104 Naishi Katika Uwepo wa Mungu

1 Mimi niko kimya mbele za Mungu kila siku, nikitafakari na kufikira neno Lake. Nikijichunguza, naona kwamba upotovu wangu mwingi bado upo mawazoni na katika usemi wangu. Mara nyingi mimi hujionyesha katika usemi na vitendo vyangu ili kuwafanya wengine waniheshimu. Mimi hutafuta daima kuwashinda wengine, mimi ni mwenye kujidai na mwenye kiburi, bila sura ya binadamu. Nikikabiliwa na hukumu na kufunuliwa na neno la Mungu, nahisi aibu sana. Naweza kuonekana kutenda vizuri, lakini tabia yangu haijabadilika. Sina uhalisi wowote na bado nina kiburi sana, Mungu amenichukia kwa muda mrefu. Nachukia kwamba nimepotoshwa kwa kina sana, na ninatamani kukubali hukumu ya Mungu.

2 Mimi niko kimya mbele za Mungu na natafuta mapenzi Yake katika mambo yote. Nazungumza na Mungu katika maneno Yake, naelewa ukweli na moyo wangu umeangazwa. Kushikilia dhana potovu ninapokutana na watu, matukio na vitu kunaonyesha kuwa sina uhalisi wowote. Mimi hulalamika kila wakati, nikitangaza kutokuwa na hatia na kujaribu kuileza, na mimi si mtiifu hata kidogo. Nielewapo ukweli, naona kwamba kazi ya Mungu ya kumsafisha mwanadamu ni halisi sana. Kadiri inavyokinzana na fikira zetu wenyewe, ndivyo kuna ukweli zaidi wa kutafutwa. Kupitia neno la Mungu na kuingia katika uhakika kweli ni kuwa ana kwa ana na Mungu. Bila mkanganyiko au kizuizi chochote, napitia upendo wa Mungu.

3 Naishi katika uwepo wa Mungu na nakubali uchunguzi Wake wakati wote. Moja baada ya nyingine, mawazo na vitendo vyangu vinakubali hukumu na utakaso wa neno la Mungu. Kwa kazi na mwongozo wa Roho Mtakatifu, moyo wangu una amani na ni mtulivu. Moyo wangu wamcha Mungu na Yeye anilinda; sitamkosea Mungu tena kamwe. Mara nyingi nikijituliza mbele za Mungu, moyo wangu humwogopa Mungu na kuepuka uovu. Natenda neno la Mungu na kutenda kulingana na ukweli, na nampenda na kumtii Mungu. Neno la Mungu laniongoza na naingia kwenye njia sahihi ya imani katika Mungu. Kwa kupata ukweli upotovu wangu unatakaswa, na ninamsifu Mungu moyoni mwangu.

Iliyotangulia: 103 Yasifu Maisha Mapya

Inayofuata: 105 Nina Furaha Sana Kuishi Mbele za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp