235 Kutubu na Kuanza Upya

1 Kwa nini sikuamka? Niliweka kila kitu katika kutafuta hadhi na sifa tu. Nililenga tu kazi na kuhubiri, lakini sikutenda au kupitia maneno ya Mungu. Kwa nini sikuamka? Nilijitahidi kupata tuzo tu. Nikijawa tamaa na matakwa badhirifu, nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili kudharauliwa sana. Maneno ya Mungu yaliniita mara nyingi sana, niliufanya moyo wangu mgumu na kujifanya sioni. Moyo wangu ulijaa tamaa za ubinafsi, ningewezaje kutambua kusihi kwa Mungu? Eh Mungu! Matendo yangu yamekuumiza sana. Nina aibu sana kuishi katika uwepo Wako, nikifurahia upendo Wako. Siwezi kuvumilia kutazama nyuma mambo ya zamani, yote yalikuwa uasi na ubaya wangu. Nilikuwa mwenye kiburi, mwenye kujigamba, mtukutu na mwenye pupa, niliacha tabia yangu ya kishetani itawale bure. Makosa yangu yanasumbua dhamiri yangu, mimi hulia katika kuungama kwangu, nawezaje kufidia muda wangu uliopotea?

2 Ni kupitia hukumu tu ndiyo niliweza kuona kwamba nilikuwa mnafiki. Mara nyingi sana niliapa mapenzi yasiyoisha, lakini sikuweza kustahimili jaribio la majaribu. Mara nyingi sana nilitubu na kusali, nikidai kuwa nimekuwa mtu mpya, lakini huo ulikuwa uwongo. Kupitia hukumu tu ndiyo niliona wazi kuwa bila kutenda ukweli, mwishowe ningefunuliwa. Kupitia shida nilitubu sana, nilikuja kuchukia upotovu wangu wa kina na kwamba sina ubinadamu. Naanguka mbele za Mungu, nimejaa majuto, nitajifanya upya kuuliwaza moyo wa Mungu. Eh Mungu! Matendo yangu yamekuumiza sana. Nina aibu sana kuishi katika uwepo Wako, nikifurahia upendo Wako; natamani tu kuweka moyo wangu katika kutekeleza wajibu wangu vizuri. Natamani kujiweka mikononi mwako, kutii mipangilio na sheria Yako. Nimeweka azimio langu kutenda ukweli, haijalishi njia ilivyopindika na kugeuka mbele, nimeazimia kukufuata mpaka mwisho!

Iliyotangulia: 234 Kuwa Mtu Mpya na Uuliwaze Moyo wa Mungu

Inayofuata: 236 Mwishowe Naishi Kwa Kudhihirisha Mfano wa Bibinadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp