Sura ya 92

Kila mmoja anaweza kuuona uweza Wangu na hekima Yangu ndani ya maneno Ninayoyazungumza na mambo Ninayoyatenda. Popote Ninapokwenda, kazi Yangu iko pale. Hatua Zangu haziko nchini China pekee, bali muhimu zaidi, ziko katika mataifa yote ya dunia. Ya kwanza kulipokea jina hili, hata hivyo, ni mataifa saba tu ambayo yamezungumziwa hapo awali, kwani hizi ni hatua za kazi Yangu, na hivi karibuni mtaweza kufahamu kabisa kuihusu na mtaielewa kabisa. Nikiwaambia sasa, Nina wasiwasi kuwa wengi wataanguka chini, kama Nilivyosema awali kuwa Ninazungumza nanyi na kutamka sauti Yangu kulingana na vimo vyenu, na kila kitu Ninachofanya kina hekima Yangu isiyo na mwisho ndani yake ambayo hakuna mtu anayeweza kuifahamu; Ninaweza tu kuwaambia kuihusu kidogo kidogo kwa wakati. Jueni hili! Nyinyi daima ni watoto machoni Pangu; kwa kila hatua mnayochukua mnapaswa kuongozwa na Mimi na kuelekezwa na Mimi. Watu, ni chini ya uongozi Wangu tu ndipo mnaweza kupitia maisha yenu yote, vinginevyo hakuna mtu ambaye angeweza kuendelea kuishi. Ulimwengu dunia wote uko mikononi Mwangu, lakini hunioni Nikihangaika hapa na pale. Kinyume chake, Mimi ni mwenye utulivu na furaha. Watu hawajui uweza Wangu na wote wanatamani kuhisi wasiwasi kwa niaba Yangu—mnajua kidogo sana kujihusu! Bado mnaonyesha takataka zenu mbele Zangu, mkijisifu wenyewe! Nilielewa hili kitambo. Na mnajishughulisha na udanganyifu mbele Zangu, nyinyi mafidhuli wa kudharaulika! Toka nyumbani Mwangu sasa hivi! Sitaki vitu kama nyinyi. Ni heri Nisiwe na mtu yeyote katika ufalme Wangu hata kidogo, kuliko kutaka mafidhuli wa kudharaulika wa aina yenu! Je, wewe unajua kwamba tayari Sifanyi kazi juu yako? Licha ya ukweli kwamba bado unakula na kuvaa kama kawaida! Lakini je, unajua kwamba wewe huishi kwa ajili ya Shetani? Kuwa unatoa huduma kwa Shetani? Na bado una ujasiri wa kusimama mbele Yangu! Wewe huna aibu kabisa!

Hapo awali, mara nyingi Nilisema, “Maafa makubwa yatakuja hivi karibuni; maafa makubwa tayari yameanguka kutoka kwa mikono Yangu.” Je, “maafa makubwa” yanamaanisha nini, na hili “yameanguka” linapaswa kuelezwa vipi? Mnafikiri kuwa maafa haya makubwa yanamaanisha maafa yasiyoepukika ambayo hudhuru roho ya wanadamu, nafsi na mwili, na mnafikiri kuwa “mitetemeko ya ardhi, njaa na mateso” ambayo Ninayazungumzia ndiyo maafa haya makubwa. Lakini msichojua ni kwamba mmeelewa vibaya maneno Yangu. Na mnafikiri kuwa hili “yameanguka” lina maana kwamba maafa makubwa yameanza; hili linachekesha! Yaani mnaielewa kwa njia hii, na baada ya kusikia maelezo yenu Ninakasirika sana. Fumbo ambalo watu hawajaweza kufumbua (fumbo la siri zaidi) pia ndilo fumbo ambalo limeeleweka vibaya sana katika enzi zote. Zaidi ya hayo, fumbo hili ni jambo ambalo hakuna aliyewahi kulipitia hapo awali (kwani fumbo hili litatimizika tu katika siku za mwisho, na katika enzi ya mwisho tu ndipo wanadamu wanaweza kuliona lakini hawalijui) kwa sababu Nimelifunga kabisa na wanadamu hawawezi kulipenyeza kabisa (hawawezi kuona hata sehemu yake ndogo zaidi). Kwa kuwa kazi Yangu imeendelea hadi hatua hii, ninawatia msukumo kulingana na mahitaji ya kazi Yangu, vinginevyo hamngekuwa na njia ya kuelewa. Sasa Ninaanza ushirika na kila mtu anapaswa kuzingatia, vinginevyo yeyote asiye mwangalifu, ikiwa ni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza, atakabiliwa na hukumu Yangu, na katika hali mbaya zaidi atapigwa kwa mkono Wangu (kumaanisha kwamba roho, nafsi na mwili wake vitachukuliwa). Maafa makubwa yanazungumziwa kuhusiana na kila amri ya utawala wa ufalme Wangu, na kila moja ya amri Zangu za utawala ni sehemu ya maafa makubwa. (Amri Zangu za utawala hazijafunuliwa kabisa kwenu, lakini msiwe na hofu au wasiwasi juu ya hili; kuna baadhi ya mambo ambayo yatawaletea manufaa madogo mkiyajua mapema zaidi. Kumbukeni hili! Mimi ni Mungu mwenye hekima.) Je, sehemu nyingine ni gani? Maafa makubwa yana sehemu mbili: Amri Zangu za utawala na hasira Yangu. Wakati ambapo maafa makubwa yataanguka utakuwa pia wakati ambapo Nitaanza kutenda kwa hasira na kutekeleza amri Yangu ya utawala. Hapa Ninawaambia wana Wangu wazaliwa wa kwanza: Lazima mhakikishe kuwa hamtadhoofika kutokana na hili. Je, mmesahau kwamba vitu vyote na mambo yote yameamuliwa awali na Mimi? Mwana Wangu, usiogope! Hakika Mimi nitawahifadhi, mtafurahia baraka nzuri na Mimi milele, na mtakuwa pamoja nami milele. Kwa sababu nyinyi ni wapendwa Wangu, Sitawaacha; kwa sababu Sifanyi mambo ya upumbavu, Nikibomoa kitu ambacho kimekamilika kwa ugumu, je, si itakua kujichoma mguuni? Ninajua unachofikiria katika moyo wako. Umekumbuka? Nini kingine ungependa Mimi niseme? Nitazungumza zaidi juu ya maafa makubwa. Wakati ambapo maafa makubwa yatafika utakuwa wakati wa kutisha zaidi na yatafichua zaidi uovu wa mwanadamu. Kila aina ya sura ya mapepo itafichuliwa kwa mwanga wa uso Wangu na hawatakuwa na mahali pa kujificha, mahali popote pa kupata kivuli; watafichuliwa kabisa. Matokeo ya maafa makubwa yatakuwa kuwafanya wale wote ambao sio wateule Wangu au sio Niliowaamulia awali kupiga magoti mbele Zangu na kuomba msamaha, kwa kutoa machozi na kusaga meno. Hii ni hukumu Yangu ya Shetani, hukumu Yangu ya ghadhabu. Kwa sasa Ninafanya kazi hii na labda kuna watu ambao wanapenda kujifanya kuwa na uwezo na kutumia njia ya udanganyifu, lakini kadri wanavyozidi kuwa hivi ndivyo Shetani atazidi kufanya kazi juu yao, mpaka wafikie hatua ambapo hali zao za awali zinafichuliwa.

Sina haraka katika kufanya kazi Yangu, na Ninampanga kila mtu Mimi Mwenyewe (hii inawadhihaki na inathibitisha kuwa wao ni wazao wa joka kubwa jekundu na Siwasikilizi, kwa hiyo kutumia “kupanga” sio kuzidi), na kufanya kila kazi Mimi Mwenyewe. Kila kitu kinafanikiwa na Mimi, na ni mafanikio salama salimini; kila kitu Ninachofanya, hatua kwa hatua, tayari imepangwa. Nawaambieni mapenzi Yangu na kuhusu mzigo Wangu kidogo kidogo kwa wakati. Kuanzia wakati huu, maneno Yangu yanaanza kuonekana kwa mataifa yote na watu wote. Kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza tayari wamefanywa kuwa kamili(lengo la maneno Yangu ni wana Wangu na watu Wangu), njia ambayo Mimi hufanya kazi imeanza kubadilika tena. Je, mnaelewa hili vizuri? Je, mmesikia toni ya maneno Yangu hizi siku chache zilizopita? Ninawafariji wana Wangu wazaliwa wa kwanza kila hatua ya njia, lakini kuanzia sasa (kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza tayari wamefanywa kuwa kamili) Mimi hubeba kisu mkononi Mwangu (kuwa maneno ya ukali zaidi). Mtu yeyote ambaye Mimi humtazama kwa wakati kama asiyefaa (kumaanisha wale ambao hawajaamuliwa awali au kuchaguliwa, kwa hivyo hakuna ukinzani), Sijali kama wanatoa huduma Kwangu, au kama wao ni kitu kingine, Nitawaondoa mara moja. Mimi ni Mwenyezi Mungu na Ninaweza kuwafanya watu wote wanihudumie. Sisiti kutengana na mtu wa aina hiyo hata kidogo; Nikisema simtaki basi simtaki. Sasa kwa kuwa wakati huu umefika, Ninahitaji tu kumwona mtu anayenichukiza na Nitamtupa mara moja bila uchunguzi. Kwa sababu Mimi ni Mungu ambaye anafuata neno Lake. Kwa wale ambao Nimewaamulia awali kuwa katika utumishi Wangu, bila kujali wema wako au kama umefanya chochote kinachonikaidi au la, ukinichukiza basi Nitakutimua. Mimi siogopi matatizo ya baadaye. Nina amri Zangu za utawala, ninafuata neno Langu na neno Langu litatimia. Je, Ninaweza kumweka Shetani? Nisikilizeni, enyi watu! Si lazima uogope; ni lazima uondoke wakati wowote Ninapokwambia uondoke. Usinipe visingizio kwani Mimi sina maneno ya kukuambia! Kwa sababu Nimekuwa na uvumilivu kama huo, na wakati wa kutekeleza amri Zangu za utawala umefika na siku yenu ya mwisho pia imewadia. Kwa maelfu ya miaka mlipotoshwa na daima mkafanya mambo kwa njia ya ukaidi na ya makusudi, lakini siku zote Nilikuwa na subira (kwa sababu Mimi ni mkarimu na huuruhusu upotovu wako ufikie kiasi fulani). Lakini sasa tarehe ya mwisho ya huruma Yangu imefika na wakati umefika kwenu kumilikiwa na kutupwa katika ziwa la moto na kiberiti. Fanyeni hima na muondoke njiani. Ninaanza kutekeleza rasmi hukumu Yangu na kuachilia hasira Yangu.

Katika mataifa yote na maeneo yote ya dunia, mitetemeko ya ardhi, njaa, maafa, kila aina ya maafa hutokea mara kwa mara. Ninapofanya kazi Yangu kubwa katika mataifa yote na maeneo yote, maafa haya yatatokea kwa ukali zaidi kuliko wakati mwingine wowote tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Huu ndio mwanzo wa hukumu Yangu ya watu wote; lakini wana Wangu wanaweza kupumzika bila wasiwasi, hakuna janga litakalowakumba, nami Nitawahifadhi (kumaanisha kuwa nyinyi baadaye mtakuwa hai katika mwili, lakini si katika nyama na damu, hivyo hamtaweza kuteseka na maumivu ya janga lolote). Nyinyi mtakuwa tu pamoja na Mimi mkitawala kama wafalme na kuyahukumu mataifa yote na watu wote, kufurahia baraka nzuri na Mimi milele katika dunia na miisho ya ulimwengu. Maneno haya yote yatatimizwa na hivi karibuni yatafanikishwa mbele ya macho yenu. Sichelewi hata saa moja au siku moja, Mimi hufanya mambo haraka sana. Usiwe na hofu au wasiwasi, na baraka Ninayokupa ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kukunyang’anya—hii ni amri Yangu ya utawala. Watu wote watanitii kwa sababu ya matendo Yangu; sio kwamba watashangilia na kushangilia tu, lakini hata zaidi watarukaruka kwa furaha.

Iliyotangulia: Sura ya 91

Inayofuata: Sura ya 93

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp