269 Maombi Ya Petro Wakati wa Kusulubiwa Kwake

1 Ee Mungu! Wakati Wako umewadia, wakati ulionitayarishia umefika. Mimi lazima nisulubiwe kwa ajili Yako, lazima niwe na ushuhuda huu Kwako, na ninatumai kwamba upendo wangu utaweza kukidhi mahitaji Yako, na kwamba unaweza kuwa safi zaidi. Leo, kuwa na uwezo wa kufa kwa ajili Yako, na kusulubiwa kwa ajili Yako, ni faraja na ya kutia moyo kwangu, kwa maana hakuna kinachonifurahisha kuliko kuweza kusulubiwa kwa ajili Yako na kukidhi matakwa Yako, na kuweza kujitoa Kwako, kutoa maisha yangu Kwako.

2 Ee Mungu! Wewe ni wa kupendeza kweli! Kama Ungeniruhusu niishi, ningenuia kukupenda zaidi. Mradi tu ninaishi, mimi nitakupenda. Natamani kukupenda kwa undani zaidi. Unanihukumu, Unaniadibu, na kunijaribu kwa sababu mimi si mwenye haki, kwa sababu nimetenda dhambi. Na tabia Yako ya haki inakuwa dhahiri zaidi kwangu. Hii ni baraka kwangu, kwa maana ninapata uwezo wa kukupenda kwa undani zaidi, na mimi niko tayari kukupenda kwa njia hii hata kama Hunipendi. Mimi niko tayari kutazama tabia Yako ya haki, kwa maana inafanya niweze kuishi maisha ya maana zaidi.

3 Mimi ninahisi kwamba maisha yangu sasa ni ya maana zaidi, kwa maana nimesulubiwa kwa ajili Yako, na ni jambo la maana kufa kwa ajili Yako. Hata hivyo bado mimi sijaridhika, kwa maana najua kidogo sana kukuhusu, najua kwamba siwezi kutimiza matakwa Yako kikamilifu, na kuwa nimekulipa kidogo mno. Katika maisha yangu, sijaweza kurudisha nafsi yangu Kwako kikamilifu; Niko mbali sana na hili. Nikitazama nyuma kwa wakati huu, mimi huhisi kuwa nina mzigo mkubwa wa madeni kwako, na sina muda mwingine ila huu kwa ajili ya kurekebisha makosa yangu na upendo wote ambao sijakulipa Wewe.

Iliyotangulia: 268 Niko Tayari Kutii Kazi ya Mungu

Inayofuata: 270 Moyo Mwaminifu kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp