tanuru kubwa’ ili wasafishwe. Nasimama juu kuangalia kwa makini watu wakichomeka motoni na, kwa kulazimishwa na miale ya moto, watu wanatoa ukweli.” Katikati ya maneno ya Mungu yanayobadilika daima, watu hawajui la kufanya; kwa kweli, kama tu Mungu anavyosema, kuadibu kumeanza kitambo, na kwa sababu watu hawajatambua jambo hili, wanajua tu wakati Mungu anaposema hivyo wazi wazi, wao huwa makini tu baada ya Mungu kuwaambia. Inaweza kusemwa kuwa watu huanza tu kuchunguza kuhusu kuadibu sasa kwa vile kazi ya Mungu imetekelezwa kufikia kiwango hiki. Ni kama tu wakati ambapo watu walitambua bomu la atomiki—lakini kwa sababu wakati haujafika, watu hawatilii maanani; wakati mtu anapoanza tu kulitengeneza ndio watu huanza kuwa makini. Ni wakati ambapo bomu la atomiki linapoonekana tu ndio watu huelewa zaidi kulihusu. Mungu anaposema tu Atamtupa mwanadamu ndani ya tanuru ndio watu hufahamu kidogo. Kama Mungu hangezungumza, hakuna ambaye angejua—je, si sivyo? Kwa hiyo, Mungu asema, “watu wanaingia ndani ya tanuru bila kujua, kama kwamba wameongozwa huko kwa kamba, kama kwamba hawasikii.” Kwa nini usichanganue hili: Wakati watu wanapotoa ukweli, je ni wakati ambapo Mungu anasema kwamba kuadibu kumeanza, au kabla ya wakati ambapo Mungu anasema kwamba kuadibu kumeanza? Kutokana na hili inaweza kuonekana kuwa, kabla ya Mungu kunena juu ya kuadibu, watu walianza kukiri, kuonyesha kwamba kuadibu kulianza kabla ya Mungu kuzungumza juu yake—je, huu si ukweli?

Iliyotangulia: Sura ya 38

Inayofuata: Sura ya 40

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp