293 Mungu Pekee Ndiye Bora Zaidi

1

Maneno yote ya Mungu ni ukweli, Anachosema na kufanya ni haki.

Tunapokutana na vitu vinavyokinzana na dhana zetu, twafuta ukweli.

Binadamu waliopotoka wanapaswa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.

Pitia maneno ya Mungu na uingie katika uhalisi wa ukweli ili utimize mapenzi Yake.

Acha majonzi yote, mtazamie Mungu na utende ukweli.

Tuimarishe azimio letu la kumwiga Petro, na tuwe na ushuhuda mkuu.

Acha tuinue sauti zetu na tuimbe; Mungu pekee ndiye bora zaidi!

Tutasifu utakatifu na haki ya Mungu milele!

2

Nipitiapo hukumu ya maneno ya Mungu, nimeona jinsi nilivyopotoshwa kwa kina na Shetani.

Nina kiburi, mwovu na mdanganyifu, kwa kweli sina mfano wa binadamu.

Baada ya kukubali hukumu na kujijua, nimetubu kwa kweli.

Upendo mkubwa wa Mungu umefichwa katika hukumu na kuadibu Kwake.

Kupata kionjo cha tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa lolote, namcha Mungu kutoka moyoni mwangu.

Kuuacha mwili na kutenda ukweli, nahisi Mungu yuko karibu zaidi.

Acha tuinue sauti zetu na tuimbe; Mungu pekee ndiye bora zaidi!

Tutasifu utakatifu na haki ya Mungu milele!

3

Mateso, ugumu, majaribu yanapotokea, lazima tumtukuze na kumshuhudia Mungu.

Kupitia uzima au katika kifo, viumbe walioumbwa wanapaswa kutii sheria za Mungu.

Kupitia ugumu na mateso tunamchukia Shetani hata zaidi; ni Mungu pekee ndiye anayependeza.

Twahatarisha maisha yetu kumwaibisha Shetani, kuwa na ushuhuda wa ushindi.

Shida nyepesi, ambazo ni za kupita tu, zinalipwa kwa ukweli na uzima.

Yote afanyayo Mungu ni upendo kwa mwanadamu, na tunaamini kwa uthabiti, bila shaka yoyote.

Acha tuinue sauti zetu na tuimbe; Mungu pekee ndiye bora zaidi!

Tutasifu utakatifu na haki ya Mungu milele!

Iliyotangulia: 292 Upendo wa Mungu Umeuyeyusha Moyo Wangu

Inayofuata: 294 Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp