Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Mwanadamu Anavyofikiria?

Kama waumini wa Mungu, kila mmoja wenu anapaswa kuelewa kwamba mmepata kwa kweli kupandishwa hadhi na wokovu mkuu zaidi kwa kupokea leo kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kazi yote ya mpango Wake ambayo Anaifanya juu yako. Mungu ameweka lengo lote la kazi Yake katika ulimwengu juu ya kundi hili la watu. Ametoa damu yote ya moyo Wake kwa ajili yenu; Ameiondoa kazi yote ya Roho katika ulimwengu na kuwapa ninyi. Hiyo ndiyo maana ninyi ndio mliobahatika. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu Wake kutoka Israeli, watu Wake wateule, kuja kwenu, na Atalifanya kusudi la mpango Wake lidhihirike kikamilifu kupitia kundi hili. Kwa hivyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi ya hili, ninyi ndio warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine ninyi nyote mnakumbuka maneno haya: "Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, inatufanyia utukufu wa uzito wa milele uzidio kuwa mkuu sana." Ninyi nyote mmesikia maneno haya hapo awali, lakini hakuna hata mmoja wenu aliyeelewa maana yake ya kweli. Leo, mnatambua kwa kina umuhimu wake halisi. Maneno haya yatatimizwa na Mungu katika siku za mwisho, na yatatimizwa ndani ya wale ambao wameteswa kikatili na joka kuu jekundu katika nchi ambamo limelala likiwa limejikuja. Joka kuu jekundu linamtesa Mungu na ni adui wa Mungu, na hivyo, watu katika nchi hii wanakabiliwa na udhalilishaji na mateso kwa sababu ya imani yao katika Mungu, na maneno haya yanatimizwa ndani yenu, kundi hili la watu, kama matokeo. Kwa sababu Mungu anatekeleza kazi Yake katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vikwazo vikubwa, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa mara moja; hivyo, watu wanasafishwa kwa sababu ya maneno ya Mungu, jambo ambalo pia ni sehemu ya mateso. Ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kazi Yake katika nchi ya joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndiyo Mungu anafanya hatua moja ya kazi Yake, ili Aweze kufunua hekima Yake na matendo Yake ya ajabu, na Mungu anatumia fursa hii kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili. Ni kupitia mateso ya watu, kupitia ubora wao wa tabia, na kupitia tabia zote za kishetani za watu wa nchi hii chafu ndiyo Mungu anafanya kazi Yake ya utakaso na ushindi, ili kwamba, kutokana na hili, Aweze kupata utukufu na wale walio na ushuhuda kwa matendo Yake. Hivyo ndivyo ulivyo umuhimu wote wa gharama yote ambayo Mungu amelipa kwa ajili ya kundi hili la watu. Yaani, ni kupitia wale wanaompinga Yeye ndiyo Mungu anafanya kazi ya ushindi, na ni kwa njia hii tu ndiyo nguvu kuu ya Mungu inaweza kufunuliwa. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi chafu ndio wanaostahili kurithi utukufu wa Mungu, na ni hili tu linaloweza kukazia nguvu kuu ya Mungu. Hiyo ndiyo maana ni kutoka katika nchi chafu, na kutoka kwa wale wanaoishi katika nchi chafu, ndiyo Mungu anapata utukufu—hiyo ndiyo nia ya Mungu. Hii ni kama tu hatua ya kazi ya Yesu: Angeweza tu kupata utukufu miongoni mwa wale Mafarisayo waliomtesa Yeye; isingekuwa kwa ajili ya mateso ya Mafarisayo na usaliti wa Yuda, Yesu asingedhihakiwa au kusingiziwa, sembuse kusulubiwa, na Asingekuwa amepata utukufu. Mahali ambapo Mungu anafanya kazi katika kila enzi, na mahali ambapo Anafanya kazi Yake katika mwili, ndipo mahali Anapopata utukufu na mahali Anapowapata wale ambao Anakusudia kuwapata. Huu ndio mpango wa kazi ya Mungu, na huu ndio usimamizi Wake.

Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, sehemu mbili za kazi zinafanywa katika mwili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo kwayo Anapata utukufu; nyingine ni kazi ya ushindi na utimilifu katika siku za mwisho, ambayo kwayo Anapata utukufu. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Kwa hivyo msichukulie kazi ya Mungu, au agizo la Mungu kwenu, kama jambo rahisi. Ninyi nyote ni warithi wa utukufu wa Mungu wa uzito wa milele uzidio kuwa mkuu sana, na hili liliamuriwa hasa na Mungu. Kati ya sehemu mbili za utukufu Wake, moja inadhihirishwa ndani yenu; ukamilifu wa sehemu moja ya utukufu wa Mungu umekabidhiwa kwenu, ili uweze kuwa urithi wenu. Huku ni kuinuliwa kwenu na Mungu, na pia ndio mpango ambao Aliuamua kabla zamani. Kwa kuzingatia ukuu wa kazi ambayo Mungu amefanya katika nchi ambamo joka kuu jekundu linaishi, kazi hii ingehamishiwa kwingineko, ingekuwa imezaa matunda makubwa kitambo na kukubaliwa kwa urahisi na mwanadamu. Zaidi ya hayo, kazi hii ingekuwa rahisi mno kukubaliwa na wale makasisi wa Magharibi wanaomwamini Mungu, kwa maana hatua ya kazi ya Yesu inatumika kama kitangulizi. Hii ndiyo maana Mungu hawezi kufanikisha hatua hii ya kazi ya kupata utukufu kwingineko; wakati kazi inaungwa mkono na watu na kutambuliwa na serikali, hakuna mahali pa utukufu wa Mungu kupata msingi. Huu hasa ndio umuhimu wa kipekee ambao hatua hii ya kazi ilio nao katika nchi hii. Hakuna hata mtu mmoja miongoni mwenu ambaye analindwa na sheria—badala yake, ninyi mnaadhibiwa na sheria. Ugumu mkubwa hata zaidi ni kwamba watu hawawaelewi ninyi: Wawe ni jamaa zenu, wazazi wenu, marafiki zenu, au wafanyakazi wenzenu, hakuna hata mmoja wao anayewaelewa ninyi. "Mnapotelekezwa" na Mungu, haiwezekani kwenu kuendelea kuishi katika ulimwengu huu, lakini hata hivyo, bado watu hawawezi kustahimili kuwa mbali na Mungu. Huu ndio umuhimu wa ushindi wa Mungu kwa watu, na ndio utukufu wa Mungu. Kile ambacho mmerithi leo kinazidi kile cha mitume na manabii katika enzi zote na ni kikuu hata kuliko kile cha Musa na Petro. Baraka haziwezi kupatikana kwa siku moja au mbili; lazima zipatikane kwa gharama kubwa. Yaani, lazima muwe na upendo ambao umepitia usafishaji, lazima muwe na imani kuu, na lazima muwe na ukweli mwingi ambao Mungu anawahitaji mfikie; zaidi ya hayo, lazima muweze kugeuka kuelekea kwenye haki, bila kutishwa au kuogopa, na lazima muwe na moyo umpendao Mungu ambao ni wa siku zote hadi kifo. Lazima muwe na azimio, tabia yenu ya maisha lazima ibadilike, upotovu wenu lazima uponywe, lazima mkubali mipango yote ya Mungu bila malalamiko, na hata muweze kutii hadi kifo. Hiki ndicho mnachopaswa kufikia, hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na ndicho ambacho Mungu anataka kutoka kwa kundi hili la watu. Kwa kuwa Anawapa ninyi, hakika Atadai kutoka kwenu kama malipo, na hakika Ataweka mahitaji yanayofaa kwenu. Kwa hivyo, kuna busara katika kazi yote ambayo Mungu anafanya. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwa nini, mara kwa mara, Mungu anafanya kazi inayoweka viwango vya juu na mahitaji makali. Kwa hivyo, mnapaswa kujazwa na imani kwa Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu inafanywa kwa ajili yenu, inafanywa ili mweze kustahili kupokea urithi Wake. Badala ya kusema kwamba ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu mwenyewe, ingekuwa bora kusema kwamba ni kwa ajili ya wokovu wenu na kwa ajili ya kulifanya kuwa timilifu kundi hili la watu ambao wameteswa sana katika nchi chafu. Mnapaswa kuelewa nia ya Mungu. Na hivyo, Ninawahimiza watu wengi wajinga ambao hawana umaizi au busara yoyote: Msimjaribu Mungu, na msipinge tena. Tayari Mungu amepitia mateso yote ambayo mwanadamu hajawahi kustahimili, na kitambo alistahimili udhalilishaji zaidi kwa niaba ya mwanadamu. Basi, kuna kitu gani ambacho hamwezi kuachilia? Ni nini kinachoweza kuwa muhimu zaidi kuliko nia ya Mungu? Ni nini kinachoweza kuwa juu zaidi kuliko upendo wa Mungu? Tayari ni vigumu vya kutosha kwa Mungu kutekeleza kazi Yake katika nchi hii chafu; ikiwa, zaidi ya hayo, mwanadamu anafanya makosa kwa kujua na kwa makusudi, kazi ya Mungu itabidi ichukue muda mrefu zaidi. Kwa ufupi, hili halinufaishi maslahi ya mtu yeyote, halimfaidi mtu yeyote. Mungu hawekewi mipaka na wakati; kazi Yake na utukufu Wake huja kwanza. Kwa hivyo, maadamu kitu fulani ni sehemu ya kazi Yake, Yeye atalipa gharama yoyote kwa ajili ya kitu hicho, haijalishi itachukua muda gani. Hii ndiyo tabia ya Mungu: Hatapumzika hadi kazi Yake ikamilike. Kazi Yake itaisha tu wakati Anapopata sehemu ya pili ya utukufu Wake. Ikiwa, katika ulimwengu mzima, Mungu hatamaliza sehemu ya pili ya kazi Yake ya kupata utukufu, siku Yake haitakuja kamwe, mkono Wake hautawaacha kamwe watu Wake wateule, utukufu Wake hautashuka juu ya Israeli kamwe, na mpango Wake hautahitimishwa kamwe. Mnapaswa kuweza kuona nia ya Mungu, na mnapaswa kuona kwamba kazi ya Mungu si rahisi kama uumbaji wa mbingu na ardhi na vitu vyote. Hiyo ni kwa sababu kazi ya leo ni mabadiliko ya wale ambao wamepotoshwa, ambao wamekufa ganzi kwa kiwango cha juu kabisa, ni kuwatakasa wale walioumbwa lakini wakasimamiwa na Shetani. Si uumbaji wa Adamu au Hawa, sembuse uumbaji wa nuru, au uumbaji wa kila mmea na mnyama. Mungu anavitakasa vitu ambavyo vimepotoshwa na Shetani na kisha kuvipata upya, na kuvifanya viwe vitu ambavyo ni Vyake, na kuwa utukufu Wake. Hili si rahisi kama uumbaji wa mbingu na ardhi na vitu vyote, kama anavyofikiria mwanadamu, na wala si kama kazi ya kumlaani Shetani atupwe katika shimo lisilo na mwisho, kama mwanadamu anavyofikiria; badala yake, ni kazi ya kumbadilisha mwanadamu, kugeuza vitu ambavyo ni hasi, na visivyo Vyake, kuwa vitu ambavyo ni chanya, na ambavyo ni Vyake. Huu ndio ukweli halisi kuhusu hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima mwelewe hili, na mwepuke kurahisisha mambo kupita kiasi. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi yoyote ya kawaida. Kustaajabisha na hekima ya kazi hii vinazidi mawazo ya mwanadamu. Mungu haumbi vitu vyote wakati wa hatua hii ya kazi, na wala Haviharibu. Badala yake, Yeye anavibadilisha vitu vyote Alivyoviumba, na kuvitakasa vitu vyote ambavyo vimetiwa najisi na Shetani. Na hivyo ndivyo Mungu anaanza shughuli kuu. Huu ndio umuhimu wote wa kazi ya Mungu. Je, unaona katika maneno haya kwamba kazi ya Mungu kweli ni rahisi kiasi hicho?

Iliyotangulia: Maarifa ya Kazi ya Mungu ya Wakati wa Sasa

Inayofuata: Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli Kwa Kuwa Unamwamini Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp