Utangulizi

Wakati w0a kazi Yake ya siku za mwisho, Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno ambayo yamekusanywa katika kitabu: Neno Laonekana katika Mwili. Kitabu hiki kina maudhui mengi, na ni chenye umuhimu mkubwa na cha manufaa sana kwa ufahamu wa watu juu ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na asili Yake. Tumepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa zaidi ya miaka 20 na tumeelewa ukweli mwingi na siri kutoka ndani ya maneno ya Mungu, tuna maarifa ya kweli kuhusu mpango wa Mungu wa usimamizi wa kuwaokoa wanadamu (pamoja na hatua tatu za kazi), na hata zaidi tumekuja kufahamu tabia ya Mungu ya haki kwa kiasi kikubwa. Maneno na kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni ya maana sana kwa watu kupata wokovu na kuachana na ushawishi wa Shetani kupitia imani yao katika Mungu. Wanadamu wapotovu wasipopitia utakaso na ukamilifu wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, basi hawataweza kabisa kumjua Mungu, na watakuwa kama makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo, wakifurahia neema ya Mungu lakini hawamjui, kumtumikia Mungu lakini kumkataa, na hata watamsulubisha Kristo wa siku za mwisho msalabani tena—huu ni ukweli usiokanushika. Nani anayejua ni viongozi, wachungaji na wazee wangapi wa ulimwengu wa dini ambao sasa wanalaani kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na je, huu si ukweli wa Kristo kutundikwa msalabani tena? Maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni ya maana sana kwa wokovu wa wanadamu wapotovu na kwa wao kupata maarifa ya kweli kumhusu Mungu. Kama vile Mwenyezi Mungu asemavyo, “Kama maneno yanayonenwa na Mungu ni, katika mwonekano wa nje, wazi ama magumu kuelewa, yote ni ukweli ulio lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; kanuni na imani ya kufanya maisha yake ya kila siku; njia, lengo, na mwelekeo ambao lazima apitie ili kupokea wokovu; kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli jinsi mwanadamu anavyotii na kumwabudu Mungu. Ni uhakika ambao unahakikisha kuishi kwa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama. Yamejaa utajiri wa ukweli wa ubinadamu wa kawaida anavyoishi binadamu aliyeumbwa, yamejaa ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwa upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, yamejaa mafunzo bila kuchoka, kuonya, kuhamasisha na furaha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo mazuri, hakika inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuelekea wokovu na njia ya mwanga” (Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu katika Neno Laonekana katika Mwili).

Kwa sababu Mungu ameonyesha maneno mengi, ili kurahisisha ufuatiliaji wa watu wa ukweli, ufahamu wao wa maneno ya Mungu na ufahamu wao juu ya kazi ya Mungu, kwa hivyo tumechagua kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili vifungu kadhaa bora zaidi na vinavyojulikana vya Maneno ya Mungu kwa matumizi ya wale wote wanaomwamini Mungu na wanaofuatilia ukweli, ili maneno ya Mungu yawe wito wa maisha yao na ukweli wa maisha yao. Tulipokuwa tukichagua vifungu vinavyojulikana vya maneno ya Mungu, tulihisi kabisa kwamba kila sentensi ya Mungu ni ya thamani sana. Kila sura ya maneno ya Mungu ni kipande kimoja kizima, kila neno na kila sentensi ya maneno ya Mungu yameunganishwa pamoja na yamekamilika; katika sehemu nyingine, haikuwa rahisi kuamua tuchague nini na tuache nini, kwa hivyo tulilazimika kuchagua sehemu kubwa. Hii ilituruhusu tutambue thamani ya kila moja ya maneno ya Mungu na kwamba kweli Kristo ndiye ukweli, njia na uzima—ni kweli kabisa! Maneno bora zaidi ya Mungu yaliyochaguliwa kutoka katika kitabu hiki yanafaa tu kudondolewa na kuchaguliwa wakati wa kueneza injili na kumshuhudia Mungu, na bila shaka yanafaa pia kwa ibada ya kiroho ya kibinafsi au kukariri vifungu bora zaidi. Ikiwa mtu anataka kutafuta na kuchunguza kipengele fulani cha ukweli, kusoma tu maneno kadhaa bora hakutoshi kufikia matokeo kikamilifu; ni bora kusoma sura nzima za maneno ya Mungu kutegemezwa kwa vifungu vilivyochaguliwa, na wakati huo tu ndipo mtu atakapofanikisha matokeo bora. Inaweza kusemwa kwamba kitabu hiki, Maneno Mashuhuri Kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Kristo wa Siku za Mwisho, ni mwongozo kwa wale wanaotamani kuonekana kwa Mungu ili kutafuta nyayo za Mungu, na kinaweza kukuongoza kupitia lango la ufalme wa mbinguni. Baada ya kusoma kitabu hiki kwa uangalifu, utashukuru na kusifu neema ya Mungu. Kwa hivyo tunatumai kwa dhati kwamba wale wote wanaotamani ukweli na wanaotamani kuonekana kwa Mungu watakukubali bila kupoteza wakati matamshi halisi ya Mungu ya siku za mwisho—Neno Laonekana katika Mwili—kwamba yawe sikukuu ya macho yako, ili yafungue macho yako na yakujaze raha, na ili ujue sauti ya Mungu, urudi mbele Yake na upate wokovu wote wa Mungu. Hili ndilo kusudi letu la pekee la kuchapisha kitabu hiki.

Julai 28, 2019

Inayofuata: Maneno Bora Zaidi Juu ya Hatua Tatu za Kazi ya Kuwaokoa Wanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya...

Sura ya 14

Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki