Sura ya 19

Kazi ya Roho Mtakatifu inapoendelea mbele, Mungu kwa mara nyingine tena ametuingiza katika mbinu mpya ya kazi ya Roho Mtakatifu. Matokeo yake, haiepukiki kwamba baadhi ya watu wamenielewa Mimi vibaya na kufanya malalamiko Kwangu. Wengine wamenipinga na kunikataa Mimi, na wamenichunguza Mimi. Hata hivyo, bado Mimi ninasubiri kwa rehema toba yenu na mageuzi. Mabadiliko katika utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe kuonekana hadharani. Neno Langu litabaki bila kubadilika! Kwa kuwa ni wewe ninayemwokoa, Mimi sitakutelekeza katikati ya safari. Lakini kuna shaka ndani yenu na nyinyi mnataka kurejea mikono mitupu. Baadhi yenu mmeacha kusonga mbele ilhali wengine wanachunguza na kusubiri. Bado wengine wanashughulika na hali hiyo bila kufanya chochote, huku wengine wanafanya tu uigaji. Nyinyi kwa kweli mmeifanya mioyo yenu kuwa migumu! Mmekichukua nilichokisema Mimi kwenu na kukigeuza kuwa majisifu yenu na majivuno. Tafakarini hili zaidi: Haya ni maneno ya huruma na hukumu tu yanayowashukia. Roho Mtakatifu, anapoona kwamba ninyi kwa kweli ni waasi, moja kwa moja anaanza kunena na kuchambua. Lazima muwe na hofu. Msitende mambo kwa kutojali au kufanya lolote kwa pupa. Msiwe bure, wenye kiburi, au kusisitiza kuwa na njia zenu wenyewe! Inawapasa mzingatie zaidi juu ya kuweka neno Langu katika vitendo, na uishi kwa kuyadhihirisha kokote uendako ili yaweze kukubadilisha kwa kweli kutoka ndani na ili uweze kuwa na tabia Yangu. Ni matokeo kama haya tu ndiyo ya kweli.

Kwa minajili ya kanisa kuweza kujengwa, ni lazima uwe wa kimo fulani, na utafute kwa moyo wote na bila kukoma, pamoja na kupokea mchomo na utakaso wa Roho Mtakatifu na kuwa mtu aliyebadilishwa. Ni katika hali kama hiyo ambapo kanisa linaweza kujengwa. Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaongozwa nyinyi kuanzisha ujenzi wa kanisa. Kama mkiendelea kutenda mambo kwa njia ilele ya kuchanganyikiwa na uzima kama mlivyofanya zamani, basi hamna matumaini. Lazima mjitayarishe wenyewe na ukweli wote na kuwa na utambuzi wa kiroho, na kutembea njia iliyo kamili kulingana na hekima Yangu. Kwa kanisa kujengwa, ni lazima muwe katika maisha ya roho na siyo tu kuiga kwa juujuu. Maendeleo ya ukuaji katika maisha yenu ni maendeleo sawa na yale ambayo kwayo mmejengwa. Hata hivyo, kumbuka kwamba wale ambao hutegemea vipawa vya kiroho au wale ambao hawawezi kuelewa mambo ya kiroho ama wanakosa hali ya utendaji hawawezi kujengwa, wala wale ambao hawawezi kunikaribia na kuwasiliana na Mimi wakati wote. Wale ambao huyashughulisha mawazo yao na dhana za binadamu au kuishi kwa kufuata mafundisho ya kidini hawawezi kujengwa, na wale ambao huongozwa na hisia zao hawawezi pia. Bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, ni lazima ujiweke chini Yake kabisa. Vinginevyo, huwezi kujengwa. Wale ambao wanajishughulisha na majivuno, kujidai, kiburi, hali ya kuridhika na wanaopenda kuwashushia wengine hadhi na kuringa hawawezi kujengwa. Wale ambao hawawezi kuhudumu kwa uratibu na wengine hawawezi kujengwa. Wale wasio na utambuzi wa kiroho, au kwa upofu hufuata yeyote anayeongoza hawawezi kujengwa, na wale ambao hushindwa kuelewa nia Yangu na ambao huishi katika hali ya zamani hawawezi kujengwa. Wale ambao ni wapole mno kufuata mwanga mpya na hawana maono yoyote kama msingi hawawezi kujengwa.

Kanisa linapaswa kujengwa bila kuchelewa, na Mimi nina hangaiko la kusisitiza kwalo. Unapaswa kuanza kwa kuzingatia uhalisi, na kujiunga na mkondo wa ujenzi kwa kujitoa mwenyewe na nguvu yako yote. Vinginevyo, utakataliwa. Ni lazima ukitelekeze kabisa cha kutelekezwa, na kula na kunywa vizuri kistahilicho kuliwa na kunywewa. Ni lazima uishi kwa kudhihirisha uhalisi wa neno Langu, na hupaswi kuzingatia mambo ya juu juu na yasiyo na mpango. Jiulize, ni kiasi gani umechukua katika neno Langu? Ni kiasi kipi wewe huishi kwa kudhihirisha neno Langu? Ni lazima uwe macho na uache kufanya chochote kwa pupa. Vinginevyo, kitakudhuru tu, siyo kusaidia ukuaji wako mwenyewe katika maisha. Ni lazima uelewe ukweli, ujue jinsi ya kuuweka katika vitendo, na uruhusu neno Langu liwe maisha yako kwa ukweli. Huu ndio ukweli wa jambo!

Kwa kuwa ujenzi wa kanisa sasa umefikia wakati muhimu sana, Shetani anapanga mipango na kufanya juu chini kulibomoa. Hampaswi kuwa wavivu lakini endeleeni kwa uangalifu na mfanye utambuzi katika roho. Bila utambuzi kama huo, mtapatwa na hasara kubwa. Hili si jambo dogo. Ni lazima mlifikirie kama suala la umuhimu. Shetani ana uwezo wa kuonekana kwa uongo na kueneza mifano ambayo hubeba tofauti kubwa ya ubora wa yaliyomo. Watu hutenda mambo kipumbavu na kizembe, na wanakosa utambuzi, ambayo ina maana kwamba nyinyi hamuwezi kuwa macho na shwari wakati wote. Mioyo yenu haipatikani popote. Huduma ni heshima na kadhalika hasara. Inaweza kusababisha baraka au balaa. Salia mtulivu mbele Yangu na kuishi kwa mujibu wa neno Langu, na kwa hakika utasalia macho na kutumia utambuzi katika roho. Shetani atakapofika, utaweza kujikinga dhidi yake mara moja, na pia kuhisi kuja kwake; utahisi wasiwasi halisi katika roho yako. Kazi ya sasa ya Shetani hujizoeza kwa mabadiliko ya mielekeo. Watu wanapotenda mambo kwa njia ya kuchanganyikiwa na kukosa hadhari, wao hubaki katika utumwa. Lazima usalie macho wakati wote na kuwa waangalifu sana. Usilete ubishi juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara, au kukokotoa kwa ajili ya faida yako mwenyewe. Badala yake, tafuta mapenzi Yangu kufanyika.

Vitu vinaweza kuonekana kufanana lakini ubora wavyo unaweza kutofautiana. Hali kadhalika, nyinyi mnapaswa kutambua watu binafsi na vilevile roho. Lazima ufanye utambuzi na kudumisha kuwa macho kiroho. Sumu ya Shetani inapoonekana, unapaswa kuitambua mara moja; haiwezi kuepuka mwanga wa hukumu ya Mungu. Lazima uwe makini zaidi kwa kusikiliza kwa karibu sauti ya Roho Mtakatifu katika roho yako; usiwafuate wengine bila kufikiri au kukosea kilicho cha uongo kuwa kitu cha kweli. Usimfuate yeyote anayeongoza, ili usije ukapata hasara kubwa. Je, hilo linakufanya ujihisije? Je, mmeona matokeo yake? Hupaswi kwa nasibu kuingilia huduma au kuingiza maoni yako mwenyewe ndani yake, la sivyo Mimi nitakuangamiza. Lakini baya zaidi, kama wewe ukisalia muasi na kuendelea kusema na kufanya unavyotaka, Mimi nitakutenga! Kanisa halihitaji kulazimisha urafiki na watu zaidi; linawataka wale ambao kwa kweli wanampenda Mungu na kweli huishi kulingana na neno Langu. Unapaswa kuwa na ufahamu wa hali yako mwenyewe halisi. Je, si ni kujidanganya wakati maskini hujifikiria kuwa matajiri? Kwa kanisa kujengwa, lazima ufuate roho. Usiendelee kwa kutenda mambo kwa upofu, lakini kaa katika nafasi yako na kutimiza kazi yako mwenyewe. Hupaswi kupiga hatua nje ya majukumu yako, lakini timiza kazi zozote unazoweza kufanya kwa nguvu zako zote, halafu moyo Wangu utaridhishwa. Si kwamba nyote mtatenda huduma sawa. Badala yake, kila mmoja wenu lazima ufanye wajibu wako mwenyewe na kutoa huduma zenu kwa uratibu na wengine katika kanisa. Huduma zenu hazipaswi kuchepuka kwa upande wowote.

Iliyotangulia: Sura ya 18

Inayofuata: Sura ya 20

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp