Maarifa ya Kazi ya Mungu ya Wakati wa Sasa

Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi ni, kwa sehemu kubwa, kujua huduma kuu ya Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho ni nini, na kile Amekuja kufanya duniani. Nimetaja hapo awali katika maneno Yangu kwamba Mungu amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) kuweka mfano bora kabla ya kuondoka. Mungu anawekaje mfano huu bora? Anafanya hivyo kwa kunena maneno, na kwa kufanya kazi na kunena kote nchini. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Yeye hunena tu, ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, na ili kila mtu akimiwe na kutiwa nuru na maneno Yake, na hivyo kuelewa wazi ndani ya roho yake na kupata uwazi kuhusu maono. Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili na kuja duniani kimsingi ili kunena maneno. Yesu alipokuja, Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, na Alikamilisha kazi ya ukombozi ya kusulubiwa. Ametamatisha Enzi ya Sheria na kukomesha yote yaliyokuwa ya zamani. Kuwasili kwa Yesu kulitamatisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema; kuwasili kwa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kumetamatisha Enzi ya Neema. Amekuja kimsingi kunena maneno Yake—Akitumia maneno kumfanya mwanadamu kuwa timilifu, kumwangazia na kumtia nuru mwanadamu—na hivyo kuondoa nafasi ya Mungu asiye yakini ndani ya moyo wa mwanadamu. Yesu alipokuja, Hakufanya hatua hii ya kazi. Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kufukuza pepo, na Alifanya kazi ya ukombozi ya kusulubiwa. Kama matokeo, katika dhana za watu, wanaamini kwamba hivi ndivyo Mungu anapaswa kuwa. Kwa maana Yesu alipokuja, Hakufanya kazi ya kuondoa mfano wa Mungu asiye yakini kutoka moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubiwa, Aliponya wagonjwa na kufukuza pepo, na Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, kupata mwili kwa Mungu wakati wa siku za mwisho kunaondoa nafasi inayoshikiliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili kusiwe tena na mfano wa Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu. Kupitia maneno na kazi Yake ya vitendo, ziara Zake katika maeneo tofauti, na kazi bora sana ya vitendo na ya kawaida Anayofanya miongoni mwa wanadamu, Anamfanya mwanadamu ajue uhakika wa Mungu, na kuondoa nafasi ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu. Kwa upande mwingine, Mungu anatumia maneno yaliyonenwa na mwili Wake kumfanya mwanadamu kuwa kamili, na kutimiza mambo yote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu atatimiza wakati wa siku za mwisho.

Kile mnachopaswa kujua:

1. Kazi ya Mungu si ya kimiujiza, na hampaswi kuwa na dhana kuihusu.

2. Lazima muelewe kazi kuu ambayo Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya wakati huu.

Hakuja kuponya wagonjwa, au kufukuza pepo, au kufanya miujiza, na Hakuja kuhubiri injili ya toba, au kumpa mwanadamu ukombozi. Hiyo ni kwa sababu Yesu tayari Amefanya kazi hii, na Mungu harudii kazi ile ile. Leo, Mungu amekuja kutamatisha Enzi ya Neema na kukomesha desturi zote za Enzi ya Neema. Mungu wa vitendo Amekuja kimsingi kufichua uhakika Wake. Yesu alipokuja, Hakunena sana; kimsingi Alionyesha miujiza, alifanya ishara na maajabu, na aliponya wagonjwa na kuondosha pepo, kama sivyo Alinena unabii, yote ili kuwafanya watu wamwamini kwa msimamo thabiti na kuona kwamba kwa kweli Alikuwa Mungu na Hakuwa na hisia za kimwili. Hatimaye, Alikamilisha kazi ya kusulubiwa. Mungu wa leo haonyeshi ishara na maajabu, wala Haponyi wagonjwa na kufukuza pepo. Yesu alipokuja, kazi Aliyofanya iliwakilisha sehemu moja ya Mungu, lakini wakati huu Mungu amekuja kufanya hatua ya kazi ambayo inapaswa kukamilishwa. Mungu harudii kazi ile ile, Yeye ni Mungu ambaye daima ni mpya na si wa zamani kamwe, na hivyo yote unayoona leo ni maneno na kazi ya Mungu wa vitendo.

Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili kimsingi ili kunena maneno Yake, kueleza yote ambayo ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu, kuonyesha kile ambacho mwanadamu anapaswa kukiingia, kumwonyesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonyesha mwanadamu hekima, uweza, na maajabu ya Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu hunena, mwanadamu huona uwezo wa juu kabisa wa Mungu, ukuu wa Mungu, na, hata zaidi, unyenyekevu na kufichika kwa Mungu. Mwanadamu huona kwamba Mungu ni mwenye uwezo wa juu kabisa , lakini kwamba Yeye ni mnyenyekevu na aliyefichika, na Anaweza kuwa mdogo zaidi ya wote. Baadhi ya maneno Yake yananenwa moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa Roho, baadhi moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa mwanadamu, na baadhi kutoka katika mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili, inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana sana, na ni kupitia maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona. Kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho ni ya kawaida na ya vitendo, na hivyo kundi la watu katika siku za mwisho limewekwa katika majaribu makuu zaidi ya yote. Kwa sababu ya ukawaida na uhakika wa Mungu, watu wote wameingia katikati ya majaribu; kwamba mwanadamu kujishusha katika majaribu ya Mungu ni kwa sababu ya ukawaida na uhakika wa Mungu. Wakati wa enzi ya Yesu, hakukuwa na dhana au majaribu. Kwa sababu kazi nyingi iliyofanywa na Yesu iliambatana na dhana za mwanadamu, watu walimfuata, na hawakuwa na dhana kumhusu Yeye. Majaribu ya leo ni makuu zaidi kuwahi kukabiliwa na mwanadamu, na inaposemwa kwamba watu hawa wametoka katika dhiki kuu, hii ndiyo dhiki inayorejelewa. Leo, Mungu ananena ili kujenga imani, upendo, kukubali mateso, na utii katika watu hawa. Maneno yaliyonenwa na Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho yananenwa kulingana na kiini cha asili cha mwanadamu, mwenendo na udhihirisho wa mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kukiingia wakati wa sasa. Maneno Yake ni ya vitendo na ya kawaida: Haneni kuhusu kesho, wala Hatazami nyuma kwa yaliyopita; Ananena tu kuhusu kile kinachopaswa kuingiwa, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Ikiwa, katika wakati wa sasa, kutatokea mtu ambaye anaweza kuonyesha ishara na maajabu, kukemea mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na ikiwa mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi huu utakuwa uigaji wa roho mwovu, kitakuwa kitendo cha roho mwovu kumwiga Yesu. Kumbukeni hili! Mungu harudii kazi ileile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekamilika, na Mungu hatawahi tena kuitekeleza hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu hailingani na fikira za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri kuja kwa Masihi, na ikawa kwamba ni Yesu ndiye aliyekuja. Kwa hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja. Yesu tayari amekuja mara moja, na itakuwa makosa ikiwa “Yesu” atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina lina sifa bainifu ya enzi hiyo. Katika fikira za mwanadamu, Mungu lazima kila mara aonyeshe ishara na maajabu, lazima kila mara aponye wagonjwa na kufukuza mapepo, na lazima kila mara awe kama Yesu. Hata hivyo wakati huu, Mungu hayuko hivyo hata kidogo. Ikiwa, katika siku za mwisho, Mungu bado angeonyesha ishara na maajabu, na bado angekemea mapepo na angeponya wagonjwa—ikiwa Angefanya sawa kabisa na Yesu—basi Mungu angekuwa anarudia kazi ileile, na kazi ya Yesu haingekuwa na umuhimu au thamani yoyote. Hivyo, Mungu hutekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Punde tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, roho waovu mara moja hujaribu kuiiga, na baada ya Shetani kuanza kumfuata Mungu unyounyo, Mungu hubadilisha na kutumia mbinu tofauti. Punde tu Mungu anapokamilisha hatua ya kazi Yake, roho waovu hujaribu kuiiga. Ninyi mnapaswa kuelewa hili. Kwa nini kazi ya Mungu leo ni tofauti na kazi ya Yesu? Kwa nini Mungu leo hafanyi ishara na maajabu, hafukuzi mapepo, na haponyi wagonjwa? Kama kazi ya Yesu ingekuwa sawa na kazi iliyofanywa wakati wa Enzi ya Sheria, je, Angeweza kumwakilisha Mungu wa Enzi ya Neema? Je, Angeweza kukamilisha kazi ya kusulubiwa? Kama Yesu angeshiriki katika mfumo wa hekalu na kutunza Sabato kama katika Enzi ya Sheria, bila kuteswa na yeyote na kukubaliwa na wote, je, Angeweza kusulubiwa? Je, Angeweza kukamilisha kazi ya ukombozi? Kungekuwa na maana gani ikiwa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho angefanya ishara na maajabu, kama Yesu alivyofanya? Ni tu ikiwa Mungu anafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, ile inayowakilisha sehemu ya mpango Wake wa usimamizi, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina zaidi kumhusu Mungu, na mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilishwa.

Wakati wa siku za mwisho, Mungu amekuja kimsingi kunena maneno Yake. Ananena kutoka katika mtazamo wa Roho, kutoka katika mtazamo wa mwanadamu, na kutoka katika mtazamo wa nafsi ya tatu; Ananena kwa njia tofauti tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi cha muda, na Anatumia njia hizi za kunena kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa mfano wa Mungu asiye yakini kutoka moyoni mwa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu inayofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu anapokuja Ataponya wagonjwa, atafukuza mapepo, atafanya miujiza, na atamjalia mwanadamu baraka za kimwili, Mungu anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuondoa mambo kama hayo katika dhana za mwanadamu, kumruhusu mwanadamu ajue uhakika na ukawaida wa Mungu, na kuondoa mfano wa Yesu kama ulivyo moyoni mwa mwanadamu, na badala yake kuruhusu mfano mpya wa Mungu kuchukua nafasi moyoni mwa mwanadamu. Punde tu mfano wa Mungu ndani ya mwanadamu unapokuwa wa zamani, basi unakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hiyo ya kazi, Hakuwakilisha ukamilifu wa Mungu. Alifanya ishara na maajabu kadhaa, alinena maneno kadhaa, na hatimaye alisulubiwa. Aliwakilisha sehemu moja ya Mungu. Hakuweza kuwakilisha yote yaliyo ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya sehemu moja ya kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu sana, na wa ajabu sana, na Yeye hawezi kueleweka, na kwa sababu Mungu hutekeleza sehemu moja tu ya kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu wakati wa enzi hii kimsingi ni utoaji wa maneno ya uzima kwa mwanadamu; ufichuzi wa kiini cha asili cha mwanadamu na tabia yake potovu; na uondoshaji wa dhana zake za kidini, mawazo ya kikabaila, mawazo, na maarifa na utamaduni uliopitwa na wakati. Mambo haya yote lazima yatakaswe kupitia kufichuliwa na maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anatumia maneno, sio ishara na maajabu, kumfanya mwanadamu kuwa timilifu. Anatumia maneno Yake kumfichua mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumfanya mwanadamu kuwa timilifu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na kupendeza kwa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, na ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Alinena maneno kadhaa kwa Waisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu ilifichuliwa, lakini kwa sababu ubora wa tabia wa mwanadamu ulikuwa na ukomo na hakuna kitu ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kuwa kamili, Mungu aliendelea kunena na kufanya kazi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu kwa mara nyingine tena aliona sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, na kusulubiwa, siku tatu baada ya hapo Alifufuliwa na kuonekana katika mwili mbele ya mwanadamu. Kuhusu Mungu, mwanadamu hakujua zaidi ya haya. Mwanadamu anajua kiasi kile tu anachodhihirishiwa na Mungu, na kama Mungu hangeendelea kumdhihirishia mwanadamu jambo lolote, basi hicho ndicho kingekuwa kiwango cha mipaka ambayo mwanadamu anamwekea Mungu. Hivyo, Mungu anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu kumhusu Yeye yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili mwanadamu aweze kuja kujua kiini cha Mungu hatua kwa hatua. Katika siku za mwisho, Mungu anatumia maneno Yake kumfanya mwanadamu kuwa timilifu. Tabia yako potovu inafichuliwa na maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinabadilishwa na uhakika wa Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili kimsingi ili kutimiza maneno "Neno linakuwa mwili, Neno linakuja katika mwili, na Neno linaonekana katika mwili," na kama hamna maarifa kamili wa hili, basi hamtaweza kusimama imara. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kimsingi anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno linaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya kazi ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Hivyo, maarifa yenu lazima yawe kamili; bila kujali jinsi Mungu anavyofanya kazi, Mungu hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Kama Mungu hangefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu kumhusu Yeye hayangeweza kuendelea zaidi. Ungejua tu kwamba Mungu anaweza kusulubiwa na anaweza kuangamiza Sodoma, na kwamba Yesu anaweza kufufuka kutoka kwa wafu na kumtokea Petro…. Lakini hungesema kamwe kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa kupitia maneno ya Mungu tu ndipo unaweza kuzungumzia maarifa kama hayo. Kadiri unavyozidi kupitia kazi ya Mungu, ndivyo maarifa yako kumhusu Yeye yatakavyozidi kuwa kamili, na ni hapo tu ndipo hutamwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako mwenyewe. Mwanadamu huja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake; hakuna njia nyingine sahihi ya kumjua Mungu. Leo, kuna watu wengi ambao hawafanyi chochote isipokuwa kungoja kuona ishara na maajabu na wakati wa maafa makubwa. Je, unamwamini Mungu, au unaamini katika maafa makubwa? Wakati maafa makubwa yatakapowasili itakuwa kuchelewa mno, na kama Mungu hataleta maafa makubwa, je, Yeye basi si Mungu? Je, unaamini katika ishara na maajabu, au unamwamini Mungu Mwenyewe? Yesu hakuonyesha ishara na maajabu Alipodhihakiwa na wengine, lakini je, Yeye Hakuwa Mungu? Je, unaamini katika ishara na maajabu, au unaamini katika kiini cha Mungu? Maoni ya mwanadamu kuhusu imani kwa Mungu si sahihi! Yehova alinena maneno mengi wakati wa Enzi ya Sheria, lakini hata leo baadhi yake bado hayajatimizwa. Je, unaweza kusema kwamba Yehova si Mungu?

Leo, inapaswa kuwa wazi kwenu nyote kwamba, katika siku za mwisho, kimsingi ni ukweli wa "Neno linakuwa mwili" ambao unatimizwa na Mungu. Kupitia kazi Yake ya vitendo duniani, Anamruhusu mwanadamu kumjua na kuhusiana Naye, na kuona matendo Yake ya vitendo. Anamruhusu mwanadamu kuona wazi kwamba Anaweza kufanya ishara na maajabu na kwamba pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo; hii inategemea enzi. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu si kuwa hawezi kufanya ishara na maajabu, bali badala yake anabadilisha njia Yake ya kufanya kazi kulingana na kazi inayopaswa kufanywa na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Hafanyi ishara na maajabu; Alifanya ishara na maajabu kadhaa katika enzi ya Yesu kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti. Mungu hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini kuwa Yeye kutoweza kufanya ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kwa kuwa Hafanyi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Je, huo si uwongo? Mungu anaweza kufanya ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, hivyo hafanyi kazi ileile. Katika enzi tofauti na kulingana na hatua tofauti za kazi Yake, Mungu hudhihirisha matendo tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu si imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali imani katika kazi Yake ya vitendo wakati wa enzi mpya. Mwanadamu huja kumjua Mungu kupitia namna ambayo Mungu anafanya kazi, na maarifa haya huzalisha ndani ya mwanadamu imani kwa Mungu, ambayo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu. Katika hatua hii ya kazi, Mungu hunena kwa kiasi kikubwa. Usingoje kuona ishara na maajabu; hutaona yoyote! Hii ni kwa sababu hukuzaliwa wakati wa Enzi ya Neema. Kama ungezaliwa wakati huo, ungeweza kuona ishara na maajabu, lakini ulizaliwa wakati wa siku za mwisho, na hivyo unaweza kuona tu uhakika na ukawaida wa Mungu. Usitarajie kumwona Yesu wa kimiujiza wakati wa siku za mwisho. Unaweza tu kumwona Mungu wa vitendo mwenye mwili, ambaye hana tofauti na mwanadamu yeyote wa kawaida. Katika kila enzi, Mungu hudhihirisha matendo tofauti. Katika kila enzi, Yeye hudhihirisha sehemu ya matendo Yake, na kazi ya kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu, na sehemu moja ya matendo ya Mungu. Matendo Anayodhihirisha yanatofautiana katika kila enzi ambayo Anafanya kazi, lakini yote yanaruhusu maarifa ya mwanadamu kumhusu Mungu kuwa ya kina zaidi, na kumruhusu mwanadamu kuwa na imani ya kweli na thabiti zaidi kwa Mungu. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo yote ya Mungu, kwa sababu Mungu ni wa ajabu sana, mkuu sana, na mweza yote, na kwa sababu Yeye hawezi kueleweka—hii ndiyo maana mwanadamu anamwamini Mungu. Kama unamwamini Mungu kwa sababu Anaweza kufanya ishara na maajabu na Anaweza kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, basi mtazamo wako si sahihi, na watu wengine watakuambia, "Je, roho waovu pia hawawezi kufanya mambo kama hayo?" Je, huku si kuchanganya mfano wa Mungu na mfano wa Shetani? Leo, imani ya mwanadamu kwa Mungu ni kwa sababu ya matendo Yake mengi na kiasi kikubwa cha kazi Anayofanya na njia nyingi ambazo kwazo Ananena. Mungu anamshinda mwanadamu na kumfanya kuwa timilifu kupitia maneno Yake. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo Yake mengi, si kwa sababu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu; watu wanapata kumjua Mungu tu kwa kushuhudia matendo Yake. Ni kwa kujua tu matendo ya vitendo ya Mungu, jinsi Anavyofanya kazi, ni mbinu gani za hekima Anazotumia, jinsi Anavyonena, na jinsi Anavyomfanya mwanadamu kuwa timilifu—ni kwa kujua tu vipengele hivi—ndipo unaweza kufahamu uhakika wa Mungu na kuelewa tabia Yake, ukijua kile Anachopenda, kile Anachochukia, na jinsi Anavyofanya kazi juu ya mwanadamu. Kwa kuelewa kile Mungu anachopenda na kile Anachochukia, unaweza kutofautisha kati ya kile ambacho ni chanya na hasi, na kupitia maarifa yako kumhusu Mungu kuna maendeleo katika maisha yako. Kwa ufupi, lazima upate maarifa ya kazi ya Mungu, na lazima urekebishe maoni yako kuhusu kumwamini Mungu.

Iliyotangulia: Unapaswa Kujua Kwamba Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Inayofuata: Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Mwanadamu Anavyofikiria?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp