Sura ya 32

Maneno ya Mungu huwaacha watu wakikuna vichwa vyao; ni kana kwamba, Anapozungumza, Mungu anaepukana na mwanadamu na kuzungumza na hewa, kana kwamba Hafikirii hata kidogo kuzingatia zaidi matendo ya mwanadamu, na Hatilii maanani kabisa kimo cha mwanadamu, kana kwamba maneno Anayozungumza hayaelekezwi kwa dhana za watu, lakini kuepukana na mwanadamu, kama lilivyokuwa kusudi la Mungu la asili. Kwa sababu nyingi sana, maneno ya Mungu hayaeleweki na mwanadamu hawezi kuyapenya. Hili halishangazi. Lengo la asili la maneno yote ya Mungu si kwa watu kupata ujuzi au ustadi kwayo; badala yake, ni njia moja kati ya zile Mungu ametumia kufanya kazi kutoka mwanzo hadi leo. Bila shaka, kutoka kwa maneno ya Mungu watu wanapata vitu vinavyohusiana na mafumbo, ama vitu vinavyowahusu Petro, Paulo, na Ayubu—lakini hili ndilo wanalopaswa kufikia, na kile wanachoweza kufikia, na, kama ifaavyo kimo chao, hili tayari limefikia kilele chake. Mbona matokeo ambayo Mungu anauliza yafikiwe si ya juu, lakini Amezungumza maneno mengi sana? Hili linahusiana na kuadibu Anakozungumzia, na kwa kawaida, yote yanafanikishwa bila watu kutambua. Leo, watu wanastahimili mateso makuu zaidi chini ya mashambulio ya maneno ya Mungu. Kwa juu juu, hakuna kati yao anayeonekana kuwa ameshughulikiwa, watu wameanza kuwekwa huru katika kufanya kazi yao, na watendaji-huduma wamepandishwa cheo kuwa watu wa Mungu—na katika hili, inaonekana kwa watu kwamba wameingia katika raha. Kwa kweli, ukweli ni kwamba, kutoka kwa utakasaji, wote wameingia katika kuadibu kukali zaidi. Kama tu vile Mungu anavyosema, “Hatua za kazi Yangu zinaungana kwa karibu moja kwa ifuatayo, kila moja ikiwa juu zaidi kila mara.” Mungu amewainua watendaji-huduma kutoka kwa shimo na kiberiti, ambapo kuadibu ni kukali zaidi. Hivyo, wanapitia hata taabu zaidi, ambayo ni vigumu kuitoroka. Je, kuadibu kama huko si kukali zaidi? Baada ya kuingia katika eneo la juu zaidi, kwa nini watu wanahisi huzuni badala ya furaha yoyote? Mbona inasemekana kwamba baada ya kuokolewa kutoka kwa mikono ya Shetani, wanakabidhiwa joka kuu jekundu? Unakumbuka Mungu aliposema, “Sehemu ya mwisho ya kazi inamalizika katika nyumba ya joka kuu jekundu”? Unakumbuka wakati Mungu alisema, “Taabu ya mwisho ni kuwa na ushuhuda mkubwa sana, wa nguvu kwa ajili ya Mungu mbele ya joka kuu jekundu”? Iwapo watu hawakabidhiwi joka kuu jekundu, wangewezaje kuwa na ushuhuda mbele yake? Nani amewahi kusema maneno kama “Nimemshinda ibilisi” baada ya kujiua? Kujiua baada ya kuuona mwili wake kuwa adui—umuhimu halisi wa hili uko wapi? Mbona Mungu alizungumza hivyo? “Siyaangalii makovu ya watu, lakini katika sehemu yao ambayo haina makovu, na kutokana na hili Napata uridhisho.” Kama Mungu angetaka wale wasio na makovu kuwa maonyesho Yake, kwa nini Amezungumza kwa subira na ari maneno mengi kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu kulipiza kisasi dhidi ya dhana za watu? Mbona Ajisumbue na hilo? Mbona Ajitaabishe kufanya jambo kama hilo? Hivyo inaonyesha kwamba kuna umuhimu wa kweli kwa kupata mwili kwa Mungu, kwamba “hangefutilia mbali” mwili baada ya kupata mwili na kukamilisha kazi Yake. Mbona inasemekana kwamba “dhahabu haiwezi kuwa safi na mwanadamu hawezi kuwa mtimilifu”? Maneno haya yanaweza kuelezwa vipi? Mungu anapozungumza kuhusu kiini cha mwanadamu, maneno Yake yanamaanisha nini? Kwa macho ya mwanadamu, mwili unaonekana kutoweza chochote, au sivyo kupungukiwa sana. Kwa macho ya Mungu, hili si muhimu hata kidogo—ilhali kwa watu, ni suala kubwa mno. Ni kana kwamba hawawezi kabisa kutatua hili na lazima lishughulikiwe binafsi na sayari za juu.—je, hii si dhana ya watu? “Katika macho ya watu, Mimi ni ‘nyota ndogo’ tu ambayo imeshuka kutoka angani; nyota ndogo mbinguni, na ujaji Wangu duniani leo uliagizwa na Mungu. Kwa hiyo, watu wamebuni fasiri zaidi za maneno ‘Mimi’ na ‘Mungu,’” Kwa kuwa wanadamu wamekuwa bure, kwa nini Mungu hufichua dhana zao kutoka kwa mitazamo tofauti? Je, hii pia inaweza kuwa hekima ya Mungu? Maneno kama hayo si mzaha? Kama Mungu anavyosema, “Ingawa kuna mahali ambapo Nimeweka katika mioyo ya watu, hawahitaji kwamba Niishi hapo. Badala yake, wanamsubiri ‘Mtakatifu’ katika mioyo yao kuwasili ghafla. Kwa sababu utambulisho Wangu ni ‘duni’ sana, Sifikii mahitaji ya watu na hivyo Naondolewa na wao.” Kwa sababu makadirio ya watu ni ya “juu sana,” vitu vingi “hayawezi kutimizwa” kwa Mungu, jambo ambalo linamweka “katika ugumu.” Watu hawajui hata kidogo kwamba wanachouliza kutoka kwa Mungu kuweza ni dhana zao. Na hii si maana halisi ya “Mtu mwerevu anaweza kuwa mwathiriwa wa ustadi wake mwenyewe”? Hii kwa kweli ni hali ya “kuwa stadi kama kanuni, lakini wakati huu mpumbavu”! Katika kuhubiri kwenu, mnawaomba watu waachane na Mungu wa fikira zao, lakini Mungu wa fikira zenu ameondoka? Je, maneno ya Mungu kwamba “Madai ninayofanya kutoka kwa mwanadamu si makubwa hata kidogo” yanawezaje kufasiriwa? Si ya kuwafanya watu wawe hasi na wapotovu ila kuwapa ufahamu safi wa maneno ya Mungu—mnaelewa? Je, Mungu mwenye mwili kweli ni “‘Mimi’ ambaye ni mwenye majivuno” kama watu wanavyofikiria?

Ingawa kuna wale ambao wamesoma maneno yote yaliyonenwa na Mungu na wanaweza kuyatolea muhtasari wa jumla, nani anayeweza kuzungumzia lengo la msingi la Mungu ni nini? Hili ndilo mwanadamu anakosa. Bila kujali ni kwa mtazamo gani Mungu huzungumza, lengo Lake la jumla ni kuwafanya watu wamjue Mungu aliye katika mwili. Kama hakungekuwa na chochote kisicho cha uungu—kama chote Alicho nacho kingekuwa sifa za kiasili za Mungu mbinguni—basi hakungekuwa na haja ya Mungu kusema mengi sana. Inaweza kusemwa kwamba kile watu wanakosa hutumika kama nyenzo za asili ambazo zinapatana na maneno ya Mungu. Ambayo ni kusema, kile kinachodhihirishwa kwa mwanadamu ni usuli wa kile Mungu husema kuhusu dhana za watu, na hivyo, watu huhudumia matamshi ya Mungu. Kwa kawaida, hili linategemezwa kwa kile Mungu husema kuhusu dhana za watu—ni kwa njia hii tu ndio hili linaweza kusemwa kuwa mchanganyiko wa nadharia na uhalisi, hapo tu ndipo watu wanaweza kufanywa kwa ufanisi kuwa makini kuhusu kujijua. Ingekuwa faida gani kama Mungu katika mwili Angelingana na dhana za watu na Mungu pia Alimshuhudia? Ni hasa kwa sababu ya hili kwamba Mungu hufanya kazi kutoka kwa upande hasi, Akitumia dhana za watu kusisitiza nguvu Yake kuu. Je, hii si hekima ya Mungu? Yote ambayo Mungu hufanya kwa ajili ya kila mtu ni mazuri—hivyo mbona msisifu wakati huu? Kama mambo yangefika mahali fulani, au siku ije, je, wewe, kama Petro, ungeweza kutamka maombi kutoka ndani yako katikati ya majaribu? Iwapo tu, kama Petro, bado unaweza kumsifu Mungu wakati uko katika mikono ya Shetani ndipo kutakuwa na maana ya kweli ya “kuwekwa huru kutoka katika utumwa wa Shetani, kuushinda mwili, na kumshinda Shetani.” Je, huu si ushuhuda halisi zaidi kwa Mungu? Hii tu ndiyo athari inayofanikishwa na “uungu kuja kutenda na Roho aliyezidishiwa nguvu mara saba Anayefanya kazi ndani ya mwanadamu,” na hivyo, pia, ndiyo athari inayofanikishwa na “Roho akitoka kwa mwili.” Je, matendo kama hayo si halisi? Ulikuwa na mazoea ya kuzingatia uhalisi, lakini una maarifa ya ukweli kuhusu uhalisi leo? “Madai ninayofanya kutoka kwa mwanadamu si makubwa hata kidogo, lakini watu wanaamini vinginevyo. Hivyo, ‘unyenyekevu’ wao unafichuliwa katika kila tendo lao. Daima wanastahili kutembea mbele Yangu wakiniongoza njia, wakiwa na hofu kubwa kwamba Nitapotea, wakiogopa kwamba Nitazurura katika misitu ya kale ndani ya milima. Kwa hiyo, watu daima wameniongoza mbele, wakiwa na hofu sana kwamba Nitaingia katika gereza la chini ya ardhi.” Maarifa yenu kuhusu maneno haya rahisi ni yapi—kwa kweli mnaweza kuelewa asili ya maneno ya Mungu ndani yao? Mmezingatia ni dhana gani zenu ambazo Mungu amezungumza maneno kama hayo kuzihusu? Je, kila siku uangalifu wenu uko kwa suala hili muhimu? Katika sentensi ya kwanza ya sehemu ifuatayo, ambayo inakuja baadaye kwa karibu, Mungu anasema, “Lakini watu hawajui mapenzi Yangu na wanaendelea kuombea vitu kutoka Kwangu, kana kwamba utajiri Niliowapa hauwezi kukidhi mahitaji yao, kana kwamba mahitaji yanashinda ugavi.” Katika sentensi hii inaweza kuonekana dhana zilizo ndani zenu ni zipi. Mungu hakumbuki wala kuchunguza kile mlichofanya katika nyakati zilizopita, kwa hivyo msifikirie tena masuala ya nyuma. La muhimu zaidi ni kama mnaweza kuunda “roho ya Petro katika enzi ya mwisho” katika njia ya baadaye—je, mna imani ili kufikia hili? Kile Mungu huuliza kutoka kwa mwanadamu ni kumuiga Petro tu, kwamba watu waweze hatimaye kubuni njia ili kuliaibisha joka kuu jekundu. Ni kwa sababu ya hili ndio Mungu anasema, “Natumaini tu kwamba watu wana azimio la kushirikiana na Mimi. Siulizi kwamba wanipikie chakula kizuri, au wanipangie mahali pa kufaa ili Nilaze kichwa Changu….” Duniani, watu wanaulizwa wawe na “roho ya Lei Feng” katika miaka ya 1990 hadi 1999, lakini katika nyumba ya Mungu, Mungu anauliza kwamba mtengeneze “mtindo wa pekee wa Petro.” Je, mnaelewa mapenzi ya Mungu? Je, kweli mnaweza kujitahidi kwa ajili ya hili?

“Natembea juu ya ulimwengu, na Ninapotembea Ninaangalia kwa makini watu wa ulimwengu mzima. Kati ya umati wa watu duniani, hakujawahi kuwa na wowote ambao wanafaa kwa kazi Yangu ama ambao wananipenda kwa kweli. Hivyo, kwa wakati huu Ninahema kwa kuvunjika moyo, na watu wanatawanyika mara moja, wasikusanyike tena, wakiogopa sana kwamba ‘Nitawakamata wote katika wavu mmoja.’” Watu wengi sana, pengine, wanaona maneno haya kuwa magumu sana kuelewa. Wanauliza mbona Mungu haulizi mengi kutoka kwa mwanadamu, ilhali Yeye huhema kwa kuvunjika moyo kwa sababu hakuna wowote wanaofaa kwa ajili ya kazi Yake. Je, kuna ukinzani hapa? Kuzungumza neno kwa neno, kunao—lakini kwa uhalisi, hakuna ukinzani. Pengine bado unaweza kukumbuka Mungu aliposema, “Maneno Yangu yote yatakuwa na athari Ninayotaka sana.” Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili, watu hukazia macho kila tendo Lake kuona kile Atakachofanya hasa. Mungu anapotekeleza kazi Yake mpya kumwelekea Shetani katika ufalme wa kiroho, kunazo, kwa maneno mengine, dhana za aina yote zinazozalishwa miongoni mwa watu duniani kwa sababu ya Mungu katika mwili. Mungu ahemapo kwa kuvunjika moyo, yaani, Anapozungumza kuhusu dhana zote za mwanadamu, watu wanajaribu yote wawezayo kuzishughulika, na hata kuna wale ambao wanaamini hawana matumaini, kwa maana Mungu anasema kwamba wote ambao wana dhana kumhusu ni adui Zake—na basi watu wangewezaje kukosa “kutawanyika” kwa sababu ya hili? Hasa leo, wakati kuadibu kumefika, watu wanaogopa hata zaidi kwamba Mungu atawaondoa. Wanaamini kwamba baada ya wao kuadibiwa, Mungu “atawakamata wote katika wavu mmoja.” Ilhali ukweli si hivyo: Kama asemavyo Mungu, “Sitaki ‘kuwazuia’ watu katikati ya kuadibu Kwangu, wasitoroke kamwe. Kwa sababu usimamizi Wangu unakosa matendo ya mwanadamu, haiwezekani kumaliza kazi Yangu kwa ufanisi, jambo ambalo huizuia kazi Yangu kuendelea mbele kwa ufanisi.” Mapenzi ya Mungu si kwa kazi Yake kumalizika wakati watu wote wameuwawa—hiyo ingekuwa na faida gani? Kwa kufanya kazi ndani ya watu na kuwaadibu, Mungu kisha anaweka wazi matendo Yake kupitia kwao. Kwa sababu watu hawajawahi kuelewa kwamba tayari kuna kuadibu katika sauti ya maneno ya Mungu, hawajawahi kuwa na kuingia katika akili zao. Watu hawana uwezo wa kuonyesha uamuzi wao, na hivyo Mungu hawezi kusema chochote mbele ya Shetani, jambo ambalo linakomesha kazi ya Mungu kuendelea mbele. Hivyo Mungu anasema, “Wakati mmoja Nilimwalika mwanadamu kama mgeni katika nyumba Yangu, ilhali alikimbia huku na kule kwa sababu ya miito Yangu—kana kwamba, badala ya kumwalika kama mgeni, Nilikuwa Nimemleta eneo la maangamizi. Hivyo, nyumba Yangu iliachwa tupu, kwani mwanadamu daima aliepukana na Mimi na daima alikuwa akijihadhari dhidi Yangu. Hili liliniacha bila namna ya kutekeleza sehemu ya kazi Yangu.” Ni kwa sababu ya makosa ya mwanadamu katika kazi yake ndio Mungu anatoa mahitaji Yake ya mwanadamu kwa dhahiri. Na ni kwa sababu watu wanakosa kutimiza hatua hii ya kazi ndio Mungu anaongeza matamshi mengine—ambayo hasa ni “sehemu nyingine ya kazi kwa mwanadamu” ambayo Mungu huzungumzia. Lakini Sitazungumzia “kuwakamata wote katika wavu mmoja” ambayo Mungu anazungumzia, kwa sababu hili halihusiani sana na kazi ya leo. Kwa kawaida, katika “Maneno ya Mungu Kwa Ulimwengu Mzima,” maneno Yake mengi yanahusiana na mwanadamu—lakini watu wanapaswa kuelewa mapenzi ya Mungu; bila kujali kile Anachosema, makusudio Yake daima ni mazuri. Inaweza kusemwa kwamba kwa sababu njia ambazo Mungu hutumia kuzungumza ni nyingi sana, watu hawana uhakika kwa asilimia mia kuhusu maneno ya Mungu, na wanaamini kwamba mengi ya maneno ya Mungu yanazungumzwa kwa sababu ya vitu vya lazima vya kazi Yake, na hayana mengi ambayo ni ya kweli, jambo ambalo linawaacha wakiwa wamechanganyikiwa na kusumbuliwa na mawazo yao—kwani katika dhana zao, Mungu ni mwenye hekima sana, Hafikiwi na wao kabisa, ni kana kwamba hawajui chochote, na hawana habari kuhusu jinsi ya kula maneno ya Mungu. Watu hufanya maneno ya Mungu kuwa ya kuwazika tu na magumu kufahamika—kama asemavyo Mungu, “watu daima hutaka kuongeza ladha kwa matamshi Yangu.” Kwa sababu mawazo yao ni yenye utata sana, na “hufikiwa kwa shida” na Mungu, sehemu ya maneno ya Mungu yanazuiwa na mwanadamu, ikimwacha Yeye bila chaguo ila kuzungumza kwa namna ambayo ni waziwazi na dhahiri. Kwa sababu mahitaji ya watu ni “ya juu sana,” na kwa sababu fikira zao ni nyingi sana—kana kwamba wanaweza kuvuka na kuingia katika ufalme wa kiroho ili kuyaona matendo ya Shetani—hili limepunguza maneno ya Mungu, kwa maana kadiri anavyosema Mungu, ndivyo nyuso za watu zinavyokuwa za huzuni zaidi. Kwa nini hawawezi kutii tu, badala ya kutafakari mwisho wao? Iko wapi faida kwa hili?

Iliyotangulia: Sura ya 31

Inayofuata: Sura ya 33

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp