188 Nimeamua Kujitolea Kabisa Kwa Mungu

1 Shetani alinipotosha na kuniangamiza kabisa, nilitafuta umaarufu na utajiri na kuishi katika dhambi. Ilikuwa kila mwamba ngoma avutie upande wake, sikujali kuhusu dhamiri au maadili. Mungu alinihurumia na kuniinua, na Akaniokoa kutoka katika ulimwengu mbaya. Maneno ya Mungu ya hukumu na mfichuo viliniwezesha kuona chanzo cha upotovu wa dunia. Akiwa amepotoshwa na kuhadaiwa sana na Shetani, kila mtu amenaswa katika shimo la giza. Maneno ya Mungu ya hukumu yalinizindua na nikaona nuru ya uzima. Umaarufu, utajiri, cheo, na furaha ya familia ni tupu kweli, nami sitavifuata tena. Kumtii Mungu, kuujali moyo wa Mungu, na kutekeleza wajibu wa mtu ni kanuni za kweli za Mbingu na dunia. Nitafanya kila niwezalo ili niufuatilie ukweli, nimjue Mungu, na kuwa mtu anayempenda Mungu.

2 Mungu anatusihi na tunapaswa kuinuka na kujitwika agizo Lake; ni jambo la kupendeza sana kujitolea kwa ajili ya Mungu. Katika shida, uongozi wamaneno ya Mungu huupa nguvu moyo wangu; siwezi kushikilia jembe na kutazama nyuma. Ni nadra sana kuweza kukubali mafunzo ya ufalme na siwezi kabisa kukosa fursa hii ya kukamilishwa. Nikimwangusha Mungu, nitajuta maisha yangu yote. Nikimwacha Mungu nitahukumiwa na historia. Kama sitekelezi wajibu wangu vizuri na kulipiza upendo wa Mungu, ningewezaje kuishi mbele ya Mungu? Moyo wangu unathamini ukweli tu na umejitolea kwa Mungu, kamwe sitaasi tena na kumfadhaisha Mungu. Nimeamua kumpenda Mungu na kuendelea kujitolea kabisa kwa Mungu na hakuna chochote au yeyote anayeweza kunizuia. Nami nitakuwa na ushuhuda wa kumtukuza Mungu bila kujali jinsi majaribu na dhiki yalivyo. Nitaishi maisha yenye maana kwa kuupata ukweli na ukamilishaji wa Mungu.

Iliyotangulia: 187 Nitalipa Upendo wa Mungu

Inayofuata: 189 Kugutuka Kupitia Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp