Sura ya 90

Wote walio vipofu lazima waondoke kutoka Kwangu na wasiwepo kwa muda zaidi hata kidogo, kwani wale ambao Nataka ni wale ambao wanaweza kunijua, wanaoweza kuniona na wanaoweza kupata vitu vyote kutoka Kwangu. Na wanaoweza kweli kupata vitu vyote kutoka Kwangu ni nani? Hakika kuna wachache sana wa mtu wa aina hii na hakika watapata baraka Zangu. Nawapenda watu hawa na Nitawachukua mmoja baada ya mwingine kuwa wasaidizi Wangu wakuu, kuwa maonyesho Yangu, na Nitayafanya mataifa yote na watu wote wanisifu bila kukoma, wakishangilia bila kukoma kwa sababu ya watu hawa. Ee, Mlima Sayuni! Inua bango la ushindi na unishangilie! Kwa maana Mimi naenda ulimwenguni kote na hadi miisho ya dunia, Nikienda katika kila kona ya milima, mito na vitu vyote, kisha kurudi hapa tena. Narudi kwa ushindi na haki, hukumu, ghadhabu na kuchoma, na hata zaidi na wazaliwa Wangu wa kwanza. Mambo yote ambayo Nachukia kabisa na watu wote, masuala, na vitu ambavyo Mimi huchukia sana Natupa mbali sana. Mimi ni mshindi na Nimekamilisha yote ambayo Nataka kufanya. Nani anayethubutu kusema Sijakamilisha kazi Yangu? Nani anayethubutu kusema Sijawapata wazaliwa Wangu wa kwanza? Nani anayethubutu kusema kwamba Sijarudi kwa ushindi? Bila shaka wao ni aina ya Shetani, na ni wale wanaoona vigumu kupata msamaha Wangu. Wao ni vipofu, wao ni pepo wabaya na Ninawachukia zaidi. Katika vitu hivi Nitaanza kufichua ghadhabu yangu na ukamilifu wa hukumu Yangu, na, kwa njia ya moto Wangu unaowaka, kuwasha moto ulimwengu na dunia kutoka mwisho mmoja hadi mwingine, Nikipa nuru kila pembe—hii ni amri Yangu ya utawala.

Mara tu mnapoelewa maneno Yangu, mnapaswa kupata faraja kutoka kwayo; hampaswi kuyaacha yapite bila kuyasikiza. Matamshi ya hukumu yanakuja kila siku, kwa hiyo mbona ninyi ni wapumbavu na msiojali hivyo? Mbona hamshirikiani na Mimi? Je, mko tayari sana kwenda kuzimu? Nasema Mimi ni Mungu wa huruma kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu na watu Wangu, hivyo mnalielewaje hili? Hii si kauli rahisi, na inapaswa kueleweka kutoka kwa mtazamo mzuri. Ee, binadamu kipofu! Nimewaokoa mara nyingi, Nikiwaleta kutoka kwa mfumbato wa Shetani na kutoka kwa kuadibu ili muweze kupata ahadi Yangu, hivyo kwa nini msionyeshe huruma kwa moyo Wangu? Je, yeyote kati yenu anaweza kuokolewa kwa njia hii? Haki Yangu, uadhama na hukumu havionyeshi huruma kwa Shetani. Lakini kwa ajili yenu, vipo ili kuwaokoa, lakini ninyi hamwezi tu kuielewa tabia Yangu, wala hamjui kanuni za matendo Yangu. Mlifikiri kuwa Natenda bila kujua ukali wa vitendo Vyangu, au kujua malengo yao—wapumbavu mlioje! Naweza kuona wazi watu wote, matukio, na vitu. Naelewa kwa uwazi kamili kiini cha kila mtu, ambayo ni kusema, Nang’amua kabisa mambo ambayo mtu anaweka ndani yake mwenyewe. Naweza kuona wazi kama mtu ni Yezebeli au mzinzi, na Najua ni nani anayefanya nini kwa siri. Usikoge hirizi zako mbele Yangu—wewe fidhuli! Ondoka hapa sasa hivi! Ili kuepuka kuliletea aibu jina Langu, Simhitaji mtu wa aina hiyo! Hawezi kulishuhudia jina Langu, lakini badala yake anatenda kinyume na maendeleo na analeta aibu kwa familia Yangu! Atafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu mara moja. Simtaki yeye. Sitastahimili kuchelewa kwa hata sekunde moja! Kwa watu hao ni bure bila kujali jinsi wanavyotafuta, kwa maana katika ufalme Wangu wote ni watakatifu na wasio na dosari yoyote. Ikiwa ni pamoja na watu Wangu, Nikisema kuwa Simtaki mtu fulani basi Namaanisha hilo; usisubiri Nibadili mawazo Yangu. Sijali jinsi ulivyokuwa mzuri Kwangu awali!

Ninawafichulia siri kila siku. Je, mnajua njia Yangu ya kuzungumza? Ninafichua siri zangu kwa mujibu wa nini? Je, mnajua? Mara nyingi ninyi husema kuwa Mimi ni Mungu anayewapa kwa wakati unaofaa, kwa hivyo mnaelewa vipi vipengele hivi? Ninafichua mafumbo Yangu kwenu moja baada ya lingine kulingana na hatua za Kazi Yangu, na Ninawaruzuku kulingana na mpango Wangu, na hata zaidi kulingana na vimo vyenu vya kweli (kuruzuku kunatajwa kwa kurejelea kila mtu katika ufalme). Mbinu Yangu ya kuzungumza ni hivi: Kwa watu walio nyumbani Mwangu Nawapa faraja, Nawaruzuku na Ninawahukumu; kwa Shetani Sionyeshi huruma, na yote ni hasira na kuchomeka. Nitatumia amri Zangu za utawala ili kuwatoa nje ya nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine wale ambao Sijawaamulia kabla au kuwachagua. Hakuna haja ya kuhisi wasiwasi. Baada ya kuwafanya wafichue maumbo yao ya asili (baada ya wao kutoa huduma kwa wanangu mwishowe), watarudi kwenye shimo lisilo na mwisho, la sivyo Sitawahi kulipumzisha jambo hili na Sitaliacha kamwe. Mara nyingi watu hutaja kuzimu na jahanamu. Lakini maneno haya mawili yanarejelea nini, na tofauti kati yao ni ipi? Je, kweli yanarejelea pembe fulani ya baridi, ya giza? Akili ya binadamu daima inakatiza usimamizi Wangu, wakifikiria kwamba kutafakari kwao kusio na mpango maalumu ni kuzuri sana. Lakini haya yote ni mawazo yao wenyewe. Kuzimu na jahanamu zote zinarejelea hekalu la uchafu ambalo limeishiwa na Shetani awali au na roho wabaya. Hiyo ni kusema, yeyote ambaye amemilikiwa na Shetani au roho wabaya awali, ni wao ambao ni Kuzimu na wao ndio jahanamu—hakuna kosa kuhusu hilo! Hii ndiyo sababu Nimesisitiza kwa kurudia katika siku za nyuma kwamba Siishi katika hekalu la uchafu. Je, Mimi (Mungu Mwenyewe) Ninaweza kuishi Kuzimu, au jahanamu? Je, huo hauwezi kuwa upuuzi usio na maana? Nimesema hili mara kadhaa lakini ninyi bado hamwelewi Ninachomaanisha. Ikilinganishwa na jahanamu, Kuzimu imepotoshwa zaidi na Shetani. Wale ambao ni wa Kuzimu ndio walio katika hali mbaya sana, na Sijawaamulia kabla watu hawa kabisa; wale walio wa jahanamu ni wale Niliowaamulia kabla, lakini kisha wameondolewa. Kwa maneno rahisi, Sijamchagua hata mmoja wa watu hawa.

Watu mara nyingi hujionyesha kuwa wataalam katika kutoelewa maneno Yangu. Kama Singeonyesha wazi wazi na kufafanua mambo kidogo kidogo, nani kati yenu angeelewa? Ninyi mnaamini tu nusu hata ya maneno Ninayozungumza, sembuse mambo ambayo hayajatajwa hapo awali. Sasa, migogoro ya ndani imeanza ndani ya mataifa yote: Wafanyakazi wakibishana na viongozi, wanafunzi na walimu, wananchi na maofisa wa jeshi wa serikali, na shughuli zote kama hizi zinazosababisha vurugu kwanza zinaibuka katika kila taifa, na yote ni sehemu moja tu inayotoa huduma Kwangu. Na kwa nini Nasema inanitolea huduma? Je, Ninafurahia bahati mbaya ya watu? Je, Ninakaa bila kusikiza? Bila shaka hapana! Kwa maana huyu ni Shetani akishambulia katika maumivu makuu ya mwisho ya kifo, na kutoka kwa upande hasi, hii inafanya kazi kama foili[a] ya mamlaka Yangu na kama foili[a] ya matendo Yangu ya ajabu. Yote ni ushuhuda wa nguvu ambao unanishuhudia Mimi, na ni silaha ambayo inatumika kumshambulia Shetani. Wakati tu mataifa yote ya dunia yanapigania ardhi na ushawishi, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tunatawala kama wafalme pamoja na kuyashughulikia, na inazidi kabisa mawazo yao kwamba chini ya mazingira haya mabaya, ufalme Wangu unafanikishwa kabisa kati ya mwanadamu. Zaidi ya hayo, wanapong’ang’ania mamlaka na wanatamani kuwahukumu wengine, wengine huwahukumu na wao huteketezwa kwa ghadhabu Yangu—ya kusikitisha jinsi gani! Ya kusikitisha jinsi gani! Ufalme Wangu umefanikishwa miongoni mwa wanadamu—ni tukio la kupendeza kweli!

Kuwa mwanadamu (iwe ni watu wa ufalme Wangu au uzao wa Shetani), lazima nyote muone matendo Yangu ya ajabu, vinginevyo Sitalipumzisha jambo hili kamwe. Hata kama uko tayari kukubali hukumu Yangu, bado haitakubalika kama hujaona matendo Yangu ya ajabu. Watu wote lazima washawishike kwa moyo, kwa neno na kwa kuona, na hakuna mtu anayeweza kuruhusiwa kupenyeza tu. Watu wote lazima wanipe Mimi utukufu. Mwishowe, Nitalifanya hata joka kubwa jekundu liinuke na kunisifu kwa ajili ya ushindi Wangu. Hii ni amri Yangu ya utawala—je, utaikumbuka? Watu wote lazima wanisifu bila kukoma na kunipa utukufu!

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Sura ya 89

Inayofuata: Sura ya 91

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp