Sura ya 33

Kwa ukweli, kutegemea kile ambacho Mungu amefanya ndani ya watu, na kuwapa, na vilevile kile ambacho watu wanacho, inaweza kusemwa kwamba matakwa Yake kwa watu sio makubwa mno, kwamba hataki mengi kutoka kwao. Wangekosaje basi, kujaribu kumridhisha Mungu? Mungu humpa mwanadamu asilimia mia moja, lakini Huhitaji tu sehemu ndogo ya asilimia kutoka kwa watu—hii ni kuhitaji mengi sana? Je, Mungu analeta tatizo pasipo na chochote? Mara nyingi, watu huwa hawajijui, huwa hawajichunguzi mbele ya Mungu, na kwa hiyo huwa kuna nyakati nyingi ambapo wao hutegwa—hili lingefikiriwa vipi kuwa ni kushirikiana na Mungu? Iwapo kumewahi kuwa na wakati ambapo Mungu hakuweka mzigo mzito juu ya watu, wangevunjika kama udongo, na hawangekuwa na ari ya kutafuta vitu. Hivyo ndivyo walivyo watu, ama ni baridi au hasi, daima wasioweza kushirikiana na Mungu kwa utendaji, kila mara wao hutafuta sababu hasi ya kukubali kushindwa na wao wenyewe. Je, wewe kweli ni mtu anayefanya kila kitu sio kwa ajili yako mwenyewe, bali kumridhisha Mungu? Je, wewe kweli ni mtu asiyetegemea hisia, asiye na upendeleo wake mwenyewe, na ambaye anatimiza mahitaji ya kazi ya Mungu? “Kwa nini daima wao hujaribu kubishana na Mimi? Je, mimi ni msimamizi mkuu wa kituo cha biashara? Kwa nini Mimi hutimiza kwa moyo kamili kile ambacho watu hudai kutoka Kwangu, lakini Nitakacho kutoka kwa mwanadamu hakitimii?” Kwa nini Mungu huuliza mambo kama hayo mara kadhaa mfululizo? Kwa nini Analia kwa hofu hivyo? Mungu hajapata chochote kutoka kwa watu, yote aonayo ni kazi wanayochukua na kuchagua. Mbona Mungu asema, “lakini Nitakacho kutoka kwa mwanadamu hakitimii”? Jiulizeni: Tangu mwanzo hadi mwisho, ni nani awezaye kufanya kazi ya wajibu wake bila chaguo lolote? Ni nani asiyetenda kwa ajili ya hisia zilizo ndani ya moyo wake? Watu huzipa tabia zao uhuru, bila kuvumilia kwa yale wanayofanya, kana kwamba wanavua siku tatu na kuziacha nyavu zao nakushinda siku mbili bila kufanya chochote. Wao huwa moto na baridi kwa zamu: Wanapokuwa moto, wanaweza kuteketeza vitu vyote duniani, na wanapokuwa baridi, wanaweza kugandisha maji yote duniani. Hii si kazi ya mwanadamu, lakini ni analojia ya kufaa zaidi kuhusu hali ya mwanadamu. Huu si ukweli? Labda Nina “dhana” kuhusu watu, labda Ninawasingizia—lakini hata hivyo, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.” Ingawa hii ni methali ya binadamu, Nafikiri inafaa kutumiwa hapa. Sivunji mioyo ya watu kwa makusudi na kukanusha shughuli zao. Hebu Nishauriane nanyi kuhusu maswali fulani: Ni nani huchukulia kazi ya Mungu kama kazi ya wajibu wake mwenyewe? Ni nani aweza kusema, “Maadamu ninaweza kumridhisha Mungu, nitatoa yangu yote”? Ni nani awezaye kusema, “Bila kujali wengine, nitafanya yote ambayo Mungu anahitaji, na haijalishi kama kiasi cha kazi ya Mungu ni kirefu au kifupi, nitatimiza wajibu wangu; kufikisha kazi Yake mwisho ni shughuli ya Mungu, si kitu ninachofikiria”? Nani ana uwezo wa maarifa kama hayo? Haijalishi mnachofikiria—labda una ujuzi wa juu sana, kwa hivyo Nakubali, Nakubali kushindwa—lakini lazima Niwaambie kile ambacho Mungu anataka ni moyo mtiifu ulio mwaminifu na ulio na shauku, si moyo wa mbwa mwitu unaokosa shukrani. Unajua nini kuhusu “kujadiliana” huku? Tangu mwanzo hadi mwisho, “mmesafiri ulimwenguni.” Wakati mmoja mko “Kunming,” na majira yake ya kuchipua daima, na kufumba na kufumbua mmewasili katika “Ncha ya Kusini” yenye baridi ya kukandamiza iliyofunikwa na theluji. Ni nani hajawahi kuvunja ahadi yake? Kile ambacho Mungu anataka ni roho ya, “Hakuna kupumzika mpaka kifo,” kile Anachotaka ni ile ambayo watu “hawarudi nyuma mpaka wafike ukuta wa kusini.” Kwa kawaida, kusudi la Mungu si kwa watu kufuata njia isiyo sahihi, bali kuwa na roho kama hiyo. Kama asemavyo Mungu, “Ninapolinganisha ‘zawadi’ walizotoa kwa vitu Vyangu, watu hutambua thamani Yangu mara moja, na wakati huo tu ndio wao huona kutopimika Kwangu.” Maneno haya yanaweza kuelezwa vipi? Labda, kusoma maneno yaliyo hapo kunakupa maarifa fulani, kwani Mungu hutoa moyo wote wa mwanadamu kwa uchunguzi, wakati huo watu huja kuyajua maneno haya. Lakini kwa ajili ya maana kubwa ya ndani ya maneno ya Mungu, watu bado hawaelewi mwili wa zamani, kwani hawajasoma katika chuo kikuu cha tiba, wala wao si wanaakiolojia, na kwa hiyo wanahisi kwamba neno hili jipya halifahamiki—na wakati huo tu ndipo wao husalimu amri kidogo. Kwa vile watu ni wadhaifu mbele ya mwili wa zamani; ingawa si kama mnyama mkali, wala kuweza kufutilia mbali wanadamu kama bomu la atomu, hawajui wafanye nini nao, kana kwamba wao ni wadhaifu. Lakini Kwangu, kuna njia za kushughulikia mwili wa zamani. Mwanadamu kukosa kamwe kufanya juhudi za kufikiri juu ya hatua ya kuzuia kumesababisha vioja mbalimbali vya mwanadamu kutokea ghafla siku zote mbele ya macho Yangu; kama tu alivyosema Mungu: “Nionyeshapo uzima Wangu kwao, wao hunitazama kwa macho yaliyokodoa, wakisimama mbele Yangu bila kujongea, kama nguzo ya chumvi. Na Ninapotazama kutokuwa kawaida kwao Mimi huwa na taabu kujizuia kucheka. Kwa sababu wananyosha mkono kuomba vitu kutoka Kwangu, Mimi huwapa vitu vilivyo mkononi Mwangu, nao huvikumbatia, wakivitunza kama mtoto aliyezaliwa hivi sasa, ishara waifanyayo tu mara moja.” Je, haya si matendo ya mwili wa zamani? Kwa vile, leo, watu wanaelewa, mbona wasiache, na badala yake bado wanaendelea? Kwa kweli, sehemu ya matakwa ya Mungu si yasiyofikiwa na mwanadamu, lakini watu hawayatilii maanani, kwa kuwa “Simwadibu mwanadamu kwa urahisi. Ni kwa sababu hii ndiyo watu daima wameipa miili yao uhuru. Hawafuati mapenzi Yangu, wamenirairai daima mbele ya kiti Changu cha hukumu.” Je, hiki si kimo cha mwanadamu? Si kwamba Mungu anatafuta makosa kwa makusudi, lakini kwamba huu ni uhalisi—ni lazima Mungu aeleze hili? Kama tu asemavyo Mungu, “Ni kwa kuwa ‘imani’ ya watu ni kubwa mno ndio wao ni ‘wa kusifiwa.’” Kwa sababu hii, Natii mipango ya Mungu, na kwa hiyo Sisemi mengi kuhusu hili; kwa sababu ya imani ya watu, Naelewa na kutumia hili, Nikitumia imani yao kuwafanya watekeleze kazi yao bila Mimi kuwakumbusha. Je, ni kosa kufanya hili? Je, hili silo hasa analohitaji Mungu? Labda, baada ya kusikia maneno kama haya, watu wengine huenda wakahisi kuchoshwa—kwa hivyo Nitanena kuhusu jambo lingine, ili kutowahukumu sana. Wakati ambapo wateule wote wa Mungu katika ulimwengu mzima watapitia kuadibu, na wakati ambapo hali ndani ya mwanadamu itarekebishwa, watu watafurahia kisirisiri ndani ya mioyo yao, kana kwamba wameepuka majonzi. Wakati huu, watu hawatajichagulia tena, kwani hili hasa ndilo tokeo lililotimizwa wakati wa kazi ya mwisho ya Mungu. Hatua Zake zikiwa zimeendelea mpaka leo, wana na watu wote wa Mungu wameingia katika kuadibu, na Waisraeli, pia, hawawezi kukwepa awamu hii, kwani watu wametiwa doa na uchafu ndani yao, na kwa hiyo Mungu anawaongoza watu wote kuingia katika tanuu kuu la kuyeyusha madini ili kusafishwa, ambayo ni njia ya lazima. Baada ya hili kupita, watu watafufuliwa kutoka kifo, ambalo hasa ndilo Mungu alitabiri katika “matamko ya Roho saba.” Sitanena zaidi kuhusu hili, ili Nisiwachokoze watu. Kwa vile kazi ya Mungu ni ya ajabu, unabii ulionenwa kutoka kinywani mwa Mungu lazima hatimaye utimizwe; Mungu anapowaambia watu wanene kuhusu dhana zao mara nyingine tena, wao huduwaa, na kwa hiyo mtu yeyote asiwe na wahaka au wasiwasi. Kama Nilivyosema tu, “Kuhusu kazi Yangu yote, kuliwahi kuwa na hatua iliyotekelezwa kwa mikono ya mwanadamu?” Je, unaelewa kiini cha maneno haya?

Iliyotangulia: Sura ya 32

Inayofuata: Sura ya 35

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp