Sura ya 20

Kazi ya Roho Mtakatifu huenda mbele kwa kasi, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yenu. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya moyo wako na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya. Kwa hakika wao watapata utukufu na heshima pamoja nami, na kushiriki baraka nzuri pamoja Nami. Sasa kuna baadhi za siri za dunia ya kiroho ambazo bado hamjaziona, kwa sababu macho zenu za kiroho hazijafunguliwa; vitu vyote bila shaka ni ya ajabu, na miujiza na maajabu, mambo ambayo watu kamwe hawajawahi waza kuyahusu, hatua kwa hatua yatakuja kuwa. Mwenyezi Mungu Ataonyesha miujiza Yake kubwa zaidi ili miisho ya ulimwengu na mataifa yote na watu wote waweze kuiona kwa macho yao yenyewe, na kuona ambako uadhama Wangu, haki na uweza ziko. Ile siku inakuja karibu! Sasa ni muda wa kipeo zaidi—je, mnajitoa au mnastahimili hadi mwisho na kamwe msirudi nyuma? Msiangalie kwa mtu yeyote, jambo au kitu, msiangalie kwa dunia, au waume wenu, watoto au kwa wasiwasi wenu kuhusu maisha, angalieni tu kwa upendo Wangu na rehema, oneni ni nini Nimelipia ili kuwapata nyinyi, ni nini Nilicho, na mambo haya yatatoa tumainisho la kutosha.

Wakati uko karibu sana na mapenzi Yangu lazima yatimizwe kwa haraka yote. Sitatelekeza wale kwa jina Langu lakini Nitawaleta nyote katika utukufu. Lakini inaweza kuonekana kuwa sasa ni muda muhimu. Iwapo mtu hataweza kuchukua hatua hio inayofuata basi wataomboleza kwa wenyewe maisha yao yote na kujuta wakati wamechelewa mno. Sasa vimo vyenu vimewekwa kwa mtihani wa vitendo, ili kuona kama kanisa linaweza kujengwa na iwapo mwaweza kutii kila mmoja au la. Kukitazamwa kutoka kipengele hiki, kutii kwako kwa kweli ni kutii ambako unachukua na kuchagua—ingawa unaweza kuwa na uwezo wa kutii mtu mmoja, unaweza kuona ni vigumu kumtii mtu mwingine. Kwa kweli hakuna njia ambayo unaweza kuwa mtiifu wakati unategemea dhana za kibinadamu. Hata hivyo mawazo ya Mungu kila mara hupita yale ya mtu! Kristo Alitii hadi kifo na Akafa msalabani. Kristo Hakusema lolote kuhusu hali yoyote au sababu, mradi ilikuwa mapenzi ya Baba Yake, Alitii bila kusita. Utii wako wa sasa ni mdogo mno. Ninawaambia nyinyi nyote, utiifu si kutii watu; badala yake, unamaanisha kutii kazi ya ndani ya Roho Mtakatifu na kumtii Mungu Mwenyewe. Maneno Yangu yanawafanya upya na kuwabadilisha kutoka ndani, vinginevyo nani angemtii nani? Nyinyi nyote ni waasi kwa wengine. Lazima mchukue wakati wa kuifahamu hii, kutii ni nini na jinsi mnaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kutii. Lazima mje mbele Yangu zaidi na mshiriki jambo hili, na polepole mtakuja kulielewa, na kwa hiyo kuachilia dhana na uchaguzi ndani yenu. Njia hii ambayo Mimi hufanya mambo ni ngumu kwa watu kuelewa kikamilifu. Sio jinsi watu ni wazuri au wana uwezo—Mimi hutumia wasiojua kabisa, wasio na thamani kabisa ili kufichua uweza wa Mungu na wakati huo Nikipindua dhana, maoni na uchaguzi wa watu wengine. Matendo ya Mungu ni ya ajabu mno, na yanapita makisio ya watu!

Kama kweli unataka kuwa mmoja anayenishuhudia Mimi, lazima upokee ukweli kabisa na si kwa kimakosa. Lazima uzingatie zaidi kwa kuyaweka maneno yangu katika vitendo, kutafuta kwa ajili ya maisha yako kukomaa haraka. Usiende ukitafuta mambo ambayo hayana thamani, siyo ya manufaa yoyote kwa uendeleaji wa maisha yenu. Unaweza tu kujengwa wakati maisha yako yamekomaa na ni hapo tu basi unaweza kuletwa katika ufalme—hii inapita shaka lolote. Bado Ninataka kunena zaidi sana kwako. Nimekupa mengi lakini ni kiasi kipi kweli unakielewa? Ni kiasi kipi cha kile Ninachosema kimekuwa hakika kwa maisha yako? Ni kiasi kipi cha kile Ninasema ambacho unaishi kwa kudhihirisha? Usifanye juhudi zisizoleta manufaa—hutapata lolote hatimaye, na utapata utupu tu. Wengine wamepata faida halisi kwa urahisi sana; Je wewe? Je, unaweza kumshinda Shetani kama huna silaha na hubebi silaha? Lazima uishi zaidi katika utegemezi wa maneno Yangu, na ni silaha bora kabisa kwa ulinzi binafsi. Unapaswa ufahamu: Usikuchukue maneno Yangu kama milki yako; kama huyajui, usiyatafute, usijaribu kuyafahamu au kushiriki nami lakini umeridhika kibinafsi na kujikinai, basi utapata hasara. Unapaswa kutumia somo sasa juu ya kipengele hiki, na ni lazima ujiweke kando na utumie nguvu za wenzio ili kufidia mapungufu yako mwenyewe; usifanye tu lolote unalotaka. Wakati hausubiri mtu yeyote. Maisha za ndugu na madada hukua siku kwa siku, wao hupitia mabadiliko na wote wanafanywa wapya siku kwa siku. Nguvu za ndugu na madada huinuka na hili ni jambo kubwa! Kimbia kwa kasi kwa mstari wa kumalizia, hakuna atakayekuwa na uwezo wa kumshughulikia mtu mwingine, fanya tu juhudi za kibinafsi kushirikiana na Mimi. Wale ambao wana maono, walio na njia mbele, ambao hawajavunjika moyo na ambao kila mara huangalia mbele wanahakikishiwa kuwa watashinda, bila shaka. Sasa ni muda muhimu. Kuwa na uhakika usivunjike moyo au kukataa tamaa. Ni lazima uangalie mbele katika kila kitu na usirudi nyuma, toa kila kitu na uachane na mitego yote na ufuatilie kwa nguvu zako zote. Mradi pumzi moja bado inasalia nawe, vumilia hadi mwisho kabisa; hii tu ndiyo inastahili sifa.

Iliyotangulia: Sura ya 19

Inayofuata: Sura ya 21

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp