795 Uhuru Hupatwa kwa Kujua Amri ya Mungu

1 Kwa hivyo kama watu hawawezi kutambua hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote ya binadamu, kama hawawezi kunyenyekea kwa kweli chini ya utawala wa Muumba, basi itakuwa vigumu sana kwao kutoendeshwa na kutiwa pingu za miguu na, fikira hii kwamba “hatima ya mtu imo kwenye mikono ya mtu,” itakuwa vigumu kwao kutupilia mbali maumivu ya kung’ang’ana kwao kwingi dhidi ya hatima na mamlaka ya Muumba, ni wazi kwamba hali hii pia itakuwa ngumu kwao katika kuweza kukombolewa kwa kweli na kuwa huru, kuwa watu wanaoabudu Mungu.

2 Kunayo njia rahisi zaidi ile ya kujifanya kuwa huru kutoka katika hali hii: kuaga kwaheri njia yako ya awali ya kuishi, kuaga kwaheri shabaha zako za maisha za awali, kuhitimisha na kuchambua hali ya maisha ya awali, mtazamo wa maisha, mambo uliyofuatilia, matamanio, na maadili, na kisha kuyalinganisha yote haya na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya binadamu, na kuona kama yoyote kati ya haya yanakubaliana na mapenzi na mahitaji ya Mungu, kujua kama yoyote kati ya haya yanakuletea maadili sahihi ya maisha, yanakuongoza katika ufahamu mwingi zaidi wa ukweli, na kuruhusu mtu kuishi kwa ubinadamu na mfano wa binadamu.

3 Unapochunguza mara kwa mara na kuchambua kwa makini shabaha mbalimbali za maisha ambazo watu hufuatilia na njia zao tofauti za kuishi, utapata kwamba hata hakuna moja kati ya hizo zote ambayo inaingiliana na nia ya Muumba wakati Alipoumba binadamu. Zote hizi zinawavuta watu mbali na ukuu na utunzwaji wa Muumba; zote ni mitego ambayo huwasababisha watu wawe wapotovu, na ambayo inawaelekeza jehanamu. Baada ya kutambua haya, kazi yako ni kuweka pembeni mtazamo wako wa maisha ya awali, kuwa mbali na mitego mbalimbali, kumwachia Mungu kuchukua usukani wa maisha yako na kukufanyia mipangilio, jaribu tu kunyenyekea katika mipango na mwongozo wa Mungu, kutokuwa na chaguo, na kuwa mtu anayemwabudu Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 794 Wale Wanaojua Amri ya Mungu Watatii Utawala Wake

Inayofuata: 796 Matokeo ya Kuielewa Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp