Sura ya 40

Kwa Mungu, mwanadamu ni kama mtu anayechezewa katika mshiko Wake, kama nudo inyoshwayo kwa mkono katika mikono Yake—inayoweza kufanywa nyembamba au nzito kama apendavyo Mungu, kuifanyia Apendavyo. Ni haki kusema kwamba mwanadamu kwa kweli ni mtu anayechezewa mikononi mwa Mungu, kama paka wa Uajemi ambaye bibi amemnunua kutoka sokoni. Bila shaka, yeye ni mtu anayechezewa mikononi mwa Mungu—na kwa hiyo hakukuwa na chochote cha uongo kuhusu ufahamu wa Petro. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba maneno na matendo ya Mungu ndani ya mwanadamu hutimizwa kwa wepesi na raha, bila kuhangaika. Yeye hapigi bongo Lake au kufanya mipango, kama wanavyofikiri watu; kazi ambayo Yeye hufanya ndani ya mwanadamu ni ya kawaida sana, kama yalivyo maneno ambayo Yeye hutamka kwa mwanadamu. Mungu anapozungumza, Yeye huonekana kusema jambo ambalo hakukusudia kusema, Yeye husema chochote kinachoingia akilini Mwake, bila kizuizi. Hata hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu huridhishwa kabisa, wao hukosa maneno, wakikodoa macho na kuduwaa. Ni nini kinaendelea hapa? Hili huonyesha vizuri hasa jinsi hekima ya Mungu ilivyo kuu. Kama, jinsi wanavyofikiri watu, kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu ilibidi ipangwe kwa uangalifu sana ili iwe barabara na sahihi, basi—ili kupeleka fikiria hizi hatua moja mbele zaidi—hekima ya Mungu, ajabu, na kutoeleweka vingeweza kupimwa kiasi chake, inayoonyesha ukadiriaji wa watu kuhusu Mungu ni duni sana. Kwa sababu daima huwa kuna ujinga ndani ya matendo ya watu, wao humtathmini Mungu kwa njia hiyo hiyo. Mungu hafanyi mipango au mipangilio kuhusu kazi Yake; badala yake, hiyo hutekelezwa moja kwa moja na Roho wa Mungu—na kanuni ambazo kwazo Roho wa Mungu hufanya kazi ni huru na bila simile. Ni kana kwamba Mungu hatilii maanani hali za mwanadamu na huzungumza Apendavyo—lakini bado mwanadamu hujiondoa kwa maneno ya Mungu kwa shida, ambayo ni kwa sababu ya hekima ya Mungu. Ukweli, hata hivyo, ni ukweli. Kwa sababu kazi ya Roho wa Mungu ndani ya watu wote ni dhahiri sana, hii inatosha kuonyesha kanuni za kazi ya Mungu. Kama Mungu angehitajika kulipa gharama kubwa hivyo katika kazi Yake ndani ya viumbe vilivyoumbwa, hiyo haingekuwa hali ya kutumia mbao nzuri kwa matumizi duni? Je, ni lazima Mungu atende binafsi? Je, ingekuwa na thamani? Kwa kuwa Roho wa Mungu amekuwa akifanya kazi kwa muda mrefu sana, lakini kotekote katika enzi Roho wa Mungu hajawahi kufanya kazi kwa njia hii, hakuna ambaye amewahi kujua njia na kanuni ambazo kwazo Mungu hufanya kazi, hazijawahi kuwa wazi. Leo ziko wazi, kwani Roho wa Mungu amezifichua binafsi—na hii ni bila shaka, inaonyeshwa moja kwa moja na Roho wa Mungu, sio kufupishwa na mwanadamu. Mbona usifunge safari kwenda kwa mbingu ya tatu na uone kama hili ndilo linaloendelea kwa kweli, uone kama, baada ya kufanya kazi hii yote, kazi za Mungu zimemwacha mchovu, mgongo Wake ukimuuma na miguu Yake ikiwa na maumivu, au hata kutoweza kula au kulala; na iwapo ilikuwa ni lazima Asome vifaa vingi sana vya marejeleo ili kuzungumza maneno haya yote, iwapo miswada ya matamshi ya Mungu yametandazwa kote mezani, na iwapo Amekauka mdomoni kutokana na kusema maneno mengi. Ukweli ni kinyume kabisa: Maneno ya hapo juu hayako sawa na mahali ambapo Mungu huishi. Mungu asema, “Nimetumia wakati mwingi, na kulipa gharama kubwa, kwa ajili ya mwanadamu—lakini wakati huu, kwa sababu isiyojulikana, dhamiri za watu zimesalia zisizoweza kamwe kutekeleza shughuli zao za asili.” Haijalishi kama watu wana ufahamu wowote wa huzuni ya Mungu, kama wangeweza kukaribia upendo wa Mungu bila kwenda kinyume cha dhamiri yao, hili lingechukuliwa kuwa la kirazini na la maana. Hofu ya pekee ni kwamba hawako radhi kutumia kazi ya asili ya dhamiri. Je, wasemaje, hii ni sahihi? Je, maneno haya yanakusaidia? Tumaini Langu ni kwamba mtakuwa wa aina ya vitu vilivyo na dhamiri, badala ya kuwa takataka isiyo na dhamiri. Mnafikiri nini kuhusu maneno hayo? Je, kuna yeyote anayefahamu hili? Kudungwa sindano ndani ya mioyo yenu hakuwaumizi? Mungu hudunga sindano ndani ya maiti isiyohisi? Je, Mungu amekosea, uzee umefifisha uwezo Wake wa kuona? Nasema hilo haliwezekani! Hata hivyo, hili lazima liwe ni kosa la mwanadamu. Mbona msiende hospitalini na mtazame? Bila shaka kuna tatiza na moyo wa mwanadamu, unahitaji kuwekewa “viungo” vipya—mwaonaje kuhusu hilo? Mngefanya hilo?

Mungu asema, “Mimi huziangalia sura zao mbaya na vioja, na Mimi huondoka kwa mwanadamu tena. Chini ya hali kama hizi, watu husalia wasiofahamu, na huchukua tena vitu Nilivyowanyima, wakingoja kurudi Kwangu.” Mbona, wakati wa “enzi hii mpya ya teknolojia,” Mungu bado anazungumza juu ya mkokoteni unaovutwa na ng’ombe? Ni kwa nini? Je, ni kwa sababu Mungu hupenda kusumbua? Je, Mungu anapitisha tu muda kwa sababu Hana jingine bora la kufanya? Je, Mungu ni kama mwanadamu, kupoteza tu wakati baada ya kujishindilia chakula? Kuna maana yoyote ya kurudia maneno haya tena na tena? Nimesema kwamba watu ni mafidhuli, kwamba lazima kila mara uwanyakue kwa masikio ili uwasiliane nao. Baada ya maneno kunenwa kwao leo, watayasahau mara moja kesho—ni kana kwamba wanasumbuliwa na usahaulifu. Hivyo, sio ukweli kwamba maneno mengine hayajanenwa, bali ni kwamba hayajatimizwa na watu. Kama jambo fulani linasemwa mara moja au mara mbili tu, watu wanasalia kuwa wajinga—lazima lisemwe mara tatu, hii ndiyo namba ya chini zaidi. Hata kuna “wazee” wengine ambao lazima lisemwe mara kumi hadi ishirini kwao. Kwa njia hii, jambo hilo hilo husemwa tena na tena katika njia tofauti, kuona kama watu wamebadilika au la. Je, mmefanya kazi kweli kwa njia hii? Sitaki kuwagombeza watu, lakini wote wanamfanyia Mungu dhihaka; wote wanajua kuchukua vijalizo vya rutubishi, lakini hawahisi hamu kwa ajili ya Mungu—na je, huku ni kumhudumia Mungu? Huku ni kumpenda Mungu? Si ajabu wao hushinda siku nzima bila kujali kitu chochote, kuhusu wavivu na watulivu. Lakini hata hivyo, watu wengine bado hawajaridhika, na wao husababisha huzuni yao wenyewe. Labda Ninakuwa mkali kidogo, lakini hili ndilo linajulikana kama kuwa mwepesi wa kuvutwa na kujipenda! Je, ni Mungu ambaye hukufanya uhisi mwenye huzuni? Je, hii si hali ya kuleta mateso juu yako mwenyewe? Je, neema yoyote ya Mungu haina sifa inayostahili kuwa chanzo cha furaha yako? Kotekote, hujakuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, na umekuwa mhasi, mdhaifu, na mwenye dhiki—mbona ni hivyo? Je, ni mapenzi ya Mungu kukufanya uishi katika mwili? Hamjui mapenzi ya Mungu, msio na utulivu ndani ya mioyo yenu wenyewe, ninyi hunung’unika na kulalamika, na kushinda siku nzima mkikunja uso, na miili yenu hupata maumivu na mateso—hilo ndilo mnalostahili! Mnawaambia wengine wamsifu Mungu kati ya kuadibu, kwamba waibuke kutoka kwa kuadibu, na wasizuiwe nako—lakini ninyi mmeingia ndani yake na hamuwezi kuhepa. Inachukua miaka mingi kuiga hii “roho ya kujitoa mhanga” kama ya Dong Cunrui. Unapohubiri maneno na kanuni, huoni aibu? Je, wajijua mwenyewe? Umejiweka kando? Unampenda Mungu kweli? Umeweka kando matazamio na majaliwa yako? Si ajabu Mungu husema kwamba watu ndio walio wa ajabu na wasioeleweka. Nani angefikiri kwamba kuna “hazina” nyingi sana ndani ya mwanadamu ambazo hazijachimbwa? Leo, mandhari yake yanatosha “kufungua macho ya mtu”—watu ni “wa ajabu” sana! Ni kana kwamba Mimi ni mtoto asiyeweza kuhesabu. Hata leo bado Sijaelewa ni watu wangapi wanampenda Mungu kweli. Siwezi kamwe kukumbuka idadi—na kwa hiyo, kwa sababu ya “kuasi” Kwangu, wakati unapofika wa kutoa hesabu mbele ya Mungu, Mimi kila mara huwa mikono mitupu, Nisiyeweza kufanya vile Ningependa, Mimi kila mara huwa katika deni la Mungu. Kutokana na hilo, Nitoapo hesabu, Mimi kila mara “hukemewa” na Mungu. Sijui ni kwa nini watu ni katili sana, kila mara wao hunifanya Niteseke kwa ajili ya hili. Watu hutumia nafasi hii kuangua kicheko, wao si marafiki Wangu kweli. Nikiwa katika matatizo, wao hawanipi msaada wowote, lakini hunifanyia mzaha kwa makusudi—wao kweli hawana dhamiri!

Iliyotangulia: Sura ya 39

Inayofuata: Sura ya 41

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp