36. Kukombolewa Kutokana na Umaarufu na Utajiri

Na Xiao Min, Uchina

Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI).

Nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa mwaka mmoja uliopita. Nilijua agizo hili lilikuwa fadhila na kuinuliwa na Mungu. Niliamua kimya kimya kufuatilia ukweli kwa dhati na kufanya wajibu wangu vizuri. Baada ya hapo, nilijishughulisha sana na kazi ya kanisa, na nilipokumbana na shida, nilimtegemea Mungu na kumtazamia. Pia nilizijadili na wafanyakazi wenzangu na nikatafuta ukweli ili tuzitatue. Baada ya muda kidogo, kila kipengele cha kazi ya kanisa kilianza kuendelea, na nilimshukuru Mungu kwa ajili ya mwongozo Wake. Muda si muda, uchaguzi ulifanyika ili kumchagua kiongozi mwingine wa kanisa, na kwa mshangao wangu Dada Xi, ambaye alikuwa amefanya kazi na mimi miaka michache hapo nyuma, alichaguliwa. Dada Xia alikuwa kiongozi mpya zaidi na uzoefu wake wa maisha ulikuwa wa juujuu sana. Wakati tulifanya kazi pamoja hapo awali, nilihitaji kumsaidia kusuluhisha baadhi ya ugumu na masuala aliyokumbana nayo. Nilihisi kwamba wakati huu katika kazi yetu pamoja, ningekuwa mwenye uwezo zaidi kumliko yeye.

Wakati mmoja, nilirudi nyumbani nikapata ujumbe ambao Dada Xia alikuwa ameniachia, akisema kwamba kulikuwa na kiongozi wa kikundi katika Kanisa la Chengxi ambaye hakuweza kufanya kazi ya vitendo na ilibidi abadilishwe, na kwamba kulikuwa na masuala mengine ya vitendo yaliyohitaji suluhisho la haraka. Alinitaka niende kusaidia. Nikiwa nawaza kuhusu hili, nilihisi kuwa lazima awe anafikiria kwamba nilikuwa mwenye uwezo zaidi kumliko, na kwa vile aliniheshimu sana, ilibidi nifanye kazi nzuri na nisijiaibishe! Kadiri nilivyolifikiria zaidi, ndivyo nilivyofurahi zaidi. Nilipofika kwenye mkutano, niligundua kuwa Dada Xia alikuwa na ufahamu wa kina juu ya kazi hiyo, na kwamba ushirika wake juu ya ukweli ulikuwa wenye mpangilio na vitendo. Nilishangaa kuona kwamba alikuwa ameendelea kwa kiasi fulani katika miaka michache iliyopita. Nilidhani nilikuwa mwenye uwezo zaidi kumliko na ningehitaji kumpa mwongozo mwingi katika kazi, lakini ilionekana kama kwamba alikuwa mwenye uwezo sawa na mimi! Sikuridhika na hilo na ilinionekania kama kwamba alielekea kuchukua uongozi, kwa hivyo nilihisi kwamba ilinilazimu nimwonyeshe kila mtu uwezo wangu! Sikuthubutu kuzembea hata kidogo lakini nilipiga bongo zangu kufikiria jinsi ningeweza kufanya ushirika wangu uwe bora kuliko wake. Kwa sababu ya hilo, ushirika wangu uligeuka kuwa unaochosha sana, na hata mimi mwenywewe sikuufurahia. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nimepoteza sifa kuu na nilivunjika moyo sana.

Kuanzia wakati huo kuendelea, sikuweza kuacha kushindana na Dada Xia. Wakati mmoja katika mkutano alipogundua kuhusu hali za kina ndugu, alipata maneno husika ya Mungu, kisha akayafuma na uzoefu wake halisi katika ushirika wake, na nilimwona kila mtu akitikisa kichwa chake kwa kukubali huku akisikiliza. Wengine walikuwa wakinukuu, na wengine walisema, “Kuanzia sasa kuendelea tuna njia ya kufuata.” Nilihisi uvutiwaji na wivu kuhusu hili, na hivyo nilikuwa nikifikiria nini? “Sasa lazima niharakishe nishiriki ushirika fulani. Haijalishi chochote, siwezi kuonekana kama nisiyelingana na yeye.” Lakini kadiri nilivyozidi kufikiria hilo, ndivyo nilivyokosa zaidi kufikiria kitu chochote cha kufanya ushirika kuhusu. Nilianza kuwa na ubaguzi dhidi ya Dada Xia, nikiwaza, “Ni lazima ufanye ushirika sana hivyo? Tayari umesema yote yalipo ya kusema. Nimekaa hapa tu kama nisiye na maana—kama mapambo tu. Hili halikubaliki, lazima nishiriki ushirika kiasi ili nirejeshe sifa yangu kiasi tu.” Wakati tu alipopumzika kupata kopo la maji, nilisogeza kiti changu mbele na nikaanza kufanya ushirika. Nilitaka kushiriki kitu kizuri sana, lakini sikuonekana kugonga ndipo. Ushirika wangu ulikuwa umechanganyika tu. Nilipowaona ndugu wakinipa sura zisizoeleweka, niligundua kuwa nilikuwa nimekengeuka kabisa kutoka kwenye mada. Nilihisi mwenye wasiwasi sana na nilitamani nipate shimo nijifiche ndani. Nilikuwa nimejifanya nionekane mjinga sana. Nilitaka tu nionekane mzuri, lakini niliishia kuonekana mjinga. Nilijiweka jukwaani, na kila mtu aliniona nikishindwa. Moyoni mwangu, nilianza kumlaumu Mungu kwa kumpa dada yangu nuru, na kuniacha mimi, na nilikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi ambavyo kina ndugu wengine wangeniona kutoka wakati huo kuendelea. Kadiri nilivyozidi kufikiria hili, ndivyo nilivyokasirika zaidi. Nilitaka kuikimbia hali hiyo na sikutaka kufanya kazi na yeye tena. Nakumbuka wakati mmoja katika mkutano, akina dada kadhaa hawakuwa katika hali nzuri sana, na hakukuwa na kuboreka kokote baada ya ushirika wa Dada Xia. Mbali na kukosa kusaidia kufanya ushirika, pia niliwaza, “Sasa kila mtu ataona kwamba hawezi kutatua matatizo, kwa hivyo hawatamheshimu huku wakinidharau.” Kwa kipindi hicho cha muda, nilikuwa nikijaribu kushindana na Dada Xia kila mara, na hali yangu ya kiroho ilizidi kuwa yenye giza zaidi na zaidi. Sikuwa na nuru yoyote nilipokuwa nikifanya ushirika, na nilipowaona kina ndugu wakikabiliwa na shida au matatizo, sikujua jinsi ya kuyatatua. Nilianza kusinzia mapema sana kila usiku, na ilibidi nijilazimishe kufanya wajibu wangu. Mateso yangu yalizidi kuongezeka. Sikuweza kufanya chochote ila kumwomba Mungu na kumsihi Aniokoe.

Nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu katika ibada zangu siku moja: “Mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Watu wote hawataki kushindwa, bali daima wanataka kushindana—hata ingawa kushindana kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. ‘Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?’ Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi. Unamwomba Mungu na unahisi nafuu kwa muda, lakini punde unapokumbana na hali ya aina hii tena, huwezi kulishinda. Je, hii haionyeshi kimo kisicho komavu? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yaliifichua kabisa hali yangu na yakaingia moja kwa moja hadi moyoni mwangu. Nilitafakari kuhusu kwa nini nilikuwa nikiishi katika njia ngumu na yenye kuchosha sana. Kiini chake kilikuwa tamaa yangu ya umaarufu na hadhi, na kwamba tabia yangu ilikuwa ya kiburi sana. Nilikumbuka wakati ambapo nilikuwa nimeanza tu kutekeleza wajibu huu. Nilipokuwa na mafanikio kidogo katika kazi yangu na ndugu waliniheshimu, nilijivunia sana na kujiona kama mwenye talanta. Kufanya kazi na Dada Xia na kumwona akifanya vyema zaidi kuniliko, kulinifanya niwe na wivu, mwenye kusumbua, na nilikuwa nikishindana naye kila wakati. Wakati sikuweza kumpiku, nilikuwa hasi na nikalalamika, na hata nikaeleza hisia zangu katika wajibu wangu. Nilipoona kuwa hakuwa ametatua hali za kina dada hao, sikukataa tu kusaidia kufanya ushirika, lakini pia nilikataa kufanya chochote na nikafurahia kutofaulu kwake. Niliazimia kumwona akiaibika. Huko kulikuwaje kufanya wajibu wangu? Kama kiongozi kanisani, sikuwajibika kabisa na sikuifikiria kazi ya kanisa hata kidogo au kuhusu ikiwa shida za kina ndugu zilikuwa zimetatuliwa. Nilikuwa nikifikiria tu jinsi ya kumshinda. Nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau sana, na nilikuwa mjanja sana. Sifa na hadhi vilikuwa vimeivuruga akili yangu. Nilikuwa tayari kuona shida za akina ndugu zikikosa kutatuliwa, kuona kazi ya kanisa ikiathirika mradi niweze kulinda umaarufu na hadhi yangu. Je, sikuwa nikiuuma mkono unaonilisha? Sikustahili kabisa wajibu muhimu kama huo. Lilikuwa chukizo na karaha sana kwa Mungu! Nikiwa nawaza hivi, nilikuja mbele za Mungu mara moja kuomba na kutubu, nikimwomba Mungu anisaidie kutupilia mbali pingu za umaarufu.

Baadaye nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kusoma maneno haya kutoka kwa Mungu kuliuchangamsha moyo wangu mara moja, na kisha nilipata njia. Ikiwa nilitaka kuwekwa huru kutokana na pingu za sifa na hadhi, kwanza ilibidi niuweke moyo wangu uwe sawa. Ilibidi niyaweke mawazo yangu juu ya agizo la Mungu na nizingatie matakwa ya Mungu, na ilibidi nifikirie jinsi ambavyo ningeweza kufanya wajibu wangu vizuri. Mambo chanya yakiujaza moyo wangu zaidi, basi mambo hasi kama sifa, hadhi, ubatili na sifa kuu yatakuwa rahisi kuacha. Niligundua kuwa wengine kudhani kwamba mimi ni mtu wa maana haimaanishi kuwa Mungu ananikubali, na wengine kudhani kwamba mimi si kitu haimaanishi kuwa Mungu hataniokoa. Kilicho muhimu ni mtazamo wangu kwa Mungu, na ikiwa naweza kutenda ukweli na kufanya wajibu wangu vizuri. Nilimshukuru Mungu kwa kunipa nuru iliyonirudisha kutoka kwa ufuatiliaji wangu mbaya. Sikutaka kushindana na Dada Xia tena, lakini nilitaka tu kufanya wajibu wa kiumbe aliyeumbwa ili nimridhishe Mungu. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilimwomba Mungu kwa kufahamu moyoni na kuuweka moyo wangu katika wajibu wangu. na katika mikutano ya kanisa, nilisikiliza ushirika wa kina ndugu kwa makini. Nilipogundua masuala fulani, niliyatafakari kwa kwa uzito, kisha nikapata maneno husika ya Mungu na nikayaunganisha na uzoefu wangu mwenyewe kwa ajili ya ushirika. Pia nilijifunza kutoka kwa uwezo wa Dada Xia ili kufidia udhaifu wangu mwenyewe. Kutenda kwa njia hii kuliniacha nikihisi mtulivu na mwenye raha zaidi, na hali yangu iliboreka sana. Nilihisi mwenye shukrani sana kwa Mungu. Lakini tamaa ya sifa na hadhi ilikuwa imekita mizizi sana ndani yangu kwamba punde hali nzuri ilipoibuka, asili yangu ya kishetani ilijitokeza tena.

Nakumbuka kuna wakati mmoja nilikuwa karibu kushughulikia matatizo fulani katika kikundi, na nilipokuwa tu njiani nikienda, Dada Xia alisema kwamba masuala katika kikundi hicho yalikuwa magumu kwa namna fulani, na alitaka kuandamana nami. Kumsikia akisema hili kulikatiza furaha niliyokuwa nikihisi. Niliwaza, “Kwa hivyo ni wewe tu unayeweza kusuluhisha mambo? Je, wewe hujionyeshi tu?” Je, unamaanisha nini ukisema haya mbele ya mkubwa wetu? Si unajaribu kunifanya nionekane mbaya kimakusudi?” Nilikasirika sana wakati huo. Niliishia kwenda peke yangu, lakini sikuweza kusahau jinsi nilivyokasirika. Nilikuwa nikilalamika sana kumhusu Dada Xia wakati wote nikiwa njiani kuelekea huko kiasi kwamba sikuweza hata kupata mahali pa mkutano na ilibidi nirudi nilikotoka. Nilikuwa nimevunjika moyo sana. Niliwaza, “Mimi bure sana hivyo? Siwezi hata kupata mahali pa mikutano. Mkubwa wetu atafikiria nini kutuhusu? Nimejiabisha sana wakati huu!” Niliporudi na kuwaona hao kina dada wengine, sikutaka kuzungumza nao.

Siku iliyofuata, mimi na Dada Xia tulielekea kanisani kila mtu kivyake ili kutekeleza kazi kadhaa, na kwa mara nyingine tena nilivurugika kimuhemuko. Nilikuwa nikiwaza, “Sijali unafikiria una uwezo gani, acha tuone ni nani atakayefanya bora zaidi!” Nilifika kanisani nikiwa tayari kabisa na nikaanza kutekeleza kazi hiyo moja kwa moja, nikifanya ushirika na kugawa majukumu mara moja. Niliwaza, “Wakati huu nimeweka bidii kweli katika hili sana. Kwa kweli litazaa matunda, halafu nitaibuka mshindi mbele ya Dada Xia.” Katika mkutano wa wafanyakazi wenzetu baadaye, niligundua kuwa nilikuwa nimefanikisha kiwango kidogo zaidi katika wajibu wangu. Sikuwahi kufikiria kwamba hilo lingetokea. Nilipoteza tumaini lote kwa wakati huo na nilihisi kuwa haijalishi nilivyofanya kazi kwa bidii, singeweza kumshidna Dada Xia kamwe. Kwa kipindi hicho cha muda, kumwona mkubwa wetu akimjali Dada Xia kila aliporudi akiwa amechelewa, nilihisi kama niliyeachwa bila mtu wa kunijali. Nilimwonea wivu sana. Nilipomwona akifanya vizuri kuniliko katika kila kitu na kwamba mkubwa wetu alimthamini sana, nilihisi kama kwamba singewahi kupata siku yangu ya kusifiwa. Nilidhani kwamba kuwa kiongozi wa kikundi ingekuwa bora kuliko kuwa kiongozi wa kanisa. Angalau kina ndugu wangeniheshimu na kuniunga mkono. Nilihisi kwamba afadhali kuheshimiwa katika ngazi ya chini kuliko kutosifika katika ngazi ya juu. Malalamiko yangu yalizidi kutoka tu. Nilikuwa mpinzani kabisa kwa kuwa katika mazingira hayo na nilitazamia kutoka huko haraka iwezekanavyo. Hali yangu ilizidi kuzorota. Nilikuwa na wivu na nilimchukia Dada Xia, na nilihisi kama kwamba singeweza kujitokeza kwa sababu yake. Niliwaza pia, “Akifanya tu kosa katika wajibu wake na ahamishwe, hilo litakuwa jambo zuri.”

Kwa kuwa nilikuwa nikiishi katika hali hii ya kupigania umaarufu na masilahi ya kibinafsi, bila kujitafakari hata kidogo, Mungu alifundisha nidhamu kabla ya muda mrefu. Wakati mmoja, nilipanga kufanya mkutano na viongozi wengine wachache. Mbali na ukweli kwamba hakuna mtu yeyote alihudhuria, nikiwa njiani kurudi mguu uliisha pumzi, na muda si muda, nilipata maumivu makali mgongoni mwangu. Nikiwa naumwa na niliyevimba, maumivu yalikuwa magumu kuvumilia. Ilifikia hatua kwamba sikuweza hata kufanya wajibu wangu. Kisha nilikumbuka maneno ya Mungu: “Matakwa mnayohitaji kutimiza leo—kufanya kazi pamoja kwa upatanifu—ni sawa na huduma ambayo Yehova alitaka kutoka kwa Waisraeli: Vinginevyo, acheni tu kufanya huduma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu). Hili liliniogofya. Inawezekana kuwa Mungu alitaka kuninyang’anya nafasi ya kufanya wajibu wangu? Baadaye nilisoma kifungu kingine kutoka katika maneno ya Mungu: “Kadiri unavyong’ang’ana, ndivyo giza litakuzingira zaidi, na ndivyo utakavyohisi wivu na chuki, na hamu yako ya kupata itaongezeka na kuongezeka tu. Kadiri hamu yako ya kupata ilivyo kuu, ndivyo utakaavyopunguza kuweza kufanya hivyo, na unapopata kidogo chuki yako itaongezeka. Chuki yako inapoongezeka, utakuwa mbaya zaidi. Kadiri ulivyo mbaya ndani yako, ndivyo utakavyotekeleza wajibu wako vibaya zaidi; kadri unavyotekeleza wajibu wako vibaya, ndivyo utakuwa mwenye manufaa kigogo zaidi. Huu ni mzunguko mwovu uliofungamana. Ikiwa huwezi kamwe kutekeleza wajibu wako vizuri, basi, utaondolewa polepole(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno makali ya Mungu yaliniacha nikiwa mwenye woga na nikitetemeka. Nilihisi tabia ya Mungu ya haki isiyovumilia kosa lolote. Hasa niliposoma haya kutoka katika maneno ya Mungu, “Ikiwa huwezi kamwe kutekeleza wajibu wako vizuri, basi, utaondolewa polepole.” Kwa kweli nilihisi kwamba nilikuwa katika hatari iliyokuwa karibu. Muda mfupi baada ya hapo, nilimsikia Dada Xia akisema, “Kazi ya kanisa kweli inazorota katika kila njia….” Alijali sana kiasi kwamba alianza kulia. Kisha nilikumbuka mkubwa wetu akichambua kiini cha kushindwa kwetu kufanya kazi vizuri kwa pamoja, akisema kwamba kufanya hivyo kuliivuruga na kuihujumu kazi ya nyumba ya Mungu. Sikuthubutu kuendelea kufikiria juu ya hilo, lakini nilikimbia tu kuja mbele za Mungu katika sala na kutafuta. Nilijua vizuri kabisa kwamba kutafuta sifa na hadhi, na kuwaonea wengine wivu hakulingani na mapenzi ya Mungu, hivyo kwa nini sikuweza kujizuia kufuatilia hivyo vitu viovu?

Baadaye nilisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu. “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, nia zake husuda ni za kuchukiza? Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). Niliweza kupata kiini cha tatizo hilo katika ufunuo wa maneno ya Mungu. Sikuweza kamwe kujizuia kufuatilia umaarufu na hadhi kwa sababu nilikuwa nimeelimishwa shuleni na kushawishiwa na jamii tangu nilipokuwa mdogo. Falsafa za kishetani na uongo vilikuwa vimekita mizizi ndani kabisa ya moyo wangu, kama vile “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake,” “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake,” “Kunaweza kuwa tu na ndume alfa mmoja,” “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini,” na “Mtu huacha urithi nyuma yake kama vile bata bukini anavyoacha sauti yake.” Nilichukua vitu hivyo kama maneno ya kuishi kwa kufuata na nilikuwa nimeyaweka kama malengo ya maisha ya kufuatilia. Ikiwa ni huko nje ulimwenguni au katika nyumba ya Mungu, nilitafuta tu heshima kubwa kutoka kwa wengine. Nilitaka kuwa mbele na kuwa kivutio, popote nilipokuwa, ili nimfanye kila mtu aniangalie. Nilihisi hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya maana ya kuishi. Ubora wa tabia yangu haukuwa mzuri sana, na sikuwa mzuri kabisa katika kitu chochote, lakini sikuweza kuvumilia kuwa chini ya mtu mwingine. Wakati mtu alikuwa bora kuniliko, nilikasirika sana, na sikuweza kujizuia kutokana na kupambana na kushindana nao. Ningejaribu kufikiria kitu chochote ili nifaulu. Ikiwa sikuweza, nilikuwa na wivu na kuwachukia, na kumlaumu kila mtu isipokuwa mimi mwenyewe. Hiyo ilikuwa njia mbaya sana ya kuishi. Mwishowe niliona kuwa kufuatilia sifa na hadhi siyo njia sahihi kabisa, na kadiri nilivyozidi kufanya hivyo, ndivyo nilivyozidi kuwa mwenye kiburi na mwenye akili finyu. Nilikuwa mbinafsi na mwenye sumu zaidi kwa asili bila mfanano wowote wa sura ya binadamu. Kisha nikamtazama Dada Xia: Alifanya wajibu wake kwa uangalifu na kwa umakini, na ushirika wake ulikuwa na mwanga. Aliweza pia kutatua ugumu wa vitendo wa kina ndugu. Hilo lilikuwa jambo la kufaa kwa wengine na kwa kazi ya kanisa. Lilikuwa jambo la ajabu na kitu ambacho kiliweza kumfariji Mungu. Mimi, kwa upande mwingine, nilikuwa mwenye kufuatilia mambo madogo madogo na mwenye wivu, kila wakati nikidhani kwamba alikuwa akiniibia umaarufu, kwa hivyo nilikuwa mwenye chuki dhidi yake. Nilikuwa nikitazamia sana ashindwe na abadilishwe. Niliona jinsi nilivyokuwa mwovu! Mungu hutumainia kuwaona watu zaidi wakifuatilia ukweli na kuyadhukuru mapenzi Yake, na kuweza kufanya wajibu wao ili wamridhishe Yeye. Lakini katika juhudi yangu ya kulinda umaarufu na wadhifa wangu, sikuvumilia kina ndugu waliofanya hivyo. Nilikuwa mwenye wivu na asiye na uvumilivu kwao. Je, hiyo haikuwa kwenda kinyume na Mungu na kumpinga? Je, hiyo haikuwa kuvuruga kazi ya nyumba ya Mungu? Je, nilikuwaje tofauti na ibilisi, Shetani? Kuongezea, kuna wale viongozi wote wa Chama cha Kikomunisti ambao huunda vikundi na hujishughulisha na mambo madogo madogo kwa ajili ya umaarufu na cheo, na watafanya chochote ili kumwangusha mpinzani, wakiwaondoa kabisa maadui zao na kuwakandamiza watu. Huwezi kujua wametenda maovu mangapi, wamewaua watu wangapi! Mwishowe, wao hujiletea maangamizo, na wanapokufa wao huadhibiwa jahannamu. Basi ni kwa nini wao huishia kuwa hivyo? Sio kwa sababu wao huthamini umaarufu na cheo kuliko kila kitu? Kisha nikiangalia tabia yangu mwenyewe, hata ingawa haikuwa mbaya kama yao, kimsingi ilikuwa sawa na yao. Nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa na sheria za kishetani, na tabia niliyoifichua ilikuwa ya kiburi, ya ubinafsi, ya majivuno, ya kustahili dharau, ya ujanja na yenye uovu sana. Nilichoishi kwa kudhihirisha kilikuwa cha pepo, bila mfano wowote wa binadamu. Hilo lingekosaje kuwa chukizo na karaha kwa Mungu? Kufundishwa nidhamu kwa njia hiyo ilikuwa tabia ya haki ya Mungu ikinijia, na hata zaidi, ulikuwa wokovu Wake kwangu. Nilipogundua yote haya, nilikuja haraka mbele za Mungu kusali. Nilisema, “Ee Mungu, Sijakuwa nikifuatilia ukweli. Nimekuwa nikifuatilia sifa na hadhi tu. Nimepotoshwa na Shetani, siko kama mwanadamu hata kidogo. Nilipopoteza umaarufu na hadhi yangu, sikutaka kufanya wajibu wangu tena na nilikuwa karibu kukusaliti. Mungu, natamani kutubu Kwako. Niko tayari kufuatilia ukweli, kushirikiana na dada yangu, na kuwa thabiti katika wajibu wangu ili nikuridhishe.”

Baada ya hapo, nilimwambia Dada Xia kila kitu. Nilizichambua njia ambazo nilikuwa nikishindana naye kwa sababu ya sifa na faida. Nilimwomba pia anichunge na kunisaidia. Baada ya hapo, tuliweza kushirikiana katika wajibu wetu vizuri zaidi. Hata ingawa wakati mwingine bado mimi huonyesha tamaa ya sifa na faida, ninaweza kuona haraka kuwa ni tabia yangu ya kishetani inayojionesha, mimi hufikiria kuhusu asili na matokeo ya kuendelea namna hiyo, na kisha mimi hukimbia kumwomba Mungu na kuyatuliza mawazo yangu kwa kujali. Mimi huenda kusikiliza ushirika wa dada yangu kwa dhati na kujifunza kutoka kwa uwezo wake. Ninapoona kwamba amekosa kutaja kitu katika ushirika wake, mimi huingilia mara moja kumsaidia. Wakati huo, mimi hufikiria kuhusu jinsi ya kushiriki ukweli ili kila mtu aweze kufaidika nao. Kila mtu huhisi kwamba mikutano ya aina hiyo ni ya kuadilisha kweli na mimi hupata kitu kutoka kwayo, pia. Ninahisi huru na mtulivu ndani ya moyo wangu. Ni kama vile maneno ya Mungu yasemavyo: “Ikiwa unaweza kutimiza wajibu wako, kutenda faradhi na majukumu yako, kuweka kando tamaa zako binafsi, kuweka kando dhamira na nia zako mwenyewe, kufikiria nia ya Mungu na kuweka maslahi ya Mungu na nyumba Yake kwanza, basi baada ya kupitia hili kwa muda, utahisi kwamba hii ni njia nzuri ya kuishi: Ni kuishi kwa uhalisi na kwa uaminifu, bila kuwa mtu wa thamani ndogo au asiye na manufaa, na kuishi kwa haki na heshima badala ya kuwa na mawazo finyu au mchoyo. Utahisi kwamba hivi ndivyo mtu anapaswa kuishi na kutenda. Polepole, tamaa iliyo moyoni mwako ya kufurahisha maslahi yako mwenyewe itapungua. … Sasa nitashiriki na ninyi mkakati rahisi: Anzeni kwa kutenda kwa namna hii. Ukishafanya hivyo kwa muda, hali iliyo ndani yako itabadilika bila wewe kujua. Itabadilika kutoka kwa hali hiyo kinzani, ambayo huna hamu sana ya kumwamini Mungu wala kuchoshwa nayo, hadi katika hali ambayo unahisi kwamba kumwamini Mungu na kuwa mtu mwaminifu ni mambo mema, na ambayo unavutiwa nayo kwa kuwa wewe ni mwaminifu na kuhisi kwamba kuna maana na lishe katika kuishi kwa namna hii. Roho yako itakuwa na msingi, itakuwa na amani na yenye kuridhika. Utakuwa na hali kama hiyo, kama matokeo ya wewe kuachilia nia, masilahi, na tamaa zako za ubinafsi. Utakuwa umestahili kuwa nayo. Matokeo haya yana kipengele cha ushirikiano wa binadamu na pia kipengele cha kazi ya Roho Mtakatifu(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Iliyotangulia: 35. Siku za Kutafuta Umaarufu na Faida

Inayofuata: 39. Kuishi kwa Kudhihirisha Mfano wa Binadamu Mwishowe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

33. Pingu za Umaarufu na Faida

Na Jieli, UhispaniaMwenyezi Mungu anasema, “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp