Sura ya 91

Roho Wangu huongea na kutamka sauti Yangu daima—wangapi kati yenu wanaweza kunijua Mimi? Kwa nini lazima Nipate mwili na kuja kati yenu? Hili ni fumbo kubwa. Ninyi mnanifikiria kuhusu Mimi na kunitamani sana siku nzima, na mnanisifu, kunifurahia na kunila na kuninywa kila siku, na ilhali leo bado hamnijui Mimi. Ninyi ni wajinga na vipofu kweli! Jinsi gani mnavyonijua kidogo! Ni wangapi kati yenu wanaweza kufikiria kuhusu mapenzi Yangu? Yaani, ni wangapi kati yenu wanaoweza kunijua? Ninyi nyote ni wenye hila, watu wenye nia mbovu, na ilhali bado mnataka kuyaridhisha mapenzi Yangu? Sahau kuhusu hilo! Ninakwambia, bila kujali jinsi vitendo vya Shetani vilivyo vyema, vyote vinafanyika kubomoa ujenzi Wangu na kukatiza usimamizi Wangu. Haijalishi jinsi anavyotenda vizuri, kiini chake hakibadiliki—kinanikana. Kwa hiyo, watu wengi bila kujua hupigwa chini na mkono Wangu na bila kujua wanaondolewa kutoka kwa familia Yangu. Leo, hakuna jambo hata moja (liwe ni kubwa au dogo) linapangwa na mwanadamu na yote yako mikononi Mwangu. Mtu yeyote akisema kuwa vitu vyote viko chini ya udhibiti wa mwanadamu basi Nakwambia kuwa wewe unanipinga, na Mimi hakika Nitakuadibu vikali na kukuacha bila mahali pa kupumzisha kichwa chako kamwe. Nini, kati ya kila kitu, hakijashikwa ndani ya mikono Yangu? Ni nini kisichopangwa na Mimi, au kuamuliwa na Mimi? Na bado unazungumza kuhusu kunijua Mimi! Huo ni uwongo ulio wazi. Umewadanganya wengine kwa hivyo unadhani unaweza kunidanganya Mimi pia? Unafikiri kwamba iwapo hakuna mtu anayejua kile ambacho umefanya, basi hakuna kitakachofanyika? Usifikiri kuwa utaponea kwa urahisi hivyo! Lazima Nikufanye upige magoti mbele Yangu na kuzungumza wazi. Haikubaliki kutozungumza; hii ni amri Yangu ya utawala!

Je, mnaelewa kwa kweli Roho Wangu ni nani, na mwanadamu Niliye ni nani? Ni nini umuhimu wa Mimi kupata mwili? Ni nani kati yenu ametafakari kwa makini jambo muhimu kama hili na amepokea ufunuo fulani kutoka Kwangu? Ninyi nyote mnajidanganya wenyewe! Kwa nini Nasema kuwa wewe ni mtoto wa joka kubwa jekundu? Leo Nakufichulia fumbo la kupata mwili Kwangu, fumbo ambalo mwanadamu hajakuwa na uwezo wa kufunua tangu kuumbwa kwa ulimwengu, ambalo limewaletea walengwa wengi wa chuki Yangu uharibifu. Na ni hivyo leo. Kwa sababu ya mwili Wangu, wengi ambao Nawapenda wamekamilishwa. Kwa nini hasa lazima Nipate mwili? Na kwa nini Nina umbo Langu la sasa (vitu vyote kama urefu Wangu, sura Yangu na kimo Changu nk)? Nani anayeweza kusema jambo moja kuhusu hilo? Kuna umuhimu mkubwa sana kwa kupata mwili Kwangu kiasi kwamba hauwezi kusemwa wote kabisa. Nitawaambia sasa sehemu yake tu (kwa kuwa hatua za kazi Yangu zimefika umbali huu, hivyo ni lazima Nifanye hivi na kusema hivi): Kupata mwili Kwangu kunaelekezwa kimsingi kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, ili Nipate kuwachunga na ili waweze kuzungumza na kuongea uso kwa uso na Mimi; inaonyesha zaidi kwamba Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza ni wandani sisi kwa sisi (kumaanisha kwamba tunakula pamoja, kukaa pamoja, kuishi pamoja na kuchukua hatua pamoja), ili kwamba waweze kulishwa na Mimi kwa kweli—haya si maneno matupu ila ni ukweli. Hapo awali, watu waliniamini lakini hawakuweza kufahamu ukweli, na hii ilikuwa kwa sababu Sikuwa nimepata mwili bado. Leo, kupata mwili Kwangu kunawawezesha nyote kuelewa hali halisi na kunawaruhusu wale ambao wananipenda kwa dhati kunijua kupitia kwa usemi Wangu na mwenendo Wangu na kanuni za jinsi Ninavyoshughulikia mambo—Mungu mwenye hekima Mwenyewe. Pia kunaruhusu wale ambao hawanitafuti kwa dhati kuona kipengele cha Mimi ambacho ni ubinadamu Wangu katika vitendo Vyangu visivyofikiriwa na hivyo kunipinga, na kisha kufa “bila sababu yoyote,” wakipigwa chini na Mimi. Katika kumdhalilisha Shetani, kupata mwili kunakuwa na ushahidi wa nguvu zaidi Kwangu; sio tu kwamba Naweza kutoka katika mwili lakini pia Naweza kuishi ndani ya mwili. Sipitii kizuizi cha hewa au kijiografia, na Mimi hakuna vizuizi vyovyote kabisa na kila kitu kinapita vizuri. Shetani anaaibishwa zaidi na hoja hii, na Ninapotoka katika mwili, bado Nafanya kazi kupitia kwa mwili Wangu, na Siathiriwi hata kidogo. Bado Natembea juu ya milima, mito, maziwa, na kila pembe ya ulimwengu, na vile vile vitu vingi ndani yake. Nimepata mwili ili kuwafichua wale wote waliozaliwa kutoka Kwangu lakini ambao wameinuka kunipinga. Nisingekuwa mwili, hakungekuwa na njia ya kuwafichua (kumaanisha wale wanaotenda kwa njia moja mbele Yangu na kwa njia nyingine nyuma Yangu). Kama Ningebaki kama Roho, watu wangeniabudu katika dhana zao, na wangefikiria kuwa Mimi ni Mungu asiye na umbo na asiyeweza kufikiwa. Nimepata mwili leo kama kinyume cha dhana za watu (kuzungumzia urefu na sura Yangu), kuonekana kama mtu wa kawaida na kutokuwa mrefu sana. Ni jambo hili ambalo humdhalilisha Shetani zaidi na ni kinyume cha nguvu zaidi kwa dhana za watu (kufuru ya Shetani). Kama sura Yangu ingekuwa tofauti na kila mtu basi hilo lingekuwa tatizo—kila mtu angekuja kuniabudu na kunielewa kupitia kwa dhana zao wenyewe, na hawangeweza kuwa na ushahidi huo mzuri Kwangu. Kwa hiyo Nilijichukulia Mwenyewe umbo Nililo nalo leo, na si vigumu kuelewa hata kidogo. Kila mtu anapaswa kutoka nje ya dhana za binadamu na kutopotoshwa na njama za hila za Shetani. Katika siku zijazo Nitawaambia zaidi kwa mfululizo, kulingana na mahitaji ya kazi Yangu.

Leo, mradi Wangu umefanikiwa na mpango Wangu umekamilika. Nimelipata kundi la watu wanaoshirikiana na Mimi kwa akili na mawazo sawa. Huu ndio wakati mtukufu zaidi Kwangu. Wanangu wapendwa (wale wote wanaonipenda) wanaweza kuwa wenye moyo na akili moja na Mimi katika kukamilisha mambo yote ambayo Nahitaji kufanya pamoja na Mimi—hili ni jambo la ajabu. Baada ya leo, wale Nisioridhika nao hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Yaani, Nitawaondoa wale ambao hawapatani na kile ambacho Nimesema hapo awali. Watu lazima wapatane kikamilifu na kile Ninachosema. Kumbuka hili! Ni kupatana kikamilifu. Usielewe visivyo; yote ni juu Yangu. Watu, msizungumze masharti na Mimi. Nikisema unastahili basi haitabadilika, na Nikisema kuwa wewe hustahili, usionekane mwenye uchungu na kulaumu Mbingu na dunia—yote ni mipangilio Yangu. Ni nani aliyekufanya ujikosee heshima? Nani aliyekufanya utende lile kosa la aibu? Hata kama husemi lolote huwezi kuficha ukweli kutoka Kwangu. Nani Ninayemlenga ninaposema Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye anachunguza moyo wa ndani kabisa wa mwanadamu? Nawaambia wale wasio waaminifu. Kufanya jambo kama hilo nyuma Yangu, hamna aibu sana. Je, mnataka kunidanganya? Si rahisi vile! Ondokeni hapa mara moja! Mwana wa uasi! Hujipendi mwenyewe, na hujiheshimu mwenyewe! Wewe hujali kujihusu mwenyewe, lakini bado unataka Mimi nikupende? Sahau hilo! Sitaki hata mmoja wa fidhuli kama hao. Wote watatoka hapa! Hili huleta aibu kubwa zaidi juu ya jina Langu na halitakubalika kwa ninyi kutoona jambo hili wazi. Lazima mjilinde kutokana na kutiwa najisi na uchafu wowote katika enzi hii nzee ya uovu na uzinzi; lazima muwe watakatifu kabisa na msio na dosari. Leo, wale walio na sifa za kutosha kutawala kama wafalme pamoja na Mimi ni wale ambao hawajatiwa najisi na uchafu wowote, kwa maana Mimi ni Mungu mtakatifu Mwenyewe na Simtaki yeyote anayeliaibisha jina Langu. Watu kama hawa wametumwa na Shetani kunijaribu, na hakika wao wote ni watumishi wa Shetani ambao wanapaswa kupigwa pia (kuwatupa kwenye shimo lisilo na mwisho).

Familia Yangu ni takatifu na isiyo na dosari, na hekalu Langu ni kubwa na adhimu (kumaanisha wale walio na kile Nilicho na kile Nilicho nacho). Ni nani anayethubutu kuingia na kusababisha vurugu bila mpango? Bila shaka Sitamsamehe. Ataangamizwa kabisa na lazima aaibishwe kabisa. Natenda kwa busara. Bila kisu, bila bunduki na bila juhudi yoyote, Nitawashinda kabisa wale wanaonipinga na kuliaibisha jina Langu. Mimi ni karimu, na kwa kasi thabiti Naendelea na kazi Yangu hata wakati Shetani anasababisha usumbufu kama huo; Simjali na Nitamshinda kwa ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Hii ni nguvu Yangu na hekima Yangu, na hata zaidi ni sehemu ndogo ya utukufu Wangu usioisha. Machoni Pangu, wale wanaonipinga Mimi ni kama wadudu wanaotambaa mchangani na, kama Ninavyotamani ambao naweza kuwavunja hadi kufa chini ya mguu kulingana na nia Zangu, wakati wowote. Hata hivyo, Mimi hufanya mambo kwa hekima. Nataka wazaliwa Wangu wa kwanza waende wawashughulikie; Mimi siko katika haraka. Natenda kwa mpangilio, kwa hali ya utaratibu, na kwa usahihi bila makosa yoyote. Hao wazaliwa wa kwanza ambao wamezaliwa kutoka Kwangu wanapaswa kumiliki kile Nilicho, na waweze kuona hekima Yangu isiyoisha katika matendo Yangu!

Iliyotangulia: Sura ya 90

Inayofuata: Sura ya 92

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp