I. Maneno Juu ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu ya Kuwaokoa Wanadamu

1. Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imekamilika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwepo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. “Kumsimamia mwanadamu” haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika hatua tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hatua hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, yaani, ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati uo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama kazi ya wokovu ilivyogawanywa katika hatua tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika hatua tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani kwa kweli ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu silo jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika hatua moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika hatua na vipindi, na vita vinapiganwa dhidi ya Shetani kulingana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Pengine, katika mawazo ya mwanadamu, anaamini kuwa katika vita hivi Mungu atajiandaa kupigana na Shetani, katika njia sawa na vile ambavyo majeshi mawili yangepigana. Hili tu ni jambo ambalo akili ya mwanadamu ina uwezo wa kukisia, na ni wazo lisilo dhahiri kupita kiasi na lisiloweza kutendeka, na bado ndilo mwanadamu analiamini. Na kwa sababu Nasema hapa kuwa njia ya wokovu wa mwanadamu ni kupitia vita na Shetani, mwanadamu anawaza ya kwamba hivi ndivyo vita vinavyoendeshwa. Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, hatua tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika hatua tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizwa kupitia kwa hatua kadhaa za kazi: kumpa mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu akamilishwe. Kusema ukweli, vita na Shetani hajiandai kupigana na Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kumshuhudia Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu. Punde unapofahamu lengo la hatua hizi tatu za kazi, basi utafahamu jinsi ya kuthamini umuhimu wa kila hatua ya kazi, na utatambua jinsi ya kutenda ili kutosheleza shauku ya Mungu. Iwapo utaweza kufikia hatua hii, basi hili, ono kubwa kuliko yote, litakuwa msingi wa imani yako katika Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe wote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu. Sasa, lazima uelewe kwamba kazi yote kutoka awamu ya kwanza hadi leo ni kazi ya Mungu mmoja, ni kazi ya Roho mmoja, ambapo hakuna shaka.

Kimetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo. Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti, na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti, yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kati ya maono yote, hili ndilo kuu zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua, na ikiwa litaeleweka kabisa na mwanadamu, basi ataweza kusimama imara.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika. Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu. Ni hatua tatu tu za Mungu zinazoweza kuonyesha kabisa ukamilifu wa tabia ya Mungu, na kuonyesha kabisa nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu wote, na mchakato mzima wa wokovu wa mwanadamu. Hili ni dhibitisho kuwa Yeye amemshinda Shetani na kumpata mwanadamu, ni dhibitisho la ushindi wa Mungu, na ni maonyesho ya tabia kamili ya Mungu. Wale wanaoelewa hatua moja tu kati ya hatua tatu za kazi ya Mungu wanajua tu sehemu ya tabia ya Mungu. Katika dhana ya mwanadamu, ni rahisi kwa hatua hii moja kuwa mafundisho ya kidini, panakuwa na uwezekano zaidi wa mwanadamu kuweka amri kumhusu Mungu, na mwanadamu anatumia hii sehemu moja ya tabia ya Mungu kama dhihirisho la tabia nzima ya Mungu. Zaidi ya hayo, mawazo mengi ya mwanadamu yanachanganywa ndani yake, hivi kwamba anaweka vikwazo imara kwa tabia, nafsi, na hekima ya Mungu, na pia kanuni za kazi ya Mungu ndani ya vigezo vyenye mipaka, akiamini kwamba ikiwa Mungu alikuwa hivi wakati mmoja, basi Yeye atasalia kuwa vile daima, na kamwe hatabadilika. Ni wale tu wanaojua na kuthamini hatua tatu za kazi ndio wanaoweza kumjua Mungu kabisa na kwa usahihi. Angalau, hawatamfafanua Mungu kama Mungu wa Waisraeli, ama Wayahudi, na hawatamwona kama Mungu atakayesulubiwa msalabani milele kwa ajili ya mwanadamu. Kama unapata kumjua Mungu kutokana na hatua moja ya kazi Yake tu, basi maarifa yako ni kidogo, kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama si hivyo, kwa nini wengi wa walinzi wa kidini wa kale walimtundika Mungu msalabani akiwa hai? Je, si kwa ajili mwanadamu humwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani?

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Hatua tatu za kazi ni rekodi ya kazi nzima ya Mungu, ni rekodi ya wokovu wa Mungu wa mwanadamu, na si porojo tu. Kama kweli mnataka kutafuta kujua tabia nzima ya Mungu, basi sharti mfahamu hatua tatu za kazi inayofanywa na Mungu, na, zaidi, sharti msiache hatua yoyote. Hiki ndicho kiwango cha chini kinachopaswa kufikiwa na wale wanaotafuta kumjua Mungu. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuvumbua maarifa ya Mungu. Si kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anaweza kufikiria, wala si matokeo ya fadhila za Roho Mtakatifu kwa mtu mmoja. Badala yake, ni maarifa yanayotokea mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, na ni maarifa ya Mungu yanayotokana tu na mwanadamu kupitia ukweli wa kazi ya Mungu. Maarifa kama haya hayawezi kutimizwa kwa ghafla, wala si jambo linaloweza kufundishwa. Inahusiana kabisa na uzoefu wa kibinafsi. Wokovu wa Mungu wa mwanadamu ndiyo kiini cha hatua hizi tatu za kazi, ilhali katika kazi ya wokovu kumejumuishwa mbinu kadhaa za kufanya kazi na namna ambazo tabia ya Mungu imeonyeshwa. Hili ndilo jambo gumu sana kwa mwanadamu kutambua na kwa mwanadamu kuelewa. Mgawanyiko wa enzi, mabadiliko ya kazi ya Mungu, mabadiliko katika eneo la kazi, mabadiliko ya wanaopokea kazi na kadhalika—haya yote yamejumuishwa katika hatua tatu za kazi. Hususan, tofauti katika njia ya utendakazi wa Roho Mtakatifu, na vilevile mabadiliko katika tabia ya Mungu, picha, jina, utambulisho, au mabadiliko mengine, yote ni sehemu ya hatua tatu za kazi. Sehemu moja ya kazi inaweza tu kuwakilisha sehemu moja, na imewekewa mipaka ndani ya wigo fulani. Haihusiani na mgawanyiko wa enzi, ama mabadiliko ya kazi ya Mungu, wala masuala mengine. Huu ni ukweli ulio waziwazi. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, ghadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ilikuwa ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ilikuwa ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, na haziwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote.

Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Mpango wa miaka elfu sita umegawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, “Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni.” Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na badala yake kazi katika Enzi ya Neema pekee, basi yote ambayo mwanadamu angefahamu ni kwamba Mungu Anakomboa tu mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Ukweli kamba Mungu alikamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria tu, na ukweli kamba alikamilisha kazi Yake ya ukombozi haimaanishi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema ikiwa imefika mwisho, huwezi basi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba pekee unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yanapaswa kufunuliwa ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kuainishwa kulingana na aina. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.

Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita.

Kimetoholewa kutoka katika “Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapaswa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaoabudu Budha. Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile Anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi. Kadiri mwanadamu alivyo na uwezo wa kushirikiana na Mungu kwa kweli, ndivyo anavyozidi kumtukuza Mungu. Ushirikiano wa mwanadamu ndio ushuhuda anaohitajika kuwa nao, na ushuhuda alio nao ndio matendo ya mwanadamu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu iweze au isiweze kuwa na matokeo yanayohitajika, na paweze ama pasiweze kuwa na ushuhuda wa kweli, ni mambo ambayo yameunganishwa yasiyochanganulika na ushirikiano na ushuhuda wa mwanadamu. Wakati kazi itakapokwisha, yaani, wakati usimamizi wote wa Mungu utakapofikia kikomo chake, mwanadamu atahitajika kuwa na ushuhuda wa hali ya juu, na wakati kazi ya Mungu itakapofika mwisho wake, matendo na kuingia kwa mwanadamu vitafikia upeo wake. Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kutii sheria na amri, na alihitajika kuwa mwenye subira na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na hatimaye bado anahitajika kumpenda Mungu katika taabu. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia kutoka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji kwa mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa njia hii, usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa ya juu kiasi kwamba tabia yake kila mara inafikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo tu ambapo wanadamu wote wanaanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani hadi, ambapo kazi ya Mungu itafikia kikomo kabisa, ndio wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Wakati huo utakapowadia, kazi ya Mungu itakuwa imefika mwisho wake, na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu ili kufikia mabadiliko katika tabia yake hautakuwepo tena, na wanadamu wote wataishi katika nuru ya Mungu, na kuanzia hapo kuendelea, hapatakuwa na uasi au upinzani wowote kwa Mungu. Pia Mungu hatamwekea mwanadamu matakwa, na patakuwepo na ushirikiano wenye upatanifu zaidi kati ya mwanadamu na Mungu, ambao utakuwa maisha ya mwanadamu na Mungu pamoja, maisha ambayo yatafuatia baada ya usimamizi wa Mungu kukamilishwa kabisa, na baada ya mwanadamu kuokolewa kikamilifu kutoka katika mafumbato ya Shetani.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili; na inaonekana inatatanisha. Watu wanahisi kwamba ni kama hadithi ya visasili, na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, sembuse kujua hadithi ngapi ambazo zimetokea katika ulimwengu na anga. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. Katika kazi ya usimamizi wa Mungu wa wakati huu, wanadamu ndio chombo cha maovu ya Shetani, na kwa wakati uo huo ni chombo cha ukombozi wa Mungu, aidha ni sababu ya vita dhidi ya Mungu na Shetani. Wakati sawia na wakati wa kutekeleza kazi Yake, Mungu taratibu Humtoa mwanadamu kutoka mikononi mwa Shetani, na hivyo mwanadamu anakuja karibu zaidi na Mungu …

Kimetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa Amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. Hatua ya kazi ya siku za mwisho, na hatua mbili zilizopita katika Israeli na Yudea, ni mpango wa Mungu wa usimamizi katika dunia nzima. Hakuna anayeweza kupinga hili, na ni ukweli wa kazi ya Mungu. Ingawa watu hawajapata uzoefu ama kushuhudia nyingi za kazi hizi, ukweli unabaki kuwa ukweli, na hauwezi kukanwa na mwanadamu yeyote. Watu wanaomwamini Mungu katika nchi zote duniani watakubali hatua tatu za kazi. Kama wajua tu hatua moja ya kazi, na huelewi hatua nyingine mbili za kazi, na huelewi kazi ya Mungu katika wakati uliopita, basi huwezi kuongea ukweli wa mpango mzima wa usimamizi wa Mungu, na maarifa yako ya Mungu yameegemea upande mmoja, kwa kuwa katika imani yako katika Mungu humfahamu, ama kumwelewa, na kwa hivyo hustahili kutoa ushuhuda wa Mungu. Bila kujali kama maarifa yako ya sasa ya mambo haya yana kina kirefu ama cha juujuu tu, mwishowe, lazima muwe na maarifa, na ushawishike kabisa, na watu wote wataona uzima wa kazi ya Mungu na kunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Mwishoni mwa kazi hii, madhehebu yote yatakuwa moja, viumbe wote watarejea chini ya utawala wa Muumba, viumbe wote watamwabudu Mungu mmoja wa kweli, na dini zote ovu zitakuwa bure, na hazitaonekana tena.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Mbona mfululizo huu wa marejeo kwa hatua tatu za kazi? Kupita kwa enzi, maendeleo ya kijamii, na uso wa asili unaobadilika yote hufuata mabadiliko katika hatua tatu za kazi. Mwanadamu hubadilika kwa wakati na kazi ya Mungu, na wala hakui peke yake mwenyewe. Kutajwa kwa hatua tatu za kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kuleta viumbe wote, na watu kutoka dini zote, chini ya utawala wa Mungu mmoja. Bila kujali wewe ni wa dini gani, mwishowe nyote mtanyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu anayeweza kufanya kazi hii; haiwezi kufanywa na kiongozi yeyote wa kidini. Kuna dini kadhaa kuu duniani, na kila moja ina kichwa, ama kiongozi, na wafuasi wameenea katika nchi tofauti na maeneo yote duniani; kila nchi, iwe ndogo au kubwa, ina dini tofauti ndani yake. Hata hivyo, bila kujali ni dini ngapi zilizo duniani, watu wote wanaoishi duniani mwishowe wanaishi katika uongozi wa Mungu mmoja, na uwepo wao hauongozwi na viongozi wa kidini au vichwa. Ambayo ni kusema kwamba wanadamu hawaongozwi na kiongozi fulani wa kidini ama kiongozi; badala yake wanadamu wote wanaongozwa na Muumba, aliyeziumba mbingu na nchi, na vitu vyote, na ambaye aliwaumba wanadamu—na huu ni ukweli. Hata ingawa dunia ina dini kadhaa kuu, bila kujali jinsi zilivyo kuu, zote zipo chini ya utawala wa Muumba, na hakuna inayoweza kuzidi wigo wa mamlaka hii. Maendeleo ya wanadamu, maendeleo ya kijamii, maendeleo ya sayansi ya asili—kila moja haitengani na mipango ya Muumba, na kazi hii sio kitu kinachoweza kufanywa na uongozi fulani wa dini. Viongozi wa dini ni viongozi tu wa dini fulani, na hawawezi kuwakilisha Mungu, ama Yule aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote. Viongozi wa kidini wanaweza kuongoza wale wote walio katika dini yote, lakini hawawezi kuamrisha viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu—huu ni ukweli uliokubalika ulimwenguni. Viongozi wa dini ni viongozi tu, na hawawezi kuwa sawa na Mungu (Muumba). Vitu vyote vi mikononi mwa Muumba, na mwishowe vyote vitarejea mikononi mwa Muumba. Mwanadamu kiasili aliumbwa na Mungu, na haijalishi dini, kila mtu atarejea katika utawala wa Mungu—hili haliwezi kuepukika. Ni Mungu tu Aliye Juu Zaidi kati ya vitu vyote, na mtawala mkuu kati ya viumbe wote lazima pia warejee chini ya utawala Wake. Bila kujali mwanadamu ana hadhi ya juu kiasi gani, hawezi kumfikisha mwanadamu kwenye hatima inayomfaa, wala hakuna anayeweza kuainisha kila kitu kulingana na aina. Yehova mwenyewe alimuumba mwanadamu na kumwainisha kila mmoja kulingana na aina na siku ya mwisho itakapowadia bado Atafanya kazi Yake Mwenyewe, kuanisha kila kitu kulingana na aina—hili haliwezi kufanywa na mwingine isipokuwa Mungu. Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejea chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapotambulishwa kwa mwanadamu, kutakuwepo katika mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati ya kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Kama kutakuwa na aliye na vipaji hivi, siku ambayo kazi ya Mungu itafikia kikomo, ama kuwe na wawili ama watatu, na kibinafsi wamekubali kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili, basi hakuna jambo la kuhuzunisha na kujutia kama hili—ingawa ni katika hali mbaya zaidi tu. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, hapo awali hakujawahi kuwa na kazi kama hii katika historia ya ukuaji wa mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe wote? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itapokea malipo. Bila kujali jinsia yao ama uraia wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni ya mwisho na ya juu zaidi kuwahi kutekelezwa katika miaka 6000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi inayodhihirisha kila kundi la mwanadamu. Kupitia kazi ya kumfanya wanadamu kumjua Mungu, daraja tofauti za mwanadamu zinadhihirishwa: Wale wanaomjua Mungu wamehitimu kupokea baraka za Mungu na kukubali ahadi zake, wakati wale wasiomjua Mungu hawajahitimu kupokea baraka za Mungu wala kupokea ahadi zake. Wale wanaomjua Mungu ni wandani wa Mungu, na wale wasiomjua Mungu hawawezi kuitwa wandani wa Mungu; wandani wa Mungu wanaweza kupokea baraka zozote za Mungu, lakini wale wasio wandani wa Mungu hawastahili kazi yoyote Yake. Iwe ni dhiki, usafishaji, ama hukumu, yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu hatimaye kufikia maarifa ya Mungu na ili kwamba mwanadamu amtii Mungu. Hii ndiyo athari pekee itakayofikiwa hatimaye.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na ubinadamu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani. Wale wanaoweza kumshuhudia Mungu wataweza kupokea ahadi na baraka za Mungu, na litakuwa ndilo kundi litakalosalia pale mwisho kabisa, lile linalomiliki mamlaka ya Mungu na lililo na ushuhuda wa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Baada ya kufanya kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, sababu ya kimsingi ikiwa ni kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Yeye huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu duniani, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Viumbe wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio Lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio duniani na viumbe wote walio duniani watauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na duniani vyote vitauona utukufu Wake, na Atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kumruhusu binadamu amsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani.

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: Utangulizi

Inayofuata: A. Kuhusu Ufunuo wa Mungu wa Kazi Yake katika Enzi ya Sheria

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp